MAPENZI YA DHATI
SEHEMU YA KUMI NA NNE:
Baridi kali ya Mbeya ilikuwa imemkataa motto wa Bite (Christian) kwa hali hiyo alipotimiza miaka miwili waliondoka na kurudi tena Iringa ambapo Bite alitaka kukaa kidogo halafu aende Mwanza kuweka makazi mapya huko.
Jambo la kushangaza licha ya baridi ya Iringa hali ya Christian ilianza kuwa njema kama awali jambo lililosababisha Bite aendelee kukaa katika mkoa huo.
Hadi anatimiza miaka mine hali yake kiafya ilikuwa njema sana na tayari Bite alikuwa amesahau suala la kwenda Mwanza. Akaanzisha genge la kuuza uji na karanga mida ya jioni na mihogo ya kukaanga majira ya asubuhi.
Ilikuwa biashara ndogo lakini iliyomuingizia kipato kizuri tofauti na matarajio yake.aliweza kupanga nyumba ya chumba kimoja na sebule aliyoishi na mwanae kwa furaha sana tu bila masumbufu yoyote hadi siku hiyo asubuhi alipokuwa anauza mihogo yake ambapo wanaume wawili ambao sura zao hazikuwa ngeni machoni pake walipofika eneo la biashara yake.Aliwapokea kwa furaha sana na bashasha kama wateja wengine aliozoeana nao.
Bite tukuone pembeni kidogo samahani lakini wawili wale walimvuta pembeni Bite
mh! Mikopo asubuhi asubuhi hamna kwakweli mtadhalilisha hizo suti zenu aliongea Bite kwa utani huku akiwafata walipo wawili hao
funga biashara tunaondoka na ukithubutu kupiga kelele au kukimbia nasambaratisha ubongo wako nadhani hujawahi kufikiria kifo cha namna hiyo,hivyo basi fanya kama unavyoagizwa aliambiwa Bite na wale wanaume huku mmoja akifunua koti lake jeusi la suti na kumwonyesha Bite kitu ambacho hakujiuliza mara mbili mbili kuwa ile ilikuwa ni Bunduki,
Kwa kuutambua uoga alioupata Bite,yule mwenye bunduki alimbandika kitu mfano wa kishikizo cha nguo na kumwambia hiyo ni sound recorder nenda ukawaambie wateja wako sisi ni ndugu zako tumekuletea taarifa za msiba nitakuwa nakusikiliza hapa, ole wako nasema ole wako usifuate maelekezo alipewa masharti hayo ya uongo Bite ambaye laiti isingekuwa pensi yake ya jinsi ambayo huwa anavaa kwa ndani ili kuhifadhia pesa zake za mauzo basi mkojo uliopenya bila yeye kujua ungemwagika palepale hadharani na wala asingepatwa ma aibu yoyote ile.
Kama alivyoagizwa aliwaeleza wateja wake wawili waliokuwa wanamalizia kuitafuna mihogo waliyokuwa wameinunua,wakampa pole za dhati .
jasho lilikuwa linamtoka alitamani kutumia ishara kuwaambia kwamba yupo katika hatari lakini alipowazia mdomo wa bunduki alikaa kimya kabisa,bila kificho Bite aliiogopa sana bunduki na hakupenda kumwacha Christian katika umri ule.
Tayari akili ilisharudi nyuma akatambua hasa,hao watu alikutana nao wapi,walikuwa ni baadhi ya wafanyakazi katika ile ngome aliyekaa miaka miwili na ni hao waliomleta Adam pale ngomeni
nimekwisha mimi Beatrice alijiwazia Bite huku akitetemeka.
Baada ya kuifunga biashara yake aliwafuata akiwa na mwanae amemshikilia mkono.
nadhani unajua hatuhitaji mtoto!!! Tunakuhitaji wewe tena sasa hivi aligombezwa Bite na bila kujijua akajikuta akimwacha mwanae pale
Christian narudi sawa nisubirie pale sokoni sawa mwanangu!
haya mama alijibu Christian kwa furaha kwani alijua amepata fursa kubwa na ya kipekee kwenda kucheza na watoto wenzake pale mtaani
ulidhani unaweza kutuzidi ujanja sisi,umepotea sisi hatupimiki hata kidogo umeumia tena umeumia sana aliambiwa Bite na wale wanaume wakiwa kwenye gari kuelekea kwenye gari kuelekea kule katika ngome jambo hilo Bite hakulitamani hata kidogo,japo alimpata Christian kwa bahati mbaya lakini alikuwa akimpenda sana kutoka moyoni na hakuwa tayari kutenganishwa naye kwa namna yoyote ile.
Alijiuliza maswali mengi sana ni nani atakayempa chakula mwanaye siku hiyo na nyingine zitakazoendelea wakati yeye hayupo,michezo ya kukimbizana aliyoipenda Chriss pia ilimtia hofu Bite na kuhisi huenda mwanae anaweza kupoteza uhai wake kwa kugongwa na gari.
Funda la hasira lilimkaba kooni alitamani kufanya lolote lile wakati huo lile jambo liwe ndoto kwake, machozi yaliyotoka ndio yaliyeyusha lile fundo japo kidogo,hasira kali ilikuwa imemkaba Bite aliyekuwa amekaa siti ya nyuma na jamaa mwenye Bunduki katika koti lake lakini maskini hakuwa na la kufanya hadi gari lilipoingia ndani ya ngome ile
* * * * *
Macho ya Reshmail yalitawaliwa na taswira ya yule mtoto Christian, zilikuwa ni siku nyingi zimepita tangu afungue album yake kumwangalia mpenzi wake (Adam) aliyeaminika kuwa tayari ni marehemu.Ni katika usiku huu alipokuwa akipitia album ya Eveline ndipo tena anakutana na picha ya Adam ambayo yeye (Adam) alimpa Eveline walipoenda Mwanza.
Eveline,Eveline,Eve
.huyu hapa ni nani???
we umechanganyikiwa tena eti hebu acha mambo yake ya ajabu huyu Adam Alijibu Eve kwa uoga.
na tuliyemwona leo kule sokoni ni nani?? aliuliza Reshmail
we Reshmail jamani wanafanana Mungu wangu mbona wamefana hivyo lakini eeh!! Eve alijikuta picha ya mtoto Christian ikiumbika kichwani mwake na Zangu kwa sababu nimekaa naye hadi saa nne tumemsubiri huyo mama yake aje wapi!! Nikaona isiwe shari ngoja nimpeleke polisi penye usalama kuepuka balaa kumbe na nyie hamjui ni wa nani he!! alitoa maelezo hayo yule mama na kueleweka vyema kwa Reshmail na Eveline.
hicho kituo cha polisi umesema kipo wapi? aliuliza Eve
kile pale kinaonekana hata kwa hapa,lile jingo la bluu nyuma yake alielekeza yule mama
Ndani ya dakika tano tayari Reshmail na shoga yake walikuwa mbele ya mapokezi ya kituo cha polisi Iringa mjini, na walikuwa kwenye foleni wakisubiri zamu yao ya kuhudumiwa ifike.
nyie ni ndugu zake? Au mmoja wenu ndio mama yake?
hapana sisi si ndugu zake ila
aliishia njiani katika maongezi yake Resh baada ya kukatishwa na yule askari ila nini? Yaani nyie wanawake wa siku hizi suala la kujali watoto wenu hamtaki kabisa kulisikia mnachojali ni urembo tu wa sura zenu
jamani sio kwamba kuna ndugu yake hapa kati yetu ila sisi tumemkuta jana kule sokoni ndio tumemnunulia chakula halafu tukajiondokea zetu,leo hii ndio tunapita pale kwa mama Fred yule mwenye mgahawa yeye ndiye ametupatia taarifa hiyo tukaona sio vibaya nasi tukifika kumwona huyo motto aliongea Eve aliyeonekana kutokuwa na hofu na kituo cha polisi lakini Reshmail alikuwa ana uoga kwa mbali kama vile anatuhumiwa kwa lolote lile.
haya yupo tumemuhifadhi na tumepeleka taarifa kwenye vyommbo vya habari wataanza kutangaza kama mama yake bahati mbaya haya atakuja kumchukua na kama amemtelekeza akajiandae kwenda kuishi kwa watoto yatima sisi hatuna uwezo wa kuhifadhi watu hapa zaidi ya mahabusu alijieleza askari yule huku akijipepea joto kwa kutumia kofia yake iliyochakaa
Majuma mawili yalipita bila mama wala ndugu wa motto kupatikana licha ya kituo cha redio maarufu mjini iringa cha Ebon fm kutangaza kila siku bila kukoma
Eve naenda kumchukua yule motto nafsi yangu inanishauri hivyo na ni lazima nifate ambacho nafsi yangu inaniamuru Reshmail alimwambia Eve siku moja wakiwa wamekaa sebuleni wakiangalia habari katika luninga.Eve alikuwa amejenga tabia ya kutobishana na rafki yake huyo kwani furaha yake ilikuwa ni kumwona Reshmail akiwa na furaha tele
lakini Resh,mama yake si atamtafuta ssana??
Eve yaani imetangazwa hivyo redioni na hajajitokeza leo hii mie tu kumchukua ndipo ajitokeze? Looh! Acha nae ahangaike kidogo alijibu Reshmail kwa jeuri
mh! Haya sikuwezi mwanasheria wangu
Polisi hapakuwa na usumbufu ni wazi kwamba walikuwa wamechoshwa na matukio ya watoto kutelekezwa na wazazi wao pasipo sababu zilizo wazi,hivyo kitendo cha Resmail kuamua kumchukua Christian ilikuwa ahueni kwao.aliandiokishwa maelezo mafupi tu kabla ya kuruhusiwa kondoka na mtoto ambaye alikuwa dhaifu tayari kutokana na lishe duni na upweke wa kutomuona mama yake kwa siku hizo zote.
Reshmail alikuwa ameyafurahia sana maisha ya Iringa,kampani kubwa kutoka Eveline na mchumba wake ilibeba nusu ya furaha yake huku nusu nyingine ikikamilishwa na uwepo wa Christian mikononi mwake,mara kwa mara alipenda kuwa naye karibu huku akimwita mume wako jambo lililompa faraja kubwa moyoni
Eve jamani nitakumiss kipenzi changu lakini nitarudi tena asanteni sana kwa ukarimu wenu mlionionyesha tangu mwanzo nimeishi kwa furaha kubwa sana hapa Reshmail aliyazungumza hayo alipokuwa anawaaga Eve na Benny usiku ambapo kesho yake alitegemea kurejea Dar-es-salaam akiwa ameandamana na Christian mtoto aliyempata katika mazingira ya kutatanisha
Kwa Christian safari ya kutoka Iringa kwenda Dar ilikuwa safari yake ya kwanza ndefu zaidi kuwahi kusafiri
Siku iloyofuata wawili hawa walikuwa ndani ya basi la budget litokalo Mbeya kwenda Dar likipitia Iringa.
Mama alisema baba yupo pale kwenye ile nyumba, tushuke nikamsalimie! Chriss aliongea hayo huku akielekezea kidole chake kwenye jingo lililoonekana kwa mbali mno kutokea pale barabarani na hapakuwa na dalili ya kuishi mtu pale hivyo Reshmail akachukulia kuwa ni akili ya utoto imemtuma Chriss kuzungumza akaamua kupuuzia
chriss alikwambia nani we muongo!!
alinambia mama siku moja hivi tulipita hapa ,halafu mama alinikataza kusema uongo ni dhambi alijieleza Christian haraka haraka
mh! Haya tutakiuja siku nyingine sawa mfalme wangu Reshmail alimjibu Chriss ili kumlidhisha kwa aliyokuwa anasema
** ** ** **