inabidi mke wako akaongee na wazazi wake, mambo ya kubebeshana nyani ukubwani kweli haifai.
Hizi mila za kukopi na kupaste wala hazina mashiko kihivyo, je siku akilazwa ukashindwa kwenda muona si utanyang'anywa mke?
Kukwazana bure tu kwa kweli, ila ningekuwa mie nisingemkopesha hata kidogo.
Wana JF kwanza kabisa
shalom. Ni jumamosi tulivu pande za hapa Dar na hali ya hewa ni manyunyu
manyunyu! Nikiwa katika harakati za kumalizia vipolo vya kazini mara
napokea simu kutoka kwa baba mkwe. Namsalimia kwa heshima na tahadhima
kwani ndiye mzaa chema (mke wangu). Ama baada ya salamu baba mkwe ana
anza kunishutumu kwamba sisi pamoja na binti yake hatuwaheshimu na
hatuwajali kwa sababu jana tulishindwa kupeleka japo ua kwa mama mkwe
kama zawadi ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa. Baba mkwe aliendelea
kutiririka kwamba sisisi tumekuwa na mkono wa birika! Na hata siku moja
hatujawahi kuwapa zawadi japokuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika
hilo.
Kikubwa ni kwamba mimi nimezaliwa na kuishi na kusomea kwenye hizi shule
zetu za kayumba! Uaratibu huu wa kushelekea siku za kuzaliwa nilianza
kukuana nao nikiwa chuo kikuu. Sikuwahi kushelekea katika kukua kwangu
wala sikumuona baba na mama yangu wakitunulia zawadi wakati wa hii siku
nyeti. Sina nia mbaya ya kutopeleka zawadi kwa mama mzaa chema lakini
mazingira niliyokulia yanachangia sana mimi kutokuwa sensitive na hizi
ishu!
Sasa wandugu nifanyeje kwani Jumamosi leo nimeambulia lawama na
shutuma.
Zipokee tuu,lawama kaumbiwa mwanadamu!!!Wana JF kwanza kabisa shalom. Ni jumamosi tulivu pande za hapa Dar na hali ya hewa ni manyunyu manyunyu! Nikiwa katika harakati za kumalizia vipolo vya kazini mara napokea simu kutoka kwa baba mkwe. Namsalimia kwa heshima na tahadhima kwani ndiye mzaa chema (mke wangu). Ama baada ya salamu baba mkwe ana anza kunishutumu kwamba sisi pamoja na binti yake hatuwaheshimu na hatuwajali kwa sababu jana tulishindwa kupeleka japo ua kwa mama mkwe kama zawadi ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa. Baba mkwe aliendelea kutiririka kwamba sisisi tumekuwa na mkono wa birika! Na hata siku moja hatujawahi kuwapa zawadi japokuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika hilo.
Kikubwa ni kwamba mimi nimezaliwa na kuishi na kusomea kwenye hizi shule zetu za kayumba! Uaratibu huu wa kushelekea siku za kuzaliwa nilianza kukuana nao nikiwa chuo kikuu. Sikuwahi kushelekea katika kukua kwangu wala sikumuona baba na mama yangu wakitunulia zawadi wakati wa hii siku nyeti. Sina nia mbaya ya kutopeleka zawadi kwa mama mzaa chema lakini mazingira niliyokulia yanachangia sana mimi kutokuwa sensitive na hizi ishu!
Sasa wandugu nifanyeje kwani Jumamosi leo nimeambulia lawama na shutuma.
Sasa kama mkeo amekulia kwenye familia ya kubofya kwa nini asikuelekeze? Angalia mkuu usije ukanyang'anywa mke bure
inabidi mke wako akaongee na wazazi wake, mambo ya kubebeshana nyani ukubwani kweli haifai.
Hizi mila za kukopi na kupaste wala hazina mashiko kihivyo, je siku akilazwa ukashindwa kwenda muona si utanyang'anywa mke?
Kukwazana bure tu kwa kweli, ila ningekuwa mie nisingemkopesha hata kidogo.
Duh! Hatupishani sana mkuu, binafsi hata siku yangu ya kuzaliwa mara nyingi nakumbushwa na mail za JF, hapa nitakumbukaje d'day za mama au baba mzaa chema . Pole mkuu:sad:
wazazi wanapoanza kuiga mambo ya ughaibuni ni shida mnoo...ila kama ni ishu ya upande wa pili na weye unataka kushiriki ni bora ukajificha nyuma ya mkeo ili usihusike moja kwa moja...kwani utakua ni mchezo kila siku ...leo mama mkwe kesho dingi. kesho kutwa kipaimara..wiki ijayo harusi...THE LIST GOES ON
Mkuu kiranga hapo ndo pana nishangaza kwani inaonekana kwamba kuna jambo nyuma ya pazia...Zawadi haiombwi wala kulazimishwa, ila pia kukosa fadhila si maungwana.
Ungepeleleza familia ikoje na wakwe wanataka nini kabla ya kuoa.
Inaonekana wakwe zako wanaweza kuwa na lao zaidi ya hili la zawadi.Haiyumkiniki mtu mzima kulilia zawadi kama mtoto anayelilia peremende.
Mkuu Bak kwa jinsi tunavyoishi na wakwe zangu hatuna matatizo na tumekuwa tunashirikiana katika shida na raha. Natumekuwa pale tunapokumbuka isipokuwa nimepata picha moja kwamba kumbe ukiona mtu anakupatia zawadi jua na wewe unatakiwa urudishe kwa kile kiwango.. am wondering ndo maana watu wakati wa harusi ubwaga machozi wakijua fika zile zawadi lazima zilipwe... je ni sahii kukataaa zawadi kama unajua hutaweza kuzilipa?
Mkuu hata ya kwangu mie huwa nakumbushwa na hii mitandao... hata wazazi wangu wenyewe sikuzao za kuzaliwa huwa nasahau