Simu zipi ni nzuri kati ya Xiaomi, OPPO na VIVO?

Simu nzuri UI mbovu, ladha mbovu kwa mtumiaji,hakuna spare na ngumu kuuza so mi nahamia oppo
MIUI sio mbovu. MIUI ni nzuri lakini jua tu MIUI sio kwa kila mtu, na ColorOS nayo sio kwa kila mtu.
Mi nitaeleza kidogo tu kwa uelewa wangu juu ya UI ya Oppo (Color OS) na UI ya Xiaomi (MIUI)
*ColorOS ni UI smooth ambayo haina features nyingi. Features zake ni chache sana inakaribiana na Stock Android. Hii inawafaa watu ambao hawahitaji features nyingi na wanahitaji smooth experience kutoka kwa hii cleaner UI. Mimi sipendi software yenye features chache, ColorOS sio kwa ajili yangu. Sio kila mtu anapenda simple OS.
*MIUI ni UI yenye features nyingi sana na sio smooth kama ColorOS. MIUI ina features nyingi, mitindo tofautitofauti kwenye user interface, tajiri wa themes, pia MIUI inapambwa sana na rangi-rangi kuliko ColorOS. MIUI ni heavy kama One UI ( ya Samsung) lakini Xiaomi anaziba hii issue kwa kutumia stronger chipsets hadi kwa simu zao za bei rahisi. Hii software ni kwa ajilli ya watu kama mimi na wengine wanaopenda software zenye features nyingi. Pia MIUI ni more battery efficient kuliko ColorOS.
Na kwa upande wa hardware Xiaomi yuko vizuri kuliko Oppo.
 
Kuna model za Xiaomi Zinamkalisha iphone&Samsung

Kuna model za Samsung Zinamkalisha iphone

Kuna model za iphone Zinamkalisha Xiaomi

Kila simu Zina ubora wake kulingana na model Zake Xiaomi ni brand inakuja Juu sana ukiachana na iphone Samsung,Google pixel
Broo nikusahihishe sio inakuja ishakua juu leo zaidi ya mwaka wa nne top 3 inakuepo kaka ni laana na nusu nazipenda xiaom tena nina hamu sana na hii Os yao mpya ijayo tune feature matata zaidi na zaidi
 
Xiaomi nunua ikiwa mpya lakini usijiroge ukafanya system update au update ya kwenda android inayofuata utatamani uhamie Infinix tu.
Mbona Mimi nimefanya system Apdate na bado Inachapa mwendo kama Kawa, Tena ni Xiaomi ya kawaida sana, ila naogopa kuiroot ili kupata Toleo jipya, yaani kwa hapa kwa KUWA watumiaji ni wengi naomba kujua waliojaribu kuroot bado inakuwa katika ubora wake?
 
Back
Top Bottom