Yako mambo ambayo Roho Mtakatifu alinifundisha na anaendelea kunifundisha kuyazingatia kwa ajili ya kulinda uhusiano wangu na Mungu kila siku za maisha yangu mambo hayo ni :_
Jambo la Kwanza
Uhusiano wangu na Mungu katika Utoaji wa Sadaka
Mahusiano ya Mwanadamua na Mungu yanapimwa kwa njia ya utoaji
Biblia inasema
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
Kwa hiyo kama Mungu alionyesha upendo wake kwa kumtoa Mwana wake tena wapekee ujue na sisi pia tunatakiwa kutoa
Kwanini utoaji unaonyesha ni kiwango gani unampenda Mungu
Kwa sababu mali yako inapokuwepo ndipo na moyo wako unapokuwepo, kwa hiyo kama unatoa sana maana yake moyo wako umeutoa sana kwa Mungu
Hata katika mahusiano kama unatoa sana mali zako kwa mwenzako hiyo ni dalili ya kwanza inayoonyesha jinsi unavyompenda mwenzako
maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi. Luka 7:5
Wazee wakiyahudi walimwomba Yesu amponye kijakazi wa akida mmoja ambaye kwa sababu aliwapenda wayahudi hata kuwajengea kanisa, kwa hiyo upendo wake ulipimwa kwa jinsi alivyo toa mali yake kwa wayahudi
Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Matendo ya Mitume 9:36.
tunaposoma habari ya Dorcas pamoja kuwa na matendo mema alikuwa anatoa sadaka, ndio maana hata alipokufa watu walimwomba Petro kwa ajili yake na Mungu akamfufua kutokana na sadaka zake
1 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.
Matendo ya Mitume 10:2
Kornelio sifa kubwa ya utawa alikuwa anatoa sadaka
Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. Luka 19:8
Zakayo baada ya kukutana na Yesu ili kuthibitisha kwamba anampenda Yesu alikubali kutoa mali zake kwa maskini
Hivyo basi njia moja wapo ya kutafakari uhusiano wetu na Mungu ni kwa njia ya utoaji wa sadaka
Kama mwakajana ulikuwa unatoa sadaka ya 10,000/=, mwaka huu unatoa 1000/= licha ya kipato kuongezeka, ujue upendo wa Mungu kwako umepoa hiyo ni taa ya njano unataliwa kuifatilia
kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Mathayo 6:21
Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu.