Mbona huyo ndio bonge la wifi? Wanawake hatuna jema, angekuja akapita kila mahali huko jikoni ungesema anaharibu bajeti. Mie wifi zangu tunapendana kweli. Manake nikienda kwa kakangu nachangia stori na kuangalia tv! Na mgeni anaekaa tu hanipunguzii wala kuniongezea. Unaingia kwa watu unajipeleka jikoni unapika kuku, kumbe kuku wao kwenye friza anapikwa jumapili tu! Si ugomvi huo!
cha kufanya bi shosti asubuhi muulize wifi unajiskia kula nini? Kama hakipo muombe mumeo, muambie wifi ana hamu na kuku, naomba hela. Mbona utapendwa kote kote? Mnashindwa ndoa wenyewe!
Nitakwenda Mars kutafuta muke aiseeeee!!!!!!!
Heshima ikurudie pia kaka....!!!!!!!
Kaka ambao hamjaoa ombeni sana mpewe wake wema waliojaa busara !!!!!!!
Hahaaaa duuuh
Kaka ambao hamjaoa ombeni sana mpewe wake wema waliojaa busara
Tatizo wapo wachache na waoaji tupo wengi!!
Hapo maombi yanashindana,ukipewa galasa ulie na moyo wako!
Ndoa ni kazi ngumu ila lazima tuifanye!!
Wee usitafute ugomvi nae mwache tu akae, mwisho atajistukia mwenyewe ataondoke ama ataanza kufanya kazi!
Yaani angekuwa na tabia kama yako au!!!?????
Matusi hayaruhusiwi...................................😛hoto:😛hoto:
[/B]Yaani sijui kama kuna tusi ambalo lingetosha!
Nimecheka tu!!!
Mi kwa kweli jikoni kwangu ndiko ufalme Wang ulipo.naamini hivyo hats nikienda kwa mtu.
Unless uniambie njoo tupike.
Kila nyumba na kila mwanamke ana namna yake ya upishi.
Sitegemei mdada analilia mtu kuingia jikoni kwake.