Simpendi ila nataka kufanya naye maisha

Simpendi ila nataka kufanya naye maisha

Atomic orbital

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
375
Reaction score
485
Ni mwanamke mcha Mungu mcheshi ana akili ananiheshimu na kunipenda pia anawapenda sana ndugu zangu nimemuumiza kihisia Mara kadhaa lakini bado upendo wake kwangu unazid kuchanua.

Hana mwonekano mzuri na Mimi sina hisia nae lkn naona kama nikiamua kuanza nae maisha atakuwa mke bora na mama bora kwa watoto.

Naomba ushauri wenu waungwana.
 
Mwanamke anayekupenda ni tofauti na unayempenda wewe,huyu kakupenda so atakua tayari kukusikiliza na kutekeleza kila utakalo.
Kimsingi mpe nafasi jiweke karibu naye mapenzi huanza na affection.
Nina wasiwasi kama inaweza kuja kuniletea mgongano wa kimantiki mkuu
 
Tuliza akili kwanza ujitafakari, usimuoe mtoto wa watu ukaenda kumtesa ndani ya nyumba.
Kama humpendi muache tu aende atapata atakayempenda mbele ya safari akaolewa nae maana hyo kitu unataka kufanya ni hatari kumbuka humuoi kwa ajili ya ndugu zako.
Kuna saa mtakua wenyewe wawili atakuhitaji na wewe utamuona sio wa maana just because huna hisia nae, ndio mwanzo wa kukesha bar na michepukoni ili usiwah kurudi kwako sababu huna furaha napo.
 
Je nitakuwa na fraha nitakapomuoa
 
Mwache akalivagae gumegume huko aje analia hapa
Naona na wewe unataka kuoa sura, "eti hana mwonekano mzuri".
Sifa ulizozitaja ni tosha kwa mtu kuwa mke bora, hayo mengine ya sura ni nyongeza tu.
Lakini kama hakuvutii mwache katafute mwenye mwonekano mzuri ambaye atapenda na ndugu zako pia.
 
Back
Top Bottom