Wana JF, Salaam!
Katika pitapita yangu weekend iliyopita nilikuta mjadala mahali kuhusu matumizi ya simu za kiganjani - mobile phones. Mjadala hasa ulikuwa kuhusiana na utunzaji wa kumbukumbu za simu za wateja hususani utumaji na upokeaji wa SMSs au text messages. Kulikuwa na hoja kuwa rekodi ya matumizi ya simu ya mteja wa mtandao wowote hapa nchini sio siri na ni jambo ambalo linaweza kutumiwa vibaya na maadui zako kwa maana ya kwamba hakuna privacy katika jambo hilo. Inasemekana kuwa print out ya rekodi za simu na sms zinapatikana unapohitaji kwa bei fulani fulani. Pia mjadala huo uliishia kwa kusema kuwa kuna baadhi ya simu, mfano Blackberry ambazo haziweki rekodi ya simu au meseji ambazo unapiga, kutuma au kutumiwa.
Endapo hayo mambo hapo juu yanatendeka, basi huo itakuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mteja. Naomba tujadili hoja zifuatazo:
1. Ni kweli kuwa simu na meseji zote hurekodiwa na kutunzwa na kwa muda gani?
2. Privacy ya mteja wa simu inalindwa vipi na makampuni ya simu?
3. Sheria gani ya nchi inamlinda mteja wa simu katika eneo hili?
4. Je kuna mtu yoyote amewahi kuathirika na hili na alichukua hatua gani?
5. How serious is the problem?
Wasalaam.