Wafanyakazi wa kampuni moja ya ndege nchini India walilazimika kutumia kifaa cha kuzima moto ili kuizima simu aina ya Samsung iliyokuwa ikifuka moshi
Simu hiyo ya Note 2 ilikuwa ikitoa miale ya moto kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni ya ndege ya Airline Indigo
Hatua hiyo ya haraka ilichukuliwa na wafanyakazi hao ilisaidia ndege hiyo kutua salama katika uwanja wa ndege wa Chennai, ikiwa ndo lengo la safari hiyo.
Kisa hicho kimetokea wakati ambapo Samsung inazirudisha simu aina ya Note 7 kutokana na matatizo ya berti
Indigo imesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa kisa hicho katika ndege ya 6E-054 iliokuwa ikitoka Singapore kuelekea Chennai.
[emoji2] unakumbuka enzi za I phone 6 plus kupinda????.Mmmh...sijui kama hivi ni vita vya kibiashara au vipi...juzi nilisoma mahali namna hivi karibuni simu Samasung galaxy ilivyolipuka kwenye gari na kuharibu gari aina ya pick up ambaye alikuwa ana-charge...mwenye gari hakuwemo kwenye gari wakati simu hiyo inalipuka lakini gari hilo liliharibika vibaya sehemu ya mbele...picha ya tukio hilo ilionyeshwa...
Kweli kabisa,hawa jamaa simu zao bomu sana sema tu watu hawajui bado.Lianguke tu maana wanatufanya ngazi yao kufika katika maendeleo yao ..!
Ila tafadhari usitaje tecno huu mtaa.Kweli kabisa,hawa jamaa simu zao bomu sana sema tu watu hawajui bado.
Ni nyingi mno mkuu na kuzitofautisha fake na original ni ngumu sana labda uwe mtaalamuNa fake nyingi sana ni Samsung
Acha kupotosa mkuu. Aina ya gari ilikuwa ni Jeep. Ungeziona hizo picha ungetambua hilo. Ila kwa kuwa amekuhadithia meku kwenye kijiwe cha kahawa na wewe umekuja kutumwagia fleva humu.Mmmh...sijui kama hivi ni vita vya kibiashara au vipi...juzi nilisoma mahali namna hivi karibuni simu Samasung galaxy ilivyolipuka kwenye gari na kuharibu gari aina ya pick up ambaye alikuwa ana-charge...mwenye gari hakuwemo kwenye gari wakati simu hiyo inalipuka lakini gari hilo liliharibika vibaya sehemu ya mbele...picha ya tukio hilo ilionyeshwa...