Simu nzuri zenye gharama osiyozidi $200

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,630
2,459
Lenovo ZUK Z2 $176
zuk-z2-2.jpg

RAM: 4GB
Storage: 64GB
Chip:
Snapdragon 820 2.15GHz Quad-core (Processor ile ile ya Galaxy S7/Edge, LG G5 na flagship zengine za 2016)
Screen: 5 inch (1080 x 1920)
Battery: 3500 mAh
Camera: 13MP back / 8 MP front
Mengineyo: Dual SIM, hakuna SD card, USB C, finger print scanner kwenye home button mbele (Lenovo ZUK Z2 - Full phone specifications)

Mazuri:
Bei: $176 delivered DSM kutoka BangGood.com.
Spidi: Snapdragon 820 pamoja na RAM 4 GB simu inauwezo wa kurun kila kitu pamoja na gemu zote bila shida yoyote na bila kunasa nasa (lag).

Mabaya:
OS skin: Inatumia Android 6.0.1 ambayo ina skin ya Lenovo juu yake, kuna malalamiko kuwa baadhi vitu ambavyo ni standard kwenye Android havipo.
Camera: Camera yake ni OK sio mbaya ila haifananishiki na simu zenye camera nzuri hasa katika mazingira ambayo yana mwanga sana au mwango mdogo.
 
kwa hio bei na specs ni simu nzuri sana, pengine ndio simu yenye value kubwa, una uhakika hao jamaa ni trusted? ni mpya?
 
kwa hio bei na specs ni simu nzuri sana, pengine ndio simu yenye value kubwa, una uhakika hao jamaa ni trusted? ni mpya?
Ni mpya yes, baggood wako trusted pia inapatikana Aliexpress kwa similar price.
 
Back
Top Bottom