Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,054
- 16,902
- Thread starter
-
- #401
Upo sahihi mkuu, kila mtu ana namna yake ya kudhibiti hisia zake, hasa kwenye zone ya uvumilivu hapa kunawatesa wengiJifunze moyo wa shukrani ili uwe na furaha na mafanikio unaamrisha utadhani unamlipa mwandishi?
Enjoy simulizi mkuumkuu we unajua mi na jack tunafahamiana vp na tunaongeleshanaje? pita hata juu uone tunavosemezana basi...we una ujuaji sana mwana naamini ni mwanaume punguza kidogo nakuona kila mahali unadakia na kurukia rukia mambo usije rushiwa rungu ukadaka ikawa mengine em kaaga kimya sometimes unaboa acha umama unajiendekeza sana mdomo umekuzidi huwez acha jambo likupite sio maisha dada we kiila kitu umo vp unataka chapati za maji utafikwa shauri yako
Mkuu punguza hasira na matusi hayakusaidii nadhani Jack Daniel kani quote na kukupa jibu zuri tu. badirikamkuu we unajua mi na jack tunafahamiana vp na tunaongeleshanaje? pita hata juu uone tunavosemezana basi...we una ujuaji sana mwana naamini ni mwanaume punguza kidogo nakuona kila mahali unadakia na kurukia rukia mambo usije rushiwa rungu ukadaka ikawa mengine em kaaga kimya sometimes unaboa acha umama unajiendekeza sana mdomo umekuzidi huwez acha jambo likupite sio maisha dada we kiila kitu umo vp unataka chapati za maji utafikwa shauri yako
Nawewe badilika sio badirikaMkuu punguza hasira na matusi hayakusaidii nadhani Jack Daniel kani quote na kukupa jibu zuri tu. badirika
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
Kama kawaida kama ada, ikiwa ni mwendelezo wa kuisaka elimu kama njia ya kujitengenezea wepesi wa maisha ya baadaye au njia ya kujikomboa na maisha magumu,japokuwa hii si kanuni ya kuwa na maisha mazuri kwa Elimu siyo ndiyo Kila kitu, wapo wamefanikiwa kwenye maisha bila kupita darasani
Samson alikuwa smart akiwa kavaa begi lake kama ambapo jumatatu huwa ina vimbwanga vyake si kwa wafanyakazi tu, hata kwa wanafunzi.
Ni siku ambayo huweza kukupa picha ya mambo yatakavyoenda kwa wiki nzima japo si kwa wote wanaichukulia jumatatu kihivyo
Alifika shule muda sahihi huku siku hiyo akishangaa wanafunzi kuwa wachache tofauti na alivyozoea, hili halikumpa tabu akaingia darasani kwake huku akijiandaa na Somo la hesabu kama timetable, ilivyokuwa inaonesha akawa anafungua fungua kitabu fulani chenye Topic ya siku hiyo kwaajili ya kujikumbusha ,
Mwalimu wa somo husika aliingia, ambaye alikuwa ndiye mkuu wa shule ile,licha ya wanafunzi kusimama wamsalimie aliwaashiria wakae tu,
Huku akimuulizia monitor wa darasa.
Wewe ndiyo monitor, mbona mchafu hivyo halafu, nywele hizooooo! Hebu njoo mbele kwanza, haiwezekani monitor mzima unakuwa rafu na ni nani alikupa huu uongozi, eti class ni vigezo gani vilitumika kumpa umonitor huyu, aliongea yule mwalimu huku akimuinamisha ili amchape viboko.
Kuanzia leo huyu namvua hiki cheo, au hamjui maana ya uongozi,
Unapopewa uongozi maana yake wewe ni mfano kwa vitu vingi, kuanzia akili darasani, nidhamu, usafi na mengine mengi Sasa wewe hapana, Sasa nawataka mchague monitor wa darasa mwingine haraka vigezo awe na uwezo wa kuandika vizuri pamoja na kumudu baadhi ya masomo. lakini wanafunzi wote walikataa wakimtaka yule yule kwani wao walimwamini kwa uwezo wake mkubwa wakipewa test alikuwa di mchoyo anaweza kuwapa majibu darasa Zima na pia alijua alichokifanya kwani alikuwa na akili sana, jambo pekee lilimfanya aonekane mchafu ni kutokana na familia duni anayotoka, ikiwa haijiwezi, hivyo kuwa na maisha ya kuungaunga.
Baada ya wanafunzi kuonesha wote wanamtaka yule monitor wao waliyemzoea mwalimu alimpandisha na kumshusha huku akionesha hajamkubali .
Haya sawa kwakuwa wenyewe mnamkubali Mimi Sina neno ila nakuachieni test tu kwakuwa Leo Nina mambo mengi nipo kwenye msafara fulani wa mkuu wa mkoa na hata hivyo wiki hii Kuna mwalimu mpya wa somo la Mathematics atakuja kwakuwa Mimi nakuwa na ratiba nyingi mno.alisema yule mwalimu mkuu
Wanafunzi wote walihuzunika sana, waliamini hawawezi kupata mwalimu genius na mwenye kipaji cha kufundisha kama yule kwani hata wale vichwa ngumu kuelewa, ilikuwa rahisi kumuelewa yule mwalimu ambaye alikuwa ni mwalimu wa hesabu wa shule nzima.
Wakati anatoka, alikuja upande wa nyuma kule back benchers akakutana uso kwa uso na Samson,
Eheee wewe nilikuwa nakutafuta sana yaani pindi natoka ofisini mtu ambaye nilikuwa nataka nikuone ni wewe hebu nifuate ofisini, aliamrisha yule mwalimu mkuu
Samson moyo ulimlipuka akijaribu kuwaza kafanya kosa gani ila hakuelewa, maana walimu wale ilikuwa wakikuita lazima Kuna mistake umefanya.
Alifika ofisini akakuta kuna walimu wawili ambao walikuwa siyo wa shule yao ila aliwafahamu vyema,
Dah samahani ndugu zangu nimechelewa kiasi , majukumu nayo ni mengi kama nilivyomuomba Afisa Elimu na kamati yake waweze kutuongezea walimu wa masomo ya Sayansi pengine itanipunguzia majukumu. aliongea huku akijiweka kwenye kiti chake, Kisha akawapa wale walimu wenzake bahasha fulani na kuwaruhusu waondoke ,
Samahani kidogo naongea na huyu kijana ila ndani ya nusu saa nitakuwa nimefika kwani mheshimiwa atapita mida ya saa tano. aliwaambia wale walimu
Enhee Samson nimekuita hapa, nahitaji kuuliza jambo moja, naomba unijibu, kwa ufasaha na ukweli, kama Kuna kitu hukukiona kwa macho ila ulisikia usikitolee maelezo, nahitaji kile uliona na kusikia kwa macho yako, hebu niambie siku ya jumamosi kulitokea Nini kwenu Kati ya familia yenu Na mwalimu Sadick, aliuliza yule mwalimu mkuu.
Samson kwakuwa alishatahadharishwa asiseme jambo ambalo hakuliona, akili ilimcheza vizuri sana, akamjibu kuwa hakukutokea jambo lolote.
Nyumbani kwenu mnaishi watu wangapi? aliuliza mwalimu mkuu
Tunaishi watu wengi tu, ila kwasasa tunaishi watu wanne yaani , baba mkubwa Mzee Mgaya, Mama mkubwa, pamoja na dada wa kazi (akimaanisha Rahma)
kwahiyo huna unalolijua, mbona nimeambiwa mwalimu Sadick aliumizwa na mtu wa familia ya mzee Mgaya, japo yeye amenificha kaniambia kuwa anaumwa, lakini kwa taarifa na vyanzo visivyo rasmi sana, kwa shuhuda za majirani inaonesha mtu alitoka mbio huku akiugulia maumivu akiwa anatoka kwenye nyumba yenu bado Samson unataka kuniambia hujui kitu. aliongea mwalimu mkuu huku akijichekesha akilazimisha Samson aongee.
Mwalimu siku ya jumamosi tulisafiri mimi na wazazi wangu kwenda huku shamba kukagua miradi ya Mzee na tuliporudi tulikuta ni salama tu, Sasa hayo mengine Mimi sijayajua. alijibu Kwa kujifanya hajui ili kuepusha mlolongo wa maswali.
Haya wahi darasani, nitaongea na Mzee Mgaya mwenyewe, maana hili kinaleta picha mbaya kwa siye walimu, alisema mwalimu mkuu
Samson aliwaza kidogo huku wakati mwingine akicheka, ni nani aliyemuona mwalimu Sadick, akitoka ndani mwetu, na kwanini amdanganye mwalimu mkuu kuwa anaumwa wakati kaumizwa na Rahma? Watajijua wenyewe. alijisemea Samson huku akiendelea na masomo yake. Muda wa saa Saba mchana Samson aliambiwa anaitwa kwenye ofisi ya walimu wote, akaingia akakuta jopo la walimu karibu wote wakiwa na mwalimu mkuu wakiwa wanaongea kwa lawama kidogo.
Hii serikali basi tu, yaani watu hawazingatii itifaki kabisa yaani, haiwezekani safari inapangwa kwa muda wa wiki nzima halafu inaahirishwa kirahisi tu, Mimi hapa nimetumia gharama kibao nikiwa kama mratibu wa Elimu kwa kuchukua walimu kadhaa ambao tungekuwa kwenye msafara lakini , Cha ajabu safari hakuna , na hakuna sababu za msingi. Alilaumu mwalimu mkuu ambaye Samson aligundua kuwa pia ni mratibu wa Elimu cheo ambacho hakukijua kabla.
Sasa ndugu zanguni hayo tuyaache tu, Wala hatuna namna Hawa ndiyo viongozi wetu wa taifa hili, hata wakituambia muda huu Kuna safari tena, hatuna budi kutii mamlaka. alisema kwa masikitiko mwalimu mkuu.
Haya Mimi natoka kidogo naenda hapo kwa mzee Mgaya nina mazungumzo naye, aliwaaga wenzake huku akiongozana na Samson hadi nyumbani kwao. Wakimkuta Mzee Mgaya akishuka kwenye gari kuonesha Kuna sehemu anatoka muda si mrefu
Karibu sana Mzee mwenzangu, naona umekuja kunitembelea na wewe navyokujua huwa huji hapa kirahisi bila shaka , kuna matatizo, vipi kijana wetu anasumbua nini. aliuliza kiutani Mzee Mgaya.
Hapana, hakuna jambo baya kwa Samson yaani huyu tangu umenikabidhi mwaka ule, naishi naye vizuri sana shuleni kwangu, Tena kitaaluma yupo vizuri ana wastani mzuri, na pia ni bonge la football player, yaani hii ndiyo winga ya shuleni kwetu . aliongea mwalimu mkuu huku akimpigapiga Samson mgongoni.
Haya mwalimu karibu ndani, karibu sana, waliingia ndani wakakutana na watu wengi kidogo,
Akiwemo muuza nyama maarufu wa mtaa ule, mama Kulwa akiwa ndiye mazahausi, alikuwepo pia Tausi mke mdogo wa mzee Mgaya, alikuwepo pia Cathy msichana ambaye ni rafiki wa mama Kulwa, pamoja na Rahma.
Samson alishangaa uwepo wa watu wale, akagundua kuwa kumbe mwalimu mkuu hajakuja kwa bahati mbaya Bali, ameitwa.hivyo watu nane ndani ya familia ya mzee Mgaya wakaanza kwa kutambulishana ili kikao husika kiweze kuendelea.
Nini kinajadiliwa kwenye hicho kikao?
Ni nini kitajiri baada ya majadiliano?
Sehemu inayofuata ina majibu,
Itaendelea..........................
Kazi nzuri Engineer niko mjini sema sehemu tupate mkojo wa shetani ikiwa huko free .SEHEMU YA HAMSINI NA TATU

Yes ni kweli niko free, baada ya kutoka mkoani nilikokuwa hata hivyo Niko home tu Kuna kijihoma kinanisumbua , nadhani hali ya hewa natamani tungepiga vyombo pamoja ila niko likizo kidogo na hivi vituKazi nzuri Engineer niko mjini sema sehemu tupate mkojo wa shetani ikiwa huko free .
Happy Valentines day too Eng. Jack DanielSEHEMU YA HAMSINI NA NNE
Sura ya mke mdogo wa mzee Mgaya (Tausi)haikuwa na nuru hata kidogo, aliongea kwa kujilazimisha na hata ilipotokea jambo la kuchekesha alicheka kwa kujilazimisha tu.
Haikujulikana nini kinasababisha japo labda kitendo cha kuonekana yeye kashindwa kuishi na Rahma kilimfanya ahuzunike.
Baada ya utambulisho kupita, Mzee Mgaya aliendelea,.....
Ndugu zanguni bila shaka kilichotukutanisha hapa, tayari kila mmoja ameweza kufahamu kama nilivyoeleza tangu mwanzo kuwa siku mbili nyuma nikiwa natoka kwenye ukaguzi wa projects zangu, niliweza kukuta hali ya tofauti hapa nyumbani kwangu, ambapo binti tunayeishi naye alinusurika kufanyiwa kitendo cha kikatili kwa mujibu wa maelezo yake, na hata hivyo hatukuweza kukubali maelezo yake moja kwa moja bado Kuna hatua za uchunguzi tuliweza kuzifanya , kwa kuanzia kwa ndugu yetu ambaye ni muuza nyama maarufu hapa mtaani kwetu jambo zuri zaidi yeye yupo anaweza kutufafanulia. Mzee Mgaya aliweka kituo.
Naam, sina maelezo mengi ila ni kwamba imekuwa ni kawaida huyu mama yangu (mama Kulwa)kuagiza nyama kilo nyingi, nadhani akiweka kwenye friji, basi siku ya jumamosi mida ya saa nne alikuja huyu Binti akiwa kaongozana na mtu ninayemjua, ambaye ni mwalimu Sadick, sikushtuka wala kushangaa kuongozana kwao, japo mienendo yao kila mmoja angeweza kujua kama ni wapenzi.
Lakini cha kushangaza baada ya Mimi kumpa mzigo huyu binti, yule mwalimu aliomba ampokee, ndipo Binti akawa anakataa na Mimi nikashangaa kuona vile hata hivyo waliondoka na kupotea kwenye upeo wa macho yangu huku nikipata jibu kuwa huenda bado hawajawa wapenzi bado jamaa anabembeleza.
aliweka kituo muuza nyama.
Baaasi, baaaaasi baba, Wala hakuna haja ya kuendelea, Kila kitu kipo wazi kumbe yule kijana ni mshenzi eeeh, aliropoka mama Kulwa huku akitulizwa na wenzake kwamba asubiri mpaka mwisho.
Muuza nyama aliaga na kuondoka akiwa katoa maelezo yaliyomridhisha kila mmoja.
Mwalimu nadhani kila kitu umesikia na umeelewa, maana hapa tupo kwenye process za kufungua kesi kwasababu huyu kijana kanikosea sana hawezi kuja nyumbani kwangu bila heshima na kufanya mambo yake atakavyo. ulinisihi kwamba nisichukue maamuzi magumu bila ushahidi, nikaamua kumuita huyo kijana nadhani umeridhika siyo?
aliuliza Mzee Mgaya
Ni sahihi kabisa japo Mimi mwalimu Sadick, kaomba ruhusa kuwa anaumwa hakuniambia anaumwa nini, hata hivyo kwakuwa nilishasikia stori hizi kabla yenu kuwa anaonekana kaumizwa huku watu wakimlaumu kwa kujishushia heshima yake, Mimi nilimfuata nikamuuliza kiufupi kakataa katakata kuwa hajawahi kuja hapa zaidi ya siku moja ambayo aliwakuta nyie wote na aliondoka kwa amani.
Lakini hata hivyo kwa mujibu wa maelezo haya, nakubali kuwa huenda kweli alikuja hapa, lakini ombi langu ni kwamba kwakuwa hakuna madhara yeyote kwa Binti yetu, kwanini tusiyamalize haya mambo kiungwana kuliko kuyakuza na kupoteza muda , kwani haya yakifika mahakamani si mambo madogo haya ndugu yangu.
aliongea mwalimu mkuu akimuomba Mzee Mgaya alegeze kamba kidogo.
Hapana mwalimu, haiwezekani, tena Bora ujitoe tu kwenye haya mambo kwakuwa aliyefanya upuuzi huu siyo ndugu yako bali ni mfanyakazi mwenzio, Sasa acha sheria ichukue mkondo wake huyu ni mwanangu, hizi habari nimezipokea kwa uchungu sana, juu ya kuwa tulikosana na yeye akaja kuishi huku, lakini nitasimama kuhakikisha huyo baradhuli anapata alichokitafuta,
Huyu Rahma ana stori kubwa ambayo ni yeye na Mimi ndiyo tunaijua Sasa haiwezekani aendelee kunyanyasika kwa Dunia hii yeye kaikosea nini? Tausi aliongea kwa hisia kali, huku mama Kulwa akimsapoti kwa asilimia zote, kiufupi wanawake wote hawakuwa tayari lile jambo liishe juu kwa juu badala yake wao walitaka mkosaji ashitakiwe tu.
Nyumba iligeuka makelele watu wakawa hawasikilizani tena, ikabidi mzee Mgaya amtoe mwalimu na Samson akiwafuata kwa ukaribu.
Sasa ticha hapa maelewano ni madogo, mimi binafsi nimekuelewa nafahamu namna muda utakavyopotea kwenye hili suala nawaza tu, tungeonana na huyo kijana Kisha tumuonye Kisha maisha yaendelee. Sijafurahishwa na kitendo chake hata kidogo ila najua Mzee mwenzangu utajua unakaa vipi na walimu wako ili wapunguze dharau .kuhusu Hawa wanawake tuwaache kwanza hawawezi kukuelewa kwa lolote nadhani unawaona wapo kwenye hali gani.
aliweka kituo mzee Mgaya
Mzee mwenzangu, kwanza nikushukuru sana kwa kuweza kutazama mbali, bila shaka na mtuhumiwa anajua Nini kitatokea pindi hizi taarifa zitakapozagaa , walimu tunaonekana tuna mapungufu sana hasa sisi wanaume kutembea na wanafunzi, ni jambo linapigiwa kelele kila siku, vipi ikionekana mwalimu mzima uliyeaminiwa na umma unaenda kubaka, ni hatari sana nakuomba tulimalize hili jambo ndugu.
Mwalimu alisisitiza kana kwamba mtuhumiwa ni mwanaye wa kumzaa.
Kwa upande wa mawazo ya kitoto ya Samson yeye alikuwa upande wa wale wanawake, alipenda asikie yule mwalimu kafungwa jela moyo wake ungetulia, alimulaumu baba yake kimoyomoyo kuwa kwanini anataka kulirahisisha lile jambo. Hata hivyo hakujua kuwa hayo mambo hata yeye yangemkuta siku si nyingi na tabia yake ya kufa na kuoza kwa wanawake.
Mwalimu mkuu na Mzee Mgaya waliagana huku Mzee Mgaya akisubiri majibu mazuri toka kwa mwalimu kwani namna Mzee Mgaya alivyopenda hela alipanga kupiga hela kwenye Lile jambo, kufa si kufaana?unajua nini Samson wewe hujui maisha ya mjini nataka nikuoneshe jambo nitahakikisha mshahara wa miaka miwili yule dogo ananipa Mimi, hawezi kuikosea familia yangu halafu nimuache.
Sasa baba kwanini msimshitaki?
aliuliza Samson
Acha ujinga wewe unadhani tukifikishana huko Mimi nitapataje hela, hebu tulia. Wakarudi ndani
Mzee Mgaya hili jambo sikubali liishie hapa, naona umekaa kimya tu hufanyi maamuzi yeyote, na mmechukuana kwenda kuongelea nje una maana gani? alilaumu Tausi.
Sasa wewe unataka kufanyaje una ushahidi gani kuwa huyu mwalimu mnayemsema, kuwa alitaka kumbaka huyu, huo siyo ushahidi hata kidogo ujue nyinyi sheria bado hamuijui , huyu binti Wala Hana maelezo yanayojitosheleza, najua mnamtegemea yule muuza nyama kama anaweza kuwa msaada kwenye jambo hili, hapana Wala hajawa shahidi bado.
Kwa maelezo yake hapa yeye aliona watu wakisindikizana Hadi kupotea machoni mwake, kilichoendelea mbele hakuona , je unawezaje kusema atakuwa shahidi?
Mtuhumiwa ana uwezo wa kukataa tu na akaachiwa huru, sisi kama sisi tunataka apewe onyo tu hata akikataa bado atakaa akijua kuwa tushamuelewa. Mzee Mgaya aliongea kwa mamlaka huku wanawake wakishindwa wafanyaje, na Samson alishindwa kumuelewa Mzee Mgaya mbona kama anakaa upande wa mtuhumiwa
Nini kitajiri, sehemu ijayo Ina majibu
Happy Valentine day jamiiforum.
Itaendelea....................
Happy valentines Day Eng. Jack Jack Daniel, pole na kijihoma hongera kwa kupumzika kupiga vyomboYes ni kweli niko free, baada ya kutoka mkoani nilikokuwa hata hivyo Niko home tu Kuna kijihoma kinanisumbua , nadhani hali ya hewa natamani tungepiga vyombo pamoja ila niko likizo kidogo na hivi vitu
Kwasasa Nina muda wiki nzima hivyo stori itawekwa vipande viwili kila siku
Ahsante sanaHappy valentines Day Eng. Jack Jack Daniel, pole na kijihoma hongera kwa kupumzika kupiga vyombo