Simulizi: Kwanini Mimi? 02

gilbert35

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
247
474
Kwanini Mimi ep
SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 02
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI: Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611

Tulipoishia - Wakati ayo yanaendelea.Hans kijana aliyetoka kufanya mapenzi na mama tatu,Mwili wake haukuwa sawa.Alihisi kama amepungukiwa na kitu. " mmmh! Mbona mwili wangu haupo kawaida.Mbona kama nimepungukiwa na kitu flan" aliwaza Hans.

Endelea nayo.

" Kwanini mwili wangu upo hivi? Kuna kauzito flan nakasikia , pamoja na uzito ninao usikia lakini kuna kitu kama kimepungua kwenye mwili wangu" aliwaza Hans. Aliendelea kujiuliza lakini hakupata majibu.

" mmmh! Au ni uchovu unaotokana na kufanya mapenzi? ,Ngoja nikaoge kwanza labda ninaweza kuwa sawa" aliwaza john huku akifungua mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani.

......

Twende kwa mama tatu na mumewe.

Mama tatu alitoa nguo zake chumbani kwao na akaweka mazingira sawa.Baada ya kuona kila kitu kipo sawa.Alimuaga mumewe.

" baba tatu mume wangu?"

" Niambie mke wangu"

" kila kitu nimekiweka sawa.Mimi naondoka nakuacha .Sitaki monica anikute hapa "

" sasa unaenda wapi?"

"Naenda kwa mama nasra pale kupiga story"

" ok poa. Mimi ngoja nimsubiri huyu mrembo.Ameniambia ameshapanda pikipiki."

" Ok sawa,me naondoka basi"

" poa" .Mama tatu aliondoka kuelekea kwa shoga yake aitwae mama nasra.Haukupita muda monica akawa amefika.Baba tatu alimfungulia geti akaingia ndani.Monica alishangaa uzuri wa ile nyumba.

" mmmh! Unataka kusema unaishi bila mke kwenye hii nyumba nzuri hivi?" aliuliza monica.Tamaa ya kuwa mama mwenye nyumba ilimuingia.Hakuwahi kamwe kufikiria kama atakuja kuingia kwenye nyumba kama ile.

" Siishi peke yangu.Naishi na mdogo wangu ambaye unawasiliana naye mara nyingi." alijibu baba tatu.Nyumba yao ilikuwa ni kubwa na ya kifahari. Ilikuwa ina fensi matata sana.Baba tatu aliongozana na monica hadi ndani.Walipiga story mbili tatu kisha wakaelekea moja kwa moja chumbani.

......

Kwa upande wa mama tatu alikuwa kwa shoga yake akipiga story. ." mmmh shoga yangu unajua maisha yenu mimi siyaelewi?,japokuwa mnajaribu kufanya siri,lakini saizi hakuna siri.Watu wengi wameshajua.Na kila aliyejua anajiuliza kwanini mnafanya hivi?" aliuliza mama nasra.

"Mmmmh! Mama nasra na wewe umesheanza.Tunafanya hivi kivipi?,sisi hatuna sababu yeyote zaidi ya upendo.Nampenda mume wangu na ninapenda aburudike,na Ndio mana nikiona msichana mzuri namtongozea "

" mmmmmmh!"

," acha kuguna.Ngoja nikuulize swali?"

" uliza tu?"

" Hivi kumpenda mtu maana yake si unataka uyo mtu aishi vizuri na ajisikie burudani?"

" Ndio ,iyo ndo maana yake"

" Sasa kama iyo ndo maana yake. Kwanini nyinyi mnatushangaa sisi.Sisi tunapendana ,na tunataka kila mmoja wetu afurahie maisha.Ndio mana tunafanya hivi"

" Mmmmh! Siyo kweli shoga.Kwenye mapenzi ayo mambo hayapo.Halafu ujue siku hizi magonjwa ni mengi sana.Hamjui mnaweza kuwa mnajitafutia magonjwa?"

" aaaah! Magonjwa hayawez kutupata sisi" aliongea kwakujiamini mama tatu.

" Shauri yenu.Halafu mtaani watu wameanza kusema mna ukimwi hivyo,mnausambaza makusudi? Wanasema mnafanya hivi kwasababu mnaukimwi ndio mana"

," sio kweli shoga .Hatuna ukimwi wala nini"

" Sasa kama hamna ukimwi.Kwanini mnafanya hivi?

" ilo mbona nilishakujibu.Ni upendo tu.Hakuna lingine" alijibu mama tatu.

Mama tatu na shoga yake , waliendelea kupiga story kwa muda mrefu sana.Mama nasra alikuwa anajaribu kumdodosa mama tatu ili amwambie sababu ya wao kufanya vile.Kila alipomdodosa alipewa majibu ambayo hakuridhika nayo.

.........

Monica na baba tatu baada ya kufanya yao,Monica alinogewa.Hakutaka kuondoka .Alitaka alale pale pale.Baba tatu alijaribu kumshawishi aondoke lakini monica alikuwa mbishi.

" sikiliza baby.Hatukukubaliana wewe ulale hapa leo.Kama unataka kulala hapa,inabidi uniambie mapema ili nijipange."

"Mmm!h! Hujipange nini mpenzi.Yaani mimi kuja kulala hapa tu mpaka ujipange,Hapana bana.Leo mimi siondoki hapa.Leo nalala hapa hapa" alijibu monica.

Kitendo cha monica kungangania kulala pale kilimkera baba tatu.Alimwangalia monica kwa jicho kali sana.". Kama tabia yako ndo hiii,mapenzi yenyewe mimi na wewe yatakuwa ndio basi.Haiwezekani yaani tumekutana siku moja tu halafu ukangangania kulala hapa hapa"

" mmmmh! Yaani ndio umekasirika "

" ndio umenikera.Hatukupanga wewe kuja kulala hapa.Kwanini unganganie "

" basi mpenzi.Sitaki kukuuzi.Ngoja niondoke." aliongea monica huku akisimama na kuvaa nguo zake.Alivaa nguo na kujiweka sawa tayari kwa kuondoka. ." mimi nipo tayari mpenzi wangu" aliongea monica.

" Sawa.Basi shika hii itakusaidia." aliongea baba tatu ,huku akimpa monica noti nne za elfu kumi kumi.

" asante mpenzi" alijibu monica.Baba tatu alimpigia simu dereva boda boda aje kumchukua monica.Alimsindikiza hadi getini nje.Haikuchukua muda dereva boda boda akawa amefika na kumchukua.Monica alipanda kwenye boda na kuondoka.Wakati anaondoka aliiangalia nyumba ya baba tatu kwa uchu sana " nitafanya kila niwezalo nije kuishi katika hii nyumba" aliwaza monica.

Lakini akiwa njiani monica alihisi mwili wake kama umepungua kitu flan." mmmmh! Mbona siko sawa. Kuna nini? Mbona kama mwili wangu unatatizo flan! Au janaba la ngono linanisumbua?" aliwaza monica.Haikuchukua muda akawa amefika nyumbani kwao.Alishuka kwenye piki piki na kuingia ndani.

Lakini wakati anashuka kwenye pikipiki mama yake alimuona.

" mmmmh! Monica.Tabia ya kuletwa na mapikipiki usiku imeanza lini?"

" mama saizi nimekuwa mtu mzima.kwanza nimepata mchumba.Siku sio nyingi nitaolewa" alijibu monica huku akiingia ndani.

"Sasa mwanangu kama umepata mchumba si inabidi umlete kwanza tumuone." aliongea mama yake monica.Wakati anaongea ayo monica hakumsikia alikuwa ameshaingia ndani.

BAaada ya monica kuondoka.Baba tatu alichukua simu na kumpigia mkewe .

" Njoo bana.Kazi imeshaisha huku" aliongea baba tatu.

" mmmmh! Mara hii.Mapenzi gani ayo ya kufanya haraka haraka ivyo. vipi umeenjoy lakini?

" Ndio,sema tatizo mwanamke mwenyewe kinganganizi huyo.Eti alitaka alale hapa hapa"

"Aaah! Yaani kuja leo tu anataka kuhamia kabisa?"

" Ndiyo ivyo,ila nimemlia ngumu.Nimemuondoa kwa lazima."

" ok safi,nakuja basi mume wangu?" alijibu mama tatu,kisha akamuaga shoga yake mama nasra na kuondoka.

.............

Majira ya saa tisa usiku.Mama tatu alimuamsha mumewe .

" baba tatu,baba tatu.Amka muda umefika.Amka" aliongea mama tatu huku akimtikisa mumewe .

" mmmmh! Niache nipumzike kidogo"

," upumzike wapi? Utaleta matatizo wewe? Muda umefika mume wangu amka" aliongea mama tatu huku akiendelea kumtikisa mumewe.Baba tatu aliamka kisha wote wawili wakaelekea bafuni kuoga.

Baada ya kuoga ,Mama tatu na baba tatu walifungua mlango na kuingia kwenye chumba chao maalum.Mama tatu alivua nguo zote na kujilaza kwenye meza ya chuma iliyokuwa mle ndani.

= kuna nini? Baba tatu na mama tatu wanafanya nini kwenye chumba chao cha siri?, kwanini walale kwenye meza ya chuma? =
Full vipande vyote 27 vinapatikana kwa buku tu kupitia WhatsApp namba 0621249611
Namba ya Malipo ni HALOPESA NAMBA 0621249611
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom