Mjema Vushanje
Senior Member
- Sep 24, 2017
- 158
- 355
SIMULIZI YA MAMA MBISSE!
Hii ni simulizi aliyowahi kunisimulia Mama Mbisse ambayo nikiifikiria nakuwa nawaza sana kuhusu mambo ya dunia hii.
ILIANZA HIVI…Baada ya mimi kuondoka kijijini siku nyingi nikiwa niko mjini kwa ajili ya msomo na shughuli zangu siku moja niliamua kurudi kijijini.
Japo wazazi wangu walishafariki na hivyo kule kijijini kuwa hakuna mtu anayeishi isipokuwa shangazi yangu bado nilikuwa nawiwa kwenda kule kwani napakumbuka sana sehemu niliyokulia.
Nilipofika kijijini nililala kwa shangazi yangu siku ya kwanza nay a pili kisha nikaaga kwenda kumsalimu Mama Mbisse ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Mama yangu kwani hata kazi walikuwa wanafanya pamoja wote wakiwa ni manesi wa hospitali moja kule kijijini kwetu.
Nilipofika kwa mama mbisse nilibisha hodi nikakaribishwa na binti yake wa mwisho aliyekuwa anaitwa Joy ambaye kwakweli nilimuacha zamani akiwa mdogo sana lakini kwasasa kwakweli Mashaalaah mtoto amekua kweli…
“Haaa jamani Kaka Jahanne”
Basi Yule binti alikuja akanirukia na kunikumbatia kwa upendo.
Wakati sijamalizana nae kisalamu mlangoni alitokea mama Mbisse mwenyewe ambaye nae alistaajabu sana kuniona.
Alinijia na kunikumbatia huku akilia kifuani kwangu.
“Karibu Johanne, Karibu sana, nimefurahi sana kukuona mwanangu”
Nilisikia majimaji yakichuruzika begani kwangu kumbe yalikuwa ni machozi ya Mama Mbisse nikabaki nikijiuliza…Ina maana mama mbisse analia kwa furaha kwasababu ya kuniona mimi!
Nilimsihi anyamaze lakini kila nilipomsihi hakunyamaza isipokuwa alikuwa akilitaja jina la mama yangu akisema amemkumbuka sana Rafiki yake.
Kwakweli alipomtaja mama hata mimi huzuni ilimijia na machozi yakawa yanakaribia ila nikajitahidi sana kuyazuia.
Mama Mbisse aliniacha pale nje nikiwa nimekaribishwa kwenye kiti kisha akaingia ndani kwake ambapo alikaa mud asana.
Hapa nje nilikaribishwa supu ya Kondoo kwani kumbe walikuwa wamechinja kondoo jana yake hivyo ikawa kama nimefika wakati muafaka. Basi niliendelea kunywa ile supu na ndizi za kuchoma hadi niliposhiba na kumshukuru Joy ambaye alikuwa ameketi pembeni yangu.
“Hivi Joy uko darasa la ngapi saivi?”
“Niko form Three kaka, Je wewe unafanyaje huko mjini?”
“Anhaa mimi nimemaliza chuo na sasa naendesha shughuli zangu binafsi na mimi ndie mmiliki wa Blogu ya ….”
Nilipoitaja tu hiyo Blogu aliifahamu na nilijua ataifahamu kwani ni maarufu sana.
Wakati tunaongea alitoka Mama Mbisse ndani nikamshukuru sana kwa ajili ya chakula alichonipatia nae akashukuru kwa mimi kushukuru.
“Mpe Pombe apoze koo kidogo” Joyce aliambiwa na mama yake.
Nilitaka nikatae lakini nilishindwa kwani kwa utamaduni wa kule kwetu ni heri ukatae chakula uwapo mgeni lakini sio Pombe.
Basi Joyce alitoka na chombo kilichojaa Pombe kisha akanywa kidogo na kunipatia nikapokea na kuinywa ile Pombe hadi ikaisha.
Wakati Joyce ametoka kurudisha Chombo nilichonywea Pombe alikuja pale nilipo na kuniambia “Mama anakuita”
“Yuko wapi?”
“Twende nikupeleke”
Basi Joyce alitangulia mbele na mimi nikafwata nyuma, tulikatisha pale sebuleni tukapita kama milango miwili hivi katika ile korido ikionyesha kuwa ni milango ya Vyumba vya kulala na hatimaye tukafika kwenye chumba cha mwisho kabisa ambapo nilimkuta Mama Mbisse amelala kitandani.
“Karibu Johanne”
“Asante mama” Niliitikia ile asante huku nikiwa nimesimama kwani tofauti na kitanda hakukuwa na sehemu nyingine ya kukaa.
“Karibu kaa hapa kitandani…wewe Joyce tupishe sasa” Alisema mama MBISSE.
Nlishtuka kidogo kukaribishwa pale kitandani lakini kilichonishtua zaidi ni baada ya Joyce kuambiwa atupishe.
Niliwaza sana lakini kuna mawazo niliyakataa kabisa akilini kwangu kuwa haiwezekani ikawa hivyo.
Nilikaa vizuri pale kitandani kisha nikamgeukia mama Mbisse pale kitandani na Kuanzisha mazungumzo mimi mwenyewe.
“Za siku nyingi mama yangu”
Niliposema hivyo mama Mbisse alinyanyuka na kusogea pembeni kidogo ya kitanda ambapo kulikuwa na kimkoba kidogo kisha akatoa karatasi Fulani iliyokuwa imekunjwa vizuri kwenye bahasha kisha akanikabidhi mkononi.
“Isome” aliniambia Mama Mbisse!
KAMA UNATAKA NIENDELEE NAOMBA UKOMENTI ENDELEA ILI NIIMALIZIE LEO LEO!