Simulizi: Nilivyonusurika kufa Mei 28, 2023 uwanja wa Benjamin Mkapa

JS Dairy Farm

JF-Expert Member
Feb 13, 2022
305
676
Nina muda mrefu sijaenda uwanja wa Benjamin Mkapa kutazama mechi mbalimbali kwa sababu ya mambo ya hovyo niliyowahi kuyashuhudia siku za nyuma lakini jana niliamua kwenda kwa sababu ni mechi ya fainali ya CAFCC na nilijua mambo yatakuwa ya kiwango cha fainali yaani ubora katika kila eneo.

Ilikuwa mechi kubwa sana ya shindano la mpira wa miguu ambayo tangu nchi hii iumbwe haijawahi kutokea lakini yaliyotokea nje ya uwanja ni aibu kubwa siyo tu kwa Tanzania pia kwa Afrika yote.

Nilikata tiketi ya VIP B tarehe 26 nikitegemea usumbufu utakuwa mdogo hasa ikizingatiwa tiketi za mzunguko zilikuwa nyingi zinatolewa bure, lakini sivyo. Nilifika mapema uwanjani muda wa saa 4 asubuhi nilikuta watu wengi sana nje ya uwanja na kadri muda ulivyokuwa unaenda na watu walikuwa wanaongezeka, pale nje ya uwanja mambo yalikuwa hovyohovyo wanauza vinywaji na chakula wateja wengi lakini vyoo vichache na mpaka ukipate kazi kubwa uifanye, nilisogea kwenye mageti.

Nikakuta yamefungwa na watu wengi wamejazana magetini kibaya zaidi hakuna matangazo ya kuandikwa au ya mdomo kwamba mageti yatafunguliwa saa ngapi au nini kinaendelea Polisi na walinzi wengine walikuwa wengi lakini mashabiki hakuna maelezo tuliyokuwa tunapewa.

Nilienda geti ambalo lipo karibu na geti kuu(mkono wa kushoto kama unauangalia uwanja) nikaambiwa na mtu aliyevaa kizibao(aliyeonekana kama mlinzi) niende geti la kushoto zaidi ambalo linatumiwa na mashabiki wa mzunguko lakini nilivyofika kule nikaambiwa na mashabiki kuwa nirudi nilikotoka kumbuka hakuna mtu rasmi wa kutoa utaratibu.Nilivyofika kwenye geti lililo karibu na geti kuu nikakuta wenzangu wengi waliokata tiketi za VIP B wamejazana watu zaidi ya 400 walikuwa wanasubiri pale lakini geti limefungwa hakuna maelezo Polisi wamejazana wanapiga stori geti kuu, walinzi waliovaa vizibao wanazunguka bila kutoa maelezo na wakitoa hayaeleweki kwa sababu hata wao walikuwa hawajui chochote.

Mpaka saa 6 mageti yalikuwa hayajafunguliwa na hakuna maelezo, matusi na fujo zikaanza, Polisi wapo wanangalia lakini hata mtoto wa darasa la tano angekuwepo angejua kitakachotokea muda si mrefu.

Mimi nilianza kukata tamaa ya kuingia uwanjani kwa sababu watu walikuwa wengi sana na walikuwa wanaongezeka kwa kasi na mageti yamefungwa mbaya zaidi hakuna maelezo na wala viongozi wa Yanga,TFF au wa serikali walikuwa hawaonekani.

Muda si muda nikaanza kuona mashabiki wa tiketi za mzunguko wanakimbia wengine wanaruka fensi na kuingia uwanjani huku VIP B walitulia kwa sababu wengi walikuwa si vijana lakini matusi na jazba zilitawala na wakati huo mvua inanyesha ambayo ilitulowesha nguo zetu za nje na za ndani.

Mara nikaona geti limefunguliwa/limevunjwa na mashabiki wa VIP B wanakimbia hovyohovyo na kwa kasi kuingia uwanjani, na mimi nikaanza kukimbia kuingia uwanjani kufika juu sehemu ya kuingiza kadi watu walikuwa zaidi ya 500 kwa kukadiria na sehemu(kifaa) ya kuingizia kadi ilikuwa moja hapo ndipo niliponusurika kifo maana nilibanwa karibu na ukuta na nikawa nashindwa kupumua, ikabidi nitumie nguvu kutoka eneo lile, kama ningezembea kidogo tu basi ningedondoka na ningekanyangwa kwa wakati ule hakuna aliyekuwa anamfikiria mwenzake kila mtu alikuwa anataka kuingia sehemu ya kukaa. Na eneo hilo halikuwa na Polisi wala walinzi wengine.

Mimi nilipona lakini kuna mtu aliyefariki na wengine kujeruhiwa lakini nimeamua kuandika haya ili kutoa tahadhari. Na kama mambo yataendelea kama jana siku zijazo tutegemee maafa zaidi.

Ushauri wangu:
1. Maafisa wa Polisi waliokuwepo uwanjani nje(kwenye mageti) hawakuwajibika ipasavyo kwahiyo wawajibishwe.

2. Tiketi zote ziwe zinauzwa, ukitangaza utatoa tiketi bure unakaribisha mafuriko ya watu uwanjani, kama tunataka mashabiki wengi wajaze uwanja tiketi hasa zile za mzunguko ziuzwe hata sh.v500 ili kudhibiti watu wengi kuja uwanjani.

3. Kuwe na MC nje ya uwanja atakayekuwa anatoa matangazo mbalimbali.

4. Kuwe na dawati la huduma ya wateja nje ya uwanja.

5. Tiketi zionyeshe namba ya siti shabiki akifika saa 2 asubuhi akae kwenye siti yake na yule atakayefika saa 9 akae kwenye siti yake, kukaa bila mpangilio inasababisha watu kufika kwa muda mmoja uwanjani na kusababisha msongamano.

6. Kama hali haitabadilika usiende na mtoto uwanjani jana kuna watu walienda na watoto na baadhi ya watoto walipotea.

Ndani ya uwanja mambo yalikuwa mazuri pamoja na mvua lakini mashabiki walikuwa wanashangilia muda wote.
 
Nina muda mrefu sijaenda uwanja wa Benjamin Mkapa kutazama mechi mbalimbali kwa sababu ya mambo ya hovyo niliyowahi kuyashuhudia siku za nyuma lakini jana niliamua kwenda kwa sababu ni mechi ya fainali ya CAFCC na nilijua mambo yatakuwa ya kiwango cha fainali yaani ubora katika kila eneo.

Ilikuwa mechi kubwa sana ya shindano la mpira wa miguu ambayo tangu nchi hii iumbwe haijawahi kutokea lakini yaliyotokea nje ya uwanja ni aibu kubwa siyo tu kwa Tanzania pia kwa Afrika yote.

Nilikata tiketi ya VIP B tarehe 26 nikitegemea usumbufu utakuwa mdogo hasa ikizingatiwa tiketi za mzunguko zilikuwa nyingi zinatolewa bure, lakini sivyo.Nilifika mapema uwanjani muda wa saa 4 asubuhi nilikuta watu wengi sana nje ya uwanja na kadri muda ulivyokuwa unaenda na watu walikuwa wanaongezeka, pale nje ya uwanja mambo yalikuwa hovyohovyo wanauza vinywaji na chakula wateja wengi lakini vyoo vichache na mpaka ukipate kazi kubwa uifanye,nilisogea kwenye mageti. nikakuta yamefungwa na watu wengi wamejazana magetini kibaya zaidi hakuna matangazo ya kuandikwa au ya mdomo kwamba mageti yatafunguliwa saa ngapi au nini kinaendelea Polisi na walinzi wengine walikuwa wengi lakini mashabiki hakuna maelezo tuliyokuwa tunapewa.

Nilienda geti ambalo lipo karibu na geti kuu(mkono wa kushoto kama unauangalia uwanja) nikaambiwa na mtu aliyevaa kizibao(aliyeonekana kama mlinzi) niende geti la kushoto zaidi ambalo linatumiwa na mashabiki wa mzunguko lakini nilivyofika kule nikaambiwa na mashabiki kuwa nirudi nilikotoka kumbuka hakuna mtu rasmi wa kutoa utaratibu.Nilivyofika kwenye geti lililo karibu na geti kuu nikakuta wenzangu wengi waliokata tiketi za VIP B wamejazana watu zaidi ya 400 walikuwa wanasubiri pale lakini geti limefungwa hakuna maelezo Polisi wamejazana wanapiga stori geti kuu, walinzi waliovaa vizibao wanazunguka bila kutoa maelezo na wakitoa hayaeleweki kwa sababu hata wao walikuwa hawajui chochote. Mpaka saa 6 mageti yalikuwa hayajafunguliwa na hakuna maelezo, matusi na fujo zikaanza,Polisi wapo wanangalia lakini hata mtoto wa darasa la tano angekuwepo angejua kitakachotokea muda si mrefu.

Mimi nilianza kukata tamaa ya kuingia uwanjani kwa sababu watu walikuwa wengi sana na walikuwa wanaongezeka kwa kasi na mageti yamefungwa mbaya zaidi hakuna maelezo na wala viongozi wa Yanga,TFF au wa serikali walikuwa hawaonekani.Muda si muda nikaanza kuona mashabiki wa tiketi za mzunguko wanakimbia wengine wanaruka fensi na kuingia uwanjani huku VIP B walitulia kwa sababu wengi walikuwa si vijana lakini matusi na jazba zilitawala na wakati huo mvua inanyesha ambayo ilitulowesha nguo zetu za nje na za ndani.

Mara nikaona geti limefunguliwa/limevunjwa na mashabiki wa VIP B wanakimbia hovyohovyo na kwa kasi kuingia uwanjani,na mimi nikaanza kukimbia kuingia uwanjani kufika juu sehemu ya kuingiza kadi watu walikuwa zaidi ya 500 kwa kukadiria na sehemu(kifaa) ya kuingizia kadi ilikuwa moja hapo ndipo niliponusurika kifo maana nilibanwa karibu na ukuta na nikawa nashindwa kupumua,ikabidi nitumie nguvu kutoka eneo lile,kama ningezembea kidogo tu basi ningedondoka na ningekanyangwa kwa wakati ule hakuna aliyekuwa anamfikiria mwenzake kila mtu alikuwa anataka kuingia sehemu ya kukaa. Na eneo hilo halikuwa na Polisi wala walinzi wengine.

Mimi nilipona lakini kuna mtu aliyefariki na wengine kujeruhiwa lakini nimeamua kuandika haya ili kutoa tahadhari.Na kama mambo yataendelea kama jana siku zijazo tutegemee maafa zaidi.

Ushauri wangu:
1.Maafisa wa Polisi waliokuwepo uwanjani nje(kwenye mageti) hawakuwajibika ipasavyo kwahiyo wawajibishwe.
2.Tiketi zote ziwe zinauzwa, ukitangaza utatoa tiketi bure unakaribisha mafuriko ya watu uwanjani,kama tunataka mashabiki wengi wajaze uwanja tiketi hasa zile za mzunguko ziuzwe hata sh.500 ili kudhibiti watu wengi kuja uwanjani.
3.Kuwe na MC nje ya uwanja atakayekuwa anatoa matangazo mbalimbali.
4.Kuwe na dawati la huduma ya wateja nje ya uwanja.
5.Tiketi zionyeshe namba ya siti shabiki akifika saa 2 asubuhi akae kwenye siti yake na yule atakayefika saa 9 akae kwenye siti yake,kukaa bila mpangilio inasababisha watu kufika kwa muda mmoja uwanjani na kusababisha msongamano.
6.Kama hali haitabadilika usiende na mtoto uwanjani jana kuna watu walienda na watoto na baadhi ya watoto walipotea.

Ndani ya uwanja mambo yalikuwa mazuri pamoja na mvua lakini mashabiki walikuwa wanashangilia muda wote.
Mipira for what?
 
Nina muda mrefu sijaenda uwanja wa Benjamin Mkapa kutazama mechi mbalimbali kwa sababu ya mambo ya hovyo niliyowahi kuyashuhudia siku za nyuma lakini jana niliamua kwenda kwa sababu ni mechi ya fainali ya CAFCC na nilijua mambo yatakuwa ya kiwango cha fainali yaani ubora katika kila eneo.

Ilikuwa mechi kubwa sana ya shindano la mpira wa miguu ambayo tangu nchi hii iumbwe haijawahi kutokea lakini yaliyotokea nje ya uwanja ni aibu kubwa siyo tu kwa Tanzania pia kwa Afrika yote.

Nilikata tiketi ya VIP B tarehe 26 nikitegemea usumbufu utakuwa mdogo hasa ikizingatiwa tiketi za mzunguko zilikuwa nyingi zinatolewa bure, lakini sivyo.Nilifika mapema uwanjani muda wa saa 4 asubuhi nilikuta watu wengi sana nje ya uwanja na kadri muda ulivyokuwa unaenda na watu walikuwa wanaongezeka, pale nje ya uwanja mambo yalikuwa hovyohovyo wanauza vinywaji na chakula wateja wengi lakini vyoo vichache na mpaka ukipate kazi kubwa uifanye, nilisogea kwenye mageti.

Nikakuta yamefungwa na watu wengi wamejazana magetini kibaya zaidi hakuna matangazo ya kuandikwa au ya mdomo kwamba mageti yatafunguliwa saa ngapi au nini kinaendelea Polisi na walinzi wengine walikuwa wengi lakini mashabiki hakuna maelezo tuliyokuwa tunapewa.

Nilienda geti ambalo lipo karibu na geti kuu(mkono wa kushoto kama unauangalia uwanja) nikaambiwa na mtu aliyevaa kizibao(aliyeonekana kama mlinzi) niende geti la kushoto zaidi ambalo linatumiwa na mashabiki wa mzunguko lakini nilivyofika kule nikaambiwa na mashabiki kuwa nirudi nilikotoka kumbuka hakuna mtu rasmi wa kutoa utaratibu.Nilivyofika kwenye geti lililo karibu na geti kuu nikakuta wenzangu wengi waliokata tiketi za VIP B wamejazana watu zaidi ya 400 walikuwa wanasubiri pale lakini geti limefungwa hakuna maelezo Polisi wamejazana wanapiga stori geti kuu, walinzi waliovaa vizibao wanazunguka bila kutoa maelezo na wakitoa hayaeleweki kwa sababu hata wao walikuwa hawajui chochote. Mpaka saa 6 mageti yalikuwa hayajafunguliwa na hakuna maelezo, matusi na fujo zikaanza, Polisi wapo wanangalia lakini hata mtoto wa darasa la tano angekuwepo angejua kitakachotokea muda si mrefu.

Mimi nilianza kukata tamaa ya kuingia uwanjani kwa sababu watu walikuwa wengi sana na walikuwa wanaongezeka kwa kasi na mageti yamefungwa mbaya zaidi hakuna maelezo na wala viongozi wa Yanga,TFF au wa serikali walikuwa hawaonekani.

Muda si muda nikaanza kuona mashabiki wa tiketi za mzunguko wanakimbia wengine wanaruka fensi na kuingia uwanjani huku VIP B walitulia kwa sababu wengi walikuwa si vijana lakini matusi na jazba zilitawala na wakati huo mvua inanyesha ambayo ilitulowesha nguo zetu za nje na za ndani.

Mara nikaona geti limefunguliwa/limevunjwa na mashabiki wa VIP B wanakimbia hovyohovyo na kwa kasi kuingia uwanjani,na mimi nikaanza kukimbia kuingia uwanjani kufika juu sehemu ya kuingiza kadi watu walikuwa zaidi ya 500 kwa kukadiria na sehemu(kifaa) ya kuingizia kadi ilikuwa moja hapo ndipo niliponusurika kifo maana nilibanwa karibu na ukuta na nikawa nashindwa kupumua, ikabidi nitumie nguvu kutoka eneo lile, kama ningezembea kidogo tu basi ningedondoka na ningekanyangwa kwa wakati ule hakuna aliyekuwa anamfikiria mwenzake kila mtu alikuwa anataka kuingia sehemu ya kukaa. Na eneo hilo halikuwa na Polisi wala walinzi wengine.

Mimi nilipona lakini kuna mtu aliyefariki na wengine kujeruhiwa lakini nimeamua kuandika haya ili kutoa tahadhari. Na kama mambo yataendelea kama jana siku zijazo tutegemee maafa zaidi.

Ushauri wangu:
1.Maafisa wa Polisi waliokuwepo uwanjani nje(kwenye mageti) hawakuwajibika ipasavyo kwahiyo wawajibishwe.

2.Tiketi zote ziwe zinauzwa, ukitangaza utatoa tiketi bure unakaribisha mafuriko ya watu uwanjani, kama tunataka mashabiki wengi wajaze uwanja tiketi hasa zile za mzunguko ziuzwe hata sh.v500 ili kudhibiti watu wengi kuja uwanjani.

3. Kuwe na MC nje ya uwanja atakayekuwa anatoa matangazo mbalimbali.

4.Kuwe na dawati la huduma ya wateja nje ya uwanja.

5.Tiketi zionyeshe namba ya siti shabiki akifika saa 2 asubuhi akae kwenye siti yake na yule atakayefika saa 9 akae kwenye siti yake,kukaa bila mpangilio inasababisha watu kufika kwa muda mmoja uwanjani na kusababisha msongamano.

6. Kama hali haitabadilika usiende na mtoto uwanjani jana kuna watu walienda na watoto na baadhi ya watoto walipotea.

Ndani ya uwanja mambo yalikuwa mazuri pamoja na mvua lakini mashabiki walikuwa wanashangilia muda wote.wenxi

Mwenzio toka Stella Abijan atupige 2 bila sababu ya msingi ndipo nilipoacha ushabiki maandazi maana bongo hakuna ustaarabu watu wanabet kuumia tuumie sie
 
Eeeh pole sana aiseh
 
Back
Top Bottom