SIMULIZI: Nyayo za Marehemu

SIMULIZI: Nyayo za Marehemu

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
1,002
Reaction score
956
Nakumbuka ilikuwa tarehe tatu march 1998,nikiwa mwanafunzi shule ya sekondari mwembetogwa pale iringa.baada ya masomo nilipata likizo fupi.nikawaomba wazazi niende kwa babu yangu aliyekuwa akiishi takribani km 30 katika kijiji cha Nyabula.Babu yangu huyu alikuwa ni mzaa mama.

Baba yangu alikubali niende kwa shingo upande mara nyingi hakupenda mimi kutembelea kwa babu yangu.Nilidandia magari yaendayo kule na kufika kijijini.Babu yangu alifurahi sana akaniambia nimefika muda muafaka.Nilipata msosi na kulala mapema.Chumba changu kilikuwa ni cha nje nanilipakana na mabanda ya ng'ombe.Ilipotimia mishale ya saa sita hivi usiku,usingizi ulikata ghafla,nikasikia upepo mkali ukivuma.mwili wangu ulisisimuka ghafla nikatazama ukutani nikaona ukipasuka na babu yangu akiwa uchi wa mnyama akiniamulu nimfuate.nilijaribu kukataa lakini sauti haikutoka.akaniambia kuna sehemu naenda kukutambulisha ukijaribu kufanya lolote utaondoka.Kimoyomoyo nikajisemea Mungu wangu ni mambo gani haya.

Nikamfuata mpaka nje nyuma ya mabanda.nikamuona fisi mdogo aliyedhoofika.akanipa ishara nikae mgongoni huku nikitetemeka nika kaa nayeye akakaa huku sehemu kubwa ya mwili wake yaani makalio yamegusa kichwa cha fisi ghafla,fisi alichukua kasi tukaanza kukimbia na kuruka hewani.tukiwa juu,huwezi amini.tulipishana na watu makundi kwa makundi wakiwa wawili wawili kwenye nyungo uchi wa mnyama.fisi wetu alikuwa na kasi sana angani,ghafla tukawa tunaliona kitu kama bahari hivi,sikujua ni wapi,tukapaa juu ya bahari tukatua kisiwani. tukamuacha fisi.tukaanza kutembea kwa miguu,tukiwa tunatembea tulipishana na watu wakirudi lakini wote walikuwa uchi.mita kama hamsini nikawaona watu wengine wakiwa uchi wameketi kama wakijadili jambo.alipofika babu wote walisimama,babu akamsalimia bibi mmoja wa makamo,ndiyo akasema vipi umemleta mbona umechelewa sana.

Akajibu nimemleta namuona anashangaa shangaa bado lakini taratibu ataelewa.basi nikaelezwa nimepata bahati ya kupewa ukubwa.na kwamba nitafaidika duniani na kamwe sitapata taabu na kusumbuliwa na yeyote kama nitafuata masharti.nilinyamaza kimya bila kuzungumza chochote.ikaletwa nyama lakini sikutambua ni ya nini nikanyweshwa supu huku wananitazama nikapewa nyama kugeuza hivi nikiganja cha mtu.mkono wake ulikuwa mweusi tii.nilikula huku ikinijaa mdomoni maana nilishindwa kumeza.nilipojaribu kumeza nilitapika.bibi mmoja akanigonga na mfupa mrefu ulio onekana kama mguu wa mtu.nikagumia chinichini kwa woga."pumbavu wee ukileta mchezo utaliwa kama mwenzio,hivi mzee umemueleza huyu" babu akanichomekea 'anaelewa sana".

Wakati tunarudi nilifanikiwa kuona neno "karibu mbamba bay" nikajua tumetoka iringa mpaka mbambabay visiwani.tukampanda fisi wetu muda mfupi tukawa kijijini.Babu alinionya kutofanya lolote au kumwambia mtu .kulipo pambazuka nilimwambia bibi ningeondoka.bibi akasema mbona umekaa siku moja tu nikashindwa kutoa maelezo ya kutosha.nikabaki tu.khofu yangu ni mkasa na safari ya jana.usiku uliofuata tena babu alikuja kwa njia ile ile akanieleza leo tutaenda shambani kutazama mifugo.nilijiuliza mifugo gani akaniambia utaiona mbele.leo hii akafanya mambo yake ghafla fisi akaja.mara hii hakupaa ila alikuwa spidi ya kati.

kwa kuwa tulikuwa tukiingia polini sikujua ni wapi.tulienda na kutokea kwenye uwazi mkubwa ambalo ni shamba.tukashuka babu akaanza nitembeza kulikuwa kuna watu takribani thelathini walikuwa wamekonda sana,wakijikongoja kulima bila nguo.babu akaniuliza unawafahamu nikakataa,akamuita mmoja kwa jina Jackson njoo hapa mnh ,jack alikuwa ni mjomba wangu aliyefariki kwa ajali takribani miaka minne imepita.mnhh,alipokuja alikonda sana,nywele zake zilikuwa ndefu sana,na kucha zake pia ndefu ma chafu,alinitazama kama alitaka kusema jambo akaishia machozi kumtoka.kumbe alikuwa msukule.

Babu akaita tena Agnesi njoo,nilipigwa na butwaa agnes alikuwa ni mdogo wake mwisho mama yangu alikuwa ni muajiliwa wa wizaraya afya Dar wakati anafariki alikuja likizo kupumzika.akaugua ghafla nakufariki siku ya pili.Nilimtizama kwa woga lakini sikupepesa macho nikajisikia uchungu sana alinitizama machozi yakamlenga.naye pia alijaribu kusema kitu lakini alishindwa.babu akawa ananipitisha taratibu kuna baadhi ya watu wazima na vijana nilishindwa kuwatambua mara moja.unajua nini kilitokea mbele..

weka likes nyingi ujue kwa nini nawapa simulizi hiii.muda wangu umekwisha nitaendelea kesho.
 
lakini si ulipewa sharti la kuto kumwambia mtu yoyote hii story mkuu?
 
Story yenyewe unaitoa kiviivu, mwishowe uje utuambie unaimalizia wasap kwa buku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom