Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 215
- 316
Karibu katika Simulizi Mwanzo - Mwisho ya PENDO HURU.
Nafasi ya Mapenzi ya kweli katika jamii,
Nafasi ya wazazi katika mapenzi ya watoto.
Mioyo migumu iliyobeba siri zinazo angamiza nchi... Utamaduni na Mila katika nchi ya Malindi.
Karibuni sana.
MTUNZI: XAVERY EMMANUEL LUOGA
SIMULIZI: “PENDO HURU’
NAMBA: 0672493994
EPISODE 01
SEHEMU YA KWANZA
Kilikuwa ni kijiji cha malindi katika nchi ya Tegemeo. Ilikuwa ni asubuhi ambayo shughuli mbalimbali za maendeleo ziliendelea, kila mja hakuacha kujishughulisha katika jambo ambalo linapaswa kufanywa kwa wakati huo, ndege, wanyama na binadamu wengine hawakuacha kupiga kelele za asubuhi kuashilia kuwa kumekucha, si kuku tu aliyesikia akiunguruma kijijini hapo hata mbuzi nao walitoka katika mabanda yao. Kijiji kiliamka vizuri siku hiyo.
“La mgambo… la mgambo… La Mgambo” tufe lilisikaka kila kona ya kijiji, hakuna aliyefanya kazi. Kila mmoja akaacha akifanyacho kujua ni nini hasa wito wa tangazo hilo. Vichwa vya watu viligongana kwa kujibizana kuwa, ulikuwa ni wito wa mfalme, lakini hakuna ambaye alijua nini sababu ya wito huo.
“La Mgambo likisikika ujuwe kuna jambo.. tunahitajika wakazi wote wa kijiji wa malindi katika uwanja wa Mbio Ndefu karibu na lango la Mfalme. Kuna wito kadhaa….” Mtoa tangazo aliendelea kuungurumisha sauti yake katika kipaza kile cha pembe la ng’ombe. Hakuna aliyetoa sababu ya kutosikia wito huo kwa sababu, heshima ya mfalme ilikuwa ni kubwa sana kiasi kwamba kukahidi agizo lilikuwa ni tatizo ambalo litapelekea tatizo lingine.
Umati wa watu ulikusanyika kwa wingi katika uwanja huo wa Mbio Ndefu kwa kusikiliza wito, kila kona kelele zilikuwa ni nyingi kwani katika sehemu hiyo watu wanakuwa ni wengi, na wengi wao ndio kwa mara ya kwanza wanakutana, wengine wanamuda mrefu toka waachane kwahiyo walitumia fursa hiyo adimu ya wito wa mfalme.
Kimya kilitanda ghafla mara baada ya mfalme kupandishwa katika jukwaa la juu lililotengenezwa kwa miti migumu, mfalme alionekena kuchoka sana kwa kushindwa hata kuonyesha nguvu ya ukakamavu mashavuni kwake, alibota sana.
Licha ya kuvaa nguo kubwa kumrudisha katika hadhi yake ya utawala kipindi cha ujana, lakini lengo la miaka kwenda mbele haikuchoka, miaka ikaendelea kumuumbua mfalme na kuthibitisha kuwa mfalme amechoka sasa.
Pembeni kidogo kulikuwa na binti mrembo ambaye kwa asilimia zote alifanana kabisa na na mwanamke mwingine aliyekuwepo upande wake wa kulia, aliyesimama upande wa kulia alikuwa ni Mama yake. Mke mkubwa wa mtukufu mfalme Bana, walifanana kuanzia sura hadi rangi na vimo vyao, kila kitu kililandana.
Nyuma ya mfalme kulikuwa na idadi kubwa ya walinzi ambao waliongozwa na kijana shupavu amabye hakuna asiyemfahamu kijijini hapo. Alikuwa mtu wa miraba minne. Mweusi kupita neno Nyeusi. Kama macho yako yatakuwa ya kulegalega unaeweza kumpita kwa kumfananisha na mkaa. Alipopanda mfalme wote wakawa kimya na kumpisha mfalme aongee.
“Wananchi, nipo hapa kutoa ufafanuzi wa kufunguliwa ghurudumu ya michezo ya kimalindi ya utamaduni katika uwanja huu wa Mbio Ndefu. Mashindano hayo yataanza kipindi kijacho cha wiki mbili baadae, wito wangu ni kuwa kila mshiriki ajiandae vyema katika kinyanganyilo cha zawadi nono ambacho kila mtu anakijua. Pia washindi wote kwa upande wa kiume na wa kike watajishindia taji na nafasi ya cheo kikubwa katika utawala wangu. Kohno!” mfalme akakohoa kidogo kisha kuendelea.
“Kila mshiliki atajiandikisha kama ulivyo utaratibu wa miaka yote na ni lazima kushiliki kama unakipaji. Siku ya hitimisho la mashindano hayo nitatangaza..” Mtukufu mfalme alibwabwaja maneno ya vishindo vya kila aina. Alikuwa serious sana na maisha. Hakuna nyau aliye mtisha katika utawala wake. Alikuwa Mungu wa Malindi lakini kibaya kuliko vyote bado hakupata mrithi. Hadi kuzeeka kwake hakuwai kupata mtoto wa kiume. Kila mbegu aliyopanda kwake ilikuwa ni mbichi, ikawa nyepesi kuharibika. Ikafia mbali. Na hakuna kidume kamwe!.
**********
“Bwanah! Sadiki eh!, lo!, mimi sina neno kabisa juu ya mtoto wa Mfalme!, sina nguvu kabisa Kaka!. Siku ukisikia nimekufa basi ni sababu ya presha ya kumkosa Binti Zawadi katika moyo wangu. Nampenda..” zilikuwa ni tambo za Saleh kwa rafiki yake Sadiki. Wote walishikana mabega na wakiongozana kurudi makwao.
“Kakaa!, Kaka!, unamjua Abunuasi wewe?. Hahahahaha!, huwa napenda sana ndoto zako za mchana mchana. Toka kuzaliwa kwangu Malindi, katu sijawai kuona Ufalme unarishishwa kwa mtoto wa fukara na asiye na hata chembe ya umaharufu… ilaa!, Jasiri hakati tamaa na mimi sio mmoja wapo watao uangaike!. Rafiki yangu!!! Kumpata Zawadi…, lazima kupigana Kufa na Kupona. Yule sio Zawadi tena. Kama baba ndio vilee umri umemtupa mkono. Nadhani madaraka yote yapo chini yake..” Sadiki naye hakuacha kumkumbata rafiki yake kwa kumpa uhalisia wa maisha. Mdogomdogo safari ikashika kasi, kila moja akitoa na kuweka mada yake kuhusu mapenzi na maisha yao. Hadi kufika kwao njia panda ya kuachana kila mmoja alikwenda kweke.
***************
Saleh na Sadiki ni marafiki wa kutupwa, usiombe ukutane na Saleh, basi umekutana na Sadiki. Alikadhalika kwa Sadiki. Wawili hao walishibana haswa katika maisha. Ufukara kwao haukuwa kikwazo kabisa katika kuendelea sebene la maisha. Walilidhika na shughuli ndogondogo za kijijini huku, Saleh akiwa moja ya wafuataji wakubwa wa ndogo ya Baba yake. Baba yake alikuwa muwindaji na mtoto hakuwa na budi kuifuata ndoto ya baba.
Sadiki yeye alikuwa bingwa katika michezo ya sarakasi, kupiga na kucheza ngoma. Sadiki alikuwa bize kuongelewa Malindi nzima katika suala la usakataji na utambaji ngoma za asili. Usiombe aanze, katu kumaliza kwake kutakukera. Utatamani sana ulale na yeye akikuburudisha kwa fanaka yake ya aina yake.
Saleh na Sadiki Waliishi katika maisha ya kufarijiana na kusaidiana katika kila hatua. Hakuna jambo la kutenganisha ndoa hii. Imefungwa kwa kufuri la roho.! Sadiki na Saleh walishibana. Hakuna aliyekula robo tatu, wote walipatiana nusu nusu angali familia zao hazikuishi karibu sana. Zilikuwa na umbali kiasi, lakini kwao wakaitumia kama fursa na sio changamoto.
**********
Pembezoni kidogo mwa kijijini cha Malindi alikuwako nyumba chakavu waliyoishi moja ya familia inayojishughulisha na shughuli ya kilimo na uwindaji. Ilitosha kabisa kuitwa familia kwa kuwa hakuna kilichokosekana.
Ilikuwa ni nyumba ya kina Saleh, pilikapilika za hapa na pale zilikuwa ziliendelea. Kwa hamu kubwa Mama Saleh alikuwa akimsubiri kijana wake kumuagiza baadhi ya vitu. Mama naye umri ulianza kumpotea. Alishindwa kabisa kuhesabu siku zake zinazoendelea.
“Ulipita hadi kwa Mzee Chomeo?..” Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mama Saleh ambalo lilimkuta Saleh akiwa bado hatua chache kumkaribia.
“Shkamo Mama.. Baba Salamu…!, Hapana Mama, Sadiki naye maneno mengi, wala hatujafika kwao. Maneno yametuchelewesha.” Saleh hakuwa mchoyo wa salamu, akazigawa kwa idadi ya wakubwa wake. Jibu lake lilimpeleka hadi ndani na masikio yake kuruhusu sauti ya mama yake iitike katika ngoma za masikio yake.
“Marhaba Baba…! Penyapo nilikuwa nakusubiri unisaidie kupeleka hivi vitu kwa Mama Zena!” Mama akatoa dukuduku lake la kumsubili mwanaye kwa kitambo.
“Baba kwani, hamjafika kwenye mkutano?” Saleh akamchokonoa baba yake aliyoko bize kuchonga zana zake za uwindaji.
“Tusiende alafu?. Hatuna jeuri hiyo. Tuliongozana sote, tukawai kurudi.” Akajibu kwa ustadi bila kupepesa macho.
Tayari Saleh iliingia ndani na kutoka nje. Mikono yake ikawa kiunoni na macho kuangalia jua, ilionesha kuna kitu aliendea kuchukua ndani na kulikosa.
“Sasa mwanangu, kipindi hiki yakupasa kuwai nyumabani, siku hizi si za kucheza cheza kabisa. Kazi ni nyingi!” Mama alitoa maneno ya kuashilia kitu, lakini Saleh alikuwa bado mbali kuwaza. Akazitoa pumzi kwa urefu zaidi na kusindikizwa na kajeri kutoka kwa baba yake ambaye aliiona hali ya saleh toka atoke ndani.
“Dogo, kama maji yamezidi unga fuata tu ombi la mama yako. Oa!” kauli hiyo ya Baba Seleh ilifanya Mama Saleh atanue mbavu zake kwa cheko la uzee. Wazazi wote hao wawili walitamani sana kuona kijana wao anashughulikia mapema suala la kuoa. Wakawa wanampiga vijembe tu.
“Mwanangu mimi nitakufa na sijaonja hata radha ya kuitwa Bibi!, huoni Haya?, mwenzako Sadiki ndio huyoooo hatua moja kama sio mbili zimebaki. Hadi posa tayari!. Wabaki wewe tu kijijini hapa. Mimi baba Saleh unajua hadi kuna muda nawaza kuwa wanawake wote wameshaisha hapa kijijini..!, waliobaki sina imani nao. Sasa mwanangu sijui ni padire?” Mama Seleh akatia kijembe kwa kumuunganisha na Mume wake.
Saleh hakujibu neno zaidi ya kutabasamu tu. Alijua fika kuwa wazazi wake wapo katika hatua kubwa mno ya kutaka kushudia ndoa na mtoto kutoka kwake. Lakini bado hawajui kwamba nafsi ya saleh imeegema kwa Binti wa mfalme na si mwingine. Ikabaki kuwa siri yake tu moyoni. Alificha nyasi karibu na moto.
“Wangejua!!!” Saleh alimungunya maneno rohoni na kukusanya vyombo kutoka kwa mama yake ambavyo Vilikuwa vinaelekea kwa mama Zena.
“Mwanangu!!! hata Zena huyohuyo mbona mzuri tu!, hurudi nae basi!!.. hahaha!” ilikuwa ni furaha na kijembe kingine kutoka kwa Mama. Kijembe kilichomsindikiza Saleh kwa juhudi kubwa kwani katu katakata kulisikia hata hilo jina la Zena ambalo Mama yake amelitaja. Alilimezea tu mate na kuendelea na safari.
***********************
“Mama vitu hivi apa nimeagizwa, mi hata sikia nipo na kazi nawahi!” Haraka ya Saleh ilikuwa ipo kasi mno. Alimkabidhi Mama Zena vyombo, na kuomba kuondoka. Hakutaka maongezi zaidi na Mama Zena kwani alijia pilikapilika za Mama huyo, anamaneno kama chiriku.
“Saleh!!” ilikuwa ni sauti ya upole kutoka kwa Mama Zena. Hakusubiri sauti hiyo ipotee bure Mama Zena, tayari alimsogelea Saleh ambaye mapema alianza kutoa mguu wake kuondoka.
“Ivi Saleh, mwanangu mimi Zena anakasoro gani?” alihoji Mama Zena na kufanya Saleh kuwa kimya uso ukimshuka.
“Huna la kunidanganya!, nafahamu kila kitu. Hana kasoro mwanangu!, kwa nini unamuumiza sasa?, yani hadi mwanamke anakupenda nusu kufa lakini hutaki?!. Mzazi gani anapenda kuona mtoto wake anaumia?!” ilikuwa ni risala fupi kutoka kwa Mama Zena kwenda kwa Seleh.
“Lakini Mama tulishayamaliza hayo na Binti yako!..”. alijitetea Saleh.
“Loh! Mwa’mwa’mwa’mwa!, Kuyamaliza? Kivipi!!. Hujui kama mwanangu anaumia? Halali, hali. Nyumba haina amani!. Mimi najua ulimtaka radhi mwanangu kwa kuwa humpendi, na na na… haupo tayari kuwa naye. Lakini mimi kama Mama. Ninalisimamia suara hii. Nitatufuta hata mganga wa nje ya kijiji. Mwanangu lazima aolewe na wewe... Babae ilo penda!, usipende!, nenda nalo. Huwezi cheza na Akili zangu hata siku moja. Khaa!” Mama Zena sasa alipandisha lile zimwi lake la wakati yupo kijana. Alipigania nafsi ya Binti yake ambaye alishaweka bayana kufa kwa ajili ya Saleh. Kila gharama itatumika lazima mbwa apate chakula.
Saleh akaondoka kwa Mama Zena. Akaondoka na furushi la maneno ya lazima ambalo alishinikizwa alibebe na Mama Zena. Kichwa chake hakina hesabu nyingine zaidi ya Binti wa Mfalme tu Zawadi. Saleh alikuwa kwingine kama Zena alivyokufa kwake.. aliondoka kwa Mama Zena bila hata kuangaria nyuma. Alikaza miguu kama askari anaye asiyelipwa mshahara wake kwa miezi. Akatoweka Saleh
ITAENDELEA…
#LIKE, #COMMENT & #SHARE..
Starxav

Xavery Luoga.