Simuelewi jirani yangu

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,659
68,626
Hii familia wapo watatu mke na mume na mama wa mke na mtoto mmoja.

Mwanzoni mke nikimsalimia aliitikia ghafla akawa haitiki salamu yangu, nikasema poa nikajikataa, nikaacha kumsalimia.

Wana tabia ya kukaa ndani sijui wanafanya kazi saa ngapi wote watatu wanatoka nje kwa nadra sana mpaka nikiikumbuka stori ya BIG ya Steve mollel naogopa, mmoja akitoka ni mafurushi tu mama mkwe hajawahi toka kabisa nje ya geti na hatujui alikuja lini hapo tulishangaa tunamuona tu.

Nikiwa Sipo home wanatoka nje wanakaa nikishinda home hawatoki kabisa wengi wanajua pale hakuna mtu maana muda mwingi wanajifungia.

Nikienda ghafla nikawakuta nje wanaingia ndani haraka au wakiniona wanajificha haraka sijui shida nini, shida imeanza nakuwa namuota huyo mwanamke anaingia ndani kwangu kama anatafuta kitu hivi anakuja hadi chumban kwangu ni mara mbili namuota, sikumuambia mtu.

Leo mtoto wangu kamuota huyo mwanamke ambae ni mke wa jamaa anaingia ndani kwetu ila akashindwa kuingia mlango wa jikoni nikamuambia ni ndoto wala hakuna kitu.

Hatuchangii umeme wala maji sijui shida nini.

Kuna sisy kaja kunitembelea walimuita wakamuambia wanajua siku yake ya kufa aende wakamuombee ndani kwao hakuenda kuombewa tukawapeleka kwa mwenyekit wakaomba radhi tukasamehe na kuna kingine kimetokea sitakisema. Sisy ananiambia mchana wanachoma udi sana ule wenye harufu kalii.

Kama wanataka nihame wala sihami na sina mpango waje tu ilimradi wasinichubue hata damu.

Nawaza tatizo sioni upande wangu sijui nimewakosea nini.
 
Ntarudi baadae kidogo..
Haya mambo ya "supanachuro" yanahitaji kujilipua.
Wakiwasha udi, wewe unawasha ndum a.k.a ganja. Au hauko Arusha mama la mama?
Screenshot_20230610-183215_Quora.jpg
 
Ukitaka kuishi kwa amani na watu wa aina hiyo wewe jifanye haujali wala hujui kinachoendelea kwenye maisha yao. Wanachokifanya ni wao kutaka kupata attention yenu alafu iwe rahisi kuwaingiza kwenye jambo lao na mwisho wa siku muwe wahanga wa kutapeliwa au vinginevyo
 
Hii familia wapo watatu mke na mume na mama wa mke na mtoto mmoja
Mwanzon mke nikimsalimia aliitikia ghafla akawa haifiki salam yangu nikasema poa nikajikataa,nikaacha msalimia,
Wana tabia ya kukaa ndani sijui wanafanya kazi saa ngapi wote watatu wanatoka nje kwa nadra sana mpaka nikiikumbuka stori ya BIG ya Steve mollel naogopa ,mmoja Akitoka ni mafurushi tu mama mkwe hajawah toka kabisa nje ya geti na hatujui alikuja lini hapo tulishangaa tunamuona tu
Nikiwa Sipo home wanatoka nje wanakaa nikishinda home hawatoki kabisa wengi wanajua pale hakuna mtu maana muda mwingi wanajifungia

Nikienda ghafla nikawakuta nje wanaingia ndani haraka au wakiniona wanajificha haraka sijui shida nin,shida imeanza nakuwa namuota huyo mwanamke anaingia ndani kwangu kama anatafuta kitu hivi anakuja hadi chumban kwangu ni mara mbili namuota,sikumuambia mtu ,leo mtoto wangu mkamuota huyo mwanamke ambae ni mke wa jamaa anaingia ndani kwetu ila akashindwa kuingia mlango wa jikoni nikamuambia ni ndoto wala hakuna kitu
Hatuchangiu umeme wala maji sijui shida nin
Kuna sisy kaja kunitembelea walimuita wakamuambia wanajua siku yake ya kufa aende wakamuombee ndani kwao hakuenda kuombewa tukawapeleka kwa mwenyekit wakaomba radhi tukasamehe na kuna kingine kimetokea sitakisema
Sisy ananiambia mchana wanachoma udi sana ule wenye harufu kalii

Kama wanataka nihame wala sihami na sina mpango waje tu ilimradi wasinichubue hat damu
Nawaza tatizo sion upande wangu sijui nimewakosea nin
Kwani wao wamekukosea nini?

Wewe endelea na maisha yako na wao waache na maisha yao.

Usiwachunguze.
 
Acha kufuatilia maisha ya watu fanya mambo Yako, tatizo ni kwamba unaonekana unaamini sana mambo ya kishirikina na kwakuwa akili yako kutwa nzima umewekeza huko ndio maana unakuja kuota usiku ndoto za ajabu, maana nijuavyo ndoto ni mjumuiko ya Yale yanayotawala ubongo wako kabla ya kulala.

Umenikumbusha kuna mpangaji mwenzangu anaishi na mama yake ambaye anaamini sana issue za kishirikina basi chochote kinachomtokea anahusisha ulonzi tu sasa juzi alikuwa anaanika nguo kwenye kamba Ile kamba ikawa inakatika Kila anapoweka nguo zake ila alikuwa anaifunga tena, kamba ilikatika kama mara 3 hivi, Ile ya tatu nikamsikia anamwambia wife. " Hapana hii sio dalili nzuri haiwezekani kamba ikatika mara 3 zote hizo", akachukua simu kumpigia mganga wake amwelezwe shida ni nini ahahahaha!! sasa mtu kama huyu hana tofauti na ww.
 
piga sala sana kula kitimoto kama ni mlaji sana na kama ikiwezekana tukua kisosi weka mkaa na wewe choma cha arusha kama udi uone kama hamtakuwa majirani wema, kama mbwai ni mwai tuu daadeki.
 
Acha kufuatilia maisha ya watu fanya mambo Yako, tatizo ni kwamba unaonekana unaamini sana mambo ya kishirikina na kwakuwa akili yako kutwa nzima umewekeza huko ndio maana unakuja kuota usiku ndoto za ajabu, maana nijuavyo ndoto ni mjumuiko ya Yale yanayotawala ubongo wako kabla ya kulala.

Umenikumbusha kuna mpangaji mwenzangu anaishi na mama yake ambaye anaamini sana issue za kishirikina basi chochote kinachomtokea anahusisha ulonzi sasa juzi alikuwa anaanika nguo kwenye kamba Ile kamba ikawa inakatika Kila anapoweka nguo zake ila alikuwa anaifunga tena, kamba ilikatika kama mara 3 hivi, Ile ya tatu nikamsikia anamwambia wife " Hapana hii sio dalili nzuri haiwezekani kamba ikatika mara 3 zote hizo akachukua simu kumpigia mganga wake amwelezwe shida ni nini ahahahaha!! sasa mtu kama huyu hana tofauti na ww.
Siamin 😂😂 kwanin wamuambie ndugu yangu atakufa wao nani???
 
Back
Top Bottom