Simulizi : Jamani Mchungaji

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
3,983
10,804
4.jpg


Simulizi: JAMANI MCHUNGAJI !!
Mwandishi: GEORGE IRON MOSENYA
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES

SEHEMU YA 1


Masikio yake hayakuamini anachokisikia lakini ubongo wake uliamini kuwa mkewe alikuwa kwenye ndoto nzito sana, jasho lilikuwa linamtoka na alikuwa anajiviringisha pale kitandani kwa staili za ajabu ajabu

"Mchungaji.,ah! mchungaji...mchungaji" ndizo sauti alizokuwa anatoa mwanamke huyu

"Mh! ndoto gani tena hizi jamani au ndio....," alisita kumalizia neno hilo kwani kwa misingi yake ya dini ilikuwa haipaswi kumuhukumu mwanadamu mwenzako bila kumshrikisha Mungu muumba wa vyote. Miguno hiyo ilikuwa inashabihiana kabisa na ile ambayo huwa inasikika katika filamu za ngono.

Alitua ‘briefcase’ yake chini na kulegeza tai yake kabla ya kuondoa koti lake la suti, tayari ilikuwa saa nne usiku akiwa ametoka kwenye kikao cha kampuni. miguno iliyoendelea pale kitandani ilimtia hasira kiasi fulani lakini jina lililotajwa ndio lilimkera zaidi
"Honey! honey, iam back" taratibu akamwamsha na kuikatisha ndoto yake.

"Mh! mchungaji ah! mume wangu, umerudi karibu, saa ngapi hivi" kwa sauti ya ulevi wa usingizi alianza kuzungumza yule mwanamke huku akiyapikicha macho yake kwa kutumia kiganja kimoja na mkono mwingine ukiishikilia kanga iliyokuwa inataka kudondoka kutoka kifuani, mwanga wa taa iliyokuwa imewashwa ilimsumbua kuizoea hali.

Hasira ilimkaba kooni kijana huyu, alijaribu kutabasamu lakini sura yake ilifanana na mtu aliyepokea barua ya kufukuzwa kazi huku nyumbani akiwa na familia kubwa pamoja na wakwe waliokuja kuchukua mahari yao ambayo ilikuwa haijamaliziwa bado. Alichukizwa sana na suala la mke wake kukosea jina lake na kumuita mchungaji, mwanzoni alilisikia hilo jina katika ndoto lakini sasa alikuwa anamsikia mkewe akilitaja jina hilo wakati ameyafumbua macho yake.

* * * *
Lilikuwa suala gumu sana kumshawishi kijana Timoth aweze kukuelewa kuhusu umuhimu wa kuwa na mwenza ndani ya nyumba. Shughuli za kufua, kuosha vyombo na kufanya usafi ndani ya nyumba yake zilimchosha sana lakini hakutaka mke.

Aliyaogopa mapenzi sana kupindukia visa vya mafumanizi alivyovisoma kwenye magazeti na kusikia redioni vilimtikisa sana kaka huyu aliyekuwa na miaka takribani ishirini na tisa (29) na tayari akiwa na mafanikio yake kama kijana kwa mshahara alioupata kutokana na kazi yake ya afisa masoko wa kampuni ya usafirishaji ya Lookman ya jijini Dar-es-salaam.

Kwa ushauri wa mama yake mzazi na pia mchungaji wa kanisa lake bwana Marko, Timoth alianza kufikiria kuhusu suala hilo na hatimaye hisia za mapenzi alizokuwa amezifungia gerezani akazipa msamaha zikawa huru na uhuru huo zikautumia kumwangukia binti mrembo mwimba kwaya hapo kanisani aliyeitwa Noela, halikuwa suala gumu sana kwani wachungaji walikuwa kati yake hvyo Noela hakuleta longolongo uhusiano ukaanza rasmi hadi walipofunga ndoa takatifu kanisani hapo. Japo alikuwa anahofu ya kutendwa lakini aliifunga akili yake na kusema maneno haya.

“Nipo tayari kumuoa binti Noela Philemon, na nitaishi naye katika shida na raha hadi hapo kifo kitakapotutenganisha” makofi, nderemo na vifijo vilifuatia.

Timoth Getafe na Noela Philemon wakawa mke na mume rasmi!!

Timoth aliamini alikuwa amekosa mengi kwa kuwa katika maisha ya ukapera muda wote ule, kwani raha alizozipata kwa kuwa na Noela kama mke wake alijihisi yupo nchi ya kufikirika ambayo ni zaidi ya jengo la kifalme huko uingereza, zaidi ya Tanzania na amani yake, zaidi ya raha anazopata mtoto kwa kunyonya ziwa la mama huku joto la asili lillojaa upendo wa kweli wa mama likipenya katika ngozi yake.
 
SEHEMU YA 2


Noela alikuwa akimpa Timoth heshima zote za kuwa mume. Alimuheshimu na kumjali sana kama mtoto wake. Alimdekeza na kumjali, Timoth akajihisi kama yupo mikononi mwa bi. Mariam ambaye ni mama yake mzazi. Taratibu akausahau msiba uliotokea mwezi mmoja uliopita, kifo cha baba yake mzazi kwa ajali ya gari.

"Mh! nisingekubaliana na mchungaji na mama haya ningeyapata wapi?" alijiuliza Tim siku moja akiwa anakula chakula kizuri cha mkewe huku glasi kubwa ya juisi iliyokuwa inatoa jasho jasho za ubaridi ikimtazama.

Wakati wote huo Noela alikuwa mama wa nyumbani hakuwa na ajira bado zaidi ya kuimba kwaya kanisani shughuli ambayo haikuwa na kipato chochote kwani ilikuwa ni ya kujitolea kwa dhumuni la kumtumikia Mungu.

Noela alikuwa na miaka saba katika mstari wa mbele wa kwaya hiyo.

"Mpenzi samahani kama nitakuwa naingilia mipango yako....nataka kuomba kitu" Noela alimwambia mumewe miezi miwili wakiwa ndoani, wakati huo alikuwa akimpapasa papasa mumewe kifuani.

"Sema tu malaika wangu usiogope ni wewe Mungu amenipangia" Timoth alimwondoa hofu mkewe huku na yeye akimsukasuka nywele zake pasi na ujuzi wowote.

"Asante mume wangu mi nilikuwa nataka hapa nyumbani japo nipate kitu cha kuniweka bize na mi sio kingine zaidi ya ufugaji mdogo mdogo, si unajua ninavyopenda kufuga mie" alijieleza Noela huku akijiumauma midomo yake. Hakuweza kumuangalia machoni mume wake.

"Hapa nina mke kweli, yaani hilo sio ombi mke wangu il-hali umependa mwenyewe, nitakutimizia" alijibu kwa furaha Timoth huku akiendelea kuchezea nywele za mkewe.

Kama alivyoahidiwa ni kweli kwa haraka mabanda yalijengwa Noela akaanza kufuga kuku, kanga na bata baadae Mbuzi na hatimaye n'gombe, kwa kweli alikuwa mwanamke mchapakazi sana na alistahili pongezi zote.

* * * * *
Zoezi la kwenda nchini Uganda kurekodi mkanda wa video katika kwaya ya kanisa lao lilimlazimu Noela kutafuta kwa haraka kijana ambaye atahudumia mifugo yake kwa hizo wiki mbili ambazo hatakuwepo pale nyumbani. Timothy asingeweza kuwahudumia mifugo kwa wakati, kazi zake zilikuwa hazitabiriki.

Kwa kusaidiana na mume wake walijitahidi kwa uwezo wao wote pamoja na kusaidiana na wapendwa wengine wa kanisa kumtafuta kijana wa kazi.

* * * *
Oscar Simon alikuwa kijana kutoka Kigoma ambaye ndio alipata fursa hiyo ya kuwahudumia viumbe wale.

Kijana huyu wa kabila la Kiha kutokana na kazi ngumu za kusukuma mikokoteni na ubebaji wa mizigo (Kuli) zilikitawanyisha kifua chake katika pande mbili zilizojaa haswa.

Urefu aliobarikiwa tofauti na Waha wengi walivyokuwa wafupi ulimfanya awe na mwonekano wa kipekee sana na kuonekana mwanaume wa shoka, weusi wake na tabu nyingi alizopitia ziliuficha utanashati wake kabisa. Kazi ya muda mfupi aliyoipata kwa Noela ilikuwa kati ya kazi nyepesi alizowahi kupitia.

Ilikuwa kama bahati, baada ya kuwa amegonga mageti mengi sana kuomba ajira jijini Dar es salaam. Hatimaye bahati yake ikawa pia bahati kwa familia hii ya Noela na Timoth maeneo ya Kinondoni Studio jijini hapo ambayo hakika ilikuwa inamuhitaji kwa wakati huo.
Timothy akawa ameipata ajira!!

* * * * *
 
SEHEMU YA 3



Picha ya ajabu ilianza kumjia Noela akiwa kwenye basi pamoja na wanakwaya wenzake. Aliona inajijenga picha ya mwanaume mbele yake, sura haikuwa ngeni sana machoni pake,mwanaume yule alizidi kupiga hatua kumfuata, kadri alivyokuwa anasogea na yeye (Noela) alizidi kutamani amfikie, alikuwa amevaa vesti nyeupe na pensi fupi ambayo ilikuwa imechakaa yeye (Noela) alikuwa amevaa kitop pamoja na skin tight, mazingra yale yalikuwa kama ufukweni lakini palikuwa na kitanda kilichokuwa na godoro tayari, taratibu Noela alijilaza chali kitandani akiwa na mategemeo kuwa na yule kijana atajilaza pale, mara akaanza kurudi kinyumenyume kwa hofu yule kijana, matamanio ya Noela yalikuwa juu alianza kumbembeleza yule kijana lakini ni kama alipatwa na hofu ya ghafla hvyo hakuweza kumsogelea Noela.

"Njoo haraka nasema!!" alipiga kelele Noela na kushtushwa na vicheko vya wanakwaya wenzake ndani ya gari.
"Aah! kumbe anaota kanishtua kweli loh!" mwanakwaya aliyekuwa pembeni ya Noela alisema huku akishndwa kujizuia kucheka. Noela alikuwa amepiga kelele sana bila kujua kama amefanya hivyo

Aibu aibu zikamkumba Noela na kujipikicha macho yake ni kweli ilikuwa ndoto lakini ndoto gani hiyo jamani!!!! alijiuliza Noela kimoyomoyo huku safari ikiendelea. Hakutaka kulala tena akachukua kitabu chake cha nyimbo za mapambio akaanza kumuimbia Mungu kwa sauti ya chini, mashairi yake yakamvutia aliyekuwa pembeni yake na yeye akaanza kuimba, na waliokuwa pembeni wakafuatisha hatimaye wakaunganisha sauti zao, Noela akapandisha sauti yake akaongoza mashairi, kicheko kikasahaulika kila mtu akawa ametekwa na wimbo huo.

Safari ikaendelea, likawa suala la bandika bandua!!!!

Hadi wanaifikia boda ya Namanga kuingia nchini Kenya bado nyimbo ziliendelea kulindima.

Ukaguzi wa hati za kusafiria ndio ulikatisha burudani yao.

Wote wakawa kimya kwa muda!!!

****
"Karibu mke wangu mpenzi jamani nimekumis namshukuru Mungu umerudi salama na kazi mliyoifanya imebarikiwa katika bwana"

Timoth alimlaki mkewe kwa maneno hayo mazuri huku akimkumbatia siku aliyokuwa amerejea baada ya kuwa mbali na nyumba yake kwa siku nyingi.

"Asante mume wangu tunamshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea katika safari yetu" alijibu kwa furaha Noela.

"Shkamoo mama!" ilitoka salamu nyuma ya Noela.

"Marah...." alisita kuitikia Noela baada ya kugundua aliyekuwa anamsalimia, macho yalimtoka hadi yule kijana akapata hofu, alikuwa ni Oscar kijana aliyekuwa amepewa ajira kwa muda kuhudumia mifugo pale nyumbani.

"We ndio nani...ah! ni Oscar ah? marahaba" alianza kujiumauma Noela na dhahiri alionyesha mshtuko mkubwa.

"Vipi mke wangu kwani.." alihoji Timoth bila kumaanisha sana.

"Ah! ah! mh? hamna kitu wala" hofu ilizidi kumwingia.
 
SEHEMU YA 4


Hofu na uoga alioupata mkewe (Noela), Timoth alitambua mara moja, hakuijua sababu hasa na hakutaka kumuuliza mbele ya Oscar kijana mlisha mifugo kwa muda.

"Kwa hiyo Oscar aondoke lini mke wangu naona mwenye mifugo mwenyewe ndo umefika" Timoth alimuuliza mkewe wakati ametoka bafuni akijiremba kidogo mbele ya dressing table,

"Vipi utendaji wake ni mzuri?" alihoji Noela

"Mh! Sijawahi kupata malalamiko kutoka kwa kuku wala mbuzi yeyote nadhani kila kitu kinaenda vizuri" alitania Timoth huku akimtekenya mkewe ambaye aliruka juu taulo ikaanguka chini, kwa aibu aibu akajiziba kifua chake lakini akakiachia tena alivyokumbuka yule ni mumewe.

"Honey kabla hatujalala ni kwamba kanisa limetoa punguzo la bei za ng’ombe kwa waumini wake, naomba kama inawezekana na sisi tuanze kufuga n'gombe, eneo letu ni kubwa linaruhusu" kwa sauti ya kunon'goneza huku akipapasa kifua cha mumewe Noela alizungumza.

"Mke wangu wewe ndo mwenye maamuzi kwenye mifugu, tutanunua hao n'gombe, basi itabidi Oscar abaki kidogo ili aweze kukusaidia au unasemaje?"

"Haina neno mume wangu, nafurahi kuwa mkeo" alijibu Noela.

Usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwa Noela alitamani pakuche ili apate fursa ya kuhakikisha ndoto yake ya ndani ya gari akiwa safarini kama ina ukweli wowote

"Hivi yawezekana nimemwota huyo kijana? Mbona wanafanana sana jamani dah!, lakini mbona siku ya kwanza nilimuona wa kawaida tu, tena sana" Noela alijiuliza wakati anagalagala kitandani kutafuta usingizi ambao tayari ulishampitia mume wake mapema kabisa.
Hatimaye usingizi ulimpitia na asubuhi ikafika.

"Mpenzi amka maji ya kuoga tayari, yatapoa na hii baridi utakoma" Noela alimwamsha mumewe kwa sauti ya upole na mahaba tele.

Bila kuhoji chochote alikurupuka pale kitandani akachukua taulo akajifunga akambussu mkewe shavuni kisha akaingia bafuni.

"Haya kwa heri mume wangu na kazi njema" Noela alimuaga Timoth baada ya kuwa amevaa nguo na kupata kifungua kinywa.

"Asante mama yangu na wewe ubaki salama na Mungu awalinde" alijibu Timoth huku akirekebisha tai yake, Noela akamsogelea akamsaidia kuirekebisha ile tai kisha akambusu katika papi za mdomo wake, Timoth akatoa tabasamu la nguvu akampiga kibao cha kimapenzi katika shavu lake lililokuwa linatangaza vishimo vidogo pande zote. Kisha akafungua mlango na kutoweka.

Noela akabaki kumsindikiza kwa macho hadi alipoishia
 
SEHEMU YA 5


Simu ya mke wake ilikuwa haipatikani na alipojaribu kupiga kwa mchungaji wa kanisa lao kuulizia kulikoni simu iliita bila kupokelewa halikuwa jambo la kawaida hata kidogo simu ya mkewe kutopatikana hewani bila taarifa.
"Mh! Kuna nini tena?" Timoth alijiuliza.
Tim hakuchoka kujaribu lakini suala likawa lile kwa pande zote mbili.wasiwasi ukachukua nafasi yake, wivu nao ukairukia nafsi yake. Akaaminiu kuna tatizo
"Hivi Oscar alinipa namba yake kweli...lahaula aliwahi kunipigia siku zile alipokuja rafiki yangu nyumbani,sijui ilikuwa inaishia ngapi" alijiuliza Tim huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake kwa jitihada kabisa.
Wakati huo zilikuwa zimepita wiki tatu tangu Tim awe amenunua n'gombe kama mkewe alivyotaka.
"Ewalaa! Imeita sijui ni yenyewe!" alijiuliza tena
"Halow shkamoo bosi..."
"Marahaba..ni Timoth naongea wewe Oscar hapo nadhani."
"Ndi..." hata kabla hajamalizia mawasiliano yalikatika simu ilikuwa imeishiwa charge.
"Hebu ngoja niende nyumbani sasa hivi huenda kuna lolote baya linatokea" aliamua Tim.
Ilikuwa bahati yake hapakuwa na foleni sana siku hiyo hivyo alitegemea kufika nyumbani salama.
"Konda niache hapa hapa nishushe tafadhali" Timoth ghafla alimwambia kondakta huku shingo yake ikiwa imekakamaa kutizama kitu flani nje.
"Vipi bosi mbona ghafla hivyo tena.."
"Hapana we nishushe...dereva tafadhali niache hapa hapa,nilegezee tafadhali nishuke" alibembeleza Timoth,jasho jembamba lilikuwa linamtoka hakuamini picha iliyokuwa mbele yake alidhani ni akili imemruka anaona vitu wasivyoviona wengine hivyo kushuka kwake ndio suluhisho pekee ili awe shuhuda wa ukweli japo alikuwa na hofu moyoni.
 
SEHEMU YA 6


Dereva hakuwa na hiana akazikanyaga breki zake gari likasimama Tim baada ya kulipa nauli akashuka, kwa mwendo wa kunyata na tahadhari kubwa akaanza kusogea.
"Zamzam guest house" macho yake yaliweza kusoma vyema jina la nyumba hiyo ya kulala wageni,kwa akili ya mwanadamu yeyote mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri hakika watu hawa wawili wenye furaha walionekana kutokea katika jengo lile,na hata kwa Timoth pia aliamini hivyo kuwa mke wake pamoja na mwanaume mrefu mwenye kipara akiwa amevaa suti nao pia walitokea hapo.

"Noela...noela ni Noela yule" aliongea peke yake Timoth huku akisogeza hatua zake taratibu kusogea enen hasa la tukio.Mkewe alikuwa na furaha sana na mara kwa mara waligonganisha mikono yao na yule wanaume.

"Atakuwa nani yule maskini wa Mungu anafanya nini hiki Noela" aliendelea kujiuliza Timoth,na punde alivyokaribia eneo la tukio tayari wawili hawa walikuwa ndani ya gari wakitokomea zao. Tim alikuwa kama chizi vile alìhaha sana eneo lile huku jasho jingi likimtoka.

* * * * *
"Karibu mume wangu" Noela alimpokea Timoth aliporejea nyumbani.

"Mbona umetokwa jasho hivi? Au ndio foleni tena, mh! Miji yetu hii jamani mateso" aliendelea kuongea Noela huku Tim akiwa kimya akimwangalia tu.

Hasira aliyokuwa nayo alitambua yeye mwenyewe,hakutaka kuionyesha hadharani kwani bado hakuwa na uhakika mkubwa sana kama ni kweli alikuwa ni mkewe na kama ni yeye je ni kweli alikuwa anatoka pale guest,maswali hayo ndiyo yalimkosesha ujasiri wa kumuhoji mkewe.

"Ni kweli gari lilikuwa limejaa sana" alijibu Timoth.

"Mh! Pole mume wangu....halafu kabla sijasahau mchungaji amekusalimia" alisema Noela.

"Nini! Ina maana...."

"Nini? Ina maana..." alishtuka Timoth.

"Mbona umeshtuka my love nilikuwa naye leo kwenye maombi" alijibu kwa furaha Noela huku akimvua mumewe koti la suti alilokuwa amevaa bado.
"Aah! Ok! Asante" alijibu Timoth lakini usoni hakuwa na furaha hata kidogo,na wasiwasi ulimtawala sana,kidogo aulize lakini akajizuia tena.
"siku yetu ilikuwa nzuri sana jamani!! Yaani...."
 
SEHEMU YA 7


"niwekee maji bafuni nioge" Timoth alimkatisha Noela alipotaka kuendelea kuongea,fundo la hasira lilikuwa limemkaba kooni.
"honey una tatizo gani leo?"
"nimejibishana na kondakta wa gari vibaya na mimi ndio nilikuwa na makosa,sijisikii vizuri nahtaji nipumzike kwanza" alidanganya Timoth
"lakini tumekuombea na mchungaji,nina upako kweli" alijibu Noela kwa furaha nyingne kubwa.
"aah!" alijikuta amesonya Timoth,jambo ambalo kamwe alikuwa hajawah kulifanya mbele ya mkewe.
"mume wangu pepo mchafu anakuingia hebu maliza kuoga twende kwa mchungaji ukaombewe" alijibu Noela kwa sauti ya upole kabisa.Timoth alianza kutetemeka,mkono wake ukaanza kuingia katika majaribu ya kumpiga mkewe lakini kuepusha shari akaingia chumbani na kumwacha Noela akiandaa maji ya kuoga bafuni.
**
"Oscar!!"
"naam mama!" aliitikia Oscar huku akiacha shughuli zake na kusogea alipokuwa Noela.
"Hivi unaitwa nani vile?" aliuliza Noela."Aah! Unaitwa Oscar kweli" alijiuliza na kujipa jibu Noela huku Oscar akijizuia kutoa kicheko kwa swali alilouliza Noela.
"umewakatia n'gombe majani tayari"
"ndio dada" alijibu bila wasiwasi.
"aah! Sawa nenda ukaendelee na kazi zako basi" alisema Noela huku akirejea ndani,mumewe alikuwa yupo ndani sebuleni anapata kifungua kinywa kabla ya ya kwenda kazini.
"kwa nini alinijia ndotoni kijana huyu mh!!" alijiuliza Noela wakati akirejea ndani.
"mi naenda mke wangu ubaki salama eeh!"
"haya na wewe kazi njema mpenzi" waliagana Noela na Timoth.
Dakika kumi baada ya Timoth kuondoka,huku akiwa na wasiwasi Noela alimwita tena Oscar kwa lengo kuu la kumuhoji kulikoni,hakujua ataanzia wapi lakini alimwita. Tangu aamke asubuhi alikuwa na nguo yake ya kulalia na alipomwita Oscar bado alikuwa na nguo ileile
 
SEHEMU YA 8


"naam dada" aliingia Oscar baada ya kuingia ndani.
"kaa hapo hv" Noela alimwelekeza kwa kidole Oscar naye akakaa wakawa wanaangaliana uso kwa uso,Oscar hakuwa na wasiwasi hata kidogo lakini Noela ambaye ni mwenye nyumba alikuwa anatetemeka,vidole havikuisha kukunjwa kunjwa bila sababu,alishindwa cha kuanza kuongea,mdomo ukawa mzito sana,hali hiyo hata Oscar aliitambua japo hakujua kuna tatizo gani limemkuta Noela,singlendi aliyokuwa amevaa Oscar ilimkumbusha ile ndoto ya kwenye basi wakati wanasafiri.
"ulisema unatokea wapi Oscar"
"mimi wa Kigoma dada" alijibu kwa heshima Oscar ambaye nayeye sasa hofu ilianza kumwingia,alidhani anataka kusimamishwa kazi.
"KIgoma pazuri eeh" alianza kuzuga Noela.
"sio kama huku kwenu lakini" alijibu Oscar.
"unatamani kurudi huko au umepapenda hapa" aliuliza Noela
"kula sitaki kurudi maisha magumu sana kule"
"basi hautarudi na mimi napenda uwe hapa" alijieleza Noela ambaye ujasiri ulianza kumwingia
"sasa Oscar nilichokuitia ni..." mlio wa simu ulimkatisha Noela kuzungumza
"hebu nipatie hyo simu yangu" alimwomba Oscar aliyetii mara moja.
"halow! ...mchungaji....ndio...haya...sasa hivi nakuja" Noela alijibu maongezi ya kwenye simu haraka haraka huku akisimama,kuna jambo la muhimu sana ambalo alikuwa ameambiawa kwani hata pale sebuleni hakuaga akaingia chumbani.
Baada ya dakika ishirini hiv alirejea tayari akiwa ameoga na kubadili nguo
"Oscar naenda kanisani mara moja nimehtajika sawa" Noela alimuaga Oscar

"akija kaka yako mwambie hvyo sawa!" alisisitiza Noela huku akipiga hatua haraka haraka kuelekea nje.
 
SEHEMU YA 9

Ilikuwa ni taarifa ya dharura iliyomtaka Timoth kwenda kushughulikia suala la kusafirisha mizigo iliyotakiwa jijini Mbeya haraka sana hivyo Timoth alitakiwa kufanya kazi hiyo hadi majira ya saa tano usiku kwa misingi hiyo Timoth alipewa ruhusa majira ya saa sita kurejea nyumbani na baadaye saa kumi na moja kurejea tena kazini.
Timoth bila hiyana alitii amri na kufunga safari kurejea nyumbani kwake
"mama watotoo! Mama watotoo!" Timo alianza kuita alipofika mlangoni,mkononi alikuwa na tunda aina ya Apple alilonunua maalum kwa ajili ya mkewe mpenzi.Halikupatikana jibu lolote lile pale hadi alipokuja Oscar kutoka kukata majani
"mama alitoka ameenda kanisani"
"ameenda kanisani? Kwa misingi ipi?"
"alipigiwa simu na mchungaji" alijibu bila wasiwasi Oscar
"eti!!"

Bila kujitambua Timoth alikuta ameangusha tunda alilokuwa nalo mkononi,"kwani vipi bosi si amekwenda kanisani au ni vibaya jamani" alihoji Oscar
"ah! Hapana sio vibaya lakini mh! Mh! Ah! Ni sawa" alianza kujiumauma Timoth huku akiokota tunda lake lililokuwa chini.
"weka hili tunda kwenye friji na hili begi niwekee ndani pia" Tim alimpa maelekezo Oscar huku akiahirisha safari ya kuingia ndani na kurudi alipotoka.
"nahisi vibaya kabisa huenda kuna kitu hapo katikati,si bure matukio haya" aliondoka huku akijiwazia.

***
"bwana asifiwe bwana Timoth!"
"amen mchungaji" alijilazimisha kujibu huku akitoa tabasamu bandia baada ya kukutana na mchungaji akiwa pamoja na mkewe mpenzi."jamani mume wangu kulikoni mbona haupo kazini mida hii" Noela alihoji kwa mshangao
"kawaida tu leo nimekuja kuwasalimia kidogo huku"
 
SEHEMU YA 10



"ooh! Vyema sana na bwana asifiwe sana" alidakia mchungaji huku akimpa mkono wake Timoth,jinsi alivyokuwa aanatokwa na jasho Timoth alishtuka sana na kupatwa wivu mkali.
"Bwana Timoth haupo katika hali yako ya kawaida una tatizo gani?" mchungaji alimuuliza Timoth baada ya kumwona hana raha hata kwa mbali.
"nahisi nina homa mchungaji" alidanganya
"shabash! Hebu tuingie ndani kidogo tulikemee pepo la magonjwa" alishauri mchungaji na wote wakarejea ndani.
Timoth hakuwa na ugonjwa wowote ule,lakini pia aliogopa kuzielezea hisia zake toka moyoni,alikuwa ni mchungaji huyo huyo aliyesimamia kidete yeye aoe lakini leo hii anapatwa na wasiwasi juu yake "ee mwenyezi Mungu niepushe na mtihani huu" alijisemea Timoth wakati maombi ya kuuombea ugonjwa wake yakiendelea,mchungaji alikuwa amemshika mkono Noela,Tim alishindwa kufumba macho akawa anatetemeka kushuhudia hilo tukio mbele yake.
"mchungaji umekuwa mtu muhimu kwangu na kila nikiwa nawe neno lako linanipa faraja nafuraha sana" Noela alimwambia mchungaji maneno hayo mbele ya mumewe,Timoth alitamani kulia lakini alijizuia kwa hilo.
 
SEHEMU YA 11


***
majira ya saa nane usiku Noela alikuwa katika joto ambalo hajawahi kulipata hata siku moja maishani mwake,halikulingana na la mpenzi wake hata kidogo,mikono yake ilikuwa imezunguka katika mgongo wa kidume hichi. Nguo nyepesi aliyovaa ilimfanya ajisikie huru sana.
Taratibu akaanza kumbana kidume huyu asitoke katika himaya yake. Alikuwa katika ulimwengu mwingine alikuwa radhi kutumia hata nguvu ilimradi akate kiu yake.

Mwanaume yule alikuwa hataki kufanya tendo lolote baya na Noela lakini alilazimishwa na dada huyu. Noela alivyoona anataka kuzidiwa nguvu akajifunua nguo yake akabaki kama alivyozaliwa,janja hiyo ikamteka yule kidume ujasiri ukamuisha kwa haraka akairukia shingo ya Noela na kutuliza kinywa chake pale kisha akauruhusu ulimi wake kuanza kutembea juu ya mwili wa Noela,ukelele kama wa mtu aliyepandwa majini ndio ulianza kusikika,alikuwa hajitambui Noela,macho yake yalikuwa yamelegea kama mtu aliyekuwa amekunywa sumu na sasa yupo katika dakika za mwisho za uhai wake,kiuno chake kilikuwa juu kabisa ni kama vile kilikuwa kinalilia huduma fulani kutoka kwa yule mwanaume.
"mchungaji please! Please! Don't kill me,jamani usinitende hvyo aah! Nakufa mie please" alikuwa analalamika Noela huku vidole vya mikono yake vikihangaika kujipapasa kwa uwezo wote huku kifuani kwake chuchu zake zikishughulikiwa na yule mwanaume
 
SEHEMU YA 12


***
Yalikuwa ni majira hayo hayo Timoth alikuwa anarejea kutoka kazini,tofauti na alivyotegemea kurudi majira ya saa kumi na moja asubuhi sasa alikuwa amerejea mapema zaidi. Huku akiwa na uchovu mwingi sana wa kazi za usiku na mawazo mengi juu ya anachokishuhudia kwa mkewe Timoth kwa kutumia funguo wake wa ziada hakutaka kumsumbua mtu yeyote yule aliufungua mlango wa sebuleni na kuanza kuingia ndani,kituo cha kwanza kilikuwa ni kwenye friji ambapo alichukua maji ya kunywa na kupooza koo lake.Wakati anameza mafunda ya maji yale anasikia kwa mbali kama kelele za malalamiko hivi."ah! Watakuwa ni majirani" alipuuzia Timoth huku akirudisha glasi ya maji mahali pake.
Hatua moja baada ya nyingine Timoth alianza kutembea kukifuata chumba chake,wakati huu sikio lake halikumdanganya katika chumba chake palikuwa na vurumai flani,kitanda kilikuwa kinachezacheza na sauti ya mwanamke ilikuwa inapiga kelele haikumchukua muda kubaini kuwa yule anayepiga kelele hizo alikuwa ni mkewe wa ndoa. Mwili wake ulikuwa ni kama umepigwa ganzi alihisi baridi kali ghafla na hakika imani yake ya dini ilikuwa imeyumba kama sio kutoweka kabisa."naua!" alijiapiza huku akirudi kasi kuelekea jikoni alipotwaa kisu pamoja na mwiko "nasema hivi! Naua leo" alisisitiza Timoth huku akitembea kwa mwendo wa kunyata kuelekea pale chumbani tena.
"safi kabisa funguo za chumbani ninazo" alikumbuka Timoth na kuzitoa funguo mfukoni mwake taratibu akaziingza katika kitasa na kufungua bila tatizo mlango ukakubali,kwa mkono wa kuume huku akiwa amechomeka kisu katika mkanda wake kwa nyuma na mwiko mkono wa kushoto alianza kushusha kitasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom