Juzi kati Dada mmoja ameaibika mbele ya wakwe zake, kisa meseji ya mapenzi kaikuta kwenye simu ya mme wake, kisa kamili jamaa baada ya kushtukia mke wake huwa anakagua simu yake akiiacha na hukagua kwa kificho jamaa asijue, jamaa akaamua kujitumia msg, kwenye simu yake ili kujiridhisha na mchezo wa mkewe, Msg"" hny ur so swt , U have crazy sex in real, I enjoyed alot," jamaa alisevu no yake mwenyewe kwenye simu yake kwa jina la Mwana, baada ya kutoka job aliiacha simu na kwenda bafuni baada ya kwenda bafuni tu Mke kama kawa akaichukua baada ya kusoma msg hiyo toka kwa Mwana,alikimbilia kwa Mama mkwe huku akilia na kudai bora apewe taraka maana mme wake si mwaminifu huku, akiwa ameshika simu na kumwonyesha msg Mama mkwe , jamaa alikuwa bafuni alipotoka akakuta mtafaruku huo, baada ya kuhojiwa na Mama yake akawashangaza baada ya kuwaambia angalieni no ya simu ya mtu aliyetuma hiyo msg ni ya nani? wote walishikwa na Butwaaa kuona ni no yake mme wake mwenyewe, Ungekuwa wewe mwana JF ungemshauri nini huyu Mwanamke aliyekurupuka,,,,,?