Simu ni Samsung kuanzia S 23 na kuendelea kama unataka kutumia kwa ajili ya picha zina picha nzuri pamoja na simu ukipiga unamsikia vizuri hata awe eneo lisilo rafiki kwa sauti mtaelewana na kwa budget yako utapata moja ya hizo simu..
Mleta mada amesema anataka simu yenye kamera nzuri kwa milioni 1.3
Soma tena uzi vizuri. Unapaswa utaje simu zenye kamera nzuri around hiyo bei
Pia unapopinga Xiaomi 15T unapaswa utoe technical reasons, why mtu asinunue hiyo simu? Brands kama Samsung na Xiaomi zina simu za gharama zote, kuanzia chini, kati hadi juu kabisa na zinatofautiana ubora na uwezo (kuanzia materials, processor, battery, camera nk) kwa hiyo unaposema simu za brand hii usinunue unapaswa uelewe unanunua simu moja, sio brand nzima
So nikuulize, kwa nini unaona Xiaomi 15T haifai kununua kwa milioni 1? Taja sababu za kisomi, kuelezea kwa nini haifa kununua Xiaomi 15T/ 15T Pro SPECIFICALLY
Dunia nzima inajua kuna simu nyingi tu nzuri za hiyo budget, kwamba Samsung Galaxy S24 FE ni simu mbaya? Au Xiaomi 15T ni simu mbaya? Unafuatilia hata review za simu wewe?