SEHEMU YA 5
Reshmail Mtoto wa mwisho na pekee wa kike kati ya watoto wanne wa mbunge wa jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Msuruli Haruna,hakupata kujua shida katika maisha yake na urembo aliojaliwa pia hakuufaham kwa sababu hakuwepo wa kumwambia kuwa yeye ni mrembo,kuta na fensi ya sen'gen'ge iliyozunguka mji wao haikumruhusu kutoka nje hovyo hovyo,tofauti na siku ya kwenda msikitini Resh alilazimika kusubiri hadi alipofikisha miaka kumi na nne alipojiunga na kidato cha kwanza katika shule ya st.marry's international ndio alipata wasaa wa kujumuika na wananch wengne wa Tanzania na nchi za jirani,elimu yote ya darasa la kwanza hadi la saba aliipatia katika jumba la kifahari la baba yake.
Mazoea ya kuish maisha ya peke yake peke yake yalimtesa sana Resh kiasi kwamba hadi anamaliza kidato cha nne aliweza kuwa karibu kiurafiki na wanafunzi wachache na weng wao wakiwa wasichana tena watoto wa matajiri na vigogo mbalimbali wa serikali.Kampani kubwa ya Reshmail alikuwa ni mama yake mzazi,yalikuwa ni mazoea makubwa sana lakini yasiyoshangaza,mara nying walikuwa wanatembea pamoja huku wameshkana mikono huku wakifurah sana.
Kidato cha tano na sita katika shule ya Arusha international school ndio kwa mara wa kwanza ilimpeleka nje ya jiji la dar-es-salaam.
Resh alilia sana kutenganishwa na mama yake lakini hakuwa na jinsi ilimlazimu kuondoka,mama alishindwa kujizuia alilia kwa uchungu ambao mumewe hakuutambua maana yake. "Nitakuwa nakuja kukusalimia" bi Gaudensia alimnon'goneza mwanae wakati akipanda gari la baba yake kuelekea airport."Usiache mama".alijibu resh huku akimbusu mama yake shavuni.
Mwanzoni ilianza kama utani pale Adam alipokubali ombi la Reshmail kuwa marafiki,walikuwa wakiulizana mambo ya kawaida sana huku katika orodha ya marafiki wa Reshmail ni Adam peke yake alikuwa mwanaume,"Mbona una marafiki wachache au ndo umejiunga facebook?" adam alimuuliza reshmail katika moja ya 'chatings' zao "No ni uamuzi 2 iam nt interested with boys i wonder why you?" "May be iam someone special,who knows" alijibu Adam, "You might be" alijibu reshmail."Yani hadi mchumba wako hujamweka kwenye orodha?" "Sina huyo mchumba unayemdhania" "What? msichana mrembo kama wewe,au hizi picha sio zako?" "Ni zangu kwani ukiwa mrembo lazima uwe na mpenzi?"alisisitiza Resh kisha akaendelea "Naona we upo kwenye uhusiano,hongera" aliandika Resh,ni wanaume wachache sana akiulizwa na msichana mrembo kama ana mpenzi halafu akubali na hata kwa Adam ilikuwa hivyo,"Mh! nimejiandikia tu,mi sina mtu nani wa kunipenda mimi?". Alidanganya Adam,"What! hawakioni hcho kifua chako au na wewe hiyo sio picha yako?"
"Ni ya kwangu,Reshmail una utani wewe"
"Sina utani nimekipenda sana"
"Haya asante,kwako wewe sina la kusema unavutia kila upande"
"Asante lakini we zaidi,Adam naingia kuoga nisindikize basi"
"Wee,si umeniambia mnakaa wanne sa wenzako watanielewaje?" alijibu Adam huku akiamini kwamba hayo yote yanayotokea ni utani mtupu.
"Kwa hyo ningekuwa peke yangu ungenisindikiza?" "Yeah? ningekusindikiza lakini ningefumba macho" alitania Adam.
"Vp ninatisha sana au,yan hadi ufumbe macho sawa tu" alilalamika Resh,"Natania mrembo lakin si unajua tena nitajiumiza"
"Ok! tuachane na hayo,simu yako inauwezo wa kufungua e-mail?"
"Inafungua tena sasa hivi nilikuwa ninasoma emails" alijibu adam.
"Ndio hii
Adamboy@Yahoo.com?" "Yap ndio hyo" "Fungua baada ya dakika tano uone zawadi yako"
Jasho jembamba huku mikono ikitetemeka,macho yakiwa yamemtoka Adam hakuamin anachokiona kwenye simu yake.