Simu imeibwa

Moo Click

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
3,495
Reaction score
3,261
Wandugu na JF Experts Poleni na Majukumu mchaka mchaka ndo uo kila siku ni Kuhangaika...salamu kwenu nyote

Okay ni Hivi Nauliza kuna Namna yoyote inaweza fanyika kwa simu iliyo ibiwa ikapatikana? Nilisha wai sikia kuhusu TCRA na Polisi huku nako kuna uhafadhali kweli?..na Taratibu zao zipoje mpaka simu kurudi?

Nawasilisha
 
nshawahi kupata simu yangu kwa kuwa nlikuwa na jamaa anafanyia Vodacom
alitresi namba ya simu inayotumia imei yangu akanipa nikamsaka jamaa kwa namna zangu hadi nikamkamata kama kuku. bahati yngu ni kuwa aliiba simu yangu alikuwa anatumia Voda
 
Polisi wanafuatilia na wana uwezo wa kurudisha simu kama una imei na ushahidi kama risiti ama boksi la simu kuwa hio simu ilioibiwa ni yako.

Sema mara nyingi hawadeal na simu za bei rahisi, ukiwa na iphone ama galaxy S/note wanakusaidia ukiwa na hela ya mafuta.
 
Ni kwenda polisi ukiwa na imei namba na namba zako za simu ,alafu unapewa mpelelezi ndo anaanza kufatilia
Muhimu.....polisi wanaangalia sana gharama ya simu na hela yako ya mafuta
 
Ni kwenda polisi ukiwa na imei namba na namba zako za simu ,alafu unapewa mpelelezi ndo anaanza kufatilia
Muhimu.....polisi wanaangalia sana gharama ya simu na hela yako ya mafuta
Duh
 
Sasa simu ya Laki 3 ndugu si hela yote itaishia huko
 
Nenda Polisi kama una IMEI number.gharama zote utakazo tumia atazilipa huyo utakaemkuta na simuyako.
 
Simu ya laki 3 ngumu kuipata, ila jaribu bahati yako.
Lakini ni vigumu pia kuitumia yaani mnakosa wote-aliyeibiwa na anayenunua. Anapata mwizi tu ikiwa atapata mnunuzi mjinga asiye makini la sivyo hana kwa kuuza. Hata Android siku hizi bila taarifa za mnunuzi wa kwanza huwezi kuifungua.
Nashangaa wanaoendelea kuiba simu siku hizi labda uibe vitochi.
We ukiibiwa simu badilisha password kwenye Emali yako basi mnakosa wote
 
Frp hio security ya Android ni danganya toto tu inatoka kirahisi.
 
kosa kwa aliye ibiwa kivpi?
 

Njia ya uhakika 100% kupata simu yako ni kununua nyingine..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…