SIMULIZI: JUMBA JEUSI

SIMULIZI: JUMBA JEUSI

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2022
Posts
2,229
Reaction score
4,345
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
Storyteller: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

UTANGULIZI.....
EPISODE 1.


BANZOKA
Pembezoni mwa barabara ndogo ya vumbi ambayo ilikuwa inaingia kwenye kichaka kilichokuwa kimemezwa na miti ya kutosha, mwanaume mmoja alikuwa akijikokota huku akiwa anavuja damu kwa wingi. Alikuwa anauburuza mguu wake ambao haukuwa kwenye hali nzuri kabisa, mguu wake ulikuwa una alama za kukatwa na makovu kadhaa ambayo hayakumfanya bwana huyo kuwa kwenye hali nzuri kiafya.
Hatua zake hazikuwa za kuridhisha kabisa kwa sababu alionekana kuwa mtu ambaye alitembea kwa muda mrefu bila kuwa na msaada. Alionyesha hofu usoni ambayo iliufanya hata moyo wake kwenda mbio kiasi cha kupiga mpaka kwenye kifua chake hata mtu ambaye angekuwa umbali kadhaa kutoka mahali ambapo alikuwepo basi angetambua kwamba bwana huyo alikuwa amemezwa na taharuki ambayo ilimnyima raha na amani kiasi cha kumpatia mawazo ya namna hiyo.

Sura yake haikuwa ikionekana vizuri huenda kwa sababu ya kiza ambacho kilikuwa kimelimeza lile eneo ukijumlisha na miti ambayo ilizungukia eneo hilo ndiyo kabisa ilizalisha kiza na kulifanya kuwa tulivu isipokuwa hatua za bwana huyo ambazo hazikuwa na umakini kwa sababu ya kukosa utaratibu maalumu kwani alikuwa akiumia. Kwa mwonekano wake wa mbali hakuwa mtu mwepesi, alionekana kuwa shupavu na shababi ambaye mwili wake ulikuwa umeshiba vilivyo kama sio kwa mazoezi makali basi bwana huyo alikuwa amezoea maisha magumu ama yale maisha ambayo hayana utulivu kabisa ndani yake.

Tafsiri ya maisha yake ilikuwa inakuja kwa namna alivyokuwa na hali ambayo alikuwa nayo kwa wakati huo, alikokuwa ametoka kwa nyakati hizo hakukuonekana kuwa na usalama wa kutosha ndiyo maana hali haikuwa inavutia kwa upande wake. Alisikika akiwa anahema kwa nguvu, ile sauti yenye kitetemeshi ndani yake mithili ya mtu ambaye alikuwa anautua mzigo mzito ambao aliubeba kwa muda mrefu kwenye mwili wake na moyo wake kwa ujumla. Mbalamwezi ilichanua nyakati hizo na kusababisha mwanga kwa mbali ambao ulifanya hata lile jasho lake kuchuruzika na kumpa nafasi ya kuona umbali mdogo ambao hata yeye mwenyewe hakuonyesha kama umbali huo ulikuwa unaenda kuwa na msaada kwa upande wake yeye.

Aligeuka nyuma mithili ya mtu ambaye alikuwa anahakiki jambo ama kuna kitu alikisahau huko ambako alitoka, aligundua kwamba hakukuwa na usalama wa kutosha kwani mwili wake haukuwa na utulivu, alikuwa anapata misisimko ambayo ilizidi kumpatia tahadhari juu ya eneo ambalo alikuwepo, mpaka wakati huo alitambua kabisa kwamba lilikuwa ni suala la muda tu kuweza kufikiwa mahali ambapo yeye alikuwepo. Mwili wake ulikuwa kama unashindana na nguvu zake za kutembea kwani alijihisi kama ana kizunguzungu kikali kwa nyakati hizo, kilikuja katikati ya hiyo safari yake na kwenye kumbukumbu za maisha yake hakuwahi kufikiria kama aliwahi kuwa na tatizo la namna hiyo kabla.

Alitikisa kichwa ili aweze kuwa sawa ila alihisi kama anaona nyota mbilimbili mbele yake, alishika kichwa huku akiwa anaguna kwa maumivu ambayo yalitosha kumfanya jicho lake kutoa chozi bila kupenda. Bwana huyo alijigeuza akiwa anazunguka hiyo sehemu na maumivu yake, hapo ndipo mwili wake ulionekana vyema. Upande wa ubavu mmoja ulikuwa na kisu ambacho kiligota hapo, kwenye mgongo wake kulikuwa na nondo fupi ambayo ilisalia kwenye huo mwili wake lakini pia upande wa nyuma wa shingo yake ulikuwa umetobolewa kidogo eneo ambalo lilikuwa linatoa damu taratibu. Mwili wake ulionekana kuchakaa vya kutosha kwa kipigo ukiacha upande wa mbele ambao alionekana aliulinda ipasavyo ndiyo maana ulionekana kuwa ngangali bado.

Bwana huyo ile hali ilionekana kabisa kumuelemea pale alipokuwepo, hakuweza kusimama tena kama mwanzo, aliyumba yumba na kujisogeza mpaka pembezoni eneo ambalo lilikuwa na mti mfupi na mnene. Alidondokea upande wa pili na kuegamia mti huo huku akiwa bado anahangaika na maumivu ya mwili, kichwa ambayo kwa pamoja yalikuwa yanashindana na mawazo yake.
“Zyra” alitamka jina ambalo lilionekana kuwa la kike kwa sauti yenye kitete lakini ambayo ilishiba vya kutosha, alilitamka neno hilo kwa sauti ndogo na nyepesi ila ule uzito wake ndio ambao uliifanya isikike kwa mbali. Haikueleweka sababu ya mtu huyo kuweza kulitaja jina hilo tena akiwa sehemu kama hiyo ambayo ilionekana kutokuwa salama kabisa kwa upande wake. Huenda lilikuwa ni jina ambalo ndiyo ilikuwa sababu ya yeye kuishia sehemu ama eneo hilo ama lilikuwa ni jina ambalo lilikuwa na maana kubwa kwenye maisha yake, kwa nyakati hizo ni yeye pekee ambaye alikuwa ana majibu ya sababu za kulitaja jina hilo eneo kama hiyo na wakati kama huo.

Aliketi kwa kuuegamia huo mti lakini akiwa anahangaika na maumivu makali ambayo yalimvaa huku akijua kabisa maisha yake yalikuwa kwenye hatari kubwa, akili yake ilimrudisha nyuma dakika kadhaa ambazo zilikuwa zimepita. Bwana huyo alikuwa anakimbia kwa spidi ambazo kama mtu ambaye alikuwa anamfukuza asingekuwa na kasi ya kutosha basi abadani asingempata kwenye maisha yake yote. Alionekana kukimbia ili kuiponya nafsi yake ambayo haikuwa na usalama wa kutosha kwa nyakati hizo, alitamani kama angekuwa anafukuzwa na mtu mmoja ama wawili lakini haikuwa hivyo, walikuwa ni wanaume wapatao sita ambao walikuwa wapo nyuma yake kula naye sahani moja.

Ile miondoko yake ambayo ilikuwa inakatisha tamaa kwa wakimbizaji, haikufua dafu kuweza kuwafanya wanaume hao kughairi safari ya kumpata bwana huyo. Akiwa anaendelea kukimbia ni kama mwili wake ulianza kuchoka mpaka akahisi ile hali haikuwa ya kawaida kwake, hakuwa mbovu namna ile kiasi kwamba kwa muda mfupi tu aweze kuwa na ule uchovu. Akiwa anaendelea kujiwazia huku akiwa anaendelea kuikata nyika ndipo alihisi hali isiyo ya kawaida, ni ile hali ya mvumo wa upepo, ni kama ilizidi kwa upande wake, alihisi kuja jambo zito nyuma yake hivyo alijivutia pembeni ambapo kulikuwa na mti. Kujivuta kwake kulimsaidia kuikwepa nondo moja ndefu kiasi na yenye makali ya kutosha ikaenda kukita kwenye mti mdogo ambao ulikuwa mbele yake kiasi kwamba nondo hiyo ilizama na kutokezea upande wa pili.

Kama ingefanikiwa kuingia kwenye mwili wake basi mpaka muda huo asingekuwa hai kwa namna yoyote ile. Alihema na kuendelea na safari yake kwani alikuwa ameshaanza kuvisikia vishindo vizito vikiwa vinakuja karibu na alipo tena wahusika wakionekana kuwa na usongo mkali na huyo bwana kama wangempata. Kila ambavyo alikuwa anajaribu kukimbia ndivyo ambavyo mwili wake ulizidi kuwa wa utofauti mpaka yeye mwenyewe akaanza kujitilia shaka na hizo harakati zake za kujiokoa. Kujiuliza uliza mara mbili mbili wakati ambao alitakiwa kuyapambania maisha yake kwanza likawa kosa lake la maisha ambalo kila dakika ilivyozidi kwenda mbele alianza kulijutia kwa maumivu makali.

Ule wakati ambao aliutumia kuwaza ni wakati ambao alikuwa amefikiwa, alichotwa kwa nguvu kubwa na kwa sababu hakuwa na balansi ya kutosha, bwana yule alibaki anaelea hewani huku akitoa sauti ile ya mshtuko wa kutoamini bado kama jambo hilo lilikuwa linamfika hizo nyakati eneo ambalo yeye mwenyewe alitambua kwamba hakuwa na msaada kutoka kwa mtu yeyote yule zaidi ya mikono yake na mbio zake tu pekee. Alitua kwa sarakasi nne ambazo zilimfanya kuyumba kwani hakutarajia, muda ambao alikuwa anaendelea kujipanga alihisi kama kuna kitu kimezama kwenye mwili wake hapo akaundua kwamba ni nondo fupi ilipita nyuma ya tumbo. Alipiga hesabu za kujivuta mbele zaidi ila huko ndiko kulioonekana kuwa na hatari kubwa zaidi ya nyuma.

Alikutana na mguu ambao ulitua kwenye shingo yake, ule mguu ulikuwa mithili ya mtu ambaye alikuwa anapiga mpira aina ya volley. Damu ilimtoka mdomoni bila kupenda huku akiwa anatokwa na jasho jingi na nondo ikiwa kwenye mwili wake. Alisogea pembeni akiwa anahema kama kuku ambaye aliwekwa kati kwa ajili ya kuliwa na wali, hapo ndipo akawaona hao mabwana ambao walikuwa wanayahitaji maisha yake kwa nyakati hizo. Walikuwa watatu, wawili mbele na mmoja nyuma, moyo wake ulipiga kite baada ya kugundua kwamba aliingizwa kwenye mtego mwingine uliohitaji muda wa kutosha kuweza kuutegua lakini kwa habati mbaya hata huo muda hakuwa nao. Aligundua kwamba wanaume hao walikuwa sita tangu mwanzo, sasa hao watatu walikuwa wapi? Haukuwa muda sahihi kwa yeye kuweza kulijibu hilo swali lake zaidi ya kuweza kuyapigania maisha yake.

“Ulitakiwa kulihama hili taifa wakati ambao ulikuwa na nafasi, unajua kabisa ambacho kimewatokea watangulizi wako ambao wamewahi kuwa kwenye hiyo nafasi yako lakini bado ukaleta jeuri. Maisha hayaendi hivyo ndugu yangu, ona sasa muda huu unaenda kufa tena kama mbwa bila msaada ndani ya kichaka kidogo kama hiki kisicho na sifa hata ya kuitwa msitu” alitamka bwana mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo zilizokuwa nzito lakini kwa upande wake hata huo uzito haukuwepo kabisa, alikuwa anaongea na mtu aliyekuwa katikati yao akiwa hana mahali pakwenda. Walionekana kutambuana kwenye maisha mengine ambayo yalipita ila kwa wakati huo ni huyo mwanaume mmoja ambaye alitakiwa kuyapigania maisha yake kutoka kwa hao mabwana.

Hakuwapa nafasi ya kuwajibu maneno yake ya thamani kwani alijua kabisa kwamba hayakuwa na msaada wowote kwa upande wake. Alizikunja ngumi zake kwa ustadi na kuwanyooshea wanaume hao ambao walimfuata kwa pamoja pale kati. Alikimbilia mbele na kuinama akipiga goti ambapo alijilaza kabisa na kughala ghala huku akiwa makini ile nondo isizidi kuingia ndani kiasi kwamba wale mabwana wakapishana naye akaibukia upande wa pili, hakusimama, bali zilikuwa ni mbio ambazo zilitakiwa kumponya. Kwenye kukimbia kwake ndiko ambako kulimponza kwa sababu baada ya sekunde thalathini tu alirudi nyuma kwa hatua kama kumi baada ya kukutanishwa na kitu ambacho yeye alihisi ni kama nyundo nzito imetua kwenye kifua chake.

Ndiyo kwanza kabisa naifunua episode ya kwanza ya simulizi hii bora mno ya JUMBA JEUSI. Ni simulizi ambayo ina mengi ya kutupatia ndani yake, utaisoma siasa kwa undani zaidi na namna inavyofanya kazi hususani kwenye mataifa ya Afrika hivyo nakusihi ungana nami kuanzia mwanzo mpaka siku ambayo nitatua nukta ya mwisho na kusema nimeimaliza rasmi.

Nyuma ya kalamu ni mwandishi wako pendwa wa siku zote, FEBIANI BABUYA wao wanapenda kuniita Bux the storyteller.

Wasalaam.
 

Attachments

  • Jumba JEUSI.jpg
    Jumba JEUSI.jpg
    272.4 KB · Views: 28
####JE WEWE NI SHABIKI NA MPENZI WA SIMULIZI ZA KIJASUSI NA KIPELELEZI?

Kama jibu ni ndiyo basi mwandishi FEBIANI BABUYA ni suluhisho la matatizo yako na kiu yako kwenye ulimwengu wa maandishi.

#### JIPATIE SIMULIZI BORA ZA KIPELELEZI KWA BEI AMBAYO NI RAFIKI KABISA LAKINI UNAPATA BURUDANI, ELIMU pamoja na UTAMBUZI wa DUNIA HII YA SIRI, SIASA na MAPIGANO ambavyo vyote vinaelezewa kwa undani kwenye simulizi hizi za KIJASUSI.


########SIMULIZI HUSIKA NA BEI ZAKE👇


1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA...4000

2. I WANT TO DIE JUDGE...4000

3. GEREZA LA HAZWA...5000

4. INNOCENT KILLER (THE REVENGE)/ MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI)...5000

5. NYARAKA NAMBA 72/ DOCUMENT NUMBER 72...4000

6. ELECTION SAGA MONEY IN BLOOD (SAKATA LA UCHAGUZI PESA KWENYE DAMU)....4000

7. JIJI LA KAMARI....4500

8. BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)....4500

9. NAFSI ZILIZO TELEKEZWA ....5000

10. IDAIWE MAITI YANGU....4500

11. THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (SEASON 2 YA IDAIWE MAITI YANGU)....5000

12. JUMBA JEUSI ....4500

13. SIKU ZA MWISHO (SEHEMU YA MWISHO YA IDAIWE MAITI YANGU)- THE DARKNESS OF AN ANGEL .....5000

14. TONE LA DAMU (THE JOURNALIST)...5000

15. KARATA YA MAUAJI.....5000


#UNAWEZA KUZIPATA KWA KULIPIA KWA NAMBA HIZI HAPA AMBAZO NI ZA MWANDISHI MWENYEWE..... FEBIANI BABUYA

0621567672 (HALOPESA)

0745982347 (M-PESA)

0714581046 (TIGO-PESA)

0689440143 (AIRTEL MONEY)

36316279 (LIPA NAMBA (M-PESA) inapokea mitandao yote)

FEBIANI BABUYA


NB
MAANDISHI YANGU NI HAKI YAKO..... 📚 📖✍️
 

Attachments

  • FB_IMG_1755268206502.jpg
    FB_IMG_1755268206502.jpg
    62.2 KB · Views: 34
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
Storyteller: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 2.

Ilikuwa ni ngumi iliyoshiba ya mwanaume mmoja ambaye alitokea pembezoni mwa mti mmoja mwembamba lakini kutokana na kwamba alikuwa kwenye mwendo, ndiyo sababu hakufanikiwa kabisa kuweza kumuona bwana huyo. Alikuwa ameinamia ardhini huku akitapika damu kwa uzito wa ile ngumi, hapo alipata majibu kuhusu wale wanaume wengine watatu ambao hakuwaona kwa mara ya kwanza, watu hao walikuwa wamegawana maeneo na nyakati hizo alikuwa amekutana nao wote sita. Nyuma yake walikuwa wamefika wale ambao alikuwa amewakimbia mwanzo na mbele yake walikuwepo wale wengine watatu hivyo hakuwa na sehemu nyingine ya kuweza kukimbilia ama kuyaponya maisha yake. Mwanaume huyo kitu pekee ambacho alikuwa anakitegemea kuweza kumtoa mahali hapo akiwa hai ilikuwa ni miujiza pekee ila kwa nguvu za mwanadamu ilihitaji bahati kubwa mno ambayo ni wanadamu wa kuhesabika huwa wanahatika kuipata kwenye maisha yote ya kuishi.

Mwili wake ulikuwa umeanza kulegea kwa kiasi baada ya kupata hayo majeraha yake mwilini na kipigo cha kushtukiza. Alisogea hatua moja mbele ili awe anawaona wote vyema maana kiza kilikuwa kimetanda kwa ukubwa na macho yake yalikuwa yanapoteza nuru ya kuweza kuona mbele vizuri hivyo alihitaji kuweza kujipa msaada mwenyewe kuendana na hali halisi ambayo ilikuwa mbele yake kwa nyakati hizo. Mikono yake ilishiba, haikuwa na udhaifu mkubwa huku kichwa kikiwa na nywele za kutosha ambazo zilisambaratika bila mpangilio lakini kabla ya hapo, zilionekana kutunzwa kwa usahihi na ustadi wa hali ya juu.

Aliona vivuli vinamsogelea karibu yake, alihema taratibu huku misuli yake ikiwa inatuna, vivuli vulikuwa viwili, aligeuka kwa kuinama kidogo ambapo alipishana na ngumi moja huku akiusikilizia upepo wake, ngumi nyingine ilikuwa inakuja kwenye usawa wake wa uso ambapo aliinamia pembeni ikamkwaruza kidogo shingoni yeye akaitua yake kwenye uso wa mwanaume huyo ambaye alisikika akipiga yowe. Ilizama kwenye pua na kuipasua hiyo pua kiasi kwamba damu ikasambaa mpaka kwenye nguo zake yeye. Wakati mwanaume yule akiendelea kuishikilia pua yake, alirusha ngumi nyingine ambayo ilitua kwenye kifua na kupelekea bwana yule kuinama kwa maumivu ambayo yalimsababishia kupokea mguu ulioshiba kwenye uso wake.

Alidondokea mbali kidogo kutoka lilipokuwa lile eneo huku akiwa anajisikilizia taratibu na kelele kadhaa, mwanaume yule aligeuka lakini aligundua kwamba muda ulienda, alikutanishwa na teke moja la mbavu lakini wakati anaendelea kujishauri kwa maumivu, ngumi moja ilitua kwenye shingo yake upande wa nyuma na hapo aligundua kwamba mhusika ambaye alikuwa ametua mkono huo alikuwa na silaha ndogo mithili ya sindano mkononi kwani ilimpatia tobo. Aliuma meno yake na kuruka sarakasi mbili za mbele, zilimfanya kusimama kando ya mti ambapo alidunda kwenye huo mti na kugeuka akiwa amejilaza kama mtu ambaye alikuwa anahitaji kulala.
Alipo mkaribia mwanaume mmoja alijigeuza na kutua ardhini ambapo alishikilia kwa mkono mmoja kisha akajifyatua, alikuja kutua kwenye shingo ya bwana yule aliyekuwa karibu naye, aligeuka naye kwa miguu yake akiwa anainyonga shingo hiyo tatatibu na kwenda kumkita bwana huyo kwenye mti ambapo baada ya kudondoka alikuwa amevunjika kiuno. Aliruka juu na kutua kwenye shingo ya huyo bwana akaivunja na mtu huyo akapoteza maisha hapo hapo. Muda ambao aliutumia kuinuka ni muda ambao aligundua kwamba alikuwa amezamishiwa kisu kwenye mwili wake, kisu kilicho mpatia maumivu makali.

Aligeuka kwa ghadhabu na kumkosa bwana huyo shingo ambapo wakati anafanya hayo yote alijisahau kwamba kwa nyuma yake kulikuwa na watu wengine, aliirusha mfulizo mikono yake mpaka alipofanikiwa kuidaka shingo ya huyo bwana, ile shingo ilivunjwa lakini wakati huo alizamishiwa nondo kubwa kiasi, nondo hiyo ilivutwa kidogo kwa nyuma na mguu mwingine ukafuatia kwenye mguu wake kiasi kwamba uliteguka pale pale. Alisikika akitoa sauti ya maumivu makali lakini wakati huo alikuwa anamrukia yule bwana ambaye alimshambulia na nondo kwenye mwili wake. Akiwa juu ya bwana huyo alipishana na mguu mzito ambao ulimkosa na kuzipuliza nywele zake, aliinuka kwa sarakasi ya mbele ambapo alitua sehemu ambayo ilikuwa na majani mengi makavu akiwa anavuja damu kila sehemu kwenye mwili wake.

Wakati anatua alifika hapo na kuyazoa majani hayo kwa nguvu kubwa akayarushia nyuma ambako alijua watu hao wanamjia kwa kasi, ni kweli wale mabwana walikuwa wanamjia alipo na kama bahati kwake yale majani yalikuwa kwenye mavumbi hivyo wakati anayarusha yaliruka na mavumbi na kuwapata wale wanaume kwenye macho yao isipokuwa mmoja ambaye aliinama na kuziba uso wake ili asikumbwe na hiyo dhahama. Watu hao walitulia baada ya sekunde kama kumi na baada ya eneo hilo kutulia, mtu wao hakuwepo, yaani alikuwa amekimbia na haonekani kama aliingia sehemu ipi kwa nyakati hizo. Walionekana kulaani mno jambo lile kuweza kutokea, huyo mtu wao hakutakiwa kuendelea kuwa hai mpaka nyakati kama hizo, alitakiwa kufa kwenye mikono yao kwa namna yoyote ile na ndipo wakaamua kuufuata ule uelekeo ambao walikuwa na uhakika kwamba alikuwa ameelekea huko baada ya pale kwani waliamini hawezi kufika mbali kwa sababu alijeruhiwa, ilikuwa ni lazima wampate tu.

Ile ndiyo ilikuwa hali iliyomfanya bwana yule aweze kuwakimbia watu wale na kuishia kuwa kwenye hali kama ile kwa nyakati ambazo alikuwa anayapigania maisha yake lakini jambo hilo lilionekana kuwa gumu zaidi kwake baada ya hali kubadilika kabisa na kuishia kwenye ule mti hali yake ikiwa imebadilika ghafla kiasi kwamba akaishia kulitamka jina ambalo ni yeye pekee ndiye alijua kwamba lilikuwa jina la nani. Alikuwa amefikia hatua amekata tamaa kabisa, alikuwa tayari kuwasubiri watu hao kuja lile eneo na kuyabeba maisha yake kwani hakuwa na jambo la ziada ambalo angeweza kulifanya kwa nyakati zile likamsaidia. Bwana huyo akiwa anahangaika na maumivu makali nyakati kama hizo huku macho yake yakiwa yamepoteza uwezo wa kuona vizuri fahamu zilianza kumtoka taratibu akiwa amekata tamaa hatimaye alijilaza mahali hapo hapo akiamini safari yake ilifika mwisho.

Wakati anakata hiyo tamaa yake, kuna mwanamke mmoja ambaye alifika eneo hilo akiwa ameufunika uso wake, alionekana kabisa kwamba hakuhitaji kutambulika na mtu yeyote yule ambaye alikuwepo kwenye hilo eneo. Alimbeba bwana huyo na kwenda kumzamisha kwenye kichaka kimoja kisha yeye akapanda juu ya mti kwa kasi ya ajabu na kujibanza kwenye matawi baada ya kusikia hatua za watu zikiwa zinakuja eneo hilo. Akiwa pale aliwaona wanaume wanne ambao waliishia ile sehemu ambapo alikuwa amepotezea fahamu yule bwana, walionekana kuongea jambo fulani huku wakiwa wanasonya kwa hasira na baada ya dakika kama moja baada ya kukubaliana jambo walionekana kuanza kuondoka ile sehemu mpaka walipo ishia.
Mwanamke yule baada ya kuhakikisha wale mabwana wameweza kupotea kutoka kwenye ile sehemu, alishuka taratibu na kusogea mpaka pale ambapo alimhifadhi yule mwanauma, alimbeba na kutokomea naye kuingia sehemu ya ndani zaidi ambako kulianza kuonekana kama kuwa na msitu mzito kiasi.



KIJIJI CHA BANZOKA
Ni kijiji cha zamani mno ambacho kilikuwa kimepotea kwenye masikio ya wengi ama kwenye dunia ya watu wengi. Kijiji hicho kilikuwa umbali kadhaa kutoka eneo ambalo lilikuwa linafikika na wengi, huenda ndiyo sababu ambayo ilikifanya kuweza kuukosa umaarufu kwa watu wengi na kuwafanya waweze kukifahamu ama kukisikia kama ambavyo ilikuwa inasikika miji mingine na vijiji vingine maarufu ambavyo vilikuwa vinatoa watu mashuhuri.

Ni kijiji kilichokuwa na idadi ya watu wa kuhesabu tu, hawakuwa wengi kabisa ndani ya eneo hilo na watu ambao walikuwa wakipatikana huko hawakuwa wakiyaishi yale maisha ya kawaida. Kilikuwa kinapatikana ndani ya msitu mmoja wa zamani ambao ulitengwa, ulitengwa kwa sababu ya mambo ambayo yalikuwa yanasimuliwa kutokea ndani ya eneo hilo. Lilikuwa ni eneo ambalo lilidaiwa kuwa na maajabu tangu enzi, eneo ambalo lilikuwa na watu wa kale wakiishi kama mizimu, ilidaiwa kwamba hakuna binadamu alikuwa anaruhusiwa kuweza kuingia huko na kama angeingia basi hakuna mtu ambaye aliwahi kurudi hata mmoja hivyo lazima angekufa. Jambo hilo ndilo lilifanya watu waanze kuogopa kwa ukubwa kuwepo kwenye hivyo viwanja huku kukiwa hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa ana ushahidi juu ya jambo hilo.

Ndani ya kijiji hicho ndipo alipokuwepo yule mwanaume ambaye mara ya mwisho alipoteza fahamu baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wanaume sita ambao walikuwa wamemvamia, hakikuwa kipigo ambacho kilimpotezea fahamu, ilionekana kwamba kuna kitu cha ziada ambacho kiliunyong’onyesha mwili wake na kuufanya kukosa kabisa nguvu kiasi kwamba akaishia kwenye ile hali yake mbaya. Bwana huyo akiwa amekata tamaa ya maisha kabisa na hajui ni jambo gani liliendelea kwa wakati ule ndipo alipo tokea mwanamke mmoja ambaye alijifunika huku kwenye mwili wake akiwa na nguo za asili mithili ya mtu ambaye aliishi mwituni kwa muda mrefu, alimbeba na kupotea naye kuelekea sehemu ambayo haikuwa inajulikana.

Episode ya pili inaishia hapa, ni muda wa kwenda kujua yaliyomo ndani ya hilo eneo lisilo julikana.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
Storyteller: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 3.

Mwanamke yule ambaye alimbeba yule bwana, alielekea naye kwenye kile kijiji ambacho kilikuwa kilomita moja tu kutoka lile eneo ambalo alimpatia. Wanaume wale ambao walikuwa wakimfukuza mpaka eneo hilo, hawakuweza kuendelea mbele kwa sababu walikuwa wanazijua sifa za eneo hilo, ni eneo ambalo hakuna mtu aliwahi kuingia akatoka akiwa hai hivyo wakaiona kama sehemu tukufu kwa ajili ya mizimu ya zamani kuweza kuishi lakini eneo hilo lilikuwa ni makazi ya watu kadhaa ambao walijichimbia kwenye hiyo misitu ambayo mwanzoni ilizungukwa na nyika kadhaa na vichaka vya kutosha.

Mwanaume huyo ambaye aliokotwa kule nyikani, alikuwa amelazwa kwenye kitanda cha ngozi ambacho kilionekana kuwa cha zamani sana. Kitanda hicho kilikuwa kimefungwa kwa kamba ngumu na kukifanya kiwe kinaelea taratibu. Ulikuwa ni mwezi mmoja umepita tangu yule bwana apate lile tatizo, mwezi mzima alikuwa ametibiwa pale na hakuwa amerudi kwenye fahamu zake za kawaida, ilionekana kwamba kitu alichokuwa amewekewa kwenye mwili wake kilikuwa na sumu mbaya ambayo ilimletea hali tofauti na ile ambayo mwili wake uliizoea tangu mwanzo. Bwana huyo alianza kuweweseka akiwa kwenye usingizi, kuweweseka kwake kulimfanya kuanza kutamka mambo mazito ambayo yalianza kuwatisha hata wale ambao walikuwa wanamtibia hilo eneo.

“Historia ya maisha yangu sio nzuri, sio nzuri kwa sababu mimi ni mtu wa tofauti, utofauti wangu unakuja kwa sababu ya kazi yangu ambayo nilikuwa naifanya, kazi ambayo nilizaliwa nikihisi nilitumwa kuja kuifanya kama sio kupewa kibali kuweza kuifanya tena kwa usahihi. Nilikuwa na kazi ambayo ni wanadamu wa kuhesabu tu duniani hapa huwa wanabahatika kuwa nayo hivyo nami nilikuwa miongoni mwa hao watu wa kuhesabu” mwanaume huyo alitulia kuweweseka, alitulia kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea tena kuongea, alikuwa anaongea mithili ya mtu ambaye yupo ndotoni lakini alikuwa analiwasilisha jambo hilo mithili ya mtu ambaye alikuwa anamsimulia mtu amjuaye na simulizi nzima ya maisha yake.

“Jina langu maarufu wananiita Bazoka, King Bazoka. Hilo ni jina ambalo nilipewa na watu lakini kiuhalisia ni kwamba sijui hata maana yake ya asili ni ipi, sina nilijualo kuhusu hili jina ila niliamua kulivaa kwa sababu sikuona ubaya wake wowote. Mimi nilikuwa mlinzi wa raisi, ndiyo mimi ndiye nilikuwa nahakikisha usalama wa mheshimiwa raisi unakuwa sawa kwa masaa ishirini na manne ya siku mpaka pale ambapo nahisi nilishindwa kuweza kutimiza hilo jukumu langu, nahisi nilishindwa kwa sababu ni wajibu wangu, jambo lolote ambalo linatokea kwa raisi basi mtu namba moja kuweza kuwajibika ni mimi hapa.

Nilifanya kosa kubwa la maisha, kosa ambalo sina imani kama nitaweza kujisamehe mwenyewe hata huko akhera kwa sababu nilileta majonzi kwa mamiliona ya wananchi. Mimi ndiye nilileta matatizo yote ya taifa hili, mimi ndiye sababu ya kufanya kuwepo kwa hali ya fujo na watu kupoteza imani kabisa na uongozi wa taifa hili. Linaweza lisiwe kosa langu moja kwa moja lakini mimi ndiye ambaye nilitakiwa kulizuia jambo hilo lisiweze kutokea lakini nilishindwa kufanya hivyo, kushindwa kwangu kufanya hivyo ndio ukawa mwanzo wa taifa hili kuweza kupoteza mwelekeo jumla, mwelekeo ambao inaweza ikatumika mikaa miamoja kuweza kuurejesha kutokana na hali ambayo ipo mpaka sasa.

Najua kwamba kuna watu watanicheka na kuna wengine wananishangaa vile vile, mlinzi wa raisi wa nchi nafikiaje mpaka kuwa hatua kama hii ambayo nipo nayo leo? Kiukweli hata mimi siwashangai hao watu kwa sababu hata ningekuwa mimi kwenye nafasi zao pia ningeshangaa, lakini jambo hilo haliwezi kuondoa ukweli kwamba mimi nilikuwa mlinzi wa raisi kwa miaka isiyo pungua minne. Miaka yangu bora ambayo niliitoa kwa ajili ya kumpambania yule mwanamapinduzi imekuja kuishia sehemu mbaya na kuacha historia mbaya zaidi kwenye maisha yangu na siku zangu ambazo nimepata kuishi juu ya uso wa dunia hii isiyo na shukrani.

Dunia imepata kushudia mengi miaka na miaka lakini jambo ambalo huwa linasisitizwa mno na watu wenye maarifa makubwa ni kwamba duniani watu ambao huwa wanachukiwa kupita kiasi ni wawili tu! Mtu wa kwanza ni ambaye ni mzuri zaidi kwenye anacho kifanya. Kwenye hili kundi la kwanza ni la wale watu ambao mara nyingi huwa wanafanikiwa zaidi kuliko watu ama makundi mengine, hawa ni watu ambao wanajua zaidi kwenye mambo ambayo wanayafanya hivyo hupelekea kufanikiwa kupita kile kiwango ambacho wanadamu wamewapangia na hilo kwao ni tatizo kubwa. Kundi la pili ni la wale watu ambao wanausema ukweli ama kusimama kwenye ukweli hata kama ukweli unaumiza, sasa mimi nimehukumiwa na ulimwengu kwa hizo sababu mbili.

Naweza kusema nilikuwa makini na bora kwenye kazi yangu, niliifanya kazi yangu kwa ufanisi mkubwa huenda kuliko mtu yeyote ambaye amepata kupita kwenye ile nafasi, niliifanya kazi kwa weledi na moyo wote lakini kwa bahati mbaya jambo la kutisha kwenye historia ya taifa hili lilitokea kwenye kipindi changu hivyo likapelekea kuniharibia sifa yangu na kunifanya mimi kuonekana kama mtu ambaye ndiye nilishindwa kutekeleza majukumu yangu. Mwanaume ambaye alikuwa kama mfano wa maisha kwangu kwa namna alivyokuwa anaufanya kwa usahihi uongozi wake mimi nahisi nilimuangusha lakini yote yametokea kwa sababu yake yeye.

Alipenda mno haki, alikuwa na mipango ya muda mrefu kuhusu taifa hili, aliamua kuyatoa hata maisha yake sadaka kwa ajili ya kuwapigania watu. Hata pale ambapo aligundua kwamba maisha yake yasingekuwa marefu bado aliendelea kuipiga kazi yake kwa usahihi kwa sababu aliamini kwamba kama asipotokea mtu wa kujitoa mhanga basi hakuna namna taifa linaweza kufika mbali wala kusogea mahali popote pale. Kiongozi huyo alikuwa ni muumini mkubwa wa falsafa za miongoni mwa waanzilishi wa falsafa duniani, Socrates. Bwana huyo ambaye alipata kuishi maelfu ya miaka iliyopita huko nyuma aliamini kwamba wanadamu wanatakiwa kuwa na uwezo wa kuhoji na kuuliza kila jambo ambalo lilikuwa linaendelea ama kufanyika. Watu walitakiwa kujua wanatoka wapi, wanaenda wapi na kwanini mambo yanafanyika? Hawakuwa mazombi wa kupelekeshwa hovyo kama watu wasiokuwa na mwelekeo wowote ule hivyo akaamua kuwa mfano.

Kwenye kuhoji kwake kulileta matatizo kwa sababu kuna watu ambao walikuwa nyuma ya hiyo mipango, hawakutaka kabisa mambo hayo yaweze kujulikana kwani watu wakiwa na maarifa mengi ni ngumu kuwaongoza ila ukiwa na wajinga wengi ni rahisi zaidi kuweza kuwaongoza. Sasa kuanza kuhoji hoji kungekuja kuwaharibia hapo baadae kwani watu wangejitoa kwenye utumwa wa fikra hivyo mwaafalsafa huyo kwao akawa kama adui mkubwa ambaye alikuwa anakuja kuwaharibia biashara yao wakaamua kumuua. Mwanafalsafa huyo hakuogopa kufa kwa sababu aliamini hata kama akifa basi ipo siku moja kuna watu watakuja kuguswa na hadithi ya maisha yake, wale watu watatamani kujua alikuwa anafanya nini hasa na kwanini alikuja kupotezwa baadae? Maana yake wangekuja kutambua kwamba alikufa kwa sababu ya kusambaza maarifa kwa watu na maarifa hayo lazima yangekuwa nuru kwa wengi ndiyo maana wakahitaji kuweza kumpoteza ili yasiwafikie. Kuanzia hapo aliamini kwamba hata kama yeye atakufa basi lazima watakuja kutokea wana mapinduzi wengine kabisa ambao wataanzia alipo ishia yeye na kuendelea mbele jambo ambalo hakuwa na uhakika kama lingetokea karibuni ila alikuwa ana uhakika kwamba ipo siku lingekuja kutokea kwa namna yoyote ile.

Hilo ndilo ambalo lilimpatia yeye imani ya kuweza kuendelea kupambana na kusimamia kile alicho kiona kwamba ni sahihi na kina manufaa kwa taifa. Kuna jambo moja kubwa ambalo wananchi wengi hawalijui na hawatalijua abadani, nazungumzia namna nchi inavyo endeshwa, siasa ilivyo kwa watu. Kwenye mitandao ya kijamii ni tofauti na siasa halisi ilivyo. Siasa yenyewe inatisha, ni maisha ambayo unayatamani ukiwa nje ila ukiingia ndani yake yanatisha, wanaweza kuyaishi watu wachache ndiyo maana wengi huwa wanakuwa watumwa, wengine wanakufa mapema na wale ambao wanaamua kuukana ubinadamu na kuwa watu wabaya ndiyo wana nafasi kubwa zaidi ya kuweza kuishi kwa muda mrefu kwenye siasa za namna yoyote ile. Hawa hawawazi kuyebeba maisha ya watu ili kutimiza malengo yao, hawa huwa wanawapa maneno matamu raia kwa sababu wanaambiwa yale ambayo wao wanataka kuyasikia na sio uhalisia ambao upo.

Sasa yule raisi hakuwa hivyo, hakuwa mtu mnafiki kukupa taarifa ya uongo eti kwa sababu tu wewe umetaka kuisikia hapana, alikuwa mtu muwazi ambaye aliamini zaidi kwenye ukweli na uhalisia. Aliamini hakuna jambo lililokuwa linakuja kirahisi kwenye haya maisha. Alielewa kwamba ni lazima kuna watu wafe, ni lazima kuna watu hususani matajiri waweze kulia, alielewa kwamba kuna watu wanatakiwa kuumia haswa ili taifa lifike kule ambako linahitaji kuwepo. Huwezi kufanikiwa kwa raha, ni lazima uvuje jasho kwanza ndipo ufike kule ambako wewe unakuhitaji na maisha siku zote yapo hivyo ila watu huwa hawataki kwa sababu hiyo njia ni ngumu.

Hivyo ile miaka ambayo nilikaa naye karibu, nilijifunza mengi kupitia yeye. Haina maana kwamba kila wakati alikuwa sahihi, hapana bali alikuwa ni muwazi, mkweli na mtu ambaye alipenda kulipigania taifa lake hata pale ambapo angehisi kwamba watu wengi hawapo upande wake. Ni kweli aliua watu wa kutosha, aliwapoteza baadhi ya watu kwenye utawala wake lakini wale watu wengine hawakuwa na hatia ila walikuwa ni hatari kwa mapinduzi ya taifa. Watu wengi ambao aliwapoteza ni wale ambao walikuja kuanza kuharibu ile mipango ambayo alikuwa nayo ya muda mrefu, mipango ambayo ilikuwa inalipeleka taifa kwenye anga za ulimwengu wa mapinduzi ya nne ya viwanja. Kiukweli hao aliwaua tena kikatili, hao aliwaona kuwa maadui wa taifa kwani aliamini hata viongozi shupavu wa zamani ambao walipata kuishi, kuna muda walilazimika kuwaua hata watu wao wa karibu kama ikiwalazimu ili kuhakikisha hawapati vikwazo kuelekea kwenye nchi ya ahadi.

Huyu bwana anajaribu kutaka kutupa taarifa gani? Episode ya tatu nabwaga kalamu hapa, panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 4.
ENDELEA.......
Sasa kwenye zile harakati zake aliingia sehemu moja ambayo naweza kusema kwamba ni mbaya, huenda raisi wa kila taifa ana mamlaka makubwa kwenye taifa lake hapa duniani lakini ukweli ni kwamba ile ni dhamani tu ya uongozi na mamlaka ya kuamuru ila nguvu ya kweli ipo kwenye pesa. Aliwagusa wenye pesa kwa sababu walikuwa wanawanyonya watu maskini, watu wale walikuwa hawalipi kodi lakini hawakuwa wakiheshimu sheria na mamlaka kwa ujumla kwa sababu walijua kwamba wangeweza kumnunua yeyote, walikuwa wana uwezo wa kumpata wamtakaye kwa muda ambao wangeutaka wao lakini kuingia kwake kulibadilisha yote hayo.

Wale mabwana walihenya na kuteseka, jina lile liliogopeka kuliko hata ukoma, watu walikuwa wakilisikia jina lake wanatamani hata kuvunja kuta za nyuma wasikutane naye ana kwa ana. Alikuwa na lengo jema na taifa lakini nyakati hazikuwa bora kwake, nyakati zilimkana kabisa na kumkataa na alipofikisha miaka minne na nusu kwenye uongozi wake ndio ukawa mwanzo wa hadithi mbaya ambayo haikuwa na ndoto bali ilikuwa ni hadithi ya maisha ya kweli. Mimi kama mlinzi wake ndiye ambaye nilishindwa kabisa kuinusa ile hatari japo kwa mambo yalivyokuwa nilielewa kwamba kuna siku inaweza kuja jambo lile likatokea ila sikutegemea kama ingekuwa kwa namna kama ile.

Lile jambo liliwahi kipindi tukiwa hatujajiandaa bado japo ni mara kadhaa niliwahi kumsikia akidai kwamba hana imani kabisa hata na watu wake wa karibu, alinusa usaliti lakini angefanya nini? Aliwabadilisha watu wengi mpaka baadhi ya ndugu zake lakini bado alihisi kuna hatari na watu wananunulika kwa pesa. Yeye ndiye alikuwa kiongozi wa juu zaidi kwenye taifa, hakuwa na mahali pa kwenda kulalamika kuhusu jambo lile zaidi ya kupambana na hali ambayo ilikuwepo ya kufa na jambo lile moyoni huku akijaribu kuwa makini na hatua zake lakini nadhani ni wakati ulifika kwamba asingeweza kuishi tena, hakukuwa na namna ya yeye kuwa salama kwa ajili ya kulijenga taifa, nyakati za giza zilikuwa zinatanda kwa mfululizo wa wingu zito ambalo halikuwa likionekana kwa uso wa kawaida. Kwa wale ambao tulimfahamu kiundani tuliona mapema hatari ya taifa kwenda kumpoteza shujaa ambaye aliletwa kwa ajili ya ukombozi lakini kwa watu wengine ambao walikuwa nje na mbali ya pale, hawakuwa na wazo lolote kuhusu kesho ya taifa lao, walikuwa wakishangilia kwenye kumbi za starehe wasijue ni wapi taifa lilikuwa linaenda.

Raisi wangu alikufa, alikufa nikiwa pembezoni mwa kitanda ambacho sikuwahi kufikiria kwamba kingeibeba maiti yake namna ile. Raisi alikufa nikiwa namuona, lakini raisi hakufa kwa sababu ya kuumwa. Ingekuwa kweli mimi ningejua, mimi nilikuwa mtu wake wa karibu huenda kuliko watu wengi kwa sababu kila wakati ilinilazimu kuwa naye, ilikuwa ni kwa ajili ya majukumu ya kazi lakini mimi naweza kuwa miongoni mwa watu wa kuhesabu ambao yeye alikuwa anawaamini kwa maisha yake yote. Kwa maana hiyo naweza kusema kwamba raisi aliuawa” mwanaume yule alitamka kwa sauti kubwa neno hilo tena kwa hisia kiasi kwamba wale ambao walikuwa karibu yake walirudi nyuma kidogo lakini wakati anatamka yale maneno ya mwisho, alishtuka na kuyafumbua macho yake.



TUNDUMA.
TAZARA.
Kwenye reli ambayo inayaunganisha mataifa mawili ya Tanzania na Zambia, karibu kabisa na eneo hilo alionekana mwanaume mmoja akiwa anaikata mitaa kuelekea kwenye hiyo reli. Alikuwa maeneo ya majengo nyakati ambazo kwa saa za Tanzania zilikuwa zinasoma kama saa nane na dakika zake usiku. Bwana huyo alionekana kuwa mzoefu wa mitaa hiyo kwani hakuwa na wasiwasi kabisa, sio kama hakuwa na taarifa juu ya mambo ambayo yalikuwa yanaendelea kwenye mji huo mdogo ambao unakua kwa kasi kubwa mno kwenye suala zima la biashara, lahasha! Bali alikuwa anajua jambo ambalo analifanya hata imani juu ya nafsi yake mwenyewe ilikuwa ni kubwa.

Alitembea kwa muda wa dakika kadhaa za kuhesabu huku akiwa anaikata mitaa kwa hatua zake kubwa ambazo zilikuwa na ukakamavu wa kutosha ndani yake. Alionekana kuwa na uhakika wa sehemu ambayo alikuwa anaelekea ndiyo maana hakusita hata eneo moja. Baada ya kufika ilipo reli hiyo, alitazama kila upande kisha akaanza kujongea taratibu kuelekea eneo ambalo lilikuwa na behewa kadhaa za treni ambazo hazikuonekana kuwa pale kwa makusudi bali zilikuwa ni mbovu ama zilikuwa kwenye matengenezo. Aliingia ndani bila hata kujiuliza mara mbili, alilivuka lile behawa la kwanza na kuingia la pili lake ambalo kwenye siti moja alimuona mwanaume mmoja ambaye alikuwa amempa mgongo huku kwenye mwili wake akiwa na koti zito ambalo hakuelewa kama bwana huyo alilivaa kwa sababu ya baridi kali ambalo linapatikana ndani ya mkoa huo wa Songwe ama kulikuwa na sababu zingine nyuma yake ambazo yeye binafsi hakuwa na uelewa nazo. Alihema mara moja na kuanza kuzitupa hatua zake kwenda kwa yule bwana ambaye bila shaka alionekana kwamba alikuwa pale kwa ajili ya kumsubiri yeye tu na si vinginevyo.

“Umechelewa sana na unajua kabisa kwamba huwa sipendi kumsubiri mtu mmoja kwa muda mrefu. Kuna sababu zipi unapuuzia amri yangu nikikuita mahali namna hii?” aliongea kwa sauti nzito bwana yule ambaye ni wazi alikerwa na mwanaume yule kuweza kuchelewa kufika eneo lile.

“Nilikuwa nahakikisha usalama na kuwa na uhakika kwamba hakuna mtu hata mmoja anajua kwamba mimi nipo au nataka kufanya jambo gani”
“Mhhhh! Naanza kuwa na mashaka na uwezo wako kwa sasa, unatakiwa upunguze kufanya mapenzi yanakupelekea pabaya. Wewe ni mwenyeji wa hili eneo, huwezi kunipa sababu ya kitoto namna hiyo kwa kuamini kwamba nitakuelewa kwa sababu unaijua kila kona na kila mtaa wa mji huu”

“Nisamehe kiongozi, hili halitajirudia kwa mara nyingine tena”
“Ni bora iwe hivyo kwa sababu utanilazimisha nije kukuua mwenyewe kwa mkono wangu jambo ambalo sitaki kulifanya”
“Nimekuelewa mkuu”

“Mtu wako atakuwa hapa ndani ya nusu saa ijayo, atakuwa Mwaka pale akisubiri saa tisa kamili usiku aweze kuvuka kwenda Zambia na baada ya hapo asubuhi asafiri kwenda Afrika ya kusini”
“Natakiwa kumuua au kuondoka naye akiwa hai?”
“Tangu lini umeanza kuondoka na watu ambao wapo hai?”
“Namanaanisha kwamba kuna taarifa ambayo natakiwa kuondoka nayo kutoka kwake?”

“Sio taarifa bali kuna begi dogo ambalo analo kwenye mkono wake ndilo ambalo linahitajika. Hilo begi ukilipata hautakiwi hata kulifungua kwa namna yoyote, lifike kwangu likiwa vile vile na baada ya hapo nadhani unajua ni kitu gani unatakiwa kukifanya”
“Ndiyo mkuu”
“Natarajia kwamba hilo begi litafika Dar es salaam kesho mapema juu ya meza yangu ofisini”
“Nimekuelewa bosi, na vipi kuhusu Bazoka?”

“Kuna watu wameenda kumalizana naye muda sio mrefu hivyo muda wowote kuanzia sasa nasubiri simu kutoka huko ili nijue kazi yote imeenda sawa kwa pamoja”
“Una imani kwamba watu ambao umewapa kazi wanaweza kumuua yule mtu?”
“Umekuwa na wasiwasi na ufanyaji wangu wa maamuzi?”
“Hapana ila najaribu kuangalia aina ya mtu ambaye wanamtafuta”

“Go and do your fucking j….” mwanaume huyo mtu mzima aliongea sentensi nusu kwa kufoka akiwa anajiandaa kutoka eneo hilo baada ya simu yake mfukoni kumshtua kwa mtetemo mkali ambao huenda ulisikika vyema kwa sababu ulikuwa ni usiku mzito na maeneo hayo yalikuwa na utulivu mkubwa.
“Nipe ripoti”
“Whaaaat?” alionekana kuongea yeye tu kwa sababu mtu wa upande wa pili hakuwa anasikika. Hakujibu kitu tena, aliyainua macho na kumwangalia bwana yule kwa umakini mkubwa usoni kwake akionekana kabisa kwamba hakuwa sawa.

“Maliza kazi yako sasa hivi na asubuhi ya mapema kabisa uwe Songwe pale uwanja wa ndege kwa sababu kuna dharura, unatakiwa kuwepo Dar haraka iwezekanavyo”
“Sawa bosi” aliondoka eneo hilo akiwa kama hayupo sawa, baada ya kutoka pale, alitembea hatua kama kumi na tano wakajitokeza wanaume wanne ambao waliungana naye mpaka kwenye gari ambayo ilikuwa imepakiwa mahali ambapo hakuna mtu angeweza kufikiria kwamba ilikuwa kwa ajili ya bwana huyo. Alipanda kwenye gari na kutulia kwa muda huku akiwataka wale vijana wake wakae nje kwanza kwani alikuwa anahitaji kufikiria jambo kwa muda tena akiwa mwenyewe tu.

Episode ya nne ya JUMBE JEUSI natundika daruka hapa, tukutane ndani ya episode inayo fuatia.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 5.
ENDELEA.......

Kwenye mfuko wake wa koti alitoa picha ambayo ilikuwa na sura ya mtoto, aliitazama kwa muda wa dakika kadhaa kisha akasikitika, alionekana kabisa kuwa kwenye jela ambayo ilimfanya yeye kuishi mtaani maisha ambayo bila shaka hakuwa anayafurahia ila hakuonekana kuwa na namna zaidi ya kuishi kama vile misingi ya asili inavyo mtaka aishi kama sio kwa maamuzi ambayo huenda aliyafanya bila kujua madhara yake ambayo yangekuja baadae.
“Nitaua hawa watu mpaka lini? ona sasa nimeliuza taifa langu kwa watu ambao huenda watalifanya taifa hili kuingia kwenye hali mbaya kwa zaidi ya miaka hamsini ijayo. Lakini nilipaswa kufanya nini? Kuna nyakati inabidi ukubali kwamba akili yako haiwezi kufanya maamuzi ya mwisho bali mazingira yanakufanya uje na maamuzi ambayo hata nafsi yako inabaki inakushangaa hivyo najua ni ngumu kuishi na hili lakini ndiyo namna pekee ya kuishi” alitamka mithili ya mtu ambaye alikuwa analijutia jambo ambalo lilikuwa linaendelea ila hakuwa na namna nyingine ya kuweza kufanya. Aligonga mlango wa gari, walinzi waliingia ndani na gari hiyo ikaondoshwa hilo eneo.


Saa nane na nusu usiku maeneo ya Sogea, ilionekana gari moja aina ya Land Rover rangi nyeusi ambayo bila shaka ilikuwa imetokea njia ya Mpemba kuelekea Tunduma. Gari hiyo ilikuwa kwenye mwendo mkali ambao ulionyesha dhahiri kwamba dereva alikuwa ana mahali ambapo alitakiwa kumfikisha mtu ambaye alikuwa amembeba kwa uharaka zaidi. Gari hiyo ilipofika Kilimanjaro, ilikunja kulia barabara ndogo ambayo iliwazungusha mpaka HIGH CLASS, moja kati ya kumbi kubwa na kongwe ndani ya mji mdogo wa Tunduma. baada ya kufika mitaa hiyo, gari ilikunja kushoto na kuanza kuitafuta barabara kubwa ambayo ulitumika muda mfupi tu kuweza kuifikia nyakati hizo.

Baada ya kuifikia, ilikunja kulia na kuanza kupandisha Mwaka ambako bila shaka ndiko mhusika alikuwa anaelekea nyakati hizo. Wakati huo ambao magari hayakuwa mengi barabarani, gari hiyo haikuwa kwenye kasi kama mwanzo bali ilikuwa kwenye mwendo wa kawaida tu ambao ulikuwa rafiki kwa kila mtu ambaye alikuwa ananufaika na hiyo barabara. Safari hiyo ilienda kuishia kwenye uwanja wa Mwaka, eneo hilo lilikuwa kimya mno majira hayo, hakuonekana mtu yeyote kuwepo eneo hilo zaidi ya taa za umeme ambazo zilikuwa kwenye majengo ambayo yalikuwa hatua kadhaa kutoka hapo.

Gari ilisimamishwa eneo hilo kwa muda kidogo, zilipita dakika kumi ambazo zilitawaliwa na ukimya mkubwa, hakukuwa na dalili za mtu kutoka kwenye gari hiyo na baada ya dakika hizo kupita ndipo mlango wa dereva ulipo funguliwa. Alishuka mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa mavazi ya kawaida ya kiraia, alisubiri mpaka mwenzake wa mlango wa nyuma alipotoka! Walitazama kila pembe ya eneo hilo wakiwa makini mno na baada ya kuwa na uhakika na usalama wake ndipo walipoufungua ule mlango mwingine ambao bila shaka ndio ambao ulikuwa na mlengwa ambaye alikuwa amefika eneo hilo. Alishuka bwana mmoja ambaye kwa mwonekano wake tu alionekana kuwa mtu mwenye asili ya taifa la Zambia, alikuwa ndani ya suti nyeusi huku akiwa amebeba begi dogo kwenye mkono wake wa kulia.

Alisimama kwa muda akiwa anayatazama hayo mazingira kwa usahihi, hayakuonekana kuwa mageni kwake lakini hata hivyo sura yake haikuwa kirafiki kabisa kuweza kusadiki ukweli wa mawazo yake. Alihema na kuangalia saa yake na kujisogeza mbele hatua kadhaa, aliangalia tena saa yake lakini ni kama kuna jambo alihisi halipo sawa.
“Mbona hafiki mpaka sasa?” aliuliza akiwa anamgeukia yule dereva”
“Alitakiwa awe hapa kwa muda wa dakika tano zilizo pita, maana yake ni kwamba kuna tatizo” yule dereva aliongea jambo ambalo liliongeza mashaka kwa yule bwana, bila shaka kuna mtu ambaye alitakiwa kuja kumpokea pale nyakati zile ndiye alikuwa anaongelewa kwa kuchelewa.
“Una maana kwamba?”

“Toby hajawahi kuchelewa hata dakika moja kwenye jambo lolote, kama mpaka sasa hajafika lazima ameuawa” ile kauli ya dereva ilimfanya bwana yule kugeuka kwa mara nyingine kuweza kuangalia ule upande ambao alikuwepo muongeaji.
“Auawe na nani?”
“Huenda wanajua kwamba wewe upo hapa hivyo tunatakiwa kuondoka haraka”
“Ni sisi watatu tu ambao tunajua kwamba nipo hapa muda huu pamoja na Toby, kwa namna yoyote ile Toby asingeweza kuniuza maana yake ni kwamba….” alipata kigugumizi kuweza kuendelea, ni kwa sababu aligundua kwamba miongoni mwao alikuwepo msaliti ambaye bila shaka alikuwa amewauza. Aligeuka kumwangalia mwanaume yule mwingine ambaye alikuwa upande wa pili wa gari, bwana yule alikuwa na bastola kwenye mkono wake tayari.
“Ni wewe?”

“Utanisamehe kwa hili, sikuwa na namna nyingine naweza kufanya. Hawa watu wanataka kila ambaye alikuwa karibu na raisi auawe”
“Wewe leo unaniuza mimi mpuuzi mkubwa wewe nimekutoa kijijini hauna hata maisha?” aliongea kwa jazba na kufoka huku hali yake ikiwa yenye hasira zaidi, hili lilijidhihirisha wazi kwa namna alivyokuwa na hasira kali.
“Maisha yanabadilika ndugu yangu, kunisaidia haina maana mimi niwe tayari kufa kwa ajili yako” bwana yule alimaliza kuongea na kurusha risasi yake kwenda kwa dereva ambayo ilipasua ubongo na kumtupa mbali. Wakati anaigeuzia kwa yule mwingine ambaye alitakiwa kusafiri kwenda Zambia kwa nyakati hizo, yule bwana alirusha begi lake kwa nguvu ambalo lilimyumbisha yule mpigaji ambaye alijikuta anapiga hewa na kurudi nyuma kwani begi lilimyumbisha hesabu zake zote.

Aligeuka ghafla lakini wakati anatekeleza hilo alikutana na goti la shingo ambalo lilimyumbisha, alitua kwa goti na kujigeuza ili aruke sarakasi na kusimama. Alipigwa na kibao usoni akarudi ardhini kwa kujibamiza, akiwa anahangaika kujiinua alikutana na mguu kwenye ubavu wake, alitoa ukelele wa mauamivu ila bwana huyo hakuwa hapo kwa ajili ya kumuonea huruma, ngumi yake moja ilipasua pua yake kisha akakitoa kisu kwenye suruali yake ya suti upande wa kiunoni. Alikizamisha kwenye sikio moja kwa kiasi akakitoa na kulikata sikio hilo

“Wamekulipa shingapi mpuuzi mkubwa wewe mpaka unanisaliti mimi?” aliuliza kwa jazba pamoja na sauti ya kukata matumaini kwani mpango mzima ulikuwa umeharibika hivyo alitakiwa kukaa upya na kuanza kupanga kwa namna nyingine na alielewa kabisa kwamba muda haukuwa rafiki kwake kwani kila sekunde moja ambayo ilikuwa inaenda, ilikuwa inayahatarisha maisha yake yote. Kabla hajafanya lolote wala bwana yule hajamjibu alishangaa kusikia mlio wa risasi ambao ulipasua kichwa cha kijana wake. Alisita kwanza kugeuka kwa sababu alitambua kabisa kama mhusika ambaye alikuwa aneo la tukio alihitaji kumuua basi mpaka ageuke angekuwa amekufa muda mrefu. Aliangalia pembeni na kugundua kwamba begi lilikuwa karibu yake hivyo akaanza kuhesabu namna ya kuondoka, alipo yasogeza macho mbele kidogo aliiona ile bastola ambayo ilitumika kumuulia dereva wake hivyo akajua kabisa ilimponyoka wakati ule begi linamtinga na wakati yeye anamshambulia, angeipataje? Aligundua kwamba ilikuwa mbali na pale hivyo asingeweza kabisa kuiwahi, wazo pekee ambalo lilisimama kwenye akili yake ni kuweza kukimbia, lakini angekimbiaje mbele ya mtu ambaye alionekana kuwa makini namna hiyo? Alijikuta anayakatia tamaa maisha yake mwenyewe kabla hata hajamuona mhusika ambaye alikuwa nyuma yake. Jambo hilo lilifanyika kwa muda wa sekunde kadhaa tu ambapo akili yake ilikuwa inafanya kazi kwa kasi kubwa zaidi ya mashine.

“Alikuwa amepewa zawadi ya uhai ila kwa sasa hana kazi tena. Najua wewe sio mtanzania kwa asili japo ulipewa uraia na watu ambao walikuona wewe unafaa kulitumikia taifa hili. Naweza kusema kwamba nakushukuru kwa kulitumikia taifa langu kwa moyo na uzalendo mkubwa kama vile la kwako lakini kwa sasa hauhitajiki tena kwa sababu kazi ambayo ilikufanya uwepo Tanzania imesha isha hivyo wamiliki mpya wa hili taifa hataki wewe uendelee kuwa hai kwani kuna siku unaweza kuwa tatizo kwao.

Hawa watu wanataka wewe ufe kabisa lakini mimi ni mstaarabu ndugu yangu, najua kuna maisha baada ya haya ya wanasiasa ambayo yanatufanya tuuane wenyewe hivyo nitakulipa fadhila ya kukupa nafasi ya kuweza kuishi kwa mara nyingine tena. Nakupa hii nafasi kwa sababu hautatakiwa kuonekana sehemu yoyote ile wala kutambulika kwamba kuna alama za uwepo wako. Nitafikisha taarifa kwamba tayari nimekuua na kwa sababu wananiamini hawawezi kuwa na wasiwasi lakini kufanikisha hili nahitaji uweze kunikabidhi begi ambalo umekuja nalo huku” hayo maelezo ya huyo mwanaume ndiyo ambayo yalimfanya bwana huyo atambue kwamba hakuwa ameliona begi hilo kwanza kutokana na sehemu ambayo alisimama kwani begi ilikuwa karibu na tairi moja ya gari ambayo alikuwa ameiziba na kwakuwa ulikuwa ni usiku, mwanga haukuwa unamulika vyema kwenye vile vivuli.

Episode ya Tano ya JUMBA JEUSI inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 6.
ENDELEA.......

Hapo sasa ndipo alipopata nafasi ya kuweza kugeuka ili aweze kumuona mtu wake ambaye alikuwa amemtembelea nyakati hizo. Alikuwa ni yule bwana ambaye alikuwa amepewa maagizo muda mfupi kule kwenye behewa kwamba alitakiwa kuhakikisha anaipata begi kutoka kwa mtu huyo na kumuua kabla hajavuka kwenda Zambia ambako kidogo ingekuwa ni ngumu kumpata kwenye mataifa ya watu hayo.
“Toby yuko wapi?”
“Huyo nimemuua muda mfupi uliopita, nadhani unaelewa kwamba ndiyo sababu hajaweza kufika kwa ajili ya kukupokea hapa. Huu sio muda rafiki wa kuanza kuzungumzia maiti, nipatie begi niweze kuondoka kabla sijabadilisha maamuzi yangu juu ya hatima mpya ya maisha yako”
“Kwahiyo unahisi maisha yangu yana umuhimu wowote ule kwa sasa?”
“Mimi sijali kuhusu maisha yako na sitaki kuamini kama maisha yako yana umuhimu au hayana umuhimu. Hili jambo linaweza kuisha kistaarabu ukapata bahati ya kuishi kwa mara nyingine hivyo punguza kiburi na ufuate yale ambayo nakuelekeza hapa”

“Huwezi kulipata hilo begi labda mpaka uniue mimi”
“Bwana mdogo, hauna huo uwezo wa kupigana na mimi kwahiyo weka akiba ya viungo vyako kwa ajili ya hiyo safari mpya ambayo wewe unaenda kuianza”
“Kama huwezi kuniua basi nakuua mimi” aliongea kwa jabza huku akiwa anahesabu hatua zake taratibu kumfuata bwana huyo ambaye aliinyanyua bastola na kuzichomoa risasi zote chini ili aweze kuutumia mkono wake kwani aliona kama dharau kubwa yeye kutumia silaha mbele ya mwanaume kama huyo ambaye kwake bila shaka alikuwa ni dhaifu tu.

Zile hatua zake ambazo zilikuwa za kikakamavu kumfuata yule mwanaume zilikuwa nzito na zenye mahesabu makali, alitua kwenye tairi la nyuma ya gari ambapo alidunda kwa mguu wake na kugeuka kwa sarakasi ya upande kwenda pale ambapo yule bwana mgeni alikuwa amesimama akiwa anamsubiria. Mguu wake ulitua kwenye bega la yule mwanaume ambaye hakushtuka hata kidogo zaidi ya kubaki amesimama, ilionyesha ni kwa namna gani bwana yule alikuwa imara kwenye mwili wake. Yule bwana mwenye begi alishtuka kuona hali kama hiyo, mguu wake ulikuwa ni imara mno, kumpiga mtu na akabaki yupo vile vile kidogo ni jambo ambalo yeye binafsi lilimshtua kwa kiasi kikubwa.

Aligeuka na mguu mwingine ambao alikuwa ameuelekezea upande wa usoni lakini haukufua dafu, alikutana na hewa ambapo wakati anashuka kutua ardhini alikutana na kiza kwenye uso wake, hapo aligundua kwamba alikuwa amepigwa ngumi nzito mpaka jino moja likadondoka, alirudi nyuma akiwa anairusha damu hewani ambayo ilitoka na jino kwa lazima. Alipokaa sawa hakuamini, bwana yule alikuwa amesimama palepale akiwa hata hatikisiki, alijiangalia yeye mwenye mkono wake ndipo akagundua kwamba bado alikuwa na kile kisu ambacho alikuwa anakitumia kumpatia mateso yule kijana wake ambaye aliamini kwamba alikuwa amemsaliti.

Alisogea tena kwa hesabu kali zaidi huku akiwa anaongeza kasi yake, alirusha mkono wenye kisu ukagusa kidogo kwenye shati ya yule bwana, alirusha mkono ambao ulikuwa mtupu ukapishana na hewa kwani yule bwana alikuwa mwepesi zaidi ya karatasi. Jambo lile lilimpatia hasira kwani alijiona kudharaulika pakubwa mno, alivua koti la suti kwa spidi kubwa na kumrushia bwana yule. Hata yeye hakuonekana kama alilitarajia jambo lile hivyo aliyumba kidogo ambapo alibaki anahangaika kulitoa lile koti ambalo lilidondokea kwenye uso wake. Alimshambulia kwa ngumi nyingi wakati huo, alizamisha kisu kwenye koti lile ambapo bwana yule alirudi nyuma na kulirusha koti hewani kwa lazima kwani lilikuwa limechanwa na kile kisu.

Wakati koti linatoka kwenye mwili wake ndipo aligundua kwamba kisu hakikumpata mwanaume yule bali kiliishia kwenye koti. Alikirushia mkono mwingine na kukishika vyema ili aweze kushambulia. Kurudi kwake kwa mara nyingine hakupewa muda na nafasi kama zile za mwanzo, bwana yule alikuwa na kasi kubwa zaidi ya ile ya mwanzo ambapo wakati anajiandaa kurusha kisu alitishwa, kutishwa kwake kulimfanya aweze kusita, kusita kwake lilikuwa ni kosa la usalama wake kwani wakati anahisi kwamba mwenzake kamtisha, alikutana na mguu wa goti ambao ulimrudisha nyuma kidogo.

Mguu ulikuwa ni mzito kiasi kwamba balansi haikuwa nzuri hivyo akajikuta anayumba akiwa anayasikilizia maumivu. Alihitaji kusimama vyema lakini aligundua muda ulimkataa kwani wakati huo alikutana na mguu wa kwenye ugoko, alibebwa kwa lazima na mguu wenye nguvu wa yule mwanaume ambao ulikuwa unazunguka. Alijibamiza kwenye pembe ya gari, akiwa pale bado hajasimama alishtuka kukutana na buti la mgongo ambalo lilimburuza tena mpaka kwenye tairi hata kile kisu kilimtoka kwenye mkono wake huku akiwa anamwaga damu na mwili wake ulikuwa umepigiga hivyo hakuwa na uwezo wa kunyanyuka kwa wakati ule. Mwanaume yule alionekana kutabasamu baada ya kuliona begi ambalo ndilo alilijia pale kwani lilikuwa umbali mfupi tu kutoka alipokuwa yule bwana.

“Sijajua kwanini wanadamu mnazidi kuwa wajeuri wakati mnajua kabisa kwamba ujeuri haujawahi kumlipa mtu hata mmoja. Ulikuwa na nafasi ya kwenda kuyaanza maisha yako sehemu nyingine lakini ukaona ujeuri na kuilinda begi ambayo kwa sasa haina kazi yoyote kwako ndilo jambo la msingi zaidi” alitamka yule bwana akiwa analisogeza begi lile kwenye himaya yake.
“Kila unapo liona giza linatanda zaidi basi ujue kwamba mwanga unakaribia kuonekana. Kuna mtu atakuja kuyamaliza haya, sijajua ni lini lakini niamini mimi, wote ambao mmehusika kwenye huu uharamia mtakufa tena kwa mateso na aibu kubwa”

“Ebu nisikilize kijana. Kabla ya kuwa mhamasishaji unatakiwa kutambua kwamba hili ambalo unaliona linatokea kwa sasa halijaja kwa bahati mbaya, ni mipango ya muda mrefu ambayo watu wenye akili zao walikuwa wamelipanga ila kwa sasa unafanyika utekelezaji tu. Hilo ambalo unaliwaza haliwezi kufanyika kwa sasa kwani hata Bazoka mpaka wakati huu ameshakufa, nina imani ndiye huyo ulijua kwamba anaweza kulifanya jambo hili liishe vile anataka ila hawezi. Mlipewa nafsi ya kuleta vitu vya mhimu ili mpewe maisha na nafasi zingine za kufanya kazi lakini mkajifanya kwamba nyie ni waaminifu mno kwa mtu ambaye tayari alishakufa hivyo mkafanya maisha yenu yawe shakani”

“Huu sio mwisho, huu ni mwanzo wa mwisho wa wewe na hao waliokutuma”
“Huenda upo sahihi ila kabla ya hilo kutimia angalau nauona mwisho wako kabla” bwana huyo alizungusha kile kisu na kukizamisha kwenye koromeo la yule mwanaume ambaye alikuwa na asili ya Zambia. Ni baada ya kusikia ving’ora vya polisi vikisogea kwa kasi kwenye hilo eneo hususani baada ya milio ya bunduki kusikika kwani ilitumika kwa mara ya kwanza na yule kijana ambaye aliitumia kumuulia dereva wa hiyo gari ambayo ilikuwa hapo mpaka muda huo.



KKKT MWANZA
Ndani ya kanisa hilo kubwa la kilutheli, alikuwa amesimama Askofu mbele ya kanisa akiwa anatoa neno kuhusu maisha, nidhamu ya kumfikia Mungu lakini uanadamu na utu jinsi unavyoweza kuyabadilisha maisha ya watu na kulifanya taifa kuwa na kizazi bora kijacho. Askofu huyo alikuwa akiheshimika na kupendwa kila kona, alikuwa ni moja ya sababu ya kanisa hilo kuongeza waumini wapya kila ilipokuwa inaitwa leo. Alikuwa ni nguzo kubwa na mhimu kwenye kanisa hilo kwa sababu ya nguvu yake kubwa ya ushawishi ambayo alikuwa nayo, alikuwa mtu safi ambaye hakuwa amepinda hata kwenye jambo moja, ni mtu ambaye alikuwa na mtazamo chanya kuhusu maisha na namna ambavyo watu walikuwa wanatakiwa kuishi kwa pomoja kama jamii ili kuitengeneza baadae ambayo ilikuwa njema.

Gwamba Makwena, ndilo lilikuwa jina lake mwanaume wa miaka hamsini na sita, bwana huyo alikuwa na asili ya taifa la Afrika ya Kusini lakini kwa wakati huo alikuwa ni mtanzania. Baba yake alikuwa ni mfanya biashara wa madini miaka ya zamani, biashara ambayo ilimuingiza kwenye matatizo kiasi kwamba wenzake wakawa wanahitaji kumuua na ndipo alipo kimbilia Tanzania kwa ajili ya kuanza maisha mapya na kwa sababu Tanzania hairuhusu uraia wa mataifa mawili, bwana huyo alilazimika kuweza kuukana uraia wake wa mwanzo ili aweze kupatiwa uraia wa Tanzania jambo ambalo lilikuja kuwezekana miaka mitano baadae tangu aingie kwenye ardhi ya Tanzania.

Kupata uraia ukawa mwanzo wa maisha yake yeye na familia yake kuwa watanzania, walizaliwa na kuishi hapa kama wazaliwa, watoto wake walisoma hapa hapa Tanzania mpaka baadae ambapo kila mtu alihitaji kuweza kupita kwenye njia yake. Gwamba Makwena yeye aliamua kuzifuata hatua hizo za dini ambazo aliamini kwamba zingemfanya kuwa moja ya nguzo za mhimu kwenye kuweza kusaidia jamii na taifa kwa ujumla. Alisoma kwa bidii kubwa mpaka alipofanikiwa kuja kumaliza masomo yake, alikaa mwaka mmoja ndipo akafanikiwa kuwa askofu huko mwanza kazi ambayo aliihudumu kwa miaka kumi. Mwanaume huyo alikuwa anapendwa na waumini wake ndiyo sababu kubwa kwa miaka yote ambayo alikuwa huko hakuwahi kuhamishwa kwa sababu hawakuwa wakimhitaji askofu mwingine aweze kuwasimamia wao zaidi ya kumtaka tu bwana huyo ambaye umri wake kidogo ulikuwa unakimbia kwa spidi kubwa.
Episode ya sita ya simulizi hii inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 7.
ENDELEA.......

“Tafsiri sahihi za jamii na maisha yetu hazipo kwenye kutafuta maana ya hayo maneno, bali zipo kwenye yale ambayo sisi tunayaishi. Nikiwa na miaka saba tu kuna siku baba yangu aliwahi kuniuliza “Mwanangu ukiwa mkubwa unataka kuwa nani au kufanya nini?” kwa mara ya kwanza nilihisi ananiuliza ili kunitania ama kunipima tu lakini baadae niligundua kwamba alikuwa anamaanisha kuliko mimi nilivyokuwa nadhani, lengo lake kubwa alitaka kujua aina ya ubinadamu ambao upo ndani mwangu. Nilikuwa bado mdogo lakini naweza kumpongeza yeye kwa sababu alinikuza vyema hivyo nilituliza kichwa na kumpatia jibu ambalo nadhani hata yeye mwenyewe hakuamini kama naweza kumjibu kwa busara namna ile “Nataka kuisaidia jamii yangu” nilimjibu kiufupi na kumpa nafasi kwa sababu alibaki ananitazama kwa muda akionekana wazi kwamba alikuwa na mambo mengi anayawaza.

“Utaisaidiaje jamii yako?” ni swali lingine ambalo lilitoka kwake kiasi kwamba nikawa kama nipo njiapanda. Nilijua lile swali ndilo lilibeba msingi halisi wa mimi nataka kuwa nani kwa baadae. Nililazimika kumwambia kwamba nataka kuyatoa sadaka maisha yangu, nitafanya kila jambo ambalo linawezekana kiasi kwamba hata kama sitakuwa mwanzo wa suluhisho kwenye matatizo mengi basi nitahakikisha siwi sehemu ya tatizo kwa mtu yeyote yule bali nitaitumia nafasi yangu na uwezo wangu mdogo na kuhakikisha natumia rasilimali yoyote ambayo nitakuwa nayo kuweza kubadilisha maisha ya watu. Hata kama ningebadilisha maisha ya mtu mmoja tu basi, kwangu ingekuwa na maana kubwa mno kwani nilikuwa na imani kwamba yule mmoja ambaye mimi nitamsaidia hata yeye alikuwa anaenda kumsaidia mtu mwingine, naye yule mwingine angeenda kumsaidia mwingine hivyo niliamini kwamba kwa mlolongo huo angalau baada ya miaka hata kumi kungekuwa na watu hata miamoja ambao wangekuwa wamesaidika kupitia mimi.” Hilo ndilo jambo ambalo nilimueleza kwamba naenda kulifanya.

Kwa mara ya kwanza kabisa nilimuona baba yangu akiwa na furaha ambayo asingeweza kuificha mbele yake. Aliniambia kwamba anajivunia mno kuwa na mtoto kama mimi lakini alinipa somo moja kubwa ambalo mpaka leo nimekuwa naliishi “mwanangu najua una hamu ya kufanya hayo yote na huenda kwa sasa imekuwa kama ndoto kwako lakini kuna jambo la msingi zaidi ya hilo. Kama kweli unataka kuwa msaada kwa watu na kubadilisha maisha yao basi hakikisha kwanza unajisaidia wewe, kwa sasa wewe bado ni mdogo na mara nyingi ukiwa mdogo unaweza ukawa na ndoto nyingi ambazo kwenye uhalisia hazipo na kama zipo basi kuzitimiza ni jambo gumu ila kadri utakavyokuwa unazidi kukua utagundua kwamba dunia ni ya tofauti na unavyo iona wewe kwa sasa. ukiwa mkubwa utakutana na wanadamu ambao wana maudhi ya kutisha, wanadamu ambao ni wakatili, kuna nyakati hata baadhi ya watu wako watakukana na ili uwe msaada kwa watu wako basi unatakiwa kwanza kuvishinda hivyo vyote na uhakikishe kwamba unabaki kwenye mstari ambao umenyooka na jambo hilo sio rahisi kwa sababu kuna vitu kwenye maisha yako inabidi ukubali kuvikosa ama kuvipuuza hata kama ni vya mhimu kiasi gani. Hakuna mafanikio ya jambo lolote bila kujitoa sadaka mwanangu” yale ni maneno ambayo aliyaongea kwa uchungu mno na hakuongea tu kama baba yangu bali aliongea pia kama mwanaume mwenzangu.

Yale maneno yake kwa wakati ule niliyaona kama mzazi anataka kuhakikisha mwanae ananiweka kwenye mstari ambao upo imara ila sikuyatilia maanani sana kwa kipindi kile mpaka nilipokuwa mkubwa ndipo nilikuja kuyaelewa vizuri. Ilifika wakati ambao mimi nilikuwa natakiwa kufanya maamuzi magumu kwa ajili ya yale ambayo niliyaongea na baba yangu nikiwa mtoto. Ni wakati ambao mimi nilitakiwa kufanya maamuzi ya kweli kwamba naenda kuwa nani kwa sababu hayo maamuzi ndiyo yalikuwa yanaenda kuibeba baadae yangu yote hivyo sikutakiwa kufanya makosa hata kwa bahati mbaya.

Sasa niligundua kwamba ni kweli hakuna jambo kubwa ambalo unaweza kulifanikisha bila kutoa sadaka kwenye haya maisha. Ni kweli niliahidi kuisaidia jamii yangu ila kivipi sasa? kumbuka wakati huo dunia ilikuwa inaanza kuwa tamu kwangu kwa sababu nilikuwa kijana, kila jambo zuri lilionekana mbele yangu lakini niligundua kwamba ile dunia ilikuwa inaenda kuniweka mbali na ndoto yangu ya kusaidia jamii. Kivipi? Maana yake ningeamua kwenda nayo basi hii leo nisingekuwa mbele yenu ndani ya hili kanisa kuwapa hili somo, ilinilazimu niyakatae yale maisha ya ulimwengu wa kawaida na kuamua kumsogelea Mungu ili niwe msaada kwa jamii kama ambavyo nilimpa ahadi baba yangu japo kwa wakati ule sikuwa nafanya maamuzi kwa ajili ya baba yangu bali kwa ajili yangu mimi mwenyewe.

Kile ni kipindi ambacho kilikuwa ni kigumu kwangu, niliwapoteza marafiki zangu wengi mno, niliyapoteza maisha yangu ya mwanzo yote nikaamua kupambana na hii safari ambayo mwanzo sikuwa na uhakika nayo. Nikiwa muwazi ni kwamba utotoni sikuwahi kufikiria kabisa kuja kuwa Askofu ila kwa baadae ilinilazimu mimi kuwa hivyo kwa sababu ya watu ambao mpo ndani ya hili jengo muda huu. Niliamua kukatisha ndoto zangu zingine niweze kuwa hapa siku ya leo nikiutaja ukuu wa muumba mbele yenu lakini kuwapa mafundisho sahihi kuhusu maisha ambayo tunayaishi ambayo muda wowote yanakuwa sio yetu tena. Namaanisha nini kusema hivyo?

Maana yangu ni kwamba hapa duniani hakuna jambo ambalo linakuja kirahisi, hakuna jambo ambalo unaweza ukalala tu usiku na asubuhi ukaamua ukakuta limetimia, kila jambo linahitaji muda, imani, maamuzi magumu lakini ambayo ni sahihi. Hili linatufundisha kwamba kwenye maisha ya mwanadamu kuna nyakati ambazo zinakuja zitakuwa ngumu kwako, kuna nyakati ambazo utalazimika kufanya maamuzi ya kuchagua kuyaacha baadhi ya mambo hata kama ni ya mhimu vipi kwako. Siku zote hauwezi kuwa na kila kitu, lazima utapoteza baadhi ya vitu ili upate kingine kwahiyo usihadaike kuingia kwenye ulimwengu ambao haufai kwa kujitoa utu wako ama kutoa utu wa watu wengine kwa sababu tu umeahidiwa jambo fulani ambalo kwa wakati huo unaona ni zuri. Ukiona jambo ni zuri kwa muda mfupi basi likimbie kwa gharama kubwa hata kama ni zuri vipi kwako kwa sababu litakuwa na matokeo mabaya kwa baadae.

Wajali ndugu zako, wajali marafiki zako, ijali familia yako lakini kabla ya hao wote jijali wewe kwanza kwa sababu kama wewe ukiweza kujijali basi bila shaka unakuwa una uwezo wa kuweza kuwajali watu wengine. Mwandishi mmoja aitwaye Steven Bartlett anasema kwamba huwezi kuwasaidia wengine kama ndoo yako bado ni tupu, maana yake ni kwamba hakikisha unaijaza ndoo yako kwanza kisha baada ya hapo ndipo uende kuwasaidia watu wengine. Hiyo ndiyo ilikuwa maana halisi ya ile kauli ya baba kwamba kama unataka kuibadilisha jamii basi wewe ndiye unatakiwa kuwa mtu wa kwanza kuweza kujibadilisha na kuibadilisha nafsi yako hapo ndipo utahamia kwa watu wengine” askofu alitoa somo kubwa ambalo lilifanya watu wote wabaki kimya wakiwa makini kuyasikiliza yale madini ambayo alikuwa anayatoa kutoka kwenye ubongo wake.

Baada ya kutulia ikiwa ni kama ishara ya kumaliza, vifijo na nderemo zilifurika kwenye hilo jengo watu wakiwa wanashangilia na kupiga makelele, ndiyo sababu kubwa ambayo hawakuwa wanahitaji bwana huyo aweze kuondoka kwa sababu kila siku alipokuwa anapanda madhabahuni basi alikuwa na mengi ya kuweza kuyazaja kwenye vichwa vya waumini wake. Hakuwa tu askofu bali kwao alikuwa kama mwalimu na msimamizi wao kuanzia kwenye suala la maisha pamoja na miongozo ya kiimani. Alikuwa ni zaidi ya shule askofu Gwamba Makwena.

Akiwa amesimama pale mbele watu wakiwa wanaendelea kushangilia kwa makofi mengi, mwanaume mmoja ambaye alikuwa amevaa suti ya blue alinyanyuka kutoka kiti cha nyuma kabisa, bwana yule alikuwa nadhivu mno. Alianza kujongea kuelekea mbele huku akiangaza pande zote za kanisa hilo, kwenye kila kona ya kanisa walikaa wanaume wawili wawili ambao walikuwa kama waumini wa kawaida lakini bwana huyo aligundua kwamba walikuwa ni walinzi wa askofu huyo kuhakikisha kwamba yupo salama kwa nyakati zote hivyo alitabasamu.

Kutembea kwake kuendelea kusogea mbele kuliwapa umakini watu wale lakini hata askofu alibaki anamtazama bwana yule kwani hakuelewa kwamba ni jambo gani lilikuwa linampeleka wakati hata ibada yenyewe haikuwa imeisha bado. Waumini hawakuwa na muda naye sana lakini wale walinzi walianza kujongea kidogo kidogo kuelekea alipokuwepo askofu. Baada ya bwana yule kuweza kusogea zaidi alisimama, kusimama kwake kulimfanya askofu amtambue mtu yule. Uso wake ulionyesha mabadiliko ya mshtuko ambao aliupata baada ya pale kwa sababu alionyesha kabisa kwamba alikuwa akimujua mtu yule bila shaka.

Akiwa anaendelea kumwangalia bwana yule kwa shauku na hofu ambayo bila shaka iligubika kwenye moyo wake hata walinzi wake walifanya kosa kwa sababu walikuwa wanakimbilia alipo Askofu na wengine wakawa wanaelekea alipokuwepo bwana yule kwani walikuwa na uhakika kwamba hakuwa ameenda pale kwa ajili ya wema bali kulikuwa na jambo baya ambalo lilikuwa linaenda kutokea lakini hilo lilikuwa kosa kubwa kwao. Walimzingatia mtu mmoja bila kutumia akili kwamba huenda kulikuwa na mtu zaidi ya mmoja na ndilo jambo ambalo lilitokea pale.

Muda ambao waliutumia kumzingatia yule bwana, alinyanyuka mwanaume mmoja ambaye naye alivaa suti, yeye alikuwa karibu na mbele na wakati ananyanyuka kwenye mkono wake alikuwa na silaha. Alipiga risasi mbili ambazo zilienda kutua kwenye moyo wa Askofu, walinzi wake walitoa silaha pia lakini muda haukuwa kwao kwa sababu milio ya zile risasi iliwatawanya watu ambao walinyanyuka na kuanza kukimbia hovyo hovyo kila mtu akitaka kuiponya nafsi yake hivyo watu wale wakaingiliana wote hawakuelewa washambulie wapi zaidi ya kujitahidi kumuwahisha hospitali Askofu. Walinzi kadhaa walihangaika kuwatafuta watu mle ndani lakini mpaka watu wote wanaisha, hawakuwaona wale watu tena na taarifa mbaya ni kwamba askofu alikuwa amekufa tayari ikiwa haieleweki sababu za msingi za yeye kuweza kuuliwa tena akiwa madhabahuni.

Episode ya 7 inafika mwisho, tukutane ndani ya episode ijayo.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 8.
ENDELEA.......


IKULU
Dar es salaam ilikuwa imenoga, jiji lilikuwa na shamra shamra za kila mahali, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vilifurika watu ambao wengine walikuwa wanatofautiana mawazo huku wengine wakiwa wamejawa na furaha isiyo na maelezo ya kutosha. Hakukuwa na utulivu ni kila mtu alivyokuwa anajisikia yeye ndivyo ambavyo alikuwa anafanya kwa nyakati hizo, watu wa vijiweni hawakuwa nyuma kabisa, walikuwa wapo makini kuhakikisha zile soga kuhusu siasa hazikauki kwa upande wao, watu hao waliamini kwamba wao siasa ilikuwa ni sehemu kubwa ya maisha yao japo wengi hawakuwa wakihitaji kujihusisha nayo moja kwa moja kwani hawakuwa na imani na vyombo ambavyo vilikuwa vikihusika kwenye usimamizi wa jambo hilo. Watu hao ambao wengi wao walikuwa vijana ambao ndio taifa lilikuwa linawategemea kwa ukubwa kuweza kulijenga taifa lijalo ni kama walikuwa wamejikatia kabisa tamaa kwenye upande huo wa siasa ila hawakukosa mambo kadhaa ya kuyazungumzia ambayo waliona kwamba yalikuwa yakiwahusu moja kwa moja kwenye upande huo.

Maeneo ya Biafra Kinondono, moja ya sehemu zenye vijiwe maarufu na vikongwe zaidi jijini, kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa wanaizungumzia siasa kwa undani wake lakini kwa tahadhari kubwa, hakuna ambaye alikuwa ana imani kwa wakati huo kwamba angekuwa salama baada ya kongea kwakuwa taifa halikuwa kwenye utulivu bado hivyo kila mtu alikuwa makini kuhakikisha anajilinda na kuwa salama yeye kama yeye.

“Haya mambo yaliwahi kutabiriwa miaka ya nyuma huko, kuna viongozi ambao walikuwa mashujaa wakubwa, walilipenda hili taifa na kuamua kulipigania kwa moyo wao wote lakini mwisho wao haukuwahi kuwa mzuri hata siku moja. Waliishia pabaya kwa sababu kwenye taifa letu wengi wanakula kwa njia ambazo sizo, taifa letu hata matajiri waliopo wengi ni wale matajiri ambao wameumiza mno roho za watu na wanafuja kodi za watu ndo wanafika pale hivyo akija mtu mzalendo kwenye taifa hili kwao anakuwa adui namba moja kwa sababu anaanza kurejesha kila ambacho walikibeba na wao hawapo tayari kwa jambo hilo” kijana mmoja ambaye alikuwa ameshika kilevi kikali majira hayo ya asubuhi aliropoka kwa sauti kubwa akiwa kama ni mtu aliyekuwa amejikatia tamaa ya maisha.

“Unamaanisha nini kuweza kusema hivyo Bili?”
“Ndugu yangu ni jambo gani ambalo haulielewi wewe hapo? Raisi amekufa kwenye njia ambazo hata hazieleweki halafu wanatutolea taarifa ya kipuuzi utafikiri kwamba ni mbwa amekufa jambo ambalo sio kweli. Hili taifa limelaaniwa ndugu yangu, hakuna hatua tunaweza kupiga kwa sababu kila mtu ni kibaraka wa mtu fulani. Raisi ambaye amekufa akiwa madarakani ndiye mtu ambaye alikuwa anaweza kulipeleka taifa hili mbali kuliko mtu yeyote yule lakini asingeweza kufika huko kwa sababu kila ambaye anamzunguka alisha iuza roho yake na tunapo elekea ni pabaya zaidi ya kule ambako tunatoka” kijana huyo aliongea kwa uchungu yale maneno yake, alionekana kabisa kuwa na jambo ambalo alilifahamu lakini kwa sababu ya ulevi wake hakuna ambaye alikuwa anamzingatia, wengi walihisi ni maisha yamempiga ndiyo maana hakuonekana kuwa sawa.

“Bili nahisi umekesha bar hakuna lolote ulijualo hivyo badala ya kuongea huu ujinga ambao hakuna ulijualo, ni bora ukaenda geto kwako uweze kulala” aliongea mwanaume mwingine ambaye kwenye mkono wake alikuwa ameshika chupa kubwa ya maji akiwa na mikogo mithili ya mtu ambaye alikuwa amejipata kwenye maisha yake.

“Nyie wote ni wapumbavu tu, mtaendelea kupelekeshwa kama manyumbu, wajinga wakubwa nyie” alitamka kauli yake tena kwa hasira zaidi huku akianza kutoka kwenye kijiwe hicho baada ya kuona watu hao walikuwa wanawaza vitu tofauti na uhalisia ulivyokuwa. Ziliendelea soga maeneo hayo huku kila mtu akiwa anazipamba siasa, kila mtu alimnadi mtu wake na kujimwambafai kwamba hakuna ambaye alikuwa anaijua siasa zaidi yake yeye hivyo kila mtu akajikuta mwalimu eneo hilo.

Hayo mazungumzo yao yalikuja kutokana na tukio ambalo lilikuwa linaendelea wakati huo, tukio kubwa mno kwa ajili ya taifa zima. Ulikuwa unafanyika uapisho wa raisi mpya ambaye alikuwa anatakiwa kuingia madarakani kuanzia siku hiyo. Hilo lilikuja baada ya raisi ambaye alikuwa analiongoza taifa kufia madarakani tena ghafla kifo ambacho kiliibua mijadala mingi kila pembe na kila kona ya nchi lakini hakukuwa na jambo lingine ambalo lingeweza kufanyika zaidi ya kukubali kwamba raisi huyo alikuwa amekufa. Raisi ambaye alifia madarakani alikuwa ni mtu ambaye alipendwa na watu waliokuwa wanaiwaza baadae, alikuwa ni mtu muwajibikaji haswa, alikuwa ni mtu ambaye hakutaka hata siku moja kuona watu wake wakiteseka lakini aliamini ili kuweza kufika huko ni lazima kwanza watoe jasho haswa, hakuna mafanikio yanakuja bila kutoa jasho, ni lazima kwanza utoke jasho haswa ndipo uweze kupata kile ambacho wewe unakitaka.

Ikulu, jaji mkuu alikuwa ameishika katiba kwenye mkono wake akiwa anamuapisha raisi mpya wa Tanzania ambaye alikuwa anaenda kuishika nafasi ya yule ambaye alifia madarakani. Bwana ambaye alikuwa anaapishwa wakati huo alikuwa ni gwiji haswa wa siasa, hakuwa mnyonge kwenye hiyo kona kwa sababu alikuwa analijua vyema kila eneo ambalo lilikuwa linagusia siasa, alikuwa ni mtu ambaye alikuwa na matamanio na matarajio makubwa mno kwenye siasa ndiyo sababu baadhi ya watu walilalamika na kudai kwamba hakuwa mtu sahihi kabisa kuweza kuliongoza taifa kwani hakuwa na maamuzi kama kiongozi wa juu, alikuwa ni mtu ambaye udhaifu wake ungelipelekea taifa sehemu ambayo siyo lakini mwisho wa siku hakuna mtu angeweza kuubadilisha huo uhalisia kwa sababu mambo yalikuwa yanaenda hivyo hata kama watu hawakuwa wakitaka iwe hivyo.

Darian Julius, ndiye alikuwa raisi mpya ambaye alikuwa anatakiwa kulivusha taifa kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ambayo wengi waliamini kwamba ilikuwa ni nchi ya ahadi japo hakuna mtu ambaye alikuwa na uhakika juu ya jambo hilo. Bwana huyo ndiye ambaye alikuwa anaapishwa nyakati ambazo vijana walikuwa wamekaa kwenye kijiwe kuweza kupiga stori na vibonzo kuhusu taifa lao, kuna ambao walionekana kujali lakini kuna ambao hawakuonyesha kujali kabisa kwani waliamini hayo hayakuwa yakiwahusu kabisa zaidi ya kuwahusu wanasiasa wenyewe.

Baada ya kuapishwa kiongozi huyo, kisheria na kikatiba alikuwa tayari ni raisi, siku hiyo ilikuwa ni ngumu na ndefu kwa upande wake kwa sababu aliitumia miaka mingi kuweza kuisubiria kwa hamu kubwa lakini alihisi kama vile haikuwa ikifika mpaka nyakati hizo ambazo zilimkutia akiwa ndani ya ofisi hiyo kubwa zaidi kwa mara ya kwanza. Alijiona mtu mwenye furaha kubwa mno kwenye nafsi yake, alijiona kuwa ni shujaa ambaye alistahili kila aina ya sifa na pongezi kutoka kwenye kila pembe ya ulimwengu kwa yeye kuifikia nafasi ambayo imekuwa ndoto ya watu wengi lakini wenye uwezo wa kuifikia ni watu wa kuhesabu.

Alikuwa anajipongeza yeye mwenyewe mpaka pale ambapo simu moja iliita kwa nguvu, alishtuka na kugundua kwamba ni simu yake binafsi ilikuwa inaita hapo ndopo akakumbuka jambo wakati anaisogelea na kuitazama kwa kina. Alikumbuka kwamba tangu jana yake hakushika kabisa simu kwa sababu hakutaka kupokea habari ambazo zingemharibia siku yake, siku ambayo aliiona kuwa siku bora zaidi ya siku zote ambazo amepata kuishi duniani. Baada ya kuwaza kuhusu jambo hilo hapo ndipo akaipokea huku akishusha pumzi yake kwa nguvu kubwa.

“Nipe taarifa kamili” aliongea akiwa anailegeza tai yake shingoni ili kupokea taarifa ya upande wa pili.
“Begi limepatikana kiongozi, muda mfupi ujao nalileta Ikulu lakini Bazoka amefanikiwa kukimbia” alipokea habari njema na mbaya kwa wakati mmoja, alitulia kwanza bila kujibu kwa sababu alipatwa na furaha na hasira kwa wakati mmoja lakini hasira zilizidi kiwango cha furaha.

“Sijakuelewa, amekimbia kivipi labda?”
“Walimjeruhi lakini alipona na bado yupo hai”
“Wewe mpuuzi nilikwambia kama hauiwezi hii kazi nimpe mtu mwingine ukajifanya unaiweza, unajiamini vipi kuja kunipa mimi taarifa kama hii?” aliongea kwa kufoka akiitupa tai mbali na pale ambapo alikuwepo.
“Mhes……”

“Mpuuzi wewe, nakupa nusu saa, uwe umefika hapa Ikulu uje unieleze kama unastahili kuendelea kufanya kazi na mimi tena” aliibamiza simu kwa kuitupa na kuonekana kukosa utulivu. Siku ambayo ilionekana kuwa bora mno kwake ilianza kuwa na dosari kadhaa ambazo yeye aliona kabisa kwamba zingekuja kuwa na madhara kwa hapo baadae, liilionekana kuwa jambo ambalo alihitaji liishe kwa muda mwafaka na mpaka nyakati hizo alikuwa anaamini kwamba habari hizo zilikuwa njema lakini baada ya kuzipokea ndipo aligundua kwamba zilikuwa tofauti kabisa na yale ambayo yeye alikuwa anayatarajia, hazikuwa njema kabisa na alitakiwa kumalizana nazo mapema.

Episode ya 8 inafika mwisho, tukutane ndani ya episode ijayo.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 9.
ENDELEA.......

Dakika thelathini na tano zilipita mwanaume mmoja alikuwa anaingia ndani akiwa na walinzi kadhaa huku mkononi akiwa na begi! Ni yule ambaye jana yake usiku alionekana Tunduma akiwa anatoa maagizo kwa mwanaume mmoja kuhakikisha anaipata ile begi ambayo ndiyo hiyo alikuwa nayo kwenye mkono wake.
“Wewe mjinga una sababu zipi za msingi za kukufanya uendelee kuwa sehemu ya watu wangu?”

“Kiongozi naomba unisikilize kwanza ndipo uweze kufanya maamuzi” aliongea akiwa anameza mate kwa shida, raisi alikuwa amemkazia macho tu ikiwa ni kama ishara ya kumtaka aweze kuendelea na lile ambalo lilimleta sehemu ile.
“Mpango ulikuwa unaendelea kama ambavyo tuliupanga sisi, yule mwanamke ambaye yeye alikuwa anamuamini alimpatia sumu ambayo ilianza kumuathiri taratibu hivyo wakatumwa vijana kuweza kumaliza kazi ya mwisho. Lakini bwana yule alifanikiwa kutoroka na kukimbilia kwenda kule msituni, huko alikuwa anafuatwa na watu wetu ambao walifanikiwa kumjeruhi wakati huo sumu ilikuwa imesambaa kwenye mwili wake kwa taarifa iliyopo lakini baada ya pale inadaiwa kwamba alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha”

“Mtu ambaye amejeruhiwa na mwili wake una sumu anapotea vipi kwenye mazingira ya kutatanisha?”
“Inaonekana kwamba kuna mtu alimpatia msaada akiwa kwenye hatua zake za mwisho”
“Kuna mtu mwingine alikuwa anajua hili jambo?”
“Hapana”
“Sasa huo msaada aliutolea wapi?”
“Hilo ndilo jambo ambalo nalifanyia kazi mpaka sasa”

“Nisikilize kwa umakini Yahya, sijali kwamba huyu mtu yupo wapi, aliokolewa na nani ila nataka kusikia taarifa ya kwamba amekufa au akipatikana hai basi aletwe kwangu, na kama ukishindwa kuitekeleza hii kazi kwa muda ambao nautaka mimi basi sahau kuhusu hiyo nafasi yako tena kwa sababu unaonekana kabisa kwamba hautakuja kunifaa huko mbeleni”

“Nakuelewa kiongozi ila inadaiwa kwamba amepotelea karibu na kile kijiji cha Banzoka”
“Samahani umesema?”
“Kuna kijiji ambacho kinadaiwa kwamba kilitelekezwa miaka mingi iliyopita ambacho kwa sasa kinadaiwa kuwa kijiji cha mizimu ndiko ambako alipotelea karibu na huko” raisi alionekana kushtuka baada ya kusikia taarifa hizo, alionekana kabisa kujua jambo kuhusu sehemu hiyo.

“Nenda” alimtamkia bwana huyo ambaye aliliweka vizuri begi mezani na kuweza kutoka lakini hata yeye mwenyewe hakuelewa kwamba bosi wake alikuwa ana shida gani haswa mpaka aonekane kuguswa mno na habari hizo. Alianza kutembea kuelekea mlangoni mpaka pale ambapo alisikia amri ikipenya kwenye masikio yake tena ikiwa ya mamalaka na sauti nzito ambayo ilikuwa imenyooka.
“Hakikisha huyo mtu anakufa kwa namna yoyote hata kama italazimu kuua watu wengine miamoja” ni sauti ambayo ilipenya vyema na kusikika kwenye ngoma za masikio yake kwa usahihi kabisa, aligeuka na kuinama kuweza kutoa heshima kwa raisi wake kisha akatoweka humo ndani. Raisi alibaki amesimama lakini hakuweza, alianza kuzunguka zunguka kila sehemu kuweza kutafuta nafasi ya nafsi yake iweze kutulia lakini ilishindikana kabisa hali ambayo iliifanya siku yake kuanza vibaya ikiwa ndiyo mara ya kwanza kabisa kuweza kuingia Ikulu kula mema ya nchi.


Nyakati hazisimami kabisa, nyakati zinakimbia haswa, ilikuwa imefika usiku majira ambayo sherehe za kumpata raisi mteule zilikuwa zikiendelea. Viongozi wengi wa kisiasa walikuwa wanazitumia akaunti zao za mitandao kuweza kumsifu na kumpamba kiongozi huyo, hawakuwa wakimpenda kweli bali unafiki wa siasa kama ilivyo siku zote watu hao wanapokuwa wanazihitaji nafasi na teuzi mbali mbali. Kila mtu alikuwa akiigiza kumkubali mno raisi huyo, wengine waliinadi kwa kuipamba historia yake ili ionekane ni safi mbele ya kila mtu jambo ambalo kiuhalisia halikuwa la kweli.

Wakati wao wanaendelea kumpamba bwana huyo, yeye wakati huo hakuwa na huo muda kabisa baada ya kuhisi kwamba mambo hayakuwa sawa, kutokuwa sawa kwa mambo yake ndiko ambako kulimfanya yeye kusafiri mpaka pwani, alienda Bagamoyo usiku huo akiwa na msafara wa gari mbili tu ambazo ziliondoka kwa siri. Alitembea na msafara mdogo kwa sababu hakutaka kabisa ijulikane kwamba alikuwa ametoka tena bila taarifa kwa watu wake wa karibu. Kutoka kwake usiku huo ilikuwa ni safari moja ambayo ilikuwa ni ya umuhimu mno kwake kwa sababu alimfuata mganga wake ambaye alikuwa akimuamini kwa miaka kadhaa na hata wakati huo aliamini kwamba bwana huyo ndiye ambaye alikuwa amemuweka madarakani hivyo kwake jambo hilo lilikuwa na umuhimu mkubwa isivyokuwa kawaida. Baada ya safari ya muda mrefu kidogo huku akiwa ana mawazo mengi, safari yake iliishia nje ya nyumba moja kubwa ila ya zamani japo ilikuwa imewekwa kwenye mazingira ambayo yalikuwa bora. Eneo hilo usiku huo halikuwa na mtu hata mmoja, taarifa za kuja kwake zilikuwa zinajulikana kwa mmiliki wa eneo hilo hivyo alihakikisha kwamba hakuna mtu mwingine ambaye anakuwepo wakati mheshimiwa anafika hapo kupata huduma.

Alipokelewa kwa heshima na furaha, huyo mganga alikuwa ni mtu wake wa karibu kwa miaka kadhaa sasa hivyo alikuwa anazijua siri zake nyingi mno mwanasiasa huyo ndiyo maana hata wakati huo baada ya kuona mambo yanaanza vibaya aliamua kumfuata mtu wake ili aweze kumpa tafsiri ya mambo kadhaa.
“Haijawahi kutokea ukaja kwangu ghafla namna hii, inaonekana kabisa ambako umetoka sio kwema”
“Ni kweli kabisa unalo liongea, sielewei mustakabali mzima wa hatima ya maisha yangu hasa baada ya kulifanikisha jambo ambalo nimelipigania kwa muda mrefu na najiona kabisa kwamba sina furaha kama ambavyo nilikuwa nategemea kuipata”

“Ni jambo gani linakusumbua kwa sasa?”
“Mlinzi wa Philip yupo hai”
“Unamaanisha mlinzi wa mtangulizi wako?”
“Ndiyo”
“Sasa yeye kuwa hai kuna shida gani labda?”
“Anajua kila kitu na kuna taarifa ambazo anazo kichwani mwake anatakiwa kufa nazo mwenyewe”
“Unamaanisha anajua kwamba wewe ndiye umemuua mwenzako?”
“Hapana, sina imani na hilo jambo, nina uhakika anajua kwamba bosi wake hakufa kifo cha kawaida, anaelewa kabisa kwamba aliuawa na ni suala la muda tu kabla hajajua kwamba mimi ndiye ambaye nilikuwa nyuma ya hili jambo”

“Kwahiyo unahisi kwamba anaweza kuzitumia hizo taarifa ambazo unadai anazo zikaja kukuathiri wewe?”
“Ndiyo maana nipo hapa muda huu”
“Sasa hilo jambo ni lako wewe, kama unajua hilo maana yake unatakiwa kumtafuta huyo mtu uone kama ana hizo taarifa kweli na kama anazo basi unaweza kumuua”
“Alitakiwa kufa jana lakini ametoroka”

“Kivipi?”
“Huyu mtu sio mtu wa kawaida wa kusema utamuua tu ukijisikia, ni miongoni mwa watu wazito mno, ukiisoma historia ya huyu bwana inatisha mno na kupona kwake jana kuuawa lilikuwa ni kosa kubwa ambalo linaweza kuja kuwa hatari mno kwangu kwa siku za hapo mbeleni”
“Bado sijakuelewa kwanini upo hapa Darian jambo ambalo unajua kabisa sina namna ya kukusaidia”
“Sipo hapa ili uweze kunisaidia kumkamata”
“Ila unataka nikusaidie nini?”

“Nataka unitabirie, nataka uangalie mwisho wangu utakuwaje, nataka kujua ili nijiandae na nijue ni jambo gani la kulifanya kabla sijaingia sehemu ambayo inaweza kuwa mbaya kwangu”
“Mhhhhh unataka nikutabirie mwisho wako?”
“Ndiyo, ndiyo”
“Hapana Darian, siwezi kufanya jambo kama hilo”
“Kwa sababu zipi?”

Wana yapi ya kuyajua hawa watu wawili? Binafsi episode ya tisa nisema nafika mwisho, panapo majaaliwa tukutane ndani ya episode ijayo.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 10.
ENDELEA.......


“Siri ya maisha bora ya mwanadamu ipo kwenye kutoyajua mambo ambayo yanakuja baadae, hata Mungu mwenyewe alikuwa na kusudi kubwa kufanya hivyo kwa sababu ukijua jambo ambalo linakuja, niamini mimi hata kiti hicho utaona kama gereza la kutisha. Hivyo sio kama mtaalamu wako tu bali kama mtu ambaye tumejuana kwa muda mrefu nakushauri, usifanye hilo jambo ni hatari mno kuijua baadae yako”
“Naelewa hatari yake ndiyo maana nipo hapa nahitaji kuweza kuijua”
“Una uhakika na hili jambo?”

“Ndiyo” mtaalamu alimwangalia kiongozi huyo ambaye alikuwa anajikaza kuongea lakini mwili wake ulikuwa ukitokwa na jasho kila sehemu, hata mapigo yake ya moyo alihisi kama vile yanamsaliti maana yalikuwa yanaenda mbio kama mtu aliyekurupushwa kwenye fumanizi. Mtaalamu alimwangalia kwa umakini kiongozi huyo na kusikitika ila hakuwa na namna kwa sababu alikuwa ni mteja wake wa miaka mingi kiasi kwamba wakawa ni marafiki wakubwa. Alisogeza vifaa vya kazi ambapo kulikuwa na dishi moja la plastic ambalo juu yake lilikuwa na kioo kimoja kizito ambacho kilifunika eneo hilo lote na kufanya ndani yake kusiwe kunaonekana kabisa. Mtaalamu alimtaka mheshimiwa kunawia juu ya kioo hicho na baada ya hapo alimkata kwenye mkono kidogo ambapo alimtaka damu hiyo aizungushie kwenye hicho kioo.

Raisi alifanya hivyo huku akiwa anahema kwa nguvu na wasiwasi ulizidi kumjaa kwenye nafsi yake. Baada ya kukamilisha hilo zoezi hapo, yule mtaalamu alianza kunuwia maneno ya ajabu huku kwenye mkono wake akiwa na upembe mmoja na mkia ambao haukueleweka ulikuwa wa mnyama gani. Alinuia kwa muda wa dakika tano kisha akatulia na kumwangalia tena raisi, alimuuliza kwa ishara kama alikuwa tayari na raisi alijubu kwa hofu kwamba alikuwa tayari kwa jambo lolote lile ambalo lilikuwa linakuja mbele yake hivyo akaambiwa aweze kuangalia kwenye kioo hicho. Aliangalia eneo hilo kwa dakika moja tu pekee, alinyanyuka na kutaka kukimbia huku akiwa anapiga kelele za hofu na kupingana na jambo lile.

Alirudi na kuketi akiwa anameza mate kwa shida mno, hakuamini kama aliyo yaona pale yalikuwa ni maisha yake ya huko mbeleni. Alivua koti la suti na kulitupia pembeni, hata ile tai yake ambayo alikuwa nayo ilionekana kuwa nzito.
“Hii ina maana gani?” alimuuliza mtaalamu akiwa anahisi kwamba alikuwa anachezewa akili yake.
“Unajua ni kwanini nilikukataza kuangalia maisha yako ya baadae?”
“Hapana”
“Kwa sababu kiuhalisia ni kwamba hakuna mwanadamu ambaye atakuwa na mwisho mwema linapokuja suala la uhai wake. Hautakiwi kujua utakufa lini wala utakufaje na kama ukifanikiwa hata kwa bahati mbaya kujua hilo basi unaweza kuwa binadamu wa hovyo zaidi kuwahi kuishi duniani hapa”

“Unamaanisha nini kuniambia haya?”
“Ni kwamba nilijua kwa mtu kama wewe tena mwanasiasa lazima mwisho wako uwe wa kutisha ila kwa sababu ulitaka iwe hivyo basi sikuwa na namna! Je unataka kumalizia kujua nini kitafuata?”
“Hapana, hapana, sitaki kujua tena”
“Basi nafikiri kazi yangu imeishia hapa”
“Ila nataka kujua uhusiano wa jambo hilo na zoezi la mimi kumtafuta huyu mtu”
“Ina maana kwamba kama wewe ukishindwa kumpata mapema, basi huyo mtu ndiye ambaye atakuua wewe tena utakufa ukiwa hauna msaada wowote”

“Hilo haliwezekani”
“Kama unataka kuthibitisha kwamba inawezekana basi hakikisha unamalizia kuangalia”
“Unataka kuniambia nini labda?”
“Ni kwamba una mawili, ukifanikiwa kumuua wewe kuna uwezekano maisha yako ya baadae yakawa tofauti lakini kama utashindwa kufanya hivyo maana yake ni kwamba yeye ndiye atakaye kuua wewe”
“Unaamini kama Mungu yupo mtaalamu?”
“Hata mizimu inajua kwamba Mungu yupo”
“Tutaonana kwa wakati mwingine tena” raisi alinyanyuka na kuondoka eneo hilo, jambo ambalo aliliona pale lilibaki kuwa siri yake mwenyewe kwenye moyo wake ila lilionekana kuwa jambo la kutisha kwa sababu baada ya pale hali yake haikuonekana kuwa sawa tena kama mwanzo. Utabiri ulikuwa unaeleza kwamba kama asingefanya haraka kumuua mtu huyo basi ni yeye ambaye alikuwa anaenda kufa.


Asubuhi wakati kunakucha, raisi Daria Julius alikutana na barua mezani kutoka kwa msaidizi wake, ilikuwa ni siku ya pili tangu aweze kuteuliwa kwenye hiyo nafasi yake. Barua hiyo ilimtisha na kumshtua kwa wakati mmoja kwa sababu ya uzito wa sehemu ambako ilikuwa imetoka. Ilidaiwa kutoka kwa papa moja kwa moja, kiongozi mkubwa zaidi wa dini duniani, haikuwa habari mbaya kupata barua kutoka kwa kiongozi huyo lakini ujumbe ambao ulikuwa ndani ya barua hiyo ndio ambao uliweza kumtisha na kumfanya aanze kuuona ule mwisho wake kuwa mbaya kweli kama ambavyo ilikuwa imetabiriwa na mtaalamu. Jasho lilianza kumtoka taratibu japo eneo hilo lilikuwa na kiyoyozi safi kabisa muda wote.

Barua ilidai kwamba raisi huyo alitakiwa kutoa majibu tena haraka iwezekanavyo kutokana na tukio ambalo lilitokea juzi yake, tukio la askofu kuuawa Mwanza lilikuwa ni taswira mbaya kwenye ulimwengu wa dini, tukio hilo lilikuwa linaenda kuleta mkanganyiko mkubwa na mpasuko hivyo kama kiongozi mkuu wa dini duniani hakuwa tayari kuweza kuona jambo hilo linatokea. Lile tukio lilitokea kwenye ardhi yake yeye na kama raisi alitakiwa kuwa na hizo taarifa mapema kuweza kulizuia hata kama hakuwa ameingia madarakani moja kwa moja. Kulikuwa na sababu kubwa za tukio lile kuweza kutokea siku moja kabla ya yeye kuapishwa hivyo papa alimtaka aje ma majibu ndani ya masaa ishirini na manne vinginevyo kanisa katoliki lilikuwa linaenda kuingilia moja kwa moja jambo hilo kama angefikisha hayo masaa ishirini na manne bado hajafanikisha jambo hilo basi kitu cha kwanza kukifanya alitakiwa kujiuzulu kwenye hiyo nafasi yake.

Mheshimiwa alihisi kama anaota ila ndio ambao ulikuwa ukweli wenyewe, jambo hilo lilitokea kwenye usimamizi wake hivyo alihesabika kama alikuwa anahusika yeye na kama alikuwa anajua haipo hivyo basi alitakiwa kuyatafuta majibu ya jambo hilo haraka iwezekanavyo na kama sio hivyo yeye ndiye ambaye alitakiwa kuubeba msalaba wa jambo hilo. Alihisi kuchanganyikiwa, badala ya mambo kupungua ndipo yalikuwa yanazidi kutokea hali iliyomfanya ajihisi alikuwa ana mikosi mingi ukizingatia mpaka wakati huo hata yule raisi ambaye alikuwa amekufa hawakuwa wamemzika bado. Kigogo huyo hakuona umuhimu wa kuendelee kukaa eneo hilo pendwa zaidi kwa mara nyingine bali aliamua kutoka hapo na kwenda kulipambania jina lake mwenyewe, kuwaamini watu wengine sehemu kama hiyo isingekuwa sawa.

Alihitaji msafara uandaliwe haraka iwezekanavyo kwani alikuwa na dharura, dharura ya kwenda mahali ambako alijiona kabisa kwamba angepata msaada ama kuweza kulimaliza jambo hilo mapema, aliielewa nguvu na ushawishi wa kanisa katoliki duniani, kanisa ambalo limejijenga kwenye kila upande kiasi kwamba kuna watu huwa wanaamini kwamba sio kanisa tu bali ni serikali ambayo imejitosheleza, sasa kwenda kinyume nao ni jambo la hatari. Alikuwa anaelekea nyumbani kwa jaji mkuu, mzee ambaye alikuwa ametoka kumuapisha masaa kadhaa ambayo yalikuwa yamepita nyuma. Hata jaji mkuu hakuwa na matarajio ya kuweza kuonana na raisi nyakati hizo kwani alienda kwake bila kutoa taarifa yoyote ya ujio wake, ilikuwa ni ishara kwa jaji mkuu kwamba ujio wa kiongozi huyo haukuwa na amani bali ulikuwa na jambo zito ndani yake kwani hakuwahi kwenda kwake bila taarifa hata siku moja.

“Mheshimiwa sio kawaida yako kuja kwangu mapema namna hii tena bila taarifa, bila shaka sio kwema huko utokako!” jaji mkuu aliongea akiwa anamkaribisha raisi wake ambaye yeye mwenyewe alikuwa ametoka kumwapisha.
“Ni kweli mzee mwenzangu, mambo hayako sawa kabisa huko nitokako na wewe ndiye mtu pekee ambaye unaweza kuyafanya yakawa sawa kabisa”
“Sijakuelewa mheshimiwa”

“Ni ngumu kunielewa ila hakuna namna, unatakiwa unisikilize kwa umakini kwa sababu jambo ambalo limenileta hapa ni kubwa na gumu mno”
“Nakusikiliza mheshimiwa”
“Unakumbuka tukio la askofu kuuawa Mwanza?”
“Ndiyo, jeshi la polisi lilisema litakuja na majibu sahihi ndani ya siku tatu”
“Ni kweli lakini kanisa katoliki wameamua kuingilia suala hili”
“Kuna uhusiano upi wa wewe kuja hapa na tukio la hayo mauaji?”
“Nadhani unaelewa ni kwanini nipo hapa”
Episode ya kumi inaishia hapa, tukutane ndani ya 11.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 11.
ENDELEA.......


“Unataka kuniambia kwamba ni wewe umemuua?”
“Ingekuwa tofauti nisingekuwa hapa”
“Kuna sababu zipi za msingi mpaka umuue askofu na unayajua kabisa madhara yake baada ya tukio kama hilo?”
“Ni siri nzito ambayo ipo nyuma ya haya yote na siwezi kukwambia kwa sababu kama ukiijua basi nitatakiwa kukuua muda huo huo”
“Umeanza uongozi wako kwa namna mbaya sana. Sasa kwanini upo hapa kwangu muda huu?”

“Nimetumiwa barua kwamba natakiwa kuijibu kwa masaa ishirini na manne kutoa majibu ya kilicho tokea na kama sitaweza kufanya hivyo basi mimi nitatakiwa kujiuzulu kwenye nafasi yangu ili wao wamuweke mtu wao ambaye wanamtaka”
“Bado sijaelewa mimi naingiaje hapo”
“Wewe unatakiwa kuibeba hii lawama yote”
“Whaaaaaaat?”

“Yeah, wewe ndiye unatakiwa kujulikana kwamba ulimuua askofu”
“Mheshimiwa umechanganyikiwa?”
“Ningekuwa kwenye hali kama hiyo mimi na wewe tusingekuwa tunafanya mazungumzo ya mhimu kama haya nyakati kama hizi ambazo nilikuwa natakiwa kuwepo kitandani kwa ajili ya kujipongeza kwa ushindi huu mkubwa ambao nimeupata lakini mpaka sasa sina amani nao kabisa”

“Mimi siwezi kufanya jambo la namna hiyo, hiyo dhambi sijaitenda mimi na kama nikiibeba nitakuwa binadamu mbaya zaidi kwenye masikio ya watu wengi miaka na miaka, historia itaniandika mimi kama kiongozi wa hovyo zaidi kuwahi kutokea wakati mhusika ni wewe hapo. Nipo tayari hata kujiuzulu kwenye hii nafasi yangu ukampa mtu mwingine lakini sio kukubali kufanya jambo ambalo ni wewe umefanya upuuzi”
“Unajua bwana Ziko wewe ni mtu unaye ielewa sheria, unalielewa taifa letu na misingi yake ambayo ipo miaka na miaka. Hili taifa linawahitaji watu ambao watakuwa na uwezo wa kujitoa sadaka, watu ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya kulipigania na kufanya hilo kwa ajili ya raisi wako ni moja ya sehemu ya kutimiza majukumu yako ya msingi. Raisi amekufa, hata hajazikwa wananchi wapokee taarifa kwamba mimi kama raisi nahusika na jambo la kumuua askofu tena ambaye alikuwa kipenzi kwa watu wengi, unahisi taifa litakuwa kwenye hali gani bwana Ziko?”

“Sijali kuhusu hilo, ulitakiwa kupima madhara ya upuuzi ambao uliufanya kabla ya kuweza kuufanya, najua hata hiyo nafasi umeipata kwa kumuua mtangulizi wako ila nilikupa heshima kwani kama jambo hilo lingeenda hadharani lingesababisha mpasuko mkubwa kwenye serikali. Hiyo ndiyo sehemu ambayo mimi nimetimiza wajibu wangu kwa asilimia zote miamoja ila hili la kuongeza kumuua askofu naweza kukuhakikishia kwamba sipo tayari kuhusika hata kidogo hivyo katafute namna nyingine ya kutoka na sijali hata kama utaondoka madarakani kwa mara nyingine”

“Nilijua hauwezi kukubali kwa sababu wewe ni mtu mbinafsi mno ndiyo maana nikaja na mpango mwingine mezani” raisi alikuwa mtulivu ila mwenye hasira, hakutaka kuona mpango wake unashindwa kwa sababu ya mtu huyo kumgomea. Kwa nafasi ambayo alikuwa nayo jaji mkuu, aliona kabisa kwamba alikuwa anafaa kubeba majukumu hayo na mambo hayo yeye yakamkalia mbali akawa salama.
“Unataka kusemaje labda?”

“Unajua wewe ni miongoni mwa watu wenye familia kubwa kwenye taifa hili bwana Ziko, una familia bora ambayo ina upendo na amani, una familia ambayo unaipenda mno. Una watoto ambao umewasomesha kwa kutumia kodi za raia wako kwenye shule za gharama na hakuna mtu amewahi kukufuatilia. Umetengeneza familia ambayo hata siku usipo kuwepo unataka ujivunie kwamba ulikuwa na familia bora ila sina imani kama itakuwa hivyo baada ya haya mazungumzo ya mimi na wewe kuisha”

“Wewe mshenzi umekuja hapa kuitishia familia yangu? Nitakuf….” Kabla hajajibu kwa jazba jaji mkuu alitulizwa, alitakiwa kusikiliza kwanza jambo la msingi ambalo mheshimiwa alikuwa anahitaji kumpasha ili aweze kujibu kwa kutumia akili yake yote na sio kuanza kukurupuka.
“Nisikilize kwa umakini. Naweza kukuhakikishia kwamba hakuna mtu anaiua familia yako hata usipokuwepo bali familia yako itaishi kwa mateso makali mno na wakati huo watakuwa na jina baya kila sehemu ambayo watakuwa wanaenda, hali ambayo itawafanya wawe maadui wa taifa zima. Mpaka mimi nakuja hapa kwako kuongea na wewe, tayari nilishafanya maamuzi kwamba wewe ni lazima ufe kwa kutaka au kutotaka ila kwenye wewe kufa kuna sehemu ya kufanya maamuzi ambayo ni sahihi ili hata wakati unakufa usiweze kujuta kwa kuiachia familia yako matatizo mazito ambayo yatakufanya ujione msaliti mkubwa kwao” mheshimiwa alitulia na kumwangalia jaji mkuu kwa umakini akiwa anampima kama alikuwa anayaelewa vizuri maelezo yake kisha akaendelea.

“Kuna wewe kufa kwa kutaka au kutotaka na hapa ndipo ambapo wewe unatakiwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa ajili ya familia yako. Kufa kwa kutaka maana yake ni kwamba utatakiwa kujiua mwenyewe na kuandika barua ambayo itakuonyesha kwamba wewe ndiye mhusika wa mauaji ya askofu hivyo Roma watajua mhusika ni wewe lakini wakati huo kesi itaisha kwa sababu utakuwa umekufa tayari na hawataweza kuihoji maiti. Kufa kwa kutotaka ina maana utalazimisha kwamba mimi nikuue na kisha baada ya hapo nitalitangaza jina lako mwenyewe kwa ubaya kila sehemu na hata familia yako itahusishwa moja kwa moja kwenye tukio hilo jambo ambalo litathibitika kwamba hata mali zako umezipata kwa njia ambazo sizo kwahiyo nitatoa amri mali zako zote ziwekwe kwenye mikono ya serikali na wewe pamoja na familia yako mtapewa kesi ya uhujumu uchumi hali ambayo itasababisha familia yafilisiwa kila kitu na kubaki na umaskini wa hali ya juu. Haya yote yana wezekana ila inategemea na maamuzi ambayo utayafanya Ziko” mheshimiwa alitoa maelezo ambayo yalikuwa mazito mno kwa jaji mkuu. Huenda alikuwa anawaelewa wanasiasa kwa kiwango kikubwa ila hakuwahi kufikiria kwamba yeye anaweza kufanyiwa jambo la namna hiyo kwa yale ambayo alikuwa ameyafanya kwenye taifa lake.

Raisi baada ya kutoa maelezo hayo ambayo kiuhalisia yalikuwa ni ya matisho tu alinyanyuka na kufunga kifungo cha koti na kuanza kutoa eneo hilo. Akiwa amepiga hatua tano tu jaji mkuu alimuita bwana huyo kwa jina lake,
“Kwanini unanifanyia haya?”
“Kwa sababu natakiwa kutoa sadaka ili niwe mahali ambapo nastahili kuwepo”
“Namaanisha kwanini umeamua kuwa mkatili kwangu namna hii?”
“Kwa sababu wewe ni mtu mkubwa, siwezi kumchukua kiongozi mdogo na kumpatia hii kesi hata wao watajua ni uongo ila kwa mtu kama wewe ikijulikana umehusika kila mtu atatambua kwamba ni sahihi kwa sababu ya nafasi yako. Kufika usiku wa leo uwe umefanya maamuzi kwa sababu siku ya kesho natakiwa kurudisha majibu kwa wahusika” hakumkopesha, alimpa ule ukweli ambao ulikuwa unauma, jaji mkuu alibaki amekaa akiwa mwingi wa mawazo kwani raisi wake mwenyewe alikuwa amemuuza tayari na hakuwa na jambo la kufanya mpaka wakati huo.


***********
Saa tano na dakika hamsini na tisa usiku zilisambaa habari ambazo hazikuwa njema kabisa, habari ambazo ziliushtua umma. Kifo cha jaji kuu wa Tanzania kilizua mjadala mpya na mrefu, ilikuwa ni ghafla mno na watu hawakutarajia kabisa kupokea habari kama hizo kwa nyakati kama hizo na taarifa hiyo ilikuwa ikihutubiwa na mheshimiwa raisi mwenyewe moja kwa moja. Bwana huyo uso wake haukuwa na furaha lakini pia haukuwa na simanzi, alikuwa kawaida kama ambavyo kiongozi anapaswa kuwa awapo mbele ya kamera ili kuonyesha matumaini mapya kwa watu wake ambao anawaongoza.

“Tanzania, ni jina zuri na la kuvutia la taifa letu, jina ambalo lilianza tangu ile siku ambayo waasisi wetu walitupatia uhuru na kuamua kuliweka taifa hili kuwa moja tukapata jamhuri. Tangu hapo taifa hili limekuwa likiongozwa kwa weledi, umoja, amani na mshikamano zikiwa ni kama nguzo zetu kubwa ya ushindi wa kuhakikisha tunaifikia nchi ya ahadi, sasa tunaifikiaje nchi ya hadi? Uzalendo.

Uzalendo ndilo jambo la pekee la kuweza kutufikisha huko ambako sisi tunaenda, uzalendo ndiyo silaha pekee kubwa ambayo sisi tunatakiwa kuwa nayo siku zote kwa sababu ndiyo ambayo pekee inaweza kutufikisha kule ambako tunaenda na tunahitaji kufika ila bila hivyo kila kitu kitakuwa ni kazi bure na hakuna jambo lolote la maana ambalo tutaweza kulifanikisha. Mashuleni tulianzisha mitaala mipya, uraia ukapewa kipaumbele sijui kama kosa ni la walimu au wanafunzi wenyewe, nina imani somo hili linafundishwa kwa ukubwa ila sielewi ni kwa sababu gani halileti matokeo ambayo tunakuwa tunayatarajia kama taifa kwa ajili ya kuyafikia malengo yetu ya miaka miamoja ijayo.
Episode ya 11 inafika tamati, 12 itaamua.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 12.
ENDELEA.......


Uzalendo unaanzia utotoni, watoto muda mwingi hawajifunzi kwa kusoma ama kufundishwa bali kwa kuona na ndiyo sababu kubwa ambayo tunasisitiza kwamba mtu wa kwanza kuwajibika kwenye hilo ni kiongozi. Kiongozi ni kioo, kila mtu anataka kujitazama kupitia yeye hivyo kama viongozi wote wakiwa wazalendo na kutimiza majukumu yao kama inavyo takiwa nina imani matatizo mengi ya watu kutolipenda taifa lao yatapungua, kila mtu akiona viongozi wanakuwa mfano bora kwao lazima naye atatamani kuwa mfano bora hivyo itakuwa rahisi kushirikiana pamoja kuweza kulijenga taifa lakini kinyume na hapo tutakuwa tunabomoa.

Mimi binafsi kama raisi mteule wa taifa hili naapa kwamba kama kuna kiongozi yeyote ataenda kinyume na yale matakwa ya katiba na sheria zetu basi sitamfumbia macho, ni lazima atawajibishwa kwa ushenzi na makosa ambayo anayafanya. Juzi wote tulipokea taarifa za kushtua, taarifa ambayo haikuwa njema kwa watanzania hususani kwa waumini baada ya askofu kuuawa katikati ya ibada. Mimi sikutaka kulizungumzia jambo hilo haraka kwa sababu nilitaka kwanza ushahidi ukamilike ndipo nije kuwajuza yale ambayo yalitokea lakini kabla sijaja hapa ndipo tumepata habari zingine mbaya ambazo binafsi zikuzitarajia kwamba majibu yake yangeelekea kwenye hizo habari.

Askofu aliuawa na jaji mkuu wa Tanzania, moja ya watu ambao mimi binafsi nilikuwa nawaamini na nilikuwa tayari kuendelea naye kwenye utawala wangu ila sikuwahi kufikiria kabla kama anaweza kuwa mtu wa namna hii ambaye kiuhalisia ni kwamba hafai kabisa kwenye jamii wala kwenye taifa la amani kama hili. Bwana huyu baada ya kupata taarifa kwamba ushahidi umepatikana na yeye ndiye mhusika sahihi wa tukio lile, kukwepa aibu ambayo ingetokea baada ya yeye kukamatwa akaamua kuyabeba maisha yake. Jambo la kusikitisha ni kwamba alikuwa ameificha mpaka familia yake, aliigiza kuwa baba bora, aliigiza kuwa mume bora nyumbani kwake, akatukosea watanzania wote heshima kwa kuigiza kuwa kiongozi bora lakini gizani alikuwa ni shetani kwa kuweza kutekeleza tukio la kipuuzi kama lile tena kwa kiongozi mkubwa wa dini namna ile.

Mimi nalaani tukio kama hili, kama angekuwa hai ningempa adhabu mbaya sana kwa mikono yangu mwenyewe lakini kwa sababu amekufa tayari basi adhabu yake ni kwamba hatazikwa kwa heshima kama ambavyo wanazikwa viongozi wengine bali atakuwa na maziko ya kawaida kama watu wengine wa kawaida pia. Nitumie nafasi hii kuweza kuwaomba radhi watu wa imani zote kwani kwenye jambo kama hili wote tunaungana na kuwa wamoja hata kama tunatofautiana kiimani, kimitazamo na kiitikadi! Hili janga sitarajii kuja kuliona tena kwenye taifa letu hata kwa bahati mbaya na niahidi kwamba watu wa Mwanza tutakuwa nanyi bega kwa bega kwenye msiba wa kumpoteza mpendwa wenu ambaye mimi mwenyewe nitafika kuhakikisha kwamba nahusika kumsindikiza kwenye safari yake ya mwisho.

Hili tukio litukumbushe sisi kama taifa kuwa na upendo, sisi kama wapenda haki kuweza kulipigania taifa letu, tuhakikishe kwamba kila sehemu ambayo tunaenda tuendelee kuwa alama ya amani na upendo, tukawe ishara bora ya maendeleo na taifa ambalo linajali misingi ya utu, umoja, na kujali kila uhai wa mtu bila kujali kasoro zake. kwa heshima hiyo ni kwamba bendera itakuwa nusu mlingoti kwa wiki nyingine moja kupisha mazishi ya raisi wetu mtangulizi wangu ambaye atazikwa siku tatu zijazo mbele lakini kwa heshima pia ya askofu naye atazikwa siku moja na mheshimiwa raisi wetu mpendwa. Mungu ibariki Tanzania”

Mheshimiwa alimaliza hotuba ambayo iliwaweka watu macho kodo usiku huo, taarifa iliyo tolewa na raisi ilikuwa ni ya ghafla mno kwao kwani hawakuitarajia kabisa na hata kama walitarajia taarifa basi haikuwa ya namna hiyo bali walihisi huenda ingekuwa kuhusu kifo cha mtangulizi wake na sio jaji mkuu kuhusika na mauaji kwa sababu ambazo hata hazikusemwa wazi ni zipi. Bwana huyo alikuwa bingwa wa propaganda ndiyo sababu kwake ilikuwa rahisi kuweza kutengeneza tukio la namna hiyo na kila mtu akamuamini kwamba ni kweli japo uhalisia ni kwamba hilo tukio lote alikuwa amelitengeneza yeye mwenyewe kwa sababu zake ambazo alikuwa anazijua yeye, aliamini kwamba ushindi siku zote huwa ni sadaka ndiyo maana hata yeye kufika pale juu alikuwa ametoa sadaka za kutosha. Jaji mkuu alikufa huku jina lake likiwa limechafuliwa kwa sababu wananchi walianza kuliaani jina hilo kwenye mitandao, walianza kumtukana na kudai kwamba hastahili kuzikwa mwili wake ungetupwa tu lakini wengine walidai familia yake ilitakiwa kulipa kwa kumuua mtumishi wa Mungu huku ukweli ikiwa ni kwamba hakuwa na kosa wala hatia yoyote ile.


Baada ya kutoka kwenye ile hotuba, raisi Darian Julius alitembea kurudi kwenye ofisi yake na kubeba sigara kubwa akaanza kuivuta taratibu huku akiwa anatoka tena kuelekea sehemu ambayo alikuwa anahitajika nyakati hizo. Ilikuwa ni kwenye chumba kimoja kikubwa cha mikutano ambacho kilipambwa na nakshi ya samani zilizokuwa zinavutia mno. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na wanaume watano ambao walikuwa wanamsubiri, wanaume hao walikuwa wamevaa suti zinazo fanana, wote walikuwa kimya mpaka pale mheshimiwa alipo ingia ndipo walinyanyuka na kutoa heshima zao kisha wakarudi kuketi kwa mara nyingine tena.

“Nimefurahi kuwaona hapa ndugu zangu, hii safari tuliianza pamoja na kwa sasa tunaendelea nayo pamoja japo kuna matatizo kadhaa yalitokea lakini kwa sasa kila jambo limekaa kwenye sehemu ambayo lilitakiwa kuwepo” aliongea akiwa ananyanyua chupa ya maji na kuigida yote.
“Kiongozi sijakuelewa bado, hili tukio uliamua kulifanya wewe mwenyewe bila hata kutushrikisha? Ina maana kwamba siku hizi hautuamini tena?” alitamka bwana aliye tambulika kwa jina la Peter Shitobe akionekana kabisa kwamba hakufurahia jambo hilo.

“Kama ningekuwa siwaamini basi niamini mimi mpaka muda huu hata hapa msingekuwepo”
“Sasa imekuaje umefanya jambo hili bila hata kuhitaji ushauri wetu au maoni yetu?”
“Ndiyo maana halisi ya kuwa kiongozi, sio kila wakati unatakiwa kumwambia kila mtu kuhusu kila kitu. Hili jambo lilikuwa juu ya uwezo wenu hata kama ningewaambia msingesaidia lolote kwa sababu kwanza lilikuwa la ghafla na jambo ambalo unatakiwa kulielewa kabla ya kuanza kunipigia kelele hapa ni kwamba nilipokea barua kutoka kwa papa mwenyewe akiwa anahitaji majibu haraka ya Askofu kuuawa au vinginevyo nilitakiwa kujiuzulu kwenye hii nafasi na baada ya hapo angetuma watu wake kuja kuchunguza, vipi bado unahitaji nikuambie kwamba nilitakiwa nije kusikiliza ushauri wako ndipo nifanye maamuzi?” raisi alijibu kwa ukali hali ambayo iliwafanya wale watu watazamane wenyewe bila kuwa na majibu ya moja kwa moja.

“Ni jambo zuri kwa sababu limeisha, najua umetuita hapa kwa sababu kuna jambo ambalo unataka kutuambia, kama isingekuwa hivyo basi ungetupatia taarifa tu kwa simu. Nina imani haujaja hapa kutujibu kuhusu wewe kumuua jaji mkuu kiongozi, ni sababu ipi imefanya tuwepo hapa muda huu?” Steven Hando, tajiri ambaye alikuwa na ukwasi wa kutosha ndiye ambaye aliuliza swali kijasiri kwenda kwa mheshimiwa.

“Ni kweli upo sahihi, huwa sina muda wa kupoteza kabisa kuweza kuwaita hapa bila sababu ya msingi. Uhalisia ni kwamba kwenye mpango wa kwanza ambao tuliufanikisha, kuna majina kadhaa ambayo yalikuwa ni hatari kwetu na moja ya majina hayo ni kwamba wawili wamekufa, jina moja halijulikani ila mmoja ambaye ndiye wa mhimu zaidi ameweza kutoroka na hivi ninavyo ongea na nyie hapa ni kwamba yupo hai. Kama mtu huyu yupo hai, maana yake ni kwamba ni suala la muda tu kabla hatujalipuka” habari ambayo aliitoa kwa nyakati hizo ilionekana kabisa kwamba haikuwa njema, ni habari ambayo iliwapa shaka na hofu wote ambao walikuwa humo ndani kwa sababu walionekana kutokuwa na taarifa hiyo.

“Unamaanisha nini mheshimiwa?” aliuliza bwana mmoja ambaye muda wote alikuwa ametulia akisikiliza. Mzee Magamba ndilo lilikuwa jina lake. Alikuwa akimiliki migodi kadhaa ya dhahabu.
“Bazoka bado yupo hai”
“Samahani, umenaanisha Oliver Jefferson yupo hai?” Eusebius Hanji, aliuliza kwa hisia swali hilo kiasi kwamba mpaka alisimama pale ambapo alikuwa ameketi huku akiwa haamini kama jambo hilo lilikuwa la kweli.
“Ndiyo”

“Kivipi mheshimiwa?” Douglas Shila aliuliza akiwa anawageukia wenzake wote kwa mashaka na maswali ambayo alitakiwa kujibiwa hapo.
“Kwa sasa sina maelezo mengi ya kuweza kuwapatia ama kuwaridhisha ila mnatakiwa kutambua kwamba ukweli ndio huo. kuna watu ambao nimewapa kazi kwa sasa wanamtafuta mahali popote pale ambapo atakuwepo, anatakiwa kuuawa. Ana taarifa za hatari ambazo kama zikipatikana litakuwa jambo la kifo kwetu kwani ndiye alikuwa mlinzi wa raisi ambaye amekufa hivyo zile habari hazitakiwi kwenda mahali popote zaidi ya kuishia nazo kwenye kaburi”
“Kiongozi mimi bado sijakuelewa vizuri, huyu mtu mara ya kwanza ulisema utamumudu kwa ukubwa na hakutakuwa na madhara, tena mkamtumia na mwanamke ambaye yeye alikuwa anampenda mno kumuwekea sumu ili kummaliza nguvu ikitokea kwamba kutakuwa na tatizo kwenye upande huo wa kupambana naye, unataka kuniambia mipango hiyo imeishia kwa wewe kutupatia sisi majibu kwamba mtu huyu ametoroka?”

Episode 12 sina la nyongeza, tukutane wakati ujao.

FEBIANI BABUYA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom