Simu zitakazopata android 5.0 aka lollipop

Simu zitakazopata android 5.0 aka lollipop

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,062
Reaction score
43,478
Tukiwa tunakaribia mwisho wa mwaka na manunuzi ya simu yanazidi kuongezeka makampuni mbalimbali yameanza kutangaza list ya simu zao zitakazopata hii update ya pipi ya kijiti. Nimeamua kuweka list ya simu zitakazopata hii update kwa pamoja ili ukienda kununua simu ujue unanunua simu gani ili baadae ipate hii update na kuondoa kero ya kununua simu kila siku.

Sony xperia
Sony wao wametangaza simu zao zote zinazoanziwa na herufi Z basi zitapata update ya lolipop hii ina include hadi simu kama xperia z, z ultra, zr na zl ambazo ni za toka mwaka 2013. Hivyo kama una plan ya kununua xperia inayoanziwa na herufi z au unamiliki simu kama hiyo usiwe na wasiwasi utapata update yako muda ukifika.

Motorola
Motorola amefurahisha wengi kwa kutoa update hii kwa karibia simu zake zote, hii ni list ya simu zake zitakazopata hii update

1.moto x zote ya mwaka jana na huu
2.moto g zote za mwaka jana na huu
3.moto e
4.droid ultra
5.droid maxx
6.droid mini

Inafurahisha kuona simu kama moto E inapata hii update kulingana na bei yake ilivyo rahisi.

HTC
HTC yeye ameconfirm simu nne tu ndio zitapata lolipop ambazo ni

1.htc one m7
2.htc one m8
3.htc one mini
4.htc one mini 2

LG
1.lg g3
2.lg g2

Asus
1.zenfone zote
2.padfone infinity
3.padfone s
HTCone m7 na m8 zitapata update hii ndani ya siku 90 toka ilipotangazwa hii update.

Hao ni manufacture watatu wameshatangaza, wengine wakiongezeka nitaupdate list.
 
Samsung haina haja ya kujitangaza wao kama ilivyokuwa ktk kitkat kuanzia s4 nadhani zitapata update hio
 
Moto g naweza kuipata duka gani hapa dar na shilingi ngapi?
 
Ngoja nitulie na ZR yangu, kumbe sitapitwa na tecnolojia.
 
Features za hiyo 'Lollpop' na manufaa yake kwa handset yangu ni nini. What's noticeable or beneficial to a common user if they upgrade to lollpop?
Can you weigh, for us here, the benefits of upgrading vs not upgrading to lollpop?

Shukrani
 
Na Kampuni yetu ya Tecno itaaupdate model gani, phantom?
 
mchapafito

Uhuru wa mtu mwache alopoke tu...ndio uhuru mkuu.lkn mwisho wa tutajua ukweli
 
Last edited by a moderator:
Na Kampuni yetu ya Tecno itaaupdate model gani, phantom?

Tecno mpaka ununue simu nyingine itakayokuja na update hiyo...mimi nilikuwa na phantom A+ mizinguo mingi niliuza hamna mambo kama hizi anasema Chief mkwawa
 
Features za hiyo 'Lollpop' na manufaa yake kwa handset yangu ni nini.
What's noticeable or beneficial to a common user if they upgrade to lollpop?
Can you weigh,for us here, the benefits of upgrading vs not upgrading to lollpop?

Shukrani

Zipo kibao ila niliyoipenda ni kill switch. Itadhibiti wezi wa simu sana. Pia chaji ya simu itaongeza kukaa kwenye simu. Security updates kila baada ya wiki sita. Sasa ivi utakuwa una upgrade via google play badala ya kudownload update au ku update via kies kwa samsung na wengine kwa update software zao

Zipo faida kibao. Pia muonekano mpya unavutia kuliko wa mwanzo.
 
Na Kampuni yetu ya Tecno itaaupdate model gani, phantom?

Tecno inabidi kununua simu mpya. Afadhali hata huawei zitapata. Na i hope hata hizi za tigo zitapata maana niliona y300 ina 4.4.4 kitkat
 
samsung haina haja ya kujitangaza wao kama ilivyokuwa ktk kitkat kuanzia s4 nadhani zitapata update hio
Mwe! ina maaa sie wenye simu vibabu (S2,S3) tuendelee kupiga kodo vijana(s4 ++) wakibadilisha sura na mwendo?
 
Mie cjui maana ya technological terms kama hizi jamani: jelly bean,kitkat,CPU,RAM,ROM,1.2GHz/1.3GHz,cjui 3G,2G,4G n.k
Wataalam kina chief Mkwawa and the like p'se nisaidieni make jf darasa tosha.
Aksanteni.
 
Moto g naweza kuipata duka gani hapa dar na shilingi ngapi?
Nimeangalia maduka mawili ya mjini kati sijafanikiwa kuona hii simu na motorola nyingine mpya. Inaonekana kama watanzania wengi hawazijui sana, tofauti na brand za samsung, iphone na htc. Hata kupata simu kama lg g2 maduka ya kawaida ilikuwa shida sana. Ukipata taarifa tujulishane
 
Alcatel wametutumia message kuwa tusiwe na hofu SIMU zetu zitawezeshwa kupokea hiyo update SIMU yangu ni Alcatel pop c9
 
samsung haina haja ya kujitangaza wao kama ilivyokuwa ktk kitkat kuanzia s4 nadhani zitapata update hio

mi mwenyewe nafkiria hivyo hivyo nahisi safari ya note 2 imefika kitkat na s4 kupanda ndio zitapata lolipop
 
Back
Top Bottom