Simu vs haki ya usiri kwa wanandoa

Simu vs haki ya usiri kwa wanandoa

Tunapo ongelea haki, ni kitu tulicho zaliwa nacho.

Kila mtu ana haki ya kutunza siri zake bila kujalisha ni siri za namna gani.

Sidhani kama ndoa ni kihalalishi pekee kuvunja haki hii.

Utakuta baba analazimisha kuingilia mawasiliano ya mkewe, au mama analazimisha kuingilia mawasiliano ya mumewe......
Haki ya usiri iko wapo hapo?

Kwenye simu kuna mambo mengi zaidi ya hayo maswala ya michepuko, mambo ya ndugu zako (wa upande wako), mambo ya wafanya kazi wenzako, mambo ya rafiki zako.....

Haya mambo haya interest kwenye mahusiano yenu, unapopukua simu ya mwenzako huoni kama unamkuwa unamkwaza?
Hebu tuache jamani.

Simu ya mwenzangu si yangu

...mkuu Bujibuji nimerudi,nilikuwa mbali sana. kwanza si kweli kwamba haki ni kitu mtu anachozaliwa nacho,pili si kweli kwamba kila mtu anahaki ya kutunza siri zake hata ikiwa za namna gani. kwa mtazamo wangu mimi siri za mtu zinatofautiana kulingana na uhusiano wa watu husika. mfano kwa suala la simu, isipokuwa pale tu endapo simu itakuwa na mambo ya siri ya kikazi ambayo mweni wako hatakiwi kuyajua(hapo tu ndo simu itakuwa siri) lakini kwa namna yeyote mke anakila haki ya kuaccess simu yaako na hii ndiyo maana ya mwili mmoja, kwani kuna lipi la kuficha kwenye simu...?je ni jambo gani la ndugu zako unalolifanya ambalo mkeo/mumeo akijua inakuwa hatari kwako..?

kuna siri gani kubwa zaidi ya mke/mume kuvua nguo mbele ya mwenzi wako na akawa kama alivyozaliwa...?, lakini hili tunalifanya bila kuhoji tukijinanga ni halali yangu si mke/mume wangu...!! na kwanini simu iwe tatizo...?

mkuu bujibuji kwa heshima na taadhima nipe mfano wa jambo moja tuuuu, ambalo mke wako hapaswi kulijua kwenye simu yako nami nitakupa sababu kuwa si usiri bali kuna kitu zaidi ya "siri"....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom