Simshauri mtu yeyote kuweka fedha benki kwa Tanzania ya sasa, ni hasara sana!

Interest ipo juu kwa sababu ya inflation na pia currency yetu si hard currency. Yaani inaweza kuporomoka au lolote laweza kutokea. Kwahiyo kama inflation rate ni 6 0r 7% unadhani benki zitafanyaje?

They should at least double the interest rate na si kutripplicate au quadruplicate....tz interest ni majanga. Unabisha kwa sababu umeumbwa kuwa hivyo.
 
They should at least double the interest rate na si kutripplicate au quadruplicate....tz interest ni majanga. Unabisha kwa sababu umeumbwa kuwa hivyo.
Ukisema wadouble unatumia formula gani? Inawezekana hata ikawa chini ya hapo lakini kuna maswali kadhaa. Ok una inflation ambayo at times inaweza kufikia asilimia 10%, kuna default risks (mtu hawezi kulipa mkopo) na hakuna credit rating agency, tunapoishi hapaeleweki, currency inafluctuate inawezekana wao wameinvest kwenye other currency, kuna administration costs, rents, electricity and other running costs. Kubwa zaidi waliiowekeza fedha zao wanataka return unafanyaje? Lingine legal institutions ni weak. Mtu akidefault hata ukitaka ku-repossess assets zake kama security it could take ages. Kwahiyo kinachofanyika licha ya kwamba macroeconomic issues ni weak mabenki wanadistribute risks.
 
Pengine ungerekebisha kichwa cha habari "Kuweka benki hela kwa Tsh maana ukiweka kwa US$ hakuna Tatizo"
 
Pengine ungerekebisha kichwa cha habari "Kuweka benki hela kwa Tsh maana ukiweka kwa US$ hakuna Tatizo"

Ni kweli, lakini pia niliona gharama za administration za foreign currency account ni kubwa mno! Kuna wakati nilifunga account na benki moja kwa sababu walipandisha gharama zao hadi USD25/month. Sasa imagine unalipia gharama za benki sawa na Tshs 50,000 kwa mwezi, nikaona bawa langu sio kubwa ngoja nilikimbize!
 
Ndio maana nikasema invest kwenye low risk areas nilizotaja na sio kuweka fedha bank au hata kununua treasury bonds




Nimesema kwamba kabla ya mfumuko wa haya mabenki tulikuwa na NBC ambayo ilikuwa haitozi gharama zozote na bado ilipata faida kubwa tu kila mwaka. Haya mabenki yalipokuja na kuambiwa juu ya modus operandi ya NBC wakati huo walisema wasingeingia soko la benki Tanzania hadi NBC ibinafisishwe ili itumie modus operandi kama yao kwa kuwa bila hivyo wasingepata wateja. Nyerere alilipinga sana hili na hata Wabunge wakakubaliana naye. Lakini Mkapa akalilazimisha na hata kuwatisha na kuwafokea Wabunge Bungeni na NBC iliyoonekana kikwazo kwa haya mabenki yanayotuibia kila siku ikabinafsishwa kwa bei ya kutupa ndio mabenki mapya yakaingia nchini na kina CRDB kulazimishwa kufuata modus operandi zao kukamua wateja.

Kwanza jiulize, mimi niliona interest niliyokuwa napewa (sikutajii benki) na benki kwenye savings account yangu ni 2.5% Niliomba mkopo wa nyumba nikaambiwa nitaulipa kwa interest ya 23%. Sasa hiyo ni biashara au utapeli? Gharama za administration zinafika hadi USD20 kwa mwezi kwa savings account ya interest ya 2.5% hata kama hujafanya transactions zozote huo sio wizi tu uliohalalishwa na serikali yetu?
Ukiwekeza kwenye low risk investment, return ni ndogo pia na inamezwa na inflation na other running costs, kwahiyo itakuwa ni kama benki. Unless uje hapa useme unamaanisha nini kusema low risk areas kwa Tanzania ambapo return itakuwa nzuru.
Kwenye mfumo wa NBC si mfumo wa biashara ya sasa. NBC ilikuwa inamilikiwa na serikali. Dhamana za serikali na transaction nyingi zilipita huko na ndio ukiritimba ule. NBC wakati wake ni mwingine kabisa, technology haikuwepo, ni mafaili mengi, state ownership/control na siasa nyingi. Kwa ujumla tulikuwa kwenye mfumo wa siasa ya ujamaa na kujitegemea. Watu wanaiba saana na hakuna usalama.
Mabenki yanaleta ushindani na upatikanaji wa huduma. Lakini ukiangalia saana upande wa mabenki angalia wale walioweka fedha zao, wawekezaji. Kuna dhana ya capital requirements et al. Hawa watu unataka wapate kiasi gani kwa pesa walizoweka? Maana siku ya siku ni lazima utambue kuna shareholders wakati unajadili. Naomba tuje na uhalisia interest rate sahihi ingekuwa ni ipi? Hapa tufikirie spread ya interest ya savers au aina yoyote ya account na borrowers, hiyo ndio faida. Kisha tuigawe kwa shareholders, running costs, reserves etc. na tukubaliane ipi ni fair?
 
endelea kusave tu! ili uanzishe benki lazima uwe na mtaji then ndo unawakopesha watu! lakini pia ili benki ifanye kazi vzr mkopaji lazima atumie benki hiyo kufanya biashara zake, means mzunguko wake upitie benki!
kama unadhan wanaosave ndo wanaendesha benki, fikiria mara mbili

Hata usipo save, pesa ikiingia tu ndani ya dakika 2 wao wanazalishia pesa hio hio, usizani kwamba ile pesa unayo weka bank inawekwa kwenye sanduku yako,no one using. Lol think
 
Hata usipo save, pesa ikiingia tu ndani ya dakika 2 wao wanazalishia pesa hio hio, usizani kwamba ile pesa unayo weka bank inawekwa kwenye sanduku yako,no one using. Lol think

Kijana seems huelewei kinachoongelewa, saving haimaanishi hela yako isipitie bank, inamaanisha hela yako iwe kwenye mizunguko muda mwingi zaidi ya kuwa bank! ndo maana watu mnahizimizwa kutafuta pa kuwekeza/kufanyia kazi hela yako instead ya hela kuendelea kukaa tu bank!
 
Mimi nimeamua kutunza pesa zangu kwenye SACCOS ya mkurugenzi ndo haina makato ya mwezi na ukikopa riba yake ni ndogo. Karibu Biharamulo
 
Unaongelea Fixed Deposit au Current Account mdau?
Mbona naona faida ipo tena kubwa tu au unaongelea aina fulani ya bank? Hebu niweke wazi.
kweli ,huyu mdau sijamuelewa kwa upande mwingine. kwahiyo unashauri wenye currrent account nao tusiweke fedha bank? can you emagine mtu anakiasi cha mil 200 kwenye account aweke wapi sasa?. au unazungumzia kwa wale wenye salary account . pia makato ni ya juu ndiyo,ila cost ya kutoweka hela bank ni kubwa kuliko kuweka pesa bank .hapa nikizungumzia risk( wizi au kushindwa kuweka akiba.......
cc to mtoa maada
 
Umezidisha sana chumvi, ili millioni moja iwe sawa na 700,000 ndani ya mwaka mmoja inflation inabidi iwe kama 30% kitu ambachoi sio kweli kwa TZ inflation ni kama 7% pia savings account inakupa 7-10% percent kutegemea na benki na kiasi unachoweka hivyo kuweka benki unakuwa kama umetoa droo na inflation au umepata fida kidogo.

Kuweka benki hela ni kwa ajili ya usalama wa hela yako, usitegemee kupata faida ya ajabu lakini pia sio rahisi kupoteza hela yako kama kwenye biashara au hisa.

Risks Vs Rewards.
youur 98% right
 
Kijana seems huelewei kinachoongelewa, saving haimaanishi hela yako isipitie bank, inamaanisha hela yako iwe kwenye mizunguko muda mwingi zaidi ya kuwa bank! ndo maana watu mnahizimizwa kutafuta pa kuwekeza/kufanyia kazi hela yako instead ya hela kuendelea kukaa tu bank!


Kama nimekupa hela uizungushe halafu unaikata the so called bank charges.
Na hiyo hela inakurudishia faida kubwa at 20%.
Hii ni fair.
 
Kama nimekupa hela uizungushe halafu unaikata the so called bank charges.
Na hiyo hela inakurudishia faida kubwa at 20%.
Hii ni fair.

kama bank unapata 20% faida (tena kwa saving account) endelea kuweka hela bank,
 
Ni kweli kutokana na high inflation rate (ongezeko la bei) na kushuka kwa thamani ya shilingi, nadhani serikali na benki kuu ingeshusha interest rate kwa sasa pia nadhani njia mbadala ya kuweka fedha benki unaweza kununua hisa au bonds
 
Kuna rafiki yangu aliweka laki 2 kwenye saving akaunti crdb eti ada ya watoto, baada ya mwaka 1 na miezi kadhaa akakuta 160,000 tu. Na hapo hiyo akaunti alikuwa hafanyi transactions zingine, aliweka tu hizo hela akaiacha akaunti hadi alipoenda kutoa akakuta zimepungua hivyo

Hakupata elimu tosha ya akaunti gani afungue.
Kuna akaunti za watoto huwa hazina charges acheni kudanganyana huko mtaani.
 
Wana JF,

Kumekuwa na ushauri mbalimbali unaotolewa kwamba watu waweke fedha zao benki. Ukweli ni kwamba kwa hali ilivyo Tanzania, nisingemshauri mtu yoyote kuweka fedha zake benki kwa sasa. Kuweka fedha benki kwa sasa ni kukubali kupata hasara juu ya fedha yako kwa mambo mawili ya msingi; kuporomoka kwa kila siku kwa shilingi ya Tanzania, na pia gharama za kupita kiasi zinazotozwa na benki.

Hali ilikuwa tofauti wakati wa enzi za Nyerere ambapo Benki ya Taifa ya Biashara ilikuwa inatoa riba ya juu kwa wateja wake, bila kuwatoza gharama zozote kwa kuweka fedha zao benki. Wakati huo, hakukuwa na gharama za kila mwezi au zakila wakati unapochukua au kuweka fedha benki. Na pia thamani ya shilingi ilikuwa haiporomoki kila siku kama siku hizi.

Siku hizi ukiweka fedha benki kwanza inabidi ulipie gharama za benki za kila mwezi,hata kama huchafanya chochote benki, na pia kila unapochukua au kuweka fedha unatozwa bank charges. Cha ajabu ni kwamba benki hizo zinatumie fedha zako kuwakopesha watu na makampuni na kuwatoza riba kubwa! Ukikopa wanakutoza riba hadi 20%, wakati wewe ukiweka fedha benki wanakupa riba kiduchu ya2%.

Napia kwa hali ya mfumuko wa bei Tanzania, kila siku hela yako iliyo benki inapoteza thamani. Kama uliweka Tshs 1M mwaka jana tarehe kama ya leo, thamaniyake leo hii itakuwa kama Tshs 700,000/-, ukitoa gharama za benki na mfumuko wa bei. Kwa hiyo kwa kila Tshs 1m unayoiweka benki kwa mwaka, unapoteza kama Tshs300,000.

Hata hivyo sikushauri utunze fedha zako nyumbani, hakuna usalama. Ni vema sana ikiwa badala ya kuweka fedha benki ukaziingiza kwenye vitu vyenye risk ya chini kama kununua dhahabu, Tanzanite na kuhifadhi vitu hivi sehemu zenye usalama. Unaweza pia kujenga au kununua nyumba, kiwanja au shamba, vitu ambavyo ni rahisi kuviuza baadaye vikiwa vimeongezeka sana thamani.


Nnakubaliana na wewe kwenye hilo la kununuwa assets (viwanja, shamba, nyumba) badala ya kuweka benki.
 
Back
Top Bottom