Simoni wa Zelote, mwanasiasa wa upinzani aliyemfuata Yesu

Simoni wa Zelote, mwanasiasa wa upinzani aliyemfuata Yesu

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,639
Katika kipindi cha karne ya kwanza BK, kulikuwa na harakati ya Kiyahudi iliyoitwa Zealots

Hawa walikuwa kama chama cha upinzani dhidi ya utawala wa Roma katika Yudea.

Mimi nawafananisha kama chadema ya sasa dhidi ya ma ccm

Walikuwa na misimamo ifuatayo

Walikataa kutawaliwa na Roman Empire
Walikataa kulipa kodi kwa Kaisari
Waliona Mungu pekee ndiye Mfalme halali wa Israeli

Walihamasisha mapambano ya kuikomboa nchi

Harakati yao ilifikia kilele wakati wa

👉 First Jewish–Roman War
Vita hiyo ilisababisha maangamizi makubwa, ikiwemo kuharibiwa kwa Hekalu la Yerusalemu mwaka 70 BK.

Hivyo, jina “Zelote” halikuwa jina la kawaida lilimaanisha mtu mwenye itikadi kali ya ukombozi wa kisiasa.

Mfano usikie mtu kama Mdude Chadema , ndio sawa na huyu Simoni wa Zelote .,

Simoni alikuwa mmoja wa mitume 12 wa Yesu.
Anatajwa katika
Injili ya Luka 6:15
Matendo ya Mitume 1:13

Pia anaitwa
👉 Simoni Mkananayo (Simon the Cananaean)
Watu wengi hudhani “Mkananayo” maana yake ni mtu wa nchi ya Kanaani (Canaan).

Lakini si hivyo.
Neno la Kigiriki lililotumika kwenye injili ni “Kananaios”, ambalo linatokana na neno la Kiaramu “qan’an” lenye maana ya

mwenye wivu mkali, mwenye juhudi kali, au mwenye msimamo mkali.,

Kila ninapochunguza habari za Simon Mkananyo au Simoni wa Zelote ,taswira inayonijia ni ya Mdude Chadema.

Mtu aliyekuwa na msimamo mkali, mtetea haki, aliyekuwa tayari kufa kwa ajili ya taifa lake .

Kwa hiyo “Mkananayo” si jina la kabila bali ni jina la sifa/tabia sawa na “Zelote”.

Simoni Mkananayo ndio huyo huyo Simoni Zelote.

Hebu tafakari hili
Mtu ambaye angekuwa na hamasa ya mapinduzi
Mtu ambaye angechukia Warumi(weka maccm kwa Leo )
Mtu ambaye angeamini silaha ndiyo suluhisho

Lakini Yesu alimwita… naye akaacha kila kitu.
Yesu hakumwita kubeba upanga, bali kubeba msalaba.

Hii inaonyesha mabadiliko makubwa Kutoka mapinduzi ya kisiasa,Kwenda mapinduzi ya kiroho

Yesu aliwaita watu wa itikadi tofauti
Huu ndio uzuri wa Injili.

Katika kundi la mitume kulikuwa na

Simoni Zelote — kutoka chama cha upinzani dhidi ya Utawala wa Roma

Mathayo — aliyekuwa mtoza ushuru kwa Warumi

Fikiria hili sasa
Mwanachama wa “chama cha upinzani” let's say CHADEMA
Na mfanyakazi wa “serikali ya Roma”Lets say Yeyote unayemjua

Wanakaa meza moja chini ya Yesu., na wanaanza kufundishwa na kuwa kitu kimoja .

Hawa Wanafunzi wa Yesu walikuwa binadamu wa kawaida.
Mathayo aliacha kazi yenye mapato na marupurupu., alikuwa mkusanya ushauru forodhani na walikuwa wanaiba sana ,rejea Zakayo mtoza ushuru.

Simoni wa Zelote yeye aliacha nafasi kubwa ndani ya chama cha kisiasa.

Wavuvi kama Petro na wale Wana wa zebedayo(Yohana na Yakobo) waliacha biashara zao.

Kama binadamu yeyote Kuna wakati waliingiwa na hofu wataishije?

Kwa kawaida, Petro ndiye alikuwa msemaji wao.

Inaaminika pia alikuwa mkubwa kiumri

Siku moja akamuuliza Yesu

Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe; basi tutapata nini?”
Mathayo 19:27

Yesu akawajibu

Amin, nawaambia, ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, Mwana wa Adamu atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi juu ya viti vya enzi kumi na viwili, mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.”
(Mathayo 19:28–29)

Yesu hakupuuza sadaka yao.
Aliwahakikishia thawabu ya sasa na ya milele.

Biblia haisemi sana kuhusu huduma yake baadaye.
Mapokeo ya kanisa yanasema alihubiri Injili katika maeneo kama

Uajemi
Syria
Misri


Hayo maeneo Hadi Leo ya wanakristo ambao kama ukifika utashangaa Imani zao ,wapo tayari hata kufa ila sio kuacha Imani ,ni matokeo ya Hawa mitume kama Simon wa Zelote .

Hayo maeneo yana mabaki ya MAKANISA ya KARNE ya 1-4

Baadhi ya mapokeo yanasema Simoni wa Zelote aliuawa kwa ajili ya imani yake (martyrdom),

Simoni wa Zelote anawakilisha Kutoka mwanasiasa wa mapinduzi hadi shahidi wa Injili., na mtume mkubwa aliyesambaza UKRISTO.

Majina ya mitume yapo katika Yerusalemu Mpya

Katika maono ya mbinguni, mtume Yohana aliandika kuhusu mji wa Yerusalemu Mpya

Ufunuo wa Yohana 21:14

Anasema
Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake majina ya mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.”

Hii ina maana
Jina la Simoni Zelote
Jina la Mathayo
Jina la Petro
Yameandikwa katika misingi ya Yerusalemu Mpya.
FB_IMG_1771338876478.jpg
 
Amina ubalikiwe sana mtumish

Endelea kutuletea madini kama haya

Hata kama hatuijui bible lakin Kuna vitu vya msingi lazima tuvijue
 
Majina ya mitume 12 ni pamoja na Yuda Iskarioti au yeye anaondolewa linawekwa na Yule mwanafunzi aliyepigiwa kura kuziba nafasi yake -Mathia?
 
Back
Top Bottom