Simulizi: Mtoto wa Kahaba

Simulizi: Mtoto wa Kahaba

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
403
Reaction score
676
Bagaili ya mambo yote, lengo la mwandishi kuandika kisa hiki anisi siyo kuwapa daawa wasichana makahaba waliyoamua kutumia miili yao kama njia ya kujipatia kipato, la hasha!

Bali ni kueleza kwa jinsi gani baadhi ya wasichana hao wamejikuta 'wakijiuza' kutokana na mazingira ya au kukua kwao ama magumu waliyokutana nayo.

Mkasa utaonesha jinsi baadhi ya mahuluku wanavyojikuta wakiishi maisha yasiyokuwa ndoto zao ili mradi wapate pesa na mambo mengine yasonge mbele.

DIBAJI/ UTANGULIZI

Rehema Nyati ni mzaliwa wa Kijiji cha Abwelili, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Mkoa huu upo Kusini mwa nchi ya Tanzania. Umepakana na nchi ya Msumbiji kwa upande wa Kusini kwa kutenganishwa na Mto Ruvuma.
Ni miaka thelathini na tisa iliyopita ambapo mama yake mzazi Rehema, Bi. Msumuka anashikwa na ugonjwa usiyojulikana.
Anashikwa kisawasawa na tumbo la kukata au kusokota mpaka analia kama mtoto mdogo.
Rehema anamfuata mama mmoja jirani yao na kumhabarisha kuhusu hali ya mama yake.
Jirani huyo baada ya kufika na kuiona hali ya mama Rehema, anamtuma binti huyo kwenda kumwita mzee mmoja wa kijijini hapo.
Rehema akiwa njiani kwenda kwa mzee huyo, anatokea kijana mmoja na kumbaka.
Baada ya kumaliza uovu huo, kijana huyo anakimbia akimwacha Rehema na maumivu makali kwa sababu mbali na kumbaka pia anamtoa usichana wake (anambikiri), anamwambukiza gonjwa la zinaa na kumpa ujauzito.
Rehema anatembea kwa kujivuta kwa sababu ya maumivu makali huku akilia hadi kwa mzee huyo.
Anampa taarifa za ugonjwa wa mama yake. Lakini hasemi analia kwa sababu ya kubakwa.
Mzee huyo anatoka na Rehema akiwa ametangulia mbele huku anamwambia asilie, mama yake atakuwa sawa.
Hali ya mama yake haina ahueni. Mwishowe anafariki dunia na kumwacha Rehema akiwa na miaka kumi na tisa tu.
Baba yake na kaka yake walifariki dunia miaka miwili nyuma.
Kwa hiyo baada ya kifo cha mama yake, Rehema hana baba, hana mama. Hana kaka wala mdogo wake.
Hivyo, anaamua kuondoka kijijini kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kufanya kazi za ndani, za kusaidia mama lishe au kuuza matunda mitaani...
TWENDE SOTE....

"REHEMA mwanangu, mimi naumwa. Naumwa sana mwanangu," mama Rehema alilalamika huku akiacha kula na kubaki ameshika tonge. Kisha likadondoka.
"Mama unaumwa nini? Mbona ghafla?" Rehema alishtushwa na hali ya mama yake.
"Tumbo mwanangu...ooh! Sujui tumbo hili ni la vipi!" alilalama mama Rehema.
Rehema: "Kwani linaumaje mama?"
"Linakata mwanangu. Tumboni kama kuna viwembe na sindano. Kuna viwembe na sindano Rehema."
"Basi lala kwenye busati mama. Mimi nakwenda kumwita mama Lydia."
Rehema alitoka mbio mpaka kwa mama Lydia.
"Mama Lydia, twende nyumbani, mama anaumwa sana. Twende nakuomba."
"Anaumwa nini huyo nyoko?" Alihoji mama Lydia.
"Tumbo mama Lydia."
"Hilo tumbo limemuanza saa ngapi? Mbona muda wa saa moja nilimuoma akitoka dukani kwa mzee Komba?" Alihoji mama Lydia huku akishika kanga na kuitupia begani juu ya gauni.
"Limemuanza sasa hivi tu. Tulikuwa tunakula. Ghafla akaacha na kujishika tumbo. Baadaye alianza kulia akisema linamkata kama ndani kuna viwembe na sindano," alijibu Rehema akitembea kwa haraka kuiga hatua za mama Lydia ambaye alishika kasi.
"Leo alikwenda kibaruani kwake?" Aliuliza mama Lydia kwa sauti iliyoonesha mshangao kwa taarifa za ugonjwa wa mwanamke huyo ambaye ni jirani yake mkubwa na ni marafiki.
"Ndiyo. Lakini aliporudi aliniambia wakati wako njiani na mama Maria wanarudi, yeye alitumbukia kwenye shimo mahali ambapo kila siku wanapita hakuna shimo," alisema Rehema.
"Hee! Kweli? Ni nini hili jamani?!" Alishangaa mama Lydia.
Walimkuta mama Rehema amekata kauli. Haongei. Ametoa macho tu.
"Mama Rehema! Mama Rehema...," aliita mama Lydia huku akimgusa. Lakini mama Rehema hakuitika.
"Mama Rehema. Kwani vipi? Eti nini kimetokea?" Aliuliza mama Lydia. Lakini hakupata majibu yoyote.
"Eti ulitumbukia ndani ya shimo wapi?" Aliuliza tena mama Lydia.
Kwa mbali, mama Rehema aliachia tabasamu kama mtu aliyefurahishwa na swali hilo kisha akafumba macho na kuacha kutabasamu.
"Rehema hapa tumpate mtu shaibu. Kimbia kamwite mzee Tiambai halafu nenda kamwite na mama Maria. Waambie waje haraka sana," mama Lydia alimwagiza Rehema ambaye alitoka mbio huku machozi yakimlengalenga.
Njiani aliwaza nini kitatokea endapo ugonjwa wa mama yake utachukua uhai wake?

********

Miaka miwili iliyopita, aliwapoteza watu wawili katika familia yao. Aliwapoteza baba yake na kaka yake kwa kuzama bwawani wakati wakivua samaki. Lilikuwa pigo kubwa katika familia.
Mwaka uliyofuata alimpoteza mdogo wake wa kike, Martha kwa ugonjwa wa U.T.I Sugu.
Hajawahi kuwaona mababu wala mabibi. Hamjui shangazi, achilia mbali kaka wa mama yake ambaye ni mjomba wake.
Alipomaliza darasa la saba, hakufanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa sababu ya kipato duni cha familia yake.
Enzi hizo hakukuwa na 'Elimu Bure' kama ilivyo sasa.
Kazi kubwa ya mama yake ilikuwa kulima vibarua kwenye mashamba ya Kahawa yaliyokuwa yakimilikiwa na makabaila, watu wenye uwezo au wawekezaji na kulipwa kwa siku. Pesa ambazo hazikutosha kuweka akiba hata ya shilingi mia tano kwa siku.
Ilipotokea mama yake anaumwa, basi siku hiyo hakukuwa na matumaini ya kula. Labda pale ilipotokea jirani yake mama Lydia 'amepewa maono' na Mungu wake, akawapa unga wa dona kwa ajili ya kukoroga uji.

***********
"Mungu wangu naomba sana umsaidie mama yangu apone. Asife," alisema moyoni Rehema wakati akibisha hodi nyumbani kwa mama Maria.
"Shikamoo mama Maria," alisalimia huku uso wake ukionesha kila kilichopo nyumbani kwao au alikotoka.
"We Rehema kuna nini?" Aliuliza mama Maria bila kuitikia shikamoo yake.
"Mama anaumwa sana. Hadi anashindwa kuongea."
"Anaumwa nini?"
"Anasema tumboni mwake kuna vitu kama viwembe vinamkatakata."
"Hee! Makubwa! Yuko wapi sasa?"
"Nyumbani. Mama Lydia ndiyo kanituma nije kukuita."
Mama Maria alishtuka kusikia mama Lydia yuko nyumbani kwa mama Rehema kwa sababu ya kuumwa na alimtuma binti yake aende akamwite. Alijua hali ni mbaya kweli! Haraka sana, alijitupia upande wa kanga kwenye bega moja na kutoka mbio.

********************************

Baada ya kutoka kwa mama Maria, Rehema alikimbia kwenda kwa mzee Tiambai.
Akiwa anakaribia kufika, alipita kwenye eneo ambalo halina nyumba na ilikuwa usiku. Ghafla alitokea kijana mmoja na kumpiga ngwara. Akaanguka!
Awali Rehema aliamini ngwara ile ilikuwa ni jaribio la tukio la uporaji. Lakini sekunde kadhaa aligundua ngwara ilihusiana na tendo la kubakwa.
Licha ya jitihada za kutaka kupiga kelele ili kuwaita wananchi wafike kumnusuru na ubakaji ule, lakini alishindwa kwa kijana kumthibiti kinywa kwa kukiziba na kiganja.
Yule kijana alimwingilia Rehema kwa nguvu na baada ya kumaliza hitaji lake haramu alikimbia.
Haikuwa rahisi kumtambua mbakaji kwa sababu alijifunga kitambaa kichwani na kuvaa miwani ya giza. Aidha, ilikuwa usiku.
Rehema alitembea kwa kujivuta akiugulia maumivu makali huku akitokwa damu hadi kwa mzee Tiambai. Alikuwa akilia kwa uchungu. Alimpa taarifa za ugonjwa wa mama yake.
Lakini hakusema kama analia kwa sababu ya kubakwa na mtu asiyemjua.
Mzee Tiambai alitoka naye akiwa ametangulia mbele huku akimwambia:
"Usilie mjukuu wangu. Nyoko atapona tu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu."
Mzee huyo hakujua kwamba, kauli yake haikuwa na uhusiano wowote na kilio cha Rehema.
Walipofika nyumbani, Rehema alipitiliza hadi chumbani kwake na kujifuta damu na gauni lake lililochakaa kisha akatoka kufuatilia hatima ya mama yake. Huku akijikaza kwa maumivu makali.
Mzee Tiambai alikuta maelezo ya mama Lydia ni yale yale aliyopewa na Rehema huku mama Maria akieleza kilichotokea wakati wanatoka kibaruani kurudi nyumbani.
"...kwa kweli hata mimi nilipigwa butwaa. Tena sana. Barabara ambayo baiskeli, pikipiki, watu tunapita kila siku, miaka yote. Hakuna cha shimo wala korongo...
"Lakini leo ghafla mwenzangu mama Rehema alitumbukia na kuzama kwenye lile shimo mpaka akawa haonekani! Haya ni maajabu ya mwaka...
"Ilibidi nimrushie kamba niliyokuwa nayo, akaishika. Nilijitahidi kumvuta hadi akatoka juu. Lakini alisema anajisikia kuishiwa nguvu...
"Cha ajabu sasa, aliniambia kule ndani ya shimo eti alimkuta mzee Satara..."
"Yule anayeuza kuni pale kwenye mikanju?" Alihoji kwa haraka mzee Tiambai.
"Ndiyo. Lakini mimi nilipochungulia, sikumwona yule mzee," alisema mama Maria kwa sauti iliyojaa mshangao.
Akaendelea...
"Basi, nilimwambia ajipe moyo mkuu. Ajikaze, tutembee polepole. Ndiyo tukafika hapa kijijini. Lakini alikuwa ameshachangamka na akaniambia anajisikia vizuri," alimaliza kusema mama Maria.
"Rehema hebu kimbia dukani kamnunulie mama vidonge vya kupunguza maumivu halafu mimi niende nikamchukue kijana wa mzee Komba. Yeye ana baiskeli atatusaidia kumkimbiza hospitali," alisema mzee Tiambai wakati akimpa Rehema shilingi mia mbili za dawa.
Mzee Tiambai na Rehema, walitoka sanjari. Rehema alitangulia kwa kukimbia. Lakini kabla mzee Tiambai hajafika mbali aliitwa...
"Mzee Tiambai, rudi...rudi mara moja," mama Maria ndiye aliyetoka akamwambia mzee huyo kisha yeye akarejea ndani.
Mzee Tiambai alirudi ndani kwa haraka na hofu kubwa...
"Kuna nini tena mama Maria? Eti, mama Lydia, kuna nini?" Aliuliza.
"Hebu mwangalie vizuri mama Rehema, tunaona kama amekuwa wa baridi halafu kama...," alisema mama Maria bila kumalizia.
Mzee Tiambai alimwinamia mama Rehema, akatega sikio kwenye kifua upande wa kushoto kisha akamshika kichwa.
Aliwaangalia mama Lydia na mama Maria halafu akamrudia mama Rehema. Akaushika mkono wake mmoja na kuuachia, ukafika chini kama kipande cha mti kinavyoaguka baada ya kutupwa.
Aligeuka na kuwaangalia tena wote. Akasema:
"Jamani! Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe."
Mama Lydia na mama Maria waliangua kilio cha ghafla wakati mzee Tiambai akimfumba macho mama Rehema ili kumsitiri.
Palepale nyumba ya mama Rehema ilijaa simanzi na sauti za vilio. Mama Rehema alifariki dunia ghafla.

************************
Akiwa amebakiza hatua chache kufika nyumbani, Rehema alitupa kikaratasi chenye dawa baada ya kusikia vilio ambavyo vilipokelewa na baadhi ya majirani walioonekana wakiingia nyumbani kwao. Alijua mama yake ameaga dunia!
"Mamaaa...mamaaa...mama umeniacha. Umeniacha na nani mimi mwanao mama? Mbona hukuniambia sasa! Itakuaje we mama Rehema?
"Umeniacha mama. Nitaishi na nani mimi? Mbona hukusema mama? Itakuaje jamani mama? Mama amka. Simama mama," Rehema alilia sana huku akitengeneza mithali.
Rehema alitia huruma kwa kilio chake na maneno aliyokuwa akiyatamka! Alianguka. Watu walimbeba na kumwingiza ndani, chumbani kwake. Wanawake wawili walibaki naye kumfariji.
Msiba ulitawaliwa na huzuni. Na maswali mengi yalikuwa juu ya hatima ya Rehema.
Mtoto aliyefiwa na baba na kaka miaka miwili nyuma. Alifiwa na mdogo wake, mwaka mmoja uliyopita. Na sasa yu pekee baada ya kumpoteza mama mzazi, tena ghafla.
Habari zilisambaa haraka kijijini kote kwamba, mama Rehema au mke wa marehemu mzee Nyati amefariki dunia ghafla.
Wengi walitengeneza maswali kama vile; aliumwa nini? Wengine walisema; mbona tulimwona jioni ya leo akirudi kutoka kibaruani.
Wapo walioamini kwamba, mama Rehema alipigwa 'dongoloji' na mzee Satara ambaye kijiji kizima kilimwogopa kwa ulozi ingawa hakukuwa na ushahidi kama kweli mzee huyo alikuwa mlozi.
Dhana hiyo ya kuhusika na kifo cha mama Rehema 'ilijaziwa nyama' na kitendo cha mzee huyo kutoonekana kwenye msiba wala maziko ya marehemu mama Rehema.
Lakini wengine walimtetea kwa kusema kwamba, mzee Satara alikuwa anaumwa kabla ya msiba.

2. MKASA WA MAISHA NYUMBANI KWA MAMA MCHA MUNGU, KUFUKUZWA USIKU

Itaendelea.
 
DONDOO

Kwa anayetaka full unatuma Sh. 1500 tu kwa Namba 0785 990097.
Inaendelea....

MKASA WA MAISHA NYUMBANI KWA MAMA MCHA MUNGU, KUFUKUZWA USIKU

Siku ya tatu ya msiba, mama Lydia alitangaza kumchukua yatima Rehema kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Waombolezaji wengi walimpongeza kwa uamuzi huo.
Hasa walipozingatia ni mwanamke aliyesifika kwa kumjua Mungu. Hata utambulisho wake katika kijiji kile ilikuwa 'kwa mama mcha Mungu.'
Lakini mama Lydia hakujua afanye nini kwa ajili ya maisha ya baadaye ya yatima huyo. Kila alichofikiria kukifanya, kilikuwa na giza nene.
Ni binti aliyejua kusoma na kuandika tu. Hakuwa na ujuzi wowote kichwani.

**************************

Baada ya mwezi mmoja, Rehema ambaye hakuwahi kumwambia mtu kuhusu ubakwaji aliyotendewa usiku wa kifo cha mama yake, alifika kwenye mabadiliko ya mwili.
Alianza kutapika! Kuhisi kizunguzungu na kutopenda kula huku midomo yake ikimkauka hata pale alipoisiliba na mafuta ya mgando.
Kwa kutojitambua kwa sababu ya kukosa elimu ya mwili wake, yeye aliamini ananyemelewa na homa za msimu au pengine ni kutokana na mawazo ya kufiwa na mama yake mzazi.
Usiku mmoja yeye na mama Lydia wakiwa wanakula, alishikwa na kichefuchefu cha ghafla. Alikimbilia nje ili kutapika. Tendo hilo lilimsimamisha pia mama Lydia.
Alimfuata hadi nje na kusimama nyuma yake akimfuatilia anachokifanya. Akamuuliza: "Nini kimekusibu Rehema?!"
"Mimi sijui mama Lydia. Labda homa," alijibu Rehema huku kinywa chake kikiangalia ardhi na kukitoa chakula chote alichokuwa ameanza kukiingiza tumboni.
"Hujui? Hujui kwa maana hujui au hujui kwa sababu hutaki mimi nijue?" Aliuliza kwa ukali mama Lydia.
Rehema: "Mimi sijui kwa nini natapika mama Lydia. Nimesema labda nina homa."
"Si una mimba wewe Rehema!" Alisema mama Lydia bila kurekebisha uzungumzaji wake. Kauli yake hiyo ilionesha ana uhakika na alichokizungumza.
Kwa hiyo hakuwa tayari kupingwa na mtoto mdogo kama Rehema.
Pia kauli hiyo iliupiga mtima wa binti huyo ambaye aligeuka na kumwangalia mama Lydia huku uso wake ukishangaa kwa alichokisikia. Eti ana mimba!
"Mimba mimi niitoe wapi mama Lydia? Mbona bado mdogo," alisema Rehema akipingana na madai ya mama Lydia ambaye ni mfadhili wake.
"Tangu juzi nilitaka kukuuliza. Kwa sababu nakuona uso wako siku hizi umesinyaa kama unashinda juani. Midomo inakukauka kama unapaka majivu. Wewe Rehema una mimba. Hebu njoo ndani nikuulize vizuri."
Mama Lydia alitangulia kurudi ndani. Rehema alimfuata nyuma hadi sebuleni na kukaa ili kuulizwa vizuri.
"Rehema. Hiyo mimba ni ya nani? Naomba uniambie ukweli," aliuliza mama Lydia kwa sauti isiyotaka utani na watoto.
"Mimi sijui kama nina mimba mama Lydia. Kwanza mimi sina mvulana. Huo ujauzito nitakuwa nimepewa na nani jamani?" alijibu Rehema kwa sauti iliyojaa hisia za kuonewa.
"Rehema usinitanie nakwambia. Tena narudia kusema usinitanie kabisa. Tangu lini mwanamke akawa hajui kama ana mimba wakati anayo?
"Nimekuwa nikikuona unavyopuyanga. Mara kwa mzee Chakumega. Mara wapi sijui! Nilikuwa sitaki tu.
"Lakini leo ndiyo kila kitu kimekuwa hadharani. Faida za kufanya umalaya umeziona sasa. Ulifanya mambo yako kwa siri sasa umeumbuka hadharani. Ama kweli mficha maradhi kitambaa cha sanda kitamuumbua."
Rehema: "Hapana mama, mimi 'nikitokaga' hapa nyumbani 'namfuataga' rafiki yangu Paskalina. Yule mtoto wa mzee Chakumega, basi. 'Siendagi" kokote kwingine."
Rehema aliamini anajitetea. Lakini kumbe alijipalia makaa.
"Sasa nisikilize mimi Rehema. Mimi sitaki mambo mengi. Msimamo wangu ni mmoja tu. Jitwike kila kinachokuhusu uondoke hapa kwangu. Sasa hivi tena. Mpelekee mimba huyo aliyekupa," mama Lydia aliyabwaga ya moyoni mwake bila simile.
Rehema aliangua kilio na kuomboleza huku akipiga magoti mbele ya mwanamke huyo akiweka wazi kwamba hajui pa kwenda.
"Mama mimi sina mimba jamani. Anipe nani wakati sina mvulana? "Unaponiambia niondoke hapa kwako nitakwenda kuishi wapi wakati unajua mama yangu ambaye alikuwa rafiki yako, alifariki dunia!" Alisema Rehema huku akiendelea kumwaga machozi.
Kwa kweli alitia huruma sana.
Hata hivyo, mama Lydia alimfokea akimtaka kuacha mara moja kusema uongo tena akamkumbusha kwamba kusema uongo ni dhambi kwenye Amri Kumi za Mungu.
"Mungu alisemaje kupitia Torati? Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga. Wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni. Wala kilicho chini dunian. Wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia.
Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wako.
Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba.
Kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba yako na mama yako.
Siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana Mungu wako. Usiue. Usizini. Usiibe.
Usimshuhudie jirani yako uongo.
"Sasa wewe Rehema unanishuhudia uongo mimi."
Pia, mama Lydia akajigamba kwa kusema kwamba yeye ndiye aliyeanza kuliona jua kabla yake Rehema.
"Mimi watoto wangu wote watano hakuna ambaye mimba yake nilikwenda kupima hospitali ili kujua kama ninayo au sina! Nilikuwa najua kutokana na hali yangu ya mwili na hesabu.
"Wewe hujui hesabu wala hali ya mwili mwako. Hata ng'ombe anakushinda. Ondoka nyumbani kwangu haraka. Isije ikaonekana mimba ulipatia kwangu," alisema mama Lydia kwa sauti iliyojaa hasira.
Rehema alibeba mfuko wake wa nguo, akaondoka asijue anakokwenda kupiga kambi...

Itaendelea.

MANENO MAGUMU

anisi-kufurahisha, kupendeza.
bagaili- licha ya.
butwaa-mshangao.
busati-aina ya mkeka.
chojoa-vua nguo.
daawa-mashitaka.
dunduliza-weka kidogo kidogo (akiba).
gugumia-meza mate kwa nguvu.
lindi-zama katika mawazo.
kwalo-kwa hilo.
kwacho-kwa hicho.
kwayo-kwa hiyo.
kibwebwe-fanya kazi kwa bidii.
machopima-kumkazia macho mtu.
mahuluku-binadamu, mtu.
maulana-jina moja wapo la Mwenyezi Mungu.
mikanju-miti ya mikorosho, mbibo.
mtima- moyo.
mtawa-sista wa kikatoliki. msalani-chooni.
nachelea- nina wasiwasi.
nyanyapaa-tenga, bagua. nyerezi-mwanamke mwenye sura nzuri.
nyoko-mama yako.
ngwara-mtama.
punde-si kitambo, muda huohuo.
sanjari- sambamba.
simile-subira.
shaibu-mwanaume mzee. seuze-sembuse.
sibu-patwa na jambo.
suria-kimada.
ua-sehemu ya nyuma ya nyumba.
uhasama-uadui.
ulozi-uchawi.
 
Back
Top Bottom