Simulizi; Bahari ya Hindi

Bahari ya Hindi
Sehemu ya 16
Kule nje Malkia wa bahari akaanza kuhisi hali ya hatari,, akasema,, “bila shaka sehemu hii kunaadui yetu!
Pia Tobi akahisi harufu hiyo ya hatari… wakatoweka kimiujiza kutoka kwenye miili ya wana ndoa hao wawili!
Punde si punde wanandoa hao wakajishangaa, kujikuta hapo!
Wakaangaza angaza macho yao wakaliona gari lao! Mwanamke huyo akamuuliza mumewe,, “tumefikaje hapa? Mbonw kila nikivuta kumbukumbu sikumbuki kitu,, zadi ya kukumbuka kuwa tulikuwa nyumbani tumelala.
Punde si punde Roda akafungua mlango,, akashtuka kuwaona watu hao.. kisha akasema,, “karibuni.
Wanandoa hao wakatazamana usoni hawakuongea neno lolote wakaondoka zao na kuingia ndani ya gari kurudi nyumbani! Huku wakiwa wametawaliwa na hofu kupita kiasi!
Malkia wa bahari pamoja na Tobi wakajitokeza kwenye ufukwe wa bahari!
Pia jua lilikuwa tayari limeanza kuzama hivyo mpango wao ukashindikana.. wakatoweka kimiujiza kurudi ujinini kule chini ya bahari!
/
Wakati huo huo kule nyumbani kwa Roda alionekana bado akiendelea kumsimulia,, yule nesi mkasa wote uliompata.. nesi huyo akamuonea huruma sana,, kisha akasema hili ni tatizo usipokuwa makini utampoteza mtoto,, kwa sababu ni lazima waje kumchukua mtoto wao!
Kisha nesi huyo akanyanyuka na kumuaga Roda,, akamrudishia mtoto wake!
Roda hakuwa na kipingamizi,, akaongozana na nesi huyo mpaka nje ya nyumba..nesi akaondoka zake Roda akaelekea kanisani kwa mchungaji… kwa bahati nzuri akamkuta mchungaji,, anatoka kwenye ofisi iliyokando ya kanisa lake.
Roda akamsalimia mchungaji,, kisha akasimulia mkasa mzima..
Bila kuchelewa mchungaji akasema,,” tuingie kanisani,, wakaongozana mpaka ndani ya kanisa,, Mchungaji akasema,, “mlaze mtoto huyo hapo juu ya meza.. nianze maombi.
Roda akafanya kama alivyoagizwa na mchungaji, akamlaza mtoto pale juu ya meza.
Mchungaji akaanza kufanya maombi……akiwa katikati ya maombi.. mtoto akaanza kulia kwa sauti kali kupita kiasi akaanza kubadilika na kuwa mtoto wa kutisha… punde si punde ukatoka mwanga mkali ndani ya mwili wa mtoto huyo… akarudi katika umbile lake la kawaida.. mchungaji akaendelea kufanya maombi kwa imani kali nila kusita.
Na baada ya dakika kadhaa kupita mchungaji akahitimisha kwa kusema,, “Amen.
Mtoto akanyamaza,, kisha mchungaji akasema,, “sasa waweza kwenda lakininusisahau kusali mara kwa mara,, usisahau kumkumbuka Mungu wako!.
Wakati huo Roda alikuwa kabaki mdomo wazi juku macho yamemtoka akimtazama mtoto wake,, yani alikuwa aamini kile alichokishuhudia… mchungaji akasema,, “ondoa shaka Mungu yu pamoja nawe,, ukimuamini na kumtumikia yeye atakulinda kwa kila jambo..kisha mchungaji akazipiga hatua akachukua biblia moja na kumkabidhi Roda huku akisema,, “mara kwa mara jifunze kusoma maandiko ya kwenye biblia…..utajifunza mabo mengi ya kumtumainia Mungu muumba.
Roda akaipokea biblia hiyo kisha akamchukua mwanae.. na kuondoka zake kurudi nyumbani!
**************************************
Upande mwingine kule ujinini, alionekana,, Malkia wa bahari pamoja na Tobi…
Malkia wabahari akasema kwa lugha ya kijini akimaanisha,, “ tumechelewa na jua limeshazama! Kule duniani usiku umeanza kuingia ambavyo huku kwetu ndio panaanza kukucha,, hivyo tutaifanya kazi hii kesho,,
Kama ilivyo kawaida viumbe wa kuzimu,, wanaishi tofauti na maisha ya binadamu!
Huku duniani,,nyakati za mchana,, lakini huko kuzimu ni usiku wa manane..
Na huko kuzimu nyakati za mchana,,,, huku duniani ni nyakati za usiku wa manane..
Kesho yake mipango ukaendelea wakajipanga kwenda duniani kumchukua mtoto wa Roda wampeleke ujinini.
Kule nyumbani kwa Roda alionekana yupo sebuleni akiwa anasali kwa imani huku kashikilia biblia.. alipomaliza akaingia jikoni kuandaa chakula wakati huo mtoto alikwa kalala usingizi juu ya sofa.
Punde si punde Tobi na Mama yake(Malkia wa bahari akasema wakajitokeza ndani ya nyumba ya Roda upande wa sebuleni,, wakastaajabu kumuona mtoto haonekani kuwa na chembechembe zozote za ujini! Malkia wa bahari akasema bila shaka hapa kunajambo limetendeka! Haiwezekani iwe hivi.. punde si punde mtoto akashtuka kutoka usingizini akaanza kulia,, Roda akatoka jikoni haraka kuelekea sebuleni.
Akashtuka kumuona Tobi pamoja na Mwanamke mzee sana ambaye ndiye
Mama Tobi(Malkia wa bahari) Roda akakumbuka maneno ya mchungaji,, kuwa afanye maombi kwa imani mara kwa mara,
Bila kuchelewa Roda akaanza kusali huku akikemea kwa imani.. Tobi na Malkia wa bahari wakaanza kuhisi wanaunguzwa na moto mkali,, walipojaribu kutoweka kimiujiza ikashindikana.. wakaanza kupiga kelele za maumivu makali!
Roda akaendelea kusali bila kusita.. punde si punde wakaanza kuwaka moto.. hatimae wakateketea kabisa na kubaki majivu… ikawa ndio mwisho wa Tobi ma Malkia wa bahari.
Roda,,akamchukua mwanae haraka akambeba.. kisha akaichukua biblia na kuikumbatia.
Akaamua kufanya mpango wa kuhama ndani ya nyumba hiyo siku hiyohiyo.. akahamia Temeke,,
Siku zilizidi kusonga,, Roda hakuona mauzauza tena.. akaishi kwa amani na furahmiaka ikazidi kusonga hatimae mtoto akatimiza umri wa miaka kumi na nane(18) binti huyo anaitwa
SIMA. /
Roda akashindwa kuvumilia kuificha siri kwa mwanae.. kwa sababu kila kukicha binti huyo alimuuliza mama yake kuwa baba yake mzazi yuko wapi… Roda akamsimulia mkasa wote… binti huyo akastaajabu sana,, lakini akajipa moyo kwa kumtumainia Mungu… huku akijisemea moyoni,, “Mungu ndiye muweza wa yote,, amenileta duniani kwa namna hii,, MUNGU ndiye baba yangu pekee.
Maisha yaliendelea,,wakaishi kwa amani na furaha.
******************MWISHO******************

Safi sana...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom