Simulizi hii inatufundisha nini kama Taifa?

Simulizi hii inatufundisha nini kama Taifa?

ong'wafaza

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
262
Reaction score
115
Hapo kale palitokea ukosefu wa chakula mkubwa na kusababasha njaa kali miongoni mwa wakazi wa mkoani Mwanza.
Hii ilipelekea wanaume wengi kuacha familia zao ili kutafuta chakula kutoka maeneo ya mbali.

Pamoja na hali hiyo,akina mama walibaki na watoto nyumbani bila kujali kama waume zao watafanikiwa na ni muda gani watawaletea chakula.

Kama ilivyo kawaida ya watoto,wao hawajui kama chakula huwa mara nyingine kinakosekana kabisa nyumbani.
Hivyo kina mama iliwabidi wawashe tu jiko na kuinjika hata mawe ili watoto angalau wawe na matumaini kuwa kuna chakula kinapikwa,hivyo watakula.

Mioto iliwaka kwa masaa mengi ili kuwahadaa watoto,na kila walipolalamika njaa,waliambiwa bado kiko jikoni hakijaiva bado!

Mungu jalia,ilifika watoto wanapatwa na usingizi wanalala bila kula.
Hali hii iliendelea mpaka hapo chakula kinapopatikana.

Ujanja huu ulifanikisha utulivu kwa watoto na familia nzima mpaka hapo hali ya upatikanaji wa chakula ilipotengemaa.

Si baba wala mama aliyewaeleza ukweli watoto kuwa chakula kisingepatikana kabisa kwa wakati huo ili kutowakatusha tamaa.

Swali la kujiuliza hapa ni je, wakati mwingine uongo unahitajika na unaweza kusaidia?

Lakini kikubwa zaidi hii simulizi unatufundisha nini kama taifa?
TAFAKARI.
 
Back
Top Bottom