SEHEMU YA 66
"Sawa tunaenda kule, ila sitaki utokee usaliti wowote ule" Martin alisema.
"Hilo haliwezekani Martin. Siwezi kukusaliti wewe ndugu yangu" Richard alisema.
Watu wote sita walipanda kwenye gari na kuelekea katika nyumba ya kulala wageni aliyopanga Martin kwa muda, waliyoyakuta huko.
Martin ndiye alikuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya kugonga mlango mara tatu bila majibu. Bastola yake ikiwa kaishika imara kwa mkono wake wa kulia. Alikaribishwa na damu zilizotapakaa mle ndani. Pembeni aliuona mwili wa Binunu ukiwa unaogelea katika dimbwi la damu! Ilikuwa ni picha ya kutisha sana kuitazama.
"Dokta Yusha, mcheck yule majeruhi" Daniel Mwaseba alimwambia Dokta Yusha.
Wakati Dokta Yusha akivaa gloves ili kumhudumia yule mgonjwa. Wakina Daniel waliendelea kupekua mle ndani. Hakukuwa na kitu chochote kile cha maana.
"Katoroshwaaa!! Elizabeth Neville katoroshwaaa" Martin alisema kwa uchungu huku akiwa anachungulia uvunguni.
Mara sauti kutoka kwa Dokta Yusha ilisikika " Huyu mwanamke amefariki!! Amepoteza sana damu, tumechelewa"
Kauli ya Dokta Yusha ilibadilisha upepo wa mle ndani. Richard na Martin waliungana pamoja katika mwili wa Binunu. Waliufikia muda gani hakuna aliyekuwa anajua. Wote kwa pamoja waliutikisa mwili wa Binunu wakiwa na matumaini kwamba ataamka. Macho ya Binunu yaliwaangalia katika hali ya mshangao, mshangao uleule wa kumwona Elizabeth Neville akinyanyuka pale kitandani kama mzimu.
"Binunu, amka Binunuuu" Richard alisema kwa uchungu.
"Comrade, usife comradeee" Martin nae alisema kwa majonzi makubwa mno.
Binunu aliwashangaa tu, kwa macho yasiyo na uhai. Martin aliyafumba yale macho ya Binunu kwa mkono wake.
"Rest in Peace Binunu" Martin alisema kwa sauti ndogo.
"Siamini, siamini huu ndio mwisho wa Binunu, haiwezekani, haiwezekani. Mtakilipia kifo hiki. Yeyote yule aliyemuuwa Binunu lazima alipe kifo hiki. Kifo cha Binunu hakiwezi kupita hivihivi tu" Richard alisema.
Martin alishindwa kuvumilia, chozi la kiume lilidondoka na kudondokea katika maiti ya Binunu.
"Ni mimi, ni mimi ndiye niliyesababisha ufe Binunu. Nilikulazimisha uje katika kazi ambayo uliikataa.
ITAENDELEA
Pseudepigraphas