Simulizi:Death Of Innocent

Asante kivuruge wangu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Pole sana Alicia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapenda wazungu inawahusu

*NAWACHUKIA WAZUNGU*

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012, kipindi ambacho nilijiunga na Mtandao wa Facebook kwa lengo la kufahamiana na watu mbalimbali na kujenga urafiki. Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, nilifanikiwa kupata marafiki wengi wakiwepo Waswahili na Wazungu.

Nakumbuka kuna siku moja nilitumiwa meseji, ilitoka kwa msichana mmoja ambaye alikuwa mzungu, aliitwa Yusnir Abdulaziz, alikuwa na asili ya Kiarabu na alikuwa akiishi nchini Scotland.

Katika meseji yake, aliniambia kwamba alifurahi sana baada ya kuona kwamba ninakuwa rafiki yake, si kwenye mitandao tu, bali hata kwenye maisha ya kawaida, nikakubali na kuona zali, si unajua maisha yetu ya kimasikini unapopata msichana ambaye kidogo anaonekana kuwa na fedha, unaona kwamba umepata bahati kubwa.

Nilipokuwa nikiziangalia picha zake, kiukweli siwezi kukuficha, niligundua kwamba nilikwishawahi kumuona msichana huyu sehemu fulani ila sikuwa na uhakika ilikuwa wapi. Nilizoeana na msichana huyu, yeye mwenyewe, akaitaka kimapenzi, yaani tuwe wapenzi.

Kipindi cha kwanza sikuamini kabisa lakini akanihakikishia kwamba alikuwa akinipenda sana na hivyo alitaka niwe mpenzi wake. Sawa, nikakubaliana naye, hapo ndipo maisha ya kimapenzi na msichana huyu yalipoanza rasmi.
Nilimchukulia kama msichana wa mtandaoni huku nyumbani nikiwa na msichana wangu.

Katika kila kitu kilichokuwa kikiendelea, nilimpa taarifa kaka yangu, naye alionekana kufurahi sana ila akanionya kwamba natakiwa kuwa makini kwani anaweza kuwa tapeli, nikamwambia hakuna noma kwani mimi ni mtoto wa mjini hivyo asiwe na wasiwasi.
Baada ya kipindi cha mwezi mmoja wa mahusiano, msichana huyu akaanza kunitumia picha zake za chumbani na mimi kumtumia zangu. Alikuwa huru sana kwangu kiasi kwamba nikaona inawezekana alikuwa akinipenda kweli.

Mahusiano yetu hayakuishia hapo, akanitambulisha kwa watu wengine ambao alidai kwamba ni marafiki zake na wazazi wake, hakika nilifurahi mno kuwafahamu watu hao. Tukauendeleza uhusiano kwa kipindi cha miezi sita, hapo ndipo akaniambia kwamba alitaka kunitumia fedha kwa ajili ya matumizi yangu binafsi. Hivyo alihitaji akaunti yangu ya benki.

Kweli nilimpenda Yusnir lakini suala la kumtumia akaunti yangu lilikuwa gumu mno, iliwezekana vipi? Nitaamini vipi kama hakuwa tapeli? Nikamwambia kaka yangu juu ya hilo, akanionya kwamba sikutakiwa kufanya upuuzi kama huo.

Yusnir hakukubali, bado aliniambia kwamba alihitaji kunisaidia, hivyo nilitakiwa kumtumia akaunti yangu ya benki, nikaona sawa, nilichokifanya ni kwenda kufungua akaunti nyingine katika benki fulani hapa Tanzania na kisha kumtumia.

Baada ya wiki moja, kwenda kuangalia kwenye akaunti yangu, zilikuwa zimetumwa milioni kumi, hakika sikuamini, nikaona kwamba Yusnir alikuwa amepania kuyabadilisha maisha yangu, nikampenda zaidi.

Siku zikaendelea kukatika, tukapendana sana huku nikiendelea kula fedha zake kama kawaida. Mara kwa mara alikuwa akinitumia picha zake za utupu na mimi kumtumia zangu.

Baada ya miezi mitatu, akaniambia kwamba alitaka kuniona hivyo nilitakiwa kwenda nchini Scotland.
Nilimpenda sana na kumuamini, hivyo suala hilo halikuwa tatio.

Kwa sababu tayari nilikuwa na passport yangu, akanitumia kadi ya mwaliko hivyo sikupata tabu kwenda huko kwani hata nauli alinitumia, baada ya wiki moja, nikawaaga marafiki zangu kwamba ninasafiri kuelekea nchini Scotland, hivyo wasitegemee kuniona Tanzania hivi karibuni,ila kitu kilichoniumiza kichwa, sura yake haikuwa ngeni kwangu, nilikwishawahi kumuona sehemu japokuwa sikukumbuka ni wapi.

Ndani ya ndege, mawazo yangu yalikuwa kwa Yusnir tu, nilimshukuru Mungu sana kwa baraka alizoamua kunipa mimi masikini kutoka Tanzania. Saa nane mchana ndege ilikuwa ikitua ndani ya Uwanja wa Ndege wa Abardeen Dyce uliokuwa katika Jiji la Aberdeen.

Hali ya hewa haikuwa kama Tanzania, kulikuwa na baridi kali mno kwani mwezi huo ulikuwa ni wa kumi na mbili, mwezi uliokuwa na baridi kali maka theluji.

Tukashuka ndani ya ndege na kuelekea katika jengo la uwanja huo ambako nikakutana na mpenzi wangu niliyedumu naye kwa muda wa takribani mwaka mzima, Yusnir.

Alikuwa msichana mrembo mno, nilimkumbatia na kumbusu sana. Baada ya hapo, tukaingia ndani ya gari na kuondoka zetu. Tukafika katka mtaa fulani, sikumbuki jina lake, tukaingia ndani ya jumba moja kubwa na la kifahari ambapo ndani kulikuwa na watu wanne, wanaume wawili na wanawake wawili ambapo akanitambulisha kwamba wawili walikuwa ndugu zake na wawili wazazi wake.

Nikasalimiana nao na maisha yangu kuanza hapo nchini Scotland.

Kuanzia hapo nikawa karibu na mpenzi wangu, kila siku tukawa tunafanya mapenzi ila kitu kilichokuwa kikinishangaza, kila tulipotaka kufanya mapenzi, aliniambia ninywe viagra, dawa za kuongeza nguvu za kiume.

“Mbona ninazo nyingi tu,” kila siku nilimwambia hivyo ila hakutaka kunikubalia, nikaona kwamba siwezi kumkatalia mpenzi wangu, nikawa nakunywa na kufanya naye mapenzi, dawa zile zilinipa nguvu ya kufanya hata kwa saa moja.

Yusnir alipenda sana kufanya mapenzi nami, tulifanya sebuleni, bwawani na sehemu nyingine.

Katika kila hatua tuliyokuwa tukifanya, tulifanya kana kwamba tulikuwa tukiigiza, alikuwa akininyonya haapa na pale na mimi kufanya hivyohivyo.
“Kuna kitu nataka unisaidie mpenzi,” aliniambia Yusnir.
“Kitu gani?”

“Marafiki zangu wana matatizo.”
“Matatizo gani?”
“Hawapendwi hapa Scotand eti kwa sababu ni Wahindi.”
“Kwa hiyo?”
“Nataka uwasaidie kuwatimizia tamaa za miili yao.”
“Kivipi?”
“Ufanye nao mapenzi.”

Nafikiri unaweza kupata picha ilikuwaje hapo. Kwanza nilimshangaa, ilikuwaje nifanye mapenzi na marafiki zake hata kama walikuwa na shida? Hakujisikia wivu? Hakika nilishangaa sana.
Kwa kuwa nilikuwa nchi ya ugenini huku nikilelewa, nikakubali kufanya hivyo. Kazi ikaanza mara moja.

Wasichana hao walikuwa watatu, kila siku nilikuwa nikifanya nao mapenzi chumbani, kwa siku mtu mmoja lakini Yusnir hakutaka kuwepo nyumbani kwa kisingizio cha kutotaka kuona wivu.

Kama ilivyokuwa kwa Yusnir, hata kwa hawa nao walitaka nitumie dawa za kuongeza nguvu, mbaya zaidi wakanita niwaingilie mpaka kinyume na maumbile.
Hilo lilikuwa suala gumu sana lakini kutokana na kulazimishwa sana, nikawa sina jinsi, nikaanza mchezo huo huku nikiwa nimevaa mpira.

Maisha hayo yaliendelea kwa mwezi mzima, kila siku wale wasichana wakawa wakinipa paundi tu kitu kilichonifurahisha sana.

Baada ya kuishi kwa miezi miwili, muda wa kuishi Scotland ukafika tamati hivyo nikatakiwa kuondoka kurudi nyumbani.
“Hatuwezi kuongeza muda, nimepapenda hapa,” nilimwambia Yusnir.
“Nitakutumia barua nyingine ukifika nyumbani kwenu,” aliniambia.

Baada ya wiki moja nikarudi nchini Tanzania kuendelea na maisha. Kuanzia hapo, Yusnir hakuwasiliana na mimi tena. Nilipokuwa nikimtumia meseji, hakunijibu na mwisho wa siku akaniblock kabisa.
“Ignas,” aliniita rafiki yangu simuni.
“Sema kijana.”

“Ulikwenda Scotland kufanya nini?”
“Kumtembelea mpenzi wangu tu.”
“Acha uongo bwana, hata mimi unanificha na wkati kila kitu kipo wazi.”
“Siwezi kukuficha. Kuna nini?”
“Huwenda kuigiza pilau?”
“Hapana.”

“Unanidanganya. Ulikwenda kuigiza filamu za ngono bwana.”
“Kweli tena sikwenda kuigiza.”
“Mbona filamu zako naziona hapa! Nimezinunua kutoka….(akautaja mtandao)”

“Mimi?” niliuliza kwa kushtuka.
“Ndiyo. Njoo uzione.”
Nikachanganyikiwa lakini mwisho wa siku nikaona kwamba jamaa alitaka kunirudha roho tu, nikafunga safari na kuelekea kwake, nilipofika huko, akaniwekea hizo video.

Mungu wangu! Nilikuwa mimi, nkajiona nikifanya mapenzi na Yusnir na mwisho wa siku wale marafiki zake. Nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nikagundua kwamba kumbe wakati tukifanya mapenzi, kulikuwa na kamera zaidi ya tano chumbani zilizokuwa zikituchukua bila mimi kujua.

Nililia sana, sikuamini kama kweli niliingizwa kwenye kundi la waigizaji wa filamu za ngono bila kujua. Nilimtafuta sana Yusnir mtandaoni sikumpata. Nikagundua kwamba fedha nilizokuwa nimepewa ndiyo yalikuwa malipo yangu ya kufanya biashara ile inayowaingizia fedha kila siku.

Kuanzia siku hiyo, marafiki zangu wa Kizungu wote nikawafuta, video zile ziliendelea kusambazwa na ndipo nikakumbuka kuwa nilipomfananisha Yusnir, nilikwishawahi kumuona kwenye mikanda ya ngono.
Ninajuta, tamaa zangu ziliishia vibaya…mbaya zaidi, kwenye kila mkanda wa ngono kulikuwa na jina langu. Nilitamani kujiua.

*MWISHO.*
 
Dah, hili ni bonge moja la funzo kwa wapenda kitonga. Ila sitoshangaa wabongo wengine wakitamani wapate mawasiliano ya huyo dada[emoji2]

the Legend☆
 
Dah, hili ni bonge moja la funzo kwa wapenda kitonga. Ila sitoshangaa wabongo wengine wakitamani wapate mawasiliano ya huyo dada[emoji2]

the Legend☆
Hahahaha na vyuma vilivyokaza mtu hataogopa kitu
 
Kweli majuto ni mjukuu...


Chapter closed...


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…