Sehemu ya 13
Nilifanya vile makusudi ili mke wangu asibaini chochote kama kuna mambo yasiyo ya kawaida nimeanza kuyashitukia.
Jambo la mwisho nililofanya katika simu ile nilifungau faili lililoandikwa ‘Play store’, nikafungua, kisha nikapakua ‘program’ iitwayo ‘Voice recoder, nikaiseti simu ile kuwa inajirekodi yenyewe simu yoyote itakayokuwa inaingia na kutoka.
Baada ya hapo, nilitulia tuli, moyoni nikiweka nadhiri ya kulifuatilia jambo lile kimyakimya.
Muda mfupi badaye, mke wangu na nduguye walimaliza kupika, aliniandalia chakula, tukala wote pamoja. Wakati wote nilimwonesha tabasamu, sikumwonesha kama kuna kitu kisicho cha kawaida nimekibaini dhidi yake.
Baada ya mlo wa usiku, tulielekea chumbani mwetu kulala huku mdogo wake, Aisha naye akielekea chumbani kwake.
Tukiwa chumbani, kama kawaida tulipeana mapenzi motomoto na kama nilivyokwisha eleza awali, katika kipindi cha miezi sita, tangu nifungue usichana wake, mke wangu alikuwa mjuzi mno kitandani. Tulipeana mapenzi mazito hadi miili yetu iliporidhika.
“Ahsante mume wangu.” “…kwa?” “Penzi tamu, unajua sana kunikuna,” mke wangu alinambia baada ya kumaliza mmenyano. “Kweli?” “Sikudanganyi mume wangu.” “Lakini hata wewe siku hizi umekuwa fundi sana kitandani.”
“Mwongo.” “Kweli mke wangu, sijui nani amekufundisha.” “Nimefundishwa na wewe mwenyewe au umesahau?” “Nikumbushe.”
“Umesahau ‘ningali’ mwanamwali ulichonieleza?” “Nilikueleza vingi, kipi unachokusudia?” Kuhusu aibu.” “Alaa! Kumbe somo hilo.” “Ndio, siku hizi ninalifaulu kwa kiwango kikubwa, ndio maana unaona nimekuwa fundi kitandani,” alisema.
Tulizungumza na kufanyiana utani wa hapa na pale kisha usingizi mzito ukatuchukua. **** Ni asubuhi ya siku mpya, wingu la mvua lilikuwa limetanda, ngurumo za radi zilidhirisha uwepo wa mvua kubwa ambayo ingenyesha asubuhi hiyo.
Magari yalikuwa mengi barabarani, watu walikuwa wakihaha huku na kule kuhakikisha wanakuwa sehemu salama ili kujiepusha na kadhia ya matone ya mvua.
Ngurumo za radi zilizokwenda sambamba na miale mikali, ilifanya asubuhi ya siku hiyo kuwa nzito kwa wakazi wengi wa jiji la Dare es salam.
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilianza kunyesha, upepo ulikuwa ukizoa