SIMULIZI: Eliza na Ndoa Yangu (Kisa cha kweli cha kusisimua)

SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 15
Man Middo Tz +255 655 969 973

Mimi nilikua najua vitu vingi tu hata kutumia hiyo laptop nilijua lakin niliogopa kufanya baadhi ya vitu maana ananidharau mno anajua mimi wa hovyo tu.

Kuna siku niliunganisha Tv na spika za redio yeye hakujua. Baadae pia simu na radio akaniangalia huku akishangaa harafu akasema

“Kumbe ni hivyo”

Yani hata kusema nielekeze yeye kimya, hata kwenye Muvi za kizungu mimi nilikua mwepesi kuelewa kuliko yeye lakin alijifanya kujua.

Kuna baadhi ya vipande mimi ndo namuelekeza wamemaanisha nini, sasa akawa analeta tukiangalia sehemu akiwa hajaelewa ananiangalia eti niseme maana yake, ahahaha yani hata kuomba au kuuliza hana hicho yani anadharau mnoo.

Siku moja niliamua kutumia laptop na yeye alikua anajua kuwa mimi sijui kuitumia hivyo alikua anaiacha tu kila siku na kuikuta hivyo hivyo.

Basi siku hiyo alivyoenda kazin nikajaribu kufungua kumbe hajaweka password nikaanza kupekua nikakuta kumbe muvi zake za ngono bado anazo yani.

Baadae ninaendelea kuangalia nikakuta chat zao na mwanamke nilikuta amemtamkia maneno mazuri mno ya kimahaba ambayo sikuwahi tamkiwa niliangalia tarehe walizo chat, maana siku nyingine anaenda nayo kazini nikagundua kuwa ni mwanmke wa muda mrefu mno na wanajuana.

Aisee nilipandwa na uchungu nilianza kulia nilia wee nakiwaza kuwa kumbe naishi na lifuska la kiume.

Baade akaja binti ambae alikua akimuita Baba mdogo nikamuonyesha angalie baba yake anayofanya maana Yule binti alitokea kuwa mtu wangu wa karibu kwa kipindi kile hivyo nikamuonyesha

“Hebu ona baba yako mshenzi anayonifanyia yani hajali kabisa hali yangu ya ujauzito”

Niliendelea kulia kama kuna msiba. Baadae Yule bint alienda kumwambia baba mkwe kuwa mama kule analia, baba mkwe akaja akaniuliza nalia nini nikamueleza kila kitu toka mwanzo alivyokua anidharau hadi akanipiga na muvi zake za ngono basi baba mkwe akaniambia

“Sasa utulie usubiri mwenzako akirudi ndio tuyaongee” Mimi nikakataa nikamuambia

“Baba haina haja ya kuongea nae ngoja tu alee mimba basi mi sitaki tena kuishi na mtu kama huyu” akanisihi pale baadae akaondoka.

Baada ya baba mkwe kuondoka ni kama nilishikwa na wazimu, nilienda hadi ndani kupekua kila sehemu nikakutana na picha ya mwanamke wake ipo kwenye fremu kabisa nikajikuta naumia mara mbili harafu alificha mbali mno.

Na kweli Yule mdada kwenye picha uongo dhambi alikua mzuri sana na kwa kipindi kile naweza sema kwake naingia mara tatu kwa uzuri wake.

Basi nikaanza kujishisi sifanani na mume wangu, Niliona kumbe anahaki ya kunidharau nilichanyanyikiwa balaa.

Baadae nikatoa laini zangu zote nikaacha pale ndani nikatoka nakuondoka sijui naelekea wapi (hapo nimepndwa na wazimu simpendi tena yani) maana hata njia sikuijua kabisa nilitembea mnoo na hapo sijala chochote toka asubuhi.

Baadae nikafika barabarani nikaendelea kutembea nikaona kabisa hapa napotea sikujali kikubwa kwangu nirudi Moro lakini nisione tena uso wa Mudy................ITAENDELEA……..

Usikose kufuatilia sehemu ya 12 KUJUA ELIZA ALIFIKIA WAPI BAADA YA KUONDOKA NA KWENDA ASIKOJUA? JE ATAKUA SALAMA NA UJAUZITO WAKE?

ANAENDA MOROGORO KWA MGUU KUTOKA KIBAHA JE INAWEZEKANA KWA MWANAMKE TENA MJAMZITO WA MIEZI 7?

“Kuna vitu vingi vya kumuomba mungu akubariki kabla hujamuomba pesa tazama eliza kapata mwanaume mwenye pesa, akitaka kwenda popote anatoka kwa gari lakini hana furaha, hapati mapenzi, na ujauzito anadiliki kuodoka bila kujua aendako mbali”

NUKUU “Sekunde moja ya kugombana na kutokuelewana ni SUMU KUBWA inayotufanya tusahau mamia ya mambo tuliyofanya katika MAPENZI YETU” Zingatia kujua thamani ya hisia za yule umpendae au uliyechagua kuishi nae.

JAMANI MWENDELEZO UPO UKIHITAJI NAKUPATIA TIME YOYOTE, CHAKUFANYA NITEXT “Naomba mwendelezo” KISHA NITAKUPA MAELEKEZO 0655 969 973
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 16
Man Middo Tz +255 655 969 973

Nilitembea sana hadi nikafika sehemu moja kuna fremu ni zile library za wanaouza na wanaokodisha CD pamoja na kuingiza nyimbo.

Nikaenda nilikua nimechoka vibaya mno maana tumboni vichomi, miguu nayo inauma balaa na mtoto tumboni amecheza mpaka akaacha, nilipofika pale nikaomba kuingiziwa nyimbo lakini nia yangu ilikua kupumzika tu nikaona tu nizuge kwanza pale.

Sikua hata na shida ya nyimbo niliomba nyimbo mbili akaingiza chap nikaona mbona huyu anataka nisipumzike nikamwambia bado niliendelea kumwambia aingize kila alipomaliza ili tu niendelee kupumzika.

Baadae alipomaliza na nilipoona nimepumzika kiasi flani nikamuuliza anielekeze njia ya kutokea barabarani. Basi akanielekeza nikafika barabarani, Sasa pale barabarani niliwaza kuwa

“Usiku huu nitaweza kweli kurudi kwetu harafu sijala toka asubuhi, si nitaumwa mimi na ujauzito huu harafu nimeacha laini kule”

Baada ya hapo nikaona nirudi tu kwa Mudy, Nikaanza kufuatisha barabara (Ila siku ile ningejua barabara mapema ningerudi nyumani kwetu) nilianza kurudi taratibu huku nawaza sana

“Kwanini huyu mwanaume haridhiki nimempa mahitaji yote ya kimwili lakini haridhiki”

(simaanishi kinyume na maumbile) namaanisha mapenzi ya kama wanandoa.
Niliwaza sana na kujiulaumu kuwa ningemsikiliza mama haya yote yasingetokea.

Baadae nikafika kwa Mudy nikakuta gari nje, nilistuka kwanza sikutaka kumkuta muda ule, nikajua tayari ashafika huyu nilipofika mlangoni nikakuta viatu vya watu wawili, nikanza kuwaza

“Huyu mwingine ni nani?”

Baadae nikasikia maongezi Mudy akiwa anajitetea

“Huyu atakua hajangalia vizuri, hii laptop hamna kitu kabisa yani amekosea tu kuangalia”

Kumbe alikua baba yake basi nikangia zangu kwa hasira nikawapita sebleni baba yake akawa anaita

“Mkwe ,mkwe njoo tuyajenge”

Sikujali nikaenda zangu hadi chumbani. Baadae Mudy akaja akaniambia

“Njoo tukaongee sebuleni baba anakuita”

Baba mkwe kweli alikua ananiita.Basi hata mimi mwenyewe nilihisi kaaibu kidogo nikatoka hadi sebleni nikakaa nilikua na hasira za ajabu hata kuongea sikuweza, Yani kama kuna kitu kilikua kinanikaba yani ilikua ni kwikwi tu nikitaka kuongea.

Nilikaa nusu saa nzima nikilia tu, baadae nilielezea kila kitu kwa baba mkwe Mudy anavyonidharau hajawahi kuniita hata mpenzi lakini nimekuta majina yote ya kimahaba nikamwambia kuwa

“Nilijua hajui kutamka kumbe yeye anadharau tu, mimi nimechoka nahisi mimba ndio imemponza ila nishajua nani anampenda ngoja mimi nikijifungua nitaleta mtoto amuoe amtakae” nilivyomaliza baba mkwe akamuuliza Mwanae

“Mudy umesikia hayo” Mudy akabaki kimya kichwa chini, mimi nikasema

“Nataka jibu narudi lini kwetu nimechoka!” Akaanza kusema

“NISAMEHE”

Kwa mara ya kwanza ndio aliweza kutamka maneno yale lakini sikufurahi nilitaka kujua lini nitarudi. Mudy akanza kusema

“Mimi sijafanya kitu ila ni kweli nimekosea, ila huyo mwanamke nimeongea nae kawaida tu!” Baba yake akasema

“Hebu acha ujinga, mimi nishasoma kabisa ujinga wako umekuja hapa umefuta, Sasa binti hamna kuondoka ila natoa onyo ni hivi hii laptop siitaki kwanzia Leo, Mudy chukua hii laptop kauze pesa zote mpe huyu binti kisha wewe binti hii pesa kwakua laptop alikua anaitumia kwa ujinga wake, sasa na wewe hiyo pesa usinunue kitu chochote humu ndani cha gharama wewe tumia tu utakavyo.

Harafu Mudy nimekuona sana ukimnyanyasa huyu binti unasafiri mwezi mzima wakati unajua mwenzio mjamzito unamsumbua hujali hali ya mwenzio, pia kama ulimpenda huyo binti wa kwenye simu si ungemuoa huyo kwanini unasumbua watu umetutoa hapa mpaka Morogoro vijijini kabisaa kule, si ungeoa huyo uliyemtaka kama ulikua huna nia ya kumuoa huyu ungesema”

Yani alimsema sana siku ile angekua wa kusikia angeskia……………….ITAENDELEA.

Yani huwezi kuamini alichofanya Mudy...

Usikose kufuatilia episode ijayo.

Mwendelezo Nitafute kupitia namba 0655 969 973. Whatsapp
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 17
Man Middo Tz +255 655 969 973

Basi kweli Mudy alienda kuuza ile laptop akaniletea pesa zote nikanunua dressingtable na begi la nguo, na nyingine zote nikatumia tu mwenyewe hapo angalau nikaanza kupata furaha na amani.

Na kwa kweli alianza kubadilika, kwanza aliawahi kurudi kazini na akirudi tulikua tunangalia muvi, muda wa kulala tunaenda wote hakuna tena ile kuchat na simu au ile kukaa sebleni na laptop.

Kwa kipindi kile hicho nikawa nampenda sana nilikua napenda kumchokoza michezo ya kimahaba ili tu asiboleke kukosa laptop yake, Na yeye pia alionyesha ushirikiano kwa kiasi kikubwa.

Basi miezi ilisogea ilipofika miezi 8 nikarudi nyumbani Moro Kama maandalizi ya kujifungua, Nilifika Moro nikaendelea kuhesabu siku na kwenda kliniki kucheki afya.

Siku ya kujifungua ikafika nikaenda hospitali ya kwaida nikaambiwa kwa umri wangu lazima niende hospitali ya mkoa niliogopa kidogo, lakini hakukua na namna nikaenda hadi hospitali ya mkoa.

Huko nako nikalazwa wakaniambia kwa umri wangu lazima kubaki pale kwanza ndipo niondoke nikiwa na mwanangu, nakumbuka nilikaa wodini wiki mbili peke yangu kabla ya kujifungua.

Mudy nilimuamwambia hali niliyokuanayo lakin hakuingiwa hata na moyo wa kuja kuniona pamoja na kumuomba aje alinipiga chenga mno niliumia sana hasa baada ya kuona wenzangu wanakuja kutembelewa na waume zao mimi hakuna hata mtu.

Kwani hata mama nae hakuruhusiwa kazini aliambiwa acahgue kukaa hospitali nikiwa sijajifungua au kuniuguza nikishajifungua, hivyo hakua na namna zaid ya kusubiri nijifungue.

Kwa kipindi kile mama mdogo nae alikua na matatizo yake binafsi kuna muda analeta chakula na muda mwingine haleti, mimi nilibaki tu nanunua chakula maana tuliruhusiwa kutoka kuchukua chakula kwa wale ambao hawana wasaidizi na pia ilikua kama mazoezi kumbuka hapo sijajifungua......itaendelea.

JE ELIZA ATAJIFUNGUA SALAMA? NANI ATAMPA MSAADA HAPO HOSPITALI AKISHAJIFUNGUA?

JE MUDY ATAKUJA AU BADO ATAPIGA CHENGA? BASI USIKOSE EPISODE YA 18.

Kama unataka episodes zote au ijayoo nicheki Inbox Man Middo au 0655 969 973 SIO LAZIMA KUONGOJA HADI NIKIPOST.

NUKUU “Hakuna Faraja Mwanamke Anaipenda Kama Ile Itokayo Kwa Yule Aliyeamua Kuwa Wa Maisha Yake, Hakuna Kitu Kibaya Kama Kuchezea Hisia Za Yule Anaekupenda. Mwanaume mwenzangu usomae hapa jifunze kumpenda mkeo kwasababu wewe ndio mfariji wake katika matatizo” Nyie mnaowadharau wake zenu kuweni makini.
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGUS
EHEMU YA 18
Man Middo Tz +255 655 969 973

Siku hiyo asubuhi uchungu ukanianza, hapo wiki ya pili sasa nipo hospitali basi nikapelekwa leba, Kwa kweli siku ile nilijifunza mengi na nilijua maana ya upendo ni nini maana niliwaza sana kuwa kumbe mama sio alikua ananipenda eeh! Kumbe Mudy ananidharau kwakua hana uchungu na mimi Dah! Kumbe mama alilia sana nilipopata mimba ya uzinzi.

Mama alilia sana nilipokonda ni kwasababu ya uchungu huu, kwa kweli siku ile nilijifunza namna ya kumpenda na kumheshimu mama.

Nilijua umuhimu wa mama, niliumia sana kipindi namjibu mama vibaya niliwaza sana huku uchungu unauma. Kwa kweli kujifungua kwangu kulikua kwa maajabu maana uchungu umenishika toka asubuhi nimekuja kujifungua saa 4 usiku tena baada tu ya kuongea na Mudy kwa simu huwezi amini baada ya yeye kupiga simu hapo hapo nikapiga kelele nikisema

“MUDY UNANIUAAAAA”

Hapo hapo mtoto huyooo nikaongezewa njia nikashonwa maana mtoto kichwa kilikua kikubwa kiasi, nilijifungua mtoto wakike.

**
Basi baadae nikaruhusiwa nikarudi zangu nyumbani kwa mama, nilitegemea Mudy angekuja kesho yake lakini akakataa kabisa yani, eti hadi aje na ndugu zake niliwaza huyu mwanaume anamatatizo gani. Kweli walikaa wiki nzima ndio wakaja, nakumbuka walileta kila kitu cha mtoto.

Mudy alifurahi sana alikua ananiangalia mara mbili mbili, ni kama alikua haamini kama nimemletea alichokua anakitaka. Siku hiyo walikaa siku nzima ilivyofika jioni wakaondoka.

Baada ya hapo maisha ya uzazi yaliendelea nikiwa kwetu mpaka ilipofika miezi mitatu nikarudi kwa Mudy sasa. Siku ambayo nilienda mama alinionya kuwa

“Mkajitahidi sio vizuri mkafika leo leo harafu mkafanya mambo yenu bila kinga mimba itaingia tena, kumbuka bado upo wazi jitahidi ukajizuie”

Nilimuitikia mama baadae nikasindikizwa na rafiki yangu mpaka kwangu nakumbuka Mudy alimtuma mtu hadi Moro kuja kutuchukua na tulipofika alikua kazini.

Usiku ulipofika alirudi alifurahi sana kumuona mtoto na ndugu zake ndo balaa mama mkwe na baba mkwe ndo usiseme ilikua furaha tupu hadi nikashangaa.

Muda wakulala ulipofika Mudy si akataka kunipalamia nikakumbuka mama alichoniambia nikasema hapa nikileta udhaifu tu nitaitwa mama tena baada ya miezi 9 mingine.

Basi nikamwambia leo hapana na hakua na kinga na hapendagi kinga nikamwambia subiri hadi nianze uzazi wa mpango alikubali kusubiri kesho.

Siku hiyo alikesha kumtazama mtoto mimi ndio nilikua na usingizi wa uzazi maana miezi 9 sio mchezo.

Basi Mudy alikua anamshangaa mtoto yani kama mshamba flani hivi. Kesho yake ikafika nikajiunga uzazi wa mpango basi ilipofika usiku alikua na hamu balaa maana alikua na papala mno.

Tukashirikiana kwa kuandana vizuri kucheza machi ya kimataifa naweza kuifananisha na mechi kati ya Simba na As Vita maana kila mmoja alitaka kufuzu robo fainali au Ile ya Yanga na Club Africain kule Tunisia, tulianza mechi vizuri mpaka tukatoana ugwadu wotee wa miezi mingi alijisifu sana siku hiyo baada ya kupata goli la ushindi dakika 89 basi akafuzu.

***
Tuliishi kwa furaha sana kipindi mtoto mdogo nilimjali alinijali tuliongea vizuri alikua anawahi kurudi kwajili ya mtoto maana alimpenda mtoto sana.

Kwa kweli akitoka kazini tu anamuogesha mtoto yani alikua ana upendo na mtoto sana alinijali alitujali huwezi amini kama atafanya mambo ya kinyoko. Basi mtoto alipofikisha miezi 9 yale mambo ya kinyoko yalianza upyaaaaa……… ITAENDELEA.

USIKOSE KUJUA MAMBO GANI YA KINYOKO MUDY ALIANZA? basi usikose kifutacho.

NUKUU “Kumbuka kama hujifunzi hapa basi hautajifunza tena, kama bado hujaoa au kuolewa jifunze hapa ni kipi hutakiwi kufanya ukiwa katika ndoa, sio kila kitu lazima upewe na kungwi”

Kama unaitaka yote au sehemu ijayo nicheki 0655 969 973
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 19
Man Middo Tz +255 655 969 973

Baada ya miezi 9 hiyo Mudy aliamua kunifungulia duka, kwa maana nisiwe mama wa nyumbani tu niwe najishughulisha.

Aliamua kumleta rafikiyake Godii ambaye amesema kuwa ndio ataweza kunilekeza mpaka nitakapojifunza ataniachia.

Mume wangu aliniambia kuwa atakaa wiki mbili lakini ikawa tofauti alikaa miezi mitatu kasoro, Baada ya wiki mbili kuisha nilimuuliza Mudy

“Mbona rafiki yako haniachii dukani?”

“Wewe unaharaka gani subiri atakuachia”

Sikubishana nae nikabaki kimya.Lakini Katika hizo wiki mbili hajawahi kunielekeza chochote yani kazi yangu ilikua kumpikia na kumpelekea chakula asubuhi, mchana na jioni.

Kwanza sikuona sababu ya kuelekezwa bei za vitu maana kila kitu nilikua najua reja reja na jumla nilijua maana maduka yaliyokuepo eneo lile nilijua bei zao na hazikutofautiana kwa chochote.

Baada ya mwezi mwingine kuisha nilimuuliza tena kwanini haniachii na pia hanielekezi chochote yeye alibaki kimya tu. Kwa muda huo kuna rafiki yangu aliniambiaga nitafute mtu tumwajili ili tusaidiane kwasababu ya mtoto dah!

Basi Yule rafiki yangu alikaa pale mpaka akaondoka maana Godii hakuonyesha dalii zozote zakuachia duka.

Niliendelea kumwambia Mudy kuwa naweza kubaki mwenyewe lakini hakuonyesha kujali kabisa.Kuna siku shem Afidh akamuliza Mudy kuwa

“Mbona dukani anakaa Godii kwani yeye hana kazi ya kufanya mbona anajibana kwa watu”

Na kweli hadi watu hapo mtaani walikua wanamshangaa kung’ang’ania dukani wakati mimi nipo, Mudy kama kawaida yake hakua na jibu lolote ni mzee wa kimya tu ukiuliza swala la Godii kukaa dukani.

Godii nilikua na mheshimu kama shemeji lakin nilianza kumpuuza kwakua alianza kunidharau, alianza kunipelekesha kama mkewe mara aulize

“Umepika nini?”

Mara akatae mboga niliyopika, mara asuse yani tafrani kila kukicha. Siku moja nikaenda kulalamika kwa wakwe kuwa Godii pamoja na kukaa dukani lakin ananidharau sana, nilisikilizwa tu na kuniambia watamuambia Mudy lakin wapi.

Sasa siku ziliendelea hivyo hivyo nikimwambia shida Mudy ananiambia kamwambie Godii yani hata iwe pesa ya kula kauli yake ni nenda kwa Godii, basi nikimwambia huyo Godii nae ananiuliza

“Pesa ya nini?” Nikisema kuna shida anauliza

“Shida gani?” Harafu anasema

“Mbona mimi hiyo pesa utakayo sina, mimi nina kiasi fulani tu” Yani ili tu anidharau.

Kuna kipindi Mudy ananidharau mbele ya huyo rafiki yake yani kitu kidogo tu anakuambia unanini wewe! Unajua nini wewe mwanamke! Nikawaza kuwa huyu ananidharau kwakua Mudy ananijibu hovyo mbele yake.

Godii alikua anajua kila kitu cha Mudy kudrive alitumia magari yote ya pale atakavyo, mambo ya pesa za Mudy benki yeye ndio alijua, biashara aliachiwa yeye yani kila kitu yeye alikua ni muamuzi yani hata huyo Mudy akiwa na shida ya pesa utasikia ngoja nimuombe Godii utafikiri Duka sio lake.

Akiwa mbali hata mkoani analalamika sina kitu nafikiria kumuomba Godii, yani nilikua naumia mno tena mno hasa ukizingatia mimi kama mkewe hanishirikishi kwenye vitu vya msingi.

Yeye anamshirikisha mtu baki tena hawana undugu wowote maana afadhali angekua mtoto wa mjomba yake au shangazi kidogo lakini yeye alipitiliza sana.

Basi Godii akaanza kuniachia dukani lakini ikiwa ana matembezi yake ndio huniachia kwa masaa anaenda nikiuza akija huku amenuna anauliza

“Umeuza kiasi gani?”

Namjibu harafu namkabidhi kisha mimi naondoka zangu. Ikaendelea hivyo hivyo baadae akanza kuniachia hata wiki lakini wiki ikiisha tu akija anakusanya pesa zote anasepa, baadae nikamuuliza Mudy kuwa

“Hivi Godii pesa zote anazokusanya yeye anapeleka wapi?” Nikaishia kuambiwa

“Wewe hujui mahesabu ngoja ujaziwe duka kisha uuze mwenyewe shida iko wapi?”

Niliumia ikawa ugomvi hauishi kila siku kisa GODII, yani kila nikikutana na Mudy lazima jila la Godii litajwe………………..ITAENDELEA.

Urafiki ni mzuri lakini usivuke mipaka kama huu wa Mudy na Godii.

Nitafute Whatsapp nikupatie mwendelezo
0655 969 973
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA 20
Man Middo Tz +255 655 969 973

Kuna siku ndugu wa Godii wakaja dukani kuchukua vitu kisha wakawa wanaondoka nikauliza

“Mbona mnaondoka harafu pesa hamjatoa?” wakajibu

“Godii anajua”

Harafu walijibu kwa dharau flani ivi, niliumia sana ikawa ndio mtindo wanakuja wanachukua nakusepa kama kwa kwao tu.

Duka likaanza kupukutika yani vitu vya juu kama vyakupendezeshea duka viliisha viibaki vya chini tu.

Kuna siku kuna mchele ulibaki harafu ulikua umeharibika haukua mzuri ila mimi nikajitahidi nikaupepeta nikamuambia Godii

“Huu mchele usiutupe kuna mtu nitaenda kumpatia”

Akaniitikia pale na pia nikamtaarifu Mudy kuwa kuna mchele nitauchukua pale hauko vizuri kwa kuuza, basi baadae naenda kuuchukua siukuti namuuliza

“Godii ule mchele uko wapi?” Ananiuliza

“Wa nini?”

“Nina shida nao” akasema tu jibu rahis kuwa

“Haupo”

Harafu Akakaa kimya niliumia sana, niliamua tu kuondoka maana nilitamani kumtusi lakin nikasema itakua lawama tu baadae, nilikuja kumwambia Mudy akanipuuzia tu kama kawaida yake.

****

Siku moja Godii aliniacha dukani alikua ameenda kwao, baadae alikuja mdogo wake.

Sasa kwakua mimi nalea nilikua ndani Yule mdogo wake aliita mimi sikusikia akaja binti akaniambia unaitwa dukani nikasema na nani akasema na mdogo wake Godii nikamuambia asubirie kidogo kwakua ni mwenyeji ili nimbeleze huyu mtoto na mtoto alikua analia kweli.

Basi baadae nikaenda kumhudumia ila kama kawaida yao hajalipa chochote akaondoka, Sasa baadae akaja Godii nilikua ndani pia kwakua sikua na binti wa kazi ilikua shida na sikuona haja ya kuwa na binti wa kazi kwani kipindi kile Godii hakuniachia duka, basi Godii akaja ndani nilikua jikoni akaniuliza kwa dharau na jaziba kaniuliza

“Mbona wewe unadharau sana” nikasema

“Dharau gani”

“Nimemtuma ndugu yangu hapa dukani harafu unamrudisha kwa dharau zako za hovyo tena kwa kumjibu hovyo hovyo unafikiri mimi silipii kama wewe na pia wakichukua naandika kama mteja mwingine tu”

(wakati kipindi hicho nilikua nakagua madftari yote hakuna sehemu aliyojiandika wala ndugu yake)

Nilibaki kumshangaa tu alivyokua ananizodoa aiseee sitakaa nisahauu nililia nililia sana kwa uchungu, kilichokua kinaniumiza ni kuwa Mudy hajanipa haki yoyote kama mkewe hadi kumfanya rafiki yake anaidharau kiasi hiki, rafiki yake ananichukulia tu kama binti wa kazi, Aisee yani pale ndio nilimchukia Mudy kabisaaa yani sikutaka hata kuongea nae kama zamani......ITAENDEEA

KAMA HUJUI YANAYOTOKEA KATIKA NDOA NYINGI BASI ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII. HUKO MBELENI NDIO INANOGA ZAIDI.

JE UNAFIKIRI MUDY AKIAMBIWA ATAJIBU NINI?

VIPI GODII ATAENDELEA KUWA MTAWALA KWA MUDY?

USIKOSE KIFUATACHO HAPA HAPA KWA GROUP LETU PENDWA?

NUKUU “Mwanaume uliyeoa tayari au ambae unatarajia kuoa, Kumbuka katika ndoa mkeo ni muhimu zaidi kuliko mtu mwingine, yeye ndo anajua udhaifu wako, yeye ndo anajua siri zako, yeye ndo anakuhudumia, yeye ndo ukiumwa anakuogesha na hawezi kukukatia tamaa,

NOTE! Jamaa mmoja alimnyanyasa mwanamke kwa miaka 8 kila mwanamke akimwambia wafunge ndoa jamaa anakataa huku akijidai kwakua amemzalisha watoto wawili hawezi kwenda popote na kweli alikua anampiga, kumdharau lakini mwanamke hakuwahi kwenda kwao, kila siku neno

‘NENDA KWENU KWANI UNAFAIDA GANI HAPA’

halikuacha kutoka kinywani mwake lakini siku moja mwanamke alichoka akaondoka na kumuachia mwanaume watoto. Jamaa amekaa na watoto kwa miezi mitatu tu, narudia miezi mitatu tuu akaanza kuhaha kumtafuta mwanamke akampata akanza kumuomba msamaha akimwambia siwezi kuishi bila wewe na siwezi kulea wale watoto peke yangu.

Mwanamke alibaki na msimamo akamwambia tayari nimepata kazi najihisi kuwa na amani sana kuwa na maisha yangu nazani ulisema sina faida yoyote pale kwako, hivyo nitakuja tu kutembelea watoto wangu siku nikipata muda. Huwezi amini jamaa alipiga magoti akilia kama mtoto akimuomba mkewe arudi lakin mwanamke moyo wake haukutaka kurudia ya nyuma’
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom