Simulizi: Mtoto wa ajabu

MTOTO WA MAAJABU: 14

Kwenye mida ya saa tano usiku, Juma alienda na ile dawa hadi mlangoni, kisha akanuiza maneno yake na kutaka kuinyunyizia ila alishangaa kushikwa mguuni, alishtuka sana na kuangalia ni nani kamshika! Alishangaa kuona ni mtoto wao ndio kamshika.
Kwakweli Juma alijikuta akiogopa sana hata akajikuta anashindwa cha kuongea chochote kile na kuita,
“Anna, Anna”
Anna akatoka nje na kwenda hadi pale ambapo Juma akamwambia Anna,
“Mbona umemuachia mtoto atembee usiku huu?”
“Hata sikujua shemeji, halafu kumbe sikufunga mlango wa chumbani kwetu. Samahani shemeji”
Anna akainama na kumbeba mtoto yule halafu kwenda nae chumbani, kwakweli Juma alishindwa kuendelea na chochote pale kwa wakati ule zaidi ya kurudi chumbani ambapo alimkuta mkewe amekaa halafu kachukia sana na kuanza kumfokea Juma,
“Ulienda kufanya nini muda huu huko nje wakati tumelala?”
“Sikuwa nje mke wangu, nilienda jikoni kunywa maji”
“Muongo wewe, toka lini ukanywa maji usiku? Hata hiyo si ulinunua maji wewe na kuweka humu chumbani, umeshindwa nini kuchukua hayo na kuyanywa?”
Hapo Juma alikaa kimya na kumfanya Mariam aendelee kuongea,
“Hebu sema ukweli kama una mwanamke huko au ni itu gani maana haiwezekani kabisa kwa kitu unachokisema”
Juma huwa hapendi marumbano na mkewe wake, hivyobasi akamuomba kwa muda huo waweze kulala tu,
“Naomba tulale Mariam, hata hivyo nimechoka sana”
Mariam akamuangalia mumewe na muda huu hakusema neno zaidi zaidi na yeye kujilaza tu pale kitandani.

Leo kulipokucha tu, Juma alijiandaa na kuondoka zake yani leo hata chai hakunywa sababu akili yake ilikuwa ikiwaza mambo mengi sana kwa wakati mmoja haswa swala la mke wake na Anna, ni mambo ambayo yalimtatiza sana.
Mariam alipoamka leo alienda kama kawaida sebleni kunywa chai huku akilalamika kuchoka sana, basi Anna alimwambia waongee kidogo akimaliza kunywa chai na kweli alipomaliza waliweza kuongea sasa,
“Dada, si unalalamika kila siku kuchoka?”
“Ndio nachoka sana, hata sijui nifanyeje kwakweli”
“Dada, unaonaje tukiwa tunasaidiana na mimi kazi”
“Sasa ndio sitochoka?”
“Ndio dada maana utakuwa unaushughulisha mwili wako”
“Hapana hapo nitachoka zaidi, jamani mimi kufanya kazi za ndani siwezi, huwa naona uvivu sana Anna. Wewe endelea tu kwakweli maana mimi siwezi kabisa kufanya hiyo kazi”
Anna alishindwa jinsi ya kuendelea kumshawishi kwahiyo alimuacha vile vile aendelee kulala na kuchoka.

Juma leo hakukaa sana kwenye shughuli zake kwani moja kwa moja alienda kwao kuzungumza na mama yake maana yale mambo yalimtatiza sana.
Alimkuta mama yake pale na kumsalimia kisha kuzungumza nae,
“Mama sikiliza, hali ya mke wangu kuamka na kusema kuwa kachoka sana kwakweli mimi binafsi hainiridhishi kabisa, ni wazi yule binti anamtesa mke wangu sana ndiomana mke wangu anachoka sana”
Mama yake alimuangalia na kumwambia,
“Pole, sasa nikusaidiaje?”
“Sasa mama nimetumia kila njia ili kumkamata yule binti lakini imeshindikana”
“Mfano njia gani uliyotumia?”
Juma alimueleza mama yake jinsi alivyoenda kwa mganga na jinsi mganga alivyompa dawa na vile ilivyokuwa usiku, mama yake alishangaa sana na kuuliza,
“Kwani mwanao anatembea?”
“Ndio anatembea mama”
“Kheeee makubwa hayo, yule mtoto anatembea jamani? Katambaa lini sasa?”
“Hata mimi sijawahi kumuona akitambaa ila tu nilimuona akitembea, inasemekana ni chakula anachokula”
“Mnampa chakula gani siku hizi zaidi ya yale maziwa mliyokuwa mkiyatengeneza kiajabu?”
“Siku hizi anakula chakula tunachokula sisi, amekua yule mtoto inasemekana alikua toka tumboni”
“Mmmmh siwezi kubisha sana, ingawa mimi ni mtu mzima ila sijawahi kushuhudia mtoto wa hivi, huenda kuna ukweli. Ila hapo usiku ndio sijaelewa, alikuwa anafanya nini sasa hadi kakushika mguu?”
“Hata sielewi, Anna alisema kuwa alisahau kufunga mlango ndio mtoto katoka chumbani kwake”
Kidogo huyu mama akashangaa na kuuliza,
“Inamaana siku hizi mtoto analala na Anna?”
“Ndio mama, analala na Anna”
Huyu mama akapumua kidogo na kusema,
“Kheeee ila Juma kweli mke wako ni mvivu, hadi kulala na mwanae anaona uvivu loh!! Haya tuachane na hayo, ila mimi kuna hisia mbaya napata kwa mtoto wenu”
“Hisia gani mama?”
“Nahisi mtoto wenu ni mchawi pia”
Hapa Juma alipinga vikali na hakutaka kumuelewa kabisa mama yake, yani kuita mtoto wao ni mchawi? Kwakweli alichukia Juma na muda ule ule akaamua kumuaga mama yake ila mama yake akamwambia,
“Usichukie Juma mwanangu, sikuwa na nia mbaya kukwambia hivyo. Ila kwa ushauri wangu, nenda kaongee na mke wako ili mumfukuze huyo Anna anayewasumbua kwenye nyumba yenu”
Juma alimuitikia tu na kuondoka zake maana alishachukia kabisa.

Wakati Anna amekaa mchana huu akila na Mariam, alianza kuongea nae kuhusu mumewe Juma,
“Dada, hujawahi kupata matatizo yoyote ya shemeji kuwataka wadada wa kazi!”
Mariam akashtuka sana na kusema,
“Hapana, namuamini sana mume wangu”
“Ni vizuri kumuamini ila wadada wengine wa kazi sio waaminifu kabisa, unaweza shangaa kumbe anatoka na mume wako”
“Nashukuru Mungu sijapata wadada wa hivyo kabisa, sema hata hivyo huwa sidumu na msichana wa kazi, wewe Anna umekuwa wa pekee sana kwangu kwakweli hadi nahitaji kuishi nawe hapa kwa maisha yote”
“Asante dada, unajua kwanini nimekuuliza hivyo?”
“Eeeeh kwanini?”
“Kuna nyumba moja hivi kulikuwa na mdada wa kazi, basi baba mwenye nyumba kila siku akawa anasema huyu mdada anaondoke, simtaki kumbe yule baba kamtaka yule mdada ila mdada kamkataa sababu ana msimamo, basi wenye nyumba wakahisi mdada wa kazi ni mbaya wakaamua kumfukuza. Kisha yule baba akamleta hawara yake kama mdada wa kazi”
“Khaaa jamani, ila wanaume wana mambo ya ajabu”
“Tena sana dada yangu”
“Ila Anna nina usingizi hapa balaa, nasubiri kidogo tu chakula kishuke shuke nikalale”
“Sawa dada”
na kweli alikaa baada ya muda mfupi tu alilala.

Usiku wa leo, Juma alikuwa na mawazo yake ambayo kayapanga toka mchana alipotoka nyumbani kwao kwahiyo walipoenda kulala na Mariam aliamua kuongea nae kwanza,
“Mke wangu Mariam, kuna jambo nahitaji tufanye kwenye nyumba yetu”
“Jambo gani hilo?”
“Nahitaji tumfukuze Anna humu ndani, kusiwe na mfanyakazi kama yeye, kama msaidizi tutatafuta mwingine”
“Kwanini umeamua hivyo?”
“Mke wangu huyu Anna simuelewi”
“Humuelewi kivipi?”
“Yupo kama mchawi jamani!”
“Khaaaa mchawi mwenyewe na huo umalaya wako ulioanza kuufikiria, unafikiri hayo mawazo yako sijayapata? Yani unachopanga wewe ujue kwangu kimeshafikiriwa muda sana, kwahiyo wewe unataka kumfukuza Anna hapa ili ulete hawara yako aje kunisaidia kazi! Hapana hilo halikubaliki”
“Kheee Mariam umekuwaje? Kumbuka ni wewe ndiye uliyekuwa unasema kuwa siwezi kukusaliti”
“Nilisema ndio ila wanaume hamuaminiki kabisa”
“Imekuwaje nisiaminike tena? Ni kipi kimebadilika kwangu Mariam? Mimi ni Juma yule yule wa siku zote, nimebadilika nini sasa?”
Mariam hakumjibu mumewe bali alijigeuza na kulala huku akilalamika kuwa amechoka kama kawaida yake.

Kulipokucha tu Juma alijiandaa vizuri kabisa na hata kunywa chai hakunywa wala nini kwani moja kwa moja alienda tena kwa yule mganga wake kwani alihisi kuwa huenda safari hii akamsaidia.
Basi alivyofika na kuingia, yule mgaga akacheka na kumwambia Juma,
“Nilijua tu itashindikana maana pale kwako pamekuwa pazito sana”
“Sasa nifanyeje babu?”
“Weka kwanza salamu ya wazee”
Basi Juma aliweka pesa na kuendelea kumsikiliza yule babu tu.
Basi babu alitoa dawa ambayo ilikuwa kama maji halafu akamwambia Juma,
“Hii dawa, nenda kaweke kwenye jagi la maji ya kunywa, weka yote halafu acha mkeo na huyo mdada wa kazi wanywe, halafu utapata jibu ya hiko unachotaka kufahamu. Najua hii utafanikiwa”
“Nitafanikiw ababu, naona kabisa nitafanukiwa, asante sana babu”
Juma alimshukuru sana na kuondoka zake, yani hakutaka hata kwenda tena kwenye shughuli zake kwani kwa muda huo moja kwa moja alirudi nyumbani kwake kwani yeye alikuwa na hamu sana ya mkewe kugundua kuwa Anna ni mchawi, alitamani sana mkewe ajue kuwa anachoka kwaajili ya Anna.

Juma alifika kwake na kukuta ndio Anna anaandaa chakula mzani, wakati huo Mariam amekaa kwenye kochi tu yani Juma aliona ndio wakati sahihi kabisa ule.
Basi alienda jikoni na kuchukua jagi la maji na kujaza, kisha akaweka ile dawa yote na kupeleka mezani huku akisema,
“Anna umeandaa chakula bila hata kuweka maji!”
“Ningeweka shemeji, ila nilienda kwanza kuchukua maji ya kunawa, ila umenisaidia shemeji asante”
Juma alitabasamu tu, basi Anna alimfata Mariam na kumwambia,
“Dada jamani yani umekaa tu wakati mumeo ndio yupo kuandaa maji ya kunywa, hukumuona dada?”
“Aaaah Anna, haya maisha ya mimi na mume wangu yaache tu kama yalivyo, kwani hajui kama mimi nachoka sana? Anajua vizuri, asikuumize kichwa”
Basi sasa Mariam alisogea mezani na kumsalimia mumewe ambapo Juma alimwambia Mariam,
“Mke wangu si unywe maji kwanza halafu ndio ule!!”
“Weeee mambo ya wapi hayo? Ninywe maji kwanza halafu nishibe maji tu niache kula chakula! Mimi nakula kwanza halafu maji badae”
Juma akamuangalia Anna na kumwambia pia,
“Na wewe Anna si unywe maji kwanza ndio ule chakula!”
“Na mimi kama dada, hata sijazoea kunywa maji kabla ya chakula shemeji”
Basi wote wakapakua kile chakula na kuanza kula, yani Juma alikuwa anatamani sana wanywe maji maana pale wakinywa maji tu ndio kila kitu kitagundulika.
Wakiwa wanaendelea kula, mara waliona tu lile jagi likisukumwa na kuangushwa chini ambapo lilimwaga maji yote, hapo Mariam alishangaa,
“Khaaaa jamani, wewe mtoto kuanza kutembea ndio unapanda hadi mezani, sasa kutupa jagi ndio nini?”
Juma aliangalia na kusikitika sana, hadi alijikuta akikosa hamu ya kula kabisa kwani hakuongea kitu zaidi ya kuacha kula na kuondoka zake.
Anna alimuangalia na kumuuliza Mariam,
“Dada, mbona shemeji ameacha chakula?”
“Sijui, labda ameshiba”
“kamuulize dada?”
“Huwa sina muda huo, mtu mzima halazimishwi kula. Akiwa na njaa atakuja mwenyewe kula, yani mimi niache kushiba nianze kuulizana na watu kwanini umeacha chakula, kama amekula huko alipokuwa nitajuaje?”
“Labda kachukia mtoto kuangusha jagi dada?”
“Yani kuangusha jagi tu ndio achukie, lingekuwa limevunjika je si angejinyonga kabisa? Aniondolee balaa mie”
Kisha Anna alienda kuleta maji mengine ambapo walikula na kumaliza pale na walikuwa wameshiba kabisa.

Juma hakutoka tena chumbani, alijikuta akitafakari sana bila ya jibu lolote yani alikuwa kama haamini chochote kile ambacho kinatokea katika ile familia yao.
Muda huu Mariam alienda chumbani na kumkuta mumewe kajiinamia tu na mawazo akamuuliza,
“Wewe vipi una matatizo gani?”
“Kwakweli Mariam, naomba tumfukuze Anna, mimi siwezi kuishi na Anna humu ndani”
“Sababu kubwa ya kumfukuza Anna ni nini?”
“Anna ni mchawi mke wangu, yule binti ni mchawi kabisa nakwambia”
“Hivi Juma uchawi unaujua wewe? Ukiambiwa toa ushahidi kwa hoja yako kuwa Anna ni mchawi utatoa ushahidi gani?”
“Sina haja ya ushahidi ila Anna ni mchawi, tena ni mchawi sana, nataka aondoke kwenye nyumba yangu”
“Sikia nikwambie Juma, siku ya kuondoka Anna hapa ujue ni siku hiyo hiyo na mimi nitaondoka, siwezi kuangalia ukitaka kumnyanyasa mtu asiyekuwa na hatia sababu tu ya mawazo na hisia zako, muache Anna Kama alivyo”
Kwakweli Juma alichukia sana hata hakujua imekuwaje hadi akili za mke wake kutekwa kiasi kile na Anna.

Siku ya leo ndio Juma alienda tena kwenye shughuli zake ila alikuwa na hasira sana kiasi kwamba alikuwa akitembea huku akiongea peke yake maana alikuwa amejaza hasira kubwa sana kwenye moyo wake.
Basi Juma alifanya shughuli zake huku akiwa na mawazo sana kwa siku ya leo, alipomaliza akaondoka ila njiani alikutana na yule binti ambaye huwa wanakutana mara kwa mara,
“Niambie baba Mishi”
“Hivi mara ngapi nikukatalie kumuita mwanangu jina hilo?”
“Haya yameisha, vipi ulifanikiwa?”
“Nifanikiwe wapi? Sikuweza kumbamba wala nini”
“Ila ngoja nikuulize!”
“Niulize tu”
“Hivi wewe hufurahii kula chakula anachopika mke wako? Hufurahii kuona kazi za nyumbani kwenu zikifanywa na mkeo?”
“Na wewe acha kunichanganya, sasa ningekuwa nafurahia ni kwanini tulitafuta msaidizi? Sipendi mke wangu achoke, ona hata unyumba sipati maana kila siku amechoka”
“Ngoja nikuulize tena, toka mkeo ajifungue umeshawahi kupata unyumba?”
“Sijwahi sababu ya mtoto”
“Kwahiyo saivi ni mdada wa kazi amekuwa kikwazo, ngoja nitakusaidia ila kwanini hakunitafuta nikusaidie?”
“Ningekutafutaje? Sijui unapopatikana”
“Ngoja tukikutana safari ijayo nitakwambia jinsi ya kunipata mimi”
Kisha yule mtu alisogea na kuchuma majani Fulani kisha akamwambia Juma,
“Haya majani, ukifika kwako yatwange halafu ukimaliza kuyatwanga jipake wewe na mkeo nataka muone kila kitu ambacho Anna huwa anafanya kwenye nyumba yenu ila mkiona msimfanye chochote kibaya Anna, kama kumfukuza basi mumfukuze kwa utaratibu tu hata msimfanye chochote kibaya”
“Sawa nashukuru sana nimekuelewa, kwahiyo haya majani ni uhakika nitambamba yule mchawi?”
“Ndio, haya majani ni uhakika, yanakufanya uone kila kitu ambapo yeye hatojua kama mnaona kila kitu”
“Asante sana”
Yani Juma alimshukuru sana huyu mdada na kumuaga kwa muda huu ambapo yeye moja kwa moja alirudi nyumbani kwake.

Juma alipofika kwake, alienda kuwasalimia tu ndani kisha akweka vizuri mzigo aliofika nao pale, na baada ya hapo sasa akatoka nje.
Alichukua kinu kidogo na kuanza kuyaponda yale majani, ila muda kidogo mtoto wake alifika pale alipokuwa anaponda halafu akamuuliza Juma,
“Baba, kwanini unapenda uvivu wa mama?”

Itaendelea….!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 likes zikifika 300 na share 100 naweka kingine chap chap
 
MTOTO WA MAAJABU: 15

Alichukua kinu kidogo na kuanza kuyaponda yale majani, ila muda kidogo mtoto wake alifika pale alipokuwa anaponda halafu akamuuliza Juma,
“Baba, kwanini unapenda uvivu wa mama?”
Yani Juma alishangaa sana leo na kujikuta akiacha hata kuponda na moja kwa moja kuingia ndani, halafu akamkunja Anna,
“Jamani shemeji nimefanyaje tena?”
“Mchawi mkubwa wewe, mchawi mkubwa, umemaliza kwa mke wangu umeanza kwa mwanangu”
Mariam akasogelea ili kujua kuwa tatizo ni kitu gani,
“Kwani Juma kuna nini?”
“Nenda ukamsikie yule mtoto nje anaongea”
“Mtoto gani?”
“Mtoto wetu, anaongea sababu ya uchawi wa huyu binti”
Mariam alianza kucheka tena alicheka sana na kumwambia mumewe,
“Unajua unachekesha wewe, sasa kuongea kwa huyo mtoto na Anna kuna uhusiano gani? Inamaana siku zote hizi ulikuwa hujui kama mtoto wako anaongea? Ameanza kuongea huyo mtoto siku ya kwanza kuzaliwa, sembuse kwasasa? Mimi nishamzoea mbona, ulitaka mtoto awe bubu? Si ndio jibu lako hili toka mwanzo? Halafu huo uchawi wa Anna una uhakika nao?”
“Ndio mke wangu, huyu Anna ni mchawi”
“Hebu muache binti wa watu”
Mariam alimvuta Anna pembeni na kuongea na mumewe,
“Unajua mara nyingine uwe unafanya vitu kwa kufikiria sio unakurupuka tu, una ushahidi gani wa uchawi wa Anna?”
“Pole mke wangu, najua sio akili zako hizo, najua huyu Anna ameshakuteka”
“Muache aniteke tu, mimi nimeridhika”
Hilo jibu lilimkera sana Juma, kiasi kwamba alienda nje na kutupa ile dawa kabisa na kurudisha kinu ndani maana anayemuhangaikia tayari amesharidhika kwahiyo akaachana nayo.

Juma alichukia sana siku ya leo na moja kwa moja alienda kulala tu kwani alikuwa na hasira sana hata chakula cha usiku hakuhitaji kula wala nini, kwahiyo ni Mariam tu na Anna ndio walikaa na kula,
“Dada, sasa shemeji hali chakula?”
“Atajijua mwenyewe kama amedhira”
“Mmmmh dada!”
Anna hakumalizia kula bali aliinuka na kumfanya Mariam amuulize,
“Vipi mbona huli tena?”
“Nimeshiba gafla dada”
“Kheeeee!! Haya”
Basi Mariam aliendelea zake kula chakula na alipomaliza alienda zake kulala ambapo alimkuta Juma amelala huku akiwa na mawazo sana ila hata Mariam hakujisumbua kumuuliza wala nini kwani alilala tu.
Kwenye mida ya saa saba usiku, Juma alijihisi njaa sana yani hakuwa na namna zaidi ya kuamka kwenda kula tu.
Alitoka na moja kwa moja alienda mezani maana bado chakula kilikuwepo mezani, basi akapakua na kuanza kula, muda kidogo alitoka na Anna ambaye alishangaa,
“Khaaaa shemeji ndio unakula muda huu!”
“Ndio, unataka kuniroga au?”
Anna hakujibu kitu zaidi zaidi aliamua tu kuondoka zake na kurudi chumbani.
Baada ya kumaliza kula ndipo alirudi tena chumbani kwake kulala.

Mapema kabisa siku ya leo, Juma alijiandaa na kuondoka zake maana alikuwa na mawazo sana ingawa aliamka usiku kupata chakula cha usiku ila alikuwa na mawazo sana yaliyompelekea kuwa na njaa sana, ila asubuhi hii hakula wala nini.
Moja kwa moja leo alienda kwa mama yake, yani hakutaka kupitia popote pale zaidi ya kwenda kwa mama yake maana aliona kuwa huko anaweza kuelewa mengi sana.
Juma alipofika kwao, cha kwanza kabisa, alikula kwanza na ndipo aliongea na mama yake ambapo alimueleza tena kuhusu yule msichana wake wa kazi na kuhusu mtoto wake alivyomwambia na jinsi alivyojibiwa na mkewe,
“Pole sana, ila hii yote Juma inayokupata ni ile inayoitwa asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hakuna mke hata mmoja uliyeoa aliyekuwa na baraka kwangu, yule wa mwanzo sikumpenda hata kidogo na ninamchukia hadi kesho, haya ukaja na mauzauza haya ya Mariam, yani hukutaka kusikia la Muadhini wala la Shabani, yani wewe ulichoamua umeamua tu, familia nzima tulikwambia Juma huyu Mariam hakufai, familia yake yenyewe inamlalamikia, ukadai oooh ananifaa sana, haya kiko wapi sasa? Unajuta kila siku, haya nakuja kuhusu mtoto wako hii wewe usishtuke ile siku aliyonisonya uje ushtuke kukwambia kuwa unaupendea nini uvivu wa mama yake? Na mimi nakuuliza kama huyo mtoto wako, unaupendea nini uvivu wa mkeo?”
“Khaaaa mama jamani, yani na wewe badala ya kunifariji unanikandamiza jamani!”
“Nikufariji nini sasa? Kuna cha kukufariji hapo jamani Juma? Mara ngapi nimekupa jibu kuhusu hayo mauzauza ya nyumbani kwako? Mara zote sikubaliani na uvivu wa mkeo, muache akomeshwe na huyo binti kama ni mchawi kweli, yule mkeo amezidi kwakweli”
Yani Juma aliona leo ndio amekoma kabisa kuja kumuuliza mama yake ingawa ni mara nyingi tu huwa anakuja kumuuliza, basi muda huu alimuaga na kuondoka zake.

Mariam akiwa na Anna nyumbani, yule Anna alimlalamikia Mariam kuhusu swala la yeye kuitwa mchawi yani alikuwa akilalamika huku analia,
“Yani mimi mchawi mimi jamani!! Yani dada hata huo uchawi siujui, hata uchawi unafanyweje dada yangu sijui kitu halafu anatokea mtu na kuniita mimi mchawi kweli jamani! Roho yangu imeumia sana”
“Pole mdogo wangu, pole sana”
“Hakuna mtu mchawi kwenu, kama mmenichoka dada niambie niondoke tu”
“Utaenda wapi sasa Anna?”
“Nitaenda kurandaranda tu huko mitaani, siwezi dada kuvumilia kuitwa mchawi! Yani nikawe mchawi mimi hamani khaaa!!”
Basi Mariam akafanya kazi ya kumpa moyo pale ili Anna asijihisi vibaya maana Mariam hakuna chochote kibaya alichokihisi kuhusu Anna.
Halafu akamuuliza Anna,
“Leo utapika chakula gani cha usiku mdogo wangu?”
“Kwani wewe unataka chakula gani dada?”
“Chochote tu utakachopika nitakula”
“Sawa dada, nitapika unachotaka wewe”
“Utajuaje ninachotaka?”
“Kwani sijui ni kitu gani unapenda jamani dada? Tumeishi muda mrefu lazima niwe najua mambo yako mengi tu”
Mariam alitabasamu na alifurahia tu vile alivyokuwa anajibiwa na Anna.

Hii siku, Juma alichelewa sana kurudi maana alirudi wakati muda umeenda sana kwahiyo moja kwa moja alifikia kulala na hivi mkewe hakuwa na muda wa kumuuliza chochote ndio kabisa yani.
Kulipokucha tu, Juma alijiandaa kwaajili ya kuondoka na wala Mariam hakujisumbua kumuuliza.
Hii ikawa ndio ratiba ya Juma kwa siku hizi yani kwa wiki nzima Juma alikuwa akifanya ratiba hii, ya kuchelewa kurudi na kuwahi kuondoka.
Leo Mariam alipokuwa amekaa, Anna alienda kumuuliza,
“Dada, mbona shemeji siku hizi anachelewa sana?”
“Sijui mwenyewe na matatizo yake”
“Ila dada, wewe ndiye unayetakiwa kuyajua matatizo ya shemeji, yani wewe ndiye unayetakiwa kujua kuwa ni kitu gani kinamsumbua”
“Hatuna ratiba hiyo humu ndani, ukiwa vibaya unatakiwa mwenyewe kusema. Halafu kingine, yani Juma huwa haumwi jamani tena haumwi kabisa, mgonjwa mgonjwa ni mimi bhana tena nimepumzika sasa hivi ila mimi huwa naumwa sana. Ila Juma yupo freshi tu kila siku”
“Ila dada kuna umuhimu wa kumuuliza, vipi mnashiriki tendo la ndoa?”
“Mmmmh yani toka nijifungue sitaki kabisa hayo mambo, nahisi kama nitabeba mimba nyingine na mimi sitaki kuzaa kwasasa”
“Kheee dada wewe jamani yani kila sehemu upo”
“Kivipi?”
“Uvivu upo, kutokupenda kulea upo, saivi tena na wasiotaka kuzaa upo, duh dada na wewe!”
“Ndio, mimi kama uvivu najijua jamani tena toka nipo mdogo. Mimi ni mvivu hatari nakumbuka wakati mdogo niliwahi kujisemea kuwa mimi nitaweka wasaidizi wa kazi hadi wa kuniogesha na kunilisha kwahiyo kwasasa uvivu nimepunguza maana sina wazo hilo ila mimi ni mvivu sana, na ninajijua na hata Juma ananijua pia”
“Mmmmh ila hongera dada yangu maana hicho kipaji chako duh! Wengine hawapendi kujisema ila wewe unajisema kabisa dada yangu”
“Kama muda huu nataka nikalale”
Halafu muda ule ule aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kulala.

Juma akiwa kazini, siku hizi mara nyingi sana kuna mdada alijikuta huwa anaongea nae hadi muda unaenda sana halafu ndio anaenda nyumbani kwake ndiomana alikuwa akichelewa sana, mdada huyu aliitwa Pendo, ni mara nyingi sana alikuwa akimuuliza Juma kuhusu matatizo ya familia yake.
“Kwakweli Pendo wewe ni mwanamke wa ajabu sana, una upendo kama jina lako hebu ona jinsi unavyonijali jamani hadi huwa napata amani na faraja”
“Ila tatizo huwa kuna mambo unanificha, mimi huwa nataka kukushauri vyema kuhusu familia yako lakini kuna mambo unanificha Juma”
“Kama yapi?”
“Mengi tu, hata huwa sielewi ni nini kinakutatiza, maana muda wote husema kuwa ni familia ndio inayokutatiza, mimi kama mimi naumia sana kusikia hayo Juma, nakuhurumia kwakweli ila nitakusaidiaje? Hapo ndio pagumu”
Waliongea mengi kama kawaida yao kisha ndio Juma akaondoka zake, ila wakati anaondoka, aliongozana na rafiki yake aliyeitwa Hakim ambapo rafiki yake alimwambia Juma,
“Ndugu yangu, yule mdada Pendo anaonyesha kukupenda sana lakini kwanini wewe hutaki kumtongoza?”
“Aaaah jamaa yangu, si unajua kuwa nina mke lakini!”
“Ndio, ila inavyoonyesha huyo mkeo ndio anakufanya ukae ofisini hadi muda huu. Najua familia yako ingekuwa na amani basi ungekuwa unawahi kurudi ila familia yako haina amani ndiomana unajichelewesha”
“Kwahiyo unataka nifanyeje?”
“Kuwa na Pendo, ningekuwa mimi ni wewe ningekuwa na Pendo, angalia upendo wake kwako. Yule binti kalelewa bhana”
Juma alitabasamu tu na kuagana na rafiki yake ila njiani aliona kama maneno ya rafiki yake yana ukweli ndani yake ila hakujua kuwa ataanzia wapi ukizingatia huyu Pendo ni amemzoea sana, je ataanzia wapi kumuhitaji kimapenzi? Hapa palikuwa pagumu sana kwa Juma.

Kama kawaida Juma alifika usiku na kukuta ndio wanakula, aliwasalimia na kutaka kwenda chumbani ila kabla ya hapo, Anna alimuuliza Juma,
“Shemeji, mbona siku hizi huli usiku? Tatizo ni nini?”
Juma alimuangalia Anna halafu akamuuliza,
“Unaniuliza hivyo wewe kama nani?”
“Jamani shemeji, sio hivyo, nimekuuliza kwa uzuri tu shemeji maana sielewi naona siku hizi unafika na kupitiliza kulala”
Juma hakujibu zaidi zaidi alienda zake chumbani kulala kama kawaida yake.
Anna alimuangalia Mariam na kumwambia,
“Dada, unaweza kupoteza ndoa yako kwa ujinga wako”
“Kwahiyo mimi mjinga?”
“Hapana dada, ulimi umeteleza tu. Nilitaka kukuuliza ni kwanini humlazimishi shemeji kuja kula?”
“Yule ni mtu mzima bhana, nianze kumbebea chakula nikakabane nae kama tunalishana na mtoto? Huyo mtoto wangu mwenyewe sijawahi hata mara moja kuchukua chakula na kumlisha”
Anna alimuangalia na kuishia kuguna tu maana alishindwa hata kuendelea kumuelekeza.

Asubuhi ya leo, Mariam aliwahi sana kuamka kuliko siku zozote na alipoamka tu moja kwa moja alienda nje na kuangalia jinsi mboga na mahindi aliyopanda Anna yalivyochipua, basi akamwambia Anna,
“Yani hadi raha, vitu vimeshtawi balaa”
“Ni raha kweli dada, kila kitu ni maamuzi tu”
“Ni maamuzi ndio ila usiwe mvivu kama mimi maana ukiwa mvivu kama mimi hakuna utakachoweza”
“Mmmmh!”
“Sasa Anna, leo nataka twende pamoja kuangalia samaki, nimetamani sana kula samaki ila huyu mtoto tumuache, upo tayari?”
“Dada hapana, kwanini mtoto tumuache?”
“Nani atambeba sasa?”
“Mimi nitambeba mwenyewe dada”
“Sawa, nenda kajiandae basi”
Anna alienda kujiandaa kisha alipomaliza, akambeba mtoto halafu akaongozana na Mariam kwenda huko kwenye samaki ambapo Mariam alikuwa akienda zamani sana ila kwa kipindi hiki hakwenda siku nyingi kwani kuna mtu alikuwa anapitisha samaki ila hakupita pia kwa kipindi kidogo ndiomana leo aliona bora aende kununua mwenyewe.
Walifika na kununua samaki, ila kuna mtu ambaye anamfahamu Mariam alipowaona aliwasalimia na kumvuta Mariam pembeni kisha akamuuliza,
“Huyu binti umemtoa wapi?”
“Kwanini?”
“Nimekuuliza tu Mariam?”
“Ni mdada wangu wa kazi”
“Mmmh sio mtu mzuri, hakufai huyo”
“Kwanini?”
“Macho yake yanafuka moshi”
Mariam alimshangaa huyu mtu kwani kila siku huwa anamuangalia Anna na wala haoni kitu cha namna hiyo, kisha Mariam akamwambia huyu mtu,
“Hapana, mbona macho yake yako sawa tu!”
Kisha yule mtu akamwambia tena Mariam,
“Tena macho yake ukiyaangalia vizuri utaona yanawaka moto”
“Kheee jamani, hebu niache na familia yangu”
Mariam aliachana na huyu mtu kisha alirudi kwa Anna na kuondoka nae kuelekea nyumbani.

Sasa wakiwa nyumbani tu, muda huu walikuwa nje halafu Mariam akamwambia Anna,
“Basi Anna kalete maji uwaoshe hao samaki”
Anna alienda kuleta maji na kusogeza wale samaki kwa Mariam na kumwambia,
“Dada, waoshe tu mwenyewe”
“Kwanini Anna?”
“Mimi huwa sipendi shombo la samaki”
“Kheeee kwahiyo mimi ndio napenda? Hata mimi sipendi shombo, napenda kuwala tu. Siwezi kuosha samaki mimi”
Mariam alikuwa akiongea hayo huku akimuangalia Anna machoni kwani alitaka kujaribu kuona kile ambacho yule mtu alimwambia, ila Anna hakujibu kitu sema baada ya Mariam kumuangalia sana Anna, akajikuta tu akivuta wale samaki na kuanza kuwaosha na kisha alienda mwenyewe jikoni kuwakaanga.
Kwenye mida ya saa moja jioni Juma alirudi ila alivyowasalimia tu alipitiliza chumbani, basi kweye mida ya saa mbili walitenga chakula huku Anna akimwambia Mariam,
“Dada, leo shemeji amewahi kurudi, nenda kamuite aje kula”
“Anna, nilishakwambia kuwa mimi sifanyi huo upuuzi. Yule ni mtu mzima, aje mwenyewe kula akitaka”
Anna alitikisa kichwa ila hakusema zaidi, basi waliendelea kula tu na maongezi mengine.

Leo, Juma kama kawaida yake aliondoka ila siku hizi alikuwa hajishughulishi kabisa na chakula cha hapo nyumbani kwake, kwahiyo alikuwa akiondoka bila kula chakula chochote.
Alipofika kwenye shughuli zake tu, akakutana na Hakim kwanza ambaye alimwambia,
“Leo nimekuandalia mazingira Juma, ushindwe wewe tu”
“Mmmmh mazingira gani sasa?”
“Sikia nikwambie, nilikueleza mapema kuwa Pendo anakufaa wewe, kwahiyo twende nyumbani kwa Pendo”
Juma alikubali tu, kiukweli kwasasa alianza kumchoka mkewe na tabia zake, basi moja kwa moja Hakim alimpeleka nyumbani kwa Pendo na kumuacha hapo ambapo Pendo kwanza aliondea nae,
“Unajua nini Juma, rafiki yako kanieleza ila ubaya ni kuwa mimi huwa sitembei na waume za watu”
“Dah!! Pendo”
“Ila sijakuangusha, kuna rafiki yangu yupo na yeye anahitaji sana mtu wa kufarijiana nae. Yupo chumbani tayari”
Juma moja kwa moja alienda kwenye chumba alichoonyeshwa, akaingia hapo na kumkuta mwanamke kalala huku mgongo ndio ukiwa juu, akamsogelea na kumpapasa mgongoni ila gafla akasikia sauti ya mtoto wake.
“Yani baba unataka kumsaliti mama?”

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 ofa kwa leo mpaka mwisho utaipata kwa 1500 tu
 
MTOTO WA MAAJABU: 16

Juma moja kwa moja alienda kwenye chumba alichoonyeshwa, akaingia hapo na kumkuta mwanamke kalala huku mgongo ndio ukiwa juu, akamsogelea na kumpapasa mgongoni ila gafla akasikia sauti ya mtoto wake.
“Yani baba unataka kumsaliti mama?”
Juma alishtuka na kuangalia huku na kule bila kuona yoyote ila alimuacha yule mwanamke na kutoka nje hata Pendo alimshangaa kwani Juma aliondoka kwa upesi sana.
Hakupita tena kwenye shughuli zake kwani moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana, alijisemea,
“Hivi yule mtoto wangu ni mtoto kweli au kuna namna hapa katikati? Hivi Mariam nilimpa kweli mimba au alikuwa akidanga nje? Yani nina mashaka na yule mwanamke aaarrgh basi tu ninampenda sina cha kufanya”
Juma alirudi hadi nyumbani kwake ambapo kwa muda huu aliwakuta wote mezani wakiwa wanakula huku Anna akila yeye na kumlisha mtoto, basi Juma aliwasalimia na kutaka kupitiliza chumbani ila mtoto akamwambia,
“Njoo tule baba, najua una njaa”
Juma alimuangalia huyu mtoto wake bila kummaliza kwakweli, akitaka kumfanya ni kiumbe cha ajabu anashindwa maana huyu mtoto anaongea kawaida tena kwa sauti ya kitoto, na pia ana muonekano wa kawaida ila jinsi anavyofanya mara aongee mara nini ndio vitu vinavyowaogopesha mule ndani.
Juma hakusema kitu, ila alikaa na kuanza kula, wakati anakula aliuliza,
“Chakula kapika nani?”
Alikuwa akiuliza huku akimuangalia Mariam ambapo Mariam alijibu,
“Kapika Anna, si ndio mpishi wa humu ndani! Kwani unaona kapika nani?”
Juma akaguna na kusema,
“Naona kama umepika wewe, maana ladha ya hiki chakula ni kama umepika wewe!”
Muda ule ule mtoto wao akajibu,
“Ndio amepika mama, ndiomana na mimi nakula”
Yani humu ndani huwa akiongea huyu mtoto inakuwa kama ni ajabu sana kwahiyo huwa hakuna hata mtu mmoja anayejibu pale mtoto huyu akiongea, huwa hakuna anayejibu, hakuna anayeuliza swali wala hakuna anayehoji. Kwahiyo wote walikaa kimya na kuendelea kula tu kwa muda huo.

Juma alipomaliza kula, aliamua kwenda chumbani kwani alikuwa na mawazo mengi sana haswa ni mawazo ya juu ya kilichotokea, muda kidogo Mariam na yeye akaenda chumbani kwa mume wake na kuanza kuongea nae,
“Mbona leo mapema maana siku hizi hata sijui umeanza mpango gani huo wa kurudi usiku wa manane”
“Dah!! Mariam wewe acha tu”
“Niache tu kitu gani? Nisipokuuliza naonekana sio mke mwema, halafu nakuuliza napo napewa jibu la niache tu ndiomana mimi huwa siulizi wala nini”
“Ni nani kakwambia kuwa usipouliza unaonekana sio mke mwema?”
“Ni hako kabinti Anna, yani kila siku ambavyo huli chakula ananilazimisha nije kukuuliza kuwa kwanini huli, sijui jambo kidogo tu nikuulize, mara anasema nikuletee chakula chumbani, sasa mapemzi ya hivyo kwetu yatoke wapi? Kwani mimi sina kawaida ya kuwa na mapenzi ya kijinga kiasi hiko”
“Kwani kumuuliza mumeo ni ujinga?”
“Ni ujinga ndio, kama jibu lenyewe ndio hili etu Mariam acha tu, ni ujinga na mimi sikuulizi tena”
Juma hakusema neno, badala yake aliamua tu kujilaza maana angesema angeweza kuongea yasiyofaa.

Usiku wa leo wakati wamelala, kuna muda Mariam alishtuka na kilichomshtua ni simu yake maana leo hakuizima wala nini, kwahiyo aliichukua na kuiangalia, akashangaa sana kuona mama yake amempigia kwa muda ule, ila alipokea na kumsikiliza,
“Mama, mbona usiku sana?”
“Ndio ni usiku sababu na mambo yenyewe ni ya usiku usiku”
“Kivipi mama?”
“Mariam, leo nimekutana na mtu yani karopoka mengi sana kuhusu wewe”
“Yapi hayo mama yangu?”
“Unajua kaanza kunieleza toka kipindi wewe upo na mimba ya mtoto wako huyo hadi kipindi umejifungua, kumbe mama mkwe wako ndio alikuletea dawa ya wewe kuweza kujifungua?”
“Ndio mama”
“Ila yule mama huwa hakupendi, unajua nilimshangaa kipindi umejifungua alivyojifanya anakupenda hadi anafanya kazi zote humo ndani kwenu, anafua anapika yani kama sio mkwe wakati kwa kawaida huwa hakupendi”
“hata mimi naelewa hilo mama ila mimba ilivyokaa muda mrefu ndio ilinipatanisha nae, na mara nyingi alikuwa akijaribu kuniletea dawa mbalimbali. Huyo mtu kasemaje”
“Unatakiwa kuja huku nyumbani mwanangu, halafu kwenye mida ya saa nane usiku kuna sehemu tutaenda kwaajili ya tiba”
“Mmmmh mama ni wapi huko? Mbona usiku sana?”
“Unahitaji kupona au la? Unajua mimi naumia kiasi gani kama mama yako? Hata muda huu nimekupigia simu sababu naumia sana, jitahidi uje kesho”
“Sawa mama, nimekuelewa”
Basi Mariam akaagana na mama yake na kwa muda huo sasa, ndio Mariam aliweza kulala vizuri kabisa.

Leo Mariam alichelewa kuamka maana siku nyingine huwa anawahi ila leo alichelewa sana hadi alijishtukia na kujiona kuwa hayupo sawa baada ya kuangalia muda na kuona kuwa ni saa tano na nusu.
Aliamka na kujinyoosha maana alikuwa amechoka sana, alienda kuoga kwanza halafu ndio akatoka, ila muda huu alikuta Anna na mtoto wake wapo nje kabisa ikabidi atoke kwenda kuwasalimia,
“Jamani Anna mbona nimelala sana!”
“Pole sana dada, nilikuwa kupalilia”
Mariam aliangalia lile shamba lao dogo na kuona limepaliliwa kabisa hata jani hakuna basi alimpongeza Anna,
“Hongera sana mdogo wangu Anna”
Yule mtoto wao akadakia,
“Hongera na wewe mama”
Mariam hapa tu ndio palimmaliza nguvu kabisa kwani aliondoka na hakutaka hata kuendelea kuisikiliza ile hongera ya katoto chao.
Aliporudi ndani moja kwa moja alienda kunywa chai, ila alikuwa na mawazo sana na vilevile alikuwa na uchovu sana siku hiyo.
Alipomaliza kunywa chai alirudi chumbani na moja kwa moja alichukua simu yake na kumpigia mama yake maana alijiona ni wazi kuwa hatoweza kwenda kwao,
“Mama, samahani, sitaweza kuja leo yani nimechoka hapa balaa nahitaji tu kulala”
“Khaaa Mariam, yani unafanya uvivu hata kwa mambo yanayokuhusu jamani!”
“Sio uvivu mama, nimechoka sana”
“Umechoka umefanya nini kwani mwanangu? Najua kama kazi za nyumbani hufanyi, sasa huko kuchoka kumekuwaje tena?”
“Yani mama hata sijui jinsi ya kukuelezea, ni kweli sifanyi chochote ila nimechoka balaa naomba nije kesho mama”
“Nimekumbuka kitu mwanangu, naomba usishiriki na mumeo tendo la ndoa mpaka tutakapomaliza haya”
“Usijali mama kwanza hata hamu ya kushiriki sina wala nini, hata usijali kuhusu hilo”
Basi Mariam akaongea na mama yake na kupatana nae kuonana nae kesho yake.

Juma akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, alipita ile njia ambayo huwa anakutana na yule binti na alivyopita tu alisimama mahali pale akiangalia angalia ila baada ya muda kidogo yule binti na yeye alisogea eneo lile na kumsalimia Juma, kisha Juma aliongea nae,
“Kuna kitu sielewi kuhusu mtoto wangu”
“Kitu gani huelewi?”
“Yule mtoto anaongea, ni jambo la ajabu sana”
“Sio jambo la ajabu, ulitaka mtoto wako awe bubu? Mbona wanadamu hamna shukrani lakini, asingekuwa anaongea napo ungesema ni mtoto gani huyu! Kaongea mapema napo unasema”
“Sina maana hiyo, hebu fikiria kuna siku nilipata mwanamke halafu nikasikia sauti ya yule mtoto eti baba unataka kumsaliti mama!”
“Ila kwanini unataka kumsaliti mkeo?”
“Jamani mimi ni mwanaume, ni mwanadamu mimi ambaye nimekamilika kabisa, na mimi nina uhitaji ila mke wangu hataki”
Huyu binti alimuangalia Juma kisha kuna maua Fulani akayachuma na kumwambia Juma,
“Nenda kamnusishe haya maua mkeo halafu utapata wasaa wa kufurahia nae tendo”
“Kwahiyo nisimwambie eeeh!”
“Ndio, usimwambie chochote, hata usimwambie kuwa unahitaji, yani utamnusisha tu hayo maua na kisha utalala nae utakavyo. Nimekupa tiba leo Juma, nadhani utaifurahia ndoa yako”
“Asante sana, maana yule mwanamke kila siku analalamika kuwa amechoka jamani, ananikosesha raha kabisa”
Basi Juma alichukua yale majani na kuweka vizuri mfukoni halafu aliagana na yule binti na kuondoka zake kwenda nyumbani kwake.

Juma alifika muda ambao walikuwa wanakula mule ndani kwake, kwahiyo na yeye alienda kujumuika nao kupata kile chakula kwa pamoja, basi walimaliza kula ndipo alipoenda ndani kuoga na kumsubiri mke wake sasa, muda kidogo ndipo Mariam na yeye alipoingia chumbani huku akilalamika kama kawaida yake,
“Jamani leo, nimechoka yani nimechoka sana leo”
“Pole mke wangu”
“Asante, hata sitaki tuongee sana. Tulale tu muda huu”
“Sawa, tulale”
Mariam alipanda kitandani na kujilaza, basi hapo hapo Juma alitoa yale maua na kumnusisha Mariam ambapo Mariam aliinuka mwenyewe kitandani na kumkumbatia Juma na hapo Juma alibahatika kulala na mkewe toka kipindi ambacho Mariam alijifungua.
Juma alikuwa na furaha sana leo, alijikuta tu akishukuru vile ambavyo yule binti amemsaidia ile dawa.
Basi wakalala hadi asubuhi, Mariam alikuwa wa kwanza kuamka na kumuuliza mume wake,
“Tumefanya nini sasa Juma”
“Kwani tatizo liko wapi mke wangu?”
“Sio tatizo liko wapi? Nakuuliza tumefanya nini?”
“Ngoja nikuonyeshe tulichofanya”
Juma alichukua yale maua yaliyobaki na kumwambia mkewe,
“Hebu nusa haya maua uone”
Mariam alinusa yale maua, na muda ule ule Mariam alilegea na kuanza kumkumbatia Juma bila kutaka kumuachia basi Juma alifurahi sana na kupata wasaa mwingine wa kulala na mke wake, baada ya hapo ndio akajiandaa na kuondoka zake, kwahiyo alimucha tu Mariam akiwa amelala.

Juma leo alikuwa na furaha sana hata alikuwa anawaza kuwa akikutana tena na yule binti atamuomba ampatie maua ya kutosha ili aendelee kufurahi na mke wake,
“Dah!! Sikujua kama kuna kitu chepesi vile katika kumpata mke wangu mbishi, kumbe kuna yale maua dah!! Akiyanusa tu kwisha habari yake, analegea na kuwa mpole mwenyewe. Yani natamani hata nipewe mbegu kabisa nikapande nyumbani kwangu”
Alikuwa akitabasamu tu mwenyewe, muda huo rafiki yake Hakim alifika na kumuuliza,
“Vipi Juma, unaonekana kuwa na furaha sana”
“Ni kweli nina furaha, acha tu”
“Dah! Haya ila hapa kuna habari zimesambaa kuhusu wewe hata sielewi ni kwanini imekuwa hivi”
“Habari gani?”
“Nasikia Pendo alikutafutia mwanamke ila hujafanya chochote nasikia una matatizo ya nguvu za kiume ndugu yangu”
“Dah!! Waache tu waseme hivyo, ila mimi sina tatizo lolote lile. Ilimradi nafurahia maisha na mke wangu basi inatosha”
“Sasa mbona ulihitaji mwanamke?”
“Sababu nilikuwa na mawazo, ila kwasasa sina mawazo tena, nipo na furaha tu moyoni mwangu”
“Haya, hongera”
Hakim hakuongea sana kwani hakuwa na kingine cha kumshawishi Juma sababu Juma alionekana kuwa na furaha sana.

Kwakweli Mariam leo alichukia sana hadi alijiuliza kuwa ameanza vipi kushiriki tendo la ndoa na mumewe wakati kashapanga mipango na mama yake? Hakuelewa kabisa, basi muda huu alikaa sebleni akiwa na mawazo sana hadi Anna alimuuliza,
“Mbona hivyo dada?”
“Aaarggh huyu mwanaume ni mpuuzi sana”
“Kwani kafanyaje?”
“Unajua leo ameshiriki tendo la ndoa bila ridhaa yangu, kwahiyo kanibaka yani”
“Kheee dada, kwani kwenye ndoa kuna kubakana?”
“Ndio, kama mtu hajataka basi ni kumbaka”
“Ila dada, ni halali yake maana hilo linaitwa tendo la ndoa kwahiyo kwa wanandoa ni halali dada yangu”
“Hata kama ni halali, alitakiwa kuniambia kwanza mimi nikubali”
“Hivi dada si uliniambia kuwa hujashiriki na mumeo toka umejifungua? Ulitaka afanyaje sasa jamani? Hata simlaumu kwa hilo, halafu ngoja nikuulize kwani kakupiga muda wa kushiriki? Kakulewesha pombe hadi useme kakubaka?”
“Sijui ni nini kilitokea ila ninachojua ni kuwa amenibaka, kwakweli kanikera sana maana kaharibu mambo yangu yote niliyopanga”
“Ilikuwaje kwani?”
“Wewe bado mdogo sana Anna, nisikukuze.”
Kisha Mariam aliinuka na kwenda chumbani ambapo alimpigia simu mama yake na kumweleza kilichotokea,
“Aaaah hapo haifai mwanangu, itabidi uje kesho basi, jitahidi usifanye nae chochote”
“Yani mama, leo nalala na nguo hata kumi, sifanyi nae chochote kile, ila mama inamaana dawa itaharibika eeeh!!”
“Ndio, hii dawa hairuhusiwi kushikwa na mtu aliyetoka kufanya tendo la ndoa ndiomana nimekutahadharisha mwanangu. Nakuomba sana uwe mwangalifu na usifanye nae kitu”
“Sawa mama yangu”
Mariam alikubaliana na mama yake pale kuwa ataenda kesho yake ila alikuwa na hasira sana, alichukia sana kwa kile kitendo kilichofanyw ana mumewe.

Usiku wa leo, Mariam alikaa na Juma na kuongea nae maana aliona ni vyema kumueleza ukweli ili asimfanyie tena kama vile,
“Mume wangu sikia, nakuomba sana tusishiriki tendo la ndoa kwasasa sababu kesho nataka kwenda kwa mama, kuna dawa tunatakiwa kufanya kwaajili ya mtoto wetu”
“Hebu nieleweshe vizuri Mariam”
basi Mariam alianza kumueleza mumewe vile ambavyo alielezwa na mama yake kuhusu hiyo dawa ili Juma asijekufanya tena akashindwa kwenda kutekeleza hiyo dawa,
“Aaaah hapo nimekuelewa, ila uwe unaongea kama hivyo mke wangu”
“Ndio hivi nimekwambia, ila umenibaka Juma sijapenda wala nini”
“Mariam, hebu rudisha kumbukumbu zako vizuri, nimekubaka mimi? Si wewe mwenyewe ndio ulikuja kunikumbatia huku ukisema kuwa unahitaji!”
Mariam aliinama chini na kusema,
“Hata sijui ni nini, sijui ni akili za ndoto au kitu gani, na ile asubuhi je nayo sielewi ilikuwaje ila tulilala wote”
“Ilikuwa vile vile Mariam, ila subuhi inanoga mke wangu jamani, natamani hata iwe kila siku”
“Nenda zako huko, usitake kuniharibia dawa zangu, unanikera tu muda huu”
Ila walielewana kwa muda ule sababu hata Juma alihitaji kwa sana ukombozi wa mtoto wake, kwahiyo alimpatia mkewe nauli na hela ya kumsaidia.
Kulipokucha tu, Juma alimuuliza mke wake,
“Kwahiyo leo utalala huko huko?”
“Ndio, itabidi iwe hivyo maana dawa yenyewe inafanyika saa nane usiku”
“Aaaah, basi sawa”
Juma alijiandaa na kuondoka zake, kwenda kwenye shughuli zake.

Muda huu Mariam na yeye alijiandaa kwaajili ya kwenda kwao, kwahiyo alimuaga tu Anna pale kuwa atarudi kesho yake,
“Kheee dada, kwahiyo leo hurudi?”
“Ndio, nitarudi kesho”
“Sasa dada, shemeji akinifukuza je?”
“Anaanzia wapi kukufukuza? Hakuna kitu kama hiko”
“Ila dada, mfano ukaenda huko na mimi pamoja na mtoto itakuwaje?”
“Hapana haiwezekani sababu hapa nyumbani panahitaji mtu wa kuangalia mazingira”
Basi Mariam akaondoka zake, leo hakuwa na tatizo la kugeuza viatu kwani aliona wazi kuwa hajaondoka kwa kutoroka ila alikuwa akitembea huku akiwa na mashaka tu ya kujikuta kwake tena.
Alifika hadi nyumbani kwao, na kuingia ndani ambapo mama yake alimkaribisha na kuongea nae kidogo,
“Bora umekuja Mariam ili tufanye hii dawa vizuri”
“Ndio mama, nipo hapa”
“Sawa, badae tutapanga vizuri ngoja kwanza nimalizane na wale ndugu zako wengine”
Mariam alimuitikia mama yake, kiukweli alikuwa na furaha sana kufika nyumbani kwao kwa siku ya leo.

Kwa muda huu sasa, Mariam alikuwa na mama yake, na waliweza kupanga mambo vizuri kabisa kisha mama yake akamwambia,
“Mwanangu, saa nane nitakuamsha halafu ndio twende kule tulikopanga”
“Sawa maam, itakuwa vizuri”
Basi usiku ule Mariam alilala tu kwenye chumba chake ambacho alikuwa akilala nyumbani kwao.
Mariam akiwa amelala fofofo, akasikia mtu anamuamsha, moja kwa moja alihisi kuwa ni mama yake anamuamsha ila alivyoamka alishangaa sana kuona kuwa aliyekuwa akimuamsha ni mumewe Juma.

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano nichek whatsapp 0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 19

Hapo na Mariam aliingilia kati kumkataza wifi yake asimpe jina mtoto ndipo mama Shamimu aliposema,
“Kheee Mariam, bado roho mbaya hujaacha tu hadi leo jamani! Mimi ni shangazi wa huyu mtoto, nampa jina sasa tuone mtafanyaje, kuanzia sasa huyu mtoto ataitwa Khadija”
Hapo hadi Juma aliogopa maana yule mtoto alikunja sura sana akionyesha kuwa amekasirishwa, na alikuwa amekaa kwenye kochi ila akashuka chini.
Walimuona mtoto wao akianza kumuelekea mama Shamimu sasa, kwakweli Juma aliinuka na kwenda kupiga magoti mbele ya yule mtoto huku akisema,
“Samahani mwanangu, huyu kapitiwa tu, naomba nisamehe mimi mwanangu”
Huyu mtoto hakujibu ila alirudi kwenye kochi na kupanda kukaa, ila muda huu Juma alimuangalia Anna na kumwambia tena kwa upole kabisa,
“Anna nakuomba kamlaze mtoto chumbani”
Anna hakubisha kwani aliinuka na kumbeba mtoto kisha akaenda nae chumbani yani Juma alibaki anapumua tu kwa hofu na uoga, yani kile kitendo kilikuwa kinamshangaza sana mama Shamimu ilibidi kulipotulia kidogo aiuliza,
“Jamani mbona sielewi kitu!”
Juma akamsogelea na kumshika dada yake mkono na kwenda nae nje yani mpaka muda ule Juma alikuwa haamini amini kama dada yake amepona maana asingejua cha kufanya nae baada ya kupigwa shavu.

Moja kwa moja Juma na dada yake walienda kwenye kivuli na kuongea ambapo Juma alimsihi kwanza dada yake kutokumuita jina lolote yule mtoto.
“Nakuomba dada yangu, usimuite jina lolote lile huyu mtoto wangu nakuomba sana”
“Kwanini Juma?”
“Dada, kwa kifupi mtoto wangu sio wa kawaida”
“Kivipi?”
“Ni hivi dada yangu, mara ya kwanza kabisa mama alisema kuwa mtoto aitwe jina lake la Ashura ila mke wangu aliambiwa na mtoto kuwa halitaki jina hilo ilikuwa balaa sana hapa nyumbani wakati mtoto amekataa hilo jina”
“Kheeee kipindi hiko mtoto alikuwa na muda gani?”
“Naona sijui kwenye siku nne hivi, halafu kuna kipindi mama akamuita mwenyewe Ashutra, khaaa mtoto huyu alimsonya mama yangu”
“Na ninavyosema ni kuwa yule mgeni aliyezimia Juzi ni sababu ya kumuita jina mtoto wangu ndiomana sikutaka ijirudie kabisa”
“Hebu subiri kwanza Juma, kwahiyo mtoto wako pale alipo anaongea?”
“Ndio, tena anaongea maneno yote. Sasa wewe unashangaa kwenye kuongea tu! Mbona hujashangaa kwenye kutembea?”
“Unajua kwasasa ndio kama unanifungua macho hivi! Sio kipindi kirefu kusikia kuwa mkeo kajifungua ila nilivyokuja na kumuona mtoto ni mkubwa sikuwa na tatizo lolote, ila swala la kuongea hapo ndio sielewi. Mbona sijawahi kumsikia akiongea? Halafu toka ana siku nne ana ongea jamani!”
“Nini siku nne dada!! Ni toka amaezaliwa huyu mtoto anaongea ndiomana nakwambia kuwa mwanangu sio wa kawaida”
“Kheeee basi mwanao ni mtoto wa maajabu jamani, kwanini inakuwa hivyo lakini? Wewe Juma upo kawaida, mkeo yupo kawaida ila unaenda kuzaa mtoto wa maajabu, kwanini lakini?”
“Hata najua basi dada, halafu kumbuka mimba ya huyu mtoto ilikaa miaka miwili, yani mke wangu alikaa na mimba miaka miwili ndio akajifungua”
“Kheeee mimba kama ya tembo loh!! Mambo ya ajabu haya unaniambia kaka, mnawezaje sasa kuishi na mtoto wa aina hii humu ndani?”
“Hatuna cha kufanya dada, unadhani tutafanyaje? Ni mtoto wetu unadhani tutafanyaje?”
“Tena futa hiyo kauli kaka, hiko kiumbe cha ajabu sio mtoto wenu kabisa, mnaonaje mkikitupa huko, mnaendelea kukikumbatia cha nini? Hayo ni maajabu”
“Khaaaa dada, tatizo nimeshamzoea tayari. Namtupaje wakati nimzoea, ananiogopesha lakini nimeshamzoea, ilimradi hatudhuru ndani basi hana tatizo kwetu”
“Kheeee umerogwa wewe, poleni sana. Sio mtoto huyo mliyenaye, usikute ni kajini, poleni sana”
Kisha Juma akamuuliza dada yake,
“Eeeeh dada, una mpango wa kukaa hapa hadi lini sababu hatujaulizana!”
“Weeee unadhani nina hadi lini hapa! Kesho naondoka, siwezi kwakweli hayo maajabu mbaki nayo wenyewe mlioyazoea. Tena ngoja nikapange nguo”
“Mmmmh dada”
“Hakuna cha kuguna, mkeo ni mvivu hatari. Kila leo niwe naangalia tu na kumuona amelala kila muda hakuna anachofanya, yeye kazi ni kula, kunywa na kulala. Huo ni ujinga, mwanamke gani anataka kuishi kama yeye? Hata kama mwanamke ni mama wa nyumbani ila anatakiwa ajishughulishe, kufanya kazi za nyumbani napo ni kujishughulisha ila mtu anakuwa kula kulala wa nini! Sipawezi hapa aisee”
Mama Shamimu aliagana na Juma pale na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kupanga nguo.

Wakati mama Shamimu akipanga nguo zake vizuri kwaajili ya safari ya kesho aliamua kumpigia simu mama yao ili kumwambia kuwa anaenda nyumbani,
“Mama, nakuja. Huku paenishinda, nakuja ili niishi kidogo hapo nyumbani mama yangu”
“Pamekushinda kwasababu gani?”
“Mama, haka katoto ka Juma sio katoto wala nini, katoto haka lazima katakuwa ni kajini. Nikija nitakusimulia vizuri mama yangu, niliyoyaona ni mengi halafu haya niliyoambiwa ndio nimeogopa zaidi, nakuja kesho mama nitakusimulia”
Muda huu Mariam alikuwa mlangoni kwa wifi yake kwahiyo alipomaliza tu kuongea na simu akaingia na kumuuliza,
“Kwani wifi uliyoyaona ni yapi tena?”
“Hivi nyie mnajiona mnaishi na mtoto humu ndani! Huyo sio mtoto ni jini”
“Mmmmh kwanini wifi?”
“Kama hamuamini, siku moja muite huyo mtoto wenu jini halafu uone kitu kitakavyokuwa”
“Mmmmh wifi jamani! Yani mtoto wetu tukamuite jini!”
“Khaaa, hivi Mariam hujafunguka macho tu! Hakuna mtoto hapo ni mauza uza tu hayo, nawahurumia sana kwa jinsi ambavyo mnashindwa kuamka na kuona kuwa hapo hamna mtoto”
“Kumbuka dada nimebeba mimba kwa miaka miwili”
“Hata ungebeba kwa miaka saba ila hujazaa mtoto, umezaa jini”
Mama Shamimu aliendelea kupakia nguo zake kwani alionekana kushukizwa sana na mambo yake.

Usiku ule, Juma alikaa na mke wake chumbani wakiongea kuhusu lile tukio la mtoto wao na mama Shamimu halafu na kuhusu mama Shamimu kuondoka,
“Yani najua dada yangu yule ananitangazia kila sehemu mambo yote na watu wote wayajua tu kuwa mimi nina mtoto wa ajabu jamani!”
“Ila na wewe kwanini ulimsimulia kila kitu dada yako?”
“Sikuwa na jinsi ili tu asirudie tena kumuita mtoto wetu kwa jina lolote lile Mariam, mimi nimefanya yote yale kumuokoa yeye mwenyewe unadhani angedhabwa kibao na mtoto wetu ingekuwaje? Nani angemsaidia kupona? Mimi naogopa sana toka lile tukio la Pendo naogopa sana”
“Lazima kuogopa ila ndugu zako hadi wanakera, unajua wana kiherehere sana, wanakera jamani sijapata kuona”
“Ila atatutangaza sana yule”
“Mwache tu atutangaze, hakuna cha kufanya. Hii ni aibu yetu, mtoto ni wa kwetu kwahiyo lazima tukubali kuaibika mume wangu”
Walikubaliana tu mule na kulala ingawa ukweli ulijulikana hapo kuwa jamii yote itajua ukweli ingawa ile mimba iliyokaa zaidi ya miaka miwili walikimbia kwa watu wao wa karibu na kuhamia huko mbali ili isitokee mtu kuuliza ni kwanini hiyo mimba huzai muda unapita tu, ila huku tangu wameamia hakuna mtu aliyekuwa akiwafatilia kwahiyo waliishi kwa amani ila yule dada wa Juma alimpa mashaka sana Juma kwani alijua pale kila kitu kitasemwa kwa watu tu.

Mapema kabia leo, mama Shamimu alikuwa tayari ameshajiandaa kwaajili ya kuondoka ila Juma alimtaka wanywe chai kwanza halafu ndio amsindikize ambapo alifanya hivyo, na walipomaliza ndio walivuta mizigo kwaajili ya kuondoka ila kitoto cha Juma kikawasogelea na kumwambia Juma,
“Baba, mwambie shangazi aniombe msamaha”
Kila mtu pale ndani alimuangalia mwenzie hakuna aliyeelewa na wala hakuna aliyejibu kwa muda ule, kisha baada ya muda kidogo Juma alimuangalia dada yake na kumwambia,
“Dada Khadija, nakuomba tu umuombe msamaha mtoto”
Ila mama Shamimu aling’aka pale na kusema,
“Weeee anitoleee balaa mimi, unafikiri huo ujini wake ndio utanitisha mimi!! Hii ni namba nyingine, mimi ni kisiki cha mpingo siendeshwi hovyo na mambo ya kijinga, nishwahi kuonana na wachawi macho kwa macho sembuse huo jini aliyejificha kwenye umbo la binadamu tena mtoto! Asinibabaishe mimi”
Mama Shamimu alinyanyua mizigo yake na kuwaambia,
“Kama mnataka nisindikizeni, msipotaka niacheni niende mwenyewe”
Juma hakuwa na la kufanya zaidi zaidi aliamua tu kumsindikiza dada yake huku akiwa ameambatana na Mariam ila nyumbani alibaki Anna na mtoto.

Basi waliondoka huku mama Shamimu akilalamika njia nzima kuwa mule ndani wanendekeza mambo ya kijinga,
“Yani sijaamini hata na wewe Juma umefungwa ufahamu na kile kitoto kidogo! Mimi siwezi kusumbuliwa na mtoto wa vile”
Kisha Mariam akamwambia mama Shamimu,
“Ila wifi, kwani ungemuomba msamaha ungepunhukiwa na nini?”
“Nimuombe msamaha kwa lipi? Na kwanini nimuombe msamaha? Mimi sio mjinga kama mnavyofikiria, sifanyi mambo ya kijinga mimi. Hii ni namba nyingine kabisa, kama anawachezea basi abaki kuwachezea nyie wenyewe na sio mimi kabisa”
“Mmmmh dada, sijaamini kama ungekuwa mkali kiasi hiko!”
“Nimekwambia Juma, mimi sipendi ujinga”
Basi walifika stendi ambako alipanda gari na kuwaaga na kuondoka zake, kwahiyo Mariam akawa anarudi na Juma nyumbani huku akimwambia,
“Yule dada yako shauri yake, asije kushangaa karudishwa tena nyumbani kwetu!”
“Mmmmh haiwezekani, arudishwe kivipi sasa?”
“Kimazingara kama ambavyo mimi nilikuwa narudishwa, nina uhakika ni mtoto ndio anafanya hayo mambo”
“Ila haiwezekani, kumbuka tumempandisha kwenye daladala kabisa na tumeshuhudia daladala ikiondoka!”
“Haijalishi Juma, kuna siku mimi nilienda kwetu kabisa, nikashuka hadi stendi ya kwetu nikapita njia ya kwetu kufika tu nyumbani kugonga mlango nikafunguliwa na yule msichana wetu wa kazi aliyepita, nilishangaa sana kuwa nimerudije kwangu wakati niliondoka kwetu? Halafu kumbuka kuwa kuna siku nililala kwetu ila nikaja kujikuta kuwa nimelala huku nyumbani kwahiyo kila kitu kinawezekana”
“Inamaana ni uchawi huo au!! Ila mke wangu kumbuka dada yangu kasema yeye ni kisiki cha mpingo”
“Kumbuka hata mimi niliwahi sema kuwa sirogeki na nilikuwa naamini hivyo sababu ya kinga niliyokuwa nimepewa kwa yule mganga ila mbona narogeka sasa? Mtoto ananiroga atakavyo”
“Ila mke wangu, inawezekana ikawa Anna ndio amesababisha mtoto wetu kuwa hivyo!”
“Weeee kale katoto kapo vile hata kabla ya Anna, ndiomana mimi nakukatalia kuhusu kumtoa Anna, unadhani ni mdada gani wa kazi ataweza kuishi na kale katoto? Hakuna, wacha yule yule Anna aliyemzoea”
Walikuwa wakiongea tu, ila wakati wanakaribia kufika kwao, walikutana na mmama ambaye ni jirani yao ila kwavile nyumba za pale zipo mbalimbali ilikuwa ni ngumu kuonana mara kwa mara, wakasalimiana pale ambapo yule mama akauliza,
“Kheeee kumbe ulishajifungua dada?”
“Ndio, nilishajifungua”
“Mtoto gani?”
“Wa kike”
“Aaaah!! Anaitwa nani?”
Hapa ndipo huwa paguma kwa Juma na Mariam, ila Mariam akamwambia huyu mama,
“Anaitwa mtoto”
“Aaaah sawa, nitakuja basi kumsalimia”
Walishindwa kumkatalia ilibidi tu wamkubalie ingawa walijua ni tatizo pindi akifika huko nyumbani kwao.
Basi moja kwa moja walirudi nyumbani kwao na kuendelea na mambo mengine.

Leo asubuhi wakati Juma anajiandaa kuondoka kwenda kwenye shughuli zake, alimkumbusha mke wake kuhusu alichosema kuwa dada yake angerudishwa kichawi,
“Umeona Mariam, dada Khadija haijawezekana kumrudisha kichawi. Yule dada ni mzito”
“Mzito wa wapi, mtaani kwake kwenyewe kakimbia wachawi, angekuwa mzito si asingekimbia wachawi sasa!”
“Lakini si unaona, wewe huwa unarudishwa ila yeye siku imepita na leo ni siku nyingine ila hajarudishwa, inabidi mtoto wetu tuwe tunamletea watu jeuri na wagumu kama dada yangu”
Mariam aliitikia tu, kisha Juma aliondoka zake halafu Mariam nae aliendelea na mambo yake ya kulala.

Siku ya leo, Juma alipita kwenye ile njia ambayo huwa anakutana na yule binti, nia yake ilikuwa ni kumshukuru maana lile jambo la Pendo kupona kabisa lilikuwa ni kubwa sana kwake. Ila alifika eneo lile na kusimama sana bila yule binti kutokea, kabidi aite kama yule binti alivyowahi kumwambia,
“Rafiki yake Mishi, rafiki yake Mishi”
Lakini yule binti hakutokea, alisubiri sana Juma na mwisho wa siku akaona ni vyema tu akaondoka na kwenda kuendelea na shughuli zake ila kiukweli Juma alikosa raha kabisa kwa kutokumuona yule bintiu.
Muda wa kutoka tena Juma alipita pale pale ambapo huwa anakutana na yule binti, alimuita ila yule binti hakuitika, wala hakutokezea hadi mwisho wa siku ikabidi tu Juma aondoke zake kurudi nyumbani kwake.
Juma alipokuwa njiani kurudi kwake, alikutana na yule jirani yao ambaye walikutana nae jana, walisalimiana kisha yule jirani alimuuliza Juma,
“Kwani mkeo ana matatizo ya masikio?”
“Kwanini?”
“Nilienda nyumbani kwako leo kama nilivyoahidi jana, nimepiga hodi sana tu lakini hakuna aliyenifungulia ila nikazunguka hivi na kumuona mkeo yupo shambani anapalilia mahindi, nikamuita pale lakini hakuitika wala hakugeuka aliendelea kupalilia mahindi tu”
“Duh!! Kwanini usingemsogelea umshtue?”
“Nisingeweza, nyumba yako kule nyumba si umeizungushia maua ya miba!”
Ndipo Juma akakumbuka kuwa huwezi kwenda nyuma ya nyumba yake bila kupita mlango wa mbele maana kule nyuma alipanda kote maua ya miba, kwahiyo ipo kama uzio wa mahali pale. Alimuangalia yule jirani yake na kumwambia,
“Ngoja nitamueleza hayo tu hakuna tatizo, itakuwa hakukusikia”
Basi Juma aliagana na yule jirani ila moja kwa moja Juma alijua tu ni kazi ya Anna, inamaana siku hiyo alikuwa amemuweka mkewe apalilie mahindi, yani alisikitika sana na kusema,
“Ndiomana mke wangu anachoka sana, apike, apalilie mahindi, afue, jamani huyu Anna ana nini! Nifanye nini kumtoa nyumbani kwangu? Ila nikimtoa tutafanyaje na yule mtoto? Aaaahh najikuta nikikosa hata maamuzi kwakweli”
Juma aliondoka tu na kurudi nyumbani kwake.

Leo baada ya kupata chakula cha usiku, walikaa pale sebleni wakiongea maana ilikuwa ni mapema sana kwenda kulala, Mariam alimwambia Juma,
“Mama yako kanipigia sana simu leo sijui kuna nini! Hebu mpigie”
Juma akachukua simu yake na kumpigia mama yake ambaye kwa muda mfupi tu alipokea na kuanza kuongea nae,
“Weee Juma, dada yako alisema kuwa jana anakuja ila hadi leo hajafika halafu simu yake ukipiga haipatikani”
“Duh!! Huku alishaondoka tangu jana, labda kaenda moja kwa moja nyumbani kwake”
“Hapana, Khadija hana mambo ya uongo. Huwa akisema kitu lazima kiwe kweli, hawezi kusema anakuja huku halafu aende nyumbani kwake hakuna kitu cha namna hiyo”
“Ila mama, huku tulimsindikiza hadi kituoni na alipanda daladala tuliacha daladala ikiondoka”
“Sasa atakuwa ameishia wapi? Nishaanza kupata wasiwasi, na haya mambo ya ajali jamani”
“Usiseme hivyo mama, sidhani kama amepata ajali hata hivyo ajali ingetokea tungesikia tu mama yangu. Hakuna ajali yoyote natumaini dada Khadija yupo salama”
“Sasa mbona hapatikani? Yani kutokupatikana hewani ndio kunanipa mashaka, hebu nenda mkaulizie vizuri kuhusu gari alilopanda Khadija, si unajua mama yenu nina presha jamani!”
“Sawa mama, nitafatilia na nitakupa jibu tu”
Juma akamuangalia Mariam na kumuelezea ila Mariam akamwambia mumewe,
“Kabla ya kujisumbua kwenda huko stendi kuulizia basi alilopanda wifi limekuwaje, muulize kwanza mtoto wako!”
“Kivipi?”
“Nakwambia muulize, maana dada yako aliondoka kwa mbwembwe hapa sijui kama yupo salama”
Juma alimuangalia Mariam kisha alimuangalia mwanae ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti huku akiogopa ogopa kumuuliza maana hakujua kuwa ataanzia wapi, ila alishangaa mtoto akimwambia,
“Niulize baba”
Juma alitetemeka kwanza na kumuuliza,
“Shangazi yako yuko wapi”
Kale katoto kalicheka kiasi na leo ilikuwa ni mara ya kwanza kuona kale katoto kakicheka, na kalikuwa kazuri sana hata Juma aliweza kuuona uzuri wa yule mtoto wake, ila baada ya kumuangalia kwa muda yule mtoto aliwajibu,
“Yupo hapo nje”
Juma na Mariam waliangaliana kwa mshangao, kisha Juma akainuka na kwenda kufungua mlango kweli kabisa alimkuta dada yake mlangoni akiwa na mafurushi yake huku kamshikilia mtoto wake.

Itaendelea…..!!!
 
MTOTO WA MAAJABU: 20

Juma na Mariam waliangaliana kwa mshangao, kisha Juma akainuka na kwenda kufungua mlango kweli kabisa alimkuta dada yake mlangoni akiwa na mafurushi yake huku kamshikilia mtoto wake.
Juma alimshangaa sana dada yake pale nje, ila alimshika mkono na kumuingiza ndani maana dada yake alionekana hadi akitetemeka peke yake, basi alimkalisha kwenye kochi na kumuuliza,
“Imekuwaje dada?”
Mama Shamimu alijibu,
“Njaa inaniuma sana”
Yani hakuna maelezo mengine zaidi ya kusema anajihisi njaa sana, ikabidi Juma amwambie Anna kuwa amuandali dada yake chakula, Anna alifanya hivyo kisha mama Shamimu na Shamimu walipata kula, walikula sana yani njaa inaonekana ilimshika sana ndiomana alikuwa akitetemeka.
Alipomaliza kula alidai kuwa amechoka sana anahitaji kupumzika yani Juma na Mariam hawakuelewa ni kitu gani kimempata huyu ndugu yao ila Mariam alimsaidia hadi chumbani ambako alijilaza tu na mtoto wake.
Muda huu Juma na mke wake hata walishindwa kumuuliza mtoto wao kuwa ni kitu gani kimetokea bali nao moja kwa moja waliamua kwenda chumbani kwao tu.

Juma na Mariam wakiwa chumbani waliulizana kuwa ni kitu gani ambacho kimetokea na kusababisha yale yaliyopo,
“Unadhani dada yako atakuwa kapatwa na nini?”
“Mmmh sijui kwakweli”
“Bado una imani na mtoto wetu humu ndani?”
“Bado sijui ila mtoto wetu ni mzuri sana”
“Ndio ana sura nzuri ila je moyo wake ni mzuri? Na mbona anafanya mambo ya ajabu na ya kutisha?”
“Kwenye mambo ya ajabu na ya kutisha hapo sielewi kitu, ndiomana nasema kuwa anayemtumia mambo ya ajabu mtoto wetu ni huyu mdada wa kazi”
“Ila kumbuka kuwa huyu mtoto kaanza kuwa wa ajabu kabla ya huyu mdada wa kazi! Nadhani hadi siku moja akufanyie ujinga ndio uelewe”
“Mmmh mke wangu tulale maana sielewi kitu”
Waliamua tu kulala kwa muda huu kwani muda nao ulikuwa umeenda.
Kulipokucha, Juma aliahirisha kazi zake leo kwani aliona kuwa anapaswa kumsikiliza dada yake kuwa ni kitu gani kilichompata.

Leo Juma na Mariam waliwahi kutoka chumbani ila sebule haikusafishwa kama kawaida wala chai haikuandaliwa ikabidi Mariam amuulize Anna,
“Mbona hujasafisha nyumba Anna?”
“Nimekatazwa dada”
Mariam akashangaa sana na kumuuliza Anna
“Umekatazwa? Umekatazwa na nani?”
“Na mtoto wenu dada, kaniambia nisifanye kazi yoyote leo”
“Kheeee kwanini?”
“Mimi sijui dada labda umuulize yeye mwenyewe”
“Kheee naanzaje kumuuliza jamani!”
Mariam alijikuta akimtazama yule mtoto wao ambaye alisema,
“Niitieni shangazi hapa”
Hakuna aliyejibu zaidi ya Mariam kwenda na kumuita wifi yake ambaye alifika pale huku akiona aibu kumtazama yule mtoto ambapo yule mtoto alimwambia mama Shamimu,
“Piga magoti uniombe msamaha”
Kiukweli kila mmoja pale alishangaa yani Juma ndio alishangaa zaidi ila mama Shamimu aliinuka alipokuwa amekaa na kupiga magoti mbele ya yule mtoto huku akimwambia,
“Naomba unisamehe”
Yule mtoto akamuuliza,
“Nikusamehe kwa kosa gani?”
“Kwa kukudharau mwanzoni”
Kisha yule mtoto akasema,
“Adhabu yako shangazi, kazi za humu ndani zote kwa wiki nzima utazifanya wewe ila tu mama atakusaidia kupika chakula maana mimi sitakula chakula ulichopika wewe”
Kisha kale katoto kalishuka pale kwenye kochi na kuelekea chumbani, kwakweli ilikuwa ni kitu cha kuwachanganya sana.
Mama Shamimu alikaa sasa maana hakuelewa kitu kwakweli, Juma alimuuliza
“Kwani ilikuwaje dada?”
“Hata sijui nianzie wapi jamani kuwaelezea”
“Tuelezee tu dada, anzia popote kumbuka tulikusindikiza hadi ukapanda daladala”
“Kweli kabisa ila cha kushangaza kituo cha mbele nikashuka na kuanza kurudi huku, nipo hapo pembezoni mwa nyumba yenu siku zote hizi, siwezi hata kuwaita”
“Kheeee mbona maajabu!”
“Dah yani sina hamu hapa nilipo, nimesimama kwa siku zote mbili, hakuna kukaa, hakuna kulala na wala hakuna kula sina hamu kabisa.”
“Pole sana dada”
“Asante, sina hata hamu hapa jamani!”
“Sasa hiyo adhabu utaiweza dada?”
“Nitajaribu ila nikishindwa itabidi mnisaidie”
Basi Mariam alilalamika kidogo pale,
“Yani mimi ndio sielewi, sijui ni nini huyu mtoto anataka kwangu jamani khaaa!”
Walibaki tu wakisikitika ila ilibidi wafanye maamuzi tu ya kuanza kufanya kazi kama mtoto alivyosema, kwahiyo kwa muda huu mama Shamimu alianza kusafisha nyumba yani alikuwa akifanya hii kazi huku akilalamika sana, alimlaani sana huyu mtoto alimuona ni mtoto asiyefaa kabisa.

Mchana wa leo, mama Shamimu akamuomba wifi yake apike chakula maana yule mtoto alisema kuwa chakula apikiwe na mama yake kwani hataki chakula kilichopikwa na mtu mwingine.
“Wifi jamani upike basi”
“Yani wiki yote hii natakiwa nipike jamani! Mbona hatari, nitaweza kweli mimi!”
“Utaweza tu Mariam, mbona kupika sio kazi ngumu”
“Sio ngumu kwako wifi ila kwangu ni ngumu sana, kwanza huwa sipendi mimoto moto mimi basi tu”
Kwa siku ya leo Mariam alienda kupika ila alikuwa akilalamika sana yani hadi amemaliza na wanakula alikuwa akilalamika sana.
Usiku huu Mariam alimlalamikia sana Juma maana kwake aliona itakuwa adhabu kubwa sana,
“Hivi mimi ndio niwe napika wiki nzima jamani!”
“Kwani mke wangu unalalamika nini? Kupika si kazi ya kike lakini?”
“Wapi imeandikwa kuwa kupika ni kazi ya kike? Acha zako Juma, kwa kifupi tu ni kuwa mimi binafsi siwezi kabisa kufurahia swala la kupika tena wiki yote hii!”
“Ila mtoto anataka kula chakula kilichopikw ana wewe tu!”
“Mmmmh mbona huwa anapika Anna, na mtoto anakula chakula hicho!!”
“Una uhakika gani kuwa Anna ndio alikuwa anapika?”
“Sasa apike nani wakati Anna ndio ilikuwa kazi yake?”
“Ngoja nikuulize swali mke wangu, je ni vizuri kupika ukiwa unajua kuwa unapika au kupika ukiwa hujui kuwa unapika?”
“Kivipi?”
“Hata nikikueleweshe hautaelewa sababu hutaki kuelewa”
“Sasa ndio nini hivyo Juma? Kama kusema si useme tu”
“Tulale tu sasa, naona tutabishana hadi kesho”
Mariam alimuangalia mumewe ila hakusema neno lolote zaidi zaidi alijilaza tu huku akiwa na hasira sana.

Juma akiwa kwenye shughuli zake leo, Pendo ndo alienda na kuanza kuongea nae hii ni toka kipindi kile ambacho Pendo alipata matatizo. Basi Pendo alimuuliza Juma,
“Hivi Juma, yule mtoto wako ni wa kawaida kweli?”
Hapo Juma ndio akaelewa kuwa Pendo anakumbukumbu za lile tukio ambalo lilimtokea ila Juma aliamua kujigelesha.
“Mmmmh Juma mbona hunijibu?”
“Sasa nikujibu nini? Mwanangu ni wa kawaida tu. Tuongee mengine Pendo”
“Tuongee mengine yapi? Mwanao kanizaba kibao hiko hadi niliona kifo jamani, khaaa yule sio mtoto, yule sio mtoto kabisa na jina la Pendo umbadilishe”
“Sawa nimekuelewa Pendo, ila naomba hayo mambo yaishie kwako na kwangu”
“Sasa nikwambie kitu!”
“Niambie”
“Unajua ni kitu gani nimejifunza kwa mwanao pale baada ya lile tukio?”
“Kitu gani?”
“Kumbe sio vizuri kushobokea shobokea watoto ambao huwajui, ni vyema kumfahamu kwanza mtoto unayemshobokea, yani mimi nilikuwa naona kifo hiki hapa kabisa kwa kitendo ambacho yule mtoto amenifanyia. Ila namshukuru Mungu nimepona, sasa hivi nitakuwa makini sana, ujinga wa kuvamia vamia watoto wa watu na kujifanya nawajua sana nauacha kabisa”
“Sawa ila usiseme kwa wengine Pendo, ibaki kuwa siri yet utu”
“Sawa, hakuna tatizo ila siwezi kusahau”
Juma alimuangalia tu Pendo na wala hakutaka kumuuliza zaidi maana alihisi pengine Pendo anaweza kujua na lile swala la kushikwa shavu na kupona kabisa, mwishowe ataona kamavile Juma ni mchawi kwahiyo Juma hakuendelea kuongea tena kuhusu mtoto wake.

Leo Mariam akiwa ametulia pale nyumbani, ndipo alipofika yule jirani yao, aliweza kuonana nae sababu alikuwa yupo nje kwa muda huu, yule jirani akasema,
“Bora hata nimekukuta hapa nje, najua ukikaa ndani ningegonga hadi ningeondoka”
“Karibu sana”
Basi na yule jirani alikaa pale nje na kuanza kuongea na Mariam, aliongea nae mambo mengi ya ule mtaa,
“Vipi mwanamke mwenzangu, huonekani kwenye sherehe, huonekani kwenye msiba, tatizo ni nini?”
“Dah! Sijazoea’
“Haya mambo kwani kuna aliyezoea? Tunafanya ili kuboresha ujirani, ushirikiano ni ushindi”
“Ndio lakini mimi sijazoeana na watu”
“Sasa hao watu utawazoea vipi kama unajifungia ndani? Huwezi kumzoea yoyote kama unajifungia, unatakiwa ushirikiane na watu, ukisikia harusi au msiba. Mfano majuzi tu hapo kulikuwa na msiba, ungekuja pale hata kujishughulisha kwenye kazi kadhaa kama kupika, kuosha vyombo watu wanasema kweli kuna mwanamke mwenzetu sehemu fulani hata ukipatwa na matatizo inakuwa rahisi kwa watu kuja kukuona ndugu yangu”
“Duh! Kwahiyo mtu akifika huko msibani lazima apike au aoshe vyombo!”
“Yani ni katika ujirani tu na kusaidiana kazi, unaweza fanya hata kugawa chakula ila uonekane na wewe unajishughulisha. Mbona unaongea vizuri tu wewe!! Ni lazima watu utafahamiana nao vizuri.”
Mariam akaguna tu, yule jirani akaomba maji kwahiyo Mariam akamuita Anna amletee yule jirani maji ila baada ya Yule jirani kupokea yale maji baada ya Anna kuondoka tu alimuuliza Mariam,
“Umemtoa wapi huyo binti?”
“Aaaaah ni msichana wangu wa kazi”
“Ndio, umemtoa wapi?”
“Alikuja tu mwenyewe, alikuwa ana shida na kazi”
“Kwahiyo hupafahamu kwao, hufahamu ndugu zake wala nini?”
“Hapana siwafahamu hata hivyo ni yatima”
“Hata kama ni yatima lakini lazima ana ndugu zake tu”
“Aaaah mimi naona kumfahamu yeye inatosha”
“Pole sana”
“Pole ya nini tena?”
Yule jirani alishusha chini kile kikombe cha maji na wala hakunywa wala nini badala yake alimuaga tu Mariam na kuondoka zake.

Usiku wa leo, Mariam alimsimulia mumewe Juma juu ya yule jirani yake na kile ambacho amekifanya, Juma alishangaa sana na kumuuliza vizuri mke wake,
“Kwahiyo hayo maji hakunywa?”
“Hakunyw andio, tuliyamwaga tu. Kaniuliza maswali kibao kuhusu Anna, na mwisho wa siku kaniambia pole sana”
“Namshukuru kwa hilo”
“Kwanini?”
“Labda wakija watu wa nje kama hivyo wataweza kubadili akili yako Mariam, na utaweza kutambua kuwa Anna ni binti wa aina gani, mimi kama baba wa familia naumia sana, nateseka maana ukweli wote ninaujua ila wewe unazidi kukumbatia makosa ya Anna”
“Niweke wazi nikuelewe”
“Nishakuelewesha hadi basi, Anna ni mchawi anatakiwa tumuondoe humu”
“Sawa, sasa tukimuondoa Anna, tunafanyeje na huyo mtoto wetu? Unadhani kuna ambaye ataweza kumlea huyo mtoto kama ambavyo Anna anamlea?”
“Mmmmh hapo pagumu mke wangu, ila kiukweli Anna hatufai kabisa, tena hatufai hata kidogo”
Mariam alitafakari kidogo na kumuomba mumewe tu kwa muda huo wapate kulala.

Leo Mariam alisema kuwa hatopika tena chakula, ila mama Shamimu na yeye alishachukia yani yeye kufanya kazi zote wakati mdada wa kazi yupo tu, akaamua kumpigia mama yake na kumueleza kila kitu,
“Hebu kampe simu Juma niongee nae, asiniletee ujinga mie”
Mama Shamimu alitoka chumbani na kumfata Juma sebleni aliyekuwa amekaa na mke wake ambaye alikuwa alimlalamikia kuwa amechoka kupika, Juma alichukua ile simu,
“Hivi wewe Juma una akili gani? Kweli unakubali dada yako ateseke sababu ya hiko kitoto!”
“Sina cha kufanya mama”
“Huna cha kufanya kivipi? Huo ni upuuzi huo”
“Sasa mama nifanyeje jamani!”
“Si mlisema kinaongea eeeeh! Mpe simu niongee nae”
Juma akampa simu mtoto ambaye moja kwa moja aliiweka sikioni ila baada ya kuongea kidogo tu, huyu mtoto alibamiza simu chini yani Juma alisikitika na kuokota simu ya dada yake ikiwa vipande vipande.
Mama Shamimu alichukia sana ila hakujua cha kufanya na hakuna aliyejua kuwa mtoto aliongea nini na bibi yake.
Basi Juma akaenda kuchukua simu yake na kumpigia mama yake ambapo simu haikupokelewa kwanza, alipopiga tena ndio ilipokelewa, Juma alimuuliza mama yake kuwa imekuwaje,
“Naumwa mwanangu, tena naunwa sana”
Hadi sauti ya mama yake ilibadilika kabisa, ilionekan ni mgonjwa haswa, Juma alishangaa na kuuliza,
“Kwani imekuwaje mama?”
“Mwanangu hako katoto kachawi, tumbo la kuhara limenishika uwiii ngoja niende chooni”
Yule mama akakata simu yani Juma hata hakujua ataanzia wapi.

Juma aliamua kutoka nje yeye, Mariam na mama Shamimu ili wajaribu kuongea na wajue cha kufanya.
“Hivi jamani tufanyeje? Mama nyumbani huko ni mgonjwa hoi sababu ya mtoto”
“Juma mdogo wangu, mficha maradhi kifo humuumbua”
“Sasa dada nifanye kitu gani?”
Mama Shamimu alifikiria jambo na kusema,
“Jamani, mnaonaje haka katoto tukakatupe baharini?”
“Mmmh jamani mtoto wangu tena tukamtupe baharini?”
“Mtoto wako ila huyo sio mtoto kaka, ona kama hivyo mama anaumwa ila chanzo ni huyo mtoto. Atatuua ukoo mzima”
“Tufanye nini?”
“Twende tukamtupe kaka, hii ni kwa usalama wako na usalama wa familia.”
“Ila dada kumbuka kuwa sina mtoto mwingine zaidi ya huyu tu!”
“Naelewa kaka ila utapata watoto wengine na usikute ni yeye ndio anakuzibia nafasi ya wewe kupata watoto wengine. Kubali tukamtupe huyu mtoto kaka”
Juma aliamua tu kukubaliana nao maana hadi ndugu zake walianza kumpigia simu ila wajue kuwa itakuja kuhusu huyo mtoto.

Kulipokucha kabisa, waliamka saa kumi alfajiri kabla wengine hawajaamka na kwenda chumbani kwa Anna kisha wakamchukua mtoto na kuondoka nae pale kabisa ilikuwa rahisi kwao na wala hawakupata maswali maana Anna alikuwa amelala fofofo. Walitoka nje na moja kwa moja walipanda bajaji ambayo Juma alikuwa ameikodi na kuanza kuelekea hukowalikopanga ili kumtupa mtoto, halafu mtoto alikuwa bado amelala kwahiyo hii ikawa ni furaha sana kwao.
Walovyofika baharini, Juma alikataa kumtupia ndani ya bahari alidai tu awekwe kwenye pango akiamka anaweza chukuliwa na mtu mwingine kwahiyo walifanya hivyo.
Na sasa waliamua kurudi nyumbani huku wakiweka mikakati ya kumfukuza na Anna pia, yani Mariam alikubali sababu mtoto hayupo tena.
Walifika nyumbani kwenye mida ya saa moja asubuhi, ile wanafungua mlango walimkuta Anna akimnywesha uji yule mtoto.

Itaendelea.....!!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 likes zikifika 500 tunaendeleza
 
MTOTO WA MAAJABU: 21

Na sasa waliamua kurudi nyumbani huku wakiweka mikakati ya kumfukuza na Anna pia, yani Mariam alikubali sababu mtoto hayupo tena.
Walifika nyumbani kwenye mida ya saa moja asubuhi, ile wanafungua mlango walimkuta Anna akimnywesha uji yule mtoto.
Yani kila mmoja alijikuta akitetemeka hapo nje palikuwa hapatokeki maana miguu ilikuwa ni mizito, basi Juma akajitoa ufahamu tu na kupiga magoto kisha kutembea na magoti hadi kwa yule mtoto ambapo Mariam na mama Shamimu nao walifanya hivyo, kisha Juma alianza kumwambia yule mtoto,
“Naomba utusamehe, tumekiri makosa, naomba utusamehe”
Yule mtoto akamuuliza Juma,
“Kwa kosa gani?”
“Kwa kosa la kwenda kukutupa wewe?”
Kisha yule mtoto alitabasamu na kuwaangalia na kuwauliza,
“Kwa akili zenu kabisa mlihisi kuwa mnaweza kunitupa mimi? Mlidhani mnaweza kuniondoa kwenye nyumba ya wazazi wangu? Hiko kitu hakipo, nimewasamehe kwanza kwa kifupi hamjanitupa ndiomana mnaniona hapa”
Juma aliwaangalia wenzake, kisha Juma akamwambia mtotlo,
“Ila hata hivyo hatukuwa na lengo la kukutupa ila tu nilikubali sababu nilijua kuwa una nguvu sana kwahiyo nilitaka tu kuona nguvu zako”
Mtoto akatabasamu tena na kusema,
“Ila muda mkija kugundua mlichokifanya mtajiona ni wajinga wa kwanza nyie, kwa kifupi mimi huwa sipendi kuongea sana maana nikiongea sana huwa naumwa na mbavu ndiomana mara nyingi huwa nawaangalia tu. Leo mshukuru sana nimechukua muda kuongea nanyi, kwa kifupi wewe shangazi adhabu yako inaendelea na badala ya wiki moja inakuwa wiki mbili maana umeniudhi, wewe mama unatakiwa uendelee kupika chakula cha humu ndani sababu mimi siwezi kula chakula kilichopikwa na mtu mwingine yoyote zaidi yako, halafu saivi nakupa adhabu na wewe baba kwa kuwasikiliza hawa wasiokuwa na akili, unatakiwa kila jioni ikifika unichukue mimi na kwenda na mimi barabarani na kurudi na mimi nyumbani kwa muda wa adhabu yote ya shangazi”
Juma akamuuliza,
“Na bibi yako je!”
“Adhabu niliyokupa wewe ndio itakayomponya huyo bibi”
Alipomaliza hapo ilikuwa kila wanachomuuliza hakuna ambacho anawajibu, basi wakajua ni kama alivyosema kuwa akiongea sana anaumia mbavu, kwahiyo wakatulia tu.

Muda huu mama Shamimu alienda chumbani kwake ila hakumuona mtoto wake na moja kwa moja alirudi sebleni kwenda kumuulizia maana hakuelewa kuwa mtoto wake kaelekea sehemu gani, alimuuliza Anna,
“Kwani Shamimu ameenda wapi?”
“Mmmmh sijui, sijamuona kabisa”
Kale katoto kalitabasamu tu, kisha Anna akasema,
“Hivi nyie si asubuhi mlienda kumtupa mtoto! Hamjaenda kumtupa huyo Shamimu kweli?”
Mama Shamimu aliwaangalia wakina Juma na kukaa chini kabisa kwani alihisi kuchanganyikiwa,
“Jamani inamaana kwenye lile pango ni mtoto wangu ndio amewekwa jamani!”
Mama Shamimu alitaka kutoka maana alichanganyikiwa sana, kwahiyo alitaka kwenda kumfata ila muda huu mtoto aliongea’
“Weee Shangazi usiende popote, unaendaje mahali wakati hakuna kazi uliyofanya hapa! Na wewe mama hakuna kwenda mahali, huyo mtoto aende baba tu kumfata, mkienda wote mnampoteza, siongei tena”
Waliangaliana pale na kutoka nje kwa pamoja kisha Juma akawaambia,
“Jamani, achene tu niende kumuangalia halafu nytie mbaki na shughuli zingine, tushaambiwa tukienda wote tunampoteza, ngojeni tu niende”
Hawakuwa na namna zaidiya kukubali maana aliyefanya kile kitendo ndio yeye aliyewaambia cha kufanya.
Juma aliondoka na wenyewe kurudi ndani, kwakweli mama Shamimu alikuwa na mawazo sana hadi aliwaza ni kwanini alikuja na mtoto wake huku.

Juma alirudi kweli akiwa na Shamimu yani kila mmoja pale alishangaa sana na kujiona walikuwa wajinga kwa kwenda kumtupa Shamimu badala ya kwenda kumtupa yule mtoto, mama Shamimu alimkumbatia mtoto wake na kulia sana, yani alilia kwa uchungu huku akimuomba mtoto wake msamaha na huku akikumbuka jinsi ambavyo alipanga kumtupa baharini kabisa, ni Juma tu ndio alizuia jambo hilo kutokea, yani wasingempata kabisa maana angekuwa amesombwa na maji ya bahari, kwakweli mama Shamimu alilia sana na kujilaumua sana. Kisha baada ya hapo ndio alifanya kazi za pale, na muda mfupi tu aliamua kumpigia simu ndugu yao ili aende kumchukua mtoto wake,
“Naomba uje umchukue Shamimu uende nae kwa mama, nitampoteza huku”
“Kwani imekuwaje?”
“Acha tu, nakuomba ndugu yangu uje, usiniulize maswali mengi maana sitakuwa na majibu, naomba uje nakuomba sana”
Yule ndugu yake akamuitikia tu kuwa atafika kumchukua mtoto kwahiyo hiyo mama Shamimu kidogo akapata amani ya moyo.
Baada ya hapo ndio akaweza kwenda kuendelea na kazi na siku hiyo hata Mariam aliingia kupika bila ya tatizo lolote lile.

Jioni ya siku hii kama ambavyo mtoto alimwambia Juma, basi Juma akambeba na kwenda nae kituoni kisha kurudi nae nyumbani yani huyu mtoto alikuwa akitabasamu tu.
Walivyofika nyumbani tu, Juma alimpigia mama yake ili kujua ile hali ya kuharisha kwa mama yake imeendeleaje, maana mchana alimjibu kuwa bado yupo katika hali ile ile,
“Unaendeleaje mama?”
“Jioni hii imekuwa afadhari hata tumbo nalo limepoa mwanangu”
“Pole mama, utapona kabisa”
“Naona Khadija kamuita kaka yenu hapa aje amchukue mtoto aje nae huku, kuna usalama huko?”
“Ndio mama ni salama, hata usijali”
Kisha akakata simu, hakutaka kuongea zaidi kwani alihisi huenda yule mtoto akawaongezea adhabu maana wakihisiwa kuwa wanamsema alihisi wataongezewa adhabu.
Juma alipomaliza kuongea na mama yake ndipo alipoenda kula, yani chakula kilichopikwa na Mariam kilikuwa na radha ile ile ya chakula ambacho kilikuwa kinapikwa na Anna, kwahiyo Juma alikuwa akijua tu pale ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.

Usiku wakati wa kulala, Mariam aliamua kumuuliza mume wake kabla ya mambo mengine kwani kuna maswali yeye binafsi alikuwa akijiuliza sana,
“Hivi ni kwanini yule mtoto kasema kuwa hawezi kula chakula kilichopikwa na mtu mwingine zaidi ya chakula kinachopikwa na mimi tu? Wakati huo huo kumbuka kuwa, kabla ya hapo alikuwa akila chakula kilichokuwa kinapikwa na Anna”
Juma akacheka na kusema,
“Yani mpaka hapo hujaelewa kitu Mariam?”
“Kitu gani sasa?”
“Mbona ni rahisi sana hapo, ni kuwa siku zote chakula huwa unapika wewe”
“Kivipi?”
“Kuna siku nimekuuliza hapa Mariam, je ni bora kupika ukiwa unajua kuwa unapika au kupika ukiwa hujui kama unapika? Ukaleta mambo yasiyoeleweka, ila kuna jambo nilitaka ujifunze hapo”
“Jambo gani?”
“Wewe ndiye unayepika kila siku huu ndani, Anna huwa anakutumikisha wewe kichawi. Wewe ndio mpishi wa hii familia”
“Khaaaa inamaana hadi zile chapati ni mimi nilipika? Zile sambusa na bagia je? Hii hainiingii akilini kabisa, yani mimi ndiye ninayepika kila chakula humu ndani!”
“Ikuingie akilini isikuingie ila huo ndio ukweli halisi, wewe ndiye unayepika vyakula vyote humu ndani”
Kwakweli Mariam hakuamini aliona kamavile anaota ukizingatia hajawahi hata kupata ndoto kuwa anapika halafu leo anakuja kuambiwa kuwa kile chakula huwa anapika yeye! Alishangaa sana, ila waliamua tu kulala.

Juma akiwa kazini leo, anamfikiria sana yule binti ambaye hivi siku za karibuni hajaonana nae, alijiuliza mno kuwa tatizo linaweza kuwa ni kitu gani? Ila hakupata jibu kwakweli. Basi alifanya shughuli zake kisha akatoka na kupita kwenye ile njia ambako huwa anakutana na yule binti ila alisimama kwa muda mrefu sana bila kumuona binti yoyote mahali pale, zaidi zaidi muda huu alipita mama mmoja aliyekuwa na mtoto mgongoni, yule mama umri wake ulionekana kama ni umri wa mke wake maana wlaionyesha wapo kwenye rika moja, basi Juma alimsalimia huyu dada,
“Habari yako dada”
“Salama, za wewe”
“Nzuri, huwa unapita mara kwa mara njia hii?”
“Ndio, hii ni njia yangu kila siku maana nakaa mitaa ya huku huku.”
“Samahani, mimi naitwa Juma maana hata sikujitambulisha. Sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“Mimi naitwa mama Rose”
“Samahani, mama Rose ni hivi kuna binti fulani huwa nakutana nae maeneo haya sasa nina siku nyingi kidogo sijamuona hata sijui kapatwa na nini, bora umeniambia wewe ni mwenyewe huenda ukawa unamjua”
“Binti gani?”
“Simjui jina lake ila alisema niwe namuulizia kwa jina la rafiki yake Mishi”
Yule mama Rose akatema mate chini na kusema,
“Sitaki kumsikia huyo kiumbe kabisa, sitaki kumsikia. Yani simpendi Mishi mimi na sitakuja kumpenda”
“Kwani tatizo ni nini?”
“Unaniona hapa nilipo eeeh!! Niliachana na mume wangu sababu ya huyo huyo Mishi, ni mwanaume ambaye nilikuwa napendana nae sana, nilimpa chochote alichokitaka, nilimvumilia na kumpenda kwa kila hali hata nilipojua alinisaliti bado nilimsamehe na kukubali kuolewa nae na tukabahatika kuzaa mtoto mmoja. Ila kitu ambacho sikufahamu ni kuwa muonja asali haachi kamwe, kwani kuna siku nikamfumania mume wangu kwa macho yangu akiwa na Mishi kitandani tena Mishi akiwa na mimba kubwa sana, simpendi Mishi mimi, simpendi kabisa. Yule mwanaume niliachana nae maana unaambiwa mficha maradhi kifo humuumbua”
“Kheee pole sana, huyo mtoto ndio huyo uliyezaa na mumeo?”
“Hapan, huyu ni mwanangu niliyezaa na mume wangu wa sasa, ila Mishi sina hamu nae, kajua kuisambaratisha familia yetu yule kiumbe, kajua kufanya tugombane, yani kaolewa na ana mimba lakini bado anahangaika na wanaume wengine, ptuuuuu”
Akatema mate chini kuonyesha kuwa hata kumuongelea Mishi kwake ilikuwa ni kichefuchefu, basi Juma hakuwa na budi zaidi ya kuagana nae tu ila alichukua mawasiliano yake kwani aliona kuwa kuna umuhimu wa kuongea zaidi na huyo mtu, kwani alihisi kuwa huenda anafahamu mambo mengi juu ya huyo Mishi.

Mchana wa leo, yule ndugu ambaye jana yake aliwasiliana na mama Shamimu, alifika sasa kwa lengo la kwenda kumfata Shamimu, basi aliwakuta pale na kuwasalimia ambapo Mariam alianza kumlaumu kwanza,
“Jamani shemeji kumbe hapa unapajua vizuri kabisa, na mbona hujawahi kuja hata kumuona mtoto!”
“Aaaah usijali shemeji, nilikuwa nasubiri nije rasmi”
“Ulikuwa unasubiri nini?”
“Nije kumuona mtoto mikono mitupu kweli! Nilikuwa nasubiri”
“Haya, na Ibra hhajambo?”
“Hajambo kabisa, yupo kidato cha kwanza sasa”
“Oooh hongera sana umekuza shemeji”
Basi hakuongea sana maana na yeye alishapata habari juu ya mtoto wa nyumba hii basi alimtaka tu dada yake amuandae huyo Shamimu ili aweze kuondoka nae, na dada yake alivyomaliza kumuandaa, ndipo na yeye aliinuka na kuondoka nae, ila walivyofika nje Shamimu akawaambia,
“Kuna kitu nimesahau”
“Kitu gani?”
“Sijamuaga mtoto”
Shamimu akafungua mlango na kurudi ndani kisha akampungia mkono yule mtoto ambapo mtoto na yeye alimpungia mkono huku akitabasamu, ndipo Shamimu alipotoka sasa na kuondoka, wakati huo mama Shamimu na Mariam walikuwa wakiwasindikiza.
Basi njiani walimuuliza Shamimu,
“Mbona ulirudi kumuaga yule mtoto?”
“Sababu nampenda halafu vile vile unawezaje kuondoka mahali bila kumuaga mwenye nyumba!”
“Kheeee, kwahiyo yule ndio mwenye nyumba?”
“Ndio, si nyumba ya wazazi wake ile? Yeye ndio mwenye mali sasa, lazima tuage ili tufike salama tuendako”
Mama Shamimu alihisi tu Shamimu atakuwa anakumbuka kile kisanga cha wao kusimama kwa siku mbili bila kula wala kulala.

Juma aliporudi tu nyumbani kwake, akashusha mizigo na moja kwa moja kumbeba mtoto ili kwenda na barabarani maana jioni ilishafika ila mtoto alimwambia,
“Sibebwi na mtu mchafu, nenda kaoge”
Yani hadi Juma alijihisi aibu, alimshusha mtoto na moja kwa moja kwenda kuoga, akabadili nguo ndio akambeba na kuondoka nae kwenda nae stendi kama ambavyo aliambiwa.
Alizunguka nae na kuanza kurudi nae nyumbani ila muda huu alikukutana na yule jirani yao ambaye alimsalimia Juma,
“Kheee huyo ndio mtoto wenu?”
“Ndio yeye”
“Hongera sana, una mtoto mzuri hadi raha, yani mwanao ni mzuri sana”
Basi huyu jirani alikuwa akiongea neno moja anamsifia mtoto kuwa ni mzuri, kila akiongea kidogo anamsifia mtoto kuwa mzuri sana huku Juma akimshukuru tu kwa zile sifa zake ila muda kidogo wakati yule jirani karudia kutoa sifa, ndipo yule mtoto aksema,
“Hakuna mtoto mbaya, kila mtoto ni mzuri”
Yule jirani hadi alijihisi aibu maana hakujua kama huyu mtoto anaongea, kile kitendo kilimfanya yule jirani amuage Juma tu na kuondoka zake maana ilikuwa ni aibu mno kwake.

Usiku ule Juma aliamua kumuelezea mke wake kuhusu yule jirani yao na kile ambacho aliambiwa na mtoto wao yani Mariam alicheka na kusema,
“Ndio akome, kheee mtu gani anatoa sifa kwa mtoto kiasi hiko, kidogo tu mtoto mzuri, kidogo tu mtoto mzuri hadi anakera bora tu kajibiwa alizidi loh!!”
“Ila kwani ni vibaya kutoa sifa?”
“Ni vibaya ndio, na hao ndio huwa wachawi wenyewe, anamsifia kila mara halafu anataka kufanya yake. Yani yeye kashakupongeza kuwa una mtoto mzuri, sasa kila mara kumpa sifa, anataka kugundua kasoro yake au ni nini? Hapo ndio amekoma mjinga sana huyo jirani, ana kimbelembele sana”
“Jamani mke wangu!!”
“Ndio, mwache akome na umbea wake, jirani gani mara aje aseme oooh sijui huyu mdada wako wa kazi kimeenda kimerudi, muache akome”
“Mmmmh!! Haya mke wangu”
Juma hakuwa na mengine ya kusema ingawa bado alikuwa na mawazo sana juu ya yule mama Rose aliyekutana nae, alijikuta akitamani kweli kumfahamu zaidi alijikuta akitamani kweli kufahamu undani wa mambo ulivyo ila sababu alichukua mawasiliano yake akaona haina tatizo sababu atamtafuta tu.

Leo mapema kabisa walivyoamka, Juma aliondoka zake halafu walibaki mama Shamimu, Mariam, Anna na mtoto pale nyumbani ila Mariam alitamani sana kula samaki kwa siku ya leo.
“Yani natamani samaki, basi Anna tutaenda wote ila mtoto muache”
Mama Shamimu akadakia,
“Kheee halafu mimi ndio nibaki nae jamani! Hapana nendeni nae tu”
“Aaaah basi nitaenda peke yangu”
Yani leo Mariam alitaka kuongozana na Anna tu nkwani kuna mambo alihitaji kumuuliza haswa mambo ya yeye kupika maana yalikuwa yanampa changamoto sana.
Basi alienda kujiandaa na moja kwa moja alienda kwenye samaki na huko alipata samaki anaowataka ila wakati anarudi alikutana na binti ambaye alimkumbuka basi alimsogelea na kukumbatiana nae kisha kusalimiana na kumwambia pale,
“Kheeee umekuwa mkubwa jamani Neema”
“Ndio dada nimekuwa”
Basi Mariam alivyomshika Neema mkono akaona pete na kumuuliza,
“Kheee ni pete ya uchumba hii au urembo?”
Neema alitabasamu na kumwambia Mariam.,
“Ni pete ya uchumba dada nimekuwa, baada ya miezi miwili ni harusi yangu”
“Kheeee unaolewa?”
“Ndio dada naolewa, mwanaume kashajitambulisha nyumbani, kashalipa mahari na kama hivi kashanivalisha pete. Mipango ya ndoa ipo moto moto kwasasa, kwahiyo baada ya miezi miwili tu naolewa”
“Sasa mwali jamani unazunguka!”
“Nipo kazini dada ila mwezi ujao nachukua likizo”
Basi Mariam alianza kumshawishi Neema pale apafahamu nyumbani kwake,
“Naomba twende ukapafahamu nyumbani kwangu tu na umlete mama yako, nimewakumbuka sana. Nakumbuka kipindi mama yako akija nyumbani na kulalamika kuhusu wewe, ila saivi umeshakuwa mkubwa hadi raha, naomba twende mara moja tu halafu utarudi kwenye shughuli zako”
Neema hakuona tatizo kwenda kupafahamu nyumbani kwa Mariam kwahiyo aliongozana nae huku wakiongea nae kwa furaha.

Neema na Mariam walifika nyumbani kwa Mariam huku Mariam akimkaribisha ili aingie ndani maana Neema alitaka aishie tu nje,
“Hapana usiishie nje, karibu ndani utie baraka mdogo wangu”
“Lakini sitakaa sana”
“Sawa nimekubali, karibu mdogo wangu”
Basi Mariam alifungua mlango na kuingia ndani na Neema, muda huu Anna nae alikuwa ametoka jikoni kwahiyo walikutana macho kwa macho na Neema, yani Neema alishtuka na kusema,
“Mungu wangu, nimekutana na wewe uwiiiii ndio ndoa yangu inayeyuka hivi!”

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 likes 500 tunaendelea
 
MTOTO WA MAAJABU: 22

Basi Mariam alifungua mlango na kuingia ndani na Neema, muda huu Anna nae alikuwa ametoka jikoni kwahiyo walikutana macho kwa macho na Neema, yani Neema alishtuka na kusema,
“Mungu wangu, nimekutana na wewe uwiiiii ndio ndoa yangu inayeyuka hivi!”
Mariam hakumuelewa kabisa, ilibidi amuulize,
“Neema una maana gani?”
Neema na yeye alimuuliza Mariam,
“Dada umemtoa wapi huyu? Ni mchawi wa wachawi huyu”
“Kheeeee kivipi?”
“Nimejuta hata kukutana na wewe, nimejuta hata kukueleza kuwa nakaribia kuolewa kwani najua ndoa yangu ndio imeyeyuka tena sijui hata kwanini nilikueleza, ni mchawi sana huyu msichana, yani Anna nakwambia ndoa yangu ikipotea Anna, nitakufanyia shughuli”
Yani Mariam alikuwa akishangaa tu, Anna na yeye alikuwa yupo kimya tu kanakwamba yale anayoambiwa hayamuhusu, kisha yule Neema akasema,
“Mimi naondoka dada, ila nkama nikipatwa na tatizo lolote lile basi ni huyu mchawi ndio amelisababisha”
Kisha Neema aliondoka bila kusema neno lingine, muda huu Mariam alijikuta akiangaliana kwa muda na Anna yani Mariam hakummaliza kabisa Anna, na swali la kwanza kabisa alimuuliza,
“Anna, wewe ni mchawi?”
Anna alikaa kimya kwa muda na kujibu,
“Hapana mimi sio mchawi dada”
Mariam alimuangalia sana Anna na kumuuliza tena,
“Anna, wewe ni mchawi?”
Anna alijibu vile vile kuwa yeye si mchawi, mama Shamimu na yeye akasogea pale na kusema,
“Yote yaliyoongelewa nimeyaona na kuyasikia, Anna kuwa mkweli. Wewe ni mchawi, yani siamini kuwa nimekimbia uchawi wa nje nilipotoka halafu nimekuja kukutana na uchawi ndani”
Anna aliwaangalia na kujibu tena,
“Hapana, mimi sio mchawi”
Hata walivyokazana kumlazimisha bado alikataa kabisa kuwa yeye sio mchawi kiasi cha kwamba walishindwa hata cha kufanya na kubaki kwa hasira zaidi.

Muda huu mama Shamimu na Mariam walitoka nje na kuongea kuhusu Anna maana yale waliyoyasikia yalikuwa na maana kubwa sana kwake.
“Sasa wifi tufanye kitu gani?”
“Yani mimi ukiniuliza cha kufanya nitakujibu kwa jibu moja tu wifi kuwa tumfukuze, maana mimi kwa kawaida huwa siwezi kuishi na mtu asiyeeleweka kiasi hiki, yani mtu haeleweki mbele wala nyuma halafu niishi nae hapana kabisa siwezi kufanya hiko kitu”
“Kwahiyo tumfukuze?”
“Ndio Mariam, utaiushije na mwanamke mchawi? Halafu kama ulivyosema kuwa sio mara ya kwanza hii, ushashangalia na watu mbalimbali kuhusu huyo mdada wa kazi, hata mumeo ameshasema mara kadhaa kuhusu huyo mdada wa kazi, ni kufukuza tu hakuna namna hata kidogo”
“Naafikiana na wewe wifi halafu nimeanza kuhisi kitu huenda alikuwa akinifanyisha kazi kichawi huyu mjinga”
“Ndio hivyo ila kwasasa ndio kajifanya kufurahi tu baada ya yule mtoto kutupa adhabu ila yule binti ni wa kuondoka, tena leo leo”
Mariam na mama Shamimu wakakubaliana hivyo, na wakakubaliana kuwa Juma akirudi waongee vizuri na kumfukuza kabisa.

Juma aliporudi tu, pale pale Mariam hakungoja hata aingie chumbani kwani alianza kumuelezea kuhusu binti aliyefika nae leo, yani Juma alitikisa kichw atu na kusema,
“Ila mimi nilikuwa nakwambia Mariam, huyu binti ni mchawi. Unaona yale mahindi pale nje, umepanda mwenyewe, umepalilia mwenyewe hata yemanza kuzaa ni nguvu zako mwenyewe, humu ndani ulikuwa ukisafisha nyumba mwenyewe na ukipika mwenyewe”
“Duh!!”
“Usishangae ndio hivyo, huyo binti ni mchawi ndiomana mimi simtaki ila ukakazana kuwa mimi sijui nimewahi kumtaka kimapenzi, hivi mimi nikitake hiko kibinti kweli!! Bora leo umeamka Mariam, fanyeni mnachotaka kufanya ila swala la mimi ni kuwa huyu binti aondoke humu ndani”
Anna alikuwa amekaa kimya tu huku akiangalia chini, kisha Mariam akarudia swali kama la mchana,
“Anna, wewe ni mchawi?”
Anna nae akarudia jibu lile lile,
“Hapana, mimi si mchawi”
Hapo mara yule mtoto akaongea,
“Anna, kubali tu ukweli kuwa wewe ni mchawi na uwaulize wanataka nini baada ya kugundua uchawi wako!”
Kimya kilitanda ila Mariam alijitoa muhanga na kujibu,
“Tunataka aondoke”
Kale katoto kalitabasamu kisha kakasema,
“Yani na wewe mvivu bila aibu unajibu tunataka aondoke, utanilisha wewe, utaniogesha wewe, utakuwa unalala na mimi? Utanihudumia wewe! Kama vyote hivi huwezi basi Anna haondoki hapa kwa amri zenu bali ataondoka pindi tu nitakapotaka mimi. Haya na wewe baba ni muda umefika wa kwenda na mimi barabarani, ila nenda kaoge kwanza”
Juma hakusema neno zaidi zaidi alienda kuoga huku Mariam na mama Shamimu wakiwa wanaangaliana tu bila ya jibu.

Muda huu Juma alikuwa ameondoka na haka katoto na kwenda nako kituoni kama kawaida yake halafu nyumbani walibaki mama Shamimu, Mariam na Anna, hapo hapo mama Shamimu na Mariam wakaungana na kuanza kumpiga Anna huku wakimwambia,
“Wewe si mchawi sana eeeh! Haya tufanyie huo uchawi wako mjinga mmoja wewe”
“Na hapa utaondoka tu, eti kale katoto kamekutetea. Jua hii ni nyumba yangu na mume wangu, sio mali ya yule mtoto kabisa kwahiyo hapa utaondoka”
Mama Shamimu alimburuta Anna na kumtoa nje kabisa huku akimtaka Mariam kwenda kumtolea mizigo yake Anna apate kuondoka.
Kwakweli mama Shamimu alimsema sana,
“Yani unajifanya mtu kweli, unajifanya mpole mwenyewe kumbe hakuna lolote. Ujinga ujinga tupu, huna hata jipya unawaza ujinga tu, unawaza uchawi tu, mtoto mdogo kama wewe kuwa mchawi hata haipendezi, huo uchawi utakusaidia nini? Hadi watu wanakuogopa wanahofia ndoa zao zitayayuka sababu ya uchawi wako!! Na humu ndani utaondoka tu, huna nafasi kabisa humu ndani”
Mariam alipeleka mzigo wa Anna pale nje huku akisema kwa kubana sauti,
“Ooooh sijui nimefukuzwa, ndugu zangu hawanitaki, watakutaka vipi wakati wewe ni mchawi! Nani atakutaka wakati wewe ni mchawi namba moja! Nenda tu, begi lako hilo ulilokuja nalo”
Anna hakujibu ila alimuuliza swali Mariam,
“Dada, kumbuka uliniahidi kuwa utakuwa dada yangu hadi mwisho wangu”
“Ndio mwisho wako umefika, sina undugu na wachawi mimi”
Anna akainuka kama kutaka kuondoka ila akamuona Juma akirudi na mtoto kisha Anna akasema,
“Mkombozi wangu huyo anakuja”
Mama Shamimu na Mariam walikaa kimya, yule mtoto alivyofika na Juma alionekana kuwa na sura ya hasira sana ila hakuongea kitu bali alishuka kwa baba yake na kumshika mkono Anna kisha kuingia nae ndani, kwahiyo pale nje Juma aliwauliza,
“Imekuwaje tena na nyie?”
Wakamsimulia kisha akawaambia,
“Mmeyataka mengine jamani, mimi sihusiki kabisa na mambo hayo”
Kisha Juma aliingia zake ndani huku Mariam na mama Shamimu wakiwaza kuwa ni kitu gani kitaendelea baada ya hapo.

Mpaka muda wanalala, yule mtoto hakusema jambo lolote lile, kwahiyo walienda kulala tu ila kiukweli Mariam alikuwa na mawazo sana kwani alikuwa anawaza ni jinsi gani alimuamini Anna halafu kuja kujua mambo kama haya, kwakweli alikosa amani kabisa moyoni kwake hata usingizi hakuupata vizuri, alimuamsha mumewe na kumuuliza,
“Hivi Juma ulijuaje kuwa Anna ananitumikisha mimi?”
“Sikia nikwambie, radha ya chakula cha Anna ni radha ya chakula chako halafu kuna siku niliwahi kukukuta chumbani na muda huo huo nikakuona upo nje ukilima”
“Kheee kivipi?”
Juma alimuelezea ilivyokuwa, kwakweli Mariam alibaki kushangaa tu ni kama akili zake kwasasa ndio zilikuwa zinarudi, Juma alimkumbusha hadi kile kisa cha wao kuwa macho kwa usiku wote halafu na kitu ambacho Anna alipika, ndio Mariam alizidi kufunguka ufahamu wake,
“Halafu ni kweli Juma, jamani binti kanitumikisha huyu balaa”
“Pole mke wangu, ila nafurahi sasa akili zimekurudia vizuri mke wangu”
“Asante, sina raha kabisa kumuamini shetani dah!”
Basi Juma muda huu alimbembeleza mke wake tu ili wapate kulala.

Mapema kabisa Juma alienda kaze kwenye shughuli zake, huku wakina Mariam wakibaki nyumbani na majukumu yao, ila walivyomaliza wakati wamekaa tu yule mtoto akaongea,
“Jamani, mimi nilishawaambia kuwa huwa sipendi kuongea sana sababu naumwa na mbavu. Mama na shangazi mmeniudhi sana siku ya jana, hivyo basi, shangazi adhabu yako haitaishia wiki mbili tu bali itaenda mwezi mzima”
“Kheeeeee!!”
Kale katoto kaliendelea kuongea,
“Na hata baada ya shangazi kuondoka, wewe mama ndiye utakayechukua majukumu ya nyumba nzima”
Yani Mariam hata hakujua alie au afanye kitu gani ila alichojua kufanya kwa muda huo ni kujuta kumpata huyu mtoto katika maisha yake.
Halafu kila mmoja aliendelea tu na majukumu yake huku Anna ndio akibaki na yule mtoto yani Anna hakuwa na kazi yoyote kwa kipindi hiki zaidi ya kubaki na mtoto tu.

Juma akiwa kwenye shughuli zake leo alijikuta akiwaza mambo mengi sana, cha kwanza kabisa alimuwaza yule mama Rose na aliwaza ukaribu wa mama Rose na Mishi, basi aliwahi kutoka na kumpigia mama Rose ili apate kuongea nae,
“Samahani dada, je tunaweza kuongea?”
“Sawa hakuna tatizo.”
Basi yule mama Rose alimuelekeza Juma mahali ambako angemkuta yeye ambapo Juma alifanya hivyo na kumfata mama Rose ili apate kuongea nae, na kweli alikutana nae ambapo alimuelekeza, na kuanza kuongea nae,
“Unajua nini, siku ile sikukuelewa vizuri kuhusu Mishi”
“Kwani wewe Mishi yupi unayemfahamu? Ndio huyo niliyemuongelea?”
“Mmmh inawezekana maana unayoyasema kama yanashahabiana”
“Hebu niambie vizuri halafu mimi nitakueleza”
“Kipindi cha nyuma nilioa mke aliyekuwa akiitwa Mishi ila mke huyu alinifanyia vituko sana, naweza kukusimulia hadi ukanionea huruma”
“Kwahiyo yuko wapi sasa?”
“Sijui na wala huwa sipendi kumuongelea ila tu nilipenda kujua kuwa wewe Mishi umemfahamu vipi?”
“Si nimekwambia jinsi ilivyokuwa, yani huyo Mishi alitembea na ndugu zangu, katembea na mchumba wangu, katembea na mume wangu, tena nikaja kumfumania akiwa na mimba kubwa tu huku akiwa kitandani na mume wangu, yani huyo Mishi ni mpuuzi mmoja asiyejielewa kabisa”
“Pole sana, ila kuna kitu huwa kinanitatiza sana kuhusu huyo Mishi”
“Kitu gani hiko?”
“Kipindi namuoa, sikujua kama ana mimba, ila kuna mtu alitokea na kusema kuwa Mishi alibakwa na kupata ile mimba, nilijitahidi kuukwepa ukweli ila ilishindikana, na Mishi aliambiwa kuwa aache kuchanganya wanaume ila kuna makosa alifanya akapotea kabisa na mimba yake, mara nyingi sana nimejikuta nikitamani kujua ni kitu gani kimeendelea katika maisha yake”
“Ila hata mimi sijui alipo, kwani huna mke kwasasa?”
“Mke ninaye, ila mke wangu hajui kabisa habari za Mishi”
“Sikia kaka, najikuta nikitamani kumfahamu mke wako”
“Kwanini?”
“Basi tu, natamani kumfahamu”
Juma hakuwa na kinyongo ila alikubaliana nae kuwa atamtafuta siku nyingine ili aweze kumpeleka kwake kwenda kumfahamu huyo mke wake, na muda huo Juma aliagana na yule mama Rose.
Muda huu wakati Juma akiwa anaelekea nyumbani kwake, alikutana na Pendo njiani ambapo Pendo alimsalimia na kumuuliza pale,
“Unajua leo umeondoka mapema sana, sikujua kama ningekutana na wewe njiani!”
“Kweli nimeondoka mapema, ila najitahidi niwahi nyumbani, kwani saa ngapi saa hizi?”
“Ni saa moja kasoro kumi hii”
Juma alishtuka sana kuona muda umeenda sana, alimuaga Pendo kwa haraka haraka na kuondoka kwani alikuwa na kile kibarua cha kumpeleka mtoto wake barabarani, sasa muda ulienda vile aliona ni balaa na aliona wazi kuwa atachelewa.

Na kweli Juma alichelewa kufika nyumbani kwake leo, kwani aliingia kwake kwenye mida ya saa mbili usiku, kitu cha kwanza kabisa alimuulizia mtoto maana hakumkuta pale sebleni,
“Mtoto yuko wapi?”
“Amelala tayari”
Juma akapumua kwa kuona kuwa mtoto amelala, basi akaamua tu na yeye kula, kuoga na kwenda kulala huku akijiambia kuwa mtoto atampeleka kesho yake.
Ila usiku ule alikuwa na maswali mengi sana kuhusu mama Rose, na alikuwa akijiuliza ni kwanini huyu mwanamke anataka kumfahamu mke wake? Hapo hakupata jibu ingawa alitamani sana kujua kuwa ni kwanini ipo hivyo.
Aliwaza na kupitiwa na usingizi tu, ila kwenye mida ya saa nane usiku, Juma alishtushwa na mlio wa simu yake na kuamua kuichukua akakuta ni mama yake ndio anampigia, alipopokea alishangaa maam yake kuongea kuwa anaumwa sana,
“Nini tatizo mama?”
“Nilikuwa mzima tu, hata nimeshangaa nikianza lile tatizo la kuendesha yani najihisi kila kitu mwilini kimeisha”
“Dah!! Pole mama yangu”
“Asante, tafuta jitihada nipate msaada Juma hata wa kwenda hospitali. Hali yangu ni mbaya sana”
Juma alikata ile simu na kujikuta akikumbuka kauli ya yule mtoto kuwa kitendo cha yeye kutoka nae hadi stendi na kurudi nae ndio itakuwa tiba ya mama yake, basi muda huo huo Juma aliinuka bila kujali kuwa muda umeenda sana.
Alienda hadi chumbani kwa Anna na kufungua mlango kisha akambeba mtoto na kutoka nae nje, yani hakujali ni usiku wala ni nini.
Alitembea na mtoto yani palikuwa ni kimya kabisa, hakuna sauti ya mtu wala kitu gani, ni yeye tu Juma aliyekuwa akitembea huku kambeba mtoto ila alikuwa akitembea kwa tahadhari kubwa sana.
Alitembea hadi stendi ambako nako palikuwa kimya kabisa, kisha ndio akaanza safari ya kurudi yani alikuwa mwenyewe njiani, ila alijivika ujasiri tu wa kutembea muda ule.
Hadi alifika nyumbani kwake, moja kwa moja alimriudisha yule mtoto chumbani akiwa kalala vilevile halafu na yeye ndio alirudi chumbani kwake.
Moja kwa moja Juma alichukua simu yake na kumpigia mama yake,
“Mama, unaendeleaje?”
“Kwakweli Juma umekuwa kama dawa yangu, huwezi amini ile hali kwasasa imekata kabisa”
“Ooooh mama, nashukuru sana kusikia hivyo maana nilikosa hata raha kabisa mama yangu”
“Pole mwanangu, usiku mwema”
Juma sasa ndio aliweza kuagana na mama yake na kuweza kulala sasa.

Leo, mama Shamimu akimuita pembeni Mariam na kuongea nae maana hata yeye binafsi kuna vitu ambavyo alikuwa haelewi,
“Hivi Mariam ngoja leo tuongee, naomba tuongee kirafiki yani hata sio kama mawifi”
“Ndio, nakusikiliza”
“Hivi Mariam kabla ya kubeba mimba ya mtoto huyu hukutumia dawa za kienyeji kweli?”
“Wifi sikia, unakumbuka jinsi uzazi wangu ulivyosumbua? Ila sikuthubutu kutumia madawa ya kienyeji”
“Mbona mtoto katoka hivi! Kuwa mkweli Mariam ili upone, ili tujue ni wapi tunaaniza kuhusu swala la huyu mtoto”
“Kweli dada, labda tu wakati mimba imekaa bila kuzaa ndipo nilipozunguka kwa wataalamu na kutumia madawa mbalimbali ili niweze kujifungua ila iligonga mwamba hadi ile dawa ambayo mama aliniletea”
“Alisema ameitoa wapi?”
“Sijui aliitoa wapi ila ile dawa ndio iliyonisaidia mimi hadi kuweza kujifungua wifi yangu”
“Kwa hili kuna umuhimu wa kuongea na mama ili tujue ni kitu gani kilifanyika maana haya mambo haya dah!! Hadi sielewi yani, nadhani kuna jambo tunatakiwa kufanya Mariam”
Wakakubaliana pale kuwa watamuuliza vizuri kuhusu ile dawa iliyomsaidia Mariam kwani walihisi huenda ikawa ni msaada juu ya yule mtoto.

Sababu Juma alihitaji sana kujua ni kwanini mama Rose anataka kumfahamu mke wake, basi leo leo akampigia simu na kumuomba kuwa atembelee nyumbani kwake,
“Basi uje kunichukua pale tulipokuwa tunaongea”
“Sawa hakuna tatizo, nakuja kukufata”
Juma aliacha shughuli zake na moja kwa moja kwenda kumfata mama Rose ambapo alimsubiri ndipo mama Rosr alitokea ila leo alikuwa yeye peke yake bila mtoto, ikabidi Juma amuulize,
“Mtoto yuko wapi?”
“Aaaah nimemuacha nyumbani, naenda huko kwako sijui nitakutana na watu gani, macho ya watu nayo sio mazuri kwa watoto”
“Aaaah kumbe!”
Kisha Juma akaongozana nae huku wakiendelea na maongezi mengine kwa muda ule.
Muda huu, Juma alifika nyumbani kwake na mama Rose ambapo alipomkaribisha ndani tu kulikuwa na Mariam ambaye alionana na mama Rose halafu mama Rose akasema,
“Kheeee huyu si ndio rafiki yake Mishi!”
Juma alishangaa kwani yeye hajawahi kufikiria kama huyo Mishi na mke wake wanafahamiana.

Itaendelea…..!!!
Kwa mawasiliano au kuipata full nichek whatsapp 0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 23

Muda huu, Juma alifika nyumbani kwake na mama Rose ambapo alipomkaribisha ndani tu kulikuwa na Mariam ambaye alionana na mama Rose halafu mama Rose akasema,
“Kheeee huyu si ndio rafiki yake Mishi!”
Juma alishangaa kwani yeye hajawahi kufikiria kama huyo Mishi na mke wake wanafahamiana.
Juma alimuangalia mama Rose na kumuuliza,
“Kwani mnafahamiana?”
Rose akajibu,
“Ndio, namfahamu vizuri huyu. Kuna siku yeye na Mishi walikuja kunichamba”
Mara alitoka Anna chumbani, yani kufika pale sebleni mama Rose alishangaa sana na kusema,
“Kheeee hii nyumba kumbe inafuga majinamizi! Kwaherini”
Mama Rose alitoka ila Anna alimfata nje huku akimkimbilia na kumuita,
“Dada, dada, dada”
Mama Rose alisimama huku akiwa na hasira maana hakutegemea kumuona Anna pale, basi Anna alimsogelea na kumwambia,
“Dada usinitende hivi!”
“Mjinga wewem ambia uchawi wako ndio usikutende hivi, unajua mimi sina makosa wala yoyote hana makosa ila ni huo uchawi wako!”
“Ila mimi ni mdogo wako dada”
“Hata kama ila ondoa huo uchawi wako kwanza”
“Kumbuka mimi sijapenda kuwa hivi, ni mama ndio kanifanya hivi”
Mama Rose hakutaka hata kuongea zaidi kwani aliondoka zake na kumfanya Anna arudi tu nyumbani, akainama kwenye kochi huku machozi yakimtoka.
Kwa mara ya kwanza Mariam tangu ajue kuwa Anna ni mchawi, leo alimuonea huruma, alimfata na kumuuliza vizuri,
“Weee Anna, yule ni nani yako?”
“Ni dada yangu, kabisa yani dada yangu kabisa”
“Aaaah kumbe!! Sasa imekuwaje mbona akuite jinamizi?”
Anna hakuona aibu kuongea, bali aliongea tu, muda huu ni kama aliona liwalo na liwe,
“Ni sababu ya hilo hilo swala la mimi kuwa mchawi, sikupenda ila imetokea nipo hivi”
“Duh! Kwahiyo Anna uchawi umeutoa wapi wewe?”
“Kwa mama, yani mama ndio aliyenirithisha mimi uchawi”
“Kwahiyo Anna wewe ni mchawi kweli?”
“Ndio dada, mimi ni mchawi. Ndugu zangu wote wamenitenga sababu ya uchawi wangu, hakuna anayehitaji kuishi na mimi sababu ya uchawi”
Yani muda huu Mariam alijikuta akimuogopa Anna zaidi maana alijidhihirisha wazi kuwa ni mchawi na wala hakumuhoji sana kwani alimuacha tu na kwenda kwenye mambo mengine.

Jioni ilipofika, Juma kama kawaida yake alimbeba mtoto wake na kutoka nae maana ilikuwa ni adhabu kwake kwahiyo alikuwa hawezi kuacha bila kuifanya adhabu hiyo maana akiacha tu basi mama yake ataanza kuumwa, kwahiyo mama Juma alikuwa hajui ni kitu gani kinachoendelea kwa mwanae.
Alienda na mtoto wake hadi stendi kama kawaida halafu na kuanza kurudi nae, ila leo walikutana na yule jirani akiwa ameongozana na mtu mwingine ambapo yule jirani alisimama pale ili kumtambulisha jirani mwenzie kwa Juma,
“Huyu ni jirani yetu”
Basi yule jirani mwingine moja kwa moja alimuangalia mtoto ambaye Juma kambeba na kuanza kusema,
“Kheee una mtoto mzuri jamani, tena mzuri sana”
Yule jirani wa kwanza akasema,
“Watoto wote ni wazuri jirani”
“Hata kama, ila peye sifa anastahili kutoa sifa”
“Mmmmh shauri yako, endelea tu na hizo sifa zako”
Ila mtoto alikuwa kimya tu akiwaangalia huku yule jirani mwingine akiendelea kumwambia Juma,
“Hongera sana jirani, mimi nina mtoto wa kiume nadhani itafaa tukijenga undugu maana utakuwa mkwe wangu”
Juma hakutaka hizi mada kwani mtoto wake alimjua vizuri sana, kwahiyo alikuwa akimzuia jirani kwa hizi mada ili zisiendelee,
“Jamani mimi nina haraka”
Yule jirani akasema tena,
“Mbona swala la kuwa mkwe hujalijibu jirani!”
Yule mwenzie akasema,
“Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama, na wewe hebu tulia ukwe gani na mtoto bado mdogo!”
Juma akaondoka zake na kuwaacha wale majirani wakibishana wenyewe, yani leo Juma aliona mtoto wake kajistai sana maana bila kujibu kitu ni jambo la ajabu sana kwa mtoto huyu.

Usiku wa leo, Juma na mke wake walipokuwa chumbani ilibidi Juma amuulize vizuri kulingana na yale madai ya Mishi,
“Samahani mke wangu, huyo Mishi unamfahamu wewe?”
“Hapana, simfahamu Mishi wala nini ila yule dada hata nimemshangaa, sijui ana mapepo loh!”
“Hana mapepo yule, huenda umefanana na mtu anayemfahamu Mishi vizuri!”
“Labda ila mimi simfahamu Mishi kabisa”
Kisha Mariam alianza kumueleza mumewe kuhusu Anna kuwa yule ni dada yake,
“Yani leo Anna kanidhihirishia wazi kuwa yeye ni mchawi, tena anasema kaupata kwa mama yake. Na yule aliyekuja leo ni dada yake”
“Duh!! Ila dunia ni duara jamani, sema nini ukweli nitaujua tu”
Waliongea ongea pale na kuamua tu kulala.

Siku ya leo, Mariam anaamka na kumuita Anna mapema kabisa, kisha akaongea nae maana alijihisi kuchoka sana,
“Anna mdogo wangu sikia, kiukweli nimechoka sana kupika, naomba leo mdogo wangu unisaidie”
“Ila mtoto hatopenda dada”
“Ndio, ila Anna si huwa unapika chakula kama changu jamani! Naomba unisaidie, chakula cha mchana tu ila pika moja kwa moja hadi jioni. Pika pilau”
“Mmmh dada, sijui kupika pilau”
Mariam alishangaa sana na kumuangalia Anna, kisha akamuuliza,
“Sijakusikia vizuri, umesemaje Anna?”
“Sijui kupika pilau dada”
“Kwahiyo lile pilau ambalo ulikuwa ukirupikia ni nani anakuwa amepika?”
Anna alikaa kimya hapo, kisha Mariam akamwambia,
“Anna, hata sihitaji maneno mengi. Naomba tu upike hilo pilau, leo nimechoka sana, nahitaji kulala mie”
“Mmmh dada jamani”
“Hakuna cha jamani hapa!”
Kisha Mariam akaondoka zake, yani alikuwa amesahau kabisa hoja ya mumewe kuwa ni yeye ndiye huwa anapika badala ya Anna.

Juma alikaa kwenye kazi yake ila bado aliona kuna umuhimu wa yeye kuzungumza na mama Rose, basi aliamua kumpigia simu ili aonane nae,
“Naweza kuonana na wewe!”
“Ndio unaweza ila sitokuja tena nyumbani kwako”
“Sawa, nitakuja mimi huko”
Muda huo huo, Juma aliondoka pale na kwenda kumfata mama Rose ambapo alikutana nae na kukaa nae kuanza kuongea nae,
“Samahani kwa leo, nilitaka nikuulize kuhusu yule mke wangu unasema ni rafiki yake Mishi kivipi?”
“Hiyo kivipi sijui ila mimi najua ni rafiki yake Mishi, nishawahi kumuona nae mara nyingi tu”
“Kwahiyo mimi nimeoa mtu na rafiki yake?”
“Ndiomaana yake, inamaana yule hajui kama umewahi kuishi na Mishi?”
“Hapana hajui, sikia nikwambie ipo hivi. Mimi kipindi cha nyumba nilikuwa na sura ya kuzeeka sana hadi walianza kuniita mzee Juma na ndio jina lililozoeleka kwangu, ila licha ya utu uzima sema kuna mambo ambayo yalinizeesha”
“Mmmmh kuna mambo yalikuzeesha kivipi?”
“Ni historia ndefu ila kuna mtu alifanya nirudi katika hali ninayotakiwa kuwa nayo na hii ni baada ya kumuacha Mishi, na hapo nikamuoa Mariam, ila ukimuuliza Mariam kama niliwahi kuoa atakukatalia. Mimi ni mkubwa ila sio mkubwa kama vile ambavyo nilizeeka”
“Duh!!”
“Haya, hebu niambie ni kweli ni yule yule mke wangu ndio rafiki yake Mishi?”
“Ndio, kwanini nidanganye? Nataka nini kwako?”
“Haya, na vipi kuhusu yule Anna! Kweli ni mdogo wako?”
“Ndio, yule ni mdogo wangu ila ni mchawi wa wachawi”
“Kaupata wapi uchawi?”
“Kwa mama yetu, mama alikuwa ni mchawi sana. Ila hatukujua, sema alikuwa ni mchawi hadi anafuga misukule ila alitupenda sana halafu alimpenda sana Anna, kumbe ndio kampa uchawi”
“Mmmmh sasa mama yenu yuko wapi?”
“Alikufa, yani tumepata shida maana nyumba yetu iliungua na kufanya trukose makazi ila tulichofanya ni kuuza ule uwanja halafu hela tulizopata tulienda kujenga nyumba sehemu nyingine na kuishi huko”
“Sasa imekuwaje huyu mdogo wenu hamuishi nae?”
“Siwezi kuishi nae kabisa, nikikwambia alichokifanya hata wewe huwezi kuniambia kuwa niishi nae, ni kweli samehe saba mara sabini ila Anna hasemeheki kabisa, siwezi kumsamehe mimi”
“Kwani alifanyeje?”
“Kwetu, mimi ndio wa kwanza kuzaliwa halafu mama alizaa mapacha wakiume tupu, na wa mwisho ni Anna, ila mtoto mjinga yule wakati tunaishi nae si amewaua wale mapacha kiuchawi”
“Duh!!”
“Kafanya mimi niwe sina ndugu maana ukoo mzima walitutenga, na mimi nikamfukuza na kuuza eneo lile kisha kwenda kuolewa, nilichukia sana kwa alichonifanyia yule mjinga na uchawi wake, hivi mtu kama huyo unamsamehe vipi jamani!”
“Dah!! Kwakweli hapo sina usemi kabisa yani. Huna kosa hapo mama Rose”
Basi Juma hakuwa na ya ziada ya kuendelea kuongea na huyu mama Rose, bali alimuaga na kuondoka zake.

Kama kawaida jioni ya leo, Juma alimbeba mtoto wake na kwenda nae kituoni kama ambavyo aliambiwa ila leo alikutana na yule jirani wa jana ambaye inaonekana aliambiwa jambo kwani hata kumsalimia Juma hakumsalimia mpaka pale Juma alipomuita na kumsalimia,
“Mbona jirani unapita tu bila ya kunisalimia?”
Yule jirani alimuangalia Juma ila hakumjibu kwani aliondoka zake, kisha Juma alijikuta tu akimuangalia mtoto wake kwani alimuhisi kama anataka kusema neno vile ila hakusema neno lolote.
Juma akaondoka na mwanae, kufika njiani walimkuta yule jirani kajikwaa na kuanguka, kwahiyo alikuwa chini akiugulia maumivu, hapo Juma alimuuliza,
“Tatizo nini tena jirani?”
“Nimejikwaa”
“Pole sana jirani, ila ilikuwaje?”
Kabla yule jirani hajajibu, yule mtoto wa Juma akasema,
“Akiwazacho mjinga ndicho humtokea”
Yule jirani alimuangalia yule mtoto kisha alimuangalia Juma na kusema,
“Kweli bhana, mimi ni mjinga yani nakubaliana na huyo mtoto kabisa, jana niliambiwa kuwa huyu mtoto anashushua sana. Leo sikutaka kuwasalimia ila nikawaza huenda mbele nikaanguka halafu wakanikuta itakuwaje? Na kweli nimeanguka na mmenikuta, kweli mimi ni mjinga, tena ni lofa, sirudii tena kuwaza ujinga”
“Pole sana”
Juma alimsaidia kuinuka pale, kisha kuagana nae na kurudi nyumbani kwake yani hakuna ambacho Juma alikuwa akiongea na huyu mtoto zaidi ya kwenda nae na kurudi nae.

Muda wa kula, Juma alipokula tu aliuliza maana alijua wazi ni mkewe kapika ila mke wake ndani alimwambia kuwa chakula cha siku hiyo kimepikwa na Anna, basi Juma akauliza,
“Kwani chakula kapika nani?”
Mariam akajibu,
“Kapika Anna”
Mama Shamimu akasema,
“Weeee wifi wewe, kapika Anna muda gani wakati nilikuona wewe upo jikoni ukipika! Tena leo hukutaka hata kuongea na mimi!”
Mariam akaweka kijiko chini na kumuangalia Anna kisha akasema,
“Yani Anna umediriki kunifanyia uchawi tena!”
Hapo ndipo Juma alipopata nafasi ya kuongea vizuri sasa,
“Mtu ameweza hata kuwaua ndugu zake ambao kazaliwa nao pamoja, sembuse wewe asiyekufahamu aliyekupata ukiwa na meno yote mdomoni. Yani kaua watu waliokuwa wakimsaidia kimaisha, waliomlea toka udogoni, sembuse kukutesa wewe mke wangu mvivu! Hapo hebu tumia akili tu kuwa huyu Anna hafai”
Mariam alichukia sana hadi aliacha chakula akataka kuondoka ila mumewe akamrudisha,
“Mke wangu, utasusaje chakula ulichopika mwenyewe! Hebu acha hizo Mariam, kwanza kumbuka kuwa wewe huwa hususi”
Mariam akafikiria kweli kuwa huwa hasusi hovyo haswaa kususa chakula hiyo kwake ilikuwa haipo kwahiyo alikaa na kula ila alikuwa na kinyongo sana na Anna.

Usiku ule, Mariam aliongea tena na mumewe kuhusu swala la kumuondoa Anna, maana alitaka yule Anna atoke kabisa katika maisha yao,
“Sasa mke wangu unadhani huyu Anna tutamtoaje?”
“Sijui ila nataka aondoke kabisa kwenye maisha yetu”
“Mmmmh sijui yani”
“Nenda kaongee na yule dada yake kuwa aende huko kwake”
Juma alimueleza mke wake kuhusu yule dada alivyomwambia hadi ile habari ya kuua ndugu zake wengine na kumfanya Mariam awe kimya tu huku akijilaumu kwa kusema,
“Yani ni mimi niliyemkaribisha vizuri yule binti ndio nimesababisha”
“Ndio ni wewe Mariam”
“Nadhani ni uvivu wangu ndio umesababisha yote haya”
Juma alitabasamu na kusema,
“Ooooh leo umejua eeeh!!”
“Tuachane na hayo, tulale tu maana nina mawazo sana”
“Ila mke wangu nahitaji”
“Hebu nitolee balaa mie, unaona kabisa nina mawazo kibao, hata hatujui ni jinsi gani tutaondokana na huyu mchawi halafu unaniambia habari za kuhitaji! Sitaki bhana”
Juma hakuwa na cha kusema zaidi ya kumuitikia mke wake tu kisha waliamua kulala tu kwa muda huu.

Leo asubuhi wakati Juma anaenda kazini, akaona ni vyema apitie ile njia ambayo huwa anakutana na yule binti maana alitamani sana kuyapata yale majani ambayo yalimsaidia sana kwenye swala la mke wake.
Alifika pale Juma na kuangalia sana, na kuita sana ila hakuitikiwa, hadi roho ilimuuma akakosa raha kabisa ila alipokuwa anashangaa shangaa akaona kama kuna maua yenye majani ya kijani sana kwa mbele kidogo, akafata pale na kukuta karatasi imeandikwa,
“Chuma maua haya”
Basi moja kwa moja Juma aliinama na kuyachuma na kuyaweka mfukoni, alisubiri maelekezo lakini hakupata ikabidi ajiongeze tu maana yale maua yalifanana na yale yale maua ambayo alipewa awali na yule binti kuwa ndio yanaweza kumsaidia katika swala zima la kulala na mke wake. Alifurahi huku akisema kimoyomoyo,
“Leo, nitamkomesha Mariam maana anachonifanyia sio kabisa”
Alikuwa akitabasamu huku akiondoka na yale maua.

Leo Mariam wakati anapika chakula cha mchana akajisahau na kuweka chumvi nyingi sana, kwahiyo wakati wa kula ilikuwa ni gumzo kwani kila mmoja alikuwa akilalamika kuwa chumvi ni nyingi hadi wifi yake akamwambia,
“Hivi Juma ndio ataweza kula chakula hiki kweli wifi?”
“Kwanini asiweze sasa? Hiki chakula ni cha moja kwa moja, siingii mara mbili jikoni mimi”
“Wifi, yani ungempikia tu mumeo chakula kingine. Umezidisha sana chumvi humu!”
“Kwani yeye hajui kama kuna kukosea? Sipiki tena”
“Mmmmh ila kwa unavyomfanyia sio vizuri, kumbuka yeye ndio baba wa familia, halafu yeye ndio mtafutaji wa kila kitu humu, angetakiwa kuwa anakula vizuri, hata kama sisi tukila visivyoeleweka lakini sio baba mwenye nyumba Mariam”
“Usinipangie maisha wifi”
Anna alichukua chakula kwenda kumlisha mtoto ila yule mtoto kabla ya kukila alimuita Mariam kwa sauti kubwa,
“Mama”
Mariam akageuka na kumuangalia,
“Nenda kanipikie chakula kingine”
Hapo Mariam hakubisha wala kukataa ila alikuwa na hasira sana, akainuka na kwenda jikoni akabandika chakula ila akapanga kuwa chakula hiko ndio atakijaza chumvi nyingi.
Basi akiwa anapika, akachukua chumvi ili ajaze, ila alishangaa kuona akishikwa mkono ni kama mtu anamzuia kuweka chumvi.

Itaendelea……!!!
 
MTOTO WA MAAJABU: 24

Hapo Mariam hakubisha wala kukataa ila alikuwa na hasira sana, akainuka na kwenda jikoni akabandika chakula ila akapanga kuwa chakula hiko ndio atakijaza chumvi nyingi.
Basi akiwa anapika, akachukua chumvi ili ajaze, ila alishangaa kuona akishikwa mkono ni kama mtu anamzuia kuweka chumvi.
Mariam alishtuka huku akiwa amejawa na hofi kwani wazo lake moja kwa moja lilikuja kuwa mtoto yule ndio kamshika mkono, yani Mariam hata aliogopa kumuangalia ila akasikia sauti ya Anna ikimwambia,
“Mtoto kasema usimuwekee chumvi nyingi maana ukirudia atakufanya kitu cha ajabu ambacho hujawahi kufanyiwa”
Mariam alipumua na kumuangalia Anna, kisha akashusha ule mkono wake wenye chumvi, halafu akamuuliza Anna,
“Kwahiyo wewe huwa unafanya maongezi kabisa na huyo mtoto?”
“Aaaah na mimi naishi nae kama mnavyoishi nae humu maana huwa hapendi kuongea, na anaongea pale anapojisikia tu kuongea na si vinginevyo”
“Mmmmh haya”
Basi Mariam alimalizia kupika, na kupakua kisha kumpatia Anna ili akampatie yule mtoto, ambapo Anna alifanya hivyo.
Mariam alikaa jikoni weee akitafakari, yani alijikuta akikosa jibu kabisa, na kujiuliza maswali mengi sana kuwa kile kinachotokea kwake ni kitu gani? Hakuwa na jibu, aliamua tu kutoka ambapo alimkuta Anna akimalizia kumlisha yule mtoto basi mtoto alimuangalia Mariam na kumwambia,
“Asante mama”
Yule mtoto alisema huku akitabasamu ila Mariam alikuwa kimya tu kwani kiukweli hakumpenda kabisa huyu mtoto.

Jioni kama kawaida, Juma anambeba mtoto wake na kwenda nae kwenye matembezi kama ambavyo alimriwa na huyu mtoto.
Ila leo wakiwa stendi, kuna rafiki yake Juma alitokea na kusalimiana pale na Juma huku akimuangalia yule mtoto wa Juma hadi Juma alimuuliza,
“Mbona unamuangalia sana?”
Ila yule rafiki wa Juma alimuuliza swali Juma,
“Ni mwanao huyo?”
Juma alikaa kimya kidogo na kujibu,
“Ndio ni mwanangu”
“Mbona umejifikiria kwanza ndio umejibu, sio mwanao nini?”
“Hapana ni mwanangu”
“Mmmmh!!”
“Mbona umeguna?”
“Huyo mtoto sio wa kawaida Juma”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Mimi huwa naona mambo mengi sana, mimi nilichanjiwa kwahiyo vitu vingi sana naona. Huyo mtoto sio wa kawaida, unamuona mzuri ila hana uzuri wowote, na hiyo sura yake kuna sura ya mtoto mwingine ameichukua”
Juma akashtuka, ingawa anajua maajabu ya huyu mtoto ila hakutegemea kukutana na mtu halafu akasema vile, Juma akamuangalia yule mtu na kumuuliza,
“Wewe kwanini usingeniita peke yangu kuniambia hayo? Maana kama kuna tatizo unasemaje mbele ya muhusika?”
“Kwani anasikia?”
“Ndio, anasikia na kuongea”
“Ila hakuna tatizo sababu mimi sijasema uongo. Huyo mtoto ni wa ajabu, mimi namuona kwa macho mengine kabisa. Nimeshindwa kukaa kimya, huyo sio mtoto Juma ni kitu kingine kabisa”
“Mmmmh tuishie hapo ndugu yangu”
“Yani ningekuwa mimi ndio wewe baada ya kukwambia hivi ningemrusha huyo mtoto nikimbie yani wewe huna mashaka, umembeba tu jamani!!”
Juma alimuangalia huyu rafiki yake na kumuuliza,
“Huogopi matatizo wewe?”
“Matatizo anisababishie nani? Huyo mtoto uliyembeba, thubutu, mimi ni wa tofauti Juma huwa siogopi kitu chochote, simuogopi kiumbe chochote katika ulimwengu huu, kwahiyo hakuna cha kunibabaisha kabisa”
Yani Juma alitamani kweli hivi alivyoambiwa na rafiki yake, alitamani ajue ni kitu gani katumia hadi hana uoga maana na yeye alitaka kutumia ili mtoto yule asiwababaishe tena. Basi akamuuliza huyu rafiki yake,
“Umetumia nini mwenzangu hadi huna uoga?”
“Nimekwambia mimi ni mtu wa tofauti sana, babu yangu mimi alikuwa anaogopewa na kijiji kizima, unadhani ni nani mwenye uwezo wa kushika wajukuu zake? Mimi ni wa tofauti Juma”
Mara mtoto wa Juma akamwambia Juma,
“Baba, tuondoke”
Yani pale Juma ndio akapata ujasiri zaidi kuwa huyu mtu ni kiboko hadi mtoto hataki kubaki pale ila Juma aliendelea kusimama pale kwani alitaka kujua vitu vingi kwa yule mtu, akamuuliza tena,
“Na mimi naweza kupata msaada huo?”
Mtoto akarudia tena kumwambia Juma,
“Baba, tuondoke”
Yule rafiki wa Juma akacheka na kumwambia Juma,
“Umeona!! Mtoto kaanza kuniogopa mwenyewe, mimi ni taifa lingine, na huyo mtoto asingekuwa na uwezo wa kuishi kwenye ukoo wangu”
Juma akataka kumuelezea pale jinsi mimba ya yule mtoto ilivyokuwa, basi alianza kumwambia,
“Yani mke wangu alibeba mimba ya huyu mtoto miaka miwili na mwezi mmoja, halafu…….”
Kabla hajamalizia yule rafiki yake alianguka chini na kuanza kutapatapa, Juma alishtuka na kutaka kumshika ila mtoto akamkataza,
“Baba, tuondoke mbona unapenda nifanye matatizo kila muda! Nimekwambia muda mrefu tu tuondoke maana sikutaka kumtesa rafiki yake, ningemuacha tu aendelee kujisifia ila kuniacha hapa kwa muda mrefu umenitia hasira, tuondoke sasa”
Muda huu Juma alimuomba mwanae,
“Nakuomba basi nimsaidie”
Mtoto akamjibu,
“Msaada wangu ni wewe kuondoka mahali hapa, ila ukiendelea kuwa hapa huyo rafiki yako atakufa hapo hapo”
Juma aliogopa na kuamua kuondoka tu na mtoto wake huku akitikisa kichwa, kiukweli alikuwa akiumia sana kwenye moyo wake.

Juma hakumsimulia yoyote kuhusu lile tukio la leo, ila usiku ulivyofika aliamua kumuomba mkewe unyumba ambapo mkewe kama kawaida yake ya visingizio, yani hata siku hiyo alikuwa na visingizio,
“Juma mimi nachoka sana, kupika ni kazi ngumu. Halafu leo kile kiumbe chako kimeniingiza jikoni mara mbili”
“Kisa nini?”
“Chakula cha mwanzo niliweka chumvi nyingi sana, kile kiumbe hakijakubali hadi nimepika tena”
“Aaaah kumbe kile chakula kingine kilipikwa muda mwingine, ila kilikuwa ni kitamu sana”
“Unafurahia mimi kutumikishwa eeeh!! Na mimi nimechoka sikupi unyumba”
Juma hakubishana sana na mke wake maana alikuwa na yale maua, alimsubiri tu alipojilaza alienda kumnusisha na muda ule ule ni Mariam mwenyewe aliyehitaji kwa mume wake na kumfanya Juma afurahi sana kwa lile jambo lililotokea, hata alisahau kila kitu kuhusu yule rafiki yake ambaye walikutana nae njiani.
Yani kulipokucha Juma alikuwa na furaha sana, basi Mariam alikaa huku akimsema mume wake,
“Unajua sio vizuri hivyo unavyofanya”
“Sio vizuri kivipi?”
“Huwezi kumlazimisha mtu mapenzi, unatakiwa ukubaliane na mtu anapokwambia kuwa amechoka, mimi nimekwambia kuwa nimechoka Juma halafu wewe unakuja kunilazimisha mapenzi kweli! Tunalala bila ridhaa yangu, unajua kuwa umenibaka?”
“Hivi Mariam hata unavyosemaga hivyo sikuelewi, mimi ni mume wako, na hutaki kunitendea vile inavyotakiwa halafu unasema nakubaka, unajua hata watu wakikusikia watacheka sana”
“Watacheka! Subiri, nitakufungulia kesi wewe!”
“Ukishafungua hiyo kesi mimi nitachukua video kuonyesha kuwa ni wewe ndiye ambaye huwa unahitaji halafu utaona pale itakuwaje”
“Khaaaa na mimi nawaambia kuwa huwa unanifanyia uchawi”
“Serikali haiamini uchawi labda useme lingine, naenda kazini mke wangu ila nimefurahi sana”
Mariam alikuwa na hasira, hakufurahia wala nini kwahiyo hakumuitikia.

Leo Juma akiwa kazini, kuna rafiki zake walikuwa wakiongea na wengi walikuwa wakizungumzia maswala ya wanawake ambao huwa wanawanyima unyumba waume zao, wengine wakasema wanawake wa hivyo ni kuwaolea mke mwingine,
“Yani mwanamke akiwa hivyo dawa yake unamuolea mke wa pili tu, akili itamkaa sawa”
Mwingine akasema,
“Hata usipomuolea mke wa pili, huyo dawa yake mtake kila siku hadi akili imkae sawa, yani hata akisema anabakwa kwanza nani atamsikiliza, unabakwa vipi ndani ya ndoa wakati ni tendo lililoidhinishwa! Kwahiyo dawa ndio hiyo, hapo ndio atajua kumbe ninavyomfanyia hivi mume wangu sio vizuri, mara nyingine kuongeza wake nyumbani kujiumiza kichwa tu maana hawa wanawake akili zao wanazijua wenyewe, yani mtake kila siku, akichoka aombe talaka aende kwao, hapo ndio unaoa mwingine, sio kumuweka ndani asiyekuwa na faida wa kazi gani? Kama kachoka aende kwao”
Ile mada kwakweli ilikuwa inamgusa sana Juma, ila yeye asingeweza kutumia nguvu kwa mke wake kwani anamtambua vizuri mke wake alivyo, ila yeye alikuwa akijiambia kuwa atatumia yale maua kila siku hadi mkewe akili imkae sawa, yani alikuwa akijisemea hivyo huku akitabasamu tu hadi wenzie wakamuuliza ila aliwaambia anatabasamu tu hakuna lingine.

Muda huu Mariam alikaa na wifi yake mama Shamimu akiongea nae kuhusu Juma kwani alikuwa amechukizwa sana na hiki kilichotokea. Basi akamuelezea kisha mama Shamimu akamwambia,
“Yani Mariam huna hata aibu kuniambia mambo ya namna hiyo?”
“Sasa aibu ya nini? Kama kaka yako kanibaka nisiseme?”
“Hivi unajua kubakwa wewe Mariam?”
“Ndio, kubakwa ni kufanya tendo bila ridhaa, na mimi sijaridhia kwa anachonifanyia”
“Wewe umezidi na ungepata wanaume wasumbufu ungejuta wewe, yani kumbania hivyo kaka yangu ndio nini? Wewe ushaolewa nae, kubali majukumu ya ndoa”
“Mimi nitafika mbali kwa hili kwakweli”
“Fika tu huko mbali, sisi tunataka wadogo zake na huyo mtoto wenu. Kitu gani sasa kumbania mdogo wangu!”
“Mimba ya kubeba miaka miwili siitaki”
“Haya, ila acha kaka yangu afurahie mema ya ndoa yake”
Mama Shamimu hata hakuwa na sababu ya kuendelea kumsikiliza wifi yake na yale malalamiko yake kwani aliyaona kuwa hayana maana yoyote ile.

Siku ya leo wakati Juma ametoka na mtoto wake kama kawaida yao, yani walivyofika stendi tu mtoto wake akamuonyeshea eneo Juma na kumtaka wakakae hapo,
“Baba, twende kukaa hapo”
Juma hakubisha kwani alienda kukaa pale na mtoto wake kisha yule mtoto akamuuliza Juma,
“Kitu gani kilikufanya umuoe mama?”
Juma alimuangalia yule mtoto na kumjibu,
“Sababu nampenda sana”
“Na kitu gani kinachofanya mama akunyime unachostahili?”
Juma alishangaa kidogo kwa swali hili ila akajibu na kusema,
“Sijui”
“Mimi najua”
“Niambie ni kitu gani?”
“Nitakwambia hadi pale mama atakapopata mdogo wangu”
“Kivipi?”
“Namaanisha kuwa ukazane sasa sio unamchekea tu”
Juma alimshangaa huyu mtoto wake, alimuangalia kwa makini sana na kumuuliza,
“Kwani wewe ni nani?”
Mtoto akacheka na kumuangalia baba yake kwa makini huku akimuuliza,
“Unataka kunijua?”
Juma alitetemeka kidogo na kuhofia ila alimjibu,
“Ndio, nataka kukujua”
“Mimi ni mtoto wako ila kuna siku utanitambua vizuri zaidi”
Juma akapumua kisha yule mtoto akasema,
“Sipendi kuongea sana, tuondoke hapa. Halafu baada ya wiki mbili njoo tukae eneo hili hili kuna kitu utaona”
Muda huu Juma hakujibu kitu bali alimbeba mtoto wake na kuondoka nae.

Usiku ulipofika, Juma alitumia tena yale maua kwaajili ya kulala na mke wake, na ilikuwa rahisi kama siku zote, Juma hakujali kabisa malalamiko ya mke wake kwani kila siku alikuwa akimfanyia hivi hadi wiki ilipita akiwa anamfanyia hivi.
Yani Leo Mariam aliamka akiwa amechukia sana na ile asubuhi asubuhi akamwambia Juma,
“Naenda kumwambia mama, siwezi kukubali kabisa huu ujinga unaonifanyia Juma”
“Sio ujinga, sikufanyii ujinga ila wewe ndio unanifanyia ujinga”
“Nakwambia naenda kuwaambia halafu utaona itakavyokuwa”
Alijiandaa na kuondoka zake, yani Juma akapata mawazo hapo kiasi kwamba alitoka sebleni bila ya kwenda hata kwenye shughuli zake kwani anamjua fika mama yake Mariam alivyo na akipewa malalamiko kama yale, yani Juma akawa na mawazo sana ila mtoto akamwambia,
“Usiwaze baba”
Juma akamuangalia kama anataka kumwambia kuwa nisiwaze wakati mke wangu kaenda kutoa aibu yangu, ila mtoto akamwambia kabla hata hajatamka yale maneno,
“Sikia baba, yule mama haendi popote. Wewe nenda tu kwenye shughuli zako na ukirudi endeleza mchezo hadi kieleweke baba”
Juma alimuangalia huyu mtoto, tena alimuangalia sana ila hakusema jambo zaidi ya kwenda kuvaa pia na kwenda kwenye kazi zake.

Mariam alifika hadi stendi huku akiwaza yale mauzauza ya mtoto wao kuwa huenda akamrudisha nyumbani, alijiuliza sana kuwa afanye kitu gani ili asirudishwe? Hakuwa na cha kufanya, aliona bora aende hivyo hivyo na kama akirudishwa basi itakuwa bahati mbaya.
Ni kweli alipanda gari na leo alifika hadi kwao, tena kwao kabisa alipogonga mlango alifunguliwa na mama yake ila mama yake alionekana kuwa na hasira sana na kuanza kumwambia Mariam,
“Kwa kitendo ulichofanya kipindi kile sina hamu kabisa”
“Aaaah jamani mama, hayo si yaliisha lakini?”
“Hayajaisha, nimechukia sana, hivyo sitaki hata uwe unakuja kuja hapa nyumbani”
“Kwanini mama?”
“Nikiwa na shida nitakuja mwenyewe ila sitaki kabisa wewe uwe unakuja, nadhani unanielewa Mariam”
Kisha mama yake akafunga mlango, hapo Mariam aligonga sana, aliita sana bila ya kufunguliwa, ikabidi tu ageuze na kurudi nyumbani kwake.
Alipofika tu nyumba ni kwake alishangaa kupokelewa na tabasamu toka kwa mtoto wao, Mariam alikaa kimya tu huku mtoto akimwambia,
“Bora umerudi mama, nina njaa”
Mariam hakujibu kitu ila alipitiliza jikoni kwenda kupika, kwakweli alikuwa na hasira sana ila alipika tu kumridhisha yule mtoto ila hakuwa na furaha wala nini.

Juma hakukutana na malalamiko yoyote maana alihisi kuwa huenda angepigiwa simu na mama mkwe wake, kwahiyo alifurahi sana kuona ni kimya na hivyo aliendelea na mambo yake kama kawaida.
Ilipita wiki nyingine ambapo leo Juma alijiandaa mapema kabisa kwenda kazini ila Mariam alikuwa amelala maana alionekana kuchoka.
Juma akiwa anataka kutoka mtoto wake akamwambia,
“Hongera baba”
Juma alitamani kuuliza hongera ya nini ila kabla hajauliza, mtoto akamwambia,
“Mdogo wangu anakuja, hongera”
Juma hakusema neno zaidi ya kuondoka, njiani ndio akawaza kuwa huenda Mariam ni mjamzito tayari, akatabasamu maana ile ndio ilikuwa furaha yake.
Akiwa njiani vile vile, akachukua simu yake na kumpigia mama yake ambaye kwa muda mfupi tu alipokea ile simu,
“Niambie mwanangu”
“Mama, nina furaha sana maana mke wangu ni mjamzito”
“Kheeee kwanini mmeamua kufanya hivyo lakini?”
“Kwanini mama?”
“Mariam hakutakiwa kubeba ujauzito hadi tufanye tambiko, mnaona sawa kwa yule mtoto wa ajabu mliyenaye ndani! Mbona huwa hamfikirii nyie, kwahiyo mnapenda vile eeh!! Mwanangu hadi leo yupo huko kwenu akihenyeka na kazi sababu ya huyo mtoto wenu mwenye mambo ya ajabu halafu bila kupanga jambo lingine kabla ya kutokea mnaenda kubebeshana mengine tena!”
“Jamani mama, nilidhani utafurahi?”
“Sikia, ni kweli watoto ni baraka ila sio kwa ule uzao mliotuletea. Kwanza Mariam kakubali vipi? Amesahau mimba aliyoenda nayo kwa miaka miwili na kuzaa kituko cha dunia yani Mariam kasahau kabisa ndani ya muda mfupi huu na kubeba mimba nyingine! Mimi kama mimi siafikiani na hilo jambo maana ilitakiw alifanyike tambiko kwanza”
“Nisamehe mama, sasa tutafanyeje?”
“Ngoja niongee na baadhi ya wazee nitakwambia, ila mimi sijapenda kabisa. Huo ni ujinga, nilikaa na Mariam alinielewa maana nilimuelewesha vizuri kabisa halafu eti mnakuja kuniletea habari hizo kweli!! Mbona mnataka tuikimbie jamii jamani! Kwanini kutujazia watoto wa ajabu?”
“Nisamehe mama”
Mama Juma alikata simu kwani hakupendezewa na ile habari kabisa tofauti na jinsi ambavyo Juma alifikiria kuwa mama yake angependa kupata ile taarifa.

Juma aliporudi nyumbani kwake, alikumbuka ahadi ya yule mtoto kuwa baada ya wiki mbili ampeleke ile sehemu ambayo walikaa, na hapo wiki mbili zilikuwa zimeshapita, kwahiyo alivyofika nyumbani tu akajiandaa na kuondoka na yule mtoto.
Moja kwa moja alienda kukaa nae kwenye lile eneo, yule mtoto alitabasamu kuona baba yake kakumbuka alichomwambia kisha akamwambia baba yake,
“Baba, angalia nyuma kuna zawadi yako”
Juma aligeuka na kushangaa sana.

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano nicheck whatsapp 0629980412 ili uweze kupata full story!!!
 
MTOTO WA MAAJABU: 25

Moja kwa moja alienda kukaa nae kwenye lile eneo, yule mtoto alitabasamu kuona baba yake kakumbuka alichomwambia kisha akamwambia baba yake,
“Baba, angalia nyuma kuna zawadi yako”
Juma aligeuka na kushangaa sana.
Ila alijikuta akitabasamu kuona alichokiona kwani alimuona yule binti ambaye huwa anakutana nae njiani, sema alimshangaa kiasi na kujikuta akiuliza,
“Ni mtu wa kawaida wewe?”
Yule binti alitabasamu pia na kusema,
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Mmmmh siku zote sijakuona pale ninapokuonaga!”
“Ningekuwa sio mtu wa kawaida basi ungeendelea kuniona, hukumbuki kuwa ulichukua nguvu zangu ziende kumponya Pendo!”
Juma alikumbuka hapo kuwa toka lile tukio la kupeana mkono na huyu dada ndio pale ambapo hakumuona tena ingawa Pendo alipona, basi Juma akamuuliza,
“Kama ni mtu wa kawaida wewe, unapata wapi hizo nguvu?”
“Kwani watu wa kawaida hawana nguvu? Waganga wanapata wapi nguvu? Watabiri nao wanawezaje kutabiri? Je sio watu wa kawaida?”
Juma alitulia na kumuuliza tena,
“Mwanangu unamfahamu kama nani?”
“Hilo sitakwambia mimi bali atakwambia mwenyewe kwa muda wake ukifika ila mimi nimefurahi sana kukuona tena”
“Kwahiyo wewe na mwanangu mnafahamiana eeeh! Mnafanya kazi pamoja?”
Yule binti alicheka na kumuangalia Juma kisha akamwambia,
“Mwanao ni mtu mwingine kabisa, hebu tafakari haya machache nitakayokwambia. Mwanao ndio aliyesababisha Pendo kuvimba shavu baada ya kumpiga kibao, mimi nikakupa mkono wewe kwenda kumuwekea Pendo na pendo akapona kabisa, ila mimi nilipotea na hatukuweza kuonana tena hadi ambapo mwanao kafurahi mwenyewe na kutukutanisha, hii ni zawadi kwako na ni zawadi kwangu pia”
Juma alipumua kwanza na kumuangalia vizuri huyu binti huku akimuuliza,
“Mwanangu ni nani?”
“Sidhani kama nitakuwa na jibu la hilo swali lako. Ila hongera kwa mkeo, hongera sana”
“Asante, umeshajua?”
Yule binti alitabasamu na kumwambia Juma,
“Nisindikizeni nikapande basi niende kwetu”
“Kwani kwenu ni wapi?”
Kwakweli Juma alikuwa haelewi kitu ingawa alifurahi sana kumuona huyu binti, kisha huyu binti akamwambia Juma,
“Kwetu ni kule ambako huwa unanikuta”
Juma hakumuuliza zaidi huyu binti kwani aliona ni vyema amuulize zaidi pindi akikutana nae mwenyewe yani hakutaka kumuuliza zaidi mbele ya mtoto wake.

Moja kwa moja walisogea hadi stendi ambapo yule binti alipanda basi na kufanya Juma na mwanae waanze kurudi nyumbani, yule mtoto akamuuliza Juma,
“Kwani baba mimi unanionaje?”
Juma akajifikiria na kumjibu,
“Nakuona kawaida tu kama watoto wengine”
Yule mtoto akatabasamu kisha wakarudi nyumbani, ila leo walikuwa wamechelewa tofauti na siku zingine ambazo Juma na mtoto huwa wanawahi.
Walikuta chakula kimeshaandaliwa mezani, moja kwa moja walienda kukaa huku Anna akimtayarishia chakula mtoto ambapo walianza kula, ila Anna alipomlisha mtoto kijiko kimoja tu akaguna na kusema,
“Mbona chakula hakina chumvi?”
Mariam alimuangalia huyu mtoto na kusema,
“Si ulisema nisiweke chumvi nyingi wewe! Nimeogopa kuweka chumvi nyingi ndiomana sijaweka chumvi kabisa”
Yule mtoto akamuuliza tena Mariam,
“Sasa tutakulaje chakula ambacho hakina chumvi?”
Mariam akaonyesha,
“Chumvi hiyo hapo, anayetaka anaweza kuongeza”
Basi Anna akataka kumchukulia chumvi huyu mtoto ili waongeze kwenye chakula ila huyu mtoto alikataa na kusema,
“Mama, mimi siwezi kula chumvi mbichi. Nenda jikoni kabandike tena hiki chakula uache chumvi ichemke”
“Khaaaa!! Najuta mimi”
Mariam alijikuta akisema hivyo na kuinuka huku amechukia sana, akachukua chakula pale mezani huku Anna akimsaidia na kwenda kukibandika tena, yani Mariam alikuwa na hasira sana, kilipochemka alienda kuwapelekea mezani ila yeye alienda chumbani, yani Juma alikosa amani kabisa akataka kwenda kumbembeleza mkewe ila mtoto akasema,
“Baba, acha muache mama kama kasusa. Yeye huwa anasema ukisusa wenzako twala, muache leo ni zamu yake”
Juma akasema,
“Mmmmh ila kumbuka ni mjamzito?”
Yule mtoto akasema tena,
“Umeshaenda kupima nae? Muache hakuna kumuita”
Yani Juma alikosa raha kabisa, hata hakuweza kulak wa raha na alikula kidogo na kuacha ila alisubiri wote wamalize ndio akaenda chumbani.

Juma alimkuta Mariam chumbani akiwa amechukia sana, akiwa amekunja mdomo huku hasira zikiwa zimemjaa, Juma akamsogelea na kumwambia,
“Pole mke wangu!”
“Niache!”
Halafu akaanza kulia na kusema,
“Hivi ni kwanini mimi Mariam nikazaa kiumbe cha ajabu kiasi hiki! Kwanini hiki kiumbe cha ajabu kimekuja katika maisha yangu! Kwanini?”
Mariam alikuwa akitoa machozi mengi sana, Juma alimuhurumia na kumshika tumbo huku akisema,
“Mke wangu, tumbo lako halitazaa tena kiumbe cha ajabu. Huyu mtoto ajaye atakuwa ni mtoto wa baraka na atakuwa ni mkombozi katika maisha yetu”
Mariam aliendelea kulia na kusema,
“Hawezi kuwa mkombozi katika maisha yetu, sababu wewe umeniingilia kimwili kwa kutumia madawa, nina uhakika huyu mtoto atakuwa mkosi kama aliyepita”
“Usiseme hivyo Mariam mke wangu, nina uhakika huyu mtoto ni baraka katika maisha yetu”
“Mimi nakwambia kuwa haiwezekani”
“Ila kosa ni la nani hadi mimi kuamua kutumia madawa?”
“Kosa ni lako Juma, kwanini utumie madawa?”
“Sababu ulikuwa unaninyima? Ningefanyeje na kukusaliti siwezi!”
Mariam alimuangalia Juma na kufuta machozi yake kisha alimuuliza,
“Unanipenda kiasi hicho cha kushindwa kunisaliti Juma?”
“Ndio, mimi nakupenda sana. Kumbuka Mariam nilipokuja kukuchumbia kwenu ili nikuoe, mama yako aliniambia sifa zote ulizokuwa nazo, alisema kuwa wewe ni mvivu sana hufai kuwa mke yani mume anatakiwa kuwa mvumilivu sana ila nikasema kuwa nitakuweza, sababu tu nilikupenda. Na kweli hata nilipokuoa ulikuwa hivyo ambavyo mama yako alisema, ila sababu nilikupenda basi nilikuvumilia na mimi nakwambia hivi Mariam siwezi kukusaliti, nakupenda sana mke wangu”
Mariam akamuangalia tena Juma na kupiga magoti huku akimwambia,
“Naomba unisamehe mume wangu kwa kosa langu la kukunyima unyumba hata sijui huwa nakumbwa na nini naomba unisamehe sana. Kuanzia leo sitakuwa nikikunyima mume wangu”
Juma alimuinua pale mke wake na kumkumbatia huku akitabasamu kwa kufurahi sana kwa kile kilichofanywa na mke wake kwa muda ule.
Basi moja kwa moja, Juma alienda kupakua chakula kidogo na kumpa mke wake ambapo Mariam alikula tu kidogo kile chakula na walilala kwa muda huu.

Usiku wakati wamelala, Mariam alihisi kama kuna kitu kinakuja na kukandamiza tumbo lake kisha akahisi maumivu makali sana na kumfanya aanze mkunyonga nyonga tumbo lake ila hakuweza kushtuka kabisa kwani alijikuta akilala kabisa kwa muda huo bila kujali yale maumivu.
Kulipokucha, alishangaa tu kuona damu kitandani na kumwambia mume wake,
“Juma, ona ni kitu gani hiki jamani!”
“Khaaaa ni damu!! Twende hospitali mke wangu”
Juma alimsaidia Mariam na moja kwa moja walienda kujiandaa kwaajili ya kwenda hospitali.
Ilikuwa ni asubuhi sana, kwahiyo walipotoka ni mama Shamimu tu ndio alikuwa macho na ni yeye peke yake ndiye ambaye walimuaga.
Moja kwa moja walienda hadi hospitali huku wakiulizana ,
“Hivi tatizo litakuwa ni nini?”
“Mmmh hata sielewi”
Daktari alivyochukua vipimo na kwa maelezo yao akawapa jibu kuwa,
“Inaonekana ulikuwa na mimba changa ila imetoka”
“Kheeee yani nilikuwa na mimba imetoka!”
“Ndio, mimba uliyokuwa nayo imetoka. Pole sana”
Daktari aliwapa ushauri pale, kisha walipomalizana nae ndipo walipoweza kuondoka sasa kuelekea nyumba ni kwao.
Njiani walijikuta wakijiuliza sana kuwa imekuwaje ila hawakupata jibu, ila kuna mahali walifika na Mariam alijikuta akishikwa sana na haja ndogo kwahiyo ilibidi waende kwenye vyoo vya kulipia ambapo Mariam aliingia chooni huku Juma akimsubiria.
Muda wakati Mariam yupo maliwatoni, alipita yule rafiki yake Juma ambaye alipatwa na tatizo siku Juma kambeba mtoto wake basi Juma alimsalimia yule rafiki yake ila yule rafiki yake hakuitikia kabisa salamu ya Juma kwani aliondoka tu hata Mariam alipotoka alimkuta yule rafiki wa Juma akiishia akmuuliza Juma,
“Imekuwaje kwani! Si rafiki yako yule!”
Juma aliamua kumuelezea jinsi ilivyokuwa, jinsi rafiki yake alivyopata tabu na kumfanya Mariam asikitike na kusema,
“Jamani, kale katoto ketu ni katoto ka ajabu kale, ona sasa haya mambo! Najua kuna siku tu ipo ambapo kuna mtu atapoteza maisha kwaajili ya yule mtoto nakwambia mume wangu”
“Nimekuelewa ila tuachane na habari za huyo mtoto maana mabalaa huwa siyataki kabisa”
Juma alikuwa akiogopa kabisa kumuongelea yule mtoto wao ingawa kwa sehemu nyingine alihisi huenda yule mtoto ndiye abaye amesababisha mimba ya Mariam kutoka ila tu hakuwa na namna yoyote ya kufanya.

Leo Juma akiwwa nyumbani na mke wake alijitolea kumsaidia mke wake kupika maana hakwenda mahali leo tangu wametoka hospitali na hakuna mtu ambaye walimwambia kuwa wameenda hospitali na kukuta mimba imetoka.
Basi chakula chote leo alipika Juma, na walipoanza kula wote wwalikula kasoro mtoto wao ambaye alisema,
“Leo chakula hakijapikwa na mama kwanini?”
Juma aliamua kumtetea mke wake,
“Nimeamua kumsaidia leo, ni mimi nimepika kwani ni vibaya? Mpunguzie adhabu mama yako nakuomba”
Juma alipiga magoti kumwambia huyu mtoto, kisha mtoto akasema,
“Nitamtolea mama hii adhabu endapo akianza kunipenda na akiacha uvivu”
Juma akamuuliza,
“Sema cha kufanya ili na yeye ajue namna ya kuacha uvivu?”
Yule mtoto akasema tena,
“Aaache kusema, mimi siwezi kufanya kazi hii, mimi kabisa nifanye kazi hii siwezi nitachoka sana. Aache kusema hivyo, halafu aache tabia ya kujisifu kuwa yeye ni mvivu sana maana uvivu sio sifa nzuri bali ni sifa mbaya, napenda mama yangu ajisifie kuwa yeye ni mchapakazi ili ifikie hatua tuwe hatuhitaji msaidizi humu ndani wakati yeye yupo tu hana kazi nyingine.”
“Sawa nimekuelewa”
“Kuanzia kesho, mama awahi kuamka. Sipendi tabia yake ya kulala hadi saa nne asubuhi wakati usiku anawahi kulala tu”
Ni Juma ndiye aliyekuwa anajibu kwa niaba ya mke wake, ila Mariam alikuwa kimya kabisa wala hakuongea jambo lolote ukizingatia na mambo yaliyompata siku hii ndio kabisa alihisi kumchanganya akili kwahiyo alikuwa kimya kabisa.

Leo mapema kabisa, Juma aliamka na Mariam na yeye aliamka, kwahiyo Juma alivyoondoka na yeye alitoka nje na kukaa sebleni ambapo alimkuta mama Shamimu yupo kusafisha sebule, mama Shamimu akacheka na kumwambia Mariam,
“Wifi, kwakweli umepatikana hadi nakuhurumia”
“Mmmmh acha tu wifi yangu”
“Halafu wifi hujaniambia, jana mlienda wapi na kaka?”
“Mmmmh acha tu, nitakwambia siku nyingine”
“Mmmmh haya, ngoja nimalizie kusafisha mimi. Maana akija huyo bosi wako tunakuwa kimya utafikiri tumefungiwa gundi kwenye midomo”
Mariam alitabasamu tu ila kiukweli hakuwa na furaha wala nini, yani alikuwa na mawazo sana, na kitu kikubwa kilichompa mawazo ni namna ambavyo ile mimba ilitoka, yani alijiuliza sana, na kuona kuwa ni kitu cha ajabu kwake.
Muda huu yule mtoto alitoka chumbani na Anna, na kumfanya Mariam aende kubandika chai ila yule mtoto akamwambia Mariam,
“Mama, usiende jikoni. Leo atapika Anna”
Kwakweli hata Anna ni kitu ambacho hakukitegemea kwahiyo alijikuta akishangaa tu, ambapo ilibidi aende tu jikoni kupika kwanza hiyo chai.

Wakati wamekaa kwa pamoja wakitaka kula chakula cha mchana, kabla ya kuanza kula mtoto akasema,
“Ila mimi sili hiko chakula, nitakunywa maziwa”
Kwahiyo Anna alienda kumtengenezea maziwa yule mtoto, wakati huo Mariam na mama Shamimu ndio walipakua na kuanza kula ila mama Shamimu aliguna kwanza,
“Kheeee hiki chakula vipi jamani!”
“Hata mimi nashangaa”
“Mmmh yani huu ugali ni kama mtu ambaye hajui kusonga ugali kabisa, huu ugali umepikwa na mtu ambaye huwa hasongi ugali, angalia unavyonata mkononi halafu angalia mabujebuje, huu ugali haujaiva kabisa”
“Unajua nini wifi, kuna siku Anna ashawahi kutupikia vituko hivi akadai kuwa anumwa ila nashangaa kwakweli na leo kapika vile vile”
“Kwakweli, mimi siwezi kula ugali wa namna hii kabisa. Ngoja niende jikoni nikasonge ugali wa kula mimi na wewe tu halafu huu atakula mwenyewe aliyeupika”
Mama Shamimu akaenda jikoni ambapo Anna alikuwa akichanganya maziwa ya mtoto, basi mama Shamimu akamsema pale,
“Inamaana Anna hujui kupika au ni kitu gani?”
“Nisamehe ni mkono umeteleza”
“Mkono umeteleza kupika ugali mbichi!! Wewe mwana wewe, una nini lakini? Kwakweli hiki sio chakula kabisa”
Mama Shamimu akasonga ugali mwingine, kisha yeye na wifi yake wakala kile chakula na kuacha kile cha Anna mezani ili Juma akirudi amuonyeshe.
Ila muda huo huo Mariam alichukua simu na kumpigia mume wake, kumueleza kuhusu chakula alichowapikia Anna,
“Ila mke wangu si nilikwambia lakini, huyo Anna alikuwa anakutumikisha wewe, yani wewe ndiye uliyekuwa ukipika hapo nyumbani na sio yeye. Poleni sana, kwa stahili hiyo nadhani niliekabisa jioni huku huku”
“Hapana, wifi kasema kuwa atapika”
“Hapo sawa, huyo Anna hafai kabisa. Nilishawaambia lakini hamkusikia”
Basi Mariam alikata ile simu ila bado alikuwa akijiuliza mambo mengi sana kuhusu Anna kumtumikisha yeye.

Juma akiwa anatoka kazini, akapita tena kwenye ile njia ambayo anakutana na yule binti, akakutana nae leo na kusalimiana nae huku akisema,
“Hatimaye nimeweza kukuona tena!”
Yule binti alitabasamu na kusema,
“Umeweza kuniona sababu mwanao ameruhusu mimi na wewe kuweza kuonana tena, kwanza pole sana”
“Pole ya nini?”
“Pole kwa kupoteza mtoto”
“Mtoto! Mtoto gani?”
“Mimba ni mtoto hata kama ni mimba ya siku moja bado inahesabiwa kuwa ni mtoto kwani huwa inaleta matunda hayo, kwahiyo mkeo anapopoteza mimba ni wazi kuwa kapoteza mtoto yani mmepoteza mtoto, pole sana”
“Asante, umejuaje?”
“Kama nilivyojua kuwa mkeo ni mjamzito basi na ndivyo nilivyojua kuwa kapoteza mtoto”
Juma akaona ni huyu wa kumuuliza vizuri kwani alimuona akifahamu mengi sana, basi akamuuliza,
“Ni kweli mke wangu kapoteza mtoto ila tumejiuliza sana kuwa mke wangu kapoteza vipi mtoto? Hapo hatujaelewa kabisa, imekuwaje mke wangu kupoteza mtoto hatujui”
“Na mimi sitakwambia imekuwaje ila kaeni wote pale upenuni kwenu na mseme kuwa mmepoteza mtoto halafu ndipo mtajua ni kitu gani kimefanyika”
“Mmmmh!!”
“Ndio, mmefanya siri sana ila mngesema basi mapema kabisa mngejua”
“Dah!!”
“Ndio hivyo ila pole sana, je nikupe maua mengine ili uweze kulala na mke wako na mtengeneze mtoto mwingine?”
“Hapana, usinipe maua mengine, kwasasa mke wangu kashakubali kunipa unyumba bila ya mimi kutumia maua au dawa yoyote”
Yule binti alipiga makofi na kumwambia Juma,
“Hongera sana kw ahilo umefanikiwa, hongera sana”
Basi Juma akumuuliza tena huyu binti,
“Yule mtoto wangu unamfahamu vipi? Ni kiumbe wa aina gani?”
“Mmmmh sishani kama nitakujibu pia, ila jipe ujasiri muulize mtoto wako mwenyewe”
“Namuogopa”
Yule binti akacheka na kumuuliza Juma,
“Toka lini mzazi akamuogopa mtoto?”
Ila kabla Juma hajajibu akamwambia,
“Naomba niende, nishachelewa tayari.”
Juma aliagana tu na huyu binti ambapo aliondoka zake na moja kwa moja Juma alienda nyumbani kwake.

Chakula cha usiku napo walimtaka Anna asonge ugali ili tu kuangalia na ule wa mchana ambapo mambo yalikuwa vile vile na kumfanya Mariam asikitike sana kwa kile ambacho Anna amekifanya, kisha mama Shamimu ndio akapika na wote wakapata kula kile chakula kilichopikwa na mama Shamimu.
Walipomaliza kula, walikaa pamoja kwani Juma aliwaambia kuwa kuna jambo anataka kulisema, na moja kwa moja walihisi kuwa Juma anataka kuongelea kuhusu kile chakula ambacho kilipikwa na Anna, ila walivyokaa tu Juma akasema,
“Jamani, mke wangu alikuwa ni mjamzito ila tumepoteza mtoto”
Mama Shamimu alikuwa wa kwanza kutoa pole na kufanya Anna nae atoe pole ila mtoto akasema,
“Anna, hebu tuonyeshe jinsi gani umemuua mdogo wangu?”
Anna alishtuka sana kuambiwa vile.

Itaendelea…..!!!
Offa kwa leo na kesho utaisoma kwa 1000 tu nichek whatsapp kwa no.0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 26

Mama Shamimu alikuwa wa kwanza kutoa pole na kufanya Anna nae atoe pole ila mtoto akasema,
“Anna, hebu tuonyeshe jinsi gani umemuua mdogo wangu?”
Anna alishtuka sana kuambiwa vile.
Yule mtoto akamuuliza Anna,
“Sasa unashtuka nini? Ulidhani watu hawatajua? Ni kweli wote wanaweza wasijue lakini sio mimi, najua kila kitu. Haya sema hapa ni kwanini umemuua mdogo wangu?”
Anna akajifanya kulia ili aonewe huruma, yani Mariam alichukizwa sana ukizingatia na yale ya yeye kufanyishwa kazi zote mule ndani na Anna, ndio akazidi kupatwa na hasira,
“Yani Anna, kukulea kote huku kama mdogo wangu bado umeenda kunifanyia vitu vya ajabu kiasi hiki! Kweli Anna wewe Anna”
Mariam akainuka na kuanza kumpiga Anna yani alikuwa na hasira nae sana, na alimpiga sana hadi Anna alianza kutokwa na damu na hakuna hata mmoja mule ndani aliyekuwa akimtetea kwani uchungu wa jambo lile alikuwa nao Mariam mwenyewe.
Baada ya kumpiga sana, ndipo mtoto akasema,
“Sasa mama inatosha, inatosha mama. Baba mzuie mama inatosha”
Ilibidi Juma amtulize mke wake ila Mariam alikuwa na hasira sana,
“Yani umenitumikisha ndani ya nyumba yangu mwenyewe, haitoshi umeenda kunitoa mimba mchawi mkubwa wewe, na humu ndani unaondoka Anna, tena usiku huu huu Anna unaondoka, sikutaki humu ndani”
Mtoto akasema,
“Tulia mama, naomba utulie. Anna hawezi kuondoka maana muda wake wa kuondoka ni bado”
Mariam alimjibu huyu mtoto yani leo hakuogopa wala nini kumjibu huyu mtoto,
“Ni nani atakayeweza kuishi na Anna humu ndani! Ni na ni atakayeweza kuvumilia matendo kama hayo? Niogope kubeba mimba eti Anna atanitoa!”
“Mama, tulia. Usijali kitu, huyu Anna kwasasa hatothubutu kukushika kwa chochote kile. Hakuna atakachoweza juu yako mimi ndio nimesema”
Juma akaamua kumwambia huyu mtoto pia,
“Basi tunaomba na sisi huyu Anna asitushambulie”
Huyu mtoto alitabasamu na kusema,
“Hakuna wa kukushambulia baba yangu, sio Anna tu wala sio yeyote yule”
Mama Shamimu akaona kuwa atabaki mboga mwenyewe, basi akapiga magoti na kusema,
“Na mimi mtoto mzuri, nisaidie mimi shangazi yako”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Kumbe kwenye matatizo huwa ushangazi unafanya kazi eeeh! Usijali shangazi yangu, huyu Anna hatokushamulia.”
Kisha huyu mtoto akamgeukia mama yake na kumwambia,
“Mama, nakuomba tu jambo moja. Acha uvivu, sitaki tena uendelee na uvivu mama yangu”
Kisha alimgeukia Anna na kumtaka kuwa waende wakalale, yani Anna aliogopa sana ila aliamua tu kwenda kulala na huyu mtoto yani liwalo na liwe.

Mariam alikaa chumbani na mume wake akilalamika sana, yani aliona ni balaa kubwa sana kumleta Anna katika maisha yao,
“Yani mume wangu, mimi ni mjinga sana. Nilikuwa najidai hata mfanyakazi akilalamika namwambia kuwa ondoka tu maana nitapata mwingine, ni kweli niliamini kuwa watu wanashida na kazi ila sikujua kuwa watu hawapendi kutumikishwa, hawapendi kuteswa huwa wanafanya tu sababu ya shida. Sasa nimeenda kumpata Anna ambaye niliona ni mchapakazi kumbe ananifanyisha kazi mwenyewe!”
Mariam akainama chini na kulia kisha akasema,
“Ulikuwa ukiniambia mume wangu ila nikapuuzia, ona sasa Anna kumbe ndio kashiriki kuitoa ile mimba yangu!”
Juma akamuangalia Mariam na kumuuliza,
“Kwahiyo kwasasa upo tayari kuzaa na mimi?”
“Ndio nipo tayari, kwanini nisizae na wewe wakati wewe ni mume wangu?”
“Aaaah nimefurahi sana kusikia hivyo mke wangu, nimefurahi sana. Mwanzoni ulikuwa hutaki kuzaa na mimi sababu ya mimba iliyokaa miaka miwili”
“Ni kweli ile mimba ilinichanganya sana, ila huyu mtoto mbona tumeshindwa kuwa mbali nae! Na unajua anatulinda huyu!”
Juma alicheka na kusema,
“Kheeee leo ndio unasema kuwa anatulinda jamani Mariam! Ila na mimi sioni baya la mtoto, tumpende tu na atatusaidia na mengi”
Wakajikuta wakijadili mambo mengi sana ya familia yao hadi walipoenda kulala.

Juma aliwahi kutoka kazini leo, na moja kwa moja alimtafuta mama Rose ilia pate kuongea nae kuhusu Anna, kwani kwa yale ya jana aliona bado kuna umuhimu wa kumuelewa zaidi Anna, na kwanini mtoto wake anaelewana na Anna.
Alienda kukutana nae pale pale ambapo huwa anakutana nae siku zote,
“Yani kilichonifanya nije, ni kumzungumzia huyo huyo mtoto Anna”
“Khaaa bado una mambo tu ya hako katoto kachawi!”
“Yani huwezi amini, yule mdogo wako amemtoa mimba mke wangu”
“Kheeee yani mkeo alikuwa na mimba halafu Anna akajua loh! Pole sana, kale katoto ni kachawi sana, pole sana”
“Kwahiyo kula mimba ndio zake?”
“Ngoja nikueleze mimi vizuri ili ujue ni kwanini namchukia ingawa ni mdogo wangu, nilikwambia kuwa ameua ndugu zetu mapacha wawili. Hilo halitoshi, ni hivi mimi nilikuwa naishi na kale katoto maana nilikuwa nakaonea huruma kataenda wapi? Pale unavyomuona hawezi kufanya kazi yoyote, ndio kalelewa hivyo na mama. Kwahiyo hakuna kazi ambayo Anna anaifanya, sasa mimi nikawa naishi nae vizuri tu kama mdogo wangu huku nikimuelekeza baadhi ya kazi na mambo ya kufanya, nikabeba mimba ya kwanza, kakaila, nikabeba ya pili kakaila….”
Juma alimkatisha kidogo na kumuuliza,
“Kakaila ndio nini?”
“Yani kamekula mimba zangu hizo, kameziondoa nikawa sina mtoto. Nikaja kupata mimba nikafanya siri hadi nikajifungua, Anna akala mtoto wangu akiwa mchanga, ndio nikapata mimba hiyo mtaalamu akaniambia kuwa mtoto nimuite Rose, jina la mama maana mama yetu alikuwa akiitwa Rose, shida kubwa ni Anna asiweze kumtani mwanangu na hapo ndipo Anna alipoua wale mapacha, nikaamua kumfukuzia mbali Anna na kuanza kuishi maisha yangu, ndio nina mtoto mwingine kwasasa sababu Anna hayupo katika maisha yangu, yule mtoto ni mbaya sana, hafai kabisa sijui kwanini mnaendelea kuishi nae. Fukuzia mbali huko”
“Dah! Pole sana, kweli ni mchawi mdogo wako, kwa hayo maelezo tu ni wazi Anna ni mchawi wa wachawi ila pale kwangu nitamfukuza tu”
“Mfukuzeni, aondoke zake. Mnakaa na lijitu chawi kama lile la kazi gani? Sipati picha mama angekuwepo uwiiii dunia ingegeuka juu chini chini juu maana mama yangu alikuwa ni hatari sana”
Juma alimsikiliza kwa makini huyu mama Rose, kisha alimuaga na leo mama Rose aliamua kumsindikiza Juma.
Njiani kuna binti ambaye Juma alishtuka kumuona, ila yule binti na mama Rose walionekana kufahamiana kwani walikumbatiana kwa furaha,
“Karibu sana nyumbani kwangu”
“Asante dada, nimeona leo nije kukutembelea”
“Jamii yote imenitenga, umebaki wewe tu katika maisha yangu!”
“Usijali dada tupo pamoja”
Juma alishindwa kuvumilia na kumuuliza mama Rose,
“Kwani nani huyo?”
“Aaaah huyu ni mdogo wangu anaitwa Salome”
Mama Rose alipojibu tu hivyo, moja kwa moja aliondoka na Salome, yani Juma alibaki akishangaa tu.

Leo Mariam akiwa amekaa ndani alimsikia muuza samaki akipita, basi alitoka nje na kumuita ambapo yule muuza samaki alisogea karibu na kumfanya achague wale samaki,
“Kheee una samaki wazuri sana leo”
“Asante dada, najitahidi kuleta vitu vizuri ili kuwafurahisha wateja wangu”
Basi Mariam akachagua pale samaki ambapo yule muuza samaki alianza kumchambulia, huku Mariam akimuita Anna aweze kumletea chombo cha wewe kuwekea samaki.
Baada ya muda kidogo tu Anna alitoka ndani akiwa na bakuli kubwa huku amembeba yule mtoto, kufika pale kwa muuza samaki yani ilikuwa kama muuza samaki kapigwa shoti kwani alijikuta akimshangaa sana Anna na yule mtoto, mpaka Mariam alimuuliza,
“Wewe una tatizo gani?”
Muuza samaki alikuwa akitetemeka na kumuuliza Mariam,
“Samahani, hao ni watu kweli”
Mariam akamshangaa na kumwambia,
“Wewe weka samaki, mambo ya humu ndani hayakuhusu wala nini”
Akamsogezea lile bakuli na moja kwa moja Mariam alimtuma tena ndani Anna,
“Nenda kalete hela kabatini tumpatie”
Anna akaenda ndani na mtoto, yule muuza samaki akaweka samaki na kuondoka zake, yani hakutaka hata kuendelea kubakli eneo lile, ni kama amepatwa na kitu cha kuogopesha sana. Hata Mariam alimshangaa sana ingawa alienda ndani kuosha wale samaki na kuanza kuwakaanga.

Juma aliporudi leo, alimuuliza mtoto wake kama yeye kashamaliza adhabu ya kumbeba na kwenda nae stendi au bado, ila yule mtoto alimuuliza pia,
“Wewe unaonaje? Umemaliza adhabu au bado?”
Juma akafikiria na kusema,
“Nadhani nimemaliza, maana mwanzoni ulisema wiki mbili ila kwasasa ni zaidi ya wiki mbili”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Ni kweli ila twende na mimi leo”
Basi Juma hakuwa na namna zaidi zaidi kuamua kwenda kuoga na kujiandaa kisha kumbeba mtoto wake na kwenda nae kule kituoni ambako huwa anaenda nae.
Wakati wanaenda, wakakutana na yule jirani yao na wakina Juma, basi yule jirani alimsalimia Juma lakini alimsalimia kwa uoga uoga sana, mpaka Juma alimuuliza,
“Mbona hivyo wewe? Mbona unaonekana kuogopa?”
“Hapana siogopi wala nini ila nashangaa tu”
“Kheeee, sasa unashangaa nini?”
“Hapana, kwaheri”
Yule jirani akaondoka kwa haraka haraka na kumfanya Juma asielewe chochote kile kinachoendelea kisha akampeleka tu mtoto wake stendi kama ambavyo huwa anampeleka.
Wakiwa stendi, akatokea yule jirani mwingine ambaye alianguka siku ile, ila na yeye alimsalimia Juma kwa uoga uoga na kumfanya Juma azidi kuhisi huenda ni sababu ya matendo ya mtoto maana yule alijibiwa vibaya na huyu alianguka na wote wanamuogopa.
Ila wakati anaondoka pale stendi, ndipo alipopita jirani mwingine ambaye jirani huyu ndiye ambaye a,likuwa wa kwanza kabisa kumkaribisha Juma katika mtaa huo, ila jirani huyu na yeye alimsalimia Juma kwa kutetemeka na hakuweza hata kuongea nae zaidi wala nini, kwahiyo moja kwa moja aliondoka na kumfanya Juma awashangae sana majirani zake ila aliamua tu kurudi nyumbani.

Usiku ule Mariam alimsimulia mume wake kuhusu muuza samaki alichokifanya na jinsi ambavyo aliondoka bila hata ya kuchukua hela yake,
“Kheee inamaana Anna na mtoto wamemtisha nini?”
“Hapo hata sijui”
“Halafu leo kila ninayekutana nae anatetemeka kunisalimia”
“Labda sababu ya mtoto anavyowajibu”
“Sidhani, maana kuna ambaye nimekutana nae hata sijawahi kuonana nae na mtoto ila na yeye katetemeka kunisalimia na kaondoka hata hatujaongea chochote, nahisi kuna kitu hapa katikati”
Walijadili sana ila mwisho wa siku waliamua tu kulala kwa muda huo.

Ile hali ya watu mtaani bado Juma ilimshangaza sana, kwani kwasasa walikuwa hawamsalimii kabisa, yani sio tu kutetemeka bali hakuna aliyekuwa akimsalimia, wote walikuwa wakimpita kama hawamuoni vile na kumfanya awe anashangaa sana ila hakuwauliza kitu chochote.
Leo alienda kazini kama kawaida, ila alipokaa na wenzie aliamua kuwaambia tatizo la msichana wake wa kazi,
“Jamani mimi nina msichana wa kazi mchawi”
Wote wakashtuka na kumuuliza vizuri,
“Kheee umejuaje?”
“Kajisema mwenyewe, kumbe alikuwa akimtumikisha mke wangu, kazi zote alikuwa akifanya mke wangu badala yako. Yani hadi sasa nahisi kutetemeka tu na sijui cha kumfanya huyu binti”
“Aaaah Juma, acha zako hujui cha kufanya? Mfukuze bhana”
“Hataki kuondoka, kila ninapomfukuza anarudi”
Mmoja akashauri,
“Basi mkorogee sumu ya panya aende akafie mbele huko”
Mwingine akasema,
“Hilo sio suluhisho, mtu mwenyewe mmesema ni mchawi, mnaweza shangaa mmekoroga sumu ya panya halafu kawawekea wenyewe, mkajikuta mmejiua wenyewe, cha muhimu hapo ni kutafuta cha kufanya tu hakuna namna”
“Sasa ndio nifanyeje?”
“Yani angekuwa kwangu ningemkatakata na mapanga, unaona shida gani kuwaambia wjirani zako wote kuwa huyo binti ni mchawi wakusaidie kumtoa?”
“Au jamani mimi naona ni bora siku moja twende nyumbani kwake tumsaidie kumuondoa huyo mchawi, ang’ang’anie kwake hapo!”
Hili wazo la mwisho kidogo lilikuwa gumu kwa Juma ukizingatia mambo ya mtoto wake ndio kabisa yani, akaona ni mtihani mzito sana huo. Ila aliwaitikia tu kuwa kuna siku atawaita nyumbani kwake sema hakuchukulia maanani.

Leo Juma akiwa anatoka kazini, kuna jirani yake alimfata tena huyu jirani hajawahi kuongea nae kabisa, na hivi karibuni alikuwa hasalimiani nae ila huyu jirani alimsalimia leo na kumwambia,
“Ndugu yangu, watu husema ninyime chakula lakini usininyime maneno, naomba na mimi nisikunyime haya maneno”
“Maneno gani hayo?”
“Ni hivi, mtaa mzima unajua kuwa nyumbani kwako unafuga majini”
“Kheeee nafuga majini! Kivipi?”
“Nasikia muuza samaki alikuja nyumbani kwako kuwauzia samaki, mara mke wako akaita watu wamletee bakuli, hao watu hawakuwa watu wa kawaida walikuwa ni majini”
“Kheeee mbona sielewi”
“Ndio uelewe hivyo, mtaa mzima ninavyokwambia wanajua kuwa unafuga majini na leo asubuhi kulikuwa na kikao cha kukujadili wewe”
“Khaaaa hadi kikao cha kunijadili kimewekwa?”
“Ndio, walikuwa wanajadili kusema kuwa ndiomana mvua hazinyeshi inavyotakiwa, ndiomana jua ni kali, ndiomana watu hawaendelei hapa mtaani sababu ya wewe kufuga majini, tena mmoja akasema kuwa mke wako amekaa na mimba kwa miaka mitatu sijui, kuna makubwa sana yanaendelea”
“Dah!! Jamani”
“Sasa kilichobnifanya nikuambie ni kuhusu kilichoamriwa kwako”
“Kitu gani hiko?”
“Ni hivi, wamesema kuwa leo usiku watakuja nyumbani kwako na kumwagia petrol nyumba yote kisha watawachoma mkiwa humo humo ndani ili wewe na yeyeyote aliyendani mteketee na kufa, hata hayo majini yako nayo yateketee na kufa”
“Khaaaa jamani!”
“Ndio hivyo jirani, mimi roho imeniuma. Ingawa hatuna ukaribu ila huwa nakuona una roho nzuri, nakumbuka kuna siku umenikuta na mwanangu mgonjwa njiani ukanisaidia hadi hospitali na tukapata matibabu sababu yako. Kwakweli nakumbuka sana fadhila zako kwangu. Nimeumia mno kusikia habari hii ya wewe kufuga majini. Nikasema ngoja nikuvizie nikwambie ili ikiwezekana muondoke kabla giza halijaanza”
“Duh!! Asante kwa taarifa”
Yani Juma aliondoka muda huo huku akiwa amepaniki kabisa, hata hakujua ni wapi pa kuanzia wala nini maana alikuwa amepaniki.

Alipofika nyumbani hata hakujua aanze na jambo gani ila aliita familia yake yote sebleni na kuanza kuwaelezea kila kitu ambacho yule jirani amemwambia, Mariam alishtuka na kuogopa sana,
“Kheeee kwahiyo wanataka kutuchoma ndani ya nyumba jamani!!”
“Ndio hivyo mke wangu, sijui tunaenda wapi muda huu”
Mama Shamimu akadakia,
“Naomba niondoke sasa hivi niende kwa mama”
Mtoto alikuwa kimya tu wakati wakijadili, na wakajikuta wakiafikiana wote kuwa waende kwa mama yao na moja kwa moja kwenda kujiandaa maana hapo ilikuwa ni kufunga nguo tu na kubeba.
Walipotaka kutoka walishangaa kuona milango haifunguki, Juma aligeuka na kuuliza,
“Imekuwaje tena?”
Mtoto akauliza pia,
“Mnaondoka wote na mimi mnaniachaje?”
Juma akawaza ila hakuwa na jinsi akaamua kumwambia huyu mtoto kuwa wanaondoka nae, ila yeye akawaambia kuwa hakuna kuondoka hadi waweze kula kwanza kwahiyo waende kupika yani mule ndani walichukia sana kwani walijua wazi wale watu wa kuchoma nyumba watawafikia tu.
Wakati wanakula ndipo waliposikia sauti za watu wakiwa wamezunbguka ile nyumba yao, Juma alienda kuchungulia dirishani na hofu ikamtanda kwani aliona wale watu wakimwagia petrol kuizunguka nyumba yao, Juma alijikuta akisema,
“Jamani ndio tumeshakufa tayari”
Mtoto wao akacheka na kusema,
“Baba unaogopa kifo eeeh!!”
Mama Shamimu na Mariam nao wakasema,
“Wote tunaogopa kufa”
Mara wale watu wa nje wakawasha moto na kuanza kushangilia pale nje huku ndani wakiwasikiliza tu na kuogopa ila mtoto alianza kucheka na alicheka sana, gafla ilianza mvua ya ajabu tena ilikuwa ni mvua ya mawe na kusambaratisha watu wote pale nje.

Itaendelea……!!!

MTOTO WA MAAJABU: 27

Mara wale watu wa nje wakawasha moto na kuanza kushangilia pale nje ila mtoto alianza kucheka na alicheka sana, gafla ilianza mvua ya ajabu tena ilikuwa ni mvua ya mawe na kusambaratisha watu wote pale nje.
Pale ndani wote walikuwa kimya, na ile mvua ilidumu kwa takribani robo saa kisha ikaanza mvua ya kawaida, yani Juma alikuwa akimuangalia tu huyu mtoto wao bila kujua ni kitu gani cha ziada kipo kwa huyu mtoto wao ambapo mtoto aliwaambia,
“Endeleeni kulak wa amani, mnaogopa nini sasa? Acha waone nyumba nzima ni wachawi na majini ili watuogope kabisa, wasitufatilie wala kutusogelea”
Walimuangalia huyu mtoto na hakuna mtu ambaye aliweza kumuhoji zaidi zaidi walipakua chakula tena na kuanza kula maana lile janga la wale watu kuzingira nyumba lilifanya kila mmoja kusitisha lile zoezi lao la kula.
Walipomaliza kula, ndipo mtoto alipowaambia kuwa wanaweza kulala sasa, ila ile mvua haikukatika wala nini yani iliendelea kunyesha tu, na hakuna aliyehoji pale ndani kwao kwani kila mmoja alienda kulala.
Leo mama Shamimu aliingia chumbani kwake huku akiwa na uoga sana, kwani hakujua hatma yake kwenye hiyo nyumba, alitamani hata itokee afukuzwe tu kwenye nyumba hiyo ila haikuwa hivyo wala nini.
Alikuwa na uoga sana, hata lala yake ya leo ilijaa uoga mwanzo mwisho.

Mariam na Juma wakiwa chumbani wakajikuta wanaanza kujadili kuhusu mtoto maana yale mambo hayakuwa ya kawaida,
“Hivi Juma unamuona mtoto wetu kuwa wa kawaida kweli?”
“Mmmh! Hapana mtoto wetu sio wa kawaida yani sio wa kawaida kabisa”
“Unahisi mtoto wetu ni nani?”
“Sijui, yani sihisi chochote”
“Ila mimi nahisi kitu sema naogopa kusema”
“Kwanini unaogopa?”
“Wewe, tu anawaletea mvua ya mawe ambayo haijawahi kunyesha kwenye mji huu halafu utasemaje hapo! Angalia sasa, mvua ya kawaida hadi sasa bado inanyesha, si balaa hili yani huyu mtoto sio wa kawaida kabisa ila vingine siongei”
“Basi mke wangu tusiongee sana, tulale tu kwasasa”
Waliamua kulala tu kwa muda huo, kwani mambo yaliyoendelea hawakuyaelewa kabisa.

Kulipokucha, Juma aliamka kama kawaida na kujiandaa ila kwakweli alikuwa anaogopa hata kutoka nyumbani kwake, alikuwa akijiuliza kama ni sawa kwa yeye kutoka nyumbani kwake na kwenda kwenye shughuli zake. Basi mtoto alipotoka na Anna ndipo alipotaka kumuuliza ila alijikuta kama anashindwa maana alijikuta tu akiwa anamuogopa huyu mtoto ila mtoto alimwambia,
“Baba, nenda tu kazini hamna kitakachokupata”
Juma alimuangalia mtoto na kumwambia tu,
“Asante”
Kisha akaenda chumbani na kutoka na mwamvuli kwani mvua bado ilikuwa inaendelea kunyesha, alipokuwa anatoka mtoto alimuuliza,
“Unaenda wapi na mwamvuli baba?”
“Kuna mvua nje”
“Aaaah kumbe bado inanyesha, acha mwamvuli hiyo mvua inakatika muda sio mrefu”
Juma akaacha mwamvuli na kutoka, na kweli baada ya muda kidogo tu ile mvua ilikatika, kwakweli hili swala lilikuwa la ajabu sana kwa upande wa Juma.

Mama Shamimu akiwa bado chumbani aliamua kuchukua mabegi yake ili akawaage apate kuondoka, basi alitoka sebleni na kumkuta Anna na yule mtoto wamekaa basi akawaam bia,
“Jamani mimi nataka kuondoka”
Muda huo Mariam nae alikuja na kumuangalia wifi yake na kumuuliza,
“Wifi jamani, unataka uende halafu mimi uniache na nani?”
“Khaaa jamani, si unabaki na mwanao na mdada wako wa kazi!”
“Jamani, wifi nakuomba usiondoke”
“Hapana, hakuna anayeweza kubadili fikra zangu”
Mariam akamuangalia mtoto wake na kumwambia,
“Tafadhari naomba asiondoke”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Leo nimefurahi sana, kumbe mama unaniamini eeeh!! Sasa shangazi na wewe unataka kuondoka kwenda wapi?”
“Nataka kwenda nyumbani kwangu”
“Nyumbani kwako ulisema mtaa mzima wamejaa wachawi, je utakuta wachawi wameisha? Wachawi huwa hawaishi maana hata akifa mama mtu basi huwa wanawaachia watoto wao, mfano mzuri ni huyu Anna, mnadhani uchawi kautoa wapi? Kwa mama yake, kwabhiyo uchawi huwa hauishi, sidhani huko nyumbani kwako kama kupo sawa!”
Mama Shamimu akajitetea,
“Ila nilikuwa nataka kwenda kuangalia mji wangu na mali zangu nione mambo yanaendaje pale”
Ila mtoto kwa muda huu akatoa kauli moja tu,
“Shangazi, hakuna kwneda popote bila ruhusa yangu”
Mama Shamimu alichukia sana na kurudisha mabegi yake ndani, alikuwa na hasira mno juu ya yule mtoto alichokuwa anafanya.
Ila badae, mama Shamimu alimuita Mariam chumbani kwake na kuanza kuongea nae,
“Ila wifi, kumbe unafurahia mambo haya?”
“Jamani, mimi nafurahia saa ngapi?”
“Kwanini umwambie mtoto anizuie?”
“Ila hebu kuwa na huruma hapo wifi yangu jamani, Anna mchawi, mtoto wangu anafanya mambo ya ajabu halafu kweli unataka kuniacha katika hali kama hii jamani wifi yangu! Hebu nihurumie jamani, usitake kunifanyia hivi nakuomba”
“Ila nimemkumbuka mwanangu Shamimu”
“Naelewa wifi ila naomba unisaidie kwa hili, nakuomba wifi yangu, nakuomba sana. Usiniache peke yangu”
Yani Mariam alikuwa akionyesha sura ya huruma sana, ila Mariam alipoondoka mama Shamimu aliamua kumpigia simu mama yao ili kumueleza yale mambo yaliyokuwepo,
“Kheeee mlitaka kuchomewa nyumba?”
“Ndio mama, wananchi wa hapa wote wamechukia wanasema tunaishi na majini ndani”
“Hivi Juma anafikiria nini kuhusu mambo hayo jamani! Juma ni mwanaume lakini kwanini anashindwa kufikiri kama mwanaume?”
“Hata mimi namshangaa mama”
“Ngoja nimuite ili niongee nae”
Mama Shamimu alikata simu ya mama yake, ila kiukweli hakupenda tena kuendelea kuishi hapo kwenye nyumba ya Juma.

Juma leo aliwahi kutoka kwenye shughuli zake maana mama yake alimpigia simu kwahiyo moja kwa moja aliunganisha kwao, ingawa kulikuwa na umbali kiasi ila huwa haoni tatizo kwenda kwao kuzungumza na mama yake kuhusu mambo yanayoendelea kwenye familia yake.
Alimkuta mama yake yupo akimsubiri, na moja kwa moja huyu mama alitaka maelezo ya kuchomewa nyumba ambapo Juma alimueleza ilivyokuwa hadi mwisho kisha mama Juma akamuuliza juma,
“Hivi wewe yule mkeo si mjamzito wewe?”
“Hapana mama, ile mimba ilitoka”
“Ooooh asante, Mungu ni mkubwa kwakweli maana yalikuwa ni mauzauza mengine hayo. Haya sasa tuongelee hayo mauza uza ya nyumbani kwako”
“Ndio kama hivyo mama”
“Kwanini msiamue moja, yani wote mje huku nyumbani ila hayo majini yenu ndio myaache huko?”
“Kwanza mama, haiwezekani kumuacha yule mtoto pale nyumbani, yani kama tukija huku ni lazima tuje nae maana yule mtoto hawezi kukubali”
“Ila Juma mwanangu kuna kitu nimefikiria ila usichukie”
“Niambie mama ni kitu gani, sitachukia wala nini mama yangu”
“Ni hivi, yule mkeo Mariam nahisi kabisa kuna jambo alilifanya pindi akiwa na mimba ya yule mtoto wenu au huenda ile mimba aliipata kwa waganga huko, unajua kipindi umemuoa ndio kipindi ambacho ulikuwa unahitaji mtoto kwa sana, kwahiyo inawezekana kabisa mkeo alienda kwa waganga huko, tena inawezekana alipelekwa hadi kwa mashetani na majini ndio kapatia mimba ile huko”
“Mmmmh! mama”
“Usigune tu, bali tumia muda wako umuulize vizuri mke wako ni kitu gani alifanya kipindi anasaka mimba ya yule mtoto, muulize kwa makini sana kitu alichofanya mke wako”
“Kama akisema hakufanya kitu?”
“Akisema hivyo ujue wazi ni muongo, hakufanya kitu wakati mambo ni wazi kabisa yanaonekana, mtoto yule ni uthibitisho tosha kuwa mkeo alifanya mambo ya ajabu. Kumbuka hadi kujifungua kwenyewe nimempelekea dawa akaogee, kumbuka mtoto yule kafanya hospitali wote wakimbie, kumbuka mtoto yule hakuna chanjo hata moja aliyopata sababu ya mambo ya ajabu aliyoyafanya hospitali. Muulize mke wako ili tujue kuwa tunaanzia wapi kwenye mambo haya kwakweli.”
“Mmmmh!! Sawa mama, nitamuuliza ingawa najua wazi hakuna jambo la tofauti ambalo mke wangu amelifanya. Ila sijui maana wanawake wana siri nyingi sana”
Juma aliongea na mama yao ambapo mama yao alimsisitiza kuwa wanatakiwa kuhama pale wanapoishi maana yule mtoto atawaletea mabalaa.

Leo usiku Juma aliamua kuongea na mke wake kuhusu kile ambacho mama yake alisema ila alipomuuliza Mariam alikataa kabisa,
“Sasa mimi niende kutafuta mtoto kwa mganga kwasababu gani? Kwani nilikuwa na tatizo la kizazi mimi? Kwa waganga tumeanza kwenda baada ya mimba kupitiliza muda wake, hapo kweli tumeenda kwa waganga na wala sikuwa peke yangu bali tumeenda wote ili kutafuta suluhisho la mimi kujifungua, hapo ndio nikanywa dawa za kila aina, nikafanya mambo ya kila namna, hapo ndipo nilipokuwa na tofauti ila mimi sikuwahi kwenda kwa mganga yoyote hapo kabla.”
“Ila Mariam ni bora ungekuwa mkweli ili tujue cha kufanya”
“Halafu mimi nahisi mama yako ndiye aliyeniroga”
“Duh!! Mama yangu tena amekuwa mchawi jamani Mariam! Kweli mama yangu tena aliyehangaika kukutafutia dawa ili ujifungue ndio kawa mchawi?”
“Ndio, huoni dawa zote zilidunda mpaka dawa aliyotafuta yeye? Usimtetee mama yako Juma, mimi nina uhakika asilimia zote kuwa mama yako ndiye aliyesababisha haya yanayoendelea sasa. Ila nadhani hata yeye hakuelewa kama anatengeneza kitu cha ajabu ila kitu alichokitengeneza ni kibaya sana”
“Hebu nyamaza Mariam, tulale tu kwasasa maana naona umeanza kunikoroga, yani mama yangu kawa mchawi dah!”
Juma aliamua tu kulala, kwa muda huo hata Mariam na yeye alilala.

Leo wakiwa wamekaa baada ya kazi zote, pale sebleni yule mtoto alimuangalia Mariam na kumuuliza,
“Mama, unaujua uchawi wewe?”
Mariam alikaa kimya hadi mtoto alimuuliza tena,
“Mama, unaujua uchawi wewe?”
“Mmmh ! Kiasi”
“Unaujuaje?”
“Mmmmh siujui ila mtu kama hivyo nasikia kwamba mtu Fulani mchawi na mtu Fulani mchawi basi”
“Sasa una uhakika gani kama bibi yangu ni mchawi?”
Hapa Mariam alijikuta katoa mimacho tu, kisha yule mtoto akamwambia Mariam,
“Na uache tabia yako ya kusema kuwa bibi yangu ni mchawi”
Yani Mariam alikaa kimya kabisa kwani hakutegemea kama huyu mtoto angemwambia hivi.

Leo wakati Juma akitoka kwenye shughuli zake, ndipo alipokutana na yule jirani ambaye alimpa taarifa za kwenye mtaa kuwa wanataka kuchoma nyumba yake huku na wenyewe wakiwa ndani, basi yule jirani alimsalimia na kuanza kumwambia,
“Hivi lile tukio la siku ile ulilishuhudia au?”
“Tukio gani?”
“La kuchoma nyumba yako”
“Mimi nilikuwa ndani yani ya nje siyajui kwakweli”
“Yani siku ile watu walikuja mapema sana kwako na kumwagia petrol na kuchoma nyumba uwiiii sijui ikawaje ile mvua ya mawe na upepo sijui vilitokea wapi jamani, unajua watu waliumia hatari waliumia sana na wengine bado wapo nyumbani kwao wakiuguza majeraha”
“Vipi wewe hukuhumia?”
“Hapana, mimi sikuhumia”
“Au hukuja?”
“Nilikuja, unajua nilikuwa na uchungu hatari. Nikasema nakuja kushuhudia hadi mwisho itakavyokuwa, basi ile mvua ilipoanza na upepo mkali ikawa ngumu kabisa na kufanya kila mtu akimbie hovyo hovyo ila huwezi amini nilikimbia hadi nyumbani kwangu na sikulowa wala nini”
Juma alimshangaa yule jirani yake na kumuuliza,
“Hukulowa?”
“Ndio, hata mke wangu alinishangaa kuwa imekuwaje sikulowa kabisa”
“Khaaaa kumbe una mke!”
“Ndio, kwani hukujua kama mimi nina mke?”
“Hapana, nimeuliza tu”
“Mmmmh au sababu nimekwambia umbea? Yani hapa mtaani huwa wanasema sana kuwa mimi mbea kama mwanamke, nashangaa na wewe unashangaa kuwa mimi nina mke! Mimi nina mke ndio na watoto wawili, wamefanana na mimi hatari”
“Hongera sana kwa hilo”
“Asante, ila bado wanaendelea kupanga mipango mingine kuhusu wewe nimewasikia. Kuwa makini sana ndugu yangu, mimi sio mbea kivile ila tu huwa nikiona kuna jambo la kumuumiza mtu ndio huwa najikuta nikishindwa kuvumilia na kusema hilo jambo. Naomba unisamehe tu kama nimekukwaza”
“Hapana hujanikwaza, kwanza umenisaidia sana”
Juma aliagana na huyu jirani yake na kuondoka zake.

Juma alipokuwa nyumbani kwake, aliwasimulia kuhusu yule jirani kitu alichomuambia ila mtoto akamsema Juma,
“Sasa, baba kwanini umshangae yule kuwa na mke wakati amekwambia mambo mazuri ya kukusaidia wewe mwenyewe!”
Juma alishangaa na kumuangalia mtoto wake, kisha akamuuliza,
“Kwani ulikuwepo kwenye mazungumzo yetu?”
Mtoto alitabasamu na kumwambia baba yake,
“Kwasasa, mimi nimekuwa na kadri ninavyozidi kukua ndivyo uwezo wangu unavyoongezeka, kwahiyo kwasasa kuwa makini sana kwa chochote unachokisema na chochote unachokifanya”
“Mmmmh!!”
Mtoto akaendelea kuongea,
“Halafu kuhusu wale watu kukubunia mbinu nyingine, usiwe na shaka maana hakuna kitu kama hiko. Hakuna watakachoweza kufanya wala nini kwahiyo msiwe na wasiwasi wowote ule”
Wote walikaa kimya wakimuangalia tu, kisha kila mmoja kuinuka na kwenda kupata chakula cha usiku.

Wakati Juma kaenda kulala, akapigiwa simu na mama yake na kuanza kuongea nae ambapo mama yake alitaka kujua kama Juma ameongea chochote na mke wake,
“Umemuuliza mke wako?”
“Amekataa mama”
“Anakataa bure, lakini kuna mahali ameenda huyo”
“Ngoja nikupe uongee nae”
Basi Juma alimpa Mariam simu aongee na mama yake, ambapo yule mama alimuuliza Mariam,
“Kabla ya kupata mimba ya huyo mtoto wenu ulienda kwa mganga gani?”
Mariam alichukia kidogo kwa lile swali na kumwambia,
“Halafu mama nakuheshimu sana, tena nakuheshimu sana, ungejua huyo mtoto bunayemjadili anavyokupenda na kukuheshimu basi hata usingehangaika kuuliza maswali yasiyokuwa na kichwa wala miguu”
Kisha Mariam aliikata ile simu na kumtaka Juma walale, yani Juma alikuwa akimsikiliza sana Mariam na kumfanya aache simu pembeni bila kumpigia tena mama yake na kulala tu kwa muda huo.

Leo wakati Juma yupo kazini, rafiki zake wakakumbusha kuhusu swala la mdada wa kazi wa Juma, kisha walimuuliza Juma,
“Vipi yule mdada mchawi ulishamuondoa?”
“Hapana, bado”
“Kwanini sasa?”
“Hata sijui ni jinsi gani nitamuondoa”
“Hebu acha ujinga Juma, sisi tulishakupa mbinu. Leo tunaenda wote nyumbani kwako kumuondoa”
“Hapana, nawaomba tusiende leo, nitawaambia siku ya kwenda”
“Sisi tunaenda na wewe leo leo”
Juma aliwakatalia kabisa ila rafiki zake waling’ang’ania.
Juma ilibidi awatoroke tu muda wa karibia na kuondoka, ila kuna mmoja alimuona na kuwatonya wengine hivyo walianza kumfata Juma yani Juma alipokuwa anafika kwake aliwaona tayari wale rafiki zake wapo nyuma yake ila kabla hajasema kitu, yule mtoto wa Juma alitoka nje na kusimama mlangoni kisha akawaambia wale rafiki wa Juma,
“Ishieni huko huko”

Itaendelea…..!!!
Offa bado inaendelea 1000 mpaka mwisho nichek whatsap no.0629980412 tukutane jumatatu😁😁
 
MTOTO WA MAAJABU: 28

Juma ilibidi awatoroke tu muda wa karibia na kuondoka, ila kuna mmoja alimuona na kuwatonya wengine hivyo walianza kumfata Juma yani Juma alipokuwa anafika kwake aliwaona tayari wale rafiki zake wapo nyuma yake ila kabla hajasema kitu, yule mtoto wa Juma alitoka nje na kusimama mlangoni kisha akawaambia wale rafiki wa Juma,
“Ishieni huko huko”
Wale rafiki wa Juma walishangaa sana maana yule mtoto alikuwa ni mdogo, halafu kile kitendo cha kuwaambia ishieni hapo hapo kilikuwa cha ajabu, wakajikuta wakimuuliza Juma,
“Ndio umelea hivi mtoto!!”
Juma akawaangalia na kuwaambia,
“Jamani, naomba muende tu mimi nitajua cha kufanya na mdada wangu wa kazi”
“Ila hapa hatumzungumzii mdada wako wa kazi tena, tunamzungumzia mtoto wako”
Juma hakujibu lile swali bali aliwafata karibu na kuwaambia,
“Naomba niwasindikize tu jamani”
Wale wakaguna, ila walifata tu ile Juma aliyosema ambapo Juma aliwasindikiza huku akiwalaumu,
“Ila na nyie rafiki zangu mna nini lakini? Yani nyie kunifata hadi nyumbani kwangu kweli!”
“Juma, tunakuonea huruma kuhusu mdada wako wa kazi ndiomana tukasema tuje ili tumfukuze wenyewe. Ila swali lipo bado kuhusu yule mtoto, ni mtoto wako kabisa yule Juma?”
“Ndio ni mtoto wangu”
“Ila vipi mbona katutolea kauli ile na anaonekana kuwa bado mdogo! Nina uhakika angeongea kwa kitoto na asingepata ujasiri wa kutotolea kauli ile au amedumaa tu mtoto wako!”
Juma akaona hapa pagumu kujibu, basi akaamua kuwaaga rafiki zake tu pale na kuondoka zake.

Juma alirudi nyumbani kwake na kuingia ndani ila hakuongea kitu chochote wala hakumuuliza kitu chochote mtoto wake, hadi muda walipokuwa wanakula ndipo mtoto alipomuuliza Juma,
“Naona kama kuna jambo unataka kuniuliza baba! Niulize tu nitakujibu”
Juma alikuwa kimya tu akimshangaa huyu mtoto, kisha mtoto akamwambia tena Juma,
“Niulize tu baba”
Juma akasema,
“Hapana, sina cha kukuuliza halafu sio vizuri kuongea wakati wa kula”
Mtoto akatabasamu tu halafu wakaendelea kula yani Juma hakuona kama kuna sababu ya kumuuliza mtoto wake kuhusu lile swala.
Wakati Juma ameenda kulala na mke wake ndipo Mariam alipomuuliza,
“Kwani ni kitu gani ulitaka kumuuliza mtoto?”
Juma alimsimulia mke wake kuhusu rafiki zake waliofika na jinsi ambavyo mtoto wao amewaambia, basi Mariam akatikisa kichwa tu na kusema,
“Yani huyu mtoto atafanya nyumba yote hii tuonekane mashetani”
“Kwanini mke wangu?”
“Unadhani watu wanafikiriaje hapo? Yani mtoto mdogo kama huyu anatoa amri kama hiyo kweli! Eti ishieni huko huko, yani lazima watu wataona kuwa sisi ni waajabu sana”
“Sasa tutafanyaje hapo mke wangu?”
“Mmmh hata sielewi kwakweli, hapo hakuna cha kufanya labda tutafute mawazo ya watu wengine ili tujue ni kitu gani tunaweza kufanya hapo?”
“Mmmmh sawa mke wangu, tulale tu kwasasa”
Wakaamua kulala kwa muda huo.

Leo Mariam anaamua kumuita Anna ili aweze kuongea nae maana aliona huyu binti anatakiwa aongee nae hata kirafiki ili aondoke tu hapo nyumbani kwake,
“Anna, mdogo wangu maana nimekuchukulia kama mdogo wangu toka mwanzoni. Toka siku ya kwanza umekuja hapa nilikuhurumia bila ya kujua tabia za ajabu ulizokuwa nazo, na hata mume wangu aliponiambia kuhusu wewe bado nilikataa ingawa nilikuwa nikiamka huku nimechoka sana. Ila mdogo wangu, naomba tuongee kirafiki ni kwanini ulikuwa unanitumikisha kichawi?”
“Hapana, dada mimi sio mchawi”
“Hapana Anna, sina nia yoyote mbaya na wewe. Niambie tu ni kwanini ulikuwa ukinitumikisha kichawi?”
“Naomba unisamehe dada, nisamehe sana dada yangu. Yani ni malezi ambayo nimelelewa mimi, kwakweli hayakuwa malezi mazuri hakuna chakula ninachoweza kupika kwa ufasaha, hakuna kazi ninayoweza kufanya kwa ufasaha ndiomana nilikuwa nakutumia wewe mwenyewe, maana ningekuwa nawapikia mimi basi mngenifukuza mapema sana, siku ile niliyokwambia naumwa ndiomana nimepika vibaya ni kisingizio tu ila kiukweli siwezi kupika”
“Duh! Kwahiyo siku zote humu ndani huwa tunakula chakula nilichopika mimi?”
“Ndio dada”
“Zile chapati, bagia na sambusa zote nilikuwa napika mimi?”
“Ndio dada”
Mariam akapumua kwanza na kutikisa kichwa kama ishara ya kujisikitikia kisha akamwambia Anna,
“Ila mdogo wangu ulikosea, sababu wewe ulitakiwa useme ukweli kuwa dada mimi kupika siwezi ili nikuelekeze. Unadhani utachukua watu wakufanyie kazi hadi lini? Kuna nyumba zingine ni nzito mdogo wangu, sio rahisi kuchukua na kuwatumikisha kwenye nyumba hiyo, sasa wewe utatumikisha watu hadi lini? Na umefanya nyumba ngapi kazi za hivi?”
“Nishafanya nyumba nyingi tu, haswa nikiona mama mwenye nyumba anapenda kulala, ndio huwa nafurahi hapo kwani kila anapolala huwa namchukua na kumfanyisha kazi zote”
“Duh!! Sasa ukipata mwenye nyumba ambaye hashindi nyumbani je huwa unafanyeje?”
“Kuna sehemu ya hivyo niliwahi kupata, mara nyingi nilikuwa namtumikisha mama mwenye nyumba usiku, ila kila aliporudi jioni saa moja usiku au saa kumi na mbili, huwa anakuta sijapika chakula cha usiku basi anasema anaenda kujilaza kidogo, ndio hapo hapo namtumia kupika chakula cha usiku, akiamka anakuta chakula tayari na kukifurahia ila anakuwa ni yeye mwenyewe amepika”
“Duh!! Kwahiyo unamchosha mara mbili, anachoka usiku, anachoka na kazi na bado jioni anarudi kujipikia duh mdogo wangu, uchawi ulipata wapi lakini?”
“Kanipa mama, yani mimi nimerithi kutoka kwa mama yangu”
Yani Mariam leo alikuwa akiongea na Anna, huku akijihisi kutetemeka ila alikuwa akijikaza tu, maana kuona mtu anayeishi nae ndani yupo vile ilikuwa ni ngumu sana kuelewa.
Kisha akamuuliza tena,
“Halafu Anna, kwanini sasa ukanitoa mimba yangu?”
“Nisamehe dada, sikukutoa mimba”
“Anna, nimekwambia kuwa tunaongea kirafiki, kindugu sina nia ya kukufanya jambo lolote baya mdogo wangu maana yaliyotokea tayari yameshatokea ni ngumu kuyakwepa”
“Dada, nisamehe sana. Mama aliniambia kuwa kunywa damu ya mtoto ambaye hajazaliwa kutaniongezea nguvu sana, ni damu ya mimba changa ndio ambayo huwa naitumia. Sikutaka kufanya hivyo dada ila pindi tu nilipogundua kuwa una ujauzito nikajikuta nina hamu ya kupata hiyo damu”
“Duh! Huwezi kujizuia?”
“Najaribu dada ila najikuta tu nashindwa dada yangu, yani hamu ya damu inanijia tu dada yangu sielewi yani sielewi”
“Ila mdogo wangu, kuna jambo nataka kukwambia, je upo tayari?”
“Niambie dada yangu”
“Yani mimi nilitaka kukupeleka wewe mahali ukakae huko kwa muda kidogo sababu naona kama patakufaa na kidogo itakuwa ngumu kwa wewe kusumbua wengine”
“Ni wapi huko dada?”
“Tuna nyumba yetu ambayo hamna mtu anayeishi, sasa ingependeza kama wewe ungeenda kukaa huko. Nakuomba mdogo wangu, kama kweli haya mambo yanakuumiza kichwa basi utakubali kwenda kukaa huko”
Anna alifikiria kidogo kisha alikubaliana na lile swala la Mariam la yeye kwenda kuishi peke yake.

Mariam alipomaliza kuongea na Anna, alijiandaa ili aende kwa mama mkwe wake kwani huko ndio kulikuwa na funguo za kwenye hiyo nyumba yao, alipomaliza kujiandaa leo alimfata mtoto wake kwaajili ya kumuomba ruhusa,
“Mwanangu, nakuomba ruhusa niende kwa bibi yako tu mara moja halafu nitarudi”
Yule mtoto akamuuliza Mariam,
“Utaniletea zawadi gani?”
Mariam alifikiria sana na kukosa hata jibu la zawadi ya kumletea yule mtoto, akaamua kumuuliza,
“Kwani wewe unataka zawadi gani?”
Mtoto akatabasamu na kumwambia Mariam,
“Mama, naomba uniletee kipande cha kuni utakachokiokota njiani wakati wa kwenda huko uendako”
“Sawa nimekuelewa”
Yani Mariam aliitikia tu ila kiuwkeli hakujua huyu mtoto wake ana maana gani kutaka zawadi ya aina hiyo maana yeye aliona ni zawadi ya ajabu sana.

Mariam alikuwa akitembea njiani huku akiwa na mawazo sana, alipanda gari na kushuka pa kuelekea kwa mkwe wake, basi akawa anatembea huku akiwa na mawazo mengi sana, mbele kidogo akajikwaa kuangalia aliona kipande cha mti uliokatwa kimekaa njiani, hapo hapo akakumbuka kuwa mwanae kamuagiza zawadi ya kipande cha kuni ikabidi abebe kile kipande cha mti na kuondoka nacho, njiani alinunua mfuko na kukiweka kisha akaondoka nacho mpaka kwa mama kwe wake.
“Kheeee maajabu haya, leo Mariam umekuja huku!”
“Jamani mama, nimekuja kukutembelea tu”
“Tena afadhari umekuja, kabla hata hatujaanza habari zingine nikwambie hili mwanangu. Kwanza nimefurahi sana kusikia kuwa ile mimba uliyobeba imetoka maana niliona wazi kuwa ni balaa lingine unataka kulileta kwenye ukoo, balaa moja halijaisha halafu unataka kuleta lingine!”
“Kwahiyo mama sitakiwi kuzaa tena?”
“Kwasasa hutakiwi kubeba tena mimba hadi pale tutakapokufanyia tambiko Mariam, unajua kiumbe ulichokileta duniani ni cha ajabu sana, yani mimi hata sijisikii kabisa kuwa karibu na yule mtoto ndiomana sijaja tena kuwasalimia. Najua hata mama yako na yeye ndio hivyo hivyo maana sidhani kama kaja tena kwenu toka kipindi kile”
“Ni kweli hata yeye hajaja”
“Kwa maajabu ya mtoto wenu, unadhani ni nani anayeweza kujitoa ufahamu na kuja nyumbani kwenu? Kwakweli hapana, tutakuja kwenye msiba wa yule mtoto”
“Mmmmh mama, kuna kitu nimekuja kukuomba?”
“Kitu gani? Kiwe na mafanikio ya kumuondoa yule mtoto”
“Ndio mama, ni hivi naomba funguo ya ile nyumba ya bondeni nataka kule aende kuishi yule mdada wa kazi, na sababu mtoto anampenda sana yule dada basi lazima atataka kwenda kuishi nae”
“Kheee ile nyumba mliyosema ina mambo ya ajabu ndio mnataka mpeleke hao watu tena?”
“Ndio mama, angalia ile nyumba kila mtu anaiogopa bora waende wakake hawa hawa ili siku yakitokea mafuriko yawabebe tu”
Mama Juma alicheka kwa hoja hii ya Mariam, kisha alienda kutoa funguo na kumkabidhi Mariam kisha Mariam hakukawia sana kwani alimuaga mama mkwe wake kwanza halafu ndio aliondoka.

Juma leo akiwa kazini kwake, alishangaa sana kwani hakuna mfanyakazi mwenzio hata mmoja aliyekuwa akimsalimia wala kumuongelesha chochote hadi alipokuwa akihitaji kitu ni mtu tu anamuonyesha ila hakuna kuongea nae, kwakweli Juma alishangaa.
Alifanya kazi zake kwenye mazingira yale yale ingawa ilikuwa ni ajabu sana maana huwa anaongea na wenzie, wanataniana na mambo mbalimbali ila leo ilikuwa ni ajabu kwakweli.
Basi aliwahi kutoka na moja kwa moja alienda nyumbani kwa Pendo kwani alihisi lazima Pendo kuna jambo anaelewa ambalo limetokea.
Alimkuta Pendo akiwa nyumba ni kwake anafua, alimsalimia na kumuuliza,
“Pendo, wafanyakazi wote wameninunia hata sijui ni kwanini! Yani hawanisalimii wala nini, nimekuja tu hapa ingawa nilijua na wewe hutoitikia salamu yangu”
“Sikia Juma nikwambie, mimi nimeitikia salamu yako ingawa mimi nimeyashuhudia kwa macho yangu hayo yanayosemwa na watu mbalimbali ila nimekuzoea ndio sababu naweza kuongea na wewe”
“Kwani imekuwaje Pendo?”
“Nasikia walikuwa nyumbani kwako, waliyokutana nayo ni makubwa sana halafu kuna majirani zako wamekutana nao wamewaambia mambo makubwa mno ndiomana wamekuwa hivyo”
“Duh!! Mambo gani hayo?”
“Mmmmh hata mimi sijui ila ndio hivyo”
Juma hakukawia kwani aliaga na kuondoka zake kwani aliona ni balaa kwakweli.

Mariam alivyofika tu nyumbani kwake, kitu cha kwanza kabisa, ni yule mtoto kumuuliza kuhusu zawadi yake na kumfanya Mariam amtolee kile kipande cha kuni ambacho aliagiza ingawa Mariam hakujua ni kwanini huyu mtoto ameagiza kipande cha kuni, yani yeye alifanya kumtimizia tu bila kujua kitu anachokitaka kufanya yule mtoto.
“Asante mama”
Mariam hakuongea jambo kwani moja kwa moja alienda kwa wifi yake mama Shamimu na kumueleza kinagaubaga kile ambacho ameongea na mama yao, ambapo Mama Shamimu na yeye aliafikiana nae, kisha akamwambia,
“Tena nimekumbuka wifi, hiyo nyumba si ndio ile wapangaji wake wanakimbia?”
“Ndio hiyo hiyo hadi mwisho wa siku tukaifunga na kumpelekea tu funguo mama”
“Ila kweli bora kuwapeleka hawa huko huko maana kuishi nao ni mtihani mkubwa sana, ila na sisi tuhame hapa”
“Ndio, tutahama maana hapa hapatufai tena”
basi walijadiliana pale na kukubaliana katika mambo ya kufanya.

Juma akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, alikutana tena na yule jirani yake ambaye huwa anamwambia maneno mbalimbali, basi alisalimia na nae na kuanza kuongea nae ambapo cha kwanza alimuuliza kuhusu rafiki zake,
“Kuna rafiki zangu nilikuja nao nyumbani kwangu jana ila nasikia kuna maneno wameambiwa ya ajabu sana”
“Mmmh ni kweli, hata mimi nimesikia hao marafiki zako walivyoambiwa, nasikia watu walikuona nao, ulivyoondoka tu wakaenda kuwaambia mambo ambayo na wenyewe waliambiwa na yule muuza samaki”
“Duh!! Hivi kwani yule muuza samaki alisema maneno gani?”
“Si alisema wewe unafuga majini ndani, sijui wewe unaishi na majini na unatoa watu kafara, mtu akiwa anakusalimia salimia ndio kiwango chake cha kutolewa kafara na wewe kinaongezeka”
“Kheeee kumbe!!”
“Ndio hivyo”
“Je wewe huogopi kwa hayo wanayoyasema?”
“Hapana, mimi siogopi toka mara ya kwanza nimekwambia kuwa mimi nakuona ni mtu wa kawaida tofauti na watu wanavyosema, kwahiyo kama nitatolewa kafara basi tena ila mimi naona upo kawaida”
“Nashukuru sana ndugu yangu kwa hilo”
Basi Juma aliagana na huyu jirani na kuondoka zake, ila kwasasa alielewa ni kwanini rafiki zake hawataki tena kumsalimia, ni kwanini wale majirani waliokuwa wakimsalimia awali walikuwa hawamsalimii tena, alielewa sasa sababu iliyokuwa ikiendelea, basi aliondoka tu na kurudi nyumbani kwake.

Usiku wa leo, Juma anamueleza mke wake kuhusu mambo yanayoendelea na kile kilichokuwepo kuwa rafiki zake wote hawamsalimii wala nini,
“Kheee ila mume wangu niliwahi kukwambia kuwa huyu mtoto ipo siku atatuletea mabalaa ndio haya sasa naona, jamii nzima itatukataa”
“Ni kweli mke wangu, hapa sina hata hamu ya kwenda kwneye shughuli zangu, nitakuwepo hapa hapa nyumbani ila kwakweli sijui ni kitu gani ambacho tunaweza kufanya ili tuondokane na hili tatizo”
Mariam ilibidi amwambie mume wake kuhusu alichoamua kukifanya kwa siku hiyo na pale ambapo ameafikiana napo, kwakweli Juma na yeye aliona kuwa wazo hili ni jema sana, kwahiyo wakapanga kesho yake waongee tena na Anna ili aweze kuhamia huko pamoja na mtoto maana Anna na yule mtoto hawakumtaka kwenye maisha yao.

Kulipokucha tu, baada ya kupata kifungua kinywa ndio walikaa sasa huku Mariam akianza ile hoja kwa Anna,
“Sasa Anna mdogo wangu, si ndio nikupeleke kule!”
“Sawa dada”
“Utaweza kwenda kuishi peke yako?”
“Sasa nitaenda kuishi na nani dada?”
“Mmmmh labda uende na mtoto”
Basi mtoto na yeye akadakia na kusema,
“Hivi mama mbona unakosa huruma kabisa kwa mtoto wako lakini kwanini? Unajua wazi kuwa Anna ni mchawi wa wachawi halafu bila aibu unasema kuwa Anna akaishi na mimi kweli!!”
Juma akaamua aseme yeye,
“Mwanetu, tunajua wazi kuwa Anna hawezi kukuroga wewe, sidhani kama mama yako ana nia mbaya na wewe, ila tu kwavile kaona kuwa unaweza kupambana na wachawi ndiomana”
Mtoto akauliza kitu kingine,
“Halafu mnasema kuwa ile nyumba ina mambo ya ajabu, je mimi mtoto mdogo na huyo Anna, tutaweza kupambana na hayo mambo ya ajabu?”
Mariam akajibu,
“Mnaweza mwanangu, wewe una uwezo mkubwa sana. Kwahiyo kule mnaweza kupambana na chochote kile”
Yani walikuwa wanafanya kila jitihada ila hawa wawili wakubali kwenda kuishi huko mbali kwani waliona kuishi nao hapo ni tatizo kubwa sana kwao, mtoto hakusema kitu kingine kwahiyo wakamwambia Anna kuwa wajiandae ili wawapeleke.
Na kweli Anna alijiandaa vizuri kabisa, kisha walipomaliza kujiandaa walimkuta Mariam na Juma nao wameshajiandaa maana walisema kuwa wao ndio watawapeleka kule kwenye ile nyumba, huku mama Shamimu na yeye akijiandaa kwaajili ya kuondoka hapo na kurudi nyumbani kwa mama yake.

Juma akiwa na Mariam, pamoja na Anna na yule mtoto waliongozana pamoja hadi kwenye ile nyumba ambapo palikuwa ni kimya sana, ni miti tu ndio ilipepea sababu nyumba yenyewe ilikuwa pembezoni kidogo ya mji halafu ilikuwa kwa bondeni kwahiyo palikuwa ni kimya sana.
Basi Mariam alifungua mlango na kuwakaribisha wengine ndani, kilichowashangaza ni kukuta nyumba ikiwa safi kabisa, wakati mara nyingine huwa wakija wanaikuta hii nyumba imejaa matandabui na vumbi ila leo waliikuta ikiwa safai sana kiasi kwamba mtu yoyote anaweza kuishi, kitu pekee ambacho kilikuwa kinawashinda kwenye hii nyumba ni kulala na kuhisi kama kuna watu wanatembea ndani ya ile nyumba na ndiomana walihama na kuifunga, na kila waliyempangisha alishindwa na kuondoka, kwahiyo waliona ni sawa kabisa kwenda kuishi Anna mahali pale.
Basi waliingia ndani ila Mariam na Juma hawakukaa mule ndani, kwani waliwaaga Anna na yule mtoto huku wakiwaahidi kuwa watakuwa wanaenda kuwasalimia.
Basi Mariam na Juma wakaondoka huku wakiwa na furaha sana kuwa wamewaweza wale watoto, waliondoka hadi nyumbani kwao walipofungua mlango na kuingia ndani walishangaa sana kujikuta wakiingia kwenye nyumba ile ile ya bondeni.

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano 0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 29

Basi Mariam na Juma wakaondoka huku wakiwa na furaha sana kuwa wamewaweza wale watoto, waliondoka hadi nyumbani kwao walipofungua mlango na kuingia ndani walishangaa sana kujikuta wakiingia kwenye nyumba ile ile ya bondeni.
Hii ilikuwa ni ajabu sana kwao na hawakutegemea wala nini, cha kwanza kabisa waliwaza kuwa ni mauzauza ya ile nyumba na kuwafanya waogope zaidi, Mariam ndiye aliyeanza kuongea,
“Nini hiki Juma?”
“Mmmmh hata sielewi, haya mambo nilikuwa nayasikia kwako tu. Si tulikuwa tumeshafika nyumbani!”
“Ndio, hata mimi huwa hivi hivi hata siku ile ilikuwa hivi hivi ambapo nikajikuta tu nimelala pale nyumbani halafu wewe ukasema eti nimerudi usiku, sikurudi mimi bali ilikuwa hivi hivi”
“Mmmh mke wangu, tusianze mjadala inabidi tujue cha kufanya”
Hapa Mariam akawa mpole kwani aliona wazi jinsi gani kale katoto kao kanavyopenda kunyenyekewa, basi alipiga magoti pale na kusema,
“Mwanangu, popote pale ulipo najua wazi unanisikia, naomba tuhurumie wazazi wako. Akili zetu fupi zinatusumbua sana, tunashindwa kufikiria zaidi yani sisi tunafikiria ya hapa hapa, tuhurumie wazazi wako”
Pale pale wakasikia sauti ya mtoto na kushtuka sana, kumbe alikuwa pale pale sebleni pamoja na Anna, yani walishtuka hadi Juma alijikuta akipiga magoti pia, kisha yule mtoto akasema,
“Mama, na baba mimi sina tatizo na nyie ila ni kwanini mtake kuniacha mimi kwenye nyumba moja na Anna? Kulala nae isiwe sababu ya nyie kunihalalisha mimi niwe kwenye mikono ya Anna!”
“Tusamehe mwanangu, basi tumuache Anna hapa halafu turudi nyumbani?”
“Hapana mama, kama nyumbani huyu Anna tutarudi nae maana kuna mambo nahitaji kuyaona zaidi kupitia yeye. Kaniahidi kubadilika, nahitaji kuyaona hayo mabadiliko, huwezi ukamuacha Anna kwenye nyumba unayosema ni ya maajabu, hivi unajua ni nani kafanya usafi kwenye hii nyumba?”
Juma na Mariam waliangaliana na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,
“Ni nani?”
“Hebu mpigieni simu shangazi”
Mariam alichukua simu yake pale pale na kumpigia simu wifi yake ambayo iliita sana na badae ndio ilipokelewa, mama shamimu aliongea kama katoka usingizini,
“Kheeee wifi ulilala?”
“Yani hata nashangaa, simu ndio imenishtua unajua nilishajiandaa hapa kwaajili ya kuondoka ila nilikaa kidogo tu na kupitiwa na usingizi hapo hapo. Nimechoka jamani hadi sijielewi
“Kheeee pole wifi”
“Ila naondoka, asanteni kwa kuniamsha. Ngoja niondoke naenda kwa mama”
“Ila ungetusubiri wifi!”
“Hapana, sitaweza”
Mariam alikata ile simu na kumuangalia yule mtoto wao kisha mtoto akawaambia,
“Ni hivi usiku wote wa jana, Anna alimchukua shangazi kiuchawi na kuja kumfanyisha kazi kwenye nyumba hii, usafi wote mnaouona ni shangazi ndio ameufanya kila kitu mnaona kipo sawa sababu ya shangazi”
Anna aliinamisha tu macho chini, kwakweli Mariam alishangaa sana na kuuliza,
“Anna kajuaje kuhusu nyumba yetu hii?”
Mtoto alitabasamu tu na kusema,
“Ambacho hujui mama ni kuwa Anna anakufahamu vizuri sana tangia zamani anakufahamu”
“Kheeee mbona sielewi”
“Utaelewa tu ila anakufahamu vizuri sana, na hii nyumba anaifahamu na ndiomana hajabisha kuletwa huku”
Kwakweli Mariam alishangaa tu ila alimuomba mtoto wake warudi ila mtoto aliwaambia kwa siku hii walale hapahapa halafu kesho yake ndio waondoke, hawakuwa na namna zaidi ya kukubali tu.

Mama Shamimu alifika muda huu kwa mama yake na kuanza kumuelezea kile ambacho kilimsibu siku hiyo,
“Yani mama ningekuwa nimefika hapa muda mrefu sana”
“Tatizo ni nini kwani?”
“Mama, hata sijui nimechoka vipi yani. Ni mejiandaa vizuri nikajilaza mara moja kheee kuja kushtuka ni Mariam anapiga simu yangu, hapo nimeamka na kukuta viungo vyote vinaniuma mama yangu”
“Dah pole sana, kale katoto eeeh!!”
“Halafu mama kale katoto ni kaajabu kweli, unajua kaajabu, yani ni kaajabu kweli unajua wewe kuna muda kanakufanyia vituko na kuna muda kanakusema vizuri”
“Kama vipi hivyo vizuri?”
“Mmmmh sijui Mariam aliwahi kusema kuwa wewe ni mchawi, basi kale katoto siku hiyo kakamwambia Mariam, sitaki tabia ya kumuita bibi yangu mchawi”
“Kheeee kumbe!!”
“Ndio hivyo mama”
“Hata kama, ukoo wetu haukataki wala kukatambua hako katoto, kila mtu ukimueleza tu kuhusu hako katoto kalivyo hakuna anayetaka kwenda kumuona Juma kabisa, yani hako katoto kamekuwa ni mkosi mkubwa sana kwenye familia”
“Ila mama, ngoja nikapumzike. Huyu mtoto namfahamu vizuri, sitaki kumuongelea sana”
“Kwani atakfanyeje na upo huku?”
“Mama, kumbuka ulianza kuharisha sababu ya kale katoto kama hujui, umepona baada ya Juma kufanya adhabu ya kukapeleka stendi kila siku, mmmh mama sitaki kukaongelea sana”
Ila mama Juma hakuona tatizo kukaongelea hako katoto kwwahiyo alikuwa akimshawishi tu mama Shamimu wawe wanakiongelea kile kitoto.

Ilipokuwa inakaribia jioni, Mariam akatoa wazo kuwa bora warudi tu maana hapo hata chakula hawajaweka watakula nini ila bado mtoto aliwakazania walale pale pale kitu ambacho Mariam alikipinga kabisa na kuzidi kumuomba mtoto wake kuwa warudi nyumbani na mwishowe yule mtoto alikubali kwahiyo wote kwa muda ule ule walianza safari ya kurudi nyumbani kwao.
Wakiwa kwenye daladala kwenye mida ya saa tatu usiku huku Mariam akiwa amempakata yule mtoto ila kuna mtu ambaye Mariam alikaa pembeni yake yule mtu alikuwa akiguna tu na alipigiwa simu na kuongea nayo kwa kiligha ila ile lugha Mariam alikuwa akiielewa ni kitu gani ingawa yeye alikuwa hawezi kuiongea ila ilikuwa ni lugha ya kwao, alimsikia akisema,
“Nimekaa na mama mmoja kwenye gari, kabeba mtoto wa ajabu sijapata kuona katika maisha yangu tangu ulimwengu uumbwe, hapa nilipo nina mashaka sijui kama nitafika nyumbani. Naomba mniombee tu”
Mariam alimuangalia yule mama kisha alimuangalia mtoto wake ambaye alimuona yupo kawaida tu, yani uajabu wa yule mtoto Mariam alikuwa akiuona kwenye matendo yake ila hakujua kama mtu mwingine anaweza kumuangalia tu huyu mtoto na kumuhisi kuwa ni mtoto wa maajabu ingawa kitu kama hiko kishawahi kutokea kwa baadhi ya watu kama yule muuza samaki aliyesema mtoto ni waajabu bila ya mtoto kuongea wala nini. Kwakweli Mariam alikuwa kamshika mtoto wake ila alikuwa na mashaka sana katika moyo wake, hata hakuwa na amani kabisa kabisa.
Basi lile daladala liliendelea kwenda, na mbele yule mama alishuka alionekana kushuka huku akisema,
“Asante Mungu, asante Mungu…..”
Yani Mariam alimuangalia huyu mama bila kummaliza, halafu kuna mtu mwingine alipanda na kukaa pale pembeni yake, yule mtu ndio alimuuliza Mariam kabisa,
“Samahani dada, kwani ni mtoto wa aina gani umebeba huyu?”
Mariam akamuangalia na kumuuliza,
“Kwani wewe unamuona ni wa aina gani?”
Mariam alikuwa amemfunika kidogo mtoto, akamfunua ambapo yule mtu alimuangalia sasa mtoto na kujikuta akisema,
“Dah!! Sijapata kuona mtoto mzuri kama huyu duniani”
Mariam akapumua kidogo maana alihisi kuna jambo baya litaongelewa, basi Mariam akatabasamu na kujibu,
“Asante”
Kisha yule mtu akaendelea kusema,
“Yani hongera sana, una mtoto mzuri sana hadi raha kumuangalia, hongera sana mtoto wako ni mzuri sana”
Hapa akajibu mtoto sasa,
“Hakuna mtoto mbaya duniani”
Yule mtu aliamua tu kukaa kimya kwani aliona hapa tena habari inakuwa nyingine na wala hawakuongea mpaka wakina Mariam waliposhuka na kuondoka zao.
Ilibidi Juma apitie kwenye vibanda wanavyokaanga viazi na ndizi na kununua kisha wakarudi navyo nyumbani kwao.

Leo wakiwa nyumbani, hakuwepo mama Shamimu maana tayari alishaondoka basi mtoto akasema,
“Ila shangazi hajaniaga jamani!”
Juma alijikuta tu akimuhurumia dada yake na kumuombea msamaha kwa mtoto wake,
“Naomba umsamehe shangazi yako, alighafirika tu naomba umsamehe sana”
“Mpigie simu na aniombe msamaha mwenyewe”
Basi Juma alimpigia simu dada yake ambaye baada ya muda mfupi tu alipokea kisha Juma akamwambia,
“Dada, naomba umuombe msamaha mtoto maana umeondoka bila ya kumuaga”
“Uwiiiii nilijisahau, naomba tu nimuombe msamaha”
Juma akampa ile simu mtoto sasa ambaye moja kwa moja alianza kuongea,
“Kwanini shangazi umeondoka bila ya kuniaga?”
“Naomba unisamehe mwanangu, nisamehe sana nao,ba unisamehe”
“Utakuja lini tena kunitembelea?”
“Nitakuja mwanangu, nitakuja tu hakuna tatizo”
“Lini sasa?”
“Baada ya miezi mitatu”
“Kheeee utakuja tena na hilo begi lako kubwa?”
“Hapana, nitakuja tu kuwasalimia na kurudi, naomba unisamehe sana”
Kisha yule mtoto alikata simu na kumuangalia mama yake ambapo alimuuliza,
“Mama, shangazi ameishi hapa kwa muda gani?”
“Mmmmh sijui miezi miwili sijui mitatu”
“Haya sawa”
Mtoto hakusema kitu kingine chochote kwahiyo walikuwa kimya tu wakiendelea na mambo mengine huku Anna akikumbusha kuhusu yale mahindi maana tayari yalikuwa ni makubwa, basi walienda kuchuma na kuchemsha kisha walianza kuyala huku wakiyasifia kuwa ni matamu, basi mtoto akasema,
“Mama, wewe ndiye tunayepaswa kukushukuru maana umelima mwenyewe, umepalilia mwenyewe na umeyahudumia haya mahindi mwenyewe”
Mariam alikaa kimya tu kwani kila akifikiria kuwa yeye ndiye aliyekuwa akilimishwa kiuchawi aliumia sana, na kufanya ashindwe kusema lolote wala kufanya lolote.

Kwasasa, Juma aliamua tu kushinda nyumbani kwake yani alikuwa haendi kwenye shughuli zake kabisa kwahiyo kila siku alikuwa akishinda nyumbani.
Siku hii alienda kununua samaki maana Mariam alimuagiza samaki, basi alipokuwa kule kwenye samaki ndipo alipomuona na yule muuza samaki ambaye huwa anpitisha mitaani, basi akamuita ila huyu muuza samaki mara nyingi huwa hamfahamu Juma, kwahiyo alisogea tu kuongea nae,
“Vipi kijana hujambo?”
“Sijambo kabisa mzee wangu, shikamoo”
“Marahaba, wewe ni kijana mdogo sana. Nilipata taarifa kuwa kuna nyumba sijui wanafuga majini ulienda kuuza samaki ni nyumba gani hiyo?”
“Mmmmh ni nyumba moja hivi ipo kama unapandisha kidogo kilima, yani ipo kwa juu juu hivi halafu eneo lile kama imejitenga maana ipo peke yake”
“Kwahiyo ana majini?”
“Ndio, anafuga majini yule kwakweli niliogopa sana hadi leo ile njia sipiti”
“Wewe ulijuaje kuwa ni majini?”
“Yani mimi mzee nimechanjiwa kwahiyo vitu ambavyo sio vya kawaida naviona mzee, yule mama mwenye nyumba huwa namuuzia samaki tena mara nyingi tu nishamuuzia, nashangaa siku hiyo aliita mtu amletee bakuli la kuwekea samaki kutoka ndani, khaaa akatoka jini mdogo na mkubwa”
“Khaaaaa!!”
“Halafu yule mama pale nje alianza kucheka pia, tena kile kicheko cha majini majini”
“Duh!! Pole sana, ukafanyaje sasa?”
“Asante, yani nilikimbia hata hela sikudai wala nini. Nilikimbia na sehemu ya kwanza nilisimama kwa mzee mmoja ambaye ni mjumbe wa mtaa na nilimueleza kila kitu kuhusu nilichokiona pale kwenye nyumba, ndipo wengine walitokea na kusema kuwa mzee wa hiyo nyumba anafuga misukule, yani kadri watu wanavyomsalimia ndivyo watu hao wanavyokufa, anayemsalimia mara nyingi ndio muda wake wa kufa unakuwa karibu halafu anageuka na kuwa msukule wa huko mzee, kwakweli niliogopa sana”
“Pole sana kijana”
“Asante”
“Nashukuru kwa taarifa, nitaifanyia kazi”
“Huwezi mzee, mtaa wote huu umeshindwa, nasikia walitaka kuchoma nyumba moto, khaaa mvua ya mawe ilipotokea ni balaa tena iliambatana na upepo mkali sana halafu badae ilinyesha mvua ya kawaida hadi panakucha, kwakweli pale pana majini, kuna njia pale karibu ila kwasasa hakuna mtu anyepita kila mtu anapaogopa”
Juma alimshukuru yule kijana na kuachana nae, kwakweli alijiuliza moyoni bila ya jibu, lile jambo la kuona anaogopewa kiasi kile mtaani lilimpa mashaka sana yani anaogopewa bila kujulikana maana sio wote wanaomjua.

Leo Mariam na Anna, alikuwa akiongea nae na kumwambia kuwa amuelekeze kupika ila isiwe kila siku anapika yeye,
“Yani Anna, hayo maswala ya kunifanya nilale halafu unifanyishe kazi siyataki kwakweli, naomba tu niwe nakuelekeza namna ya kupika. Ndio mama yako alikulea vibaya, ila isiwe tatizo la kututesa sisi wengine tusiohusika, naomba uje jikoni niwe nakufundisha hadi ujue kupika”
Kwahiyo Anna alienda jikoni ambapo Mariam alianza kumuelekeza namna ya kupika ila kila alipokuwa akimuelekeza aliona anajiwa na uzito sana kwenye mikono yake hadi aliamua kumfokea Anna,
“Yani nakuelekeza hapa hapa unaniroga! Mbona huna akili wewe janmani, akili zako ni vipi Anna, mbona unafanya mambo ya kijinga?”
“Samahani dada”
“Napoteza muda wangu kukuelekeza hapa kwa faida yako mwenyewe, ila wewe hutumii akili yani upo kutumia sijui vitu gani eti unaniroga mikono khaaa sijapata kuona mtoto mwehu kama wewe Anna jamani!”
“nisamehe dada”
“Nikusamehe nini mwehu wewe, haya kaa chini hapo uanze kupika yani nitakuwa nakuelekeza kwa mdomo tu na ukase mkono hapo jikoni”
Mariam aliamua kuinuka na kumuacha Anna akae jikoni huku akimuelekeza, yani kiukweli kwasasa Mariam hakumtaka kabisa Anna ila hakuwa na jinsi sababu ya mtoto wake.

Walipomaliza kula, Juma alikaa na familia yake na kuanza kuwaeleza yale ambayo aliongea na yule muuza samaki kisha aliwauliza,
“Jamani, kati yetu kuna jini?”
Mtoto akauliza pia,
“Kwani nani unamuona ni jini hapa baba?”
Juma alimuangalia huyu mtoto na kusema,
“Mimi sijui ila nimueuliza tu sababu ya haya mambo ambayo yametokea na jinsi ambavyo muuza samaki amesema”
Yule mtoto akasema,
“Hakuna jini hapa baba, labda angesema kamuona mchawi ambapo moja kwa moja jibu lingekuwa ni Anna tu hapo bila wasiwasi wowote”
Mariam akasema,
“Au Anna ni mchawi halafu ni jini pia maana mtu anawezaje kumchukua mwenzie wakati amelala na kwenda kumfanyisha kazi! Kiukweli Anna hadi unaniogopesha jamani, ni bora hata ungebaki kule kule”
“Nisamehe dada”
Yani Anna kwa kipindi hiki alikuwa akitumia zaidi neno nisamehe kuliko neno lingine lolote lile, walikuwa wakimuangalia tu ila walikuwa wakimchukia sana.

Zilipita kama wiki nne ambapo Mariam alianza kujihisi tofauti na kujihisi kuwa huenda akawa ana mimba maana aliona dalili zote za kuwa hivyo ila alitaka uhakika zaidi kwa siku hiyo kwenda hospitali.
Alimuaga kawaida tu mume wake kuwa anaenda hospitali maana siku hii hakutaka hata kusindikizwa na mume wake.
Basi akajiandaa na moja kwa moja kwenda hospitali kupima, na alipopima tu akaambiwa kuwa ni mjamzito basi alipotoka tu pale alimpigia simu mama mkwe wake ili kumuambia habari ile ingawa alijua wazi kuwa mama mkwe wake lazima achukie,
“Mama, nina mimba tena”
“Kheee Mariam, una wazimu wewe au ni kitu gani? Si tumekwambia hadi tufanye tambiko”
“Najua mama, sasa hilo tambiko hadi lini? Maana kila siku unasema hivyo hivyo, mimi nina mimba tayari”
“Sasa hivi hata ukibeba hiyo mimba kwa miaka mitatu usinisumbue maana mimi nimekwambia cha kufanya hutaki”
“Sasa mama ndio ishatokea nifanyeje sasa?”
“Unadhani nitakwambia nini hapo? Eeeeh nimekumbuka, sib ado mnaishi na yule mdada mchawi au ndio ulimuacha kwenye ile nyumba?”
“Alikataa mama, tunaishi nae bado”
“Basi nenda kamwambie kuwa una mimba, najua atakutoa tu hiyo mimba, halafu akishakutoa uende hospitali ukaweke kitanzi huko usituletee balaa kwenye ukoo sie”
“Mmmmh mama! Hutaki wajukuu kabisa”
“Wajukuu wa kishetani nani anawataka? Sitaki ushetani katika maisha yangu, hao watoto wa kishetani bakini nao wenyewe, mimi siwataki”
Ile simu ilikatika kisha Mariam akatabasamu tu na kusema,
“Kheee yani huyu mama mkwe jamani loh!! Ila huwezi jua pengine huyu mtoto anaweza kuwa bora mmmh!!! Ngoja nikifika tu nyumbani niseme kuwa nina mimba nione usiku wake itakuwaje!”
Mariam alijisemea kisha akarudi nyumbani kwake.

Mariam alipofika tu, kitu cha kwanza kabisa aliwaita wote kisha akawa pale kama anamwambia Juma ila ujumbe ulikuwa unafika kwa wote maana wote walikuwepo pale sebleni,
“Juma mume wangu, nina mimba. Karibia tutampata mdogo wake mtoto wetu”
Juma alitabasamu na kufurahi sana, yani akajikuta amesahau kabisa kama kuna mimba iliharibika mule ndani sababu mule ndani wanaishi na mchawi.
Juma alikuwa tu akimpongeza mke wake na kumlaumu kwenda peke yake hospitali,
“Ilitakiwa twende wote jamani Mariam”
“Usijali hakijaharibika kitu”
Ilikuwa ni siku ya furaha tu kwao, ni Mariam pekee ambaye kwa muda huo alikuwa na wazo kuwa Anna ana uwezo wa kuiharibu ile mimba.
Usiku wakati wa kulala, yani Mariam alipopitiwa na usingizi tu alihisi kama kuna mtu anamkandamiza tumboni halafu kama alitokea mtu mwingine na kumsukuma yule mtu halafu akasikia,
“Mama, amka”
Aliposhtuka alishangaa kumuona mtoto wake akiwa pembeni yake.

Itaendelea……!!!
Ofa nichek whatsapp kwa 0629980412 kwa Tshs 1000 tu
 
MTOTO WA MAAJABU: 30

Usiku wakati wa kulala, yani Mariam alipopitiwa na usingizi tu alihisi kama kuna mtu anamkandamiza tumboni halafu kama alitokea mtu mwingine na kumsukuma yule mtu halafu akasikia,
“Mama, amka”
Aliposhtuka alishangaa kumuona mtoto wake akiwa pembeni yake.
Kwakweli Mariam alijikuta akiogopa na kutetemeka, alikaa kitandani kwa uoga na kutaka kuuliza ila aliona mdomo mzito ila mtoto wake akamwambia,
“Mama, usijali kitu nipo kwaajili ya kukulinda”
Mariam kila alichotaka kuongea aliona kamavile mdomo wake unasita kusema neno lolote lile, yani alikuwa anaona tofauti sana, kisha mtoto akamwambia,
“Unaweza kulala sasa mama, kuwa na amani, hakuna kibaya kitakachoweza kukupata”
Mariam alimuangalia huyu mtoto ila hakusema neno bali alijilaza tu.
Kulipokucha, Mariam alikumbuka kila kitu na kuanza kumsimulia Juma vile ilivyokuwa,
“Kheeee au Anna alikata kukutoa tena mimba?”
“Nahisi hivyo ila kiukweli huyu mtoto wetu simuelewi mimi”
“Kwanini?”
“Hivi unadhani ni kitu cha kawaida kweli? Mtu anasema nipo kwaajili ya kukulinda? Yeye ni nani hadi aweze kunilinda mimi? Yani hapo ndio penye utata mume wangu, huyu mtoto ni nani?”
“Mmmmh hata mimi hapo sielewi, ila nadhani humu ndani tunaishi na binadamu mbaya kuliko huyo mtoto. Kwakweli huyu Anna ni kiumbe mbaya tena asiyefaa kabisa maana mambo yake sidhani kama binadamu wa kawaida anaweza kufanya”
“Natakiwa kumsema, siwezi kunyamaza kimya kwenye hili”
“Ila Mariam hukusema kwa makusudi kweli jana?”
“Ni kweli nilisema kwa makusudi ila huwezi amini, alipotokea mtoto na kusema yupo tayari kunilinda nimejikuta nikiumia moyo sana kwa kutaka mimba itolewe kichawi, nimejikuta nikimpenda mwanangu huyu niliyembeba kupita kiasi, sitaki hii mimba itolewe, nataka kumpata mtoto wangu”
Juma alimsogelea mke wake na kumshika tumbo lake kisha akasema,
“Huyu mtoto aliyekuwepo humu tumboni atakuwa ni mtoto wa tofauti sana katika maisha yetu, na yeye ndiye atakayeyabadilisha maisha yetu”
Mariama alitabasamu yani alijikuta tu akihisi furaha moyoni mwake.

Mariam alitoka chumbani muda huu na kumkuta Anna akijikongoja tu kusafisha nyumba, kidogo alimshangaa maana siku hizi mara nyingi Mariam alikuwa akisafisha nyumba mwenyewe, basi Mariam alienda kukaa na kumuuliza Anna,
“Vipi mbona unasafisha nyumba leo?”
“Nimepewa adhabu na mtoto mama”
Hapo Mariam alimuita karibu kwanza, kisha Anna aliposogea, Mariam akamnasa kibao Anna kisha akamwambia,
“Hivi wewe Anna, ni nani ambaye anaweza kukuvumilia ujinga wako unaoufanya, ni nani anayeweza? Ukizingatia sio ndugu wala nini? Hivi wewe kwanini utake kunitoa mimba mimi?”
“Nisamehe dada”
“Ndio unachoweza pekee hiko au ni kitu gani? Hivi wewe unashindwa kujifikiria hata kidogo kuwa ni kitu gani unachokifanya?”
“Nisamehe dada, hata mimi mwenyewe najishangaa maana najikuta tu nikiwa na hamu ya kunywa damu ya mimba changa, yani ulivyoniambia tu kuwa una mimba nikapata hamu ya kunywa damu”
“Khaaaaa kwakweli siwezi kuendelea kuishi na wewe humu ndani maana ipo siku utatamani kututafuna nyumba nzima, mchawi mkubwa wewe, ndiomana dada yako hakutaki kabisa khaaaa unakera!”
“Hata mimi sipendi kuwa mchawi dada, hata mimi sipendi hii hali naomba unisaidie tu. Ukinifukuza sitakuwa na cha kufanya katika dunia hii”
“Unataka nikusaidiaje?”
“Nisaidie niweze kuacha uchawi”
“Uchawi unaachwa vipi?”
“Dada, mbona mimi nimekusaidia kuacha uvivu”
“Khaaaa usinichefue mjinga kabisa wewe”
Mariam hakuendelea tena kuongea na Anna kwani kwa muda huu aliamua tu kwenda jikoni kwaajili ya kubandika chai kwani ni kweli kabisa kwa kipindi hiki Mariam hakuwa na tabia ya uvivu kabisa.
Mariam aliandaa chai yake huku akifikiria vitu vingi sana, akaona kuwa kwa siku hiyo anatakiwa ajitoe muhanga na akazungumze na yule mtoto wao ili ikiwezekana Anna aondoke kabisa katika maisha yao.

Mariam kwa muda huu alienda kuongea na mtoto wake kwani alikuwa hamuogopi sana siku hizi ukizingatia mambo mengi ya ajabu mtoto alikuwa akiwaonyesha ndani kwao, basi alianza kuongea nae,
“Mwanangu nakuomba jambo moja tu, nakuomba huyu Anna tumuondoe hapa”
“Halafu ataenda wapi mama?”
“Mmmmh inabidi aende kwa ndugu zake, kwani hana ndugu?”
“Mama, huyo Anna katengwa na ndugu zake wote sababu ya huo huo uchawi yani hakuna ndugu yake hata mmoja anayemuhitaji katika maisha yake. Mimi nakuomba kuwa huyu Anna usimfukuze tu, kwani hata wewe kakusaidia mambo mengi sana”
“Kanisaidia nini sasa?”
“kakusaidia uvivu, huoni kwasasa mama yangu unaamka mara nyingine unasafisha nyumba na unapika tunakula, unaosha vyombo na wala hulalamiki kuchoka kama zamani, huoni kuwa Anna amekusaidia sana kuacha uvivu! Basi nakuomba mama huyu Anna tusimuache ahangaike tu landa umpeleke kwenye ile nyumba mliyotaka kutuweka mimi na Anna”
“Sawa hakuna shida, aende hata huko ila hapa aondoke”
“Ila ngoja nikuulize, kwasasa utakuwa unanihudumia? Hutoniogopa tena?”
“Nitakuwa nakuhudumia, yani kuhusu kukuhudumia hapo jipe maksi zote maana nitakuwa nakuhudumia kwa kila hali mwanangu”
Basi mtoto akakubali kuwa Anna aende kwenye ile nyumba nyingine, Mariam hata hakutaka kupoteza muda kabisa kwani alijitahidi kuongea na mume wake ili siku hiyo hiyo Anna apelekwe huko na kweli Anna aliambiwa kuwa ajiandae ili aende huko na Juma ndiye aliyesema kuwa atampeleka.
Basi walipomaliza kujiandaa, Anna na Juma waliondoka na pale nyumbani alibaki Mariam na mtoto.

Juma aliondoka na Anna hadi kwenye ile nyumba ila alipomfikisha alimtaka tu mwenyewe aingie maana Juma hakutaka hata kuingia ndani akihofia uchawi wa Anna, yani alikuwa akihofia kufanywa kitu kibaya na Anna.
Kwahiyo Juma aliondoka zake na njiani alikutana na jirani yao wa maeneo ya kule na kusalimiana nae maana huyu jirani walionana nae siku nyingi sana,
“Vipi mkeo alijifungua eeeh!!”
“Ndio, siku nyingi sana”
“Naona na mtoto atakuwa amekuwa sana”
“Ndio, amekuwa sana kwasasa”
“Hengereni jamani, sijui ni nani nilikutana nae akasema mke wa Juma hajajifungua ana mimba kubwa kama kabeba taifa”
Juma alicheka tu na kutikisa kichwa huku akisema,
“Ila watu wa wa ajabu sana, alikuwa na uhakika gani kama hiyo mimba ndio ya yule yule mtoto?”
“Ndio hapo sasa, kwahiyo una watoto wawili sasa?”
“Ningekuwa nao wawili ila huyo mwingine ni bahati mbaya”
“Dah! Pole sana, kazi ya Mungu haina makosa. Ila Juma naomba nikwambie kitu leo ya kwanini wapangaji wako huwa wanakimbia kwenye ile nyumba yenu”
“Eeeeh kwanini?”
“Yani historia ya eneo lile sikuijua kumbe bhana nasikia lile eneo lilikuwa na kaburi na mwanzoni walikuwa wanapaita kaburi moja ila kuna mtu akafanya figisu na kuliuza ndio nyie mkajenga”
Juma akashangaa maana hii stori hajawahi kuisikia hata mara moja, akauliza tena,
“Sijakuelewa jirani”
Yule jirani akarudia maelezo yale yale,
“Kwahiyo ndio historia ya eneo lile kuitwa kaburi moja kumbe!”
“Eeeeh ndio, nasikia ndio historia yake ila watu walivyojenga jenga ndio kidogo pakabadilika jina, ila si umeona kule bondeni ipo nyumba yenu tu! Ni kwamba pale bondeni ndio ambako kulikuwa na hilo kaburi moja”
“Duh!! Asante kw akunielimisha”
Yani Juma hata hakuongea sana na huyu jirani yake wa huku kwani muda huu huu alienda kupanda basi na kurudi nyumbani kwake.

Juma aliporudi tu nyumbani kwake, jambo la kwanza kabisa kuongea na mke wake ilikuwa ni kuhusu yule mpangaji alivyomwambia kuhusu ile nyumba yao nyingine, hata Mariam alishangaa sana na kusema,
“Haya ndio matatizo ya kujenga nyumba bila kuuliza historia ya eneo hilo”
“Ndio mke wangu, yani wakati ananisimulia nimehisi hadi ubaridi ukipenya katika mwili wangu, najiuliza hapa au mambo yote haya ya kuhusu mtoto ni sababu ya pale?”
“Mmmmh inawezekana ujue maana nakumbuka hata mimba nimeipatia pale, au umesahau?”
“nakumbuka vizuri sana, si tulipoona inasumbua ndio tukaenda kupanga na mwishowe tukaja kujenga huku! Nakumbuka vizuri sana Mariam, kwahiyo unahisi kitu gani hapo?”
“Mmmmh hata sijui cha kusema, ila huyu mtoto wetu huwa unamuelewa yani leo nimekaa nae hapa roho juu juu”
“Ila kakuongelesha kwani?”
“Hapana, hajaniongelesha kitu chochote nilikuwa nafanya kazi zangu tu ila ndio roho juu juu kama naunguliwa na nyumba vile”
“Basi kesho naenda kwenye shughuli zangu”
“Hapana usiende, tuangalie upepo kwanza, sijazoea mwenzio kukaa peke yangu na hiki kiumbe chetu Juma”
Yani kwa muda huu walianza kuongelea kuhusu mtoto na kusahau kuwa walikuwa wakiongelea ile nyumba yao yenye mambo ya ajabu ambayo wamempeleka Anna aende kuishi huko.

Siku ya leo kulivyokucha tu, ilibidi Mariam aende kumfungulia yule mtoto wao mlango maana walimlaza chumba kile kile alichokuwa analala na Anna, basi mtoto akatoka na kukaa sebleni ambapo Juma na yeye alitoka chumbani na kuanza kufanya kazi huku akisaidiana na mke wake yani huyu mtoto alikuwa akiwaangalia tu jinsi walivyokuwa wakifanya kazi, na walipomaliza kufanya kazi zote walikaa sasa na kuanza kula ambapo Mariam aliweka chakula ili amlishe mtoto kama ambavyo Anna alikuwa akifanya ila mtoto akamwambia,
“Acha tu mama, nitakula mwenyewe”
Basi walikaa kula huku na yule mtoto akilam yani Mariam alijikuta akimuangalia yule mtoto wake kwa macho ya wizi wizi hadi wanamaliza kula ila walipomaliza kula yule mtoto alimuuliza Mariam,
“Kwani mama huwa unanifananisha na kiumbe gani?”
Mariam akajiumauma na kujibu,
“Hapana, hakuna ninayekufananisha nae”
“Na mbona huwa unaniangalia kiwiziwizi?”
“Hapana mwanangu, suinifikirie vibaya huwa naangalia tu jinsi ulivyokuwa mzuri, yani huwa nakuona wewe ni mzuri sana”
Huyu mtoto alitabasamu na hii kitu Mariam na Juma walitambua kuwa huyu mtoto alipenda sana kusifiwa kuliko kitu chochote kile, basi walitulia tu pale bila ya kuendelea na maongezi mengine wala nini.

Usiku wa leo, Mariam alimuuliza Juma kuhusu maisha yao na hatma ya maisha yao na yule mtoto,
“Hivi Juma mume wangu tutaishi hivi hadi lini?”
“Kivipi?”
“Huyu mtoto ataishi hivi maisha yote? Atakuwa hivi? Mbona sio mtoto wa kawaida, hivi Juma umeshawahi kufikiria kuwa huyu ni mtoto wa maajabu?”
“Mmmh hata mimi huwa naona hivyo hivyo Mariam ila sasa tutafanyeje? Maana hatuna pa kwenda na wala hatuna cha kufanya”
“Tukiwa tunajadili tutapata tu cha kufanya”
“Hivi unajua kama hata tukijadili huwa yule mtoto anajua kila kitu tulichojadili hivi unajua hilo? Yani huyu mtoto huwa anajua kila kitu, hata hapa tunamsema yani kashajua kila kitu anataka tu kusikia kuwa tuna mipango gani? Mariam bado nayapenda sana maisha halafu naona maisha yana mengi ya kufanya zaidi ya huyu mtoto, ninachoamini mimi, huyu mtoto kaja kwenye maisha yetu kwa lengo maalumu, sidhani kama kaja kutuumiza maana kama angekuja kutuumiza basi angeshatuumiza, ila nadhani kazi yake ikiisha basi ataonndoka”
“Kwahiyo hata wewe unaona kuwa huyu mtoto sio binadamu eeeh!!”
“Mmmh hilo sijasema Mariam”
“Kama umesema kaja kwa lengo maamulu lazima huyu sio binadamu, sasa uliona wapi mtu anaweza kuvumilia kuishi na kiumbe chenye muonekano wa binadamu na sio binadamu?”
“Mariam naona tunaenda pabaya, mwishowe tushindwe hata kulala bure. Hebu tuachane na hayo Mariam na kwa muda huu tulale tu nakuomba mke wangu”
Mariam hakuongeza neno hapo kwani aliamua tu kumsikiliza mume wake na kulala kwa muda huo.

Kulipokucha, wakati Mariam yupo jikoni simu yake ilianz akuita na kumfanya aipokee ile simu na kuongea nayo ambapo aliyekuwa akipiga alikuwa ni mama yake, ambapo mama yake alianza kumlaumu,
“Yani Mariam juzi ulikuja hapa nyumbani hata kusema?”
“Mmmh nilikuja nyumbani hapo?”
“Ndio, si umetuletea kipande cha kuni wewe?”
Mariam akashangaa na kumuuliza mama yake kuwa kipande hiko kipo vipi na mama yake alianza kumuelekeza na mkumfanya moja kwa moja Mariam ajue kuwa ni kipande ambacho alimuokotea mtoto wake kama zawadi sababu alimuagiza, yani alijikuta akipumua tu kwa uoga, kisha akamuuliza mama yake,
“Kwahiyo mmefanyia nini hicho kipande?”
“Yani hiki kipande mwanangu kina maajabu ndiomana nimeamua kukupigia simu”
“Kivipi mama?”
“Yani ni hivi, juzi nilitoka kwenye safari zangu nikiwa nimechoka ila nikataka kuoga maji ya moto maana kuna kiubaridi siku hizi, sasa nikaona kuna hakuna ila kuna kipande hiko kimoja tu cha kuni halafu si unajua hili jiko ambalo alinitengenezea mjomba wako kuwa halitumii kuni nyingi! Nasi nikachemshia maji na kuoga na sio mimi tu kwani nyumba nzima walichemsha hapo na kuoga na wala kile kipande hakikuisha, basi jana nikasema siwashi jiko lingine napikia kuni leo, nimepika vyakula vyote na kule kipande hakijaisha mwanangu. Nikauliza kwani kipande kimetoka wapi hiki ndio naambiwa ile jioni kuwa ni wewe ulikuja juzi na kukileta ila hukukaa ukaondoka, ndiomana leo nilivyoamka tu nikaamua kukupigia, sasa kwanini mwanangu hata usinisubiri kunisalimia? Hujanikumbuka au ni kitu gani?”
“Hapana mama, nimekukumbuka sana tu”
“Sasa ulishindwa nini kunisubiri unisalimie?”
Hapa Mariam alikuwa kimya maana hata hakujua ni jinsi gani apate kujieleza kuhusu yeye kwenda kule na kile kipande cha kuni, yani Mariam hakuelewa kitu, alimuomba tu msamaha mama yake, kisha alipokata simu alijaribu kwenda kuangalia alipomuona yule mtoto anaweka kile kipande cha kuni na kweli hakukikuta halafu kumuuliza yule mtoto ilikuwa ni mtihani mkubwa sana kwake akajikuta akiwa kimya tu na kuingia chumbani kwenda kumsimulia Juma.
Mariam alimueleza maongezi yote ya kwenye simu na mama yake hata Juma alishangaa na akashauri pale,
“Kwanini tusimuulize mtoto ili tujue kuwa imekuwaje?”
“Eeeeh utamuulizaje?”
“Unamuuliza hivi, wewe uliniagiza kipande cha kuni mbona bibi yako anasema nimempelekea wakati mimi sijaenda huko?”
“Mmmmh!!”
Wakashauriana pale na mwisho wa siku wakaamua tu kwenda kumuuliza yule mtoto ili wajue imekuwaje.

Mariam alianza kumuuliza yule mtoto kama ambavyo Juma alisema kuwa wamuuliza, kisha yule mtoto akacheka na kumuuliza pia Mariam,
“Kwahiyo hapo mama umehisi kuwa ni mimi ndio nimefanya hivyo?”
“Mmmh sijui”
“Ila mama, hata ikiwa ni mimi ndio nimefanya hivyo kwani ni vibaya? Bibi anapenda sana kupikia kuni, na huwa anapata shida sana kwenye kupata kuni, aliishi na wewe miaka yote lakini hakuna hata siku moja ambayo ulijishughulisha kuwa uende kumsaidia kutafuta kuni ili apikie kile anachokipenda, je nimefanya vibaya kama ni mimi kweli?”
Mariam alimuangalia mume wake na kujibu kwa pamoja,
“Hapana, hujafanya vibaya”
Kisha Juma akauliza,
“Kwahiyo ni wewe ndio ulienda na kujigeuza ni Mariam?”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Mimi ni mtoto mdogo sana, hivi mimi naweza kujibadilisha na kuwa mama? Nitakuwa binadamu wa kawaida kweli? Hivi mimi nina uwezo wa kwenda hadi kwakina mama wakati sipajui? Ni lini mama umenipeleka kwenu? Mama nasema tu mambo kwa hisia zangu maana ni kweli mama yangu ulikuwa mvivu wewe na usingeweza kubeba kuni kwaajili ya bibi ila mimi siwezi kujigeuza mama, mimi ni mtoto mdogo sana”
Juma na Mariam waliangaliana bila ya kujua cha kusema zaidi.

Usiku wa leo, Juma alimuomba mke wake kuwa kesho yake aende kuangalia shughuli zake na kuangalia mambo yameendaje maana hakwenda kwa siku nyingi sana,
“Sasa Juma unataka kuniacha na huyu mtoto kweli?”
“Jamani si ulisema umemzoea kwasasa?”
“Ndio nimemzoea ila kiukweli bado kuna uoga flani ninao juu ya huyu mtoto, yani naogopa kweli kubaki nae peke yangu jamani!”
“Basi usijali nitawahi kurudi yani hata sichukui muda mrefu kwakwlei, naenda kuangalia tu mambo yanaendaje”
Yani Mariam alikubali tu kwa shingo upande maana hata hivyo Juma atakaa nyumbani hadi lini wakati pale wanahitaji kula, kuvaa na kuishi vizuri.
Kwa muda huo walilala, na kulipokucha tu Juma alijiandaa na kuondoka zake.

Leo Mariam alibaki mwenyewe na huyu mtoto wake ila kwasasa alikuwa akijivika ujasiri wa hali ya juu katika kubaki na kuishi na huyu mtoto hata pale alipoulizwa na mtoto alikuwa akishtuka ila alikuwa hashtuki sana, muda huu mtoto alimuuliza,
“Mama, unamfahamu Mishi?”
Swali hili lilimshtua sana Mariam kwani hakulitegemea kutoka kwa mtoto wake.

Itaendelea…….!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 unaipata full kwa 1000 tu watu 10 wa mwanzo ntawapa kwa 500
 
MTOTO WA MAAJABU: 31

Leo Mariam alibaki mwenyewe na huyu mtoto wake ila kwasasa alikuwa akijivika ujasiri wa hali ya juu katika kubaki na kuishi na huyu mtoto hata pale alipoulizwa na mtoto alikuwa akishtuka ila alikuwa hashtuki sana, muda huu mtoto alimuuliza,
“Mama, unamfahamu Mishi?”
Swali hili lilimshtua sana Mariam kwani hakulitegemea kutoka kwa mtoto wake.
Yani Mariam hata hakujua amjibu vipi huyu mtoto wake ila mtoto wake akamuuliza tena,
“Mama, unamfahamu Mishi?”
Mariam akamuangalia kwa uoga mtoto wake na kujibu,
“Simfahamu”
Yule mtoto akatabasamu na kusema,
“Mama, humfahamu Mishi wakati Mishi alikuwa ni rafiki yako toka nitoke! Ila tu kitu ambacho hufahamu ni kuwa Mishi amewahi kuwa mke wa baba, yani yeye ndiye aliyeolewa na baba kabla yako”
Hapo Mariam alishangaa sana na kuuliza,
“Kwani Juma aliwahi kuoa kabla yangu?”
Mtoto akatabasamu tena na kusema,
“Ndio, na Mishi ndiye aliyekuwa mke wa baba kabla yako. Kule ambako ulimsindikiza Mishi kipindi kile alikuwa ni mke wa mtu halafu mimi ni….”
Mariam alijikuta hata kuogopa kuendelea kuongea na mtoto wake kwani alitoka nje na kukaa nje huku akiwa na uoga mkubwa katika moyo wake, yani alikuwa akitamani tu Juma arudi maana alikuwa ameanza kumuogopa mtoto.

Juma leo alipoenda kwenye shughuli zake bado alikuta na ile hali kama ya siku ile ya watu kutokumsalimia wala nini ila hakukawia sana na kuondoka zake, muda anaondoka alipita ile njia ambako huwa anakutana na yule binti na kweli alikutana nae, basi alimsalimia na kuanza kuongea nae ambapo swali la kwanza alimuuliza,
“Najua wewe binti una utashi mkubwa kuliko wangu, wafanyakazi wenzangu wote hawataki kunisalimia yani hakuna anayetaka kuwa karibu na mimi kabisa kutokana na maneno ambayo wameyasikia kunihusu mimi ingawa kiukweli mimi siwezi kufanya hivyo na ile kazi ninayofanya bila kuwasiliana na watu ni ngumu sana, kwahiyo napata wakati mgumu haswa”
“Pole sana, tena pole ila ngoja nikwambie waite wafanyakazi wenzio wote kama kikao. Unajua kwenye lile eneo wewe unasikilizwa sana na mmiliki wa pale kuliko yeyote yule, mwambie awaite wote, halafu ukikaa nao waulize ni kwanini hawataki kuongea na wewe, wakikwambia hizo sababu walizoambiwa waulize kuwa je umewahi siku yoyote kumuua mtu yoyote yule? Kuna mtu yoyote umemfanya msukule nyumbani kwako? Halafu wakaribishe wote nyumbani kwako ambapo wataenda kupata chakula kizuri kilichopikwa na mkeo kwa hakika watafurahia sana”
“Mmmmh na mtoto je! Maana yeye ndiye aliyewatisha”
“Tatizo lako wewe unashindwa jinsi gani uishi na yule mtoto, mbona kitu rahisi tu. Ongea na mtoto wako mwambie kuwa naomba ukae chumbani mwanangu wakati wageni wangu wamekuja halafu wakiondoka utatoka, yule mtoto wako mbona ni muelewa sana? Tatizo lako wewe unaonekana kumuogopa na kumuwekea hofu na mashaka, yani achana na hayo mambo kabisa, usimuogope, ongea nae kama mtoto wako, kwa hakika atakuelewa”
“Mmmmh!! Haya nashukuru”
Basi Juma aliagana na huyu binti halafu yeye akaondoka zake na kurudi nyumbani kwake.

Juma akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, alipigiwa simu na mama yake na kuipokea ile simu na kuanza kuongea nae,
“Ndio mama,
“Nakuomba kesho uje nyumbani maana nina maongezi na wewe”
“Mmmmh sawa mama”
“Jitahidi uje maana ni maongezi ya muhimu sana”
“Sawa mama, nimekusikia mama yangu”
Juma alikata ile simu ila hakujua ni kitu gani ambacho mama yake amemuitia huko kwao.
Juma alipofika nyumbani kwake alishangaa sana kumkuta Mariam akiwa nje ya nyumba yao, alimsalimia na kumuuliza pale pale nje,
“Mbona upo nje? Nini tatizo?”
“Kwakweli mimi huyu mtoto simuwezi?”
“Humuwezi kivipi?”
“Inakuwaje anajua mambo mengi sana? Mimi namuogopa ingawa na wewe nina maswali na wewe”
“Unajua sikuelewi Mariam, kuna mtu nimekutana nae kanipa ushauri wa namna ya kuishi na huyu mtoto wetu, kasema kuwa tumchukulie kama mtoto, tumpende na kumjali na pia tunapoona sio sawa tumwambia kuwa usifanye hivi, yani yule kanielekeza vizuri sana. Nakuja nakuta na wewe upo nje eti unamuogopa mtoto khaaa Mariam jamani! Umepika?”
“Hata bado sijapika”
“Haya, twende ndani halafu hayo unayotaka kuongea na mimi tutaongea tukishashiba”
Mariam aliinuka na kwenda ndani ambapo mtoto alikuwa amelala tu katika kochi, basi moja kwa moja walienda kupika na walipomaliza, ni Juma ndio aliyemuamsha mtoto wapate kula.
Na kweli mtoto alikaa nao na kula nao, yani Mariam alikuwa na mashaka sana, anamuangalia mtoto huku anakula kwa uoga hadi anamaliza kula, mtoto akasema,
“Mama, utanizoea lini?”
Mariam alikuwa kimya tu, ambapo Juma alimuangalia mke wake na kumwambia,
“Mariam, mtoto anakuuliza unatakiwa kumjibu”
“Sawa, nitamzoea tu taratibu taratibu”
Kisha Mariam akainuka na kutoa vyombo yani kwa kifupi Mariam alikuwa hataki kuongea sana na huyu mtoto.

Usiku wakati wa kulala ndio Mariam aliona ni muda sahihi wa kumuuliza mumewe vizuri kuhusu swala la yeye kumuoa Mishi,
“Juma, ngoja nikuulize hivi kwanza kumbe kabla ya mimiulishawahi kuoa?”
“Nani kakwambia?”
“Hamna mtu nimekuuliza tu, kuwa mkweli kuna jambo nahitaji kujua”
“Nikweli niliwahi kuoa ila niliachana na mke wangu huyo ndio nikakuoa wewe”
“Unajua Juma unanichanganya, tena unanichanganya kabisa, nakumbuka jinsi ulivyokuwa ukinifatilia tena ulisema kuwa hujawahi kuoa na ulikuwa ukinifatilia asubuhi, mchana na jioni hadi nikakubali kuolewa na wewe, sasa swala la kuniambia kuwa uliwahi kuoa halafu sijui ukaacha ndio ukanioa mimi mbona sikuelewi?”
“Ngoja nikuelekeze kidogo pengine utanielewa, ni kweli nilikuwa nakufatilia sana na kipindi hiko nilikuwa sijaoa kweli, yani nilipokuwa nakwambia sijaoa ni kweli kabisa nilikuwa sijaoa sema nilikuwa nahitaji sana kupata mke maana umri nao ulikuwa umeenda sana ila wewe ulikuwa unazingua sana Mariam. Ndio akapatikana huyo mwanamke ambaye alikubali kuolewa na mimi, nikamuoa haraka haraka tu, ila nikaja kugundua kuwa yule mwanamke ana matatizo mengi sana shetani anasubiri, nilishindwa kumvumilia na alisababisha hadi binti Fulani anitokee na kunipa laana sababu ya kuishi nae, nikaamua kumuacha kiukweli nilikuwa nimechanganyikiwa kwa kipindi hiko. Ila Mungu ni mwema maana nilipokutana na wewe tena tu ukaniambia mwenyewe kwasasa nipo tayari kuolewa na wewe, sasa ningeanzaje kukwambia kuwa nilioa Mariam? Sikuweza kwakweli ndiomana hukujua hadi leo”
“Mmmmh kwahiyo huyo mkeo alikuwa anaitwa Mishi?”
“Kwani wewe unamfahamu huyo Mishi? Maana toka siku ile ambayo alikuja yule dada, hebu niambie mke wangu unamfahamu vizuri huyo Mishi?”
“Mmmmh hapana, tulale”
Yani Mariam likifika eneo la kumuongelea Mishi alijikuta akikosa raha kabisa, kwahiyo alimwambia mumewe walale na kwa muda huo, Juma aliamua tu kulala na mkewe.

Juma leo alijiandaa na kuona safari ya kwanza kabisa ni kwenda kwa mama yake ili kumsikiliza mama yake alikuwa akitaka kusema nae kitu gani.
Moja kwa moja alienda hadi nyumbani kwa mama yake na kumkuta ambapo mama yake alifurahi sana kwa Juma kwenda mapema,
“Yani nimefurahi sana kwa wewe kuitikia wito wangu!”
“Tupo pamoja mama, lazima niitikie wito wako kwa haraka na mapema iwezekanavyo maana nisipokuitikia wewe nitamuitikia nani tena?”
“Haya ni vizuri sana, ila unayoyasema kama ungekuwa unanisikiliza mimi hivyo hivyo ingekuwa vizuri sana”
“Nisamehe mama yangu kwa sehemu ambayo sikusikilizi vizuri ila kwasasa nipo kwako kukusikiliza mama yangu kwa chochote kile unachotaka kuniambia”
“Mwanangu, ni hivi. Huyo mkeo Mariam ana nini lakini? Ni kwanini kaamua kubeba tena mimba?”
“Mmmmh mama jamani!! Mbona nahitaji watoto mimi”
“Hao watoto wa ajabu kweli!! Hapana mwanangu, ukoo mzima hapa upo kupinga maana habari za huyo kiumbe chako tumezidi kusikitika tulivyoambiwa na Khadija, kumbe mwanao ni kiumbe cha ajabu sana”
“Sio hivyo mama”
“Ndio hivyo, haya nisikilize, ni hivi Juma sisi kama ndugu zako tumekaa na kufikiria tumeona bora tukutafutie mke, huyo ndiye utakayekuwa ukizaa nae watoto ila sio huyo Mariam wako. Yani hata kama utakuwa unaenda kule kumgelesha tu Mariam lakini mke wako wa kweli unajua wazi yupo huku, kuna binti tumempata mzuri, mtulivu na ana tabia njema, na kwa hakika mwanangu huyu binti anakufaa”
“Khaaaa mama jamani!!”
“Hakuna cha mama jamani, huyu binti anakufaa na tena ndio anafaa kuwa mke wako. Fanya ufdanyavyo Juma ila weka akilini kuwa ukoo wako mzima hakuna hata mmoja anayehitaji wewe uwe na Mariam mtuongezee watoto vituko kwenye ukoo, na umwambie mke wako kuwa hiyo mimba sisi hatuifahamu kabisa”
Juma aliitikia tu ingawa anajua wazi kuwa hakuna chochote kinachoweza kumfanya yeye amuache Mariam maana anampenda sana Mariam, kwahiyo alimuitikia mama yake tu na kumuaga pale,
“Khaaaa mbona unataka kuondoka mapema hivyo!! Mimi nataka kukuonyesha huyo mwanamke, mdogo wako kaenda kumuita nyumbani kwao”
“Mama, samahani leo nina haraka kidogo nitakuja kumuona tu siku nyingine. Nakuomba sana mama yangu”
Muda huu Juma aliinuka na kuondoka zake yani hata hakutaka ruhusa kwani kwa muda huo wazo lake kubwa lilikuwa ni kwenda kufanya kikao kwenye kazi zao kule ili apatane na wafanyakazi wenzie.
Kwahiyo aliondoka kabisa pale kwao na moja kwa moja alielekea ofisini kwake ambapo alienda kuongea na yule mmiliki wa pale ili aweze kuitisha kikao ambapo yule mmiliki alikubali maana alikuwa akipatana sana na Juma.

Watu wote pale ofisini walikusanyika kwenye kikao ambapo Juma alianza kuzungumza sasa ili kujua tatizo lililopo kwa wanzie,
“Jamani ndugu zangu ni kitu gani kimeingilia hapa kati? Ni kwanini kwasasa hamtaki tena kunisalimia wala kuniongelesha? Hebu niambieni ni kitu gani kimeingia hapa katikati?”
Mmoja ndio alijitolea kuelezea na alitoa maelezo yale yale ambayo Juma aliambiwa na yule jirani yake, basi Juma akawauliza,
“Ila ndugu zangu twende mbele na turudi nyuma, ni lini mmesikia nimemuua mtu? Ni lini mmesikia kuwa kuna watu nawaweka misukule?”
“Hapana hatujawahi kusikia ila tumeogopa tu na kama ujuavyo kinga ni bora kuliko tiba, kwahiyo sisi tumeogopa na kujikwepesha”
Basi yule mmiliki wa eneo lile ambaye ndio kama bosi wao akawaambia,
“Kumbe kuna mambo yanaendelea hapa halafu hata mimi siyajui, jamani dunia ina mambo. Msikute mlikutana na mtu ambaye ana ugomvi na Juma ndiomana kawaambia mambo kama hayo, sio kila kitu ni cha kukiamini maana huwezi jua aliyesema alikuwa na lengo gani”
“Mmmmh sasa hapo unatushauri nini bosi”
“Mimi ninachowashauri ni kuwa muache ujinga, acheni kufikiria mambo ya kijinga kabisa, hivi mtu kama ni mbaya si angewamaliza watu wote! Mrudi kama zamani”
“Tatizo bosi huyu jamaa nyumbani kwake ana viumbe vya ajabu, toto lake halina hata heshima na tumeambiwa yule mtoto hafai kabisa”
“Jamani kwasasa pale naishi mimi na mke wangu tu, maana wale nimewapeleka kijijini”
Hakuna aliyemuamini Juma hadi aliamua kuwakaribisha nyumbani kwake kesho yake ili wakapate chakula cha mchana, waliafikina nae katika hilo.

Juma alipotoka tu kwenye shughuli zake leo alipitia mboga ya kupikiwa kesho wageni wake na baadhi ya vitu gengeni, wakati anatoka kule ndipo alikutana na yule jirani yake ambaye huwa anakutana nae mara nyingi,
“Ooooh kumbe na wewe huwa unaenda gengeni?”
“Ndio, ni mara nyingi tum bona!”
“Kheeee umekuwa kama mwanaume wa kipemba sio!”
“Kwanini?”
“Maana wapemba ndio zao, wake wanabaki nyumbani halafu mahitaji wananunua wanaume sababu wana wivu sana huwa wanahisi wake zao wakienda gengeni watatongozwa”
Juma akacheka na kusema,
“Khaaaa mimi sikufahamu hilo jambo kabisa, ila mimi huwa nafanya hivi kama kumsaidia mke wangu tu. Ona kama muda huu nimewahi kutoka kazini naona bora nipitie kabisa sokoni ninunue mahitaji na kumpelekea mke wangu nyumbani ili asihangaike”
“Ila kuna muda mwingine ni vizuri kuwapa nafasi wake zetu kwenda kukutana na wenzao huko masokoni na hata saluni, maana naona mkeo hata nywele hasuki”
“Aaaaah hapendi kusuka yule”
Yani Juma alisema tu hivyo ila kiukweli mke wake hasuki sio sababu hapendi kusuka bali anaona uvivu kukaa chini na kuanza kusukwa nywele, basi yule jirani akamwambia,
“Ila mwanamke akisuka anapendeza sana”
Juma akamkata maneno pale,
“Wa kwangu hata akinyoa kipara anapendeza sana”
Hapo jirani hakuwa na usemi zaidi, basi aliagana tu na Juma halafu Juma akaondoka zake kurudi nyumbani kwake.
Juma alipofika kwake alimkuta mkewe leo yupo ndani ila mtoto ndio hayupo na kumuuliza Mariam,
“Kwani yuko wapi mtoto?”
“Mmmmh leo amelala, yani nimefurahije”
“Khaaaa kumbe!! Basi mke wangu kesho kuna wageni watakuja, nimeleta tu mboga ili wapikiwe chakula”
“Khaaaa Juma umeanza mambo yako sasa, kupika chakula chetu tu naonaga shida ndio kupika na chakula cha wageni jamani mbona unataka kunipa kazi jamani!”
“Sasa mke wangu unadhani itakuwaje jamani! Nimeongea na rafiki zangu kuwa watapata hapa chakula cha mchana”
“Yani walishe huko huko maana hapa utaumbuka nakwambia, maswala ya kuniingiza jikoni nipike majungu makubwa makubwa siwezi jamani, huko ni kunitesa hayo ni mateso bila chuki”
Juma akapumua kwanza maana hata hakujua ni jinsi gani aongee na mke wake huyu.

Usiku wakati wa kulala, Juma alimwambia tena mke wake kuhusu huo ujio wa rafiki zake ambapo bado Mariam aliendelea kulalamika,
“Labda waje kunywa maji tu, hebu kuwa na huruma basi Juma. Unajua fika kuwa mimi nina mimba changa kwasasa halafu unaniletea habari zako za kupikia wageni hizo!”
“Aaaah samahani mke wangu, yani nilisahau kabisa. Naomba unisamehe mke wangu, unajua sababu nimekusoea kuwa ni mvivu nikajua unabisha sababu ya uvivu wako, naomba unisamehe mke wangu tafadhali”
“Haya nimekusamehe”
Juma alilala kwa muda huu huku akiwaza cha kuwaambia rafiki zake maana hata hakujua ila alisema kuwa atawahi mwenyewe kuja kupika au la atawanunulia chakula rafiki zake na kuja kula pale nyumbani.
Kulipokucha, Mariam alikuwa kashaamka, yani siku hizi alikuwa anaamka mapema kupita maelezo ya kawaida, mtoto na yeye alikuwa kaamka, basi Juma akajiandaa na kutoka kumuaga mkewe ambapo Mariam alimuuliza tena,
“Kwahiyo hutokuja na wageni wako eeeh!!”
Juma akajibu,
“Nitakuja nao ila itabidi nile nao huko huko kabisa”
Mtoto akasema,
“Baba njoo nao, watakula hapa hapa nyumbani”
Juma alimuangalia mtoto na kumwambia,
“Mama yako ana mimba changa, itakuwa ngumu kwa yeye kuanza kupika mavyakula mengi mengi, bora wale huko huko. Hakuna wa kupika hapa na hakuna wa kumsaidia mama yako”
Yule mtoto akasema,
“Mimi nitamsaidia”
Yani Mariam na Juma walijikuta wakimuangalia yule mtoto huku wakimshangaa sana kuwa anasema vipi kuwa atamsaidia Mariam katika kupika? Ila hakuna aliyeitikia pale zaidi zaidi ya Juma kuondoka zake na kumuacha Mariam na yule mtoto ambaye alimwambia Mariam,
“Mama usiogope, wala usiwe na wasiwasi, hii ndio raha na faida ya kuzaa mtoto wa kwanza mwenye jinsia ya kike, mimi ni mwanamke lazima nijishughulishe, lazima nifanye kazi za wanawake wengine, mimi nitakusaidia mama kupika. Najua unashangaa sababu mimi bado mdogo, mama usinishangae wala usiniogope, unapoishi na mimi chukulia kama unaishi na mbilikimo ili usiwe unaniona sijui nafanya vitu vya ajabu, mimi nafanya vitu vya kawaida kabisa mama yangu”
Yani Mariam hakujibu kitu, alibaki kimya tu akimuangalia huyu mtoto wake.

Mariam akiwa bado anashangaa yale ambayo mtoto kayasema ni muda ule ule mtoto akamwambia Mariam kuwa,
“Mama, na tuanze kupika”
Mariam akajikaza tu,
“Unataka tuwapikie nini?”
“Baba, si ameleta nyama! Tuwapikie pilau basi”
“Mmmmh sawa, ila viungo vya pilau vinanichefua!”
“Nitapika mimi mama”
Yani Mariam alizidi kushangaa kwakweli kwa hiki ambacho mtoto wake anakisema.

Itaendelea……!!!
Offa bado inaendelea 500 tu mpaka mwisho......Nani yupo dsm tumeet tupige mastory kabla sijasepa😁😁😁😁😁
 
MTOTO WA MAAJABU: 32

Mariam akajikaza tu,
“Unataka tuwapikie nini?”
“Baba, si ameleta nyama! Tuwapikie pilau basi”
“Mmmmh sawa, ila viungo vya pilau vinanichefua!”
“Nitapika mimi mama”
Yani Mariam alizidi kushangaa kwakweli kwa hiki ambacho mtoto wake anakisema.
Mtoto alimuangalia na kumwambia,
“Mama, mbona unashangaa?”
Mariam hakujibu ila mtoto akamwambia tena mama yake,
“Tena mama, yale maharage kidogo nayo uyabandike, yaanze kuchemka hapo nitayaunga halafu nenda kachume ile mboga aliyopanda Anna ili nayo tuipike”
Hapo Mariam aliuliza,
“Sasa si umesema ni pilau! Inakuwaje tena na maharage, mara mchicha vya nini hivi?”
“Aaaah mama, hizi ni mboga tu kama mboga zingine huwa zinanogesha chakula na kufanya uchangamfu wakati wa kula. Aliyesema ukila pilau usile na mboga ni nani? Sasa leo nitakupikia na utafurahi, nyama nyingine itakuwa kwenye pilau na nyingine nitairosti pembeni”
Yani Mariam alimuangalia huyu mtoto wake bila kummaliza, kiukweli alikuwa akishangaa tu mpaka mtoto alipomwambia,
“Mama, acha kushangaa muda unakwenda inabidi vyote nilivyosema viandaliwe”
Mariam baada ya kufikiria kidogo akaamua tu kwenda kuwasha moto na kuandaa kila kitu kisha yule mtoto alimwambia Mariam aweke kiti ili asimamie juu na kupika yani Mariam bado alibaki kaduwaa kwakweli na kufanya vile vile ambavyo mtoto wake amemwambia basi Mariam akachukua kigoda na kukiweka karibu na jiko ili kumuangalia huyu mtoto kitu ambacho atakifanya pale jikoni, na kweli kabisa yule mtoto alisimama pale na kuanza kupika yani Mariam alisimama tu pembeni akistaajabu yale mambo.
Kwakweli Mariam hakubanduka pale jikoni ili aone kama kuna uchawi wowote unatumika pale ila alimuona tu huyu mtoto akipika kama wale watu wafupi sana wakipika na alipika kila kitu alichokisema huku Mariam akimshuhudia pale na kumsaidia baadhi ya vitu vidogo vidogo tu, kwakweli Mariam alikuwa akimshangaa sana kiasi kwamba mtoto akamwambia,
“Mama, si utaenda kukata kachumbari au vitunguu vinakuchefua pia?”
Mariam alimuangalia mtoto na kumjibu,
“Nikikata vitunguu vingi vinanichefua”
Mtoto akamwambia Mariam,
“Usijali mama, niandalie hapo vitu vyote vya kukatakata”
Kwakweli Mariam leo alikuwa akistaajabu tu, akaanza kumuandalia yule mtoto vitu vyote vinavyotakiwa kukatwa katwa kwaajili ya kachumbari na alipomaliza alimkuta yule mtoto nae akimaliza kugeuza chakula ambapo alimwambia Mariam,
“Sasa mama, ni kazi yako kupalilia chakula hapo”
Mariam akamshusha yule mtoto kwenye kile kiti halafu yeye akapalilia kile chakula huku muda huu mtoto akiwa anakatakata kachumbari, yani kila kilichokuwa kikifanywa na huyu mtoto kilimuacha Mariam mdomo wazi maana Mariam alibaki kushangaa tu kwa kila kitu kilichokuwa kinatendeka mahali pale.

Hadi chakula kilipokuwa tayari na kwenda kukiandaa mezani, bado Mariam alikuwa akishangaa tu kwakweli huku akitamani kumuuliza yule mtoto maswali mengi lakini aliona wazi akishindwa, kisha yule mtoto akamwambia Mariam,
“Mama, nipakulie kidogo nile kabisa ili nikakae ndani maana baba kasema hao wageni wasinione”
Mariam alimpakulia chakula ambapo yule mtoto alikula kisha akainuka na kwenda kukaa ndani kama ambavyo alisema, kwakweli bado Mariam alikuwa akistaajabu kwa yale yote ambayo yametendeka pale nyumbani, ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwake ukizingatia hajawahi kukutana na jambo kama hili hapo kabla.
Muda kidogo, Juma alifika na wageni wake, wale wageni walikuwa ni watano ambapo Mariam aliwakaribisha vizuri tu ndani kisha Juma akamshika mkono Mariam na kwenda kuongea nae chumbani,
“Mmmmh hawa wageni nimewaambia kuwa tupitie tukale wamegoma na kusema kuwa niliwaahidi kwamba leo wataenda kulak wangu, wamekataa kabisa kupita na kula popote pale, wamesema watakula kwangu hapa hata sielewi cha kufanya na wewe ulisema hupiki. Hebu tupeane ushauri mke wangu”
“Ushauri wa nini? Chakula kipo mezani”
Yani Juma alimkumbatia mke wake kwa furaha maana hata ile asubuhi wakati mtoto anasema kuwa atamsaidia mama yake kupika, wala hakutilia maanani hii kauli kwahiyo hakujua kama ni kitu hiko kimetokea ila alimshukuru tu Mariam na moja kwa moja walitoka sebleni ambapo Juma aliwaambia rafiki zake,
“Tena tumekuja muda muafaka maana mke wangu ameshaandaa chakula jamani, karibuni tujumuike”
Wale rafiki wa Juma walitabasamu na wote waliinuka kuelekea sehemu ambayo Juma aliwaelekeza yani pale kwenye meza ya chakula na kila mmoja anakaa na kupakua kile chakula huku wakila na kila mmoja alikuwa akiguna kwa utamu wa chakula kile, mmoja aliamua kuongea tu pale pale huku akimuangalia Mariam ambaye alikuwa amekaa pembeni maana yeye hakwenda kula,
“Shemeji, mimi sio mpenzi wa pilau na wala huwa sili pilau kabisa ila tulipoitwa hapa mezani na kuona pilau nikasema leo nimepatikana nikapakua kidogo sana ila naongeza shemeji, sijapata kula pilau tamu kama hii jamani khaaa!”
Wenzie wakacheka huku akiongeza kile chakula na kula huku wengine wakisifia pale pale na kuendelea kula, yani Mariam alikuwa akitabasamu tu hadi walipomaliza, mwingine akasema,
“Mimi huwa sili maharage nyumbani kwangu ila hapa natamani hata haya maharage niyabebe na kuondoka nayo kabisa kwa utamu huu”
Walicheka tena, huku wakimalizia tu
Walipomaliza walikaa kidogo tu na kuaga ila wote walikuwa wakimshukuru Mariam kwa kile chakula na kumshukuru Juma kuwakaribisha nyumbani kwake kupata chakula kitamu vile.

Juma aliamua kuwasindikiza yani njia nzima walikuwa wakisifia tu utamu wa kile chakula, mwingine akasema pale,
“Jamani mimi huwa sipendi kachumbari, yani huwa sili kachumbari kabisa khaaaa sio kwa kachumbari ile, bwana Juma naomba mke wangu aje kujifunza kwa mkeo maana mke wangu ananipikia chakula hicho mchuzi bahari nyama unatafuta jamani khaaa!! Mke wako ni noma”
Yani Juma alikuwa akitabasamu tu, na yeye aliona utamu wa kile chakula, ingawa huwa mke wake anapika chakula kizuri sana ila hiki cha leo kilikuwa kimezidi uzuri na kumfanya kila wanapomsifia atabasamu tu mpaka wanafika stendi na kupanda basi na kuondoka.
Juma alikuwa akirudi nyumbani kwake na kukutana na yule jirani yake ambaye walikuwa wanakutana mwanzoni kabisa na kuna siku alishushuliw ana mtoto wa Juma, ila leo alimsalimia Juma kama ambavyo alikuwa akimsalimia zamani,
“Jirani naomba unisamehe tu kwa yale yote ambayo yamepita baina yetu”
“Aaaah usijali jirani, mimi huwa sikai na kinyongo, nilishakusamehe jirani”
“Nashukuru sana jirani, vipi lakini mama na mtoto wanaendeleaje?”
“Hawajambo, ni wazima wa afya”
“Basi ni vyema”
“Sasa, kuna msiba kwa majirani zetu wa kule juu, mwambie mama nitakuja kumpitia siku ya kuzika ili na yeye akaonekane kwenye msiba”
“Aaaah hapana usije, hawezi mke wangu kwenda kwenye msiba bila ya mimi”
Yule jirani alishindwa kusema zaidi na kumuacha tu Juma aondoke zake maana yeye hakuona kama ni tatizo kwa yeye kumpitia Mariam kwenda naye kwenye msiba.

Usiku wa leo Juma anamuuliza vizuri mke wake kuhusu kile chakula maana uzuri wake kilivunja rekodi,
“Mke wangu, kwanza hongera halafu kile chakula jamani mbona kilikuwa ni kitamu sana kuliko vyakula vyote ambavyo umewahi kupika”
Mariam akacheka na kusema,
“Sio mimi niliyepika kile chakula”
Juma alishangaa na kuuliza kwa makini,
“Ni nani sasa kapika?”
“Ni mtoto ndio kapika”
Juma alishangaa zaidi na kutaka kujua yule mtoto amepika vipi hiko chakula, kisha Mariam alianza kumuelekeza yani Juma alishangaa sana,
“Hata mimi nimeshangaa pia, huwezi amini sijatoka jikoni toka alivyoanza kupika hadi mwisho, nilitaka kuona kama yule mtoto anafanya mambo ya miujiza au ni kitu gani maana pale nilitegemea kuona mkono mrefu ukikoroga yani siku ote huwa sina imani na huyu mtoto”
“Hivi mfano mke wangu ingekuwa kama hivyo ambavyo unawaza ingekuwaje?”
“Mmmmh hata sijui yani kwa uoga huu nilionao sijui jamani ingekuwaje duh! Ningeogopa sana, sijui hata ningefanyeje mimi. Ila nilijikaza huku nikimuangalia kila alichokuwa akikifanya, nilikuwa naangalia kama atatumia nguvu nyingine ila hapana alisimama kwenye kigoda na kupika kwa mikono yake mwenyewe”
“Mmmmh haya, tujiulize nani kamfundisha kupika?”
“Hilo swali hata mimi nimejiuliza tena sana na wala sijapata jibu kabisa, naogopa mimi naogopa kabisa. Huyu mtoto tuseme alikulia tumboni au ni kitu gani? Maana haya mambo ni makubwa jamani sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza akategemea kwa mtoto mdogo vile kupika chakula kama kile”
“Unajua nashangaa hadi muda huu mke wangu, ila tulale tu maana sielewi”
Wakaamua kulala ila lile lilikuwa jambo la ajabu sana kwao.

Leo Juma alipokuwa kazini tu alipata sifa za kila namna, yani kila aliyefika kwake alikuwa akisifia jinsi mke wa Juma alivyokuwa anajua kupika, yani kuna mwingine alienda kuzungumza na Juma,
“Hivi kwanini ndugu yangu mkeo asifungue chuo cha mapishi?”
Juma akatabasamu na kuuliza,
“Hivi inawezekana eeeh!!”
“Ndio inawezekana, kuhusu kupata wanafunzi sio shida maana wake zetu ndio watakuwa wanafunzi wake namba moja”
Mmoja akadakia na kusema,
“Tena mke wangu mimi ndio anapaswa kuwa mwanafunzi wenu wa kwanza, sababu hayo maharage anayopika mke wangu ni Mungu tu anajua, harage kama unataka kupigana nalo! Ila wanaume tunakutana na mengi sana tunavumilia tu, huo wali siku nyingine mara apike bokoboko, siku nyingine mara ukukabe kila tonge unalomeza, siku nyingine mara aunguze basi tabu tupu, bora mkeo aanzishe chuo cha mapishi tu, na akianzisha niambie nimuandikishe mke wangu huko maana nimechoka kupikiwa mauza uza”
Juma alikuwa akicheka, mwingine akasema,
“Sasa ile mboga ya majani uwiiii kama sio mchicha vile, jamani Juma mkeo kajifunza wapi mapishi?”
Juma akatabasamu na kusema,
“Ndiomana nampenda sana yule mwanamke yupo vizuri kila idara”
“Kwakweli hongera sana, unastahili kusifiwa kwa hilo, nina uhakika hapa kila mtu anatamani kupata mke kama ambaye umempata wewe. Hongera sana ila swala la kufungua chuo cha mapishi naomba ulifikirie, tunahitaji sana wake zetu wapate ujuzi hapo”
Yani Juma ilikuwa ni furaha sana kwake kwa kila sifa ambayo ilitolewa kwaajili ya kile chakula ambacho walikula rafiki zake, akajisemea moyoni kuwa akitoka siku hiyo ni lazima apitie kuwachukulia zawadi mke wake na mtoto kwani aliona wazi kuwa wanastahili kupata zawadi.

Mariam kama kawaida alikuwa akibaki na huyu mtoto na alikuwa akimuangalia kwa karibu sana kila kitu ambacho kilikuwa kinafanywa na huyu mtoto, alitaka kuhakikisha kama huyu mtoto ni wa kawaida ila hata kama bado kuna mambo ambayo sio ya kawaida mengi tu kwa huyu mtoto.
Basi muda huu alikuwa amekaa sebleni na huyu mtoto ambapo mtoto alimwangalia Mariam na kumwambia,
“Najua mama hapo unatamani sana kuniuliza kuwa nimejifunza wapi kupika!”
Mariam akashtuka na kumwambia mtoto,
“Ni kweli, nilikuwa natamani sana kujua jambo hilo”
“Ni hivi mama, nimejifunza kupika kutoka kwako. Wewe mama ni mpishi hodari sana, kwahiyo nimerithi kutoka kwako”
“Mmmmh ila mbona chakula kilikuwa kitamu sana”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Ndio hivyo mama, vya kurithi vinazidi, umesahau hilo mama yangu?”
Mariam hakuwa na jibu kwahiyo alikuwa akimuangalia tu huyu mtoto kisha mtoto alimuuliza Mariam,
“Hivi bado tu hujanizoea mama?”
“Mmmmh hapana nimekuzoea”
Mariam alijibu tu vile ila kiukweli bado hakuwa na mazoea ya kiasi kile na mtoto wake maana bado kuna mambo alikuwa na mashaka nayo.

Muda huu Juma alirudi akiwa na zawadi zake mkononi ambapo alimkuta mkewe na mtoto wapo pamoja na kuwasalimia pale kisha akawaambia,
“Nimewaletea zawadi, kwakweli nimefurahishwa sana na kazi ya jana, kila mtu ananisifia kwakweli”
Akatoa zawadi kwanza aliyomletea mkewe na kumkabidhi ambapo Mariam aliifungua pale pale huku akiiangalia na kufurahi sana,
“Asante sana mume wangu, yani nimefurahi nilikuwa nahitaji kitenge hiki balaa. Asante sana”
“Sijui utashona sijui utafanyaje”
“Nitashona gauni moja zuri la kuvaa kipindi mimba yangu ikiwa kubwa”
Juma akacheka tu na kutoa zawadi aliyomletea mtoto ila kabla ya kumkabidhi mtoto akasema,
“Hebu ifungue baba”
Juma aliifungua ile zawadi, ilikuwa ni mdoli ambapo alijua mtoto wake angafurahi sana sababu watoto wengi huwa wanapenda midoli, ila alishangaa mwanae akimwambia,
“Khaaa baba, umeniletea mdoli jamani. Wa nini mimi?”
“Mmmmh jamani, wewe si mtoto na watoto hupenda kuchezea midoli”
“Baba, ni mtoto gani anaweza kupika kama mimi? Mimi ni mtoto kweli ila akili zangu na mawazo yangu sio ya kitoto, sipaswi kupewa mdoli mimi”
“Kheeee kwahiyo ni zawadi gani gani inakufaa?”
“Mimi niletee kipande cha kuni”
Hapa hata Juma mwenyewe alishangaa kusikia kipande cha kuni maana hakumuelewa mtoto wake ila hakuwa na budi zaidi ya kumuitikia tu kuwa atamletea hicho kipande cha kuni.

Usiku wakati wa kulala, Juma alizungumza na Mariam kuhusu hicho kipande cha kuni kwani moja kwa moja Juma alihisi mkuwa lazima huyu mtoto anataka kufanya mambo kama yale ya kupeleka kuni kwa mama Mariam, basi akamwambia Mariam,
“Haya sio kama mambo yako kweli?”
“Mmmmh au anataka na wewe upeleke kwenu kuni kimiujiza?”
“Itakuwa, ila mimi naogopa hayo mambo ya kimiujiza yani uambiwe umeleta kitu wakati hujaleta kweli?”
“Hapo sasa jamabi, mambo mengine ni ya ajabu sana”
“Kuna kitu nitafanya cha tofauti ila hicho kipande cha kuni nitamletea”
“Kitu gani hicho mume wangu?”
“Utaona tu, wewe subiri ila kuna kitu cha tofauti sana nitakifanya maana huyu mtoto anataka kutufanya humu ndani kama mapunguani vile, mimi nimemletea zawadi eti amekataa zawadi yangu anataka kipande cha kuni khaaa”
“Mmmmh!!”
Mariam aliishia kuguna tu na muda huo walilala tu.

Kulipokucha asubuhi na mapema Juma aliondoka zake kwenda kwenye shughuli zake, nyumbani walibaki Mariam na mtoto kisha mtoto alimuuliza Mariam,
“Mama, mbona wewe nilipokwambia uniletee zawadi ya kipande cha kuni ulifanya haraka sana kwanini baba anakaidi?”
“Anakaidi kivipi? Kwani kasema hakuletei? Atakuletea tu siku haijaisha”
Sawa, ila anachotaka kufanya kitamgharimu badae”
“Kwani anataka kufanya nini?”
Yule mtoto hakumjibu na kufanya kidogo Mariam ashikwe na mashaka pale na kuamua kumpigia simu Juma ila Juma hakupokea ile simu kabisa, kila Mariam alipompigia hakupokea mpaka Mariam akamtumia ujumbe,
“Juma kama unataka kufanya kitu tofauti na kuleta hiyo kuni tafadhari usifanye maana mtoto anasema itakugharimu”
Akatuma ule ujumbe na kuendelea na mambo mengine.

Juma hakukaa sana ofisini bali aliondoka na kuelekea kwao ambapo njiani alikota kipande cha kuni, moja kwa moja alienda nacho hadi kwao akakikata katikati na kukiacha kimoja kwao na kingine kuondoka nacho. Kwahiyo alimsalimia tu mama yake na kumuacha na kile kipande cha kuni halafu akaanza kurudi nyumbani kwake.
Alipokuwa anakaribia na nyumbani kwake alisikia simu yake ikiita, akaitoa na kukuta imekatika ila akaona ujumbe wa mke wake na kushtuka sana maana tayari alishafanya tofauti, mara simu yake ikaanza tena kuita akaangalia na kuona mpigaji ni mama Shamimu, basi akapokea na kuanza kuongea nae,
“Kheeee wewe Juma umefanya nini wewe! Haya sijui gongo uliloliacha hapa sijui kuni lipo kumchapa mama”
“Kivipi?”
“Linamchapa hadi mama kazimia”
Yani Juma hakuelewa kabisa kile alichoambiwa.

Itaendelea…..!!!
Kwa mawasiliano 0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 33

Alipokuwa anakaribia na nyumbani kwake alisikia simu yake ikiita, akaitoa na kukuta imekatika ila akaona ujumbe wa mke wake na kushtuka sana maana tayari alishafanya tofauti, mara simu yake ikaanza tena kuita akaangalia na kuona mpigaji ni mama Shamimu, basi akapokea na kuanza kuongea nae,
“Kheeee wewe Juma umefanya nini wewe! Haya sijui gongo uliloliacha hapa sijui kuni lipo kumchapa mama”
“Kivipi?”
“Linamchapa hadi mama kazimia”
Yani Juma hakuelewa kabisa kile alichoambiwa.
Akamuuliza tena dada yake,
“Unasemaje wewe?”
“Nakwambia hivi lile gongo lako uliloliacha limemchapa mama hadi kazimia”
Yani Juma hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuamua tu kurudi nyumbani kwao ili kwenda kumuona mama yake.
Juma alifika kwao na kukuta mama yake amezimia kweli yani hakuweza hata kusema neno ila alichukua kile kipande cha kuni na kuondoka nacho yani hakuna mtu aliyemuongelesha hata mama Shamimu hakumuongelesha kwahiyo walibaki wakimshangaa tu.
Yani Juma aliondoka kwao huku akiwa na mawazo sana.
Njiani wakati anarudi nyumbani kwake kuna mtu alikutana nae ila mtu huyu ni rafiki yake wa siku nyingi sana ambaye alimsimamisha Juma na kuanza kuongea nae,
“Jamani Juma za siku nyingi?”
“Nzuri ila nina haraka sana”
“Kheee haraka ya nini ndugu?”
“Mjini hapa, mambo ni mengi sana”
“Pole ila vipi mkeo hajambo?”
“Hajambo kabisa”
Juma alikuwa akijibu huku akiongoza njia ya kuondoka ila yule mtu akamwambia Juma,
“Khaaa unasema hajambo wakati yupo akitangatanga tu”
Hapo Juma alishtuka na kumuangalia yule rafiki yake, kisha akamuuliza,
“Kivipi? Anatangatanga kivipi?”
Yule rafiki wa Juma akamjibu,
“Mjini hapa, mambo ni mengi sana nina haraka”
Halafu akaondoka zake, yani Juma alibaki akimuangalia tu bila kumuelewa wala nini.

Yani Mariam alikuwa na mashaka sana na mume wake ukizingatia alikawia sana kurudi, halafu na maneno ya yule mtoto yalifanya Mariam akose raha kabisa. Ila muda ulipoenda sana aliamua kumuuliza huyu mtoto,
“Je unajua baba yako kapatwa na nini?”
“Mmmh sijui ila ninachojua ni kuwa baba atarudi tu. Mimi naenda kulala mama”
Kisha akainuka pale alipo na kwenda chumbani yani Mariam alibaki na roho juu juu maana alikuwa haelewi kabisa kuwa ni kitu gani kitaendelea au ni kitu gani kitatokea.
Mariam alimsubiri sana mume wake ambaye alifika kwenye mida ya saa nne usiku, Mariam alimkaribisha na kumuuliza
“Umechelewa wapi mwenzangu leo?”
Ila Juma alikuwa kafura kwa hasira na akamuuliza Mariam,
“Haka katoto kako wapi?”
“Mmmmh mbona umefura hasira hivyo?”
“Niambie kwanza haka katoto kako wapi?”
“Kameenda kulala”
“Yani kajinga sana haka katoto”
“Kamefanyaje tena mume wangu?”
“Dah!! Siamini kabisa na wala sijui kama mama yangu atapona”
“Kivipi tena Juma?”
Ikabidi Juma amsimulie mke wake kuhusu vile ilivyokuwa, alimuelezea jinsi alivyopeleka kile kipande cha kuni na jinsi alivyoenda kumkuta mama yake.
“Nimejikuta nikimchukia huyu mtoto”
“Usiseme hivyo mume wangu maana wewe mwenyewe ndio chanzo cha yote hayo, uliambiwa ukakaidi tena unatakiwa kuwa mpole kwa sasa”
“Sasa nimekaidi kitu gani? Huyu mtoto tumemzaa au ametuzaa? Maana kila siku anazidi kutupanda vichwani tu na kutukosesha raha ya maisha”
“Pole mume wangu najua jinsi gani ulivyo na hasira ila kwasasa tupumzike mume wangu ili hasira zako zipungue”
Kisha Mariam akamtuliza mumewe pale ambapo aliweza kula na waliwezà kwenda kulala.

Kulipokucha tu, Juma alindelea na swala lake la kulalamika dhidi ya alichokifanya yule mtoto hadi Mariam akamwambia,
“Hebu Juma usiwe unalalamika kutwa kucha, piga na simu huko ili ujue wanaendeleaje”
Juma akaamua kupiga simu ambapo dada yake alipokea na kuongea nae,
“Bora umepiga Juma maana nilitaka kukupigia muda sio mrefu, hali ya mama sio nzuri”
“Kheeee bado tu!”
“Ndio, hajazinduka hadi muda huu”
“Duh!!”
Juma akakata simu yani alikuwa amechukia sana na kuinuka, ni Mariam ndio akamzuia na kumuuliza,
“Unataka kwenda wapi sasa Juma?”
“Nataka kwenda kukachapa haka katoto, kamezidi sasa kwanini kututolea amani kiasi hiki! Naenda kukapiga labda katajifunza adabu”
Mariam akacheka na kumwambia mume wake,
“Hebu kuwa mpole Juma usitake kuleta balaa, kabisa unataka kushindana na huyo mtoto mdogo anayepika kila aina ya chakula, mbona utaumbuka Juma! Achana na mambo hayo kabisa, angalia afya ya mama nenda kakaombe msamaha hako katoto ili mama apone ila ukijifanya mbishi tutampoteza mama hivyo!”
“Lakini haka katoto tutakachekea hadi lini?”
“Juma usiwe mbishi, hebu kumbuka matukio yote ambayo yametokea tangu nipate mimba ya huyu mtoto, hebu kuwa mpole tu ili tuweze kusonga mbele na kufanya mambo mengine. Nenda kamuombe msamaha mtoto ili mama awe mzima, usijifanye mbishi wakati ukisikia mama amekufa hapo utakuwa nusu kichaa”
“Khaaa usiseme hivyo Mariam”
“Basi nenda kamuombe mtoto msamaha kwaajili ya uzima wa mama”
Juma akaona anachoambiwa ni kweli, ikabidi tu awe mpole na kwenda kumuomba msamaha mtoto ili apate amani ya moyo na mama yake apone.
Alimfata mtoto sebleni alipokaa na kumpigia magoti kisha akamwambia,
“Naomba unisamehe mwanangu”
Yule mtoto akatabasamu na kumuuliza Juma,
“Kwa kosa gani?”
“Kwa kosa la kukaidi maagizo yako”
“Chagua mwenyewe adhabu ya kukupa”
“Dah!! Naomba adhabu ya kwenda kwetu kumsalimia mama kila siku”
Mtoto akatabasamu na kutikisa kichwa kama kukataa halafu akamwambia Juma,
“Hiyo sio adhabu, huo ni wajibu wako maana yule ni mama yako ila adhabu yako ni kuwa katika hii wiki unatakiwa kila siku kuniletea kuni moja, sasa ole wako ukiuke na hii”
“Nimekuelewa mwanangu, asante kwa kunisamehe”
Juma aliinuka ila hakuwa na furaha wala nini, alienda kujiandaa muda huo na kuondoka zake.

Juma akiwa kazini leo anafuatwa na Pendo maana na yeye Pendo alisikia kuhusu sifa za mke wa Juma akajikuta hadi na yeye akitamani,
“Juma nahitaji kuja nyumbani kwako ili mkeo anifundishe kupika”
“Karibu sana”
“Asante ila je yule mtoto wako yupo? Hivi wakina nanii hawa hawakunaswa vibao kweli walivyoenda huko kwako”
“Wanaswe na nani?”
“Na mtoto wako, mbona mimi alininasa kibao”
“Aaaah tuachane na hayo bhana, mwanangu kabadilika siku hizi kawa mtoto mzuri”
“Kwani ulimpeleka kwenye maombi?”
“Kufanya nini kwenye maombi?”
“Hivi unaona mwanao ni wa kawaida yule? Mwanao anahitaji maombi yule maana sio wa kawaida”
“Mmmh tuachane na hayo, tuongelee mengine tu”
“Haya nitakuja kwako, mwambie mkeo aniandalie na mimi chakula”
“Sawa usijali, karibu”
“Nakuja kesho, mwambie mkeo kabisa”
Juma aliitikia tu ila alimuona huyu mwanamke kuwa na kiherehere maana alimjua vizuri mke wake, hakudhani kama angekubali kupika.

Leo wakati Juma anarudi nyumbani kwake, aliona ni bora apitie kwanza kwa mama yake ila alipokuwa njiani akaona kipande cha kuni na kukumbuka maagizo ambayo alipewa na yule mtoto kuwa katika wiki hiyo yote atatakiwa kupeleka kipande cha kuni kila siku, Juma aliamua tu kukiokota.
Basi Juma alivyofika kwake, mama yake alimuona na kile kipande cha kuni na kumwambia pale pale,
“Juma ishia huko huko na hicho kipande chako cha kuni”
“Kwani tatizo ni nini mama?”
“Mjinga wewe, ulitaka kuniua jana halafu unasema nini? Sitaki uje nyumbani kwangu na hivyo vipande vya kuni, bakia huko huko mjinga kabisa wewe. Unaniletea vitu vya uchawi kweli Juma? Kwa jinsi mimi ninavyokupenda, kwa jinsi nilivyohangaika kukulea halafu unakaa kuniletea vitu vya uchawi? Naomba uondoke na kipande chako cha kuni”
“Jamani mama, nashindwa kukuelewa kwakweli”
“Utanielewa tu, ila sitaki huo ujinga wako. Nenda tu nyumbani kwako”
“Ila nimekuja kukusalimia mama yangu”
“Mimi ni mzima, naomba uende”
Juma hakuweza kuongea zaidi kwani aliondoka muda ule na kurudi nyumbani kwake, moja kwa moja alimpelekea mtoto wake kile kipande cha kuni ambacho mwanae amemwambia kuwa wiki nzima atakuwa akipeleka kama adhabu.

Usiku wa leo Juma aliamua kumwambia mke wake kuhusu ujio wa Pendo na kile ambacho Pendo alisema kuwa aandaliwe chakula. Kwakweli Mariam alichukia sana na kuuliza,
“Hivi huyo Pendo ni mwanamke au mwanaume?”
Juma akamjibu mke wake,
“Ni mwanamke”
“Sasa ananitakia nini mwanamke mwenzie? Yani mimi nihangaike kumpikia mwanamke mwenzangu chakula kweli! Hilo swala halipo, yani dada ako mwenyewe huwa simpikii sembuse huyo mende nisiyemjua? Akitaka aje apike mwenyewe”
“Aaaah mke wangu mbona umekuwa mkali hivyo? Pendo kasikia sifa ambazo wamezitoa kazini kuhusu wewe kwahiyo hata sio kosa lake jamani, umemuhisi vibaya tu”
“Haya, kile chakula sikupika mimi, nenda kaongee na mtoto wako kuwa apike tena chakula kumpikia huyo Pendo ila sio mimi niingie jikoni kumpikia mwanamke mwenzangu”
“Mmmmh haya mke wangu nimekusikia wala sina mambo mengine ya kuongea, atakuja tu kusalimia”
“Haya sitaki habari zake”
Mariam alilala yani alichukia kabisa kuhusu huo ujio wa Pendo yani hakutaka hata kumfahamu alitamani hata kumwambia mume wake kuwa huyo Pendo asifike kabisa mahali hapo.

Kulipokucha, Juma alijiandaa ili kuondoka kwenda kwenye shughuli zake ila Mariam alirudia kitu kile kile,
“Juma, sitaki kusikia habari za kumpikia huyo Pendo hapa natamani hata usije nae kabisa”
“Usiwe hivyo mke wangu jamani, najua huna roho hiyo mke wangu naomba usiwe hivyo”
Mariam hakusema kitu, muda huo huo Juma na yeye akaondoka zake, ndani kama kawaida alibaki Mariam na yule mtoto wao ambapo mtoto alimuuliza mama yake,
“Kwanini umetokea kumchukia huyo Pendo mama?”
“Aargh siwezi kumkubali mimi, yani mwanamke mwenzangu halafu nimpikie chakula!”
“Ila ni mgeni mama”
“Hata kama, siwezi kuingia jikoni kumpikia mwanamke mwenzangu mimi”
“Ila mama ukimuona huyo Pendo wewe mwenyewe utajihisi haya, sio kama hivyo unavyodhani alivyo. Ni mwanamke mzuri halafu ni mstaarabu na mcheshi ndiomana baba anapenda sana kuongea nae. Ukimuona kwa hakika utampenda na kumfurahia”
“Mmmmh ila wewe nawe umejuaje hizo habari za Pendo?”
“Namjua sana Pendo, unadhani simjui? Hata wewe umewahi kumuona ila tu huwezi kumkumbuka maana siku ile alipatwa na maswahibu”
“Maswahibu gani? Unaongelea kuhusu tukio gani?”
Yule mtoto hakumjibu ila alidai kuwa njaa inamsumbua na kumfanya Mariam ainuke kwa hasira kwenda kumuandalia huyu mtoto chakula.

Juma alijitahidi kwa siku ya leo ili huyu Pendo asikumbuke chochote na wala asiondoke nae, basi alifanya kazi zake na kuwahi kuondoka ila alipita kwanza sokoni ambapo baada ya kununua bidhaa akakutana tena na yule jirani yake ambaye alimsalimia na kusema,
“Nakuona mwanaume wa kipemba”
“Dah wewe jamaa jamani! Sasa mwanaume wa kipemba ndio nini! Acha zako bhana”
“Haya nimeacha ila umesikia yaliyopo?”
“Yapi hayo?”
“Kulitokea na msiba mtaa wa pili kule, sasa kuna yule mama jirani nasikia alikutana na wewe na akakwambia kuwa anakuja kumfata mkeo ili waende msibani, sasa kamfata mkeo lakini mkeo kamfukuza, swala lile limefanya watu waseme kuwa yule mtu umemuua wewe”
“Khaaaa hayo mambo ya kusema mimi naua watu bado yapo tu!”
“Yapo ndio, yani inasemekana umemuua huyo kijana. Pole sana ndugu yangu”
Juma aliitikia tu na kuagana na yule jirani ila alijiuliza sana kuhusu mke wake kumfukuza huyo mama aliyeenda kumchukua waende msibani, alishangaa sana na akaona ni vyema akirudi amuulize mkewe.

Mariam na mtoto wao wakiwa wametulia, mara Mariam akasikia mtuakibisha hodi na kwenda kumfungulia hapo alimuona mwanamke mmoja mrembo na mnene amesimama, basi akamsalimia na kumkaribisha,
“Karibu”
“Asante, bila shaka wewe ni Mariam mke wa Juma”
“Ndio ni mimi, na wewe je ni nani?”
“Mimi naitwa Pendo”
“Haya karibu Pendo”
Basi Pendo aliingia ndani na kumkuta yule mtoto amekaa kwenye kochi, kwakweli alimuogopa sana na hata kumsalimia alishindwa ila yule mtoto alimsalimia,
“Shikamoo anti Pendo”
Pendo alijibu kwa kisitasita,
“Marahaba”
Kisha yule mtoto akamwambia Pendo,
“Hujaja na njaa? Kama umekuja na njaa basi jiko lipo kwaajili yako na ukajipikie mwenyewe maana mama yangu hawezi kuingia jikoni kumpikia mwanamke mwenzie”
Yani hata Mariam alishangaa kwa ile kauli ya mtoto wake.

Juma akawaza njiani kuwa apitie kwa yule jirani ili akamuulize vizuri halafu ndio aende kumuuliza mke wake, wakati anaenda kwa yule jirani aliona kuni njiani na kuikota ile kuni ili kumpelekea mtoto wake.
Halafu moja kwa moja alienda hadi kwa jirani yake na kugonga ambapo yule jirani alitoka pale nje ila yule jirani alipomuangalia Juma mkononi alianza kupiga kelele na kufanya watu waanze kujaa mahali pale.

Itaendelea…..!!!
Kwa mawasiliana nami kwa no.0629980412 sasa itaruka kwa wiki mara moja ukitaka full ni 1000 tu
 
MTOTO WA MAAJABU: 34

Halafu moja kwa moja alienda hadi kwa jirani yake na kugonga ambapo yule jirani alitoka pale nje ila yule jirani alipomuangalia Juma mkononi alianza kupiga kelele na kufanya watu waanze kujaa mahali pale.
Yani Juma kila upande alioangalia aliona watu wanazidi kujaa na kumfanya aogope sana wala asijue ni kitu gani ambacho yule jirani yake amekiona kwake, Juma aliogopa sana na pale alifanya tu maamuzi ya kukimbia tena alikimbia sana.
Alikuja kusimama mahali akiwa amechoka sana na kuona kuwa hata nyumba yake ameipitiliza, kuna mtu alimsalimia pale njiani,
“Vipi mbona unahema hivyo?”
“Kuna watu wananikimbiza”
“Khaaaa watu wanakukimbiza? Kivipi?”
“Nilienda kwa jirani yangu kumuuliza kitu, hata sijui imekuwaje baada ya kuniangalia mikononi akaanza kupiga makelele”
Yule mtu na yeye alimuangalia mikononi Juma halafu yule mtu alianza kukimbia pia kamavile anamuogopa Juma yani jambo lile lilimfanya tena Juma aanze kukimbia kurudi nyumbani kwake.

Kwakweli Pendo alikuwa akishangaa sana pale, hata alishindwa kujibu kabisa kwa jinsi mtoto alivyokuwa akisema, kisha yule mtoto akasema tena kwa kumuuliza mama yake,
“Au mama naongopa? Si ulisema kuwa huyu anti akifika na apike mwenyewe chakula maana wewe huwezi kumpikia mwanamke chakula!”
Mariam alitazama chini kwa aibu, aliona huyu mtoto amemdhalilisha sana sababu hakutegemea kabisa kama angesema kitu cha namna ile, ila muda huo huo Juma alifika na kufungua mlango huku akiwa anathema sana hakuna mtu aliyemuelewa kuwa kapatwa na nini, Mariam anamsogelea na kumuuliza,
“Tatizo ni nini mume wangu?”
Kwakweli Juma hakujibu kwa wakati huo maana hata hakujihisi kujibu kabisa, basi moja kwa moja alienda zake chumbani hata Mariam alishangaa na kumfata chumbani kwahiyo pale sebleni alibaki Pendo na mtoto ambapo Pendo aliogopa na kumuaga yule mtoto kisha mtoto akamwambia,
“Utaondoka vipi bila kula? Kwani huna njaa?”
“Mmmh hapana sina njaa”
“Jamani! Wewe si ulimwambia baba kuwa unataka kula chakula alichopika mama?”
“Ndio nilisema hivyo ila hapana, naondoka tu”
“Hapana usiondoke, ngoja nikwambie kitu. Yale niliyokuwa nakwambia hapa ni utani tupu, hakuna la ukweli hata moja pale nilikuwa nakutania tu. Mama na yeye alikaa kimya sababu nilishamtonya, ila mama kakupikia chakula mbona kile pale mezani”
“Mmmmh hapana, asanteni mimi naondoka tu”
“Hapana, usiondoke bila kula. Usiondoke bila kuonja mapishi ya mama yangu”
Kwakweli Pendo alimshangaa sana huyu mtoto ila hakuweza kumbishia zaidi hivyo aliamua kwenda hapo mezani na kupakua chakula kidogo kuanza kula ila kile chakula kilikuwa ni kitamu sana hata kumfanya Pendo aongeze mara mbili na kisha alivyoshiba alienda kukaa ila mtoto akamwambia,
“Unaweza kwenda, unadhani mama na baba watatoka muda huu? Hawawezi wapo kumtafuta mdogo wangu”
“Kheeeeee!!”
Pendo akainuka na kuondoka zake, kwakweli mambo ya huyu mtoto yalimshangaza sana Pendo.

Kwakweli Juma hakuwa sawa kabisa na moja kwa moja alijilaza kitandani tu ambapo Mariam alianza kumbembeleza pale na kujikuta wakiwa wamelala, walikuja kushtuka saa tano usiku wakati njaa zimewashika haswa, tena aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Juma,
“Wewe Mariam, hata kunishtua mwenzio niende kula ndio nini?”
“Mmmh hata mimi sijala, njaa imenishika hatari hapa nilipo”
“Ila chakula si kipo?”
Mariam hakumjibu na kuendelea kulala tu, hapo Juma akaona kuendelea kumuamsha Mariam ni kujipa kazi ya bure tu, basi akaamka moja kwa moja na kwenda kuangalia chakula, akakuta chakula mezani na kukaa na kuanza kula , kisha alivyomaliza ndio alienda kuoga na kurudi kulala tena, kwakweli alikuwa amechoka sana sababu ya zile mbio ila alishukuru sana kukuta chakula ingawa mke wake hakuamka wala nini.

Kulipokucha sasa ndio Juma alianza kulalamika kwa Mariam kuhusu ile kuni aliyoibeba,
“Khaaa yani zawadi ya huyu mtoto imeniletea balaa jamani, sina hamu kabisa sina hamu yani”
“Pole imekuwaje tena?”
“Ngoja nikuulize kwanza kabla sijaendelea, na wewe ndio nini kumfukuza jirani aliyekuja kukuchukua kwenda msibani!”
“Mmmmh jirani gani huyo?”
“Yule jirani yetu ambaye huwa tunaongea nae, kwanini umemfukuza?”
“Ila Juma mambo mengine yanachekesha kweli, hivi mtu ambaye alikuwa mstari wa mbele kusema tuchomewe nyumba na tufie humu ndani eti anakuja kunichukua niende msibani, ulitegemea ningekubali? Toka lini nimeenda msibani mimi? Yani sio msiba si sherehe hakuna mahali nilipowahi kwenda, sasa anakuja kunifata kwa misingi ipi? Nimemtimua ndio”
“Khaaaa Mariam kumbe umemtimua kweli?”
“Ndio, tena mtoto ndio kanikumbusha na kuniambia mama kumbuka hao ndio waliotaka kuchoma nyumba ili kuwamaliza mkiwa humu ndani, halafu pia huwezi jua kama huo msiba wamewasingizia nyie je utakuwa salama kweli huko mama? Labda anataka kukuweka kwenye mtego? Maneno ya mtoto yaliniingia akilini kweli, niliweza kutambua na kuelewa kuwa ni kitu gani alichokuwa anacungumzia, nimemtimua mbali na mambo yake ya misibva, akafie huko mbele ya safari, asiniletee ujinga mie”
“Duh!! Sikutegemea kabisa kupata jibu kama hili kutoka kwako”
“Ndio umelipata sasa, haya sema kilichokuleta jana unahema juu juu ni kitu gani?”
Juma akamsimulia mke wake kuhusu ile kuni ambayo mtoto kamuagiza na kumfanya Mariam asikitike huku akimuuliza,
“Sasa wewe umeenda kuleta kuni ya aina gani? Kwanini iwe na maajabu kiasi hiko? Uliitoa wapi?”
“Mmmh sijaitoa sehemu yoyote ya ajabu, ni njiani tu nimeitoa ila nashangaa kufika kwa huyo jirani ndio nikakutana na hayo maswahibu”
“Ila na wewe ni kiherehere chako, nini kilikupeleka kwa huyo jirani kama sio kiherehere”
“Khaaaa yamekuwa hayo? Ngoja nijiandae tu niende kwenye shughuli zangu”
Moja kwa moja Juma alienda kujiandaa na kuondoka zake kwenda kwenye shughuli zake.

Mariam alibaki na huyu mtoto sasa na muda huu Mariam alikuwa na njaa sana, alienda kupika chai na kukuta kuna vyombo vichafu basi akalalamika,
“Yani huyu Juma na yeye sijui vipi kachafua vyombo halafu nioshe mimi jamani khaaaa!”
Akatoka na chai yake hadi mezani ambapo alikuta chakula na kusema,
“Ooooh kuna kiporo leo, ach anile mie. Ila huyu Juma huyu, ona na hapa mezani sahani chafu jamani wanaume wengine kazi tupu na kuosha naona uvivu hatari”
Mariam alipokunywa chai tu alirudi kukaa akiwa amechoka na kulalamika kuwa anaona uvivu kufanya kazi zingine, mtoto wake akamuuliza,
“Unaona uvivu kufanya kazi gani mama na zipo kazi ngapi?”
“Yani kuna kazi nyingi sana humu ndani ndiomana huwa nahitaji msaidizi wa kazi, ona chumbani kwangu sijasafisha, nyumba sijasafisha, uwanja sijafagia halafu vyombo vichafu vimejaa jamani. Huyu huyu Mariam ambaye ni mjamzito ndio afanye kazi zote hizo loh!! Nimechoka mimi”
Mtoto akatabasamu na kusema,
“Mama, usisingizie mimba maana hata usingekuwa na mimba bado ungelalamika ukizingatia uvivu ni tabia yako tu mama yangu. Haya tukianza na kusafisha nyumba, wiki yote hii hujasafisha unadhani nyumba itaacha kuwa chafu, huo uwanja hujawahi fagia toka aondoke shangazi, tukija chumbani kwako ndio kabisa nahisi hadi chumba kinatamani kukwambia kuwa nisafishe, hivyo vyombo toka juzi hujaviosha halafu upo kushangaa kuwa ni vingi khaaa mama yangu jamani acha uvivu”
Mariam alimtazama mtoto wake na moja kwa moja alienda kutoa vile vyombo vyote nje kwaajili ya kuviosha ila hata hakujua aanzie wapi na vile vyombo kisha mtoto wake akamwambia,
“Andaa maji na kila kitu kwenye vyombo halafu mimi nitaosha ila wewe usafishe nyumba mama na ukasafishe chumba chenu cha kulala”
Hapa Mariam hakusema neno ila tu alienda kuandaa maji na sabuni ili yule mtoto akaoshe halafu yeye akarudi kujikongoja kusafisha ndani.
Ila alianza kusafisha ndani huku akili yote ipo nje kujua ni jinsi gani yule mtoto anasafisha vyombo wakati bado mdogo sana.
Basi kuna muda alivizia na kwenda kumchungulia dirishani ili kuona anaosha vipi vyombo, akamuona anaosha tu mwenyewe yani hakuna aliyekuwa akimsaidia wala hakuna ajabu lolote lililokuwa likifanyika, kwahiyo alishangaa kwa muda na kwenda kuendelea na kazi ya kusafisha ndani.

Juma alipokuwa kwenye kazi yake, alifatwa na Pendo muda huu ambapo Pendo alianza kumwmabia Juma,
“Mmmmh jamani Juma yule mtoto wako jamani mmmh!!”
“Kwani vipi?”
“Yani jana kanishushua sijapata kuona hadi nimeshikwa na aibu Juma, sirudii mimi kufata chakula kwenye vijumba vya watu”
“Mmmmh pole sana”
“Ila chakula nilikula na kilikuwa kitamu sana, nilitaka kuondoka bila kula ila yule mtoto wako hapana jamani, ndio akaniambia kuwa siruhusiwi kuondoka hadi nile chakula, nilipakua kidogo kwanza, ila chakula kilikuwa kitamu sana na kufanya niongeze mara mbili yani nilirudi nyumbani kwangu bila kula tena. Ila sirudii kuja kwenye vijumba vya watu kula, mtoto wako anashushua sana”
“Pole sana, mzoee tu, sisi tushamzoea”
“Halafu uliniambia kuwa hayupo kwa kipindi hiki mbona nimemkuta tena?”
“Ndio karudi jana ile ile ila alikuwa kwa bibi yake yule”
“Halafu kaniambia kuwa mpo chumbani kutafuta mdogo wake, mbona mtoto wenu ni waajabu sana?”
“Mmmmh tuachane na hayo, tuendelee na shuguli nyingine Pendo maana hata sioni umuhimu wa kuongea yote hayo tunayoongea”
Yani Juma alikatisha yale maneno maana aliona akiendelea kuongea anaweza kuongea mengine yasiyohusika bure.

Mariam akiwa amepumzika muda huu maana alijihisi kuchoka hatari, akapigiwa simu na mdogo wake Zayana na kuanza kuongea nae,
“Dada, nimepata mchumba”
“Ooooh hilo ni jambo jema sana mdogo wangu, mchumba huyo ni mtu wa wapi?”
“Ni mtu wa pwani dada na ananipenda balaa”
“Hongera sana mdogo wangu, kashakuja nyumbani kujitambulisha?”
“Bado, ila kasema anakuja mwezi ujao, yani nimefurahi sana dada. Nimechoka kukaa nyumbani mimi. Natamani kuolewa ili niishi kwenye mji wangu kama wewe”
“Usijali mdogo wangu, ilimradi umempata mchumba basi ni jambo la kushukuru maana uchumba ndio mwanzo wa ndoa huo mdogo wangu”
“Naelewa dada na nimefurahi sana dada yangu”
Basi akampongeza mdogo wake na kuagana nae kwenye simu, kisha alikata ile simu ila muda ule ule mwanae akamwambia,
“Mama, huyo mchumba anayetaka kumuoa mamdogo hafai kabisa”
“Mmmmh kwanini hafai sasa?”
“Huyo mwanaume ni mchawi, hamfai mamdogo na akiolewa nae atajuta maisha yake yote”
“Unaongelea nini wewe?”
“Hamna kitu mama ila huyo mchumba hamfai mamdogo, mwambie kabisa aelewe”
“Mmmmh haya nimekusikia”
Mariam alimuitikia tu huyu mtoto wake ila kiukweli hakumuamini wala nini tena hakumuamini kabisa.

Usiku wa leo, Juma aliamua kumuuliza mke wake kuhusu chakula ambacho Pendo alikula maana anakumbuka mara ya mwisho kuwa hatopika,
“Vipi mke wangu uliamua kumpikia Pendo?”
“Mmmh sikupika halafu mtoto wako kaniumbua kwa huyo Pendo hatari, bora hata nikaja na kulala maana niliona aibu sana kutoka”
“Kivipi mke wangu?”
“Yani alivyokuja si akaanza kusema kuwa mimi nimesema sipiki chakula kwa mwanamke mwenzangu? Yani kaniumbua huyu mtoto balaa”
“Pole ila Pendo ameshukuru sana kwa chakula ulichompikia ingawa kasema kuwa hatorudia tena kwenda kwenye vijumba vya watu kula sababu ya maneno aliyoyapata kwa mwanao”
“Sasa ananishukuru kwa chakula gani?”
“Si anasema ulipika chakula, alishindwa kuondoka sababu mtoto alimzuia kuondoka hadi ale, anasema kuwa alipokula kile chakula eti kilikuwa ni kitamu sana hadi akaongeza mara mbili”
“Mmmmh sasa hiko chakula kakitoa wapi?”
“Kakitoa wapi kivipi wakati wewe ulipika?”
“Mimi sikupika ujue, ingawa laity ningejua jinsi yule Pendo alivyo basi ningepika”
“Kwahiyo chakula kile kilipikwa na nani?”
“Labda na mtoto”
“Hivi Mariam mzima kabisa wewe? Yani unajibu kwa ujasiori kabisa kuwa chakula labda kimepikwa na mtoto, ni wa kupika chakula huyu jamani!”
“Unashangaa nini sasa wakati chakula cha wageni alipika na nilikueleza”
“Nakumbuka ila hiki inaonyesha hata maelekezo hukumpa, anapikaje?”
“Na wewe hebu acha kumuwaza mtoto mwenye uwezo hata wa kuosha vyombo, mambo mengine tukimtafakari huyu mtoto tunaweza kuwa vichaa humu ndani. Naomba habari zingine za huyu mtoto tuwe tunazipotezea tu”
“Mmmmh ushamzoea eeeh!”
“Kiasi, nitafanyeje sasa zaidi ya kumzoea? Mimi ndio mama ujue, halafu ujue nikiondoka najikuta nimerudi hapa! Unaambiwa kuwa kama huwezi kupigana nao basi jiunge nao, na mimi nimejiunga na yeye, ingawa kuna vitu namchunguza ila nishamzoea”
“Hongera ila sijamzoea jamani huwa naona mauza uza tu kwa huyu mtoto tena ananichanganya hatari, ipo siku nitamvizia nimuone anavyopika”
Mariam akacheka tu na kumshauri Juma kuwa walale muda huo sababu wakiwaza sana na kutafakari juu ya yule mtoto wakakuwa vichaa.

Leo Juma hakwenda kwenye shughuli ake kwani mapema kabisa alipigiwa simu na baba yake mdogo,
“Juma, nakuja huko kwako”
“Sawa, karibu baba”
“Nikukute maana nasikia mambo yako watu hawakukuti wanamkuta tu huyo mke wako”
“Utanikuta baba”
Juma akatulia tu na akampa mkewe habari ya ujio wa huyo baba mdogo wa Juma na kumfanya Mariam aanze kulalamika kama kawaida yake,
“Aaaah huwa sipendi haya mambo ya wageni, basi kupika pika kunaanza tena”
“Mmmmh jamani Mariam utafikiri kupika ni kitu gani jamani!”
“Hata kama sipendi, halafu kubwa zaidi utashangaa kaja na mizigo ya kukaa wiki nzima, huwa sipendi mimi basi tu”
“Ndoja nikuulize Mariam, kwanini huwa hupendi wageni sasa?”
“Sipendi biashara ya kupika pika na kuanza kuhudumia wageni, sijui kuwasalimia na kuanza kuongea ongea nao huku nikijifanya ni mstaarabu wakati sina huo ustaarabu hata robo”
“Mmmh hapa mke nimepata kwakweli”
“Ndio, tena umepata haswaa. Nenda jikoni ukapike mwenyewe, mimi sipiki leo”
Yani hili eneo ndio lililokuwa linamkera sana Juma kwa huyu mke wake, yani mke wake alikuwa ni mvivu sana kiasi cha kumfanya awe anachukia kwa hilo.
Juma akatoka nje na kwenda kusafisha uwanja maana ulikuwa ni mchafu sana sababu Mariam hakufagia, muda huu mtoto alimfata Juma na kumwambia,
“Pole baba kw akuoa mke mvivu kama mama yangu”
Juma alimuangalia huyu mtoto na bila kusema neno lolote lile ila aliendelea kufagia tu, kisha yule mtoto akamwambia Juma,
“Unajua dawa ya mama kuacha uvivu ni nini?”
Hapo Juma alimuangalia na kumuuliza sasa,
“Ni nini?”
Mtoto akatabasamu na kumwambia Juma,
“Dawa ya mama kuacha uvivu ni Anna tu, umemuondoa Anna bure hapa. Asingefanya ule ujinga tena ningemkomesha”
Juma akamuangalia na kusema,
“Ila Anna angemtesa mama yako akiwa kalala, na mama yako kwasasa ni mjamzito”
Basi yule mtoto akamuuliza tena Juma,
“Je unaniruhusu mimi nimfanye mama aache uvivu?”
Juma akashtuka na kumuangalia huyu mtoto kisha akamuuliza,
“Mmmmh na wewe unataka kumfanya kama Anna alivyokuwa akimfanya?”
“Kheee mbona wewe baba unashangaza? Siku zote huwa nakwambia mimi sio mchawi wala nini, sasa nimfanye mama kama Anna alivyokuwa anafanya natoa wapi uwezo huo?”
Hapo Juma alimtazama tu kwani kila alichokuwa akitaka kumuuliza yeye mwenyewe binafsi hakukielewa, ila muda huo huo Mariam alimfata Juma pale nje na kumwambia,
“Baba, ameshafika”
“Khaaa kumbe alikuwa akiniambia wakati yupo kwenye gari!”
Basi Juma aliacha lile fagio lake ili kwenda kumkaribisha yule baba yake mdogo ila muda huu na mtoto na yeye alikuwa kamfata Juma nyumba.
Walipoingia sebleni, yule baba ndio alikuwa anakaa ila yule mtoto akamwambia,
“Babu, toka nje”
Yani Juma na Mariam walijikuta wakimuangalia huyu mtoto bila majibu.

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 Whatsapp tu
 
MTOTO WA MAAJABU: 35

Basi Juma aliacha lile fagio lake ili kwenda kumkaribisha yule baba yake mdogo ila muda huu na mtoto na yeye alikuwa kamfata Juma nyumba.
Walipoingia sebleni, yule baba ndio alikuwa anakaa ila yule mtoto akamwambia,
“Babu, toka nje”
Yani Juma na Mariam walijikuta wakimuangalia huyu mtoto bila majibu.
Ila mtoto akazidi kusema,
“Babu toka nje”
Yule babu alisimama kwa uoga sana bila kujua ni kwanini atoke nje ila hata yeye alijikuta akiogopa kumuuliza huyu mtoto, yule mtoto akatabasamu na kusema,
“Hivi wote mnachoshangaa mnashangaa nini? Unawezaje kumruhusu baba yako na mkwe wako aingie ndani kukiwa kuchafu hivi!”
Wote walijikuta wakiangalia mule ndani, ni kweli nyumba ilikuwa ni chafu kisha mtoto akasema,
“Kama nyie mnapenda uchafu basi sawa ila mimi sipendi uchafu na kwamaana hiyo, babu yangu hawezi kukaa mahala pachafu, naomba babu utoke nje ili mama asafishe kwanza humu ndani halafu ndio babu utaingia ndani, lazima uheshimiwe wewe ni baba na ni mkwe wake, huwezi kukaa kwenye sebule chafu hivi”
Yani Mariam alijihisi aibu sana, basi Juma na yule babu waliamua kutoka nje maana Juma ilibidi tu aende kumuomba radhi yule babu ila muda huo huo yule mtoto na yeye alitoka nje na kumfanya Juma asiongee sana na yule baba yake mdogo na kubaki tu wakimuangalia yule mtoto ambaye alionekana kama kucheza michezo ya kitoto.

Mariam alichukia sana, tena sana yani hakujua kama huyu mtoto angemuumbua kiasi hiki, akakumbuka jinsi alivyomwambia kuwa yeye aoshe vyombo halafu yeye asafishe ndani ila kwa uvivu wa Mariam aliona shida kusafisha vizuri mule ndani ila leo mtoto kamuumbua, alichukia sana na kuanza kusafisha nyumba hivyo hivyo huku kachukia.
Alipomaliza kusafisha, alienda na kuwakaribisha ndani ambapo waliingia sasa na kukaa huku yule babu akimwambia Mariam,
“Pole sana mkwe”
“Asante”
Mariam alijibu kwa aibu huku macho yake ameyainamisha chini.
Walipokuwa wakiendelea na maongezi, mtoto akasema,
“Mama, kamuandalie babu chakula maana lazima atakuwa na njaa si unajua katoka safari”
Yani Mariam alitamani hata kumtukana huyu mtoto ila hakuwa na cha kufanya tu, na moja kwa moja aliinuka na kwenda kuandaa chakula.
Alipika huku akiwa amenuna kabisa, kisha akakitayarisha kile chakula mezani na kumkaribisha mgeni ila alikuwa amenuna sana.
Yule babu na wengine walienda mezani na kula chakula huku babu akisifia uzuri wa kile chakula na kumsifia sana Mariam kwa mapishi yani Mariam alikuwa amechukia sana hata hakufurahia jambo lile hata kidogo.

Jioni ilipofika, wakiwa wanaongea ongea pale mtoto yule akawakatisha maongezi yao na kusema,
“Mama, unajua babu amechoka, ungeenda kumsafishia chumba chake ili aweze kupumzika”
Yule babau na yeye aliongezea pale,
“Dah! Na kweli nimechoka sana mjukuu wangu”
Basi Mariam aliinuka kwa hasira yani alikuwa amevuta mdomo haswa na kwenda kusafisha kile chumba ila alikuwa anaona uvivu hatari yani alikuwa anafanya ile kazi basi tu, ilimradi amefanya ila kiukweli hakupenda hata kidogo na alipomaliza ndipo alipoenda kumuita ambapo yule babu alishukuru sana na kwenda kupumzika, ila wakiwa pale sebleni Mariam alimuuliza Juma,
“Huyu babako mdogo anaondoka lini?”
“Mmmmh Mariam mke wangu, mbona mapema sana?”
“mapema kitu gani? Mimi nilishakwambia sipendi wageni halafu wewe unaenda kuniletea wageni ili iweje?”
“Sasa tutakuwa ni watu wa aina gani mke wangu ambao hatutembelewi na wageni?”
“Lini nimeenda kwao kulala mimi? Nikienda huwa nawasalimia na kurudi ila wenyewe wanataka kufanya maamo kabisa, mbabu huyo si ana mji wake jamani, halafu licha ya hivyo ana watoto wake kwanini asiende huko kukaa? Hadi aje kwako wewe mtoto wa kaka yake?”
“Hebu Mariam mara nyingine uwe na staha, kumbuka yule ni baba yangu mdogo yani mdogo wake baba yangu mzazi, halafu kumbuka baba yangu mimi alikufa zamani sana kwahiyo yule unayemuona ndio kabeba asilimia kubwa ya maisha yetu kwasasa, mimi ni mtoto wake pia, na hata hajasema bado alichokuja kufanya halafu tayari ushaanza kumuwekea vikwazo kweli tutafika mke wangu?”
“Aaarrgh muone vile”
Mariam akainuka na kwenda chumbani yani hakupenda kabisa jambo lile.

Usiku wakati wa kulala, Mariam alianza tena kumlalamikia Juma maana aliona sasa atateseka na kazi za mule ndani,
“Juma, ni wewe ndiye umekubali kuwa baba yako mdogo aje mahali hapa halafu mtoto wako akiwa ananiumbua unachekelea mwenyewe, inamaana wewe hujui kusafisha nyumba? Hujui kupika wewe? Hujui kusafisha chumba wewe? Kwanini kuacha niteseke ilihali unajua fika kuwa mimi ni mjamzito?”
“Mmmmh naomba unisamehe mke wangu, nisamehe sana kuanzia kesho nitajitahidi ila mimi nitaenda kazini”
“Hakuna kwenda kazini hadi huyo mbabu wako aondoke, mimi siwezi kufanya kazi kama mtumwa, unalijua hilo kabisa, sikuwa na mimba tu na sikuweza kufanya kazi, sembuse kwasasa nina mimba!! Kwakweli siwezi kufanya kazi, nisamehe bure tu”
“Haya mke wangu nimekuelewa hakuna tatizo mke wangu, naomba tulale”
“Ndio ila niliyokwambia yaweke akilini, nisije nikajibu vibaya mimi nikaonekana sijui mke gani”
Yani Mariam alikuwa akiongea kwa jazba kabisa kuonyesha jinsi gani kachukia kwa swala la yeye kuambiwa afanye kazi kwaajili ya yule mgeni aliyewafikia.

Asubuhi ya leo walikaa pamoja wakipata kifungua kinywa, na baada ya hapo walikaa kufanya maongezi huku Mariam akisinzia tu pale ila alishtuliwa na kauli ya mtoto,
“Mama, jamani vyombo hadi vinanuka toka juzi usiku havijaoshwa jamani mama!”
Mariam akamuangalia Juma ambapo Juma akasema,
“Hakuna tatizo, nitaenda mimi kuviosha”
Mtoto akatikisa kichwa na kumuangalia babu yake kisha akamuuliza babu yake,
“Eti babu ni halali hiyo? Mama yupo amekaa tu halafu baba aende kuosha vyombo, ni halali hiyo?”
Babu na yeye akasema,
“Hapana si halali, kijijini sisi huwa hatuishi hivyo sijui kwa watu wa mjini ila si halali kwakweli. Kusaidiana kupo ila sio huku yani mke amekaa tu halafu mume aende kuosha vyombo hapana si halali”
Mariam hakujibu kitu pale ila aliondoka kwa hasira sana na kubeba vyombo hadi nje kwenda kuviosha yani alikuwa amechukia sana.
Mariam alikuwa akiosha huku akiwaza ni kitu gani cha kumfanya huyu mtoto maana aliona kamavile mtoto anamfanyia makusudi tu na usikute ni jambo ambalo mtoto amepanga kulifanya kwake kwahiyo Mariam alikuwa akinuna muda wote.

Usiku wa leo ndio Mariam alianza kulalamika zaidi kuhusu zile kazi yani alilalamika sana na kumwambia Juma kwa ukali,
“Jamani Juma nimechoka, yani nimechoka kabisa inaonyesha wazi unafurahia hiki ambacho mtoto anakifanya, mimi nimechoka kwakweli. Kwanini Juma lakini”
“Ila mke wangu, ulitegemea mimi nifanye nini sasa? Ulitaka nifanyeje jamani? Kumbuka kila nikitaka kukusaidia kazi, mtoto anaanza kumwmabia yule babu sijui inaruhusiwa kufanya hivi na hivi mpaka bamdogo anaanza kunihisi vibaya kwakweli, yani nashindwa mke wangu”
“Kama unashindwa mwambie huyo bamdogo wako aondoke, kwani Juma unashindwa nini jamani khaaaa!! Kwakweli nimechoka mimi, tena nimechoka sana jamani Juma. Usinifanyie hivi jamani”
“Pole mke wangu ila nitajua cha kufanya usijali”
“Nisijali nini sasa jamani kwa mambo kama haya? Hata huna huruma na ujauzito wangu, hata hunihurumii kwa hali niliyokuwa nayo?”
“Nakuhurumia mke wangu, tena nakuhurumia sana ila sina cha kufanya”
“Usinichanye na jibu lako hilo la sina cha kufanya, nitakuja kufanya jambo hapa na kukufanya ujutie katika maisha yako yote”
Mariam akalala muda huu bila kuongezea neno hapo.

Kulipokucha tu, Mariam akamuomba Juma pesa ili akaangalie mboga ila Juma alisema kuwa ataenda mwenyewe,
“Hivi wewe mwanaume una nini lakini? Ndiomana yule anakuitaga mwanaume wa kipemba, ni wivu gani huo uko nao? Tumezaa na hapa nilipo ni mjamzito, unadhani nitachepuka na nani? Niache nikanunue mboga na mimi niangalie mji nipunguze mawazo”
“Basi twende wote”
“Uende wote na nani? Nisamehe sana, siwezi kwenda popote na wewe. Naomba leo nikanunue mwenyewe”
Juma akapumua ila hakutaka marumbano na mke wake, hivyo akampatia pesa ili aende kuangalia hiyo mboga aliyokuwa anaisema na muda huo huo Mariam alijiandaa na kutoka nyumbani kwake, kwahiyo Juma alibaki yeye na baba yake pamoja na mtoto wake.
Waliamua kupika chai na kunywa ila yule babu alikuwa akisikitika na walimpomaliza kunywa chai alimuomba Juma waende kuongea kidogo ambapo Juma alitoka nje na yule babake mdogo.
“Kwanza kabisa Juma unajua kilichonileta hapa?”
“Mmmmh sijui baba, nilijua umekuja kusalimia tu”
“Licha ya kusalimia ila kipo kilichonifanya nije hapa”
“Kitu gani hiko baba?”
“Ni kuhusu mtoto wako”
Juma akashtuka kidogo kwani akajua ni lazima na ndugu zake nao washatangaza mambo ya ajabu ya yule mtoto,
“Ndio baba, kafanyeje?”
“Sikia, kwa habari nilizosikia ni kuwa Juma ana mtoto wa ajabu sana sijui mtoto anafanya mambo ya miujiza, sijui mtoto anafanya mambo ya uchawi, nikasema acha niende kujishuhudia huko huko ili nijue jinsi ya kumsaidia huyo Juma”
Basi Juma alitulia akimsikiliza baba yake,
“Ndio baba nakusikiliza”
“Ila toka nimekuja sijaona kama mtoto ana tatizo ila tatizo hapa ni mke wako”
“Kivipi baba?”
“Mmmmh sijapata kuona mke mvivu kama mke wako”
“Kwanini baba?”
“Jamani mke hadi anakumbushwa usafi wa nyumba yake na mtoto! Mke hata hajui kama wageni wanatakiwa kula hadi mtoto amkumbushe? Mke hata hajui wajibu wake hadi aambiwe na mtoto, tena unaona sawa tu kwa wewe kufanya shughuli za kike wakati mkeo amekaa jamani Juma ni aibu gani hii? Umeoa au umeolewa?”
“Jamani baba ni kusaidiana”
“Kusaidiana sio kwa namna hiyo mwanangu, labda uniambie mmeamua kwenda kuosha wote vyombo au mmeenda wote kufua, ila sio wewe uende kuosha vyombo kwa niaba ya mkeo halafu yeye amekaa tu, sio heshima hiyo kabisa, wewe ni mwanaume”
“Mmmh ila baba mke wangu ni mjamzito”
“Aaaah kumbe ni mjamzito?”
“Ndio baba”
“Basi sina usemi zaidi ila mke wako ni tatizo kushinda huyo mtoto wako, nimemaliza”
Juma hakujua cha kuongea zaidi na baba yake maana aliona aishie pale pale kuongea nae kwani tatizo la mke wake alikuwa analijua yeye mwenyewe.

Mariam alipokuwa sokoni alikutana na mdogo wake wa siku nyingi na kumfurahia sana, alimsalimia pale na kumuuliza,
“Vipi ushaolewa?”
“Namshukuru Mungu, ndoa yangu umepita yani yule kiumbe nyumbani kwako alinitia uoga sana”
“Yule Anna!”
“Ndio dada, bora ungeniambia mapema”
“Ila nimeshamuondoa pale nyumbani kwangu, hayupo tena. Unaweza kukaribia muda wowote”
“Sawa nitakaribia dada, vipi huku sokoni?”
“Nimefata mahitaji ila nimechoka jamani, kazi nyingi mdogo wangu. Nahitaji msichana wa kazi kiukweli”
“Mmmmh dada, wadada wa kazi wanasumbua siku hizi, unamuhitaji kweli?”
“Ndio namuhitaji, ngoja nikupe namba zangu ili hata ukisikia anapatikana mahali unitafute ili awe binti yangu wa kazi”
Basi yule binti alibadilishana namba na Mariam na kisha kuagana nae, ambapo Mariam alienda kununua mahitaji ila alipotoka sokoni alienda stendi kukaa maana hata hakutaka kuwahi nyumbani kwake sababu ya zile kazi, yani Mariam hakuna kitu alichokuwa akichukia kama kufanya kazi.
Alikaa pale stendi kwa muda mrefu hadi kuna watu walikuwa akifika pale na kuongea na yeye hadi kumzoea kidogo, kwahiyo alikuwa akisikiliza stori za watu wale na inapobidi na yeye alikuwa akichangia, mmoja alianza kusema kuhusu mtoto wake,
“Jamani mwanangu kaongea mapema huyo, huwa ananiumbua hatari, kitu kidogo tu unakuta kashaenda kusema kwa muhusika”
Wenzie wakawa wanacheka na kusema,
“Hivyo ndio vitoto visivyofaa”
Mwingine akawaambia,
“Ila na sisi wazazi mengine tunayataka, sasa mtoto kama kafikia hivyo mpeleke shule, wanapelekwa shule watoto wasioweza kuongea sembuse huyo anayeongea? Mpeleke shule mtoto wa hivyo, akacheze na wenzake huko, akacheze na walimu hata usumbufu nyumbani anapunguza kwa kiasi kikubwa sana sababu anarudi akiwa amechoka”
Lile wazo la kumpeleka mtoto shule ikaonekana wengi sana wanalisapoti na kumfanya Mariam na yeye aone kuwa ni jambo jema kuwa akamshauri mume wake waweze kumpeleka yule mtoto wao shule maana aliona kama ni sehemu ya kumfanya mtoto arudi amechoka basi ni sehemu nzuri sana ilia ache kufatiliwa mambo yake na yule mtoto.

Wakina Juma walimsubiria Mariam hadi walichoka yani hadi Juma aliamua mwenyewe kuingia jikoni na kufanya mapishi ya siku hii maana aliona wazi wakiendelea kumsubiria Mariam basi wataumbuka kabisa.
Basi Juma aliandaa chakula na kumkaribisha baba yake halafu yeye alitoka ili aende kumfata Mariam, ila alipofika nje tu naye Mariam ndio alikuwa anafika,
“Khaaa jamani wewe mwanamke, kuniweka roho juu juu kiasi hiki ndio nini?”
“Kheee kumbe unanipenda eeeh!!”
“Khaaaa jamani Mariam, unajua wazi ni jinsi gani mimi ninakupenda wewe, Kila siku nakwambia Mariam kuwa wewe ni kila kitu katika maisha yangu. Usinifanyie ujinga tafadhari.”
“Sasa ujinga gani niliokufanyia mimi? Ujinga umeutaka wewe kumuacha babako mdogo akae hapa hadi leo”
“Mmmmh usiongee kwa nguvu Mariam, nitajua cha kuongea na huyu mzee na kesho ataondoka ila usiongee kwa nguvu mke wangu”
Mariam akaingia ndani na mboga zake, akamsalimia tu huyu baba kisha moja kwa moja akaenda chumbani kupumzika.

Jioni ilipofika, Juma akasema kuwa ataenda kupika mwenyewe chakula cha usiku ila mtoto akadakia na kusema,
“Kwanini asipike mama jamani wakati yupo?”
Juma akamwambia mtoto,
“Na wewe, mama yako ni mjamzito”
“Hata kama, ila mama ni mvivu kwa asilia, kwani anaumwa? Kuna wengine wanakuwa wajawazito halafu wanaumwa, hao afadhali kidogo ila mama haumwi hata ukucha ila kazi kusema mimi mjamzito, mimi mjamzito, kwakweli mama ni mvivu sana tena sana”
Juma hakujibu kitu ila aliinuka tu na kwenda kupika kwani alimuona jinsi mkewe alivyokuwa na amenuna kwa muda huo.
Leo walipomaliza kula, yule babu alimuita Juma na kuongea nae,
“Mwanangu, kwakweli mimi kama baba yako siwezi na sifurahishwi na hii hali kabisa kabisa”
“Mmmh kwanini baba?”
“Ni aibu na kunifedhehesha sana kama mzazi, mwanangu kesho naondoka narudi kwangu. Tayari jibu la maswali yangu nimeshapata, tatizo la nyumbani kwako sio mtoto wako bali ni mke wako ndio tatizo tena ni tatizo kubwa sana. Unatakiwa kuwa makini mno”
Juma akapumua ila lile swala la huyu baba kuondoka kesho, alilifurahia kwakweli maana hata yeye alitamani tu huyu baba aondoke ili awe huru na mke wake.

Usiku wa siku ile, Mariam alimwambia Juma lile wazo la mtoto yule kupelekwa shule ila Juma alishtuka kidogo na kumuuliza Mariam,
“Unaona ni sawa kwa mtoto yule kwenda shule?”
“Ndio, wanapokea watoto wasioongea sembuse huyo wa kwetu anayeongea?”
“Hiyo hivyo tu ila tambua wa kwetu ni mtoto wa aina gani”
“Natambua mume wangu, ila bora aende huko tupunguze karaha zingine”
“Sawa, sasa huko shule tutasema mtoto anaitwa nani? Kumbuka hata sisi wazazi wake hatujui jina lake”
“Mmmmh hilo nalo neno ila kesho nitamuuliza ili atutajie jina lake yeye mwenyew,e ila huyu mtoto aende shule bhana itakuwa vizuri maana nyumbani ananipa presha tu kila siku”
Wakakubaliana kuhusu jambo hilo kuwa huyu mtoto wao aende shule tu.

Leo mapema kabisa, babu alijiandaa kwaajili ya kuondoka, kwahiyo walimtayarishia chai akawa anakunywa.
Mariam alitoka nje, ila na mtoto na yeye akatoka nje ambapo Mariam akaona ndio muda mzuri wa kumuuliza yule mtoto anaitwa nani,
“Eti mtoto wetu, jina lako ni nani?”
Mtoto akatabasamu na kumwambia Mariam,
“Angalia kule”
Mariam akageuka na kuangalia, ila alipatwa na kizunguzungu cha gafla na kuanguka.

Itaendelea……!!!
Kwa mawasiliano 0629980412
 
MTOTO WA MAAJABU: 36

Mtoto akatabasamu na kumwambia Mariam,
“Angalia kule”
Mariam akageuka na kuangalia, ila alipatwa na kizunguzungu cha gafla na kuanguka.
Mtoto wake akacheka sana na kumuita Juma,
“Baba, baba njoo mama kaanguka huku”
Juma alitoka mbio ndani hadi pale nje ambapo mke wake alikuwa ameanguka, yani hakuelewa kabisa ni kwanini mke wake kaanguka, basi akawa anashangaa na kumuuliza mtoto,
“Nini kimetokea kwani?”
Mtoto akacheka na kumwambia Juma,
“Mama, kawaona wale wanakuja ndio kaanguka na kuzimia”
Juma akageuka na kuwaangalia akashangaa tu kuona ni mjomba wake na watoto zake wa kiume watatu wakiwa na mabegi, kwakweli Juma alishangaa na kujiuliza,
“Sasa wale nao wanakuja kufanya nini? Na kwanini mke wangu aanguke kuwaona?”
Mtoto akacheka na kumwambia Juma,
“Inamaana baba hujui kama mama hapendi wageni?”
Juma alimuangalia huyu mtoto kisha akasema,
“Hata mimi sipendi wageni sio yeye tu”
Kisha Juma akambeba mke wake na kumpeleka ndani, yani yule babu alikuwa akishangaa maana ndio alikuwa katika harakati za kuondoka.
Muda huo huo wale wageni nao walifika mahali pale na kumsalimia yule babu ila mtoto aliwaambia,
“Ni bora mkageuza na kuondoka na huyo babu, yani kwenye nyumba hii sio mama wala sio baba wote hawapendi wageni, mama hadi kazimia alipowaona”
Wale wageni waliangaliana kwa muda huku wakiwa hawaelewi, kisha yule babu akawaambia,
“Asemacho huyo mtoto ni cha kweli kabisa, sababu hata mimi sikupanga kuondoka leo ila imenibidi tu niondoke leo. Huyo mke wa Juma ndio hataki wageni kabisa, hata akiamka asubuhi utakuta amenuna tu, na yeye muda wote ananuna tu”
“Duh!!”
“Ndio hivyo, kilichopo hapa ni kugeuza pamoja na mimi na kuondoka”
Waliangaliana na walishaindwa cha kufanya, ila wakaona bora tu wafate ushauri huu maana mjomba wa Juma akasema,
“Kama Juma wewe tu ambaye ni kama baba yake mzazi hakutaki, sembuse mimi mjomba! Mmmmh tuondoke tu”
Basi wale wageni wote kwa pamoja wakaondoka huku wakimuaga huyu mtoto maana kwa kipindi hiki walikuwa wengi hawaoni uajabu wa huyu mtoto kwani walihisi ni kawahi tu kuongea na walijua ni mkubwa tofauti na umri anaoujua mama yake.

Wakati wa kula chakula cha usiku, Juma ilibidi amuulize huyu mtoto maana wale wageni hakuwaona tena,
“Samahani mtoto wetu, mbona wale wageni hawakuingia tena ndani?”
“Khaaaa nimewaambia ukweli kuwa humu ndani hampendi wageni kwahiyo waondoke tu”
“Kheee kwanini umefanya hivyo?”
Hapo Mariam na yeye akaongea,
“Mwache mtoto kama kawaambia ukweli, aaah sipendi wageni mimi siwapendi kabisa”
Juma alimuangalia mke wake alimuona anaongea tu bila ya kufikiria wala nini.
Walipomaliza kula tu walienda kulala ila Juma alijihisi vibaya sana kwa ile kauli ya mtoto wao kuwa aliwaambia ukweli wageni wao.
Usiku ule ule Juma alipigiwa simu na mama yake,
“Ndio mama”
“Kesho nakuhitaji nyumbani, nimemaliza”
Mama Juma alikata ile simu kisha Juma alimuangalia mke wake na kumwambia,
“Mmmh mama alivyoniita hata sijui kuna nini?”
“Aaaah na wewe humzoei tu mama yako, usikute hakuna hata jipya ila ni kawaida yake tu kupaniki”
Juma hapo hakutaka kuendelea kuongea bali aliamua kulala tu.

Leo, Mariam alikuwa amebaki na mtoto wake yani wawili tu ndani, basi yule mtoto akamwambia Mariam,
“Yani mama hivi ndio unapenda, unajisikia amani mwenyewe eeeh!!”
Mariam akapumua na kumletea huyu mtoto hoja nyingine,
“Inabidi tukupeleke shule wewe”
Mtoto akacheka na kumuuliza Mariam,
“Nina umri gani mama?”
“Umri wako sijui ila nahisi umri wako ulianza kuhesabiwa toka sijui inatungwa mimba maana hata sielewi”
Mtoto akaceheka tena na kumwambia Mariam,
“Inaonyesha mama huwa unanishangaa sana, huwa unaniona mimi wa ajabu sana lakini mama mimi sio wa ajabu kama unavyofikiria, nimepewa kipawa tu hiki cha kuongea mapema ndiomana ila mimi sio wa ajabu”
“Na mimi sijasema kuwa wewe ni wa ajabu ila nimesema kuwa inabidi uende shule”
“Nikafanye nini huko shule?”
“Ukasome”
“Niulize swali ambalo silijui halafu nikishindwa kujibu basi nitaenda kusoma”
“Mmmmh makubwa haya, ngoja nikuulize”
“Niulize”
“Bibi yako kamuitia kitu gani baba yako?”
Hapo mtoto akacheka tena na kumwambia mama yake,
“Nilijua ungeniuliza swali la maana kumbe swali hilo, anataka kumsema kwa kitendo chake cha kukataa wageni”
Hapo Mariam hakusema neno kwani alibaki akimuangalia tu huyu mtoto.

Juma akiwa kwa mama yake, ni kweli kabisa huyu mama alianza kumsema kwani aliambiwa yale mambo na shemeji yake kwahiyo alimsema sana Juma,
“Wewe tushakwambia mara nyingi, oa mwanamke mwingine hutaki, kumbe Mariam anatia aibu hadi kwa wanaume jamani!! Nilijua kwa sisi wanawake tu”
Juma alikuwa kimya akiendelea kumsikiliza mama yake,
“Haya nimekuita hapa nataka unijibu jibu moja tu, upo tayari kumuoa yule mwanamke tuliyekutafutia au haupo tayari?”
“Lakini mama…..!”
“Sitaki cha lakini, ninachohitaji ni jibu tu, mwanamke gani anatuletea uzao wa ajabu, amekaa na mimba miaka sijui mitatu huko, amezaa mtoto wa ajabu hadi hospitali hawamtaki, mtoto ana mambo ya ajabu anafyonya hovyo, kwasasa anaongea kama chiriku halafu unataka nini kwa mwanamke kama huyo Juma? Mwanamke kila sifa mbaya anayo”
“Ndio mama, kila sifa mbaya anayo ila nampenda Mariam mama, sababu Mariam ni mwanamke aliyetulia sana, toka nimuoe sijawahi kumsikia na kashfa yoyote ile, tofauti na yule ambaye nilimuoa kipindi kile, alikuwa na kashfa chafu mtaani na hadi kwenye ndoa lakini Mariam hana hayo mambo mama halafu nampenda sana na nimemzoea, siwezi kumuacha Mariam”
“Kwani nimekwambia umuache? Nimekwambia uoe mwanamke mwingine, hata kwa siri ila uwe na mke mwingine zaidi ya Mariam, anatutia aibu jamani. Halafu hiyo tabia ya kutokupenda wageni umeitoa wapi Juma? Huo ni uchoyo na mkeo ni mchoyo ndiomana hapendi wageni”
“Mama, kwenye sifa ya uchoyo mke wangu naomba umtoe maana sio mchoyo kabisa yule ila mke wangu ni mvivu na mara zote anajua wakija wageni lazima atahitajika kuwashughulikia ndiomana hapendi wageni”
Mama Juma alitikisa kichwa kama kumsikitikia mwanae kisha akamwambia,
“Ukisikia mtoto kapewa limbwata ndio hapa sasa, usikute ndugu wa Mariam wanakuja hapo, wanakula wanalala na hakuna tatizo ila ndugu zako ananuna na kuzimia”
“Hapana mama, hakuna ndugu wa Mariam ambaye huwa anakuja”
“Haya hatubishani, ukweli unaujua wewe ila siku isiyo na jina nakuja hapo kumpasha mke wako maana huu ni ujinga kabisa, nitampasha ukweli”
Hapo Juma hakutia neno lolote alimsikiliza tu mama yake maana hakuwa na jibu la aina yoyote kwa wakati ule na aliona kila anachoshutumiwa na mama yake ni cha kweli.
Baada ya hapo, Juma alimuaga mama yake kuwa anarudi nyumbani kwake ila kwa muda huu mama yake alimuomba Juma kwenda kumuona mwanamke ambaye walimtafutia ila Juma alikataa kabisa na kusema,
“Mama, mimi nampenda mke wangu, kwanini niende kumuona mwanamke mwingine? Kwangu mimi ni Mariam tu ndiye ninayemtaka”
Kisha Juma akaondoka zake kuelekea nyumbani kwake maana hakwenda hata kwenye shughuli zake kwani moja kwa moja alienda nyumbani kwake.

Leo Juma alimkuta mke wake akiandaa chakula cha usiku ila alikuwa akilalamika sana, basi ikabidi Juma aingilie kati kupika mwenyewe, Mariam akasema,
“Yani njaa inaniuma sana ila hakuna mpishi humu ndani, nateseka na njaa mimi nitafutie binti wa kazi bhana Juma”
“Je mwanao yupo tayari utafutiwe binti wa kazi?”
“Aaaah Juma ukimsikiliza huyo mtoto utaweza? Nitagutie binti wa kazi tafadhari, mimi siwezi peke yangu”
Juma alipika kile chakula na walienda kula, ila mtoto wao alikuwa akiwaangalia tu muda huu na wala hakusema kitu chochote kile.
Walipoenda kulala, bado Mariam alikuwa akimsisitiza jambo moja tu Juma kuwa amtafutie msichana wa kazi ila muda huo huo wa usiku Juma akapokea ujumbe toka kwa Pendo,
“Habari, mimi niliagiza mdada wa kazi toka kijijini ila sasa huyu kaniletea wadada wa kazi wawili na mimi namuhitaji mmoja tu. Kwahiyo kama ukisikia kuna mahali wanataka mdada wa kazi nishtue maana siwezi kuhudumia wawili”
Juma alitabasamu kwa ule ujumbe na kumwambia mke wake ambaye alifurahi sana na kumwambia Juma,
“Basi kesho nenda kamchukue huyo mdada wa kazi jamani”
“Sawa, hakuna tatizo ngoja nimjibu Pendo huu ujumbe maana labda katuma kwa wengi halafu wengine wakaniwahi”
Muda huo huo Juma akamtumia ujumbe Pendo kuwa huyo mdada wa kazi ataenda yeye kumchukua maana hata yeye ana shida na mdada wa kazi.
Mariam akafurahi sana maana alikuwa na uhitaji sana na mdada wa kazi.

Wakati Juma kajiandaa ili aelekee kwenye shughuli zake, Mariam alimkumbusha kuhusu huyo mdada wa kazi ili ikiwezekana amlete asubuhi hiyo, mtoto wao alikuwa pale sebleni na kusema,
“Yani mama umesahau kabisa mambo yote ya Anna, huna hata kumbukumbu hata kidogo!”
Mariam akajitetea pale,
“Anna ni tofauti na huyu tuliyeambiwa, maana huyu kaletwa kwa makosa kwahiyo hana pa kwenda anatufaa”
“Hivi umejiuliza lakini? Kwanini atake mdada mmoja aletewe wawili? Huyu mwingine hamuhitaji kwanini asingemrudisha au asingempa aliyemletea amrjudishe maana aliyeleta ndio akosea, kingine una shida na mdada wa kazi na kupokea huo ujumbe kuwa kuna mdada wa kazi kapatikana, huoni kama hapo unatafuta tatizo juu ya tatizo? Ilimradi mimi nipo humu ndani basi sitaki kumuona mdada yoyote wa kazi, sihitaji kabisa”
Mariam na Juma waliangaliana, kisha Juma aliondoka bila kuaga tena sababu aliona hapa huyu mtoto kaanza mambo yake yasiyoeleweka.

Walipokuwa kazini, Pendo anamuuliza Juma kuhusu mdada wa kazi maana alishawakatalia watu wengi tu sababu ya Juma kusema kuwa anamtaka huyo mdada wa kazi,
“Vipi Juma, utamchukua jioni hii eeeh!!”
“Mmmmh hapana, sihitaji tena”
“Sasa ndio nini Juma? Unajua nimekatalia wangapi kwaajili yako? Yani mambo ya Kiswahili huwa siyapendi kabisa”
Kisha Pendo akampigia simu mtu mwingine mwenye uhitaji na huyo mdada wa kazi, na alipomaliza kuongea na hiyo simu bado alimlalamikia Juma,
“Umeniangusha kweli Juma yani bora hata ungeniambia mapema kuliko hivi yani”
Juma hakuongea neno maana Juma huwa sio mshindani na wala huwa hawezi kujitetea kwahiyo mara nyingi akiona mtu anamjia juu huwa yeye anaamua tu kukaa kimya.

Muda huu Mariam akiwa ametulia baada ya kula chakula, alifika pale mama yake pamoja na mdogo wake Zayana, kwakweli alifurahi sana kuwaona na kuwakaribisha vizuri sana,
“Karibuni sana”
“Asante, leo tumekukumbuka Mariam”
“Nashukuru sana kwakweli maana hadi mmekuja ni hakika mmenikumbuka sana”
Kisha mama Mariam akaanza kumwambia Mariam kilichowaleta pale,
“Mwanangu, naomba umshauri mdogo wako huyu maana kapata mchumba na mchumba ameshajitambulisha na ameshatoa mahari yani hapa bado ndoa tu ila kaja kugundua kuwa yule mwanaume kuna mwanamke alikuwa akiishi nae na yule mwanamke amezaa nae watoto watatu ila mwanaume hakumwambia ukweli ni majirani tu ndio wamemwambia na Zayana amegundua kuwa yule mwanamke kaondoka kama siku tatu zilizopita inamaana kipindi chote cha kujitambulisha sijui mahari alikuwa yupo na yule mwanamke, naomba umshauri mdogo wako hapo sasa aendelee na ndoa au?”
“Duh! Kwani mama umemshauri vipi hapo?”
Zayana akajibu,
“Mama kaniambia kuwa niachane nae ila kasema kama ndio nimeandikiwa huyo ndio mume wangu inamaana kuwa sitakuja kuolewa, sasa ndio tukasema tuje kukusikiliza na wewe”
“Mmmmh ngoja niseme hivi siku ambayo Zayana uliniambia umepata mchumba yule mtoto wangu alisema nikwambie kuwa huyo mwanaume hakufai, na alichosema mwanangu ni kuwa huyo mwanaume ni mchawi”
Zayana alishtuka sana kusikia kuwa huyo mwanaume ni mchawi,
“Kheeee mbona mnanitisha jamani!”
“Sikutishi ndio hivyo”
“Kwahiyo katoto kako umekazoea sana siku hizi hadi unaongea nacho yote hayo?”
Mariam akacheka na kusema,
“Nimemzoea kiasi chake”
“Yuko wapi muda huu?”
“Amelala, siku hizi huwa na yeye analala mchana tofauti na zamani alikuwa akikodoa macho muda wote”
“Haya, nishauri hapo”
“Nikushauri nini? Achana nae huyo”
“Ila nina mimba tayari”
Hapo Mariam aliguna maana palikuwa pagumu zaidi na hakuwa na jibu zaidi basi mama Mariam akasema,
“Sasa Mariam naona na wewe una babaika, ngoja sisi twende”
“Aaaah hapana mama, msiende naomba leo mlale hapa halafu mtaenda kesho. Nitakuwa na jibu zuri sana nikiongea na Juma”
Mama Mariam na Zayana wakakubaliana kulala mahali pale ili waondoke kesho yake.

Usiku wa leo, Mariam anamsimulia Juma kuhusu mchumba ambaye mdogo wake amempata basi Juma anasema,
“Kama wanapendana waoane tu, sijaona tatizo hapa”
“Tatizo lipo, ni kwanini hakusema mapema ili mwanamke ajue kama yeye ni kimeo na kuna mwanamke alikuwa akiishi nae na ana watoto watatu?”
“Mmmmh naona aliogopa kusema mapema sababu hakutaka kumpoteza mdogo wako ndiomana”
“Mmmh ila mwanao kasema kuwa huyo mwanaume hamfai Zayana sababu huyo mwanaume ni mchawi”
Juma akacheka na kusema,
“Khaaaa hako katoto kenyewe ni kachawi, mbona sisi tunakavumilia humu ndani! Hebu aache watu waoane asituletee ujinga hapa”
“Sasa mdogo wangu aolewe na mwanaume mchawi kweli? Mmmmh naogopa yasije kumpata makubwa”
“Kwahiyo hiyo mimba utamshauri nini?”
“Nitamshauri aende kwa Anna akalale kule, najua kesho yake Anna atakuwa kamtoa hiyo mimba basi hakuna tatizo hapo”
“Yani Mariam kuna muda sijui huwa unafikiria vitu gani, sasa kwenda kutolewa mimba na mchawi Anna na kwenda kuishi na mwanaume huyo bora nini? Mwanaume kampenda huyo acha aishi nae tu”
“Hapana, sikubaliani na wewe kwa swala hilo”
Kilivyokucha tu Juma alienda kuongea na shemeji yake na kumpa ushauri ule ule ambao alikuwa akimwambia Mariam usiku, kwa upande mwingine Zayana alikubali na kwa upande mwingine alikataa kwani alikuwa anaona itamuwia ngumu sana kuishi na mwanaume ambaye wengi wamemuonya, basi Zayana akamwambia Juma,
“Lakini shemeji inasemekana kuwa mwanaume mwenyewe ni mchawi”
“Una uhakika gani kama huyo mwanaume ni mchawi maana naona una mashaka sana”
“Mmmmh shemeji sina uhakika”
“Sasa mbona useme ni mchawi?”
Muda huo mtoto nae akasogea kwenye maongezi yao na kumuuliza Juma,
“Baba una uhakika gani kama mimi ni mchawi?”

Itaendelea…..!!!
Kwa mawasiliano 0629980412 kuipata full nichek whatsapp kwa Tshs.500 tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom