SEHEMU YA 12
***
Yalikuwa ni majira hayo hayo Timoth alikuwa anarejea kutoka kazini,tofauti na alivyotegemea kurudi majira ya saa kumi na moja asubuhi sasa alikuwa amerejea mapema zaidi. Huku akiwa na uchovu mwingi sana wa kazi za usiku na mawazo mengi juu ya anachokishuhudia kwa mkewe Timoth kwa kutumia funguo wake wa ziada hakutaka kumsumbua mtu yeyote yule aliufungua mlango wa sebuleni na kuanza kuingia ndani,kituo cha kwanza kilikuwa ni kwenye friji ambapo alichukua maji ya kunywa na kupooza koo lake.Wakati anameza mafunda ya maji yale anasikia kwa mbali kama kelele za malalamiko hivi."ah! Watakuwa ni majirani" alipuuzia Timoth huku akirudisha glasi ya maji mahali pake.
Hatua moja baada ya nyingine Timoth alianza kutembea kukifuata chumba chake,wakati huu sikio lake halikumdanganya katika chumba chake palikuwa na vurumai flani,kitanda kilikuwa kinachezacheza na sauti ya mwanamke ilikuwa inapiga kelele haikumchukua muda kubaini kuwa yule anayepiga kelele hizo alikuwa ni mkewe wa ndoa. Mwili wake ulikuwa ni kama umepigwa ganzi alihisi baridi kali ghafla na hakika imani yake ya dini ilikuwa imeyumba kama sio kutoweka kabisa."naua!" alijiapiza huku akirudi kasi kuelekea jikoni alipotwaa kisu pamoja na mwiko "nasema hivi! Naua leo" alisisitiza Timoth huku akitembea kwa mwendo wa kunyata kuelekea pale chumbani tena.
"safi kabisa funguo za chumbani ninazo" alikumbuka Timoth na kuzitoa funguo mfukoni mwake taratibu akaziingza katika kitasa na kufungua bila tatizo mlango ukakubali,kwa mkono wa kuume huku akiwa amechomeka kisu katika mkanda wake kwa nyuma na mwiko mkono wa kushoto alianza kushusha kitasa.