Simulizi: Mke Wangu Juliana

Ahsante sana mkuu....arosto zilitupelekesha hatmaye tumemaliza
Sehemu ya 129

Stori ya maisha yake ikawa gumzo Kigoma nzima, hapakuwa na watu waliokuwa wakiamini kwamba yule kijana aliyekuwa akiishi kwenye maisha ya kimasikini, John alikuwa tajiri kama alivyokuwa.

Wapo waliokuwa wakibisha ambao walichukuliwa na kupelekwa mtaani kwake ambapo huko watu waliwajibu kwamba ni kweli kile walichokuwa wakikisikia ndicho kilikuwa ukweli wenyewe.

Wengi walibadilika, waliokuwa na dharau dhidi ya watu masikini wakaanza kuwaheshimu watu hao kwani waliamini kama mzee Masako ilimtokea yale yaliyomtokea basi kulikuwa na uwezekano hata wa kuwatokea wao.

Maisha yake yaliwabadilisha watu wengi. Vijana wengi wakajifunza, mabosi wakabadilika, masikini wakaheshimiwa. Kuanzia mwaka 2017 ambapo John alianza kuishi mkoani Kigoma, mpaka leo hii historia ya maisha yake ilibaki kuwa vichwani mwa watu wengi.

MWISHO.

Asanteni kwa kuwa nami toka mwanzo mpaka mwisho wa story hii na kuvumiliana na arosto za apa na pale

Mwisho wa story hii ndio mwanzo wa story nyingine nyemo chilongani na shunie tunawapenda sana

Tuendelee kumuunga kijana mkono kwa kununua vitabu vyake no ya simu hii 0718 069269 piga mda wowote
 
Back
Top Bottom