Simulizi: Nyumba Iliyojaa Dhambi

Simulizi: Nyumba Iliyojaa Dhambi

SEHEMU YA 15

Nilishtuka sana, nilijiona kama mtu ambaye alikuwa kwenye mlango wa kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Ile ilikuwa ni almasi, kipande kikubwa kabisa ambacho kama ningekiuza basi ningepata pesa nyingi mno na kuwa tajiri mkubwa.

Hii ilimaanisha kwamba ningechukua msichana yeyote ninayemtaka na kulala naye, ningenunua simu kubwa zaidi, kujenga nyumba ya kifahari na kukunua gari moja matata kabisa.

Nilifurahi lakini sikutakiwa kuwa na pupa, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutaka kumfahamu zaidi yule mzee, nilimfanyia utu, hii haikumaanisha kwamba nilitakiwa niachache naye kisa tu nimepata almasi.

Siku hiyo mchana nikaondoka na kuelekea hospitalini kumuona mzee huyo. Nilipofika hapo, nikakutana na manesi ambao walinipeleka mpaka kwenye chumba alichokuwa ambapo huko nikakutana na familia yake iliyokuwa na majonzi mno.

Kulikuwa na mwanamke mmoja mtu mzima ambaye nahisi ndiye alikuwa mke wake, mabinti wawili wazuri wa umri wangu lakini pia kulikuwa na kijana mwingine.

Nesi akanitambulisha kwao kwamba mimi ndiye niliyemuokoa kutoka kwa wauaji na kumchukua kumpeleka hospitalini hapo. Walifurahi na kunishukuru kwani mimi ndiye niliokoa maisha yake.

Niliwahadithia kilichokuwa kimetokea, walinisikiliza na kunishangaa, haikuwa rahisi kwa binadamu wa kawaida kwenda kumuokoa mtu kwa watu waliokuwa na bastola na wakati hakukuwa na kitu mkononi.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa urafiki wangu na familia hii, tuliendelea kuwa karibu na kukutana hospitalini hapo kuzungumza huku upande mwingine wa moyo wangu nikiwa na hamu ya kufahamu kuhusu yule mzee.

“Mimi naitwa Nurat,” aliniambia msichana mmoja miongoni mwa wale watoto wa mzee yule.
“Ulijitambulisha mule ndani!” nilimwambia huku nikicheka.

“Najua! Ila ninahitaji kukufahamu zaidi!”
“Naitwa Edward Francis! Nipo singo, sijaoa, sina demu, mpenzi wala mke,” nilimwambia huku nikitabasamu, akaanza kucheka.
 
SEHEMU YA 16

Huyu Nurat ambaye nilikuwa nazungumza naye alikuwa msichana mrembo mno, alikuwa na nywele ndefu, sura nyembamba na macho ya goroli.

Kwa kumwangalia tu ilikuwa ni rahisi kusema kwamba alikuwa Mwarabu halisi na hata Kiswahili chake alichokuwa akiongea kilikuwa ni kile Kiswarabu kabisa.

Nilimpenda kutoka moyoni, tangu nizaliwe sikuwahi kufanya mapenzi na Mwarabu, siyo hivyo tu, hata kushika kiuno chake sikuwahi kufanya hivyo.

Nilikuwa na hamu kubwa, nilitamani kumwambia kwamba nilimpenda na hivyo nilihitaji penzi kutoka kwake. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea, lipsi zilivyokuwa zikicheza, kifua saa sita nilipagawa kupita kawaida.

Kila nilipomwangalia, moyo wangu uliniambia ‘Edward! Unasubiri nini?’. Sikutakiwa kuwa na presha kwa sababu watoto wazuri kama hawa unatakiwa kuwafuata kwa mahesabu makali sana.
Naweza kusema kwamba huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuzoeana na Nurat.

Kila siku tulikuwa tukionana na yeye ndiye aliyejaribu kuyabadilisha maisha yangu baada ya kufika katika chumba kidogo nilichokuwa nikiishi.

Alininunulia kitanda cha chuma, chumba kikapigwa rangi na kunipa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya matumizi yangu mengine.

Kumbuka mpaka kipindi hicho sikuwa nimeiuza ile almasi kwa sababu sikujua soko lipo wapi na sikuwa na mtu wa kumwamini hata kidogo.

Wakati hayo yakiendelea, upande wa pili niliendelea kutafuta soko taratibu. Siku ziliendelea kukatika na baada ya siku mbili nikapata taarifa kwamba rafiki yetu, Mrisho aliuawa na mwili wake kutupwa baharini.

Nilishtuka sana, huyu Mrisho alikuwa mlinzi mwenzangu pale Kariakoo na alikuwa miongoni mwa watu ambao tulimsaidia yule mzee kumpeleka hospitalini.

Msiba wake uliwagusa watu wengi, alikuwa kijana mpole, sasa ilikuwaje awe na maadui na wakati kila wakati alikuwa mcheshi na hakubagua ni nani wa kuongea naye?

Tulihuzunika sana hivyo tulichokifanya ni kwenda kwenye mazishi na baada ya kumzika tukaendelea kufanya mambo mengine kama kawaida.
 
SEHEMU YA 17

Katika hayo yote, sikuacha kuwasiliana na msichana Aisha. Nilimkumbuka na wakati mwingine alikuwa akija na kwenda naye chumbani. Aisha alikuwa malaya tu lakini kitu cha ajabu kabisa alionekana kunikubali kupita kawaida.

Nilikuwa masikini, aliujua ukweli lakini wala hakujali kiasi kwamba nikawa nashangaa kwamba ilikuwaje anikubali kiasi kile?

“Hivi unanipenda kweli ama?” nilimuuliza.
“Nakupenda sana Edward! Huamini?”
“Naamini ila si unajua tena jinsi nilivyo! Mtoto mzuri kama wewe kuwa na mimi, huwa naona kama naota,” nilimwambia huku nikitoa tabasamu pana.

Maisha yaliendelea, sikumwambia mtu kuhusu ile almasi, niliificha chumbani sehemu salama kabisa. Siku zikakatika, baada ya wiki mbili tukapata msiba mwingine wa jamaa yetu wa karibu (Selemani) ambaye alikuwa mlinzi kama mimi.

Taarifa za awali zilisema kwamba jamaa alichomwa kisu na mtu asiyejulikana usiku wa manane nyumbani kwake kwa sababu siku hiyo hakuja kazini.

Kama ulivyotuuma msiba wa kwanza, hata huo ulituuma sana kwa kuwa alikuwa Selemani alikuwa kama Mrisho, kijana mchangamfu ambaye alizungumza na kila mtu. Ilituuma sana lakini hatukuwa na jinsi, Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihidiwe.

Siku hiyo usiku wa saa tisa nilipokuwa nimekaa sehemu nikiyafikiria maisha yangu huku nikiendelea kufanya kazi ya ulinzi hapo sokoni nikaanza kujiuliza swali moja muhimu sana.

Lilikuja tu kichwani, nadhani kama Mungu alihitaji kunifumbua kitu fulani. Nikaanza kujiuliza kuhusu vifo vya watu waliokuwa wameuawa. Nilichanganyikiwa kidogo kwa sababu niligundua kwamba walikuwa walinzi, kwa nini wauawe ndani ya siku chache?

Wakati nikiendelea kujiuliza hilo, moyo wangu ulikuwa na shaka mno, nilihisi kabisa kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.

Sikutaka kubaki kimya, nikawaita wenzangu na kuwaambia kuhusu maswali niliyokuwa nikijiuliza, kwamba kwa nini waliokuwa wakiuawa walikuwa walinzi?

“Unaogopa sana! Acha kuogopa mtoto wa mama,” alisema Fred huku akiniangalia, sura yake ilikuwa na tabasamu pana.
“Fred! Unajua siriazi wazee inabidi tujiulize kuhusu haya mauaji!” niliwaambia.
 
SEHEMU YA 18

“Kwa hiyo unahisi watu wanaanza kutuua sisi walinzi? Kama wanatuua, kwa nini hawaibi?” aliuliza mwingine, huyu aliitwa Msekwa.

Kiukweli hili lilinichanganya kichwa sana lakini wenzangu hawakuwa na hofu hata kidogo.

Nilichanganyikiwa mno ila kwa kuwa wenzangu hawakuonekana kuwa na hofu, basi na mimi nikajifariji kwamba hakukuwa na tatizo hivyo sikutakiwa kuhofia hata kidogo.

Japokuwa nilikubaliana nao lakini sikutaka kupotezea kabisa, kichwa changu kiliniambia kwamba kulikuwa na jambo lililokuwa likiendelea nyuma ya pazia.

Asubuhi ilipofika, huku nikiwa katika chumba changu, Nurat akapiga simu kwamba alikuwa akija kuniona kwa kuwa hakwenda chuo siku hiyo.

Nikamkaribisha! Ndani ya dakika chache, akafika, akatulia na kumwambia niende kumnunulia kinywaji dukani. Alikataa lakini si unajua lazima mwanaume uonyeshe umwamba, nikaenda hivyohivyo huku yeye akinisubiri ndani.

Duka halikuwa mbali sana na mahali hapo, kulikuwa na vichochoro vichache kabla ya kuingia kwenye barabara kubwa iliyokuwa na maduka mengi.

Nilipofika kwenye barabara hiyo, macho yangu yakatua kwenye gari moja lililosimama pembeni, ilikuwa Noah Nyeusi. Sikulitilia maanani, nilielekea dukani, nikanunua soda na kuanza kurudi.

Ghafla mlango wa gari lile ukafunguliwa na mwanaume mmoja kuteremka huku akiwa na sigara mkononi. Akaniita kwa kuniomba sana, nikamsogea.

“Samahani ndugu yangu, wewe ni mwenyeji maeneo haya?” aliniuliza huku akiniangalia.

“Ndiyo! Kuna nini bosi?”
“Unamfahamu huyu?” aliniuliza huku akinionyeshea picha ya mwanamke mmoja.

Niliiangalia kwa makini, sikuwa nikimfahamu na sikuwahi kumuona hata siku moja. Nilimrudishia na kumwambia kwamba sikuwa nikimfahamu.

“Haina shida! Unaweza kuingia ndani ya gari twende tukazungumze?” aliniuliza huku akiwa na tabasamu pana.
“Ndani ya gari? Hapana! Nina haraka,” nilimwambia.

“Kweli?” aliniuliza huku akinionyeshea bastola yake iliyokuwa kiunoni.
Nilishtuka mno, nilitamani kukimbia lakini nilipokumbuka kwamba bastola ilikuwa na uwezo wa kukuua hata ukiwa mbali, niliogopa kupita kiasi.
 
SEHEMU YA 19

Sikumjua mtu huyo alikuwa nani, alihitaji nini ila alichotaka ni mimi kutii kile alichokuwa akiniamba.

Sikubisha, mlango ukafunguliwa, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wengine kama watatu hivi, wote kwa kuwaangalia tu sura zao zilikuwa ngumu, yaani zilionyesha kuwa ni watu wasiokuwa na masihara hata kidogo.

“Ingia fasta dogo tusije kukumwaga utumbo,” alisema mwanaume mmoja aliyekuwa ndani ya gari, kusikia hivyo, haraka sana nikaingia ndani.

Gari likawashwa na kuondoka mahali hapo.
Nilikuwa na hofu, nilijua kabisa kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wangu. Niliogopa na kutetemeka mno, nilitekwa na majamaa hao waliokuwa kwenye Noah Nyeusi, nililia lakini sikutakiwa kuongea kitu chochote kile kwani vinginevyo wangeweza kuniua.

“Tukifika tutakuuliza swali moja tu kuhusu almasi, na ukijifanya kuwa mjanja kama wale walinzi wenzako, tutakuua kama tulivyowaua,” alisema mwanaume mmoja huku akinipigapiga kibao shavuni.

Moyo wangu ukapiga paaa! Kumbe hawa ndiyo majamaa wale waliowamaliza marafiki zangu, sasa zamu yangu ilifuata.

Je, nini kitaendelea?
Je, nilikufa?
 
Shunie asanteh kwa vigongo vitamu kama hiviii, nmepata faraja ya kweli haswaaa......
Ila leo umeniacha katikati ya bahari kabisa mwenyewe na nilitegemea utanifikisha!! Na sijui nafkaje ng'ambo huko, naomba nitoe hapa katikat ya bahari kwa kutupia kigongo kimoja tuuu angalau nitoke hapa..! Vinginevyo mwenzako nafaaa
 
nenda kwa karim
Shunie asanteh kwa vigongo vitamu kama hiviii, nmepata faraja ya kweli haswaaa......
Ila leo umeniacha katikati ya bahari kabisa mwenyewe na nilitegemea utanifikisha!! Na sijui nafkaje ng'ambo huko, naomba nitoe hapa katikat ya bahari kwa kutupia kigongo kimoja tuuu angalau nitoke hapa..! Vinginevyo mwenzako nafaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom