Simulizi: Mji tulivu ulionipa ugonjwa wa milele

Simulizi : Mji Tulivu Ulionipa Ugonjwa Wa Milele
Sehemu Ya Sita

Baada ya kupokea simu ile na kugundua kuwa mpigaji alikuwa ni yule mganga wa jadi na alikuwa ananieleza kuwa kuna jambo baya ambalo limemtokea mama kwa sababu yangu, nikajua wazi kuwa yawezekana kile kitendo cha kumshirikisha mama juu ya mambo yanayonikabili ndo chanzo cha wazi kabisa cha yeye kukumbwa na balaa lolote lililomkumba.

Lakini niliomba sana hilo balaa lisijekuwa eti ni kifo kwa mama yangu.
Nilimsihi sana yule mganga anieleze nini kimemsibu mama yangu, akanieleza kuwa mizimu imemchukua na itakuwa tayari kumrejesha ikiwa tu nitatimiza ahadi yangu, lakini vinginevyo nitakuwa nimemtoa mama yangu kafara.

Akanilaumu kuwa nimeikasilisha sana mizimu kwa kumshirikisha mama yangu juu ya jambo linaloendelea.
Damu ilichemka sana kusikia hivyo, nikaituliza akili yangu na kujiuliza ni kipi nitafanya.

Mama ndo mtu pekee ambaye alikuwa akinifariji hasahasa nikiwa nimezidiwa na mawazo kama hivyo, sasa naambiwa kuwa amechukuliwa na mizimu.
Licha ya kujaribu sana kuituliza akili bado nilikuwa katika mchecheto.

Nilichukua simu yangu na kumpigia mwanasheria wangu kumsihi anifanyie hima sana juu ya zile nyaraka za kuhakikisha kuwa hisa zimeuzwa.
“Joshua!” mwanasheria aliniita baada ya kuwa nimezungumza naye na kumsihi. Nikamuitikia, akanieleza kuwa kama ninaweza nionane naye usiku huohuo kuna maswali anahitaji kuniuliza ili aweze kukamilisha vizuri zile nyaraka bila dosari yoyote.

Laiti kama angekuwa ananiitia mambo mengine hata nisingeweza kwenda, lakini kwa sababu ilikuwa ni juu ya nyaraka zile muhimu niliamua kwenda.
Tukakutana katika mgahawa mmoja tulivu sana usiokuwa na kelele na vurugu za hapa na pale.

Yule mwanasheria ambaye kiumri alikuwa ananizidi alinitazama kwa muda bila kuuliza chochote, kisha akaniuliza kuhusu ndoa yangu kama imetulia na ni salama.
Nikamjibu kuwa kila kitu kipo sahihi kabisa.
“Joshua mdogo wangu, nahitaji tuzungumze kirafiki tafadhali usinijibu kana kwamba mimi ni adui yako.” Alinisihi kwa upole.

“Ndugu, niulize maswali juu ya mkataba na sio vinginevyo..” nilimfokea kidogo. Akatabasamu kisha akapiga funda moja la bia aliyokuwa amenunua kabla sijafika.
“Mkeo ana biashara gani anazofanya na Revo?” aliniuliza swali ambalo sikujua lilikuwa na mantiki ipi.

Sikumjibu na nilizidi kupagawa kwa sababu huyu bwana nilimwona akinipotezea muda wangu angali mimi nina tatizo kubwa sana.
Nilikuwa nahema juu juu huku hasira nazo zikichukua nafasi katika nafsi yangu, kitendo cha yule bwana kuzungumza juu ya mke wangu kikanifanya nikumbuke kuwa alikuwa ameniomba shilingi milioni nne na hadi wakati huo nilikuwa sijampatia na sikuwa na dalili hizo,

“Joshua… sina maana mbaya kukuuliza hivyo. Naomba tu unijibu.” Alinisihi.
Nilijitahidi hasira zangu zisije zikavuka mpaka na kumvunjia heshima yake.
Nikamjibu kuwa hakuna biashara yoyote kati ya mke wangu na Revo.
“Na unadhani kwa nini Revo aliuza hisa zake ghafla baada ya wewe kumtolea mahari Nyambura?”

Hili swali likanilainisha kidogo, ni swali ambalo kama jibu lake lingepatikana basi lilimaanisha kuwa kuna mahusiano kati ya Revo kuuza hisa zake na mahusiano yangu na Nyambura.
“We umewaona wapi Revo na Nyambura?” nikauliza, sasa nikirejea juu ya lile swali la kwanza Nyambura ana biashara gani anafanya na Revo.

Mwanasheria akanitajia mazingira ambayo amewahi kuwaona Nyambura na Revo akauelezea uhusiano baina yao tangu niliposafiri na unavyoendelea hadi wakati huu ambao nina matatizo.
“Unavyosema juzi umewaona, unamaanisha juzi kabla hajajifungua mtoto ama akiwa na mtoto?” nilimuuliza kwa namna fulani ya kumsuta uongo nikijifanya namuamini sana Nyambura wangu.

“Juzi katika maana halisi ya juzi, na hakuwa na mtoto, si mara moja wala mara mbili.. nadhani ni mara tatu. Wanakutana katika baa fulani iliyojificha mtaani kwetu… ni baa ambayo huwa napenda kujificha hapo nakunywa bia kwa amani kuliko kwingine ambapo nitasumbuliwa na marafiki wapenda ofa.” Alinijibu kwa utulivu sana huku akijiamini mno.

Sasa sikuwa na hasira tena bali wingi wa maswali pasi na majibu.
“Kwa hiyo kaka unadhani wanafanya biashara gani?” nilijikuta natokwa na swali la kipuuzi.
Akatabasamu kisha akapiga funda moja la kinywaji chake.

Hakunijibu!!
“Huwa wanakuwa watatu wakati mwingine wanne, sidhani kama ni biashara ndogo. Ila we si ulinambia mkeo anafanya biashara?? Labda ndo hiyo?”
“Hapana, hawezi kufanya biashara na Revo halafu asinishirikishe, anaujua urafiki wetu vyema, na Revo hawezi kuacha kunishirikisha juu ya hilo.” Nilipinga.

“Unaonyesha unapenda sana kuamini kwa asilimia mia eeh!” alihoji kwa kebehi kiasi fulani. Nikagundua alichomaanisha.
“Siwezi kujua anyway, ila nimeona tu nikushirikishe kama mdogo wangu, uzuri ni kwamba ukimwambia mkeo kisha akanichukia atakuwa anamchukia mtu ambaye hamjui na hata Revo akijua nimekwambia akachukia haitafaa chochote maana sisi wanasheria tunachukiwa sana na tunapendwa vilevile, mimi ni mwanasheria wako!” alimaliza akapiga funda moja la mwisho na kutaka kunyanyuka. Nikamsihi asiondoke.
Nilikuwa nahitaji sana kusikia zaidi kutoka kwake.

Yaani kwa ufupi nilikuwa hoi kimawazo, huku nawaza juu ya mizimu na upande wa pili nikiwaza kuwa eti yawezekana mke wangu ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu wa karibu kiasi kile??
“Kaka tafadhali naomba uniambie basi unahisi kuna nini ukiniacha hivi kaka nitagongwa na gari mimi,

nimechanganyikiwa kaka yaani kuna mambo yananiendea kombo kiasi kwamba ninajiona nina kitu kama jini la mitihani nimetupiwa…” nilimsihi
“Kwani unahisi mkeo anaweza kujihusisha kimapenzi na Revo ama alikuwa akijihusisha naye hapo kabla hujamuoa ama?” alinihoji,

wakati huohuo akampungia muhudumu mkono na kuongeza kinywaji kingine.
Nikafarijika kuwa ataendelea kubaki zaidi.
“Kaka, sina walau hata hisia potofu kidogo tu dhidi ya mke wangu, nimekuwa naye kiuaminifu sana na ninaamini ananipenda.” Nilimjibu nikiwa namaanisha.

“Aisee! Umesema kuwa huwa anasafiri mara kwa mara kwa shughuli zake za kibiashara, je? Umewahi kufuatilia walau tiketi za mabasi na ndege ambazo anatumia?”
Lile lilikuwa swali zito sana na nikajiona ni mzembe sana kutofuatilia nyendo za mke wangu eti kisa tu naamini kuwa ananipenda.

“Haya basi nambie na wewe ni kwanini unauza hisa za kampuni, tena unauza zote tisini, unayemuuzia simjui unanilazimisha tu kuandaa makubaliano. Joshua ni nani anayekulazimisha kuuza hisa zako najua hauuzi kwa hiari yako mwenyewe… ni mkeo ama?” alipouliza vile akanikazia macho yake nikakosa ujasiri wa kuendelea kumtazama.

Nafsi ilikuwa inanisuta.
Nilikosa cha kujibu. Nilitamani kumweleza ukweli lakini kwa yaliyomtokea mama yangu. Nilihofia kuyakuza zaidi nikimsimulia na mwanasheria.
“Kesho makubaliano yatakuwa tayari, kumbuka kama unanidanganya mimi unajidanganya mwenyewe.

Mimi ni mwanasheria mteja wangu akiniongopea balaa huja kwake si kwangu…”
Alimalizia maneno yale kisha akainuka na kuondoka zake hata bia yake hakuimalizia.

Maneno ya mwanasheria wangu yalikuwa yameniletea ugonjwa mpya uitwao mashaka, nilikosa kujiamini… nikimtazama mke wangu machoni namwona asiyekuwa na hatia lakini busara za mwanasheria nazo zilikuwa na makali yake katika upande wa kuishtua akili yangu.

Usiku huu niliporejea nyumbani nikawa namuwaza mke wangu, namuwaza rafiki yangu Revo, namuwaza mwanasheria na maneno yake lakini zito zaidi nikimuwaza mama yangu mikononi mwa ile mizimu inayotaka kuimiliki kampuni yangu na kila kitu kilichomo.
Niliyafumba macho yangu, nikaanza kulijengea picha wazo la kwanza.

Nyambura na Revo!
Nikafikiria jinsi ambavyo huwa tunacheza bafuni huku tukiyaacha maji yamwagike pasi na jambo la msingi. Ananigusa huku nami namgusa kule.
Nikajitoa pale bafuni kisha nikamuweka Revo.

Yaani Revo naye anamgeuza nyuma Wambura na kumuuliza hii alama hapa mgongoni ulikuwaje?
Nilijiuliza huku nikipambana kuidhibiti ghadhabu yangu.

Lakini si ana mke kabisa Revo! Halafu mkewe mrembo haswa kuliko hata huyu Nyambura, sasa kama wana mahusiano kweli… kampendea nini?
Nilizidi kuumia kichwa nikiyakosa majibu kabisa.

Nikiwa ningali katika mawazo mazito kabisa, Nyambura mke wangu akanitikisa nakuniambia kuwa kuna mambo kadhaa anahitaji kuzungumza na mimi.

Nilimweleza kama inawezekana tuzungumze asubuhi akakataa akasema ni lazima iwe usiku uleule!
Nikakubali japokuwa niliamini kuwa sikuwa tayari kumsikiliza kwa umakini.

Akaanza kwa kunikumbusha juu ya zile pesa alizoomba nimsaidie kuweka kwenye nambari aliyonipatia, nikazuga kushtuka na kumtaka radhi kuwa nilisahau.

“Sawa achana na hilo, nahitaji kuzungumza juu ya mama.” Akasema kisha akasita.
Ile kutaja jina mama, moyo wangu ukalipuka vibaya sana. Nikaingiwa na ganzi na ubaridi ukitambaa katika mwili wangu.
“Nilizungumza na mama kabla hajaondoka!” akaweka mkato tena, kisha akaendelea, “Kwanini umemfukuza mama?” akanirushia swali la ghafla.

“Nani? Mimi?” nikatokwa na swali la kizembe. Nyambura hakusema kitu akaniacha nibabaike.
“Mimi nimemfukuza mama? Nani kakwambia? Ni mama kakwambia mi nimemfukluza?” nikabaki kujiuliza na kujipa majibu katika namna ya kutaharuki.
“Baba Agness…” akaniita kwa utulivu, akaendelea baada ya mimi kuitika,

“Ulinieleza kuhusu historia yako, na mama pia alinieleza juu ya hilo. Leo hii umekuwa mtu mzima unamficha mama mambo yako, mimi je? Si ndio utaniua kabisa kwa kunificha siri zako?” aliuliza katika namna ya kulalamika.
Nilikuwa nimekamatika!
“Tazama! Unadhani sikuoni unavyokonda kila siku, unadhani sioni kuwa hauna raha wala amani? Nayaona yote haya….

Lakini mimi ni uchafu tu mbele yako, hata nikiuliza najua hautanijibu, kama mama yako mzazi umemkatalia katakata je mimi mpita njia!” aliendelea kulaumu, sasa alikuwa amejinyanyua na kuegemea mkono wake akinitazama vizuri.
“Ni nini chanzo cha kuapa kanisani kuwa sasa mimi ni ubavu wako rasmi, nakuaje ubavu wako! Nakuaje kiungo katika mwili wako ikiwa siyajui maumivu yako? Sijui hisia zako… sijui unachopitia!!” alishindwa kuendelea sasa machozi yakaanza kumtiririka.

Looh! Nilichanganyikiwa kupita awali, nikaanza kumbembeleza lakini Nyambura katukatu hakutaka kunisikia.
“Joshua! Nalala sebuleni, naomba usinifuate huko, na kesho usiku nitalala kitandani ikiwa tu aidha mama amerejea hapa! Au utanipa nafasi mimi kama mke wako kujua nini unapitia… la sivyo! La sivyo Joshua …..” akaiacha hewa sentensi yake akaondoka zake.

Kama ni mpambano wa masumbwi, nilikuwa nimepigwa ngumi mfululizo nazipangua halafu nikajisahau nikatoa mikono na nikaingizwa pigo moja mahususi liitwalo ‘uppercut’, huu ni mtindo wa ngumi ambapo mpinzani wako anaikunja ngumi yake na kisha anairusha kwa kutokea chini inatua katika kidevu chako.

Pigo hili linaweza kuvunja taya ya mlengwa!
Nami nilivunjwa vibaya, nikabaki kama tahira kitandani.
Moyo wa kike ukanivaa, nikaanza kulia kana kwamba nimefiwa!
Ama! Yalikuwa yamenifika Joshua mimi.

JIFUNZE!
KATIKA mahusiano ya kimapenzi, hususani ndoa. Mahusiano mengi huanza katika namna sahihi kabisa ya tatu jumlisha tatu jibu ni sita, lakini kuna nyakati katika ndoa mahesabu hayo hubadilika, mmoja ataiona ile sita ni tisa na mwingine ataiona sita ni sita. Na kila mmoja akiamini kuwa yupo sahihi!
Ni hapa FUKUTO huanzia!

ITAENDELEA...
Sehemu Ya 7

Asubuhi ilipowadia Nyambura alikuwa ameninunia na hata hakunisalimia wala kunibusu kama ilivyokuwa kawaida yake siku zote.
Na macho yake yalikuwa yamevimba sana.
Bila shaka alilia usiku kucha!
Niliondoka pale nikiwa sina la kufanya,

niliona uamuzi sahihi wa kuniweka mimi salama ni kuwapa mizimu kile walichokuwa wanahitaji ili mama yangu aweze kurejea salama mikononi mwangu. Kwani kwa kitendo cha mama kuonekana tu basi Nyambura naye angetabasamu na kunielewa.

Siku iliyofuata nikiwa tayari na zile nyaraka muhimu, nilienda hadi kwa yule mganga nikampatia na kumweleza kuwa kila kitu sasa kipo tayari ila watatakiwa kufanya uhakiki wa kisheria ili ile kampuni iwe yao.
Nikaongezea kuwa wafanyakazi sijawaambia jambo lolote ili kutoyumbisha utendaji kazi wao, mganga akapokea ile hati ya umiliki na kunieleza kuwa ataiwasilisha kwa wazee yaani mizimu.

“Lakini masuala ya kibenki hamna namna lazima tukabidhiane benki hukohuko sasa hii itakuwaje? Mizimu itafika benki?” nilimuuliza yule mganga.
Swali langu likamshtua sana hadi mi mwenyewe nikafahamu kuwa amebabaika. Akajirekebisha baada ya muda kidogo kwa kuanza kuchekacheka.

Akanieleza kuwa mizimu haishindwi kitu, atawasilisha kisha majibu atanieleza kwenye simu.
“Vipi kuhusu mama yangu sasa…” nilihoji jambo lile la msingi ambalo nd’o lilinisukuma kumlazimisha mwanasheria kufanya kila awezalo kampuni itolewe katika umiliki wangu kwa asilimia tisini.

Niliondoka kwa yule mganga kichwa chini mikono nyuma, kila hatua niliyopiga nilikuwa nakumbuka jinsi nilivyotokwa jasho hadi kufanikiwa kuimiliki ile kampuni. Nikafikiria ni mara ngapi nilianguka na kuinuka tena, watu wangapi waliniunga mkono hadi kufanikiwa kuifungua ile kampuni.

Niliyakumbuka majibu ya mkato niliyokuwa napewa pale BRELA (Ofisi inayohusika na usajili wa makampuni), lakini bado nilikuwa mnyonge na kufuata walichohitaji.
Hata pesa ya mtaji haikuwa inajitosheleza, tukahangaika na Revo hadi tukalikamilisha lile jambo ambalo liliniacha nikiwa na uzito wa kilo hamsini na tano kutokea sitini na nne nilizokuwanazo.

Halafu leo hii napoteza kila kitu kwa mkupuo.
Sasa sina kampuni tena!
Nilijiweka pembeni ya barabara na kuanza kulia bila kukoma. Nililia huku nikikumbuka kumlaumu Mungu kwa kunipa mitihani mikubwa kuliko uwezo wangu wa kuitatua.
Nililia sana mpenzi msikilizaji….

Na ninakusihi hata wewe ukikabiliwa na tatizo.. usijikaze jiweke mahali na ulie kwa kiasi utakachohisi nafuu.
Kilio ni tiba, hupunguza msongo wa mawazo mwilini na kulifanya tatizo kubwa lililopo walau lipungue makali.

Nilifika nyumbani, tofauti na ilivyo kawaida sikumkuta mke wangu nyumbani, haikuwa tarehe ya kumpeleka mtoto kliniki labda ningeweza kusema ameenda hospitali.
Ameenda wapi sasa? Nilijiuliza huku nikijilaza kitandani.

nikiwa nasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa, nikapokea simu kutoka kwa mwanasheria wangu.
“Acha nionekane mnafiki na mchonganishi lakini kama mbele ya Mungu nitapata thawabu kwa kukueleza ukweli mdogo wangu basi acha niabike duniani.” Alianza kuzungumza bila hata kunipa salamu.
“Kulikoni kaka…” nilimuuliza kinyonge.

“Nipo hapa nakunywa bia.. mkeo na wenzake wana kikao kidogo sijui ndo kikao cha biashara?” aliniuliza katika namna ya kunisanifu.
“Wapo wawili tu leo, yupo na mfanyabiashara mpya kabisa sijawahi kumuona…. Kutana nami jioni nikupe swali moja ambalo mimi sina majibu wewe ndo unayo. Ila akirudi nyumbani usimuulize sana juu ya alikuwa wapi….

Aisee mkeo kiboko yaani ana mtoto mdogo ila bado anapiga bia kama maji!!” alizidi kunichanganya mwanasheria.
Akamaliza akaniaga na kukata simu, sasa kichwa kilikuwa katika maumivu makali kupita maumivu yote niliyowahi kupitia.
Yaani mke wangu ninayemuamini kupita wanawake wengine duniani ukimweka kando mama yangu, leo hii kuna hila anafanya juu yangu…. Yaani yawezekana ananisaliti?

Nilihamanika vibaya mno. Nikaenda kujitazama kwenye kioo na kushuhudia macho yangu yakiwa mekundu sana.
Nilitambua wazi kuwa mke wangu akinikuta pale nyumbani kisha nikamuuliza swali lolote halafu akaniongopea basi naweza kujikuta nambamiza vibaya sana.
Nilikuwa katika kiwango cha juu kabisa cha ghadhabu! Na nisingeweza kujiongoza kwa namna yoyote ile.

Naweza kuua! Niliwaza.
Nikaamua kuondoka pale nyumbani hadi jioni kabisa nilipokwenda kukutana na mwanasheria.
Kabla sijafika kwa mwanasheria nikapigiwa simu na yule mganga, akanieleza kuwa hakuna muda wa kupoteza mizimu imemtuma mtu wao ambaye wamemvika ubinadamu atafika kwa ajili ya kukamilisha taratibu zilizobaki kisheria ili kampuni iwe mikononi mwa mizimu.

Mganga akanisisitiza kuwa natakiwa kuacha chochote ambacho nilikuwa nafanya na wakati huohuo niende Posta maeneo ya City Garden kwa ajili ya kukutana na wajumbe kutoka kambi ya mizimu.

Maneno yale yakanifanya nikabadili uelekeo na kwenda Posta kukutana na wajumbe ambao mganga alinielekeza kuwa walikuwa wamevaa nguo nyeupe wote aina ya suti.
Hivyo nilipofika tu niliwaona, nikaenda hadi walipo.
Walikuwa wanazungumza Kiswahili kibovu kabisa chenye lafudhi ya kongo, waliniuliza maswali kadhaa nami nikawajibu, nilipotakiwa kuweka sahihi yangu nikaweka.

Kisha wakanitaka wakati uleule niwapeleke ilipo kampuni yangu, nikatii.
Tukaongozana hadi ofisini.
Wakatazama nyaraka kadha wa kadha, kisha wakanieleza kuwa mizimu imewaagiza kunielekeza ni wapi mama yangu mzazi alipo.

Wananipa maelekezo mara moja na nitatakiwa kufanya utekelezaji mara moja.
Wakanieleza kuwa ninatakiwa kusafiri hadi katika wilaya ya Tunduma mkoani Mbeya, niende hadi mpaka wa Tanzania na Zambia na huko nitakabidhiwa mama yangu akiwa hai kabisa na baada ya hapo nitaendelea na maisha yangu.

Hakuna nilichopinga, kwanza nilikuwa ninawaogopa sana na pili nilitaka haya mambo yaishe upesi niendelee na maisha yangu hata kama ni ya kimasikini lakini sio ya mashaka kwa kiwango hicho.
Wakati mmoja akinipa maelekezo yale, mwingine alikuwa amekalia kiti ambacho nilikuwa nakikalia mimi kama mkurugenzi mtendaji wa kampuni. Alikuwa anazunguka kwa kujinafasi.

Anajinafasi katika mali niliyoichuma kwa jasho sana.
Ningefanya nini?
“Hiyo gari unayoendesha sio ya kampuni?” aliniuliza na lafudhi yake ileile.
Nikatikisa kichwa kukataa na kudai kuwa ni mali yangu.
Wakacheka na kunong’onezana. Sijui hata walisema nini.

“Tukitoka hapa tunaenda benki, utatoa pesa yote kama ilivyo katika akaunti, pesa hiyo itapelekwa kwa mizimu kwa ajili ya kubarikiwa kisha itarudishwa kwenye akaunti…” walinielekeza.
Nikatii!
Wakati tunatoka ilikuelekea benki, simu yangu ikaita.

Alikuwa ni mke wangu ananipigia.
Ile kuliona jina la mke wangu, mapigo yangu ya moyo yakapiga vibaya mno nikawa nimekumbuka na ujumbe kutoka kwa mwanasheria juu ya mke wangu kuonekana mahali akiwa anakunywa pombe huku akiwa na mtoto. Nilitaka kuipuuzia kwa sababu nilikuwa naendesha gari lakini hakuacha kupiga alifanya hivyo tena.

Alipopiga kwa mara ya tatu nikapokea kwa sababu nilijua kuna tatizo, mke wangu si mtu wa kupiga simu zaidi ya mara mbili na kuendelea kupiga tu hata isipopokelewa.
Nikaipokea na kumsikiliza.
“Baba Agness mume wangu upo wapi?” aliniuliza huku sauti yake ikisikika kama mtu ambaye anakaribia kulia.

“Naendesha gari naelekea posta Kariakoo mara moja, vipi?” nilimjibu huku nikiwa makini barabarani.
“Nahitaji kukuona sasa hivi!” aliniambia bila kuongeza neno.
“Dah! Nyambura, kuna jambo la kiofi…”
“Hakuna cha jambo la kiofisi, muda huu nahitaji kukuona kisha utaendelea na jambo hilo. Waambie watu unaoenda kuwafanyia hilo jambo kuwa unahitaji kuonana na mkeo kwanza.” Alinisihi na kuzidi kunichanganya. Hawa watu wametumwa na mizimu, na mizimu inamshikilia mama yangu, sasa inakuwaje niwape kero nyingine? Je wakimuua mama yangu?

Mama anayenipenda kuliko huyu Nyambura anayenisaliti kwa kushiriki mapenzi na rafiki yangu Revo!
Nilijiuliza kisha nikaweka katika mzani na kuchukua maamuzi.
Sitaenda kwa mke wangu, nitamalizana na hawa watu kwanza kwa masilahi ya mama yangu.

“Nyambura nitaonana nawe baada ya dakika arobaini tafadhali.” Nilimsihi na kukata simu.
Hakupiga tena!
Tulifika hadi benki, wao wakaketi mahali pa kusubiria huduma, mimi nikapanga foleni kuelekea katika dirisha tayari kwa kuzichota zile pesa, nilikuwa natetemeka sana nilipofikiria milioni mia moja na sabini inaweza kufanya nini katika maisha ya kawaida tu.

Nikatambua kuwa ni pesa nyingi sana naenda kuzipoteza kwa sababu ya ujinga wangu tu wa kuupinga utendaji kazi wa Mungu na kuamua kuingiza mambo ya waganga wa jadi katika ndoa yangu.
Walikuwa wamebaki watu watano kabla haijawa zamu yangu kuchota pesa.
Mwanamke mwenye baibui akasimama pembeni yangu, alikuwa amejiziba hadi usoni yakabaki macho tu.

“Samahani!” alisema kwa sauti ya chini. Sikuju kama anasema na mimi.
“Samahani Joshua.” Sasa alinitaja, nikageuka kwa mashaka.
“Noo! Usinitazame we angalia mbele tu….. naomba uje hapa uwe kama unanisaidia kujaza hii fomu. Kuna ujumbe wako muhimu tafadhali nakuomba..” alinisihi. Sikushawishika, nilijua ni mizimu inanipima.

“Joshua njoo, ni ujumbe kutoka kwa mke wako.” Aliposema vile moyo ukapiga kwa nguvu. Nikaamua kuthubutu nikaenda alipohitaji niende.
Akawa anajaza fomu ya kuomba mkopo kwa kuzuga.
“Mke wako amesema usifanye lolote lile unalotaka kufanya, nenda ukaonane naye kwanza.

Tafuta sababu yoyote ile ambayo itasababisha usifanye unalopaswa kufanya… zingatia ni mkeo amesema. Yule pale nje katika pikipiki.” Akamalizia kwa kuniambia uelekeo alipo mke wangu, nikageuka na kutazama.
Kweli alikuwa ni mama Agy akiwa na Agy mgongoni!
Nilipagawa sana na kujiuliza ni nini hiki kinatokea katika maisha yangu.

Hadi nafika dirishani na kukabidhi matakwa yangu kwa muhudumu bado sikujua lipi nifanye ama lipi nisifanye.
nilipomkabidhi na kuanza kuishughulikia alinitazama na kuniuliza kuwa ni kwanini nimeamua kutoa pesa zote. Nilimtazama sikumjibu!
Akafanya alichostahili kufanya.
Nikasema pesa ni makaratasi acha wazichukue wanipe mama yangu!
Nikakabidhiwa kiasi kile...

Lakini sikutoka ndani ya benki salama bin salmini kabla hakijazuka kizaazaa cha funga na fungua mwaka!

*************
Nyambura aliendelea kulia nilipomkaribia kumuuliza alinisukuma na kudai kuwa nikae mbali naye.
Kwa sababu na mimi nilikuwa nimepagawa nilirejea katika kochi, nikatulia.
Akalia hadi aliponyamaza.

Akamuita yule mwanadada anayeitwa Mariam Sumra!
Akamnong’oneza huku akipambana na kwikwi za kilio.
“Amesema si hapa labda pengine!” alinieleza, kitu alichosema sikukielewa kabisa.

“Nani? Aah! Mbona mnanichanganya jamani!” nililalamika.
Nyambura akamuita tena kwa ishara, mwanadada akaenda kwa unyenyekevu kabisa. Akanong’ona tena..
Yule dada akaomba maelekezo zaidi, alipoelewa akaondoka kuelekea jikoni.
Aliporejea alikuwa ana chupa ya mvinyo katika mkono wake mmoja na mkono mmoja akiwa na glasi.

Alifikisha hadi kwa Nyambura!
Nikazubaa, sikuwahi kumwona nyambura akinywa kilevi cha aina yoyote ile… kulikoni leo anakunywa mvinyo.
Dada yule alipotaka kummiminia katika glasi Nyambura akakataa…

Akaishika chupa na kuanza kuigida kwa fujo hadi yule dada akawahi kumpokonya ile chupa.
“Nyambura inatosha mama… inatosha….” Alimsihi huku akimzuia kuendelea kunywa.
Nyambura akasimama ghafla, akaichukua ile glasi na kuirusha ukutani ikapasuka vipande vipande.

Ebwana eeh! Nilichachawa nikahisi Nyambura anakumbwa na wendawazimu mbele yangu…..
Nilitaka kumkabili nimzuie lakini yule mwanamama akanizuia, akanisihi nikae kuwa kila kitu atamaliza.
“Tuondoke hapa!” Nyambura akamweleza Mariam Sumra!

“Ni wapi sasa unapendelea…. Tafadhali kuwa mtulivu Nyambura, tulia kila kitu kitakuwa sawa kama nilivyokueleza hapo kabla. Nakuomba sana uniamini, niamini Nyambura!” Mariam alimsihi kwa nidhamu ya hali ya juu. Hakujishughulisha kabisa na ile glasi iliyopasuka vipande vipande.
“Twende ofisini kwangu!” Nyambura alitoa maelekezo.

Mariam akanigeukia na kunitazama kama nimesikia alichosema Nyambura.
Nikawa kama msukule nikafuata kile kinachotakiwa hata nisijue nini kinaendelea.
Tulimchukua Agness aliyekuwa amelala bado, tukaingia garini na kuondoka.
Moja kwa moja hadi ofisini, hapo tayari giza lilikuwa limeingia.

Nyambura akachagua twende katika ofisi yangu!
Tukaenda, nikataka kuketi katika kiti cha wageni akanizuia na kunisihi nikalie kiti changui.
Nilipoketi akazungumza.

“Nakupenda sana Joshua. Nafsi yangu inajua, mwili wangu unajua, na ulimi wangu haudanganyi!”
Akasita, chozi likamtoka!
Mariam akawahi kumpatia kitambaa, Nyambura akakikataa.

Sasa alikuwa anayumbayumba kiasi, bila shaka sasa pombe zilikuwa zimeanza kukikung’uta. Akaketi na kunitazama kwa muda.
“Je unaweza kuzungumza sasa….” Mariam alimuhoji Nyambura.
“Na wewe upo tayari kusikiliza?” naye Nyambura akanihoji mimi ghafla, nikatikisa kichwa kukubali.

Wakati wote huu nilikuwa najiuliza kuwa inamaana Nyambura amejua kila kitu nilichokuwa nafanya, kuhusu kwenda kwa mganga na mengineyo ya kutaka kuwamilikisha kampuni yangu ikiwa ni makubaliano kwa kunipa mtoto.
Wazo hili lilinifanya nijisikie aibu na kukosa ujasiri wa kufanya lolote lile.

Sikuwa najiamini, hivyo nikabaki kuwa msikilizaji tu.
Nyambura akasimama na kufika ukutani, akaigusa kalenda huku akitembeza kidole chake hadi akaifikia tarehe aliyoihitaji.
Tarehe kumi na tano!
Akaitaja kisha akanigeukia.

Akanitazama kwa jicho kali.
“Joshu…a… Na.. nakup..en..nda!” akabwabwaja maneno haya huku mwili wake ukilainika na kutua chini kama mzigo hakuna aliyewahi kumdaka.
Hapo sasa ikawa hekaheka tena.
Hekaheka ya kumpepea Nyambura, lakini hakuna kilichosaidia.

Tukalazimika kumuwahisha hospitali.
“Alikuwa anataka kusema nini?” nilimuuliza Mariam ambaye kwa mara nyingine alikuwa akiendesha ile gari.
Mariam akadai kuwa anachotaka kukisema Nyambura anakijua yeye mwenyewe Nyambura.
Jibu lake lilinivuruga sana.

“Na wewe ni nani hasa, maana sielewi.”
“Mimi ni Mariam Sumra, nielewe hivyo.” Alinijibu kwa mkato huku akiongeza umakini barabarani.
Safari ya kumpeleka Nyambura hospitali.
Wakati safari inaendelea, simu yangu iliita.

Kutazama ilikuwa nambari mpya,
nikapokea upesiupesi nikitarajia kuwa watakuwa wale wavaa nguo nyeupe wanataka kunipa maelezo mengine, nami nilikuwa tayari kujitetea.
“Joshua mwanangu, haujambo!” ilikuwa ni sauti ya mama yangu mzazi.
Nilipagawa sana.

“Mama.. mama upo wapi? Upo wapi mama?” nilimuuliza.
“Nipo Morogoro ila sijui panaitwaje hapa hata. Nimeazima simu ya mtu tu, naomba umtumie pesa humu nifanye nauli kurudi Dar es salaam Joshua! Yaliyonikuta ni makubwa…” alizungumza mama kwa sauti iliyotia huruma sana. Nilimjua mama yangu vyema ni mtu wa kujikaza lakini hadi kuongea kama anavyoongea basi kuna jambo zito.

Mwili ukaingiwa ganzi.
Nikamsihi abaki na ile simu nampigia kumpa maelekezo zaidi.
Nilipokata simu nikaanza kupambana kutafuta majina katika simu yangu, nilikuwa nimechanganyikiwa sana nisijue ni jina la nani natafuta.

“Nani huyo mama? Au!” aliniuliza yule binti bila kuonyesha kushtuka.
Nikamjibu ndiye.
“Mchezo unaelekea ukingoni.” Akazungumza kwa sauti ya chini.
“Mchezo? Mchezo gani?” nilimuuliza.
“Mtumie mama anachotaka umtumie….” Alijibu kitu kingine.

Wakati nazama katika taharuki mpya, akamalizia kunijibu.
“Kila kitu anajua Nyambura sio mimi.”
“Na mama anasema yupo Morogoro, wakati walisema yupo Zambia sijui.” Nilijiuliza huku nikihisi kuna mchezo nachezewa.

“Joshua hizi nyakati huwa haziepukiki, nyakati za kugeuzwa gunia!”
“Gunia?”, “Gunia kivipi?”
“Kila mmoja anakufanyia mazoezi, kila mmoja anakupiga na wala hauwezi kurusha ngumi hata moja. Kwani gunia linapenda kufanywa vile?” alinijaza katika fumbo nikashindwa kuelewa maana yake ya moja kwa moja.

Nilipojaribu kupiga simu ambayo awali mama aliitumia haikuwa inapatikana tena.
Huku mama hapatikani, na miguuni mwangu Nyambura akiwa amepoteza fahamu.
Haya yakiwa hayajanichanganya vizuri, Agness akaamka na kuanza kulia kilio kitakatifu!
Bila shaka alikuwa akihitaji titi la mama yake.

Muunganiko wa haya mambo ukanifanya nami niaanze kulia kama mtoto mdogo tena.
“Acha ujinga Joshua! Bembeleza mtoto….” Mariam Sumra mwenye tabia nisizozielewa alinipa kauli iliyonitikisa.
Mbona kama naye ananigeuza gunia!? Nilijiuliza.

Nikataka kumkaripia lakini nikaona ni heri niendelee kumbembeleza mwanangu.
Kadri safari ilivyokuwa ndefu nikaanza kugundua jambo jingine lisilokuwa la kawaida hata kidogo.
Hapakuwa na safari ya kuelekea hospitali, tulikuwa tunaelekea mahali nisipopajua kabisa.
Kwanini tuelekee huku!
“Mariam Sumra! Ni wapi tunaelekea?” nilimuuliza.

“Mbembeleze mtoto Joshua…. Acha upuuzi.” Alinijibu.
Nadhani jibu lake lilizua kimya ambacho hata Agness mtoto wangu alikigundua, akanyamaza kimya ghafla!
Hali ilikuwa tete!!

ITAENDELEA
 
Sehemu Ya 8

_____
KAMA nilivyohisi kuwa hakuna safari ya hospitali ilikuwa hivyo, hatukwenda hospitali badala yake gari lilisimama mbele ya nyumba fulani ya kifahari. Honi ikapigwa na geti likafunguliwa…

Gari lilipoingia tu, Nyambura akajigeuza.
Mariam Sumra akachukua maji na kumwagia, fahamu zikarejea akiwa anapepesa macho huku na kule.
“Mtoto wangu yupo wapi?” akaulizia, lakini kabla sijamjibu tayari Aggy alisikia sauti ya mama yake akaanza upya kulia.
Nyambura akamchukua na kumpa alichohitaji.

Titi akanyonya!
“Nyambura hili jambo linatakiwa kumalizika sasa!” Mariam alimsihi.
“Asante kwa kuja katika maisha yangu kwa wakati sahihi dada Mariam. Nadhani machache umejionea na kuyasikia..” alizungumza huku akimlaza Aggy ambaye tayari usingizi ulikuwa umempitia.
Wakati huo tulikuwa katika sebule iliyosheheni samani za kutosha.

“Umemsikia vizuri Joshua ambaye hadi sasa anamlilia mama yake na kukonda kwa sababu yake… Joshua mbinafsi asiyebadilika tabia yake.” Alizungumza tena kwa sauti ya chini akiwa anatazama dari.

“Dada Mariam, aliyekutuma uje katika maisha yangu awali nilimchukia lakini sasa natamani kumuona najisikia kwa mbali naanza kuwa mwanamke!” aliweka kituo na kunitazama. Hapo sielewi lolote lile.
“Nafsi yangu haitachoka kukiri kuwa ninampenda sana mume wangu na baba halali wa mtoto wangu wa pekee Agness.” Akakohoa kidogo na kuendelea, “Lakini bila ujio wako dada Mariam nisingejali kama ninampenda ama la.

Alichotakiwa kupata alistahili….. nadhani nilikwambia kuwa mambo mengine sitakueleza wewe pekee bali nitakueleza siku moja mbele ya mume wangu na siku hii ni leo.”
Nikaketi vizuri kusikiliza hukumu niliyotaka kusomewa ambayo ingenipa mwangaza wa haya niliyokuwa napitia.

“Ni tarehe kama ya leo, tarehe ambayo ilinifanya nianze kumchukia Joshua….. hii tarehe mama yangu mzazi aliaga dunia. Sitabadili msimamo wangu kuwa aliyemuua mama yangu ni Joshua ambaye sasa ni mume wangu…” akasita na kunitazama nami nikamtazama nikiwa na viulizo vingi.

“Nimekuwa jasiri sasa, na nimekubaliana na matokeo, Joshua wewe haukuwa wa kuninyima mimi nauli pekee ya kwenda kumzika mama yangu, ukaacha mama yangu azikwe na manispaa ya mji wa Musoma. Sidhani kama ungejisikia ahueni ama ungekuwa na moyo wa kusamehe kama ungetendwa hivi! Ni kweli unaweza kujitetea kuwa ulikuwa hunifahamu, lakini ni mara mbili nimekujia nikiuweka wazi moyo wangu kwako ili unisaidie… haukunifaa kitu”

“Mama yangu aliniuma sana Joshua, niliumia sana kwa sababu niling’atwa mbu sana usiku ule sikumwambia yeyote shida yangu bali wewe. Sijui hata ulinionaje…. Mimi sikuwa najirahisisha kwako na nilikueleza vile nafsi yangu imenituma. Badala yake ukanisaliti na kuniacha niingie katika janga baya kabisa, janga la kuuza mwili wangu ili nipate kula, nikapoteza vyeti vyangu katika namna nisiyoelewa….

Ulivyo mtu wa kupuuzia mambo yasiyokuhusu haukujali kuona ninaitwa Neema! Haukujali kuniona nikiwa bikira angali nina umri mkubwa na nimepitia mengi, ukajidanganya kwa faida yako mwenyewe.
Jitazame ulivyokonda sasa, jitazame ulivyoaibika katika lolote ulilopitia.

Unadhani nayafurahia haya Joshua, sifurahii hata kidogo lakini nataka upate somo katika maisha yako kuwa ni heri utende wema na uliyemtendea akupuuze kuliko kuacha kabisa.
“Mariam Sumra, kama hajajitambulisha kwako huyu ni mke wa mwanasheria wako. Hujui lolote hata kuhusu watu wako wa karibu, unajijali wewe tu Joshua.

Kama mke wa rafiki yako humjui ni mangapi haujali kuhusu wanadamu wenzako?
Nd’o maana hata siku ile haukujali yule rafiki yangu ambaye ni changudoa alipogongwa na gari.. ukasema huyu ni changudoa acha tu afe!
Kwa sababu changudoa hana damu sio?
Mariam Sumra ameagizwa na mumewe kwa ajili yako, huyu ni mwanasaikolojia… na hakika bila huyu sidhani kama ningehairisha nilichohitaji kufanya.

Ametumia ushawishi mkubwa sana kunifanya nighairi kile ambacho nilitaka kufanya juu yako ili nihakikishe moyo wako unatoboka matundu mengi kama ulivyokuwa wangu
Ulikuwa haujateseka inavyofaa Joshua, haujateseka walau nusu ya nilivyopanga tangu siku ile nilipoivaa pete kidoleni kuwa wewe ni mume wangu.

Haukuwa mume wangu bali adui uliyekubali kuishi karibu na mimi nitimize matakwa yangu.
Hauna tatizo la kizazi na haujawahi kuwa nalo, hakuna mganga hata mmoja hapa ila ni faraja yangu kuwa umelala makaburini na kupelekeshwa inavyotakiwa. Japokuwa huo ulikuwa ni mwanzo tu.

Joshua! Mimi nilibadilika na kuwa kiumbe wa ajabu sana kuanzia pale niliposhuhudia wadogo zangu wawili wakinusurika kufa kwa njaa.
Na wakati huohuo unajisifu kwangu kuwa umetoka familia ya kimaskini na ulipata tu msaada kutoka kwa watu wema ukasomeshwa na kuikomboa familia yako.
Leo hii kusaidia wenzako unadhani ni mojawapo kati ya mitihani migumu kabisa.”

Akasita kisha akamtazama Mariam Sumra.
“Da’ Mariam hebu imagine, licha ya yote haya lakini… lakini… hebu tufanye mfano wewe Mariam utajisikiaje mume wako akiwa anafanya mambo pasipo kukushirikisha?”
“Nitajisikia vibaya na sina umuhimu kwake!” alijibu Sumra.

“Sasa Joshua ambaye mimi na yeye ni wamiliki wa kampuni, akafanya hila na kutaka kuuza hisa zake karibuni tisini bila kunishirikisha, huyu ni mwanaume kweli? Eeh! Ni mwanaume ambaye unanishauri kila siku kuwa nimsamehe kwa sababu yeye ni mwanadamu??” alifoka Nyambura kiasi cha kuanza kutetemeka. Hapa sasa nilijikaza na kuzungumza.

“Nyambura… ina maana,aah! Ina maana hujui kuhusu hawa wanaume….niliokuwanao pale benki?”
Akanikata jicho la chuki huku akiwa bado anatetemeka.
“Ningewajua ningekuvizia benki kukupokonya hii bahasha, huna huruma wewe mwanaume, una mtoto mdogo unauza hisa kimyakimya una mpango wa kunikimbia ama?” alinihoji, sasa alikuwa amesimama wima mbele yangu.

Nyambura alikuwa ameiva kwa hasira na alikuwa ananitisha mno. Hapo sasa nikakiri kuwa wanawake wa kutoka mkoa wa Mara sio wa mchezo hata kidogo.
“Nyambura mke wangu..” nilipotamka vile sikuweza kumaliza kabla hajaninasa kibao kikali usoni na kisha akaanza kulia huku mimi naugulia maumivu.

“Unaendelea kuwa mwongo na mnafiki mkubwa katika ndoa yetu, unaendelea kuutoboa moyo wangu Joshua, kwa nini lakini? Maria Sumra ungeniacha, ungeniacha usingenizuia!” alilalama zaidi.
“Nyambura nisikilize kwa sekunde tafadhali..” nilimsihi na sikusubiri jibu lake.

Sasa kama ni uchi tayari nilikuwa uchi nimevuliwa nguo zote. Sikuona haja ya kufichaficha lolote lile.
Nikamueleza Nyambura pamoja na Mariam Sumra juu ya maagizo kutoka kwa mizimu!
Nikawaeleza juu ya masharti yao kuwa nikipata mtoto wanahitaji zawadi, na zawadi waliyoichagua ni kampuni yangu na pesa yote ya akiba iliyomo.

“Nyambura! Nilishindwa hata kukusaidia kila kiasi cha pesa kwa sababu hiyo mizimu ilinikataza mke wangu, hapa nina madeni kila kona kwa sababu sina chanzo cha pesa. Na pale tulikuwa katika makabidhiano kwa sababu wamemshikilia mama yangu mzazi.” Nikaishia pale na kumsubiri Nyambura aseme neno.

Si Nyambura peke yake bali hata Mariam Sumra hili jambo la mizimu kuhitaji pesa zote katika kampuni lilikuwa geni kabisa. Nyambura akaanza kuhaha akiniuliza maswali ya kizembe ambayo majibu yalikuwa wazi tayari.
“Milioni mia moja sabini? Mungu wangu! Wanataka kuniwekea dhambi ya kudumu hawa watu…. Nooo! Hayakuwa maelewano haya hata kidogo… na hapo kabla wamechukua pesa ama?” alinitupia swali.

“Ndio nilitoa kama milioni zisizopungua nne kwa ajili ya shukrani….”
“Uuuuwi! Mungu wangu, pesa pekee niliyoichukua kwako ni ile ya daktari tu pale hospitali… na ipo ndani hadi leo. Mimi sio tapeli Joshua….. what’s going on sasa… mbona wameingiza tamaa katika jambo lisilowahusu!” aliendelea kubabaika.
Akaichukua simu yake akapiga namba ambazo alizijua yeye.

Sisi tukabaki kimya kabisa.
Kwa kimya kile tuliweza kuisikia simu hata ilivyopokelewa.
Aliyepokea simu alikuwa ni mwanaume, lakini zaidi ya kusema ‘halo’ hakusema neno jingine la ziada.
Ikasikika sauti ya mwanamke.

“Mama Agness wapeni wanachokitaka hawa watu… wataniua!” ilikuwa ni sauti ya mama yangu mzazi.
Tumbo la kuhara likanishika!
Awali ulikuwa mchezo wa kuigiza ila sasa kila mmoja aliitambua kuwa ni vita rasmi.
Kama mchezo wa kuigiza ulinigalagaza huku na kule nikabaki hoi, vipi kuhusu hii vita kamili?
Niliulizia choo kilipo, nikatimua mbio nisije kuzua balaa!

Huku nyuma Agness akashtuka usingizini na kuanza kutokwa na kilio...

ITAENDELEA.....
 
Sehemu Ya 9

BAADA ya kutoka maliwatoni kujistiri maumivu yangu ya tumbo nilirejea sebuleni pale nilipowaacha Mariam Sumra mke wa mwanasheria wangu pamoja na Nyambura mke wangu.
Nyambura alikuwa anaongea vitu visivyoeleweka. Alikuwa amepagawa zaidi….

Simu ikapigwa tena na safarihii aliipokea Mariam Sumra. Alizungumza kwa takribani dakika sita hivi kabla hajakata simu na kutugeukia.

“Inatakiwa bahasha yenye dola!” alitamka akinitazama mimi kisha akamgeukia Nyambura.
“Noo! Hatutawapatia….” Alipiga kelele Nyambura.

“Nyambura, wamemshikilia mama yenu… huyo ndiye mama pekee mliyebakiwa naye hamna mwanamke mwingine wa kumuita mama.

Nyambura sahau kabisa kuhusu mafarakano yako na mumeo, fikiria kuhusu mama aliyekuwa nawqe bega kwa bega katika uzazi wako.” Mariam Sumra sasa alizungumza akimkazia macho Nyambura.

Maneno yale yalimyumbisha sana Nyambura, akaonekana kutamani kusema kitu lakini hakuweza kusema, bila shaka alikuwa akitamani nyakati zitupatie maajabu kwa kurejea nyuma ili asifanye yote aliyoyafanya?

Ama labda ili asikubali kuolewa na mimi? Ama labda asikubali kuusema ukweli ulivyo!
Sikujua anawaza nini.
“Tutawapatia bahasha wanayohitaji.” Hatimaye na mimi nilizungumza.
Nyambura akanitazama huku akinionea haya, akanisogelea na kunikumbatia.

“Yuda msaliti!” nilijisemea kimoyomoyo huku nikimtazama mwanamama huyu kama shetani!
Lakini sikudumu katika fikra za kumtazama kama shetani kwa sababu ndiye mwanamke pekee aliyenizalia mtoto.

Mtoto wangu hajazaliwa na shetani! Nilijirekebisha.
“Nisamehe Joshua wangu, sijawahi kupanga hata siku moja iwe hivi. Hata kama ningekuwa na kisasi kikubwa zaidi kwako lakini sio kufikia hatua ya utapeli wa aina hii. Nimesalitiwa Joshua….”

Alizungumza huku nikiyahisi machozi yakichuruzika na kunilowanisha.
“Niwapigie simu kuwa tunaipeleka bahasha?” aliuliza Mariam huku akiwa tayari na simu mkononi.

“Naomba nizungumze nao..” aliomba Nyambura lakini Mariam alidai kuwa huu haukuwa muda wa mazungumzo bali vitendo.
Nikamweleza kuwa awaambie kuwa tunawapelekea bahasha kama ilivyo.

Akanyanyua simu na kuwapigia, wakatoa maelekezo yao. Wakahitaji niende peke yangu, na kwa namna yoyote ile Nyambura asionekane kuwa karibu na eneo la tukio.
Walitoa vitisho zaidi kuwa nikithubutu kuleta ujanja wowote ule basi nijiandae kumsafirisha mama yangu kwenda kijijini akiwa katika jeneza.

Kitisho hiki kiliniingia zaidi!
Nikakubalianana Mariam abaki na Nyambura pamoja na mtoto na mimi niende kuwapa ile bahasha yao wanipatie mama yangu!
Makutano haya tulikubaliana yafanyike Morogoro, ni huko nitapewa mama yangu na kuondoka naye salama kabisa.

Nilitoweka siku iliyofuata nikambusu Aggy katika paji la uso na mama yake nikambusu shavuni, nikamsihi Nyambura awe mtulivu kabisa kila kitu kitaenda sawa na asifanye lolote baya kwa sababu yupo Agy asiyejua nani mbaya kati ya baba na mama anatutegemea wote kama wazazi wake.

ITAENDELEA....
 
Sehemu Ya 10

MOROGORO, Tanzania
Nilipokelewa katika kituo cha mabasi ukiwa ni kama ugeni wa kawaida kabisa. Nilishangaa watu hawa walikuwa wanajiamini kiasi gani kuwa siwezi kuambatana na askari katika safari yangu.
Walikuwa wanaojiamini mno. Walinichukua katika taksi yao, safari ikaanza, tulipita kona kona kadhaa kwa zaiddi ya dakika ishirini kabla hatujaingia katika hoteli yenye hadhi ya wastani palepale Morogoro lakini sikuwa naifahamu mitaa tuliyokuwa.

Niliingizwa katika chumba kimoja, na kwa mara nyingine tena nikakutana na wale wavaa suti wenye lafudhi ya kikongo.
Walinitazama kwa jicho la chuki kali.
Na walipoanza kuzungumza nilibaki kustaajabu.
Walikuwa wanaongea Kiswahili safi kabisa na sio kile kibovu chenye mahadhi ya kongo.

Duh! Nilibaki kuduwaa, kumbe walikuwa wanaichezea akili yang utu muda wote ule.
Wakaiomba bahasha, nami nikaweka ngumu nikasema ninamuomba mama yangu.
Mvaa suti mmoja akasimama na kunirushia kibao, nikawahi kutega mkono nikawa nimekipangua.
Hawa watu vipi? Nilijiuliza.

Nilichohitaji nikaletewa.
Kweli walikuwa wanamshikilia mama yangu mzazi, hawakuwa wamemdhuru hata kidogo lakini alikuwa na hofu kuu, nadhani kuna vitisho walikuwa wamempatia.
Nilipomuona mama yangu nikawa tayari kuitoa bahasha, nikawakabidhi wakaifungua na kuzihesabu dola zile zilizokuwa katika mafungu mafungu.
Nyuso zao zikang’ara kwa matabasamu mazito.

Hapo sasa wakaanza kuzungumza maneno mabaya sana juu ya Nyambura, wakasema mengi ya kutisha, kama ni siasa basi walikuwa wamemchafua kiasi cha kukosa hadhi ya kupigiwa kura hata moja.
Yote haya sikujali japokuwa waliyasema mbele ya mama yangu.

Walipomaliza kuhesabu na kuhakikishakuwa sio feki, wakaturuhusu kuondoka kwa amani huku wakitusihi kuwa wao sio mashetani bali mke wangu ndiye shetani mkubwa.
Wakati nataka kuondoka wakahesabu noti mbili za dola mia moja na kunipatia wakidai ni nauli.
Tulishuka ngazi nikiwa nimekabwa na kitu kooni ambacho nilijua nikikiruhusu kitoweke basi niwe tayari kuangua kilio.

Tuliondoka pale mapokezi tukipishana na watu kadhaa ambao sikuwatilia maanani bali nilikuwa makini kuzishusha ngazi nisije nikaporomoka.

Tulipofika nje niliinama ukutani, jasho likinitoka nikaanza kulia sana. Nililia mama akawa ananibembeleza kuwa niwe mwanaume upya!
Alisema mengi ya kunipa nguvu lakini moyoni nilikuwa nimekufa ganzi.
“Nyambura siso shetani kama walivyomuita wao, Nyambura amefanywa kuwa shetani. Nani aliyemfanya kuwa shetani hili ni swali wapaswa kujiuliza…” akasita na kunitazama huku akinifuta machozi.

“Hata wewe kwa sasa unaelekea kuwa shetani, usijiruhusu hata kidogo kufika huko. Humchukua mwanadamu dakika chache sana kuwa shetani na kisha akadumu katika ushetani na asiweze kubadilika kamwe.”

Maneno ya mama yakanipatia jibu kulingana nay ale maelezo ya Nyambura awali, ni mimi nilimfanya yeye kuwa shetani. Nilijaribu kufikiria ni namna gani nitaweza kuishi na mwanamke aliyenifanyia haya yote….

Nikakosa kujiamini kabisa.
Nisingeweza kulala kitanda kimoja na Nyambura.
Siku hiyohiyo tulisafiri na mama kurejea jijini Dar es salaam. Mji ambao sikujua utanipokea vipi hasahasa kuonana ana kwa ana na Nyambura mke wangu.

Masaa manne yakapita na hatimaye nilikuwa pamoja na mama tukiufungua mlango wa kuingilia nyumbani kwangu.
Kimya kilikuwa kikubwa sana……
Hatua ya kwanza tu kuingia sebuleni, kuna mwili ulikuwa umejilaza hovyo kabisa.
Kidevu kikijibwaga katika meza ya kioo, huku akiwa amepiga magoti!
Nini hiki? Nilijiuliza, mama yeye alishtuka na kupiga kelele.

Licha ya kelele hizo bado mwili ule haukutikisika.
Sura yake ni mimi pekee niliyeweza kuifahamu, mama hakuifahamu kabisa.
Mariam Sumra!

Tulihaha huku na kule kumtafuta Nyambura na mtoto lakini hatukuziona dalili zozote zile.
Hapa sasa hofu kuu ikatanda.
Ni kitu gani kimetokea?? Hili likibaki kuwa swali kuu….
Mariam Sumra akaendelea kusujudu pale sakafuni na kidevu kikijibwaga mezani!
************
NUKUU
MKE/MUME ni kitu kingine. Awali unapoingia katika mahusiano ya kimapenzi mwenzi wako anakuwa kama mtu wa ziada kwako ambaye hata akikumbwa na jambo inakuwa mbali na wewe, baada ya muda mnaanza kufanana mitazamo, na hapo unajihisi huwezi kufanya lolote la maana bila yeye… unaamua kuingia katika ndoa. Damu zinakutana na mnakuwa mwili mmoja.

Mwenza wako anageuka kuwa ndugu yako wa karibu zaidi wa kila siku……
Ukifika wakati huu, waweza kufanya lolote kwa ajili yake.
Umewahi kusikia watu wanakuwa vichaa kwa sababu ya mapenzi? Umewahi kusikia wanaojinyonga kwa sababu ya mapenzi?
Haya yote hutokea wakati mwili wako umeungana na wa mwenza wako!
HII NI SEHEMU YA KUMI NA SABA….
Nilikimbia huku na kule kutafuta muafaka wa jambo nisilolijua kabisa.

Nilishika simu nikaicha, mama naye alikuwa amechanganyikiwa akiulizia ni wapi Nyambura atakuwa ameenda. Sikuwa na jibu la kumpatia….
Kwa sababu yeye mwenyewe alifahamu fika kuwa tulikuwa wote Morogoro na sasa tupo jijini Dar es salaam.

Nilifahamu fika kuwa mimi nikionyesha kuchanganyikia na mama naye aonyeshe kuchanganyikiwa basi patakuwa hapakaliki pale ndani, nikatulia na kuchukua tena simu yangu nikajisahaulisha kama kuna lolote ambalo limetokea.
Sasa niliweza kupata mtu wa kumpigia.
Mume wa Mariam Sumra ambaye ni mwanasheria wangu!
Simu ilipokelewa upesi sana.

“Nilitaka kukupigia simu muda huu huu!” alianza kuzungumza bila salamu yoyote. Nikamsikiliza.
“Simpati Nyambura hewani, sijui kama upon aye?”
“Nyambura? Wa nini?” nikamrushia swali.
“Upon aye?” aliendelea kuuliza badala ya kujibu.
“Hapana! Kuna tatizo lolote?” nikarusha tena swali.

Hapohapo bila kutarajia chochote, ghafla mama akanipokonya ile simu.
“Mje mtusaidie tumekuta mtu ni mwanamke ndani ya nyumba yetu, hatujui kama amekufa ama ni mzima. Na mke wa mwanangu hayupo, nje mtusaidie jamaniii!” alizungumza upesi upesi mama akiwa amechanganyikiwa sana.

Ni tukio ambalo sikulitarajia kabisa na lilizua mshikemshike.
Alipomaliza akanipatia simu huku akinilaumu kuwa ninazunguka zunguka mbuyu badala niseme shida inayotukabili.
Sikumlaumu mama!
Niliporejea kumsikiliza mwanasheria alinisihi nimweleze ukweli nini kinatoke.

Nikamweleza hali kwa ufupi kama ilivyokuwa inaonekana machoni pangu. Lakini sikumgusia juu ya safari yangu ya Morogoro!
Akasema anakuja pale nyumbani.
Sisi tulibaki mbali kabisa na mwili wa Mariam Sumra, mama alikuwa ananionya kabisa nisiusogelee mpaka polisi wafike.
Yeye alijua niliyekuwa nazungumza naye anahusika na mambo ya kipolisi.

Baada tya dakika kumi na tano na ushee, pikipiki ilisimama mbele ya nyumba yangu. Geti lilikuwa wazi nikasikia vishindo vya mtu akija mbiombio.
Nikaufungua mlango na kumtazama kwa mbali mwanasheria wangu akitimua mbio.
Ama! Mapenzi ni kitu cha ajabu sana.
Usiombe yakakumeza na kukutupa katika mji unaoamini ni tulivu kupita yote.

Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mwanasheria huyu akiwa na hofu kubwa kiasi hiki.
Alipofika akanisalimia mimi ‘SHKAMOO’ kisha akamwambia mama yangu ‘HABARI ZA KAZI’
Nilijikuta nachekea mbavuni, baada ya muda mrefu kupita nikiwa sina hata tabasamu.
“Amekuwaje mke wangu eeh! Amekuwaje jamani?” alihoji.

“Kama nilivyokueleza katika simu mkuu. Hakuna ajuaye.. wote tumeingia muda huu.”
“Hata mama nawe haukuwepo?” alimtupia swali mama.
Mama hakujibu!
Mwenye mke akamsogelea mkewe.
Akamgusa hapa na pale….

“Anapumua!!” alisema….
“Nini kimemtokea jamani eeh!” sasa alikitoa kichwa pale mezani na kumnyoosha sakafuni.
Sasa hata mimi niliweza kuona akiwa anapumua.
Hapakuwa na muda wa kupoteza zaidi, tukakubaliana kumpeleka hospitali.
Nilijikaza na kuendesha gari kwa sababu mwanasheria alikuwa amepagawa zaidi.

Tukiwa katika gari alikuwa akirudia rudia maneno ambayo awali niliyachukulia kuwa ya kawaida sana lakini alipozidi kuyarudia nikaanza kupatwa na hasira.
Alikuwa akisema, ‘Joshua unajua mkeo ni shetani eeh! Shetani kabisa huyu mwanamke, sijui hata ulikosea nini ukaoa shetani.’
Anatulia kidogo ananikumbusha tena kuwa mke wangu ni shetani.

Hasira zikanikaba, lakini nikapambana nisije kufanya jambo lolote la kishenzi.
Hii hali ya kukasirika baada ya mke wangu kuitwa shetani ilinifanya nitambue kuwa licha ya haya yote yaliyotokea, alama za penzi zito la Nyambura zilikuwa katika sehemu kubwa tu ya moyo wangu licha ya hayo yote yaliyotokea.
Unaweza kunishangaa sana na kusema kuwa laiti kama ingelikuwa ni wewe usingelichukia kabisa.

Ni kweli kwa sababu si wewe uliyeshuhudia penzi zito na la dhati kabla ya mkasa huu!!
Tulifika hospitali, tukasaidia kumshusha Mariam Sumra!
Akapokelewa na wauguzi akaingizwa wodini.
Baada ya kutoa maelekezo na sisi kupewa maelekezo sasa tulibaki nje kusubiri kitakachojiri.

Mwanasheria akaanza tena kusema vibaya juu ya Nyambura.
Nikaona huyu bila kumwonyesha makucha sekunde si nyingi atanivuruga upya akili yangu.
“Brother! Achana na masuala ya Nyambura na ushetani wake, unapomzungumzia Nyambura kama shetani unamzungumzia mke wangu wa ndoa, mama wa mtoto wangu mmoja.

Unaposema ni shetani ni kipi mkeo alifuata kwa Nyambura kama sio shetani kumfuata shetani mwenzake? Wote ni mashetani tu, shetani mmoja yupo wodini amepoteza fahamu, shetani mwenzake anazurura popote anapojua yeye. Acha kumsema Nyambura hivyo tafadhali….” Niliwaka!!

“Joshua acha baba…. Yaishe tupo matatizoni, na wewe baba mwingine acha kusema ushetani wa mtu usiyemjua…. Hivi mnajua Nyambura mnayemuita shetani alinitolea damu nyingi sana alipokuja kuniuguza kijijini, bila yeye ningeweza kufa. Hakutaka sifa zozote hajatangazia mtu…

hebu mtunzie na haya mazuri yake basi…. Hata kama ni shetani basi tuyatunze katika mioyo yetu.” Mama alitusuluhisha.
Yakaishia pale.
Lakini sikutaka tena kuwa jirani na mwanasheria nikaketi mbali kiasi.
Nusu saa baadaye majibu yalitoka kuwa Mariam Sumra alilishwa madawa ya kuleta usingizi, hakuwa na tatizo lolote zaidi ya pale.

Huduma zikaendelea kutolewa hadi mjajira ya saa kumi jioni tukaondoka pale.
Niliendesha gari hadi nyumbani kwa mwanasheria, wakati huo maelezo ya Mariam Sumra hayakufaa kitu chochote.
Kwa sababu alidai kuwa Nyambura hakumweleza mpango wowote aliokuwanao.
Tulipowashusha, mwanasheria alinifikia na kunipigapiga begani kisha akajutia kauli zake.

Nikamwambia yamekwisha kabisa.
Tukaondoka na mama hadi nyumbani, tukiwa kimya kabisa katika gari.
Tulifika na kuikuta nyumba ipo kama vile tulivyoiacha. Hii ilimaanisha kuwa Nyambura hakuwa amerejea.
Niliufungua mlango na kuingia pale ndani….
Mara mama akapiga mayowe, nikaruka mbele kukwepa hatari yoyote ambayo ingejitokeza.

Nikageuka na kumtazama mama alikuwa anatazama chini…..
Damu!!
Palikuwa na alama za damu ambazo hazikuwepo hapo kabla.
Kutazama vizuri ulikuwa ni mchirizi wa damu…..

Sijui pale tulipouona ndo ulikuwa unaanzia ama ulikuwa unaishia…
Mchorizi ule ulikuwa unatokea chumbani ama kuelekea huko.
Mapigo ya moyo yakaanza kufukuzana tena……
Nini hiki?
Tulijiuliza, nikatimua mbio mpaka chumbani bila uoga wowote ule.
Matatizo yalikuwa lukuki sana sasa sikuwa naogopa lolote lile.

Niliingia na kuufuata mchirizi ule.
Nikainama uvunguni, mama naye akinifuata nyuma hapakuwa na mauaji wala hapakuwa na mtu yeyote yule.
Tulibaki kustaajabu.
“Bahasha hiyo ina damu..” mama aliona na kusema, nikageuka na kutazama upande alionionyesha.

Kweli kulikuwa na bahasha yenye damu.
“Mama wamemuua Agy wangu!!” nilianza kulia sasa.
“Agy! Umejuaje?” alinibambika swali lililokatisha kilio changu, kwa sababu nilikuwa nalilia kitu nisichokijua.

Nikaiokota ile bahasha huku nikitetemeka.
Nikaifungua na kukuta ndani kuna kipande cha barua.
Nikatoa huku nikiomba Mungu pasije kuwa na masharti ya kipesa kwa ajili ya kumkomboa mwanangu.
Sikuwa na pesa kabisa, hivyo mwanangu angeweza kuuwawa.

Safari hii sikuwaza sana juu ya Nyambura!
Kutazama ulikuwa ni mwandiko wa Nyambura, mwandiko niliouzoea pindi tulipokuwa ofisini.
Nikaisoma kwa sauti mama awe shuhuda kwa kusikia.

NYANBURA ANAANDIKA!!
Joshua, mume kipenzi kabisa.
Ndugu yangu pekee, na baba halali wa mtoto wetu!
Niligundua kuwa nakupenda sana lakini nilikuwa nimechelewa, tayari nilikuwa nimeharibu kwa kutunza kisasi kisokuwa na tija.

Kisasi cha kipuuzi!
Umeteseika nimeona kwa macho, nami ninateseka moyoni hakuna anayeweza kuona.
Nikiulizwa peponi nini maana ya pendo la dhati nitajibu Joshua, hata wakihitaji orodha ya wanaume wa uhakika niliowahi kukutana nao jibu litakuwa Joshua.

Yaliyopita yamepita! Wewe ni baba bora sana ambaye unastahili kupata mwanamke safi asekuwa na visasi katika nafsi yake.
Lakini ni mwanaume ambaye haustahili kutendewa haya yaliyotokea kwako.
Nimeona na kwa dakika za mwisho nimejaribu walau kupigania kidogo kilicho chako walichotaka kukupokonya,

Ulipishana nami katika hoteli Morogoro.
Usingeweza kunijua, nilikutazama na kuuona uso wako ulivyosononeka kwa haya yaliyotokea, niliona jinsi ulivyokonda kwa mawazo.
Nilimuona mama yetu alivyokuwa anakusikitikia.

Niliingia ulipokuwa na niliua!
Ndio niliua….
Kuhusu niliuaje na niliua wangapi? Haya hayana tija lakini kwa sababu walikiuka makubaliano yetu niliona hawa ndo wanafaa kuadhibu na sio wewe Joshua.
Mimi ni binti imara kabisa kutoka mkoani Mara, nimepitia suluba zote na pale mtu anapokiuka tulichokubaliana nipo radhi hata kuua.

Narudia tena niliua na nimeirejesha bahasha iole kwako. Sikutoa hata noti moja.
Halali yangu ipo katika akaunti yangu, ulinilipa mshahara mzuri sana unanitosha kuanza maisha mapya nikiwa namlea mtoto wako.

Kama nisipokamatwa mapema basi mwanao akifikisha miaka minne, nitamleta kwako.
Lakini kama ukisikia nimekamatwa mapema tafadhali usiache Agness akatua katika mikono ya watu wabaya.
Mchukue wewe uliyesota kumpata!
Mchirizi huo wa damu usikushangaze sana…

Nimejikata maksudi na kuiacha damu hii iishi nawe katika nyumba yako milele yote.
Nawapenda sana!
Nakusihi sana usiyafuatilie tena mambo haya kwa namna yoyote kwa sababu yatakuumiza kichwa.
Naomba msamaha mimi kwa niaba ya wote nilioshirikiana nao.
FUNUA GODORO MUDA HUU!!
Nyambura Joshua!!
Barua iliishia pale, nami upesi nikafunua godoro.

Macho yangu yakakutana na ile bahasha niliyoipeleka Morogoro.
Nilijikuta natokwa na kilio huku moyo wangu ukiuma sana, nilitamani Nyambura angerejea tena katika maisha yangu!!
Lakini Nyambura hakujulikana ni wapi alipo…..

Baada ya muda nikaendelea na shughuli zangu katika kampuni yangu ambayo ilikuwa imeacha kufanya kazi kwa sababu wafanyakazi hawajalipwa mishahara yao.
Siku niliyoingia ofisini kwangu, nilijikuta natabasamu tu, nilikuwa nimewakumbuka wale matapeli waliodai kuagizwa na mizimu….

Nikatambua kuwa hata wao huko walipo kuzimu watakuwa wakikumbuka wananicheka sana.
Nikatulia katika kiti changu cha kuzunguka, nikaanza kuandika majina na madhara katika akili yangu.

NYAMBURA: Sitakaa niwaamini wanawake katika maisha yangu hasaha katika sekta ya mapenzi, sikuwaza kuoa tena. Mpaka hivi sasa sitaki ushauri!!
REVO: akili yangu haikuwa na nafasi tena kwa ajili ya rafiki wa dhati, hata mwanasheria aliyenisaidia bado sikutaka kumwamini sana. Ikiwa naye alimuita mke wangu shetani, ipo siku nami anaweza kuniita baradhuli.

MGANGA: Sitathubutu kwenda kwa waganga wa jadi tena, ni waongo na wanafiki wakubwa.
Majina haya yalinitosha sana kwa wakati ule.

Na niliapa kuwa hata wanasaikolojia wahamie nyumbani kwangu na wengine waje kuishi ofisini kwangu hawataweza kulitibu gonjwa langu la kihisia juu ya marafiki na mapenzi.
“Ama hakika Nyambura ulikuwa ni mji tulivu, mji bora kabisa niliowahi kuishi lakini gonjwa uliloniachia ni la milele nitadumu nalo….”

JIFUNZE:
KATIKA maisha kuna nyakati huja katika maisha ya watu wengine, nawe utaziona na kuishia kusema yamemtokea fulani. Lakini halahala litokealo kwa jirani yako hata nawe laweza kukutokea. Majaribu shida na mateso tumeumbiwa wanadamu!!!
Jifunze kupitia uyaonayo ili ujiandae kuyakabili yakija kwako…..

MWISHOO!!

#TAFADHALI USIPITE BILA KUTOA MAONI SIKU HII YA LEO!!
ASANTENI SANA kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho
 
shukran sana mkuu na asante kwa kuweza kuimaliza simulizi yote, nakungoja utuletee na nyingine tena

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom