Simu ya milioni moja, usafiri wa bajaji, bodaboda au daladala

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
60,502
Reaction score
139,545
Naomba nieleweke,sina tatizo na mtu kutumia bajaji/bodaboda/daladala, mimi mwenyewe huwa nashika bomba kwenye daladala na mara nyingine natumia bajaj....sasa nielezee nini kimenifanya niandike hii mada.

Mwezi mmoja hivi uliopita nilikwenda kumpitia mpenzi wangu kwake. Wakati anapanda nilimuona ana simu mpya samsung galaxy s5! Anafanyakazi na sitaki maswali kaipataje! Huyu msichana anafanyakazi ya kawaida, hana gari usafiri wake ndio huo daladala/bajaj/bodaboda au nimpitie na gari.

Wakati niko nae kwenye gari alikuwa busy sana na hiyo simu yake na mimi nilikuwa nimefungua vioo halafu mitaa yetu ya uswazi, nikamwambia hiyo simu watachukua wenyewe muda si mrefu lakini akawa anaendelea tu basi mimi nikapandisha kioo upande wake.

Katika mazungumzo yetu nikamwambia sasa hiyo simu ya gharama hivyo na wewe unapanda daladala au bajaji si utakuja kuibiwa upate hasara.

Akanitupia jicho kama naongea kichina. Baada ya siku tatu tu yuko ndani ya bajaji anascroll screen yake wajanja wakachukua simu kama yao 1.2 Million gone in 2seconds.

Wiki iliopita nimekwenda nyumbani kumsalimia bi mkubwa. Kuna mdogo wangu wa kike wa mwisho, ameanza kazi kama miezi mitatu iliopita nikamkuta ana NOKIA LUMIA sijui, likubwa hivi kama s4.

Nikamwambia simu nzuri lakini na unavyorudi kutoka kazini peke yako mida ya usiku [saa moja hadi mbili] huoni hatari na hio simu ya milioni sijui laki nane?

Kama kawaida nikapewa jicho fulani kama naongea kichina. Leo nimepigiwa simu wajanja wamempora simu, handbag wakiwa kwenye bodaboda yeye anatembea kwa miguu again 1M gone in 2secs.

Dada zangu kuweni makini na hizo simu zenu za mamilioni, kuwa na kitu cha milioni au zaidi halafu unatembea kwa miguu au unapanda bajaji ni hatari.

Ni sawa na kutembea unaning'iniza tsh 1M au zaidi begani. Wezi wanakufuata mpaka wanapata sehemu nzuri wanachukua hiyo simu kama yao.

Siwakatazi kuwa na hizo simu lakini kuweni makini, nishashuhudia wanawake wanaburuzwa na wezi wa simu wanaotumia bodaboda. Sijazungumzia wakaka kwa sababu wanaweza kujitetea kwa njia moja au nyingine na hata wezi mara nyingi wanawa-target akina dada na akina mama.
 
Seeing can be deceiving.....sio kila unaemuona na simu za gharama basi ametoa. Kweli milioni kununua hiyo simu...hii nchi mipango mipango mno...kuna simu za dili nyiingi sana..mi naweza kukwambia wanaolipia milioni Tanzania kununua simu wako very few but wanaomiliki 'simu za milioni' wako weeengi sana...nyingi clones..
 
Umeniwahi....nilitaka kusema mostly hizo simu ni knockoffs....

Maisha ya kibongo bongo nani anaweza kumudu kununua simu genuine ya shilingi milioni moja!?

Hivi hujawahi kujiuliza inakuwaje designer clothes kama za Burberry, Gucci, LV, na kadhalika zipo zimezagaa mitaani ilhali hakuna maduka yanayouza designer products kama hizo?
 
uko sahihi kabisa....lakini waangalie usalama wao,kuwa na simu ya milioni na zaidi[hata kama umepewa] halafu unakaa madongo kuinama usafiri bodaboda bajaji ni hatari kwako
 
Very true ni hatari...but zipo simu vibaka hawazipendi na nzuri tu..so labda wa avoid popular brands...kuna simu hazina majina but very good still
 
yani nisinunue simu ya bei kubwa kisa sina gari binafsi! kuibiwa kupo tu popote pale na ktk mazingira yoyote, sasa M1 inatosha kununua gari? halafu nna wasi wasi na hizo shuhuda naona kama za kupikwa.
 
Daah umenigusa niliibiwa sim wiki moja toka niinunue tena kwa kubana kamshahala kangu

Nililia had basi

Ila nmepata somo la kutokutumia sim njian
 
true....
 
Tell them....

Girls think big when it comes spending... saving to them is like showing them the way to guantamo!

I like chagga girls... they rock when it comes to saving and future life in general..
 
umesoma mada vizuri....wala sijasema usinunue coz huna gari nunua tu ay your own risk hela si yako....kuhusu ushahuda kama unaona wa kupikwa sawa.....inaonyesha unakaa ndani ya boksi,watu kuibiwa simu kwa staili ya kuburuzwa na bodaboda ni kawaida sana.
 
Daah umenigusa niliibiwa sim wiki moja toka niinunue tena kwa kubana kamshahala kangu

Nililia had basi

Ila nmepata somo la kutokutumia sim njian

pole sana, ukitembea peke yako tembea upande wa kulia,ukiwa unaona magari yanayokuja na kuwa makini na madereva wa gari/bodaboda wanaojidai wanakuuliza kitu.
 
Umeniwahi....nilitaka kusema mostly hizo simu ni knockoffs....

Maisha ya kibongo bongo nani anaweza kumudu kununua simu genuine ya shilingi milioni moja!?

Hivi hujawahi kujiuliza inakuwaje designer clothes kama za Burberry, Gucci, LV, na kadhalika zipo zimezagaa mitaani ilhali hakuna maduka yanayouza designer products kama hizo?

Ustaadhi Swaleh habari yako.....
 
Una mdomo mbaya wewe. Usije ukanisema na yangu ikachukuliwa

hapana....ni kuona mbali tu,mtu ana simu ya 1m mnapita manzese yeye yuko busy ana 'touch screen' mwisho wake nini?!
 
yani nisinunue simu ya bei kubwa kisa sina gari binafsi! kuibiwa kupo tu popote pale na ktk mazingira yoyote, sasa M1 inatosha kununua gari? halafu nna wasi wasi na hizo shuhuda naona kama za kupikwa.

jaman hiyo M1 chukua aya baiskel huwe unapigia misele unaenda nayo na kazini, btw hautasumbuliwa na foleni lol!!!
 
Tell them....

Girls think big when it comes spending... saving to them is like showing them the way to guantamo!

I like chagga girls... they rock when it comes to saving and future life in general..

Mhhhhhhhhh
 
jaman hiyo M1 chukua aya baiskel huwe unapigia misele unaenda nayo na kazini, btw hautasumbuliwa na foleni lol!!!

ha ha ha ha ha ushauri mzuri sana huu.....au bodaboda ampe dereva awe anakuja kumchukua jioni mchana anapiga kazi hesabu inaingia swaaaafi!
 
Back
Top Bottom