Boss
kagoshima Baada ya Uchaguzi Mkuu 2020, Tunarudi kwenye Mfumo wa Chama Kimoja, Hakuna Mpinzani atakayepewa Jimbo, Yaani tunashinda 100 % kwenye Udiwani, Ubunge na Urais. Jiandae Kisaikolojia Boss.
Kwani kuna Mtu au Watu ... Wanateseka??? !!!
Baadhi ya Giants wa dunia kipindi cha nyuma waliamini kama wewe lakini ghafla mambo yaliwageukia na kugharimu maisha yao na wakazikwa.
Ni lazima tujifunze kuendana na wakati.
Vazi likibana shona lingine la sivyo utavaa nguo isiyo na staha pengine ukajikuta uchi.
Ujinga wa ccm ni kudhani wanayo support ya watu wengi wenye afya ya mwili na akili nyuma yao , kumbe wamejaa watu dhaifu, wanyonge na wajinga waliokata tamaa na wasio na matumaini ya kuishi, wakidhani umaskini wao umesababishwa na watu wenye afya ya mwili na akili ambao wengi wako nyuma ya fikra huru.
Siku hadi siku kundi hili la fikra huru linazidi kuongezeka mtaani logarithmically.
Wakati hao wajinga ambao ni mtaji wao wanapungua arithmetically na sasa kuna kila dalili hili kundi la wajinga ambao ni mtaji wao linataka kulingana na hawa wenye afya ya mwili na akili, hii inamaanisha mtaji wao unaisha.
Katika mazingira hayo uchaguzi huru ni kizungumkuti na ikitokea mtu akawahakikishia ulinzi wapiga kura machafuko huwa makubwa kwa mazingira hayo ambayo kimsingi huleta mabadiliko makubwa ambayo hawata yataka siku zote.
Ni vyema ccm ijiongezee mtaji wa wapiga kura kwa kukoma kuwapa watu maisha magumu na manyanyaso kwa kibri na jeuri. Kupanga na kuunda sera rafiki kwa maisha ya watu.
Kama sivyo anguko litawaramba na kuanza kung'ang'ania madaraka na hatimaye mtavuna mnachokipanda
Sent using
Jamii Forums mobile app