Simu zangu zina shida gani? msaada tafadhali

Evelyn Salt

Platinum Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
77,673
Reaction score
167,735
Wazima humu?
Nilikua na simu aina ya tecno, nimeitumia baada ya muda ikaanza kuleta manotification mengi mara battery sijui imekuaje ni update niki click update inanipeleka kwenye play store ni install, niki install inaleta tena zingine yani ni kila dakika...
Sahivi natumia tecno nyingine na yenyewe imeanza hizi notifications, shida ni nini? Nifanyeje?
Screenshot_2015-11-28-09-35-19.png
Screenshot_2015-11-28-09-38-45.png
Mfano wa notification ni hizi
 
Itakuwa uliweka app ambazo sio za playstore, ndo zina tabia hiyo, kama kuna apps hazina umuhimu kivile hukuzipata playstore zitoe tu. Jitahidi utumie zilizokuwa verified na Google hizo nyingine ndo huwa zinaleta virus kama hizo otherwise nikuitie Chief-Mkwawa
 
Last edited by a moderator:

Mbona hata sina hizo app? So nifanyeje kuondoa hizi mambo
 
Solution ni Ku root simu yako...mm mwenyewe ilikuwa hivo kwa techno yangu....techno ni janga Dada....ila sasa limeisha ilo tatizo...ilikuwa kero kila second
 
Nakushauri ui-reset tu, ama ulifanya hivyo ikarudia
 
Wazima humu?
Nilikua na simu aina ya tecno, nimeitumia baada ya muda ikaanza kuleta manotification mengi mara battery sijui imekuaje ni update niki click update inanipeleka kwenye play store ni install, niki install inaleta tena zingine yani ni kila dakika...
Sahivi natumia tecno nyingine na yenyewe imeanza hizi notifications, shida ni nini? Nifanyeje?
View attachment 308574
View attachment 308575
Mfano wa notification ni hizi

hizo ni ads zinakuwepo kwa apps wakati unatumia mtandao

cha msingi kule juu kulia kuna alama ya x means close, kila ikija ad we close ukiclick inakupelekea ku install malwares

hata kama nitakwambia your phone is running out of space or battery low don't click

kuna apps ambazo ni ad blocker waweza install pia

na kuna kulipia kwenye app kuzuia ads

hiyo ni biashara
 
Usijidanganye ku-root hiyo simu kama mtu moja hapo juu alivyosema, you don't need to root your phone huku there's nothing technical ambacho unataka kufanya, rooting iache kwa watu wanaopenda kuchokonoa simu zao. Na aliyesema reset simu pia usimsikilize simply because ukireset ukarudisha the same applications still tatizo litakua palepale sanasana utakua umepoteza tu muda kufuta all your apps na kuanza upya.

Hizo ni ads tu, matangazo yanayojaa fullscreen yanaitwa "interstitial ads", swala ni angalia hiyo app unayoitumia either usiitumie uifute, coz am sure hayo matangazo yanatokea ukifungua app flani, tafuta alternative application isiyo na hizo interstitial ads au kama ni ya kulipia basi uilipie kuondoa ads, solution nyingine kama app haihitaji internet basi ukitaka kuifungua take down the net, sababu ads zinaload only when there's internet.

Wanaotengeneza haya matangazo kua "simu yako ina tatizo flani, click kulisolve" hua ni njia tu ya kufanya watu mclick matangazo yao, wewe cha kufanya ukiyaona weka "x" ufunge tu, hizo apps kama umeziinstall kama hiyo "Clean Master" ifute, hizo apps kusema zinasaidia kusave battery au ram au anyother thing hua ni fix tu, reality ni kwamba they don't do anything. Android OS yenyewe inafanya yote hayo automatic vizuri tu.
 
Simple ndugu!
Hizo ads una zuruhusu mwenyewe kwa kujua ama kutokujua,
kivipi?
----> Pale unapoanza kutumia simu at very first time hua unaambia kuweka google email either new ama existing,
---->Ukiweka hiyo email hua kunatoke msg ikikwambia je ungependa kupokea updates from google store?,uki click ok baadae ndio unapata msgs kama hizo
---->Ili kuondoa hizo msgs and other blahs,reset your ili uweze kuweka email upya kudisable hzo notifications..
Kila la kheri
 
Solution ni Ku root simu yako...mm mwenyewe ilikuwa hivo kwa techno yangu....techno ni janga Dada....ila sasa limeisha ilo tatizo...ilikuwa kero kila second
Kuroot hata sijui ndo kufanyaje mweh ushamba mzigo
 
hizo ni ads zinakuwepo kwa apps wakati unatumia mtandao

cha msingi kule juu kulia kuna alama ya x means close, kila ikija ad we close ukiclick inakupelekea ku install malwares

hata kama nitakwambia your phone is running out of space or battery low don't click

kuna apps ambazo ni ad blocker waweza install pia

na kuna kulipia kwenye app kuzuia ads

hiyo ni biashara

Kuiclose tu haisaidii, natamani ziondoke kabisa make zinainterfere, nikisikiza mziki yakija hayo mziki unastop ni kero sana
 
Jinsi ya ku ‘root’ simu yako ya Android.

Utangulizi:
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika Mawasiliano, Kuhifadhi kumbukumbu za muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program ambazo huwekwa kwenye mfumo wa simu (Operating System). Programu hizo hubeba maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji kufanyia mambo mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti), Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji wa Simu au Computer ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi yake. Katika miongo michache iliopita zimetengenezwa program nyingi mpya na zenye maboresho makubwa na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika program mbalimbali unaleta ukuaji katika Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia zimeleta urahisi na ufanisi. Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na Kuran), Kamusi, Camera, nk.. vyote vimetengenezewa PROGRAM na kuwa rahisi kuvitumia katika simu muda wowote, mahali popote.
SASA TUJE KWENYE MADA;
Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake. Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho;
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda Settings – About phone – Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara! kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!! Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni. Sasa watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT’ kua ni kuifanya simu ikubali Program zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers). Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.
JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.
Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root, SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root, Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa kutumia Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya simu za Android. Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha I isearch na kui download. Kwa msaada uliza……

Maandalizi:
(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%
(ii) Wezesha ‘’Developer Options??� kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer??�
(iii) Sasa nenda Settings>eveloper options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)
(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa download KingRoot 4.0 (in MB 6.34) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is unavailable’. Chini gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!

--

Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this Device??� HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!

FAIDA ZA KU ROOT SIMU:
1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila kuwa rooted!
2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.
3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano (performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root

ZINGATIA:
Rooting inaweza kuharibu kabisa kuharibu simu yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote) Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki zangu zisizopungua 20 bila madhara yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..
Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’

HITIMISHO:
Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno H6, baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzima!!
 
Simple ndugu!
Hizo ads una zuruhusu mwenyewe kwa kujua ama kutokujua,
kivipi?
----> Pale unapoanza kutumia simu at very first time hua unaambia kuweka google email either new ama existing,
---->Ukiweka hiyo email hua kunatoke msg ikikwambia je ungependa kupokea updates from google store?,uki click ok baadae ndio unapata msgs kama hizo
---->Ili kuondoa hizo msgs and other blahs,reset your ili uweze kuweka email upya kudisable hzo notifications..
Kila la kheri

Oooh thanks, nahisi basi shida ipo hapo niliruhusu kupokea notification, so na reset email kwenye Google? Ngoja nifanye hivo nione
 
Thanks pia NullPointer Ila mi nataka ziondoke kabisa sio tu kuclose
 
Last edited by a moderator:
Thanks pia NullPointer Ila mi nataka ziondoke kabisa sio tu kuclose

Nasikitika kusema huna jinsi, hiyo app unayotumia developer kaweka matangazo hayo kama njia ya kumpatia pesa, hakuna jinsi ya kualter software yake isionyeshe matangazo coz yeye peke yake ndiye mwenye key ya kuruhusu au kublock matangazo, kama hajakupa option ya kununua ili yasitokee basi labda usiitumie hiyo app utafute nyingine yenye functionalities sawa na hiyo isiyo na hayo matangazo..

Zaidi ya hapo utapoteza muda tu kukomaa na mambo ambayo watu watarecommend ufanye ukifikiri yatatoka ila nothing will work, mwisho wa siku utajikuta hadi unaformat simu for nothing, nimedevelop android apps nyingi tu kwa hiyo najua exactly kilichotokea.
 
upo sahihi mkuu

me nimejaribu kumwelezea juu juu kama wewe Ila ni same content

watu hawana uelewa wa vitu tunalalamika ni tatizo Kumbe ni jambo la kawaida
 
Nasikitika kusema huna jinsi, hiyo app unayotumia developer kaweka matangazo hayo kama njia ya kumpatia pesa, hakuna jinsi ya kualter software yake isionyeshe matangazo coz yeye peke yake ndiye mwenye key ya kuruhusu au kublock matangazo, kama hajakupa option ya kununua ili yasitokee basi labda usiitumie hiyo app utafute nyingine yenye functionalities sawa na hiyo isiyo na hayo matangazo..

Zaidi ya hapo utapoteza muda tu kukomaa na mambo ambayo watu watarecommend ufanye ukifikiri yatatoka ila nothing will work, mwisho wa siku utajikuta hadi unaformat simu for nothing, nimedevelop android apps nyingi tu kwa hiyo najua exactly kilichotokea.

Sorry leo ntakuchosha kwakweli, unavosema labda nisitumie hii app, unamaanisha app ipi au browser nnayotumia?
 
Jinsi ya ku ‘root’ simu yako ya Android.

Utangulizi:
Simu zetu za Android zimekua sehemu ya Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika Mawasiliano, Kuhifadhi kumbukumbu za muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program ambazo huwekwa kwenye mfumo wa simu (Operating System). Programu hizo hubeba maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji kufanyia mambo mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti), Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye simu, bali hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji wa Simu au Computer ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi yake. Katika miongo michache iliopita zimetengenezwa program nyingi mpya na zenye maboresho makubwa na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika program mbalimbali unaleta ukuaji katika Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia zimeleta urahisi na ufanisi. Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na Kuran), Kamusi, Camera, nk.. vyote vimetengenezewa PROGRAM na kuwa rahisi kuvitumia katika simu muda wowote, mahali popote.
SASA TUJE KWENYE MADA;
Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake. Haya ni Matoleo (Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho;
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
Matoleo haya huboreshwa kadri yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda Settings – About phone – Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara! kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!! Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni. Sasa watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT’ kua ni kuifanya simu ikubali Program zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android Developers). Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.
JINSI YA KU ‘ROOT’ SIMU YAKO.
Kuna aina za simu ni rahisi sana ku root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root, SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root, Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa kutumia Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye asilimia kubwa ya simu za Android. Program hii haihitaji Computer. Kuipata nenda Google kisha I isearch na kui download. Kwa msaada uliza……

Maandalizi:
(i) Charge Simu yako, angalao ijae kwa 50%
(ii) Wezesha ‘’Developer Options??� kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida. Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer??�
(iii) Sasa nenda Settings>eveloper options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama haipo)
(iv) Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
Hapo maandalizi yatakua ni tayari. Sasa download KingRoot 4.0 (in MB 6.34) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android 4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is unavailable’. Chini gusa ‘START ROOT’. Hapo KingRoot itakua inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!

--

Ili kuhakikisha kama simu yako imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this Device??� HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!

FAIDA ZA KU ROOT SIMU:
1. Utaweza ku update toleo la mfumo wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila kuwa rooted!
2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni Cerberus.
3. Utakua na uwezo wa kuweka Program nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano (performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root

ZINGATIA:
Rooting inaweza kuharibu kabisa kuharibu simu yako na kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote) Usiogope, hii huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot simu yangu na za Marafiki zangu zisizopungua 20 bila madhara yoyote kutokea. Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..
Pia Rooting inaharibu Warranty ya simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo, ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’

HITIMISHO:
Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno H6, baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzima!!

Asante kwa elimu Ku root smartphone. Nikidandia Uzi,Nina Huawei ascend y600,nikiiwasha inatoa Logo tu haifiki kwenye menu, nakuanza kupata joto mpaka naamua kutoa betri.kuna wakati naibahatisha ina waka na inafika kwenye menu,ila ukigusa Apps hazifunguki japo internet inakuwepo.nimefanya hard resert lakini hakuna suluhu.ina mwezi mmoja tu.unanishaurije hapo?
 
Back
Top Bottom