Simu vs haki ya usiri kwa wanandoa

Simu vs haki ya usiri kwa wanandoa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,683
Tunapo ongelea haki, ni kitu tulicho zaliwa nacho.

Kila mtu ana haki ya kutunza siri zake bila kujalisha ni siri za namna gani.

Sidhani kama ndoa ni kihalalishi pekee kuvunja haki hii.

Utakuta baba analazimisha kuingilia mawasiliano ya mkewe, au mama analazimisha kuingilia mawasiliano ya mumewe......
Haki ya usiri iko wapo hapo?

Kwenye simu kuna mambo mengi zaidi ya hayo maswala ya michepuko, mambo ya ndugu zako (wa upande wako), mambo ya wafanya kazi wenzako, mambo ya rafiki zako.....

Haya mambo haya interest kwenye mahusiano yenu, unapopukua simu ya mwenzako huoni kama unamkuwa unamkwaza?
Hebu tuache jamani.

Simu ya mwenzangu si yangu
 
Hapo mkuu umenena cmu zimeleta karaha kwenye ndoa, cmu nimenunua kwa hela zangu ila masharti anatoa mwingne mara kwanini umeweka password lazma una michepuko, sasa kaolewa n cmu au mimi hpo wenzetu wanakosea
 
Mke atabakia kuwa mke wangu, Na simu itaendelea kuwa simu yangu.

Kama ambavyo simu haiingilii uhuru wa mke wangu, mke pia yampasa asiingilie uhuru wa simu.

Ila kwa sababu ya tamaa na wivu, nimeamua kuilinda simu yangu dhidi ya ubabe wa mke wangu. Password na Iheshimiwe na watu wote. Amina.
 
Tunapo ongelea haki, ni kitu tulicho zaliwa nacho.
Kila mtu ana haki ya kutunza siri zake bila kujalisha ni siri za namna gani.
Sidhani kama ndoa ni kihalalishi pekee kuvunja haki hii.
Utakuta baba analazimisha kuingilia mawasiliano ya mkewe, au mama analazimisha kuingilia mawasiliano ya mumewe......
Haki ya usiri iko wapo hapo??
Kwenye simu kuna mambo mengi zaidi ya hayo maswala ya michepuko, mambo ya ndugu zako (wa upande wako), mambo ya wafanya kazi wenzako, mambo ya rafiki zako.....
Haya mambo haya interest kwenye mahusiano yenu, unapopukua simu ya mwenzako huoni kama unamkuwa unamkwaza?
Hebu tuache jamani. simu ya mwenzangu si yangu

'mbebez' sampuli yako huwa ni makahaba, maguberi,wazinzi, na wachafu wa ngono waliokubuhu.
Lemme tell ya sumthin 'mbebez'...when ur married yo privacy'z no longer yo'z...it'z yo hubby'z!..tatizo la 'mbebez' wa bara la giza wanahusudu sana ngono you know!!
 
Tunapo ongelea haki, ni kitu tulicho zaliwa nacho.
Kila mtu ana haki ya kutunza siri zake bila kujalisha ni siri za namna gani.
Sidhani kama ndoa ni kihalalishi pekee kuvunja haki hii.
Utakuta baba analazimisha kuingilia mawasiliano ya mkewe, au mama analazimisha kuingilia mawasiliano ya mumewe......
Haki ya usiri iko wapo hapo??
Kwenye simu kuna mambo mengi zaidi ya hayo maswala ya michepuko, mambo ya ndugu zako (wa upande wako), mambo ya wafanya kazi wenzako, mambo ya rafiki zako.....
Haya mambo haya interest kwenye mahusiano yenu, unapopukua simu ya mwenzako huoni kama unamkuwa unamkwaza?
Hebu tuache jamani. simu ya mwenzangu si yangu

Mkuu angalia Kiswaili chako!
 
hili linahusu pande zote mbili. Pia msiangalie simu za wake zenu/ wapenzi wenu wa kike. Na wakiongea na simu, msitake kujua wanaongea na watu gani, au wanachat na nani whatsup
 
Habari waungwana.

Kila siku ninazungumza hili...

Ukiona unabania simu yako lazma utakuwa na mambo ambayo si mazuri.

Mimi simu yangu ni kama ya mke wangu. Na yake ni yangu. Hatuna siri yoyote. Siri ili iweje na tu mwili mmoja?

Akitaka kushika, akitaka kusoma, akitaka kupiga sina tatizo vivyo hivyo kwake.

Akiona labda kuna messages au calls hazijakaa vizuri au mimi pia nikiona basi tunaulizana kivizuri na kueleweshana.

Narudia tena, ukiona unaficha ficha simu katika NDOA basi unaandaa bomu
 
A very big pole for you mkuu...
 
Mimi password weka ukiwa kazini ila nyumbani password free
 
Mie huwa sina shida na simu ya mwenzangu, ila nitakuwa na shida iwapo niko naye afu anakuwa busy na kuchat. Pia calls ziwe za msingi, sio kuanza kupiga story za kombolela na rafikiye wa miaka ya 70.. Wapigiane huko huko!

Vitu vya msingi tu ndio viongelewe wakati tuko pamoja...

Nafuata hii kanuni na mwenzi wangu afuate...

Issue ya password kila mmoja afahamu password ya mwenzie... Baaaaas!!!
 
Usiri wa nini wakati nyie ni mwili mmoja??
Tatizo ni kwamba wanaume wengi simu yake ni ya kwake peke yake,simu ya mkewe ni yake pia.,hapo ndo shida za kukaguana huanza.
 
Lazima mtu ulinde chako,kuna majanga mengine kwa kushirikiana simu mnakuwa mnajipusha,je kama anawasiliana na ex wake,we bado hutaki kisa unalinda privancy.

Nye ni mwili mmoja bhana hata siri iwe mmoja,sisi ni binadamu lazima tuwe na wasiwasi haiwezakani mko sebuleni au mpo kitandani mwenzako kila saa anabrowse hata hujui anachofanya.
 
simu ya mtu sitaki na wala ya kwangu asishike pia

na pia sipendi ubussy wa simu wakati tupo wote...simu za muhimu tuu
 
Acha tu ninyimwe na ninyime haki
simu ya mupenzi siwezi kuacha kuikagua daima na milele najua na yangu anaikagua asubuhi, mchana na usiku
hayo ndo maisha tuliyochagua na tumeyazoea
 
Majambazi wengi huwa wanatengeneza mazingira ya kutokaguliwa simuzao...utawasikia, "Simuyako siikagui, kwahiyo nawewe usikague yangu"..
 
Back
Top Bottom