incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,533
- 4,286
My LIFE MY HISTORY SHORT FILM STORY.
1. 1992-1995 Kwa kipindi hiki nilipendwa sana na Mzazi wangu kila nilipokuwa nikilia alinibembeleza na kuninyamazisha na kunipa vitu vizurii na vya kuvutia ili tu vinipatie faraja na kunifulahisha Mama alinipa maua, pamoja na Majani mazuri ya kuvutia labda alinipa vyote hivi kwasababu hakuwa na uwezo wa kuninunulia Vimagari vya watoto pamoja na Vindege vya kuchezea, hakika kwa kipindi hiki sikuwa najua lolote kuhusiana na maisha wala ndoto za baadae..!
2. 1996-2000, Kwa kipindi hiki nilikuwa mbali na Mikono ya Mama, hapa mama aliniacha nikacheze na watoto wenzangu, na kwa kipindi hiki nilipata malezi ya kaka zangu ambao ndio walionekana kuwa karibu sana na mimi waliniadhibu nikikosea na kuniogesha, nahata siku zingine pia walinisemea kwa Mama pale nilipokuwa nimefanya makosa ya uvujanji wa sheria za kimalezi, Kwa kipindi hiki nilikula peke yangu bila kulishwa na mtu na pia kuna baadhi ya siku zingine kaka waliniogesha na pia kuna baadhi ya siku walinitaka nioge peke yangu, hapo ndio ilikuwa fulaha yangu maana nilikuwa nikiambiwa nioge peke yangu hapo siku hiyo nitajipaka maji nitalala bila kujisugua na kujitonesha makovu ya vidonda nilivyokuwa napata kutokana na michezo ya kitoto ambayo nilikuwa nikiumia kila siku,
Kwa kipindi hiki nilichukia sana kuoga na hapa ndipo akili yangu ilianza kupata ndoto, Ndoto zenye asili ya kitoto, ndoto zenye makusudio ya kitoto,
Kwa hapa nilianza kupata ndoto ya Nikija kuwa mkubwa sitakuja kulazimishwa kuoga tena, wala sitakuja kuwa natoneshwa vidonda vyangu katika mda kuogeshwa nitaishi kivyangu na sitaumizwa tena na kaka waliokuwa wakiniogesha,
Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kuanza kupata ndoto, kwani kwa kipindi hicho adui yangu mkubwa alikuwa maji ya baridi sabuni na dodoki.
3. 2001-2006 Kwa kipindi hichi nilikuwa sipo tena mikononi mwa uangalizi wa kaka na Mama yangu tena, bali nilikuwa chini ya uangalizi wa Walimu wangu ambao walikuwa wakiniimbisha A E I O U
ITAENDELEA......