Simulizi: Jeneza la ajabu

barikiwa

Senior Member
Dec 4, 2018
145
263
"JENEZA LA AJABU
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
***SEHEMU YA 01****
Ikulu kwa mfalme ;
"Siwezi kufa kirahisi namna hii, dunia tamu bwanaaa
weeeh, mali zangu hizi nitamuachia nani??
",yalikuwa ni maneno ya kejeli kutoka kwa mfalme
wa nchi ya Mwamutapa, baada ya kupokea taarifa
kutoka kwa mganga wake wa kienyeji kuwa
kashindwa kumtibu maradhi yaliyokuwa
yakimsumbua, hivyo asubili kufa tu. Hali
iliyopelekea mganga yule kujuta kauli yake kwani,
mfalme aliamuru auawe kwa kukatwa kichwa chake,
na kisha kiwiliwili chake kitupwe ndani ya bwawa la
mamba waliofugwa na mfalme kwa ajili ya kula
watu waliomchukiza na kumpinga katika uongozi
wake. "Yani mimi nife, siwezi kufa mimi, labda
utangulie mpuuzi wewe ",mfalme Mutapa, alijitamba
kwa mala nyingine tena, huku akishuhudia kichwa
cha mganga wake kikitenganishwa na kiwiliwili,kuto
kana na kushindwa kumtibu mfalme na kumwambia
asubili kifo tu, jambo ambalo mfalme alilichukulia
kama katukanwa na kudharauliwa.
*****
LIPIA SH 2500 UTUMIWE STORI HII YOTE MWANZO
MPAKA MWISHO,AU JIUNGE NA GRUPU LA
WHATSAP KUSOMA STORI TATU KWA SH 3000
MWEZI MZIMA.
*****
Mitaani katika nchi ya Mwamutapa;
Hali ngumu ya maisha inazikumba familia nyingi
katika ardhi ya Mwamutapa, huku lawama nyingi
zikitupwa kwa mfalme, kwani wanaume wengi
wenye nguvu na vichwa vya familia, walitumikishwa
kwa nguvu katika mashamba ya mfalme na kisha
kulipwa ujira mdogo,jambo ambalo lilimchukiza kila
raia wa Mwamutapa. Kelele zao za mateso
hasikusaidia chochote, kwani kila mtu aliyejifanya
kupinga kunyanyaswa, alijikuta akiuawa kikatili, hali
iliyowaogopesha wengine na kujikuta wakikubaliana
na manyanyaso kutoka kwa mfalme, kwani
waliogopa kifo.
"Naamini ipo siku yatakwisha, usilie mama yangu
",ilikua ni sauti kutoka kwa kijana mkakamavu
Njoshi, akimunyamanzisha mama yake, baada ya
kupokea taarifa za kifo cha mume wake kwani
alishindwa kumtibu mfalme. "Mwanangu baba yako
kaondoka, tumebaki wawili tu, nakuomba uachane
na Grace, mfalme atakuua na wewe, tegemeo na
faraja langu lililobakia ",mama Njoshi alizidi kulia
kwa uchungu, huku akimusisitiza mwanae kuachana
na Grace,msichana mrembo sana na mtoto pekee
wa kike wa mfalme. Jambo ambalo kwake aliliona
ni gumu sana na halitowezekana, kwani alimpenda
sana Grace licha ya kupokea vitisho mala kadhaa
kutoka kwa mfalme ili aachane na Grace. Na kila
mala mfalme alipojaribu kumuua Njoshi alishindwa,
kwani alifanikiwa kutegua mitego yote aliyotegewa
ili aweze kufa, kwani alikua ni hodari sana na
aliweza kulishinda jeshi la mfalme mala nyingi,
moja ya sababu ambazo Grace zilimfanya ampende
sana Njoshi, kwani alihitaji mwanaume atakaye
muoa awe ni shujaa na si mwanaume suruali tu,
asiyeweza kumlinda na hatari yoyote.
"Usjali mama, mimi nipo siku zote, nitakulinda,
lakini naamini ipo siku Mwamutapa itakua huru, na
mimi nitakuwa kiongozi wake ",kijana Njoshi
aliongea kwa ujasiri na kujiamini kwani ziku zote
alifanya mazoezi ya kila aina, ili tu siku moja afanye
mapinduzi na kuokoa wananchi dhaifu kutoka
kwenye utumwa na uongozi wa mabavu wa mfalme
Mutapa, jambo ambalo mama yake aliliona kama
ndoto ya mchana, ambayo Njoshi alikuwa akiota.
"Mwanangu banaa unanifurahisha, hebu toa upuuzi
wako huko ",mama Njoshi aliongea huku
akitabasamu kwa mbali kutokana na maneno
aliyoambiwa na mwanae, na kumfanya asahau
machungu ya kumpoteza mume, japokuwa alikuwa
ameshazoea na kuona kama vifo ni jambo la
kawaida katika familia yake, huku akikumbuka jinsi
wanae watatu walivyopoteza maisha kutokana na
njaa kali iliyotokea miaka kadhaa iliyopita, na
kumuachia Njoshi pekee. "Nakuombea mwanangu,
ndoto zako ziwe kweli ",mama alizungumza huku
akimkumbatia mwanae, bila kutambua kuwa Njoshi
alijawa na hasira, huzuni na machungu kwa
kumpoteza baba yake na kuapa kulipiza kisasi,
kwani hakutaka mama yake agundue huzuni hiyo na
kuzidi kumpa machungu mama yake aliyempenda
sana.
Ikulu kwa Mfalme :
Mganga maarufu wa kienyeji aliyesifika katika nchi
ya Mwamuyeshi, nchi iliyopakana na
Mwamutapa, na kuongozwa na mfalme Muyeshi
,anafika ikulu kumtibu mfalme maradhi yake, baada
ya Muyeshi kupata taarifa za rafiki yake mpendwa
kuugua kwa muda mrefu, hali iliyopelekea
kumtafuta muganga katika ardhi yake ili amsaidie
rafiki yake asiweze kupoteza maisha. "Karibu sana
katika ardhi ya Mwamutapa,,, naamini rafiki yangu
ndiyo kakutuma hapa ",mfalme Mutapa aliongea bila
shida yoyote huku akitabasamu,huku akiwa amelala
katika kitanda chake kwa takribani mwezi mmoja
sasa bila kuamka kutoka kitandani, japo aliweza
kuzungumza vizuri kama vile hakuwa mgonjwa.
"Ndiye mimi mtukufu mfalme, mganga kutoka
katika ardhi ya rafiki yako Muyeshi, nimekuja
kukusaidia ",mganga yule aliongea huku akijiamini,
na kumfanya mfalme atabasamu kwani hakupenda
kufa, na alitamani aishi milele jambo ambalo
mganga yule alikua ameshalitambua.
"Usjali mtukufu mfalme, mpaka sasa
nimeshachelewa siwezi kukutibu, muda wowote
kuanzia sasa utaweza kufa, lakini inatakiwa ukifa
uzikwe ndani ya jeneza lililotengenezwa kutoka
katika miti iliyo katikati ya msitu hatari wa Majini,
msitu ambao uko katika ardhi yako ya Mwamutapa,
ukizikwa ndani ya jeneza hilo, utaweza kufufuka
baada ya wiki moja na kuishi milele ",mganga yule
alizungumza maelezo marefu sana, huku jina la
kijana Njoshi likijirudia rudia ndani ya kichwa cha
mfalme, kwani ndiye kijana pekee aliyemuona
anafaa kufanikisha swala hilo, na kutoka akiwa
salama katika msitu hatari wa Majini, msitu ambao
hakuna aliyewahi kuingia humo akitaka mali, watoto
au ufalme kutoka kwa mizimu ya msitu huo na
kutoka salama bila kupoteza maisha. "Na pia
inatakiwa iwe siri, raia wako wasifahamu labda tu
atakayekwenda huko msituni ",mganga alizidi
kuzungumza huku mfalme mawazo yakiwa mbali
sana, kwani mwanae Grace alishamuonya kuwa
Njoshi siku akipata matatizo yaliyosababishwa na
yeye, ataweza kujiua, jambo ambalo mfalme hakuwa
tayali kumkosa mwanae wa kike pekee aliyenaye,
kati ya watoto arobaini kutoka kwa wake watano
alionao ,mtoto ambaye alizaliwa na mke wa tano
baada ya wake zake wanne waliotangulia kushindwa
kumzalia mtoto wa kike.
"Sawa …sawa sa…wa ni…me…kusikia ",mfalme
alijibu bila kujitambua huku mawazo na maswali
lukuki yakikisumbua kichwa chake .
……ITAENDELEA ……
SOMA KISA HIKI MWANZO MPAKA MWISHO KWA
SH 2500 TU,MALIPO YAFANYIKE MPESA
0763338857,JINA HAKIKA BUCHA.JIUNGE NA
GRUPU LANGU LA WHATSAP KWA SH 3000 ADA
YA NWEZI USOME JENEZA LA AJABU,KAHABA
YUAN LIANG NA JINI MWEUPE.
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
***SEHEMU YA 02****
Ikulu kwa mfalme;
Ngome ya mfalme inakumbwa na majonzi mazito
,kutokana na hali ya mfalme kuwa mbaya sana.
Wapo waliofurahi kumuona katika hali ile, hasa
wananchi wake ambao hawakupendezwa na uongozi
wake huku wakitamani afe haraka, waweze kuwa
huru kutoka katika taabu na mateso
yaliyosababishwa na uongozi wake wa kikatili wa
mfalme Mutapa. Lakini wachache walihuzunika
sana, hasa watoto wake pamoja na wake zake
mfalme, huku wakimuomba Mungu amuepushe na
umauti.
"Mfalme mimi ninaondoka kurudi nyumbani, lakini
zingatia yale yote niliyokuambia, kwani kama
unavyoiona hali yako inazidi kuwa mbaya,
usipokuwa makini mali zako na ufalme wako
utakwenda na maji ",asubuhi na mapema, mganga
kutoka katika ardhi ya Mwamuyeshi, akiwa
ameshika kila kitu kwa ajili ya safari yake ya kurudi
nyumbani, anamuaga mfalme huku akimsisitiza
kuzingatia maelekezo aliyompatia na kisha kupanda
farasi na kuondoka, huku akiongozana na askari
wawili aliokuja nao kwa ajili ya kumlinda njiani,
askari waliotoka katika ngome ya mfalme Muyeshi.
Mfalme Mutapa akitikisa kichwa chake kuashiria
kukubaliana na maelekezo ya mganga, na
kumshuhudia akitokomea mbele ya uso wake,
anaamua kutoa amli kwa kutumia maandishi Njoshi
kufika ikulu haraka sana, kwani mfalme alishindwa
hata kuzungumza hali iliyowatia hofu watoto wa
mfalme pamoja na wakeze.
"Baba nakuomba usimdhuru Njoshi kwa chochote
kile, lolote baya likimtokea sitajali hali yako mbaya
uliyonayo, nitakuua ",Grace aliongea huku akionesha
kumaanisha kwa maneno aliyoyazungumza, bila
kujali ni kiasi gani alimpenda baba yake aliapa
kumtoa roho kwa mikono yake, kama tu kipenzi
chake Njoshi akidhurika na jambo lolote na kuacha
familia nzima ya mfalme ikiwa midomo wazi, kwani
hawakuamini maneno yale kama yalitoka kinywani
kwa Grace, msichana aliyependwa sana na mfalme.
"Hahaa, sasa mpaka wewe unamuua baba, sisi
tutakua wapi, labda uanze kutuua sisi ",Kijana
mkubwa wa mfalme, kijana ambaye Mutapa
alimuamini sana na kumuahidi kumrithisha ufalme
na mali zake, kutokana na uhodari wake
alizungumza kwa kejeli, na kupelekea familia nzima
kucheka na kusahau hali mbaya ya mfalme
aliyokuwa nayo.
Ghafla mfalme alitoa amli ya familia nzima kukaa
kimya kwa kutumia ishara, huku akitaka agizo la
Njoshi kufika ikulu, litekelezwe mala moja bila kujali
onyo kali alilopokea kutoka kwa binti yake Grace,
mtoto pekee wa kike aliyempenda sana.
Nyumbani kwa kina Njoshi;
Ilikua siku ya jumatatu asubuhi, kama kawaida
Njoshi hufanya mazoezi makali katika siku hii kwani
wiki nzuri huonekana siku hii, hivyo aliamini akifanya
vizuri mazoezi siku ya jumatatu, atakuwa fiti wiki
nzima. Aliamka saa kumi na moja asubuhi, na
kuanza mazoezi ya kukimbia, siku zote alipenda
kukimbia huku akiimba, kwani alikatiza mitaa karibu
yote ya nchi ndogo ya Mwamutapa, bila kujitambua
kwani nyimbo alizoimba zilimtia moyo na
kumuondolea uchovu. "Ngoja nikimbie, nikimaliza
nije kunyenyua vyuma, ukombozi sio lelemama
lazima wachache tuumie ",Njoshi aliongea kwa
ujasiri huku akitamani siku moja aweze kuishika
nchi na yeye kuwa mfalme, huku Grace akiwa
malikia, kwani msichana mrembo Grace alipendwa
sana na wananchi na aliwaokoa mala nyingi
walipokuwa wakionewa na baba yake pamoja na
kaka zake, kwani aliwaombea msamaha na
kusikilizwa. Walimuona kama ndio kondoo pekee
aliyeishi ndani ya kundi la simba. Njoshi alizidi
kukimbia lakini bila kutegemea alijikuta akiishiwa
na pumzi haraka sana tofauti na siku zingine, bila
kupoteza muda aliamua kurudi nyumbani kufanya
mazoezi mengine. "Mwanangu kweli wewe ni
shujaa, natamani ndoto zako zitimie nikiwa hai
nishuhudie ukiwakomboa Wanamutapa wote ",ilikua
tayali imeshafika saa moja asubuhi, mama yake
Njoshi aliweza kuamka na kumkuta mwanae
akiendelea na mazoezi, na kuzungumza maneno
makali yaliyomshitua sana Njoshi, haikuwa kawaida
kwa mama yake kumwambia maneno mazito kiasi
kile.
Njoshi alisitisha mazoezi na kisha kutaka kumuulza
mama yake, kwanini alizungumza vile, kwanini
mama yake asishuhudie ukombozi ambao mwanae
alikuwa akiupanga, mama yake kaona nini mbeleni
katabili nini. Njoshi alizidi kujiuliza maswali
kichwani mwake, huku akimsogelea mama yake,
mke wa marehemu Nyangoma, mganga na mtabili
aliyekuwa akitegemewa sana na mfalme Mutapa.
Kutokana na kutabili kuwa ipo siku mfalme atamuua
kikatili bila kujali mema yote aliyomfanyia, aliamua
kumfundisha uganga na utabili mke wake, ili siku
akifa mke wake aweze kurithi mikoba.
"Mwanangu Njoshi Nyangoma, naona hatari kubwa
iko mbele yako, utasafiri safari ndefu yenye visa na
mikasa ya ajabu ,mkanda huu mweusi na panga hili
ndio siraha yako kuu, iliyomuwezesha baba yako
kutoka salama katika msitu wa majini, usikatae
kwenda huko, huko ndipo utaupata ufalme wa nchi
hii, lakini ukirudi nyumbani utakuta kabuli langu,
mimi nikiwa tayali nimeshakuwa mifupa ",mama
Njoshi alizungumza kwa uchungu sana huku
machozi yakimtoka, na kumkabidhi mwanae begi
dogo jeusi,kwani ndio ulikuwa mwisho wa kuonana
yeye na mwanae mpendwa Njoshi.
"Sikuelewi mama unaongea nini, mimi msituni huko
niende kufanya nini sasa, kwanza huwezi kufa mimi
nitakulinda mpaka dakika ya mwisho ",Njoshi
aliongea huku akimfuta mama yake machozi, huku
mama yake akiukumbuka ule msemo wa wahenga,
msemo ambao ulikua maarufu sana enzi zile afrika
ikitawaliwa na wazungu, msemo uliosema jambo
usilo lijua ni kama usiku wa giza.
Njoshi akiwa amemkumbatia mama yake, akizidi
kumbembeleza aweze kunyamanza, alishangaa
kuona kundi kubwa la vijana shupavu, likiwa
limevalia bukta fupi nyeusi, pamoja na ngozi ya
chui, huku mikononi wakiwa wameshika mikuki na
kila aina ya siraha za kivita, bila shaka aliweza
kuwatambua, lilikuwa ni jeshi la mfalme Mutapa.
"Aiweeeeeeh ………Njoshi, aiweeeeh ………",askari
wale waliweza kumsalimu Njoshi, na kumfanya
mama yake kuacha kumkumbatia mwanae na
kushuhudia watu wale waliomsalimia mwanae.
"Aiweeeeeh ………askari waaminifu wa mfalme wangu
wa ardhi ya Mwamutapa, niwasaidie nini? ",Njoshi
aliitikia salamu kwa upole na hekima, huku akiificha
hasira yake na kisasi kizito kilicho rohoni mwake,
kutokana na baba yake kuuawa kikatili na mfalme.
Kwa upande wa mama yake hakushangaa chochote,
kwani alikwishaona kila kitu kitakachotokea mbele,
na pia siri ya mfalme ambayo wananchi
hawakutakiwa kuifahamu, kuhusu kuzikwa mala
atakapokufa na kisha kufufuka bila wananchi
kutambua chochote, ili aweze kuishi na kutawala
milele.
"Tumekuletea ujumbe huu wa maandishi kutoka kwa
mfalme, mkwe wako tafadhali pokea ……iweeeeh
"askari wale waliongea huku, mmoja aliyeonekana
kuwa na cheo kikubwa kuwazidi wenzake kutokana
na kuvaa ngozi ya simba, ngozi iliyokuwa ikivaliwa
na kila kiongozi wa nchi ya Mwamutapa,
akimkabidhi Njoshi karatasi yenye maandishi na
kisha kuisoma.
"Iweeeeeh …mkwe wangu, nakuomba katika ikulu
yangu, ninashida na wewe, nataka tuwekeane
mkataba ili uweze kumuoa binti yangu Grace
",Njoshi alisoma maneno yale na kisha kutabasamu,
tabasamu ambalo liliwafanya askari wale wa
mfalme kuangaliana na kisha kukonyezana, hali
iliyoonesha kutambua siri fulani iliyokuwa
imefichika.
"Mama peleka begi hili ndani, mimi ngoja nikaonane
na mfalme ",Njoshi aliongea huku akionekana
kufurahia sana, kwani hakuamini kama ipo siku
mfalme atamtamkia kuwa yeye ni mkwe wake,kwani
siku zote aliambulia matusi na kutishiwa kifo,
alipoingia anga za mfalme Mutapa.
"Hapana mwanangu, kama unanipenda, naomba hilo
begi lisitoke mgongoni mwako ",mama yake Njoshi
aliongea huku akiwa na huzuni moyoni, huku
akijaribu kutabasamu kuficha huzuni yake, kwani
huo ndio ulikuwa ni mwisho wa kuonana na
mwanae katika ulimwengu huu.
****ITAENDELEA ***
PATA PUNGUZO LA BEI KUTOKA SH 3000 MPAKA
SH 1000,,LIPIA SH 1000 MPESA NAMBA
0763338857,NA KISHA NITAKUTUMIA SIMULIZI
YOTE FB INBOX AU WHATSUP ...WAKIFIKA WATU
KUMI SIMULIZI INARUDI BEI YAKE YA KAWAIDA.
Like page yangu ya fb Simulizi za Hakika Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
***SEHEMU YA 03****
Msitu wa Majini;
Ilikua mida ya jioni siku ya jumatatu , tetemeko la
kutisha linatokea katika msitu wa majini,Malikia wa
msituni, kiongozi aliyemiliki msitu na kuongoza
viumbe vyote vilivyopatikana ndani ya msitu
anaamua kuitisha kikao, kwani tetemeko lile
liliashiria jambo fulani, kama ilivyozoeleka katika
msitu huo, tetemeko likitokea basi muda wowote
msitu ulikua hatarini kuvamiwa.
"Ndugu zangu majini, mapepo na mizimu ya
mababu zetu, msitu wetu uko hatarini kuvamiwa ,na
niwajibu wetu kuulinda msitu huu, pia inatakiwa
tulipize kisasi kwani mtu anayekuja kuvamia msitu
huu, baba yake aliwahi kuja hapa msituni na kuua
ndugu zetu na kisha kutokomea na baadhi ya mali
zetu ili awe mganga na mtabili hodari, japo
ameshapoteza maisha ",malikia alizungumza kwa
hasira, katika kikao cha ghafla alichokiitisha muda
mfupi baada ya tetemeko kutokea, huku umati wa
viumbe hatari sana wa msitu wa majini, msitu
uliokua na utajiri mwingi, zikiwemo dhahabu na
almasi, wakiwa makini kumsikiliza malikia wao na
kujiandaa na mapambano.
"Aiweeee mtukufu malikia wa msitu huu,tuko tayali
kutekeleza maagizo yako, na kuua chochote
kitakachokanyaga ardhi hii ",ilikua ni sauti ya majini
waliohudhuria kikao, huku wakijawa na uchu wa
kulipiza kisasi hasa wakikumbuka jinsi mzee
Nyangoma, baba yake Njoshi jinsi alivyofanikiwa
kuiba mkanda pamoja na panga lenye nguvu za
ajabu, na kutoroka navyo huku akiua baadhi ya
majini, kitendo kilichowakasilisha viumbe wote wa
msituni.
Ikulu kwa mfalme;
Kijana Njoshi anafika ikulu kwa mfalme na
kushangazwa na jambo aliloliona mbele ya macho
yake, hali ya mfalme ilikua mbaya sana kiasi
kwamba hakuweza hata kuinuka kitandani wala
kufungua kinywa chake na kutamka neno lolote lile,
kwa upande mwingine alitamani mfalme apoteze
maisha kwani aliona ndio utakuwa mwanzo wa ardhi
ya Mwamutapa kuwa huru kutoka katika uongozi
wake wa kidikteta ,na pia yatakua ndio malipo ya
dhambi zote za mauaji aliyoyafanya, huku baba yake
akiwa miongoni mwa watu waliouawa kikatili na
mfalme.
Njoshi akiwa bado amepigwa na butwaa, alianza
kupata picha kuwa inawezekana aliweza
kudanganywa kuwa aliitwa na mfalme ili aozeshwe
Grace,kwani kwa wakati ule, machozi ya huzuni
hayakukatika machoni kwa Grace,na kumfanya
aamini mawazo yake, kuwa palikuwa na tatizo
nyumbani kwa mfalme.
"Aiweeeeeh mtukufu mfalme, mtumwa wako Njoshi
Nyangoma nimeitika wito wako, aiweeeeh ……
mfalme Mutapa udumu milele",Njoshi aliongea huku
akiwa amesimama mbele ya kitanda cha mfalme,
huku familia nzima ikiwa imekaa kimya,
wakimuomba Mungu Njoshi akubaliane na ombi la
mfalme, kwani waliamini mfalme hata akipoteza
maisha ataweza kufufuka ndani ya wiki moja, jambo
ambalo lingewezekana kama angezikwa ndani ya
jeneza la ajabu, jeneza ambalo Njoshi inatakiwa
akalitengeneze kwa kutumia miti inayopatikana
katikati ya msitu wa majini na kisha kuja nalo ikulu
kwa mfalme.
"Kijana wangu Njoshi, utafanikiwa kumuoa binti
yangu Grace, na kumiliki nusu ya ufalme wangu,
kama tu ukikubali kwenda katika msitu wa majini,
na kutengeneza jeneza kisha kuja nalo hapa
",yalikuwa ni maneno yaliyoandikwa kwa maandishi
na mfalme, maneno ambayo Njoshi aliyasoma na
kisha hofu ya kifo kumuandama, kwani hakuna mtu
aliyewahi kupona kutoka katika msitu wa majini,
isipokuwa baba yake pekee.Njoshi alikumbuka
maneno ya mama yake alimwambia kuhusu hatari
hii, na kisha kumsihi asikatae kwenda kwani huko
msituni ndiyo sehemu pekee ya kuupata ufalme, pia
Njoshi alikumbuka siraha alizopewa na mama yake
na kuziweka ndani ya begi kisha kumsihi asiweze
kulitupa begi hilo.
"Ndiyo mfalme wangu mtukufu, nimekubali, aiweeeh
mfalme udumu milele, "Njoshi alikubali ombi la
mfalme, na kufanya nyuso za familia nzima ya
mfalme kutabasamu kwa furaha, isipokuwa Grace,
kwani hakutaka mpenzi wake kwenda msituni ndio
maana alikuwa akilia toka mwanzoni, na wala
hakulizwa na hali mbaya ya baba yake aliyonayo,
bali jambo ambalo Njoshi aliweza kuitiwa ikulu,
lilikuwa la hatari sana na aliamini atampoteza
mpenzi wake kama atakubali ombi la baba yake.
*****ITAENDELEA ***
PATA STORI YOTE KWA BEI YAKE YA KAWAIDA SH
2500,Lipia 2500 kwenda namba 0763338857
mpesa!!!!
Share stori hii ili marafiki zako wasipitwe na
simulizi katika page yangu Simulizi za Hakika
Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
***SEHEMU YA 04***
Nyumbani kwa kina Njoshi;
Jua likiwa tayali linazama, huku sauti za ndege
zikipungua na kuufanya mji wa Mwamutapa kuwa
kimya.Ukimya huo unatokea pia katika nyumba ya
kina Njoshi, ukimya unatawala tofauti na siku zote,
kwani familia ilibakiwa na mtu mmoja tu,ambaye ni
mama yake Njoshi huku mwanae akiwa hajarudi
kutoka kwa mfalme. Akiwa ameketi barazani, nje ya
kibanda chao cha udongo, kilichoezekwa kwa nyasi,
aliendelea kupunga upepo huku akiwa na huzuni
sana,
"Siamini,hatimaye leo hii nimebaki peke yangu, sina
cha kufanya ndio tayali imeshatokea ……,eeeh
mizimu ya babu zangu mlindeni mwanangu " ,mama
Njoshi aliongea peke yake kwa huzuni huku
akinyanyuka sehemu aliyokuwa ameketi, na kisha
kuelekea ndani kulala, hakuwa na njinsi kwani aliona
kuketi pale nje kulizidi kumuongezea machungu.
Ikulu kwa mfalme;
Giza likiwa tayali limeshaingia huku, ukimya ukiwa
umetawala katika ngome ya mfalme. Kijana Njoshi
anamfuta machozi Grace, huku akiwa
amemkumbatia,
"Usjali Grace, naamini nitarudi salama ndani ya siku
tatu ",Njoshi alimtoa hofu binti mfalme, msichana
aliyempenda sana, na aliamini atamuoa atakaporudi
kutoka katika msitu hatari wa majini, msitu ambao
aliambiwa na mama yake hana budi kwenda huko,
kwani huko ndiko angeupata ufalme na ukombozi
wa Mwamutapa.
"Sawa Njoshi, nakuamini wewe ni shujaa,
nakuombea kwa mizimu yetu, urudi ukiwa mzima
",Grace aliongea kwa huzuni huku akitoka mikononi
mwa Njoshi aliyekuwa amemkumbatia, na
kumruhusu kuianza safari yake haraka sana, kwani
alitakiwa kuondoka usiku huo. Na bila kupoteza
muda, kijana shupavu na hodari, kijana pekee
aliyeogopwa na askari pamoja na mfalme Mutapa
kutokana na uhodari wake wa kupambana, anatoka
katika ngome ya mfalme iliyojengwa kwa ukuta
mrefu, huku wafanyakazi pamoja na familia nzima
ya mfalme wakimtazama na kumtakia kila laheri
katika safari hiyo, bila kutambua kuwa Njoshi
alikuwa na malengo yaliyompeleka msituni huku
swala la kuchukua jeneza la ajabu, likiwa la ziada
tu.
Mwamutapa
Kijana ambaye alikuwa ni rafiki yake Njoshi, urafiki
ambao ulitokana na kijana huyo kuokolewa katika
kipigo kizito kutoka kwa askari wa mfalme, mala tu
alipofanya kazi asubuhi mpaka jioni katika shamba
la mfalme, na pale alipojaribu kudai haki yake,
askari wale walimnyima pesa, jambo ambalo kijana
yule alishindwa kulivumilia, alijikuta akilusha ngumi,
na kuambulia kipigo kikali kwani asingeweza
kuwashinda askari zaidi ya kumi, huku yeye akiwa
mmoja tu, lakini bila kutegemea ghafla alishangaa,
askari wale wakipigwa mateke ya haraka haraka na
kutimua mbio.
"mimi naitwa Njoshi, na pole sana ndugu yangu,
hawa ndio askari wetu, inatakiwa tuungane kuitafuta
haki ",kijana yule aliikumbuka sauti ya mtu
aliyemsaidia kutoka mikononi mwa askari wa
mfalme, ikijitambulisha na kisha kumuomba
waungane katika harakati za ukombozi wa
Mwamutapa. Na huo ndio ukawa mwanzo wa urafiki
wao, urafiki ambao umedumu kwa muda mrefu na
wamekuwa kama ndugu sasa.
"Inabidi kesho niende kwao nikamuone rafiki yangu,
tangu jana sijaonana naye ",rafiki yake Njoshi,
aliyejulikana kwa jina la Ngesha, alizungumza peke
yake huku akijifunika shuka lake na kisha kuuchapa
usingizi, bila kutambua kuwa muda huo ambao yeye
analala, rafiki yake yuko safarini bila kujali giza wala
hatari yoyote usiku huo, akielekea katika msitu wa
majini, msitu ambao ulipatikana umbali wa kilomita
arobaini kutoka katika makazi ya watu wa
Mwamutapa.
Msitu wa majini;
tangu asubuhi tetemeko lilipotokea, na malikia
kutangaza hali ya hatari katika msitu, mitego ya kila
aina iliweza kutegwa katika kila njia ya kuingilia
msituni, huku jeshi la msituni likiwa tayali limeshika
dhana mbalimbali za kivita ikiwemo mishale, na
kuuzunguka msitu wote.
"Aiweeeh jini mweupe, kiongozi wa askari wangu wa
msituni, adui wetu yuko njiani anakuja, nakuomba
jiandae kwa mapambano, uko huru kutumia nguvu
za kichawi na kijini ulizonazo ",malikia alimpatia
taarifa mkuu wa jeshi lake la ulinzi msituni, na
haraka bila kupoteza muda alitoweka mbele ya uso
wa malikia, kwenda kutekeleza amli aliyopewa ya
kudumisha ulinzi kila kona ya msitu, na kujiandaa
kwa ajili ya kulipiza kisasi.
**ITAENDELEA IJUMAA****
JIPATIE SIMULIZI YOTE KWA SH 2500 tu, lipia 2500
kwenda mpesa namba 0763338857
Share, comment na like page yangu ya fb Simulizi
za Hakika Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
****SEHEMU YA 5****
Giza likiwa linazidi kuwa la kutisha,ikiwa imefika
mida kama ya saa nne usiku, kijana Njoshi akiwa
amevalia bukta yake nyeusi, huku chini akiwa miguu
peku, kwani watu wa Mwanamutapa kutokuvaa viatu
ilikuwa kama tamaduni yao, kijana Njoshi aliendelea
kutembea huku akinyosha balabala kubwa ya vumbi,
balabala iliyokuwa ikiunganisha nchi ya Mwamutapa
na nchi zingine za jirani, ikiwemo nchi ya
Mwamuyeshi. Sauti za miguu yake ndizo zilizosikika
balabala nzima, kwani watu hawakupita balabala
hiyo mida ya usiku, kutokana na kuogopa kutekwa
na kunyanganywa mali zao, na pengine hata
kuuawa.
Ilikuwa tofauti kwa Njoshi, hakuogopa jambo lolote
lile, akiwa kifua mbele kwani hakuvaa shati lolote
lile huku akiwa amebeba begi jeusi alilopewa na
mama yake, aliendelea kusonga mbele huku
akitembea kwa mwendo wa haraka, na muda
mwingine alikimbia, ili aweze kufika katika ardhi ya
msitu wa majini kabla hapajakucha siku ya jumanne.
"Mpaka sasa nimeshakimbia umbali mrefu sana,
sina budi kuongeza bidii ",Njoshi aliongea peke
yake moyoni mwake, huku akiwa tayali
ameshayaacha majumba ya Mwanamutapa mbali
sana. Kila alipokumbuka mateso yote ya
Wanamutapa, nguvu za ajabu ziliongezeka mwilini
mwake na kumfanya azidi kuongeza mwendo ili
apate kuikomboa nchi yake haraka sana, huku
mbalamwezi ikiangaza vema njia aliyotakiwa kupita.
"Hahaha eti jeneza, siamini kama kuna watu
hawataki kufa, yani uishi milele, na kututesa milele,
hili ni jambo ambalo haliwezekani ",Njoshi aliongea
maneno ya kejeli kwa mfalme, huku akitabasamu na
kumuona mfalme kama mtu wa ajabu sana, mtu
aliyemkabidhi fisi bucha na kula nyama zote za
buchani.
"Hapa mimi ninachofuata ni fimbo ya ufalme, fimbo
ambayo inapatikana katika ngome ya malikia wa
msituni, malikia wa majini, jeneza nitalishughulikia
nikishapata fimbo yangu ya kuiongoza
Mwanamutapa ",Njoshi alizidi kuongea peke yake,
huku akisisitiza jambo lililompeleka msituni, kwani
ili uwe mfalme nilazima umiliki fimbo ya kifalme
kutoka katika msitu huo, na mfalme Mutapa aliipata
fimbo hiyo ya uongozi kutokana na kurithi kwa
wazazi wake,huku chanzo cha fimbo hiyo
kikisemekana ni katika msitu wa majin. Fimbo hiyo
ilimpatia mamlaka mfalme kutodhurika na majini wa
msituni, kwani msitu wa majini ulipatikana katika
nchi ya Mwamutapa. Wengi walifunga safari kwenda
msituni kuchukua fimbo nyingine ya ufalme,
inayofanana na fimbo ya mfalme lakini walishindwa
kurudi wakiwa hai.
Pia wasingeweza kupambana na mfalme kwani
fimbo aliyonayo ilimpatia kiburi sana, hata
ukilishinda jeshi lake na kumuua, usingeweza
kuongoza nchi, kwani fimbo iliandikwa jina la
mfalme Mutapa,. Hivyo njia ambayo ni rahisi,
ilikuwa ni kuitafuta fimbo ya ufalme msituni ,na
kuiandika jina lako binafsi ili majini wakutambue na
wasikusumbue katika uongozi wako,hapo ndipo
ufanye mapinduzi na kumuua mfalme ili uongoze
nchi ya Mwanamutapa.
"Ngoja nipumzike kidogo hapa chini ya mti ,ninywe
maji, nichukue siraha zangu kwani muda wowote
nitaufikia msitu ",Njoshi aliongea huku akiketi katika
majani mafupi chini ya mti wa ubuyu, na kisha
kufungua begi alilopewa na mama yake. Huzuni ya
kutokumuona tena mama yake ilimuandama, kwani
aliyakumbuka maneno ya mama yake kuwa
hatomuona tena na kufanya machozi kumtoka ,
mithili ya mtu aliyefiwa na mtu anayemtegemea.
Alifungua begi na kutoa kitambaa cheusi, kitambaa
ambacho alitakiwa akifunge kiunoni kama mkanda,
huku akishikilia panga kali, panga ambalo linauwezo
wa kuua majini. Ikiwa tayali imeshafika mida ya saa
saba usiku, Njoshi ananyanyuka sehemu aliyokuwa
amepumzika kwa takribani dakika tano, na kisha
kusonga mbele kuusogelea msitu wa majini.
Msitu wa majini
Malikia wa majini anaingiliwa na hofu kubwa sana
kwani mtu aliyekuwa anakuja kuuvamia msitu
alionekana kuwa hatari sana, kwani kila alipojaribu
kumtambua sura yake alishindwa, na ghafla
mawasiliano yalipotea, hakuweza kumuona tena
katika kiganja chake, kiganja kilichokuwa
kikimuonesha mtu aliyekuwa njiani akielekea
msituni. "Huyu anayekuja huku natambua kuwa ni
mtoto wa mtu aliyewahi kuja huku na kutuibia mali
zetu, lakini sura yake ningependa niifahamu lakini
nimeshindwa, na kwanini kapotea ghafla, nashindwa
kumuona tena katika viganja vyangu ",Malikia wa
msituni alizungumza kwa hasira na mshangao
mkubwa, bila kutambua kuwa Njoshi aliweza kuvaa
kitambaa cheusi kiunoni, na kumfanya kutoonekana
kama akiwa anafuatiliwa na majini.
"Hapa nikizubaa, watu wangu watakufa ",malikia wa
majini, msichana aliyekuwa mrembo sana, na
mwenye umri sawa na Grace, alizungumza huku
akitafuta kichupa kidogo cha maji, na kisha
kumpatia askari wake mmoja, kunyunyizia maji hayo
kuzunguka ngome yake yote ili kujilinda. Maji hayo
yalikuwa na uwezo wa kumgandisha mahali pale,
mtu yeyote mwenye asili ya ubinadamu,
atakapokanyaga eneo lile.
"Hapa tayali nimemaliza kazi, hata kama
akifanikiwa kuwapita askari wangu msituni, mimi
lazima nitamkamata ",malikia aliongea kwa
kujigamba, na kuachia tabasamu zuri lililoonesha
vema uzuri wake.
Nje ya msitu;
Kwa mbali kijana shupavu na hodari Njoshi
Nyangoma, anakamatilia panga lake kisawasawa,
kwani alianza kuuona msitu hatari wa majini, ukiwa
kama hatua mia moja mbele yake, baada ya
kutembea na kukimbia kwa usiku mzima, na ilikua
imeshafika mida ya saa kumi usiku, kuamkia siku
ya jumanne.
"Aiweeeh mizimu wa mababu zangu, mizimu wa
ardhi ya Mwamutapa, asanteni kwa kunifikisha
salama, naomba mnilinde tena na kunirudisha
nyumbani salama ",Njoshi aliongea kwa hofu na
woga, kwani alikuwa na kazi nzito, tena ya hatari
ikiwa mbele yake.
"Hapa ni mwendo wa kuua tu kiumbe chochote,
kitakachokatiza mbe…le…y…a…ngu ",Njoshi
alishindwa kumalizia sentesi yake baada ya
kukanyaga mtego wa kamba, na kisha mtego huo
kumning'iniza juu ya mti huku miguu ikiwa juu na
kichwa kikiwa chini, mala tu alipokanyaga mguu
wake msituni.
Njoshi bila kupoteza muda, aliikata kamba ile
mguuni kwake, kwa kutumia panga lake na kisha
kudondoka chini kama mzigo huku akiwa haamini
kilichokuwa kimetokea ghafla namna ile, na
kumuongezea hofu na woga huku akitakiwa kuwa
makini sana ndani ya msitu.
****ITAENDELEA ****
Ofa! Wenzio walishasoma yote kwa sh 1000 tu
mpaka tar 25 ndio mwisho wa ofa,lipia 1000mpesa
namba 0763338857
Au karibu whatsup group usome stori kibao kwa sh
1500 tu @0629905923
Comment yako na kulike page yangu, ni jambo la
muhimu sana kwangu,
Page yangu ya fb Simulizi za Hakika Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
****SEHEMU YA 06***
Msitu wa majini;
Viumbe hatari wa msituni ghafla wanasikia kishindo
katika moja ya mitego waliyokuwa wametega, hali
hii inawafanya wagundue kuwa tayali adui yao
alikuwa ameshaingia msituni, kwani hawakuweza
kumuona katika ramani zao, na hata walipotumia
uwezo wao wa kijini, walishindwa kumuona adui
yao, mala baada ya Njoshi kujifunga kiunoni
kitambaa cheusi alichopewa na mama yake.
"Jamani tayali adui alishaingia msituni, fanyeni kila
njia mumkamate akiwa hai au amekufa ",jini
mweupe, kiongozi wa askari wa msituni, alitoa amli
ya kuanza kumtafuta adui, baada ya kufika katika
eneo ambalo kishindo kikubwa kilisikika, na sehemu
ambayo walitega mtego wao, na kukuta kamba ya
mtego ikiwa inaning'inia baada ya kukatwa huku
adui akiwa ameshatoweka.
"Nazani mnaisikia harufu ya binadamu, hayuko
mbali, mtafuteni haraka sana " ,jini mweupe alizidi
kuongea na kuliamlisha jeshi lake la msituni,
kumtafuta adui baada ya kuhisi harufu yake katika
eneo lile la mtego, eneo ambalo lilizungukwa na
vichaka pamoja na miti mirefu.
********************
Baada ya Njoshi kuponea chupuchupu kutoka katika
mtego, haraka sana anaingia ndani ya kichaka
chenye majani marefu, kwani alitambua kuwa majini
wa msituni lazima wafike katika eneo lile muda sio
mrefu baada ya kusikia kishindo kile kikubwa, hivyo
asingeweza kukimbia na kufika umbali mrefu bila
kukamatwa.
Lakini ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni,
Njoshi alishangaa sana baada ya kuliona kundi
kubwa la majini, likifika eneo lile haraka sana huku
akiwa hata hajajificha vizuri kwenye majani. Kwani
viumbe wale walikuwa na uwezo wa kupotea na
kufika eneo lolote walilolitaka wao, ndani ya
sekunde tu, kwani hawakuwa binadamu bali majini,
tena majini hatari wa msituni, msitu ambao ulikuwa
maarufu katika nchi ya Mwamutapa, pamoja na
ulimwengu mzima, kutokana na utajiri wake.
"Mungu wangu, mbona hawanioni ",Njoshi
alistaajabu sana kwani kiongozi wa askari wale, jini
mweupe alisimama karibu sana na kichaka kile, na
ilikuwa imebakia kidogo amkanyage Njoshi kwani
alikuwa hata hajajificha vizuri katika kichaka, eneo
ambalo mtego ulikuwepo.
Njoshi ujasiri ukiwa umetoweka, alianza kutetemeka
kwa woga kwani majini wale walitisha sana kwa
kuwatazama, wengine walikuwa na mguu mmoja
huku wakiwa na vichwa vingi sana, pamoja na
mikono zaidi ya miwili. Njoshi akiwa anatetemeka
aliamua kufumba kinywa chake asiweze kupiga
kelele, kwani jini mweupe, aliyekuwa na kichwa cha
nyoka aina ya koboko, huku akiwa na mwili mweupe
tena wa binadamu, alitoa amli ya kumsaka Njoshi
katika kichaka kile, kwani waliweza kuhisi harufu
yake.
"Asante mizimu ya mababu, sionekani, leo nilikuwa
nimekwisha ",Njoshi akiwa amejifumba mdomo
wake kwa kutumia viganja vya mikono, aliishukuru
mizimu, kwani majini waliokuwa wanatisha sana
walipita karibu yake bila kumwona, jambo ambalo
lilimshangaza sana kwani sehemu kubwa ya mwili
wake ilikuwa wazi na hakufunikwa vizuri na majani,
bila kutambua kuwa mkanda ule wa kitambaa
cheusi aliouvaa kiunoni, ndiyo uliyosababisha majini
wasiweze kumuona.
"Msitu huu niliuskia tu, leo nimejionea mwenyewe
",Njoshi aliongea moyoni huku akiwa anamshangaa
askari mmoja wa msituni,mwili wake ukiwa
umebakia mifupa tu,huku akiwa ameshika mshale,
na kusonga mbele, lakini Njoshi alishindwa kutumia
hata panga lake kuwaangamiza majini wale kwani
hakutambua matumizi yake, huku yeye akiwa
anashangaa muonekano wa majini wale na kuzidi
kumuongezea woga.
Mwamutapa
Asubuhi mida kama ya saa moja, kijana Ngesha
aliamka kutoka usingizini, na kunawa uso ili aelekee
nyumbani kwa rafiki yake, ili asikute
wameshaondoka kwenda shambani.
"Mwanangu mbona haraka sana asubuhi hii,
unaenda wapi " ,ilikuwa ni sauti ya mama yake
Ngesha, mama ambaye alibaki mjane baada ya
mume wake kuitwa na mfalme,na alipokwenda huko
hakuweza kurudi.Kwani alipofika ikulu kwa
mfalme,alikuta kundi kubwa la wanaume wakiwa
huko wanasaga unga wa mahindi kwa kutwanga
kwenye vinu,lakini baada ya kumaliza kazi hiyo na
kudai malipo yao ,kundi lote lilitupwa kwenye
bwawa la mamba bila huruma ,amli iliyotoka kwa
mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme.
Lakini mama Ngesha kila alipojaribu kuulizia kwa
mfalme kuhusu mumewe ,hakuweza kupatiwa jibu
sahii zaidi ya vitisho.Kitendo kilichomfanya mama
Ngesha pamoja na mwanae kuweka msiba
nyumbani kwani tayali waliamini mzee wao
aliyejulikana kwa jina la Mugina,alikuwa
ameuawa,jambo ambalo lilikuwa kweli.
"Naenda kumsalimia rafiki yangu Njoshi,mara moja,"
Ngesha alimjibu mama yake na kisha kutokomea
huku akikimbia ili kumuwahi Njoshi,kwani ilikuwa
ndio mida ya Njoshi na mama yake kwenda
shambani.
Ikulu kwa mfalme;
Asubuhi na mapema siku ya jumanne,siku ambayo
usiku uliopita kijana Njoshi alitoweka ikulu kuelekea
katika msitu wa majini,kwenda kuchukua jeneza la
ajabu kwa ajili ya kumzikia mfalme atakapokufa ,na
kisha kufufuka ndani ya wiki moja.
Vilio vinatawala katika ngome yote ya mfalme,huku
familia nzima ya mfalme pamoja na wafanyakazi
wote wakilia kwa kwikwi,ama kweli mkuki kwa
ngurue kwa binadamu mchungu,leo hii maneno haya
yalijidhirisha waziwazi.Walizoea kuona wengine
wakilia,lakini leo ilikuwa ni zamu ya familia ya
mfalme kulia.
"Baba rudi,baba rudi baba yangu nakupenda",msic
hana Grace alilia kwa huzuni,huku akitamka maneno
ambayo yaliongeza uchungu katika familia nzima ya
mfalme.Walitamani sana Njoshi afanikiwe kurudi na
jeneza salama,ili mfalme afufuke ndani ya wiki moja
na kuishi milele,lakini hawakuamini kama kweli
Njoshi atafanikiwa kurudi salama,kwani huko
msituni alikoenda ni hatari sana.
Nyumbani kwa kina Njoshi;
Mama yake Njoshi,akiwa ameshika jembe kama
kawaida yake tayali kuelekea shambani,huku
kichwani akiwa na mawazo mengi juu ya hatma ya
mwanae.
Akiwa anatoka nje ya uzio wake wa nyumba,uzio
ambao ulitengenezwa kwa nyasi,Kwa mbali
alishangaa kumuona kijana akija uelekeo wa
nyumba yake huku akikimbia.Kitendo hicho
kilimfanya aweze kuweka jembe lake chini,pamoja
na kikapu kilichokuwa na maji ya kunywa pamoja na
chakula kwa matumizi ya shambani siku nzima.
"Aiweee…mama ,Njoshi ni memkuta…aiweeh"
,Ngesha alimsalimia mama yake Njoshi na
kumuulza kuhusu rafiki yake,huku mama akipumua
baada ya kumtambua kijana aliyekuja nyumbani
kwake,na pia hakuweza kuleta taarifa mbaya.
"Aiweeeh mwanangu,rafiki yako aliitwa na mfalme
tangu jana asubuhi,mpaka sasa sina taarifa
yoyote,aiweeeh",mama Njoshi alimjibu rafiki yake
mwanae,na kumtia hofu sana,kitendo ambacho
kilimfanya Ngesha kutoweka bila hata kuaga
kuelekea ikulu,kwani alitambua kuwa rafiki yake
lazima atakua hatarini kama kweli alienda ikulu
tangu siku iliyopita na hajarudi mpaka wakati ule.
****ITAENDELEA***
Kifo cha mfalme,haitakiwi wananchi wa Mwamutapa
wafahamu,zaidi ya familia ya mfalme na mtu
aliyelifuata jeneza msituni,lakini Ngesha kaelekea
ikulu kwenda kujua nini kinaendelea kwa rafiki yake
Njoshi.…tukutane sehemu ya 07 katika page yangu
ya fbSimulizi za Hakika Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
***SEHEMU YA 07****
Mwamutapa;
Mama yake Njoshi akiwa mwenye huzuni, huku
mawazo mengi kuhusu mwanae, yakishindwa
kumtoka kichwani mwake. Anachukua jembe lake,
pamoja na kikapu na kisha kuanza safari kuelekea
shambani, lakini pia kitendo cha Ngesha kuondoka
bila kumuaga na kushindwa kutambua mahali
alipoelekea ghafla . Kilizidi kumwongezea maswali,
kwani alihisi kuna jambo ambalo Ngesha alitaka
amweleze Njoshi, jambo la muhimu sana, na ndio
maana alishtuka baada ya mama yake Njoshi
kumweleza kuhusu mahali ambapo Njoshi
alielekea,kitendo kilichomshitua rafiki yake,na kisha
kuondoka haraka sana bila hata kuaga.
"Labda kaelekea kwa mfalme kuangalia usalama wa
rafiki yake,lahasha!,si angeniambia tu kuwa
anaelekea huko,"mama yake Njoshi alizungumza
peke yake,huku akiwa njiani kuelekea
shambani,akiwaza na kuwazua kitendo cha rafiki
yake mwanae ,kuondoka ghafla bila hata kumuaga.
Msitu wa majini;
Njoshi akiwa na hofu,huku akitetemeka mithili ya
mtu aliyenyeshewa na mvua ya masika,mnvua
inayoandamana na baridi kali.Alinyanyuka kutoka
mahali alipokuwa amejificha,huku akiwa
haamini,kama kweli kundi lile la askari hatari wa
msituni walimpita bila hata kumwona ,na kisha
kutokomea upande mwingine wa msitu,kwenda
kumtafuta.
"Hapa ngoja nipite upande mwingine nielekee
kwenye ngome ya malikia,lazma leo nifanikishe
misheni yangu na kisha kesho nirudi
nyumbani",Njoshi aliongea peke yake kama
kichaa,na kisha kushika panga lake,ambalo tayali
alikuwa amelitelekeza chini bila kujitambua,kuto
kana na hofu aliyokuwa nayo kipindi akiwashuhudia
askari wale wa msituni,wakipita mbele yake.
"Eeeeh mizimu wa mababu,niokoeni na balaa hili
kijana wenu",Njoshi aliomba mizimu huku akifumba
macho yake kwa dakika chache,na kisha kutamka
maneno ya kitamaduni bila kutoa sauti,na baada ya
sala hiyo,Njoshi alitokomea kuingia ndani kabisa ya
msitu,kwa kupitia upande mwingine tofauti kabisa
na upande ambao jeshi lililokuwa likiongozwa na jini
mweupe,waliweza kuelekea huko.
"Miii……zi…mu niokoeniii……na ku…faaa!!", zilikua ni
kelele za Njoshi ghafla,kwani sehemu aliyokuwa
akipita,ni kama vile aliruka mkojo na kukanyaga
mavi,kulikua na shimo ndefu sana kuelekea chini,
likiwa limetegwa huku juu kukiwa kumefunikwa na
fito nyembamba kama kuni,ambazo zingevunjika
pale tu mtu atakapozikanyaga .Pia fito hizo
zilifunikwa na majani makavu pamoja na
udongo,kiasi kwamba mtu asingeweza kugundua
kitu chochote,bali sehemu hiyo ilionekana kuwa
kama njia nyingine,kwani kulikuwa hamna tofauti
yoyote ile.
Mtego huo kweli ulifanikiwa kumnasa Njoshi,ujanja
wote aliokuwa nao,pamoja na uhodari,uliweza
kumwishia,na kumfanya kuwa mpole,tangu
alipoikanyaga ardhi ya msitu wa majini.Alijilaumu
sana kupita njia ile ,njia ambayo ilionekana
kupaliliwa vizuri bila kutambua kuwa katika njia hiyo
kulikuwa na mtego wa shimo uliotegwa na kisha
kufunikwa na udongo.
"Pwaaaaah…………",ilikua ni sauti ya maji mengi
ikimpokea Njoshi,baada ya kusafiri umbali wa kama
mita mia mbili kwenda chini,sawa na urefu wa
viwanja viwili vya mpira wa miguu.
"Duuuh kweli leo nimepatikana,lakini mimi
nishujaa,kwa vyovyote vile lazima niishinde vita
hii",Njoshi aliongea maneno ya kishujaa na kujipa
moyo,huku akiziba pua yake kutokana na harufu kali
ya maji yale yaliyoonekana kuwa machafu sana,maji
yaliyomfika Njoshi kifuani mwake
"Mungu wangu!,nini tena hiki……yalaa……aaa",.Njoshi
alipigwa na butwaa,huku sauti kubwa ya hofu
ikimtoka kinywani mwake,kwani alipojaribu
kupapasa maji yale kwa kutumia mkono
wake,alijikuta ameshika kichwa cha binadamu
kilichokuwa kimeliwa na kuoza vibaya,kitendo
kilichomfanya akitupe haraka sana na kisha kupiga
kelele kutokana na hofu kubwa aliyokuwa nayo.
Ikulu kwa mfalme;
Ikiwa yapata mida kama ya saa nne asubuhi,Ngesha
anafanikiwa kutoboa tundu,baada ya tofali moja
kupasuka na kuachia nafasi katika ukuta
uliozunguka ngome ya mfalme,nafasi hiyo iliweza
kuonesha kila kitu kilichoendelea ndani ,kama mtu
akiweza kuchungulia.
Kijana Ngesha baada ya kuangalia huku na kule,na
kugundua kuwa hakuna mtu yeyote aliyekuwa
akimtazama,tofauti na siku zote kwani walinzi wa
mfalme walizunguka muda wote,kuhakikisha hakuna
mtu yeyote aliweza kuusogelea ukuta huo.
"Duuuh leo,pako shwaliii,kulikoniii??,yaani hamna
hata wale mbwa wanaojiita askariii ",Ngesha
aliongea maneno ya kejeli huku yakiwa na
mshangao ndani yake,na bila kupoteza muda
aliweza kuchungulia ndani ya ngome ya
mfalme,ngome ambayo ilijitenga mbali kidogo na
makazi ya watu,huku msitu mdogo ukiizunguka
ngome hiyo,na haikuruhusiwa mtu yeyote kuuvuka
msitu,na kisha kuisogelea ngome hiyo bila sababu
maalumu,ukikamatwa adhabu ilikuwa ni kifo tu na
sio kitu kingine.
Kutokana na sheria hiyo,watu wengi waliogopa sana
kuisogelea ngome ya mfalme,na ndio maana
Ngesha alifanikiwa kutazama ndani bila kuonwa na
mtu yeyote,baada ya kujidhihirisha kuwa askari
hawakuepo eneo lile.
"Aiweeeh……mizimu wa mababu,mbona watu
wanalia!!,mbona Njoshi simuoni,mmmh mfalme
kafa???",maswali mengi yalimuandama
Ngesha,mala tu baada ya kuchungulia ndani ya
ngome ya mfalme,alishangaa kuona familia yote ya
mfalme ikilia sana,wake kwa waume,wakubwa kwa
wadogo.Lakini pia alipojaribu kuangaza vizuri kila
kona,hakuweza kumuona Njoshi,hali iliyomfanya
azidi kupigwa na butwaa. Lakini bila kutegemea,
kuna jambo kubwa sana lilimshitua kuliko yote,
alishangaa kumuona binti mfalme, na si mwingine,
alikuwa ni msichana Grace, msichana ambaye rafiki
yake Njoshi alimpenda sana, akilia kwa kwikwi huku
akimtazama mfalme aliyeonekana kulala bila
kumjibu chochote kile. Grace alitamka maneno ya
kumtaka baba yake asife, na kumwacha akiwa hana
baba, kitendo kilichomfanya Ngesha kushtuka,
kwani hakuona sababu ya kumfanya mfalme afe
haraka sana kiasi hicho.
"Mmmmh au ndio maana mfalme haonekani mtaani,
na imepita mwezi sasa, manyanyaso yamepungua,
lakini kwanini baba yake Njoshi kauawa?, sababu
ilikuwa nini nini?, inawezekana kweli mfalme kafa,
ngoja nielekee shambani kwa mama yake Njoshi
nikampatie taarifa hii, ninaweza kutambua kitu fulani
",Ngesha aliahirisha kuchungulia ndani kwa mfalme,
na kisha kufunga safari kuelekea shambani kwa kina
Njoshi, huku maswali lukuki yakimsumbua bila
kuwa na majibu yoyote ya maswali hayo.
Shambani kwa kina Njoshi;
Mama yake Njoshi akiwa amejipumzisha chini ya
mti wa maembe, mti pekee uliopatikana shambani
kwake, aliendelea kula chakula chake taratibu, huku
akishushia na maji kwani tayali ilikua imeshafika
saa sita, mida ambayo tayali jua lilikuwa
limechanganya vilivyo na kuwa kali sanaa.
"Eeeeh mizimu ya mababu, muokoeni mwanangu
",ilikua ni sauti ya mama yake Njoshi akimuombea
mwanae kwa mizimu, iweze kumpatia msaada,
kwani kutokana na uwezo wa kitabiri pamoja na
uganga ambao mumewe alimrithisha, aliweza
kutambua kuwa mwanae yuko hatarini, tena hatari
kubwaa, baada ya ndege aliyekuwa juu ya mti ule
wa maembe, kumnyea na kisha kinyesi chake
kudondoka katika matiti ya mama yake Njoshi.
Mama yake alikitafakali kitendo kile, na kugundua
kuwa ilikuwa ni kama ujumbe kwake, kuwa mtu
aliyenyonya maziwa kutoka katika matiti yake, yuko
kwenye shida na matatizo, huku kinyesi cha ndege
yule kikisimama kwa niaba ya matatizo
yanayomsibu mwanae. Utabiri ambao ulikuwa
sahihi, kwani wakati huo Njoshi alikuwa ndani ya
shimo kubwa msituni, huku akisubili kukamatwa na
majini hatari wa msituni.
****ITAENDELEA ***
"Aiweeeeeeeh mashabiki zangu, nawatakia sikukuu
njema, na ninawapenda sanaa aiweeeeh "
LIPIA SH 1000 TU USOME STORI TATU NDANI YA
GROUP LANGU LA WHATSAP, HUTAJUTA KULIPIA
BANDO HILI LA MWEZI AMBALO NI OFA YA
SIKUKUU KUTOKA SH 1500.
AU LIPIA SH 1000 UPATE STORI YOYOTE KATI
YAJENEZA LA AJABU AU MUUAJI MWEUSI! MALIPO
MPESA 0763338857 AU TIGOPESA 0658386459
"Aiweeeeh!!!!! Like page yangu Simulizi za Hakika
Jonathan
 
Simulizi; "JENEZA LA AJABU "
Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
Whatsup; 0629905923
****SEHEMU YA 10***
Mwamutapa;
kila familia katika nchi ya Mwamutapa, wanaingiwa
na hofu kubwa, baada ya kusikia sauti za kutisha
kutoka msituni,asubuhi siku ya jumanne. Sauti hizo
waliziipuuzia mwanzoni. Lakini, sauti hizo zilisikika
tena kwa mala nyingine jioni ya siku hiyo hiyo, na
tena sauti hizo zilikua nzito na za kutisha kupita zile
zilizosikika kwa mala ya kwanza. Kelele hizo
zilisababisha familia nyingi kujifungia majumbani
mwao, huku giza likiwa hata bado halijaingia
japokuwa jua lilikuwa tayali limezama kutokana na
uoga waliokuwa nao, kwani walifahamu sauti hizo
zilitokea katika msitu wa majini bila kutambua
chanzo chake, wala maana yoyote kuhusu sauti
hizo.
Familia ya kina Ngesha ilikuwa moja ya familia
zilizokuwa na hofu sana, kwani mama yake Ngesha
alifunga milango yote na kisha kuketi sebuleni,
katika nyumba yao ya udongo, na kisha kumsubili
mwanae ambaye alikuwa hajarudi tangu alipoondoka
asubuhi, na kumuaga mama yake kuwa ameenda
kumtembelea rafiki yake Njoshi.
Lakini mama yake Ngesha alipojaribu kumsubili
mwanae ili waweze kuelekea shambani pamoja,
alishangaa mwanae alipochelewa sana. Kitendo
kilichomlazimu mama yake kwenda shambani peke
yake, kwani aliamini Ngesha atamkuta
shambani,mala tu atakaporudi kutoka kwa rafiki
yake.
Ama kweli, nani kama mama ?,kwani mama yake
Ngesha alifanya shughuli za shambani mpaka
mchana, lakini bila kutegemea, hakuweza kumwona
mwanae akimfuata shambani. Hali hii ilimfanya
mama yake Ngesha kuwa na hofu sana, na
ukizingatia alikuwa tayali ameshazisikia sauti za
kutisha asubuhi, mida kama ya saa nne. Hivyo basi,
mama yake Ngesha alitambua kuwa siku hiyo ilikua
tofauti sana na siku zingine, na haikuwa kawaida
mwanae kuchelewa kiasi kile na kushindwa kumfata
mama yake shambani, jambo ambalo
lisingewezekana kwani Ngesha alipenda sana
kumsaidia mama yake kazi za shambani.
Hivyo basi, baada ya mama yake Ngesha kuwaza
na kuwazua, aliamua kusitisha shughuli zake za
shambani mapema sana, mida kama ya saa sita
hivi na kisha kurudi nyumbani, aweze kujua usalama
wa mwanae, chezea Mwamutapa wewe!, muda
wowote kifo kinaweza kukutokea bila mungu
kupenda.
Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza,
mama yake Ngesha alifika nyumbani kwake, lakini
hakuweza kumkuta mwanae. Haraka sana wazo
likamjia na kisha kufunga safari kuelekea nyumbani
kwa kina Njoshi. Huko pia alipofika getini tu,komeo
la mlango liliweza kumkalibisha,komeo
lililomaanisha hakukuepo na mtu yoyote nyumbani
pale.
Asikwambie mtu,mama yake Ngesha alichoka!,alipi
gwa na butwaa huku maswali mengi yakimsumbua
kichwani,kwani hakujua mwanae yuko wapi.Alihisi
labda atakuwa hatarini,tena katika hatari kubwa
sana.Hatari ya kutekwa na askari wa mfalme,na
kwenda kutumikishwa kazi nzito,kazi ambazo watu
wengi walikamatwa na kwenda kuzifanya bila
kupumzika ,na bila malipo yoyote.Na pale ambapo
mtu yeyote alipojaribu kufumbua kinywa chake,na
kudai haki yake,bila huruma kifo ndio zawadi na
tuzo pekee aliyolipwa kama malipo ya jasho
lake,chezea mfalme wa Mwamutapa wewe!.
Haya sasa,tuachane na hayo.Jua likiwa linaanza
kufifia huku ndege wa angani wakiruka ruka
angani,na kuipendezesha anga ya
Mwamutapa.Mama yake Ngesha anaamua kurudi
nyumbani baada ya kusimama kwa dakika kadhaa
mbele ya geti la kina Njoshi, huku akiwa haamini
kile alichokuwa anakiona.
Ikiwa tayali mida ya jioni, akiwa anarudi
Nyumbani,bila kufahamu ilikua ni saa ngapi, alisikia
kelele nzito na za kutisha kutoka msituni ,kelele
ambazo alizisikia kwa mala ya pili japokuwa kelele
hizi zilitisha sana kuliko zile za awali, kwani
zilisababisha mpaka ardhi kutetemeka. Lakini bila
kupoteza muda, mama yake Ngesha aliamua
kutimua mbio kuelekea nyumbani, mbio ambazo
zilimfikisha nyumbani baada ya muda mfupi tu,
kwani alitimua kama swala. Na mala baada ya
kufika nyumbani, jambo la kwanza lilikuwa ni
kufunga milango na madirisha ya nyumba yake, na
kisha kuketi sebuleni kumsubili mwanae.
Msituni;
Njoshi akiwa ameshikilia kamba yake kwa mkono
wa kushoto, ghafla alishangaa majini wale
wakipotea. Aliamua kutoka haraka sana shimoni,
huku akiwa amelowa na mwili wake kutoa harufu
mbaya, harufu ambayo ilisababishwa na maji
machafu ya shimoni, maji ambayo yalichanganyika
na na viumbe wengi wakiwa wamekufa na kuoza
ndani yake.
"Mmmh wamekimbia?, au wamenitega tena?
",Njoshi aliongea baada ya kutoka ndani ya shimo
na kushangaa kutokuta kiumbe yoyote yule, kitendo
ambacho kilimtahadharisha aweze kuwa makini,
kwani alifikili labda atakuwa amebadilishiwa mtego,
aweze kunaswa kirahisi ,jambo ambalo lilimfanya
aweze kuwa makini na asiweze kunaswa kwa mala
nyingine tena.
"Hapa ngoja nisonge mbele, na giza tayali
limeshaingia, inatakiwa nifike katika ngome ya
malikia haraka sana, niweze kuiba fimbo ya kifalme
na kuiandika jina langu, harafu nikachonge jeneza la
ajabu kisha kesho asubuhi na mapema nirudi
nyumbani ",Njoshi aliongea huku akianza kutimua
mbio na kuelekea katika ngome ya malikia, kwa
kutumia njia ile ile iliyokuwa imetegwa shimo na
kufunikwa na udongo juu yake. Bila kutambua kuwa
tayali kulikuwa na mtego mbele yake, mtego
ambao ulikuwa katika ngome ya malikia, ngome
ambayo ilihafadhi madini ya kila aina pamoja na
vitu mbalimbali ikiwemo fimbo ya kifalme. Fimbo
ambayo mtu anayetaka kuongoza Mwamutapa
lazima aimiliki, na kuandika jina lake, na hiyo ndio
itakua tiketi ya kuongoza nchi ya Mwamutapa.
Njoshi alizidi kusonga mbele huku akipanga
mipango ya namna ya kufanikisha kutengeneza
jeneza la ajabu haraka sana ili aweze kurudi
nyumbani siku ya jumatano asubuhi, siku ambayo
ilikuwa ya mwisho kukaa msituni, kwani mfalme
alitakiwa azikwe ndani ya siku tatu baada ya kufa,
na kama angezikwa katika jeneza la ajabu nje ya
siku hizi tatu, au angezikwa huku wananchi wa
Mwamutapa wakiwa wamefahamu kuwa amekufa,
mfalme hatoweza kufufuka kwani inatakiwa iwe siri.
Njoshi baada ya kukimbia ndani ya muda mchache
tu ,kwa umbali kama wa mita mia moja aliweza
kuiona ngome ya malikia, ngome ambayo
ilizungushiwa nyasi na kisha kupambwa na maua
mazuri sana, maua ambayo yalikuwa na harufu nzuri
na kuwavutia ndege wengi pamoja na wadudu
kuruka ruka katika ngome hiyo kufuata maua.
"Adui hayuko mbali, muda sio mrefu tutamtia
nguvuni, yani atajuta kuingia katika ngome na msitu
huu ",Malikia alizidi kuongea kauli za laana, kauli
ambazo baadae zitamgharimu kwani ilikua ni mala
ya pili akitamka kauli mbaya na za visasi kwa
Njoshi
Hii ilikuwa ni kama miiko, kauli ambayo anaitamka
malikia lazima aitimize, bila hivyo watu wake
wataweza kufa ghafla,na kisha ngome yake
itateketea. Jambo ambalo baadae linaweza kutokea,
kwani malikia alishindwa kumwadhimbu Njoshi na
kulipiza kisasi ili atimize kile alichokuwa akikisema,
na kuepusha balaa kwa watu wake.
"Aiw…eeeh mizimu wa babu zangu, niepu…sheni na
bal…aa h…ili ",Njoshi aliomba mizimu iweze
kumsaidia kwani bila kutegemea, alishindwa kutoka
mahali alipo, wala kujitikisa , baada ya kukanyaga
maji ya ajabu, maji ambayo malikia alinyunyizia
kuzunguka ngome yake, pale tu Njoshi alipotaka
kuingia ndani, katika ngome hatari ya malikia wa
majini wa msituni.
"Aiweeh mtukufu Gutamanya, mkuu wa majini wote
ulimwenguni, tayali nimemtia mikononi mwangu
adui yangu",malikia wa majini,msichana aliyekuwa
mrembo sana,aliongea huku akiwaongoza majini
wote kuelekea getini ,kwenda kumtazama adui wao
na kumtambua,kwani maji yale yalikuwa na nguvu
sana kiasi kwamba Njoshi aliweza kuonekana
machoni kwa majini,bila kusaidiwa na kitambaa
alichokivaa kiunoni.
Mwamutapa;
Ngesha na mama yake Njoshi walishangaa kukuta
kila nyumba ikiwa kimya huku milango na madirisha
yakiwa yamefungwa baada ya kutoka shambani.
Haikuwa kawaida mji kuwa kimya kiasi kile muda
wa saa moja jioni, hali hii ilimfanya Ngesha
kumuaga mama yake Njoshi na kisha haraka sana
akaelekea nyumbani kwao, ili aweze kujua usalama
wa mama yake.
Akiwa katika hali ya mshangao, alishangaa mama
yake akimkimbilia na kisha kumkumbatia huku
akilia, baada ya kufungua mlango na kukuta mama
yake akiwa ameketi sebulini akimsubili.
"Uko salama mwanangu, nilikuwa na hofu sana juu
yako ",mama yake Ngesha aliongea maneno mazito
yenye upendo ndani yake, maneno yaliyomfanya
hata Ngesha aweze kutokwa na machozi, kwani
alijiona mwenye makosa makubwa kumfanya mama
yake awe na hofu juu ya usalama wake, kwani
aliondoka tangu asubuhi bila kurudi nyumbani
mapema.
***ITAENDELEA **
Ili kujuwa hatma ya Njoshi msituni, tukutane katika
sehemu ya 11
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Back
Top Bottom