briophyta plantae
Senior Member
- Feb 18, 2017
- 120
- 140
SIMULIZI FUPI: NDOTO YA DANIEL
MWANDISHI: MOSSES MLAY
Siku moja Daniel alipata safari ya kikazi ikiwa ni siku mbili tu kabla ya shughuli maalum ya washenga kuja nyumbani kwaajili ya kumposa dada yake, alikuwa na taarifa ya ugeni huo na ilikuwa na umuhimu mkubwa wa yeye kuwepo. Katika shghuli hiyo kwani ilimbidi aiwakilishe nafasi ya baba yake aliyekuwa amefariki miaka michache iliyopita kwa tatizo la kisukari hivyo kuiacha familia ikiwa na mama pamoja na watoto watatu ambao ni Daniel, Caroline na Emanuel.
Daniel aliondoka huku akiahidi kurudi siku inayofuata jioni au siku yenyewe ya shughuli kama atashindwa kurudi hiyo kesho yake. Daniel alianza safari majira ya jioni akielekea nje ya jiji la dar es salaam mkoa wa jirani tu nikiwa na maana mkoa wa Tanga. Aliondoka akiwa peke yake mapka alipofika maeneo ya kibaha ambapo alisimama katika kituo kimoja cha mafuta pale kwaajili ya kuongeza mafuta.
Akiwa pale Daniel alikutana na watu wanne waliiomba wasogezwe mji wa mbele kidogo huku wakisisitiza watamlipa hela yoyote kutokana na ugumu wa kupata usafiri siku hiyo pamoja na umuhimu wa sehemu husika wanapoenda. Kwa upande wa Daniel hakuona kama ni tatizo na alikubaliana nao baada ya mazungumzo na malipo kufanyika.
Daniel alianza tena safari huku gari yake aina ya RAV4 ikiwa imepata wakaaji katika kila siti yake kwani nyuma walikaa watu watatu huku mbele akiwa yeye pamoja na abiria mmojawapo. Daniel alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana akijitahidi kukimbizana na muda kutokana na usiku kuwa umeshaingia wakati huo akipiga story mbili tatu na abiria wake.
Jinsi story zilivyonoga ndio jinsi safari ilivyonoga pia. Walitembea kwa umbali mrefu na hatimaye ukimya ulitawala huku kila mmoja akionekana kusinzia kutokana uchovu wa safari, ukimya ulivyozidi Daniel aliamua kuwasha redio ya gari ili atomize ule msemo wa “safari na mziki”. Alijaribu kutafuta stesheni yoyote nzuri lakini hakufanikiwa, alijikuta akipata wazo la kuweka CD ya nyimbo aliyokuwa nayo kwenye gari.
Kutokana na CD hizo kuwepo kwenye ki mkebe maalum ilimbidi asimamishe gari kabisa kwa usalama wake na abiria wake ili aanzae kuitafuta CD nzuri itakayomfanya asisinzie wala kochoshwa nayo. Daniel alipaki gari pembeni na kisha aliwasha taa ya ndani ya gari ili aweze kupata mwangaza mzuri wa kumwezesha kuona sawia….
Lahaulaaa!!!!! Ilikuwa almanusura Daniel azimie baaada ya kugundua ndani ya gar yoko peke yake na wala wale abiria hawakuwamo garini tena. Alitamani apige hata kelel lakini aliona zinaweza zisimsaidie chochote, hakuelewa abiria wake walishukaje mule ndani ya agari ilihali hakusimama popote tangu watoke pale kibaha. Kengele ya hatari iligonga kichwani mwake na kufanya maamuzi ya kuondoka mahali pale haraka sana, alipojaribu kuondoka alishangaa gari likizima ghafla kama vile kuna tatizo katika mfumo wa umeme au mafuta kuisha, alishangaa hali ile huku hofu ikianza kumtawala.
Alipiga stata ili kuliwasha lakini gari haikuwaka, aliendelea kujaribu mara kadhaaa huku akiwa amechanganyikiwa asijue afanye kitu gani. Alifanya maamuzi ya kushuka ndani ya gari ili aangalie kama kuna tatizo anaweza kuligundua kwenye injini ya gari yake..
Mama yangu!!! Alijikuta akitamka maneno hayo huku akiwa aamini anachokiona kwenye mazingira yale, alikuwa katika eneo la barabara lililozungukwa na makaburi pande zote. Alijaribu kuvuta picha kutokana na uzoefu wake katika barabara hiyo ili kujua yupo sehemu gani lakini aligundua hakuna chochote anachokijua au kukumbuka kama kuna sehemu kama hiyo ameshawahi kupita.. mwili ulimuisha nguvu hata akashindwa afanye kitu gani usiku ule.
Akiwa katika mshangao na hofu ile Daniel aliweza kuona mwanga wa taa za gari kwa mbali kwa uelekeo ule aliokuwa akiuendea lakini baada ya kuona mwanga ule lile gari lilionekana kusimama na kisha taa zilizimwa ghafla. Daniel aliondoka pale haraka kuelekea alipoliona lile gari ilia one kama anaweza kupata msaada wowote wa yeye kutoka eneo lile.
Alitembea kwa haraka kuelekea ale alipoona ile gari imesimama, alisonga mbelekwa tahadhari mapaka alipofika pale alipoona ile gari. Yalikuwa ni maajabu ya mwaka kwa Daniel kwani eneo lile hakukuwa na gari yoyote ile,alishindwa kuelewa kama ni aliona vibaya au vipi na kama aliona sawa sawa ile gari iliondokaje tena mazingira yale pasipo hata kuwasha taa usiku ule,ilikuwa ni zaidi ya kihoja kwa kwake. alijikuta akitimua mbio kurudi kuelekea alipoacha gari yake, hakuwahi kuogopa kama alivyoogopa siku hiyo, mwili ulikuwa ukitweta kwa jasho licha ya baridi kali usiku ule huku akihema kama mtu aliyekimbia umbali mrefu mno.
ITAENDELEA...