Habari zenu wadau wa MMU
Kwa mara ya kwanza naingia jukwaa hili kuomba ushauri juu ya kile kilinikuta;
Mnamo mwaka mmoja na kitu umepita nilikuwa home tz kwa bahati mbaya au nzuri nikagongana na mrembo flani mitaa ya hapo kati'kwa kweli nilivutiwa nae sana na kwa sababu nilikuwa katika mchakato wakutafuta jiko nikaona si vibaya nikifungua nae ukurasa mpya wa mapenzi,kwa kweli kwa muda mfupi tulizoeana kwa sababu likizo yangu haikuwa ndefu nikaondoka, lakini nilishamueleza dukuduku langu lote kama nahitaji mke.
Basi kadri siku zinakwenda tuliendelea na mapenzi yetu, Huyu bint hakuwa natabia ya umalaya laa,ila alikuwa Selfish'anapenda afanyiwe kila kitu kizuri yeye. Basi mwaka huu mwezi april nilikuja tena likizo tz ya miezi 2 na kitu,basi kadri nilivyokaa nae huyu ndio nikagundua kuwa kweli Selfish,mbinafsi sana hakupenda mimi nikae na ndugu yeyote kama ingetokea nikamuowa,yeye alitaka tuishi wawili tu,kwakweli hilo lilinishinda ikabidi nimwambie ukweli kuwa sitaweza kuishi nae,nikaamua kuvunja ule uhusiano wote kila mmoja akashika njia yake.
Sasa hapa swala limejitokeza kama wiki 2 zimepita mimi huku ng'ambo naishi na mtoto wa baba yangu mdogo anafanya kazi,na yule my X anamfahamu hata kipindi niko nae walikuwa wakiwasiliana kwa kuchat,Sasa hapa kuna swala moja limetokea huyu mdogo wangu na huyo my X wanachat sana sana'mpaka saa 8 usiku,yule bint anamtumia mdogo wangu mapicha kibao,hapa nashindwa kufaham nini kinaendelea,ila mdogo wangu nimeshampa warning juu ya huyo bint kwa sababu she was my gf anajua,lakini nahisi hanielewi.
Khofu yangu nahisi kutokea mgogoro mkubwa kati yangu na mdogo wangu,kwa sababu mimi ndio nilimleta hapa na kazi nikampa nafikiria nimrudishe tu home tz ili wakutane vizuri huko,hebu niishie hapa naombeni ushauri wenu,maana nina mengi yakuandika naona ntawachosha kusoma.