Simuelewi huyu mwanamke

Deva

JF-Expert Member
May 29, 2018
1,238
1,801
Habari za asubuhi wakuu.

Kwanza nianze na mtiririko wa matukio.

Asubuhi nimeenda kwenye shughuli zangu,nikawasiliana naye vizuri tukaagana kama ilivyo kawaida ya wapenzi wengi, jioni nimetoka kwenye shughuli, nikampigia simu tukawasiliana vizuri nikamuambia kuwa nimechoka sana ngoja nijipumzishe lisaa limoja hiyo ilikuwa saa 12:30 jioni, akasema haya basi tutawasiliana kesho, nikamuuliza kesho? Kwanini iwe kesho na ninajipumzisha lisaa limoja tu? Hakujibu akakata simu, nikamtumia sms kwamba nalala lisaa limoja, akanijibu usiku mwema, hiyo ilikuwa saa 12:30 jioni, sikuijibu.

Nimeamka lisaa limoja baadae sikumtumia sms tena maana niliona kama ananizuia nisiwasiliane naye, hapo hatuna ugomvi wowote, nikawa namuona tu online whatsapp, ila sikumtafuta maana alinionesha dalili za kunikwepa kwa siku hiyo, nikajiongeza labda ana mood mbaya, nikampa uhuru kidogo, sikutaka kulazimisha mawasiliano, mida ya saa tano usiku akanitumia sms ya usiku mwema nikamjibu asante, siku ikawa imeisha hivyo.

Kesho yake asubuhi nikampigia sinu kumjulia hali hakupokea na sms hakujibu, basi nikaenda kwenye shughuli zangu, niliporudi nikamtafuta tena, nikakuta simu ipo busy nikamtumia sms kuwa akimaliza anitafute, ila hakunitafuta, muda ulipopita mwingi nikamtafuta mimi, nikazungumza nae kidogo akasema nikate, anataka kuzungumza na mtu kwenye simu, nikasema sawa ukimaliza nitafute, hakufanya hivyo, na mimi nikakaa kimya mpaka pale alipokuja kunitumia usiku mwema, nikaijibu asante, siku ya pili ikawa imeisha, tatizo halijulikani ni nini.

Kesho yake akaamka akihitaji tuachane, nikauliza sababu ni nini, akasema mimi namdharau, simuheshimu wala simthamini namchukulia wa ziada tu, tulivutana kwa muda nikijaribu kumuelezea mahali anapokosea, hakukubali, nilimueleza dalili zote na yote aliyokuwa anafanya, mimi siwezi kulazimisha mawasiliano, pale aliponikwepa nilikaa kimya.

Matokeo yake ni tumeachana, kwa yeye kunilaumu mimi, mimi nimeshafanya kinachonipasa kufanya, maana sidhani kama ningeweza kuendelea kumsumbua mtu anayenitakia usiku mwema saa 12 jioni, na story yetu ya mahusiano ikaishia hapo.
 
Alitaka useme we we kuwa muachane lakini ulichelewa.
Mshukuru sana Mungu kwa kuachana nae kwa maana kulazimisha penzi ni kutafuta kifo.
Nilikuwa kwanza mpole mkuu ili nione kilichomo kwenye akili yake.
 
Ni kweli mkuu maana malalamiko yalikuwa mengi sana yasiyo na ukweli wowote.
Kuna vitu vyaweza kuwa vidogo sana kwako ila kwa mwenzio vina maana sana, wakati mwingine tunapowalalamikia mtuelewe jamani na sio kuchukulia ni ujinga.
 
Kweli humjali, wewe kumpigia simu mpaka utoke kazini ? Ukiwa kazin kunashindikana nini ? Halafu inaonesha ulikuwa huna cha kuongea nae zaidi ya salamu .Bora alivyokuacha unampotezea muda. Mawasiliano ni jambo la msingi katika mahusiano.
Nimefikiria the same, mtoa mada yawezekana haoni makosa yake na analazimisha tu bibie ndio amuelewe, sidhani kama alichukua muda wake kumuelewa mwenzie.

Alisense something is wrong ila wala hakujali kufuatilia ni nini ili wayaweke sawa. Hapa naona yeye ndio alimchoka mwenzie akawa anamtafutia sababu.
 
Mwanamke akipata mwanaume mwingine ndo anakuwa hivo hasa km anajisikia guilt kuachana na wewe bila sababu...

Piga kimya hawajui wanataka Nini...nakuahidi atarudi mwenyewe hata km itapita Miaka 10.
 
Bro,nimesoma vzr,Huyu demu inaonekana ile siku ulivyo mwambia unataka upumuzike kwanza baada ya kutoka job alihisi kama uko ma demu mwingne,japo hataki kukuweka wazi ila nahis hicho ndo chanzo,Chamsingi acha kumtafuta ovyo ovyo uta onekana kama unajipendekeza na kuzid kukuletea jeuri,Pia nahis Anaweza akawa kapata mwanaume mwingine na hyo akawa anataka kuifanya kama sababu ili muachane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom