Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 454

“Najua wengi sana mtashangaa imekuwaje kuja kusimama hapa mbele na kutoa ujumbe huu ninaotaka kutoa, kwanza naomba mtambue kwamba sina nia mbaya ila nimekuja kwa upendo tu. Kuna kitu nimejiuliza sana jana usiku na ndio kimenifanya leo nije kuzungumza hapa, nimejiuliza san asana NINI MAANA YA MAPENZI? MAPENZI NI NINI? MAPENZI NI KITU GANI? Nimejiuliza sana ndugu zangu, ila nikasema naomba kupeleka kwa wadau labda watanisaidia kwa kile nilichonacho. Mimi kama Bahati nakiri kwenye umati huu mkubwa kuwa nilimpenda sana Ericana bado nampenda ndiomana nimekuja hapa kwani nimeona kama nampenda basi nimuache afurahi na furaha ya Erica ni kuolewa na Erick, asante Erick kwa kufanikisha hilo. Erica hakunipenda mimi kimapenzi ila alinipenda kama binadamu mwenzie, ila swala la kutonipenda kimapenzi halikumfanya anitenge kwani alinijali na kunithamini na kufikia hata hatua ya kuniokoa kutoka kwenye gonjwa la ukimwi, unaweza sema alifanya yote hayo sababu alinipenda kimapenzi hapana, ila aliniokoa sababu ndani mwake kuna upendo wa dhati na ndani mwake kuna kitu kinaitwa kujali. Naweza sema Erica ni mwanamke wa tofauti sana, na Erick ni mwanaume wa tofauti sana, nilimpenda Erica ila yeye hakunipenda na ikawa ngumu kutimiliza swala la mapenzi, ila Erica na Erick ndio maana halisi ya neno mapenzi kwa nionavyo mimi, nimefikiria na kuchambua nimeona mapenzi ni kupendana, kama mna mengine mtayaongezea ila nimeona mapenzi ni kupendana. Mungu awajaalie Erica na Erick nawaombea mpate watoto mapacha tena wakike na wa kiume nao muwaite Erica na Erick, asanteni”
Watu walipiga makofi, mama Erica aliinuka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea Bahati maana hakuamini kama Bahati angeweza kuongea vitu vya maana kiasi kile, alijua tu angelia lia pale mbele kuwa anampenda sana Erica.
Basi watu wengi wakafatana na mama Erica kwenda kumsindikia Bahati na kumpongeza.
Ulifika muda wa watu kwenda kusalimiana na maharusi na kugonga glasi za vinywaji kwa pamoja, ni muda huu ambao Derick alienda pia, ila alipofika pale Erick alimvuta karibu na kumnong’oneza,
“Sasa kile alichofanya Bahati ndio tunaita uanaume yani kule ndio kuwa mwanaume unakubaliana na matokeo sio mwanume unakuwa na wivu na dada yako”
Derick aliondoka na kurudi kwenye kiti ambapo pembeni yake kuna mdada alikuwa akivutiwa nae aliamua kutoa swaga zake,
“Nakupenda, natamani na mimi ifikie wakati nifunge ndoa”
“Ila umenipenda lakini mimi ni mjamzito”
“Ooh sawa, ila hata hivyo sidhani kama utanikubali maana mimi ni muathirika”
Yule dada akamwambia,
“Natamani kupata mume wa kunioa sana, na wala sijali kuhusu kuathirika kwako kama utanikubali na mimba yangu”
“Kweli umenikubalia? Unaitwa nani?”
“Naitwa Siwema, na wewe je?”
“Naitwa Derick, naomba twende kwa mama yangu pale akufahamu Siwema tafadhali”
Basi Derick na Siwema waliinuka na kwenda alipokaa mama yake Derick.
Kuna meza alikaa James, Dora na watu wengine akiwemo George, Dora alimtania George,
“Na wewe utaoa lini eeeh! Au bado unasubiri kuoa bikra?”
“Aaah Dora mbona hilo wazo limepotea kwangu sema tu sijampata wa kumuoa”
Pembeni yake kulikuwa na binti aliyebeba mtotot mdogo mikononi, alimwambia George
“Nioe mimi basi”
James na Dora walicheka kisha Dora akamwambia George,
“Eeeh mke huyo kajitokeza”
George alimuangalia Yule mwanamke na kumwambia,
“Dada, mimi natafuta muathirika mwenzangu maana mimi nina ukimwi”
Nipo tayari kuishi na wewe hivyo hivyo”
“Unaitwa nani dada?”
“Naitwa Nasma”
Dora akajaribu kumshauri Nasma,
“Usiharakie sana kuolewa angalia maisha yako na mtoto, usikimbilie kuolewa mdogo wangu. Unatakiwa kuangalia maisha yako yani ukauzoe ukimwi sababu ya kutamani kuolewa! Hapana kwakweli, jifikirie mara mbili”
Ujumbe ule ulimuingia Nasma ingawa alikuwa na hamu sana ya kupata mume na kuolewa tu.
 
SEHEMU YA 455 ................ MWISHO


Basi walicheza na kusherekea hadi muda chakula ambapo watu walikula na kusaza na muda wa zawadi ulivyofika watu walianza kupeleka zawadi zao ambapo Bahati alienda na kumkabidhi Erica hati ya shamba na kuongea kidogo,
“Napenda kutoa zawadi hii ya shamba kwa Erica maana ulikuwa ni mpango wangu wa muda mrefu sana, siwezi kuacha kwakweli. Shamba hili likawe faida kwa Angel, nampenda sana huyu mtoto na nilisema kuwa napenda sana kuwa baba yake sema mambo yaliingiliana ila bado sio kwamba ni mwisho wa kuwa familia, nampenda na ninatoa shamba hili kama zawadi kwake, naomba mpokee zawadi hii”
Bahati alijua kama akisema ni zawadi kwaajili ya Erica basi Erick anaweza kuigomea kwahiyo akasema ni zawadi ya Angel, muda kidogo Rahim nae alienda kutoa awadi yake ambayo pia aliielekeza kwa Angel, alikuwa na hundi ya milioni kumi na tano na kusema,
“Nakumbuka Erica uliwahi kuniomba pesa hii ili ufanyie biashara kwaajili ya kulea vyema mtoto wetu ila sikutaka kwani nilijua nakukomesha na lazima utanyenyekea sana kwangu, sikuwa na haja na wewe sababu nilikuwa na wanawake wengine ambao nilikuwa naona wananifaa kumbe sikuangalia ya mbeleni, natoa hundi hii ukaiweke kwenye akaunti ya Angel na ajue kwamba nimetubu na nitamjali”
Erica alipokea ile hundi kwa uzuri kabisa sema hawa watoa zawadi walikuwa wakiongea moja kwa moja na wahusika kwahiyo watu walikuwa wakisikia ni wale wa karibu tu.
Basi muda wa zawadi uliisha na walikuwa wakicheza tu, kisha ukawa muda wa kuaga wale maharusi ili wakapumzike, Mc akawataka wale mabibi harusi waeushe maua akiamini kuwa atakayedaka ndio harusi inayofatia.
Basi Erica alirusha ua lake na likadakwa na Bite, walifurahi sana na kuona kumbe harusi ya Bite inanukia, kisha Tumaini nae akarusha ua lake, likadakwa na bi.Aisha, watu walicheka sana kuona bi.Aisha kadaka lile ua maana walimuona ni mtu mzima, walicheka sana. Mzee Jimmy alimvuta pembeni bi.Aisha na kumuuliza,
“Na wewe unahitaji kuolewa?”
Bi.Aisha alicheka tu, kisha mzee Jimmy aliendelea kuongea,
“Niambie ukweli una mpango wa kuolewa? Maana hata mimi nahitaji kuoa ila nimeathirika”
“Na mimi ni muathirika pia”
Mzee Jimmy alimsogelea bi.Aisha na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Wewe utakuwa mke wangu”
Watu waliowaona walicheka sana.
Kisha maharusi wakaruhusiwa kwenda kupumzika, ila kabla hawajaondoka walimuomba Yule mama wa maombi aseme neno moja nae alisema,
“Alichokiunganisha Mungu basi mwanadamu asikitenganishe”
Ukumbu wote ulisikika ukisema,
“Ameeeen”
Na vigelegele, nderemo na vifijo vilisikika kisha maharusi ndio wakaondoka kwa furaha.

Siku ya birthday ya Erick na Erica ni siku ambayo waliamua kwenda kupima ule ujauzito ambao Erica alikuwa nao kwa ultrasound, na furaha iliongezeka maradufu baada ya kuona kuwa mimba ya Erica ilibeba mapacha wa kike na kiume. Erick alifurahi sana na kumkumbatia Erica kwa furaha kwani aliona kuwa ile ni zawadi kubwa sana kwenye siku yao ile muhimu.

---------MWISHO---------
 
AlmasMAlmas kili255 jacobcm8 loviesundy moneytalk kyakumwanya bubblymolly nyakisese Teta ukhty khadija ikhatibu Depal aggyd Vampiree Shabdullah Lusius haule Mine eyes isaacklawa01 Nuhu39 TzDee jKingSenior chullu big jambo kanyembwe Eco mangonifera indica Lovi pius kijogoo Dreamliner787 Coping Strategy chacha nyangaka unprejudiced famad Shupavu jonta ilu paul samky assey yna2 lamisa BrainIndependent Lengutee Ayanda85 Flava90s Joseph lebai Wang Shu jay pelle evonik Kaijadan enjai ya kyasha NDABANINGI STHOLE mdachi khan kanonb kilambon billduke KigaKoyo Mr no Kilosaone Authority Msichana wa jana anwarez lameckkawawa anawoo Luge brown Smart911 amsr mbogagambo Jovet The Hurricane Fundi_Mjasiriamali Kiwarhoapandenga LOCAL SPONSOR negronites Mr Cu Mshughulishaji danymTZ francoo1 helment subadesubking mkulima2 Mimi ni huyo Mogambi Lewis18 Mdex Daynv song 16 Gobole dafity instanbul Sangoma Kanyigoboy Thadeus Thadeo stacia sojobizzy Chabrosy leechan de ommykhan mwanaspotiapp MENO YA UKU Gwappo Mwakatobe G'taxi Interlacustrine Region chrisbleez femalepilot benjamin kayombo kitalembwa joefrancy binti mapozi EnnoMX Nimetoka Katavi kaka kaka kax bedui Jr kuchikubwa Baharia wa Buza crix pronto Mkatauzi mpasta MR KUO charrote babu chilau Secret Man Mtende Teleshkova Hades NEIMAA Keijay Lex luther kipanta SangaweJr Litro qim SIFUGIKI Mnazareth chabeen ummul khaulaty mgaka ivan1212 josephat mugisha longola FrankMakeps jonoma elvas kizeze mandella DENAMWE Troisième Ceil mlyn Cappuccino Mkare_wenu Machmadem bioto yona raphael denhoo manji h cariha havanna Muigai Jr Nyabhakangala kukumsela Mkulima Jr majangatz ELY NE Ibanga 53 Tonyblair asahd kidawisee fj44556 Angrybird muyakb24 Matts Reptilia Majjipolo 3lly da prophet creaty gal rehanishabani Franky Samuel MR MO CONFIDENCE meshack mnyambwa Active Dayone dumejeuri Joseparty manyanga21 dluv Enguraruu m.k Usher raymond Joharia makedonia Sir D Laurent apolinary network search von tosy qinglong Req Chemagati anunnaki kashata mactal project planner Magema jr benybeny Queen M NOHEMBRE Mhariri Da'Vinci Blackninja Kilindila kisukari makubia Super AMOLED Sky Eclat mkanyikivega nipo2 sophiere fred tarimo Mamaya Rural Swagga Elly Kiwango Nemesis Baba Mkubwa Dr. Poor Brain Dharra Lordrank Erickford4 AMBURIA Mweweso uhaale Mshuza2 Don Clericuzio Ochumeraa nyaiboko Isinika Bruno mbunda client3 Thadeo sijaona Bayser17 libeva Chiefmzala Disneyland Ukwaju sinyora edson Dominic Jr Sweta LA Tanzania Mkushi Mbishi Sangomwile stable Pettymagambo Ben Kaozlee Behaviourist Clkey bugza Boqin Phlagiey Mkulungai


MWISHO WA SIMULIZI YA NINI MAANA YA MAPENZI:

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati wa makundi yafuatayo:


1. Wale wote walionyesha ushirikiano wao kwa ku-comment na kulike, wakuu, asanteni sana, nguvu zenu zimenifanya niendelee kupost.

2. Wale wote ambao wamekuwa wakifuatilia simulizi hii kimyakimya, Wakuu natambua uwepo wenu, natumaini mtakuja ku-comment na kulike siku za mbeleni.


Tuendelee kuwa pamoja katika Riwaya, Visa na Simulizi nyingine.

SIMULIZI HII IMELETWA KWENU NA BURE SERIES
 

AlmasMAlmas
kili255 jacobcm8 loviesundy moneytalk kyakumwanya bubblymolly nyakisese Teta ukhty khadija ikhatibu Depal aggyd Vampiree Shabdullah Lusius haule Mine eyes isaacklawa01 Nuhu39 TzDee jKingSenior chullu big jambo kanyembwe Eco mangonifera indica Lovi pius kijogoo Dreamliner787 Coping Strategy chacha nyangaka unprejudiced famad Shupavu jonta ilu paul samky assey yna2 lamisa BrainIndependent Lengutee Ayanda85 Flava90s Joseph lebai Wang Shu jay pelle evonik Kaijadan enjai ya kyasha NDABANINGI STHOLE mdachi khan kanonb kilambon billduke KigaKoyo Mr no Kilosaone Authority Msichana wa jana anwarez lameckkawawa anawoo Luge brown Smart911 amsr mbogagambo Jovet The Hurricane Fundi_Mjasiriamali Kiwarhoapandenga LOCAL SPONSOR negronites Mr Cu Mshughulishaji danymTZ francoo1 helment subadesubking mkulima2 Mimi ni huyo Mogambi Lewis18 Mdex Daynv song 16 Gobole dafity instanbul Sangoma Kanyigoboy Thadeus Thadeo stacia sojobizzy Chabrosy leechan de ommykhan mwanaspotiapp MENO YA UKU Gwappo Mwakatobe G'taxi Interlacustrine Region chrisbleez femalepilot benjamin kayombo kitalembwa joefrancy binti mapozi EnnoMX Nimetoka Katavi kaka kaka kax bedui Jr kuchikubwa Baharia wa Buza crix pronto Mkatauzi mpasta MR KUO charrote babu chilau Secret Man Mtende Teleshkova Hades NEIMAA Keijay Lex luther kipanta SangaweJr Litro qim SIFUGIKI Mnazareth chabeen ummul khaulaty mgaka ivan1212 josephat mugisha longola FrankMakeps jonoma elvas kizeze mandella DENAMWE Troisième Ceil mlyn Cappuccino Mkare_wenu Machmadem bioto yona raphael denhoo manji h cariha havanna Muigai Jr Nyabhakangala kukumsela Mkulima Jr majangatz ELY NE Ibanga 53 Tonyblair asahd kidawisee fj44556 Angrybird muyakb24 Matts Reptilia Majjipolo 3lly da prophet creaty gal rehanishabani Franky Samuel MR MO CONFIDENCE meshack mnyambwa Active Dayone dumejeuri Joseparty manyanga21 dluv Enguraruu m.k Usher raymond Joharia makedonia Sir D Laurent apolinary network search von tosy qinglong Req Chemagati anunnaki kashata mactal project planner Magema jr benybeny Queen M NOHEMBRE Mhariri Da'Vinci Blackninja Kilindila kisukari makubia Super AMOLED Sky Eclat mkanyikivega nipo2 sophiere fred tarimo Mamaya Rural Swagga Elly Kiwango Nemesis Baba Mkubwa Dr. Poor Brain Dharra Lordrank Erickford4 AMBURIA Mweweso uhaale Mshuza2 Don Clericuzio Ochumeraa nyaiboko Isinika Bruno mbunda client3 Thadeo sijaona Bayser17 libeva Chiefmzala Disneyland Ukwaju sinyora edson Dominic Jr Sweta LA Tanzania Mkushi Mbishi Sangomwile stable Pettymagambo Ben Kaozlee Behaviourist Clkey bugza Boqin Phlagiey Mkulungai


MWISHO WA SIMULIZI YA NINI MAANA YA MAPENZI:

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati wa makundi yafuatayo:


1. Wale wote walionyesha ushirikiano wao kwa ku-comment na kulike, wakuu, asanteni sana, nguvu zenu zimenifanya niendelee kupost.

2. Wale wote ambao wamekuwa wakifuatilia simulizi hii kimyakimya, Wakuu natambua uwepo wenu, natumaini mtakuja ku-comment na kulike siku za mbeleni.


Tuendelee kuwa pamoja katika Riwaya, Visa na Simulizi nyingine.

@ Pseudepigraphas
nimefatilia kimya kimya hadi nimemaliza,daah iliweza kuniweka bize na kusahau stress zangu zote kwa muda,shukran mkuu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

💥 💥 💥NEW 💥💥💥

8. RIWAYA: Mume Gaidi

Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
Nimetumia week moja kuisoma hii simulizi, kiukweli simulizi ni nzuri na inamafunzo mengi sana na ni yakimaadili. Shukurani kwa mwandishi wa simulizi hii. Nitaendelea kufatilia simulizi zako mkuu
 
Nimetumia week moja kuisoma hii simulizi, kiukweli simulizi ni nzuri na inamafunzo mengi sana na ni yakimaadili. Shukurani kwa mwandishi wa simulizi hii. Nitaendelea kufatilia simulizi zako mkuu

Nashukuru sana mkuu kwa kuwa nami, endelea kuburudika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom