Simu za mkopo

Habari ndugu ninaomba kuuliza kama kuna uwezekana wa kufungua sehemu ya laini mama kwenye hizi simu za mkopo ili hiyo sehemu ambayo huwa ni laini namba 1 iweze kutumika kwa laini yoyote kama umeshamaliza deni!

ahsante.
Kufanya hivyo ni kukiuka mashariti ya mkopo ambayo uliyakubali na ukasaoni kuwa umeyakubali

Kuwa makini usije ukafingwa
 
Mkuu kwan hizo simu mnakopa barabarani? Si uwafuate ofisini ulikochukulia
Siku hizi mpaka road wanakopesha kama malaya wanafunga tent sijui gazebo hata mpita njia unakopa kigezo kianzio na NIDA.
 
This is interesting. Sikuwa najua ni kwa namna gani hawa jamaa wanaweza kucontrol simu yako endapo ukadefault mkopo wao. Nilihisi labda wanaiblock simu kupitia imei number. Kumber its a software wana install na kuipa admin privelledge.


Sasa nataka kujua, hakuna namna unaweza kuiby-pass iyo software..either by flashing the smarthphone au kwa kuinstall custom rom?
 
Zinaflashiwa vizuri tu ila wanaoflash wanakuwa wagumu sana wanaogopa kuchomeshwa labda mpaka akujue.
 
Habari ndugu ninaomba kuuliza kama kuna uwezekana wa kufungua sehemu ya laini mama kwenye hizi simu za mkopo ili hiyo sehemu ambayo huwa ni laini namba 1 iweze kutumika kwa laini yoyote kama umeshamaliza deni!

ahsante.
Wasailiana na waliokukopesha Ina maana umewasahau
 
Hai

Haitamsaidia chochote
Bonyeza *#06# tuone kama zipo imei mbili, tuanzie hapo, kama hazipo mbili hawezi kupata mtandao

Najadili na wewe mimi kama fundi simu
Am not closed minded, please be advised to learn about MDM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…