Simuelewi mke wa mpangaji mwenzangu

Simuelewi mke wa mpangaji mwenzangu

Gwele

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2016
Posts
2,761
Reaction score
3,510
Mimi ni kijana niliyeanza kujitegemea baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikajifunza fani fulani mtaani ambayo kwa sasa inaendesha vizuri maisha yangu

Mwezi wa nne nilipanga chumba hapa mjini na niliwakuta wapangaji watatu wawili wakiwa wameoa na mmoja single kama mimi.

Baada ya kukaa kama wiki moja mke wa jirani yangu alinifuata na kuniambia shemu kuna suala la usafi wa choo na mazingira kwa ujumla hivyo nilitakiwa kushiriki au kuwapa wao hela waweze kunisaidia kama ntakuwa bize basi nilijifikiria japo sikuwa bize sana niliamua tu niwape hela nikatoa elf 30 nikampatia nikaona kashtuka kidogo akashukuru na kuondoka

Siku iliyofuata nikiwa sina hili wala lile yule mke wa mpangaji mwenzangu alinigongea asubuhi mume wake akiwa kaenda kazini akanikaribisha chai huku akisisitiza si vizuri kwa mimi kujipikia kila kitu hadi chai ambayo anaweza kuwa anapika tu kwan asubuhi hubaki peke yake mumewe akiwa kazini (fundi ujenzi) nilikataa kwa siku hiyo lakini jioni nikiwa ndani alinigongea tena akiniambia alikuwa anaosha vyombo na hivyo kama nilikuwa na vyombo vichafu nimpatie anisaidie nikampatia bila hiyana akaosha na kuniletea

Juzi aliniomba namba yangu akisema si vizuri kuwa nyumba moja bila mawasiliano akidai mume wake anakosa nafasi ya kuniomba namba hivyo ameamua achukue ampatie cha ajabu asubuhi alituma meseji nying akinichombeza kuwa tunaweza kutoka kwenda beach fulan hapa mjini kiutani nikajifanya kumuitikia ili asijisikie vibaya.

Usiku wa jana amenitumia mesej akisema kesho lazma tutoke nami nikashtuka kuona yupo serious nikamwambia si vizur kwan ni mke wa mtu na muda huo mumewe angeweza kuziona chat zake lakn akasisitiza kuwa hakuna tatizo kwani mumewe sio muelewa na muda wote yupo bize na mikazi migumu na hurud amechoka kama guruwe kuona mesej hiyo nikaacha kujibu txt zake akawa anatuma nyingi nyingi mimi nikawa kimya na leo asubuhi nimetoka mapema asubuhi amenitumia txt et mbona umekimbia chai yangu gwele leo, mara vipi ule mtoko jamani.

Yaani nimechanganyikiwa sijua nifanyaje nataman kuhama lakin kodi yangu ya miezi iliyobak inaniuma halafu pia mwenye nyumba wa hapa ni muelewa sana na mazingira ni mazuri lakin kiukweli sina amani hapa namuheshimu kijana mwenzangu ndoa yake haina hata mwaka mmoja na bado hawajabahatika kupata mtoto lakini huyu mwanamke ananiweka majaribuni mno japo kiukweli ni binti mzuri hata sikudhani kama kweli ameolewa katka maisha kama yale.
 
Kwakushtuka kwake baada ya kumpa hiyo elfu 30 ilikuwa ni dalili tosha kwamba "yajayo yanafurahisha".

Fanya ufanyavyo lakini elewa mke wa mtu sumu, kwahiyo kama majaribu yakikushinda, jua tu siku ukikamatwa huna wa kumlaumu zaidi yako mwenyewe. Na wanawake wengine ni wepesi sana kujisahau hasa wakinogewa na penzi la nje. Kwahiyo watch out!
 
Kwakushtuka kwake baada ya kumpa hiyo elfu 30 ilikuwa ni dalili tosha kwamba "yajayo yanafurahisha".

Fanya ufanyavyo lakini elewa mke wa mtu sumu, kwahiyo kama majaribu yakikushinda, jua tu siku ukikamatwa huna wa kumlaumu zaidi yako mwenyewe. Na wanawake wengine ni wepesi sana kujisahau hasa wakinogewa na penzi la nje. Kwahiyo watch out!
Hilo ni muhimu au kumchimba mkwara
 
Back
Top Bottom